Professional Documents
Culture Documents
Kisima Cha Maji 18102020
Kisima Cha Maji 18102020
UJUMBE
Kisima ni chanzo cha maji
Kisima ni mahali zinapotoka baraka zako
Kisima ni mahali penye hazina yako
ANDIKO KUU
Mwanzo 21:14-19
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji,
akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka,
akapotea katika jangwa la Beer-sheba. 15 Yale maji yakaisha katika kiriba,
akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. 16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye
kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa
akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. 17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika
wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri?
Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. 18 Ondoka,
ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa
kubwa. 19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda
akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
Mwanzo 26:19-22
18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za
Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa
kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
19 Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji
yanayobubujika. 20 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka
wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu
waligombana naye. 21 Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena.
Akakiita jina lake Sitna. 22 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala
hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa
Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Wapo wanaogombania kazi yako; wakisema nafasi hiyo uliyonayo ni yao.
Wapo wanaogombania ardhi yako; wakisema ni mali yao;
Wapo wanaogombania mchumba wako, hata kama hawakwambia, wakisema
hustahili wewe kumpata huyo.
Hata kama ni haki yako achilia; Yakobo alikuwa na haki ya visima ambavyo
Ibrahimu Baba yake alichimba huko Gerari lakini Wafilisti wakavigombania.
Isaya 43:2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito,
haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto
hautakuunguza.