You are on page 1of 6

Data Mode Go to Free

9+ 36

Enea Mwakamyanda Friends Who Like Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry)

2 hrs ·

SEMINA YA NENO LA MUNGU-IRINGA MJINI UWANJA WA GANGILONGA


NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
SOMO: NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA
SIKU YA KWANZA
TAR 19-OCT-2016
LENGO LA SOMO: Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya Ardhi iliyokwamisha mafanikio yako
iondoke na ufanikiwe.
Kuna uhusiano sana kati ya ardhi na mafanikio yako kwa hiyo ni muhimu sana kulifuatilia kwa karibu
sana somo hili
Tuangalie mifano inayoonesha uhusiano wa ardhi na kufanikiwa kwa mtu.
#MFANO WA KWANZA
Mwanzo 3:17-19
"Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao
nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku
zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso
wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi
wewe, nawe mavumbini utarudi"
Laana maana yake ni
Kutostawi
Kutofanikiwa
Kutokuwa na Furaha
Kutofikia kiwango cha mafanikio ambacho Mungu kakikusudia kwa ajili yako. Na Laana ni kinyume
cha baraka.
Mungu aliposema ardhi imelaaniwa alikuwa anataka kumuambia Adamu kuwa ukitaka kujua kitu gani
umebeba kwa kutofuata maelekezo yangu kuwa kuna laana iliyoko kwenye maisha yako na utakapoilima
ardhi haitakuzalia matunda yake.
#MFANO WA PILI
Mwanzo 4:11-12
"Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa
mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani."
Laana ya hapa sura ya nne ni tofauti na ile sura ya tatu kwa sababu laana ya Adamu ilikuwa ndani ya
Adamu lakini katika sura ya nne tunaona kuwa laana ipo kwenye ardhi moja kwa moja.Maana yake kwa
kila mtu atakaye kanyaga eneo hili anapata ile laana iliyoachiliwa kwenye ardhi .
#MFANO WA TATU
2 Mambo ya Nyakati 7:11-14
"Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni;
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na
kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi
yao"
Uponyaji tunaoungalia hapa ni uponyaji wa ardhi na nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki,biblia
inaposema kuwa nchi maana yake ni ardhi na sio watu au taifa. Taifa ni ni kundi la watu waliokubaliana
na mfumo wa uongozi na wakae kwa pamoja. Kwenye biblia unaona kabila linageuka kuwa Taifa au
familia kuwa taifa. (Angalia katika Kitabu cha Mwanzo 49)
Mwanzo 49:1,28
"Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.Hizo
zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja
mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki"
Hapa biblia haizungumzii uponyaji wa watu bali ni ardhi .Biblia inasema tena nikiamuru nzige kula nchi
maana nzige ni wadudu waharibifu na wanaoharibu mazao au udongo na Tauni ni ugonjwa wa
kuambukiza na kibiblia ikitokea ugonjwa wa kuambukiza ina maana kunakuwa na shida kwenye ardhi.
Ukitokea ugonjwa wa kuambukiza katika eneo fulani huwa wanaweka karantini na kufunga mipaka.
Kitendo cha kuweka mpaka ni Roho Mtakatifu anawajulisha kuwa shida hii imeishia mpaka hapa.
Suala hili la kufunga mipaka ili kuzuia maambukizo ya ugonjwa ni ya kiroho kwanza kabla hayajawa ya
kimwili.
#MFANO WA NNE
Yeremia 22:29-30
"Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana
watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake
atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda."
Huyu ni Mungu anazungumza na nchi (ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki) anaposema
Ee nchi ,nchi sikia ---- ina maana nchi inasikia
Andika maana yake inaweza tunza kumbukumbu
Kuwa hatafanikiwa maana yake ni kuwa inaweza fuatilia
Wakati adhabu inatolewa kwa mtu huyu alikuwa bado hana watoto, lakini kumbukumbu iliandikwa
kwenye ardhi kuwa hata watoto wake wakija nao wasifanikiwe. Adhabu ilitolewa kwa sababu gani;
angalia mstari wa 21 Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii
ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.
Fikiria wewe ni mtoto na umeingia kwenye adhabu ya baba au mama na unatafuta kufanikiwa na
haufaninikiwi sio kwamba akili huna bali unazo lakini umezuiliwa kufanikiwa na ardhi kwa sababu ya
kosa la baba yako na mama yako je unaombaje?
#MFANO WA TANO
Mwanzo 28: 10-20
"10-13"Yakobo akatoka Beer-sheba , kwenda harani. Akafika mahali Fulani akalala huko usiku kucha ,
maana jua lilikuwa limekuchwa ,akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake ,
akalala usingizi palapale. Akaota ndoto, na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake
yafika mbinguni .Tena tazama malaika wanapanda na kushuaka juu ya yake. Na tazama Bwana
amesimama juu yake , akasema mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahim baba yako na Mungu wa Isaka , nchi
hii uilalayo ntakupa wewe na uzao wako"
Lile Neno nchi hii ulalayo Kwa lugha nyingine ardhi unayolala iwe ni nyumba uliyojenga au hoteli au
umejilaza mahali kwa muda mfupi au ni kwenye basi umelala au uko shambani umelala na ghafla unaota
ndoto, sio kila mahali angeweza kulala ila eneo lile lilikuwa na umiliki kamili wa Mungu.
USHUHUDA
Wakati tunafudisha somo hili Morogoro kwa staili tofauti. Kuna mtu mmoja wakati huo kuna mtu mmoja
alikuwa anafuatilia akiwa yuko ulaya na sisi tulikuwa Morogoro kwa ajili ya semina. Anasema alikuwa
anatufuatilia kwa mtandao.
Anasema kila akiwa ulaya alikuwa halali (Yaani anapata shida ya kupata usingizi) na akija Tanzania ndio
analala vizuri kwa hiyo akitaka kupata usingizi mzuri alikuwa anapanda ndege kuja Tanzania na akifika tu
huku analala vizuri kabisa. Akasikia tunafundasha na namna ya kuombea ardhi ya mahali unapolala
akaomba jinsi tulivyo fundisha akiwa huko huko , Tangu siku hiyo akaanza kulala vizuri.
#MFANO WA SITA
2 Samweli 21:1
"Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu , mwaka hadi mwaka naye Daudi akautafuta uso
wa Bwana , Bwana akasema ni kwa ajili ya Sauli na nyumba yake yenye damu kwa kuwa aliwaua hao
wagibeoni​"
Daudi katika kipindi chake cha uongozi kulitokea shida ya njaa na ilidumu kwa muda wa miaka mitatu. Na
alikuwa hajaomba kutafuta sababu na alishindwa kuhusianisha kati ya hali ya kiroho ya ardhi na shida ya
njaa iliyotokea.
USHUHUDA
Tulikuwa tunapita mkoa mmoja tuliona kitu cha ajabu sana, tuliona mahindi marefu na wakati tunapita
mahindi yalikuwa yameanza kunyong’onyea karibia na kunyauka ila sasa tunaona nyasi na vichaka ni vya
kijani kabisa. Sasa swali linakuja ni ardhi gani inachagua kutoa maji kwa nyasi na kuacha kutoa kwa
mazao ya chakula.
Kama ardhi imekugomea jaribu kupanda mahindi na maua na baada ya muda utaona mahindi
yananyauka lakini maua yanastawi. ukimuita mtalaamu wa kilimo ataanza kupima unyevu na
atakuelekeza na sababu za kitalaam, lakini shida ni kuwa kunakuwa na kitu kwenye ardhi ambacho
hakipo sawa.
#MFANO WA SABA
Ufunuo 12:12- 15
"Kwa hiyo shangilieni; enyi mbigu ,nanyi mkaao humo ole wanchi na bahari ! kwa maana Yule ameshuka
kwenu kwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana mda mchache tu. Na Yule joka alipoona ametupwa
katika nchi alimwudhi mwanamke Yule aliyezaa mtoto mwanaume. Mwanamke Yule akapewa mabawa
mawili ya tai Yule mkubwa ili aruke aende zake nyikani , hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na
nyakati na nusu ya wakati mbali na nyoka huyo,Nyoka akatoa katika kinywa chake nyuma ya huyo
mwanamke maji kama moto amfanye kuchukuliwa na mto ule"
Huyu mama angejuaje kuwa kufanikiwa kwake kulitegema sana msaada wa ardhi ambayo uliumeza mto
uliotolewa na Joka. Kwa hiyo hakikisha kila ardhi iko upande wako, iwe ni ya kanisa au unapolala au
unapofanya biashara.
kwenye semina zetu kuwa tunahakikisha mbingu na ardhi inakaa upande wetu ili kumzuia shetani. Sasa
hujiulizi kwanini kambi nyingine huwa wanachimbia hiziri ardhini?. Jibu ni rahisi kabisa kuwa wanataka
msaada wa ardhi
Kwani wanapofanya mambo ya mila wanapoweka maziwa mdomoni na kuweka na kutemea juu na chini
kwenye ardhi wanakuwa wanatafuta nini, wanatafuta msaada wa mbingu na nchi.
#MFANO WA NANE
Yoel 1:9-13
"Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana; Hao makuhani,
wahudumu wa Bwana, wanaomboleza. Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka
imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka. Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi
watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea. Mzabibu
umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba
imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu. Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni
yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa
Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu
wenu"
Unaombaje ikiwa hali ya kiroho ya ardhi imesababisha kuzuiwa kwa sadaka kanisani. Mungu kakataza
sadaka ili waombaji waombe ili hali zao za Uchumi ziwe vizuri na watoe sadaka.
Na kama unafanya semina au mkutano wa nje kama sisi usipojua namna ya kuombea ardhi utakuta watu
wanarudi na sadaka nyumbani kwao kwa sababu hali ya kiroho ya ardhi ina uhusiano mkubwa sana na
utoaji wa sadaka kwa watu
#MFANO WA TISA
Kumbukumbu la torati 8:7,12
"Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi,
na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na
kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;"
Kuna uhusianio na Baraka za Mungu na watu waliongizwa kwenye eneo lenye mipaka halali ya kiumiliki.
Ndio maana kati ya adhabu mojawapo inaifikia nchi ni miji kubomolewa au kukosa wakazi, kuwa ukiwa.
Sasa unaweza jiuliza swali hili gumu kuwa kwanini Sauli hakupata adhabu yeye katika kipindi chake
baada ya kuwaua wagebeoni. Lakini aliyepata madhara ni Daudi, kwa hiyo si tu kwamba Daudi alirithi kiti
bali na ile adhabu iliyokuwa kwenye kiti. Pia kuna uhusiano gani uliopo kati ya ardhi na cheo kosa la kiti
na kosa la mtu aliyekaa kwenye kiti na kosa la kiti.
Kosa la kiti adhabu yake atapata kila mtu atakayekaa kwenye kiti, kwa hiyo kumfukuza kwa jinsi ya mwili
kwa sababu amekosea haitatui tatizo la kiroho lililofanya akakose mtu mwingine atakayekuja atajikwaa
palepale alipojikwaa wa kwanza.
Usikose kufuatilia mfululizo wa pili wa somo hili, Ahsante na Mungu akubariki sana.
Hallelujah Glory to GOD

Like Comment Share

42

14 shares

Verona Eugene
Amina
See translation
2 hrs Like Reply More

Joyce Mwamafupa
Aminaa
See translation
2 hrs Like Reply More

Jemedari Wavita
,WATUMISHI WA MUNGU NYOTE MNA ITWA HUKU KARIBUNI TUFUNDISHANE BIBILIA
KARIBUNI

https://www.facebook.com/groups/270676177297955/

WAKRISTO HALISI ( REAL...

See translation
1 hr Like Reply More

Angela Chuwa
Ameen
See translation
1 hr Like Reply More

Apostor Joshua Kimaro


Limeeleweka Vema, Barkiwa.
See translation
1 hr Like Reply More

Apostor Joshua Kimaro


Limeeleweka Vema, Barkiwa.
See translation
1 hr Like Reply More

Olyvier Saruni
Amen
1 hr Like Reply More

Ayubu Mwampamba
AMEN
1 hr Like Reply More

Ayubu Mwampamba
AMEN,MUNGU AKUBARIKI.
See translation
1 hr Like Reply More

Amani Mushagalusa Mushagalusa


Amen! Mungu awa bariki sana, na pia huduma yenyu ibarikiwe!
See translation
1 hr Like Reply More

Janeth Malungu
Amen
1 hr Like Reply More

Mary Vitalis
Ameen.
See translation
1 hr Like Reply More

Amani Mushagalusa Mushagalusa


Amen! Mungu awa bariki sana, na pia huduma yenyu ibarikiwe!
See translation
59 mins Like Reply More

Bupe Daud
Amen mungu awabrk sana
See translation
55 mins Like Reply More

Catarina Kokushubira
Amen
9 mins Like Reply More
9 mins Like Reply More

Write a comment... Post

You might also like