You are on page 1of 4

JUMAPILI YA 17 YA MWAKA “A”

Wapendwa Taifa la Mungu, leo ni Dominika ya 17 ya Mwaka “A” wa Kanisa. Na


wazo kuu kutoka masomo yetu ya leo ni kwamba Ufalme wa Mbinguni ni kitu cha
thamani kubwa kiasi kwamba kila anayetambua hilo, lazima auze vyote alivyonavyo ili
kuupata. Basi ndugu zangu, tunalikwa sote kuutafuta kwa gharama yote. Tutumia
vizuri mdaa wetu, uhai wetu ili tuutafute Ufalme wa Mbinguni.

UFAFANUZI
Somo la Kwanza: 1 Wafal. 3:5, 7-13
Katika somo la kwanza, tunasikia jinsi gani Mfalme Sulemani alipohiji/aliposafiri
Gibeoni aliomba hakima/busara kwa Mungu ili aweze kuliongoza Taifa lake. Mungu
alikubali ombi lake, akamwongezea fahari, mali na maisha marefu.
Wapendwa, baada ya kifo cha Baba yake Daudi, Sulemani alisimikwa/alifanyawa
Mfalme wa kabila zote 12 za Israeli. Na kabla ya kuanza utawala wake, Mfalme
Sulemani alikwenda kumsifu Mungu kwa kumtolea sadaka/dhabihu katika madhabahu
ya Gibeoni na kuomba ulinzi wake katika utawala wake. Na ni uko madhabahu ya
Gibeoni ambako Sanduku la Agano, yaani Hema ya kukutania na Mungu wa Israeli
lilikuwa limewekwa huko kwa miaka 50 kabla ya kujenga Hekalu la Yerusalem, na ni
kilometa kumi na Yerusalemu (Cf. 2 M. Nya. 1:3). Na akiwa huko Gibeoni, wakati wa
usiku, Mungu alimtokea Sulemani katika ndoto na kumwambia aombe kwa Mungu
chochote apendacho. Mfalme Sulemani kwa kutambua kuwa yeye bado ni mtoto
katika mambo ya uongozi, aliomba moyo wa adili katika kuwahukumu watu wa Mungu
kwa haki, aliomba ufahamu katika kupambanua mema na mabaya. Na Mungu akampa
moyo wa hekima na wa akili, kupita wote waliokuwepo, waliopo na watakaokuwepo.
Na kwa wa Israeli, Mtu akiwa na Hekima vitu vingine atavipata kwa ziada kwa sababu
Hekima ni kila kitu (Cf. Mithali 3:13-18). Na Hekima ni Mungu mwenyewe. Hapo,
Sulemani aliomba mwanga wa kuelewa mpango wa Mungu na uwezo wa kutekeleza
mpango huo, moyo mpole ili aweze kuongozwa na Mungu wakati wote. Basi ndugu
zangu, kwa kifupi, katika somo hilo, tunamuona Sulemani mwanzoni kabisa mwa
utawala wake, uongozi wake, alielewa vema nini cha thamani katika maisha: kuongoza
na kuongozwa na Mungu ni hazina ya thamani kubwa kuliko vitu vyote. Na huo ndio
mwaliko wa somo la Injili yetu ya leo.
1
Somo la Injili Matayo 13:44-52
Katika somo la Injili, Yesu, kwa kutumia mifano, anaelezea thamani ya Ufalme wa
Mbinguni. Yesu anatumia lugha ya mifano kuuelezea ufalme wa Mungu. Kwa
Dominika Tatu mfululizo, Mama Kanisa anatualika kutafakari mifano ya Yesu
inayozungumzia juu ya Ufalme wa mbinguni katika sura ya 13 ya Injili ya Mathayo.
Dominika 15, tulialikwa kutafakari mfano wa mpanzi/mpandaji, na Dominika ya 16,
yaani iliyopita, tulialikwa kutafakari mfano wa magugu yaliyopandwa katika shamba la
ngano, Na Dominika ya leo, ya 17, tunalikwa kutafakari juu ya mifano mitatu ya
mwisho kati ya mifano 7 yanaongelea juu ya ufalme wa mbinguni katika Injili ya Mt.
1) Katika Mfano wa kwanza, Yesu anafananisha ufalme wa mbinguni na Hazina
iliyositirika katika shamba. Na Mkulima mmoja kwa bahati aliiona. Na alipoiona,
aliificha. Akaenda kwa furaha kuuza yote alivyo navyo na kununua shamba lile.
Mazingira: zamani za kale, uko Palestina, na Afrika pia, kwa sababu ya vita,
uhamishoni na kutokuwa na Benki, watu walificha hazina zao: Pesa za noti, dhahabu,
fedha na vitu vingine vya thamani kubwa katika majengo au shamba ardhini/katika
shimo. Wakitegemea kuzipata tena vita itakapoisha. Ila mara yingi ilitokea kuwa
baadhi ya wamiliki wa hazina zile kufariki au kushindwa kurejea tena kumakwao.
Hapo wale walioyachukua majumba au mashamba yao waliweza kwa bahati nasibu
kuzipata mali/hazina zile zilizofichwa. Ndio maana, katika Injili ya leo, Mkulima moja,
bila shaka mtumishi wa mmiliki wa shamba aliyeajiriwa, amegonga sanduku la chuma
lenye hazina wakati akiwa akilima shamba. Aliifisha tena sanduku ilo la hazina na
kwenda kuuza vyote alivyo kuwanavyo akalinunua shamba lile kwa sababu ameona
kitu cha thamani kubwa. Ila kwenye Mfano wa pili/2, ambao ni mfano pacha,
tunakutana na mfanyabiashara tajiri anayezunguka duniani kote ili kuisaka lulu ya
thamani kubwa. Ila tofauti na mfano wa hazina, mkulima alipata hazina ile kwa bahati
na sio kwa juhudi wala bidii zake binafsi, haikuwa mastahili yake bali ni zawadi tu
iliyogundulika kwa nasibu akiwa analima. Mfanyabiashara anaisaka kwa juhudi na
bidii kubwa kwa kuzunguka duniani. Mfanyabiashara huyo ni ishara ya wale wote
wanaosaka na kutafuta kwa bidi maana ya Maisha yao, ni wale wanaousaka wokovu
na ufalme wa Mungu kwa juhudi zao. Ndio kusema mifano hii miwili
inakamilishana ili kuweza kuuelewa ufalme wa mbinguni. Ufalme wa mbinguni kwa
nafasi ya kwanza ni zawadi lakini pia kwa nafasi ya pili kila mmoja wetu lazima
2
ajibidishe ili kuupata kama alivyofanya mfanyabiashara. Wote wawili, mkulima na
mfanyabiashara wanafanana katika kugundua kitu cha thamani kuliko vyote na kwa
kuuza vyote kusudi wakipate kitu hicho cha dhamani. Na ni bora tuelewe kwamba
ufalme wa mbinguni hatuwezi kuuuza na pesa zetu. Kuuza vyote, katika lugha ya
kibiblia, maana yake kuachana na vitu vyote ambayo vinatuzuwia kumfuata Yesu na
kuwa katika utawala wake na wanafunzi wake (Rej Mk 10: 21 va, vend; Lk 14:33 kila
mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.)
3) Mfano wa Tatu ndio ule wa juya/wavu lililotupwa baharini na kukusanya samaki
wa kila aina. Mfano huu unaendana na ule tuliousikia Dominika iliyopita wa ngano
pamoja na magugu. Mfano wa juya/wavu unatukumbusha mazingira ya ziwa lile la
Galilaya ambapo wavuvi walitumia wavu kuvua samaki na daima walipata samaki wa
kila aina wanaoweza kuliwa na wale waliotambulika kama najisi kadiri ya mapokeo
yao (Mambo ya Walawi 11:10-11). Na baada ya kuwavua, wavuvi walipaswa
kuwachambua ili kuwatenganisha samaki wasafi au wanaoweza kuliwa na wale
waliojulikana kama wabaya/najisi ili kutupwa. Na wazo katika mfano huu wa wavu, ni
kwamba kama vile wavu unavyovua samaki ya kila aina ndivyo ilivyo katika Kanisa la
Kristo. Kanisa ni mchangayiko wa watu wa kila aina: wema na wabaya, wathamani na
wasiyo na thamani, watakatifu na wakosefu. Ila katika hukumu ya mwisho, siyo watu
wote watakaoingia katika ufalme wa Mungu. Watu wabaya/wakosefu kama
hawajiweki katika hali njema ya kiroho wataukosa ufalme wa Mungu.

KATIKA MAISHA
Basi Ndugu Zangu, Fundisho Kwetu leo ni Nini?
1) Kwanza, Tunalikwa kutambua na kuona kitu gani cha muhimu/thamani maishani
mwetu. Ulimwengu wetu wa leo wa sayansi na Teknolojia umejaa vitu yingi sana. Vitu
vya kila aina. Siku hizi ni vigumu sana kwetu kuona kitu cha thamani na kipi kisicho na
thamani. Ndio maana siku hizi utamuona mtu moja ana simu 2, 3, 4, 5, nakathalika.
Simu za gharama sana. Nguo/Computer/Gari za gharama sana ili yeye mwenyewe
hana hata uwanja, hana hata nyumba. Na Mke hana. Kama ni Mke hana Mume. Na
kula anakula vibaya mno, wazazi wake wana lala mahali pa baya. Kama ni baba wa
Familia kila siku ni mlevi tu, Mama mlevi pia. Unaona maisha ya familia siyo mazuri
kwa sababu hakuna mipango maishani ya kugunduwa kitu cha thamani kitu cha
3
muhimu kwa ajili ya Familia. Tunalikwa ndugu zangu kuangalia na kugunduwa
nini cha thamani maishani mwako, kwenye Familia yako, kwenye utawa wako, kwenye
shule yako, nk. Na unapokigunduwa, fanya mipango yote ili ukipate. Hujikatalie
hata baadhi ya vitu ili ukipate kile kitu. Kama wewe ni mwanafunzi ukitaka
kupata matokeo mazuri shuleni, lazima uuze uvivi wako. Soma kwa bidii. Kuwa na
nidhamu ili upate kufikia malengo yako. Na swahali lingine ni kwamba, Je tunapo
kipata hiki kitu cha thamani, tunakitunza je? Wakati mwengine tunakipata kitu cha
thamani na tunaanza tena kukipoteza. Tunaanza kuwaza tena mambo ambayo si
yamuhimu maishani. Kwa mfano ndoa. Kila wakati unamuomba mungu kwamba uowe
au uolewe. Baadae ya kufanikiwa, unaanza tena kujuuta kwanini nilioa? Nilikoa au je?
Watawa vile vile, niwe Padre, niwe Mtawa, baadae hauoni tena thamani ya utawa,
unataka kuacha utawa na kwenda kuoa. Tuelewe ndugu zangu kwamba changamoto
na migogoro katika ndoa au utawa hiyipotezi uthamani/thamani ya ndoa au utawa.
Kwaiyo, tunapopata kitu cha thamani, kitu ambacho tulifanya mipango na
kutumia nguvu zote ili tukipate, tusikipoteze rahisi tu hivyo. Tukitunze na mbambwe
zote. 2) Pili, Sisi kama Wakristo, tunalikwa kutambua kwamba ufalme wa mbinguni ni
kitu cha thamani kuliko vitu vyote vya dunia. Tuutafute kwanza ufalme wa mbinguni
kwa gharama yote. Tuwe kwanza Raia wa Ufalme wa Mungu mengine yote tutayapata
kwa ziada.

Basi, Tumuombe Mungu awajalie viongozi wetu wa Serikali na wa Dini na Sisi pia
Hekima maishani mwetu ili tupambanue mema na mabaya, ili tugundue ni kipi cha
thamani maishani mwetu na ni kipi ambacho siyo cha thamani katika maisha.

TUMUSIFU YESU KRISTO!

You might also like