You are on page 1of 84

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA

(TAWLA)

MWONGOZO WA TARATIBU ZA
KISHERIA KATIKA UMILIKI WA ARDHI
Kimechapishwa na:
Tanzania Women Lawyers Association(TAWLA)
S. L. P. 9460, Dar es Salaam - Tanzania
Tel: +255 22 2110758, Fax: + 255 22 2110758.

Barua pepe: tawla.information@gmail.com or info@tawla.or.tz

© Haki zote zimeifadhiwa (2012)

ISBN: 978–9987– 9489–4–9

Kimesanifiwa na kuchapwa na:


Martisayi Investments Company Limited
YALIYOMO

SHUKRANI..................................................................................................i
MUHTASARI..............................................................................................ii
ANGALIZO................................................................................................iii
KUHUSU TAWLA...................................................................................... iv

SURA YA KWANZA:............................................................................... 1
HISTORIA, UMILIKI NA MATUMIZI YA ARDHI TANZANIA.............1

SURA YA PILI: ..................................................................................... 11


SHERIA YA ARDHI NA. 4 YA 1999.........................................................11

SURA YA TATU:.................................................................................... 24
SHERIA YA ARDHI YA KIJIJI NA.5 YA 1999.........................................24

SURA YA NNE:..................................................................................... 31
SHERIA YA FEDHA NA REHANI...........................................................31

SURA YA TANO:................................................................................... 36
SHERIA YA UMILIKI WA VIPANDE......................................................36

SURA YA SITA:..................................................................................... 42
SHERIA NYINGINEZO ZINAZOHUSIANA NA UMILIKAJI WA ARDHI
..................................................................................................................... 42

SURA YA SABA:.................................................................................... 57
UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI................................................57

SURA YA NANE: .................................................................................. 68


ULINZI WA MWANAMKE DHIDI YA VIPENGELE VYA
KUBAGULIWA.........................................................................................68
Tanzania women Lawyers Association

SHUKRANI
Mwongozo huu unalenga kuelezea malengo na mikakati ya TAWLA
ambayo moja wapo ni kuhakikisha haki za wanawake zinazingatiwa
na zinalindwa. Muongozo huu unalengo la kuwaelimisha na
kuwapa ufahamu wanawake juu ya sheria na haki zao katika
masuala mbalimbali yanayohusiana na ardhi. TAWLA inapenda
kutoa shukrani zake za dhati kwa watu wafuatao waliochangia kwa
kiasi kikubwa uandaaji wa mwongozo huu.

TAWLA inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Latifa A. Mwabondo


na Naseku Kisambu, maafisa mradi kitengo cha ardhi kwa mchango
waO tangu mwanzo wa kuandaa mwongozo huu hadi mwisho
wake.

Pia tawla inatoa shukrani kwa Ashura Mnzava, Yussuf Aboud,


Julius Titus, Khadija Tekka, Esther Phabian na Staille Kiko kwa
mawazo na mchango wao wa kuandaa na kurekebisha mwongozo
huu ili uwe katika mpangilio mzuri. Pia tawla inashukuru Athanasia
Soka, Grace Kazoba wajumbe wa kikosi kazi cha ardhi tawla,
Charles Mnzava mwenyekiti baraza la nyumba na ardhi wilaya
ya kinondoni kwa mchango wao katika kufanyia marekebisho
mwongozo huu.

Pia tunawashukuru kwa dhati viongozi wa TAWLA kwa mchango


wao mkubwa katika kufanikisha malengo yote ya chama.

Shukrani zetu za pekee na za dhati ziwaendee wafadhili wa


mwongozo huu kwa mchango wao wa hali na mali.

TIKE MWAMBIPILE

Mkurugenzi

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi i


Tanzania women Lawyers Association

MUHTASARI
Mwongozo huu umeandaliwa na TAWLA kusaidia katika kuelewa
sheria na taratibu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi
kwa wanawake Tanzania.

Mwongozo huu unaelezea sheria na taratibu za kufuatwa katika


kumiliki kutumia ardhi kwa wanawake na utatuzi wa migogoro
inayohusiana na ardhi.

TAWLA inatambua kwamba mwongozo huu utasaidia wanawake


wa Tanzania kuweza kuelewa na kujua haki zao za msingi katika
kumiliki, kutumia na kutatua migogoro ya ardhi kwa mujibu wa
sheria mbali mbali za ardhi,

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitasaidia watu wa jinsia


zote katika maeneo yaliyoko ndani ya Tanzania.

Tawla inatumaini ya kwamba wanawake, na umma kwa ujumla,


watapata na kutumia mwongozo huu rahisi, kutafuta haki zao kwa
njia ya mfumo rasmi wa sheria

ii Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

ANGALIZO
ILANI
Mwongozo huu umeandaliwa na TAWLA kwa lengo la kusaidia
watanzania wote kupata ufahamu wa kuweza kujua na kufahamu
taratibu mbali mbali za kufuata katika kumiliki kutumia na kutatua
migogoro ya ardhi katika vyombo mbali mbali.

Mwongozo huu unatoa mafunzo tu na hauwezi kutumika kama


sheria au kidhibiti mahali popote.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi iii


Tanzania women Lawyers Association

KUHUSU TAWLA
TAWLA ni shirika lisilokuwa la kiserikali, lililoanzishwa mwaka
1990 chini ya sheria ya vyama na moja ya kazi zake ni kutetea na
kulinda haki za binadamu hasa hasa wanawake.

Uachama wa Tawla ni wa wazi kwa wanasheria Wanawake. TAWLA


in wanachama wasiopungua 470. Makao Makuu ya TAWLA yapo
jijini Dar Es Salaam na matawi mengine katika mioa ya Arusha,
Dodoma na Tanga.

TAWLA imegawanyika katika idara kuu tatu kama ifuatavyo:

Msaada wa kisheria , utafiti na matangazo na idara ya utawala


bora, TAWLA inatekeleza mikakati ya maradi katika mstari wa dira,
dhamira na malengo.

iv Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

DHAMIRA YA TAWLA.
Ujumbe na dhamira ya TAWLA ni kuwa na nia ya kuendeleza
wanachama wake kitaalamu na pia kukuza haki na usalama bora
kwa wanawake na watoto.

MAONO YA TAWLA
Maono ya TAWLA ni kulenga jamii yenye kuheshimu haki za
binadamu na kuzilinda.

Maadili ya msingi ya TAWLA ya miaka mitano ijayo


ambayo ni:
• Kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wanawake na
watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
• Kutetea haki za ardhi kwa ajili ya wanawake na watoto
• Kuongeza ufahamu juu ya masuala ya ajira ya watoto na
kushughulikia mahabusu ya watoto.
• Kampeni ya utawala bora
• Kufanya utafiti wa sera na utetezi juu ya marekebisho ya sheria
• Kuimarisha uwezo na uendelevu wa shirika
Kufanikisha matokeo ya hapo juu, shirika limeanzisha mwongozo
huu kam njia mojawapo ya kutekeleza mikakati mbalimbali.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi v


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Kwanza
HISTORIA, UMILIKI NA MATUMIZI
YA ARDHI TANZANIA

UTANGULIZI
Sehemu hii inaangalia mfumo wa umilikaji ardhi na haki ya
mwanamke kwenye maswala ya ardhi. Inaangalia dhana nzima ya
mabadiliko ya sheria za ardhi hapa Tanzania na jinsi mabadiliko
hayo yanavyomlinda mwanamke. Kwa hiyo sehemu hii pamoja
na mambo mengine inajaribu kuchanganua mapungufu yaliyo
sababisha mabadiliko ya sheria za ardhi pamoja na dondoo muhimu
kwenye sheria za ardhi. Inajaribu pia kufanya mlinganisho wa
masuala yanayowagusa wanawake kwenye ardhi pamoja na jinsi
masuala hayo yanavyo elezewa kwenye sheria za ardhi. Sehemu hii
haiangalii tu jinsi sheria za ardhi zinavyolinda haki za mwanamke
kwenye ardhi bali inaangalia pia jinsi baadhi ya vipengele
vinavyoweza kutafsiriwa ili kulinda haki ya mwanamke katika
masuala ya ardhi.

Wigo wa Umiliki wa Ardhi


Mtu anapo jaribu kuangalia suala la haki ya ardhi nchini Tanzania
anakumbana na maswali kadhaa ya msingi yanayohusu mfumo
wa umiliki na kanuni zinazosimamia umiliki huo. Umilikaji wa
ardhi, nyumba na mali nyingine una faida za moja kwa moja na
ambazo si za moja kwa moja. Hii ni pamoja na mahali pa kuishi
panapotambulika kisheria na namna ya kumudu maisha. Haki
ya ardhi inajikita kwenye kiini cha maisha ya kijamii, kisiasa na
kiuchumi katika nchi nyingi kama chanzo cha msingi cha mali,
hadhi ya kijamii, na uwezo, kwasababu inasaidia upatikanaji wa
mahali pa kujihifadhi/ makazi, chakula na shughuli mbalimbali za
kiuchumi.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 1


Tanzania women Lawyers Association

Kimsingi, haki ya ardhi inaweza kuangaliwa katika mtazamo


wa umiliki wa ardhi. Umiliki katika mfumo wa sheria za Kirumi
unamaanisha kifurushi cha haki kadhaa za kumiliki, kutumia,
kuharibu au kuhawilisha. Hizi sifa zinakuwa dhahiri katika mfumo
wa umiliki kamilifu au usio na ukomo ambapo mwenye ardhi
anaishikilia bila ukomo. Chini ya mfumo wa hati miliki, haki izi
tunazoziona kwenye mfumo wa umiliki usio na ukomo zinaminywa.
Kwa mfano, mwenye ardhi anakuwa na haki ya kuimiliki kwa
kipindi cha muda aliopewa tu. Ikiwa muda utaisha itabidi aombe
kuongezewa muda. Wakati mwingine maombi ya kuongezewa
muda yanategemeana na ridhaa ya mwenye mamlaka ya kusimamia
ugawaji wa ardhi. Hivyo basi, kitu cha muhimu kwenye mfumo wa
hati miliki ni ulinzi wa kutumia na ulinzi wa kumiliki hiyo ardhi
kwa kipindi husika.

UTUNGAJI WA SHERIA ZA ARDHI


Mchakato wa kupata sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji
ya Mwaka za 1999 ulianza tangu mwaka 1992. Wakati huo Tume
ya Rais ya kuchunguza migogoro ya Ardhi (Shivji Commission
(The Presidential Commission of Inquiry into Land Matters)
iliundwa. Kwa mujibu wa mwandishi Tsikata, serikali iliandaa
warsha ya kitaifa juu ya Sera ya Ardhi ambayo ilifanyika Arusha
mnamo Januari 1995. Kambi ya wataalamu ya Tropical Research
and Development, Inc, kwa msaada wa fedha kutoka Benki ya
Dunia ilipewa kazi ya kuandaa ripoti ya kitaalamu kutokana na
serikali kutokuafiki mapendekezo ya Tume ya Shivji hasa juu ya
kuondoa mamlaka ya Rais kwenye kusimamia ardhi. Taarifa hiyo
ya kitaalamu pamoja na Ripoti ya Tume ya Shivji vilikuwa msingi
wa uundwaji wa Sera ya Taifa ya Ardhi (1995). Kazi ya kutengeneza
sheria ilitolewa kwa Kampuni ya Uingereza iliyoko chini ya taasisi
ijulikanayo kama Department of International Development (DFID)
au idara ya maendeleo ya kimataifa kwa lugha ya Kiswahili. Profesa
Patrick McAuslan alipewa jukumu la kuandaa rasimu ya sheria
,.hiyo mwaka 1999 . Rasimu ya sheria hiyo ilijadiliwa na kupitishwa
Bungeni kama sheria mbili tofauti yaani Sheria ya Ardhi (1999,

2 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Sheria Na. 4) inayosimamia ardhi isiyo ya kijiji na Sheria ya Ardhi


ya Kijiji (1999, Sheria Na. 5), inayosimamia ardhi iliyoko vijijini.

Sheria hizi yaani sheria ya ardhi ya kijiji na sheria ya ardhi ya jumla


zilianza kutumika rasmi mwaka 2001 na zimeshatimiza miaka
zaidi ya kumi sasa. Kabla ya kutungwa kwa Sheria za Ardhi za
mwaka1999 mapungufu kadhaa yalikua dhahiri. Mapungufu hayo
yalichochea jitihada za makundi mbalimbali kutaka mabadiliko.
Hata hivyo jitihada hizo zililenga zaidi mapendekezo ya Tume ya
Shivji. Mathalani, dhana ya ardhi kuwa chini ya Rais ilionekana
kutia dosari uhakika wa ulinzi wa umiliki ambao mmiliki wa ardhi
anakuwa nao kutokana na matukio ya ukwapuzi wa ardhi na hata
kuondolewa kwenye makazi kinyume cha taratibu. Mamlaka hiyo
ilizidisha nguvu, mamlaka ya serikali na maamuzi juu ya maswala
ya ardhi. Nguvu ya usimamizi, ugawaji na uhawilishaji wa ardhi
ulitawaliwa na mamalaka ya serikali. Si hilo tu bali, mwendelezo
wa urasimu kwenye ugawaji, matumizi na uendelezaji wa ardhi
ulionekana kuwa changamoto kubwa kwa watanzania wengi. Pia,
kulikuwa na ukosefu wa uwazi, uangalizi na uwajibikaji kwa umma,
matumizi mabaya ya madaraka, na ubadhilifu kwenye maswala ya
ardhi.

Pamoja na haki ya kikatiba ya kumiliki mali, usawa na uhuru


dhidi ya ubaguzi, bado vitendo vya ubaguzi na kutokuwepo
usawa hasa kwa makundi yaliyo katika makundi maalum kama
wanawake, jamii za wawindaji, wafugaji, na wakulima wadogo
wadogo viliendelea. Kwa mfano, jinsi ya kike hasa katika jamii za
wakulima na wafugaji zilikosa umiliki na nguvu ya kisheria juu ya
usimamizi wa ardhi. Wanawake walinyang’anywa haki ya kumiliki
na kusimamia mchakato wa uzalishaji na uratibu wa matunda
yatokanayo na uzalishaji huo. Wanaume waliweza kuuza ardhi na/
au kuitumia wapendavyo bila kushirikisha wake zao. Kulikuwa
hakuna ushiriki wa usawa kati ya wanaume na wanawake kwenye
maamuzi ya ardhi. Pia kulikosekana usawa na ushirikishwaji makini
wa wanawake kwenye usuluhishi wa migogoro.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 3


Tanzania women Lawyers Association

Sheria za Nchi Kuhusu Mwanamke na Ardhi


Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(1977), kila mtu ana haki ya kumiliki mali. Kutokana na kutungwa
kwa sheria za ardhi, sheria ya ardhi na sheria ardhi ya kijiji, haki
ya kumiliki ardhi imeongezewa nguvu. Sheria hizi zinaondoa
na kubatilisha mila na desturi zinazoathiri haki ya mwanamke
kumiliki ardhi. Sheria zimetambua usawa kati ya mwanamke na
mwanamume kumiliki mali (ardhi) kwa kugawiwa au kupata,
kutumia, kurithi na kuuza.

Sheria hizi pia zinamlinda mwanamke dhidi ya ubaguzi wa kimila


au desturi za kimila zinazominya fursa halali na ya kisheria ya
mwanamke kumiliki, kutumia na kukalia rasilimali-ardhi. Pia sheria
ya ardhi ya kijiji unatoa fursa kwa mwanamke na mwanamume
kuomba haki ya kimila ya kumiliki ardhi (customary right of
occupancy) na uwakilishi katika baraza la ardhi la kijiji na kamati ya
usuluhishi ya migogoro ya ardhi ya kijiji.

Ulinzi wa Haki ya Mwanamke kwa Mujibu wa Kanuni Kuu


za Ardhi
Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Kanuni kuu za Sera ya Ardhi ndizo
zinazounda malengo ya Sheria ya Ardhi. Katika kutafsiri sheria za
Ardhi lazima kutilia mkazo Misingi Mikuu ya ardhi.

Katika Sheria ya Ardhi mahakama zina wajibu wa kuhakikisha


kwamba zinapotafsiri vifungu au kutumia Sheria ya Ardhi ikiwa
ni pamoja na sheria nyingine zote zinazohusiana au kugusa ardhi
lazima zitilie mkazo na kuongozwa mara zote na Kanuni Kuu za
Sera ya Ardhi. Pia sheria hii inaainisha kuwa watu wote wenye
mamlaka chini ya Sheria ya Ardhi, lazima watilie mkazo Kanuni
Kuu za Sera ya Ardhi wanapotumia au kutafsiri Sheria ya Ardhi.

MISINGI MIKUU YA ARDHI


Misingi hii iliandaliwa mwaka 1995, nayo ni kama ifuatayo.

4 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

1) ardhi yote kuwa mali ya umma


Mojawapo ya kanuni hizo ni ile inayotambua ardhi yote kuwa
mali ya umma. Ardhi ya umma imewekwa chini ya usimamizi
wa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi wote.

ANGALIZO: Ijulikane kwamba kinachozungumzwa


hapa ni usimamizi na sio umiliki. Hivyo Rais sio mmiliki
wa ardhi ya Tanzania bali msimamizi tena kwa manufaa
ya kijamii na kiuchumi ya wananchi wote wa Tanzania.

Rais pamoja na wale waliokaimishwa madaraka chini ya


Sheria ya Ardhi wanapaswa kutekeleza wajibu wao kama
wadhamini kwa manufaa ya watanzania. Ni lazima waweke
mbele maslahi ya kiuchumi na kijamii ya watanzania. Wana
wajibu wa kuhakikisha ardhi inasimamiwa kwa umakini kwa
faida ya wananchi wa Tanzania. Kwa mujibu wa falsafa ya
sheria matendo ya Rais na watendaji wake lazima yawe kwa
manufaa ya wananchi wa Tanzania. Kwa kuwa nguvu ya Rais
ni ya usimamizina mamlaka ya juu kwenye usimamizi wa ardhi
yako kwa wananchi. Ridhaa ya wananchi lazima itafutwe na
ipatikane kupitia mifumo shirikishi. wananchi kwenye ardhi
wana haki ya kushirikishwa, kutoa maoni yao, kusikilizwa,
kuhoji maamuzi yasiyo na manufaa kwao au yasiyozingatia
maslahi na maoni yao.
2) Ulinzi wa haki tangulizi kwenye ardhi.
Haki tangulizi ni haki zilizokuwepo kwenye ardhi au zilizokuwa
zinawanufaisha watu kabla ya kubatilishwa kwa haki miliki
au kuchukuliwa au kuingiliwa kwa eneo la ardhi. Haki hizi
tangulizi zinategemeana na asili au aina ya umiliki.Haki hizi
zinapaswa kutambuliwa na kulindwa kisheria. Hii ina maana
kwamba pale ambapo umiliki ulikuwa ni wa kimila, haki
hizo zitakuwa na asili ya kimila pia na kama umiliki ulikuwa
wa sheria za kutungwa basi haki hizo zitatokana na umiliki
huo. Haki au maslahi yenye asili ya kimila zinapaswa kuwa
zile ambazo pasipo hizo mmiliki atakuwa amenyang’anywa
namna yake ya kujitosheleza kimahitaji. Baadhi ya haki au

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 5


Tanzania women Lawyers Association

maslahi yanayotokana na kutumia na kukalia ardhi ni pamoja


na kilimo cha msimu, kulisha mifugo, kuchota maji, kupata
kuni, kukusanya matunda na nyasi kwa ajili ya kufuma
vikapu/mikeka, udongo mfinyanzi kutengenezea vyungu;
kuwinda kwa ajili ya kitoweo, malazi, maendelezo kama
mimea na nyumba, majengo, na haki ya njia, haki ya kuendea
maji nk. Ni kanuni hizo zinazo hakikisha ustawi wa mtu.
Bila haki hiyo kunaweza kuwepo usumbufu kwa jamii iliyo
athirika hasa wanawake na watoto.
3) Kupata fidia halali na kwa wakati.
Msingi wa kanuni/haki hii ni uthibitisho wa uzito wa haki
ya mtu kumiliki mali (ardhi) ambayo imetambuliwa katika
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977). Haki hii
inatokana na ukweli kwamba pale mtu anapotumia nguvu
kazi yake kupata mali yoyote, anayetaka kuichukua lazima
amlipe. Hitaji hili la kulipwa fidia haliwafungi watu tu bali
hata serikali. Kile kinacholindwa na kanuni hii ni jitihada,
nguvu kazi, na rasilimali nyingine alizowekeza kwa kupata
hiyo ardhi au kwa kuongeza thamani yake.
Kilichoko katika kanuni hii ni haki ya wananchi kushiriki
faida au matunda yatokanayo na uwekezaji katika eneo
lao, hasa uwekezaji ulioathiri maeneo hayo. Dhana ya
kushirikishana faida inachukuliwa kuwa haki inayotokana
na haki ya kulipwa fidia. Haki ya fidia haiishii tu kwenye
kufidia ardhi aliyochukuliwa/ kunyang’anywa bali pia
kunyang’anywa haki ya matumizi ya kawaida ya hiyo ardhi.
Fidia halali inatafsiriwa kuwa haki ya jamii kunufaika na
faida zinazopatikana kutokana na fursa za wananchi zilizo
minywa au kunyang’anywa kufurahia au kutumia kwa uhuru
maeneo ya asili na rasilimali zilizopo kwa manufaa yao.
Kanuni hii inaweza kutumiwa kuhakikisha haki ya ardhi ya
mwanamke inazingatiwa pale ardhi ya mtu, familia au jamii
inapochukuliwa.
Hivyo basi fidia inahusiana moja kwa moja na kanuni nyingine
ya haki ya umma kushirikishwa katika maamuzi. Mchakato
au zoezi la fidia lazima lihusishe ushirikishwaji wa umma /

6 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

wananchi wakati wa kuandaa mipango, kutathmini fidia na


utoaji wa fidia pia. Ushirikishwaji katika usimamizi wa ardhi
ni muhimu katika kutia nguvu dhana ya uongozi /utawala
bora katika usimamizi wa ardhi.
4) Haki ya wanawake ya kushirikishwa
Ikumbukwe kwamba kushirikishwa ni haki ya wananchi
na ni wajibu kwa watendaji na sio hisani. Haki hii inaweza
kuhakikishwa pale ambapo kunakuwepo na ushirikishwaji
makini wa wananchi, utoaji wa taarifa na mawasiliano ya mara
kwa mara. Sio tu, kwamba inatakiwa wananchi washirikishwe
bali kushirikishwa lazima kuwe kwa nia njema kwa kufuata
taratibu zilizowekwa.
Kuhusiana na kanuni hii inashauriwa ushirikishwaji ufanyike
katika hatua za mwanzo za mradi au mpango wa uwekezaji na
sio tu pale inapohitajika kupata ridhaa ya wananchi ili mradi
uanze.
Endapo kuna athari (risks) zozote lazima ziainishwe na
wananchi wajulishwe ikiwa ni pamoja na athari za kimazingira
na kiafya za mradi unaokusudiwa ukubaliwe kwa kujua na
kwa hiari. Ushirikishwaji unapaswa kuwa zana ya kupata
ridhaa yenye kutokana na uelewa/ ufahamu wa hiari ya awali
kabla ya mradi kufika kwa wananchi. Ni kutokana na msingi
huo ushirikishwaji wa viongozi wachache ulichukuliwa kuwa
sio ushirikishwaji wa wananchi .
Vilevile, vipo vifungu vinavyoelezea dhana hii ya
ushirikishwaji wa wananchi kwenye maamuzi yanayohusu
ardhi kwenye Sheria ya Ardhi ya Kijiji. Vifungu hivi pia
vinalenga kuhakikisha ushiriki wa wanawake kwenye
maamuzi katika ngazi ya kijiji kama sheria ya ardhi ya vijiji
inavyosema. Baraza la ardhi la kijiji ambalo linafanya kazi ya
usuluhishi wa migogoro katika ngazi ya kijiji linatakiwa kuwa
na angalau wajumbe watatu wanawake kati ya wajumbe
saba wa baraza. Hata katika mchakato wa kuendesha kikao
ni lazima idadi ya wanawake isipungue wawili vinginevyo
lazima kikao kiahirishwe. Idadi hii inalenga kupunguza

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 7


Tanzania women Lawyers Association

mfumo dume katika maamuzi yanayohusu maswala ya


ardhi kwa wanawake. Hata hivyo, kusudio hili linaathiriwa
na baadhi ya wanawake kuwa wamepoteza imani na
mabaraza au wametingwa na majukumu ya kifamilia kwa
hiyo kuogopa kupoteza muda mwingi kusuluhisha migogoro
kwenye mabaraza haya kwani kwa kiasi kikubwa hawashiriki
ipasavyo. Matokeo yake kumekuwepo na changamoto kama
mapambano yakuhakikisha ushiriki wa wanawake kwenye
usuluhishi wa migogoro umekuwa wa tija au la.
5) Haki sawa kati ya wanawake na wanaume katika
kumiliki ardhi.
Msingi huu unatambua kwamba haki ya haki ya mwanamke
kupata, kushikilia, kutumia ardhi inapaswa kuchukuliwa
kama haki ya mwanaume na iko chini ya vigezo vile vile
vinavyotumika kwa wanaume. Hii inalenga kuongeza na
kuhakikisha haki ya wanawake katika kupata ardhi na ulinzi
wa kisheria katika kumiliki ardhi. Matokeo yake mfumo wa
kisheria unamuwezesha mwanamke kupata ardhi mwenyewe
sio tu kwa kununua ila pia kugawiwa na kurithi. Chini ya
Sheria ya Ardhi ya Kijiji, haki hii inamruhusu mwanamke aliye
talakishwa kugawiwa ardhi na serikali ya kijiji. Kipengele hiki
vilevile ni muhimu hasa kuhusiana na uthabiti wa ulinzi wa
haki ya kumiliki mali. Kwa kuangalia sifa za haki ya kimila
ya kumiliki ardhi, sheria inaainisha kwamba haki ya kimila
inaweza kurithiwa na kurithishwa kupitia taratibu za wosia
na mirathi.

ANGALIZO: Mila au desturi zozote inayokwenda


kinyume na kanuni hii ya usawa wa kijinsia ni kinyume
cha sheria na maamuzi yoyote yatakayofikiwa chini ya
mila hiyo au desturi hiyo ni batili.

Hii ni pamoja na maamuzi yoyote yanayopendelea wanaume


kuliko wanawake kuhusu maswala ya ardhi. Chini ya kanuni
hii pia mahakama na vyombo vyote vya maamuzi vinatakiwa
kuhakikisha kwamba maamuzi yanazingatia jinsia na yako

8 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

huru dhidi ya upendeleo kwa wanaume. Kipimo hicho


kinachotumika kwa wanaume kinapaswa pia kutumika kwa
wanawake. Msimamo huu wa kisheria wa usawa wa kijinsia
umeainishwa pia kwenye Sera ya Taifa ya Ardhi (1995) kwa
kutambua ukweli kwamba maamuzi ya ardhi hasa katika
ngazi za chini huamuliwa kwa kuzingatia mila na desturi za
makabila yetu!
6) Haki za asili (natural justice)
Hivyo basi, kama ilivyoainishwa kwenye Sera ya Ardhi
maswala ya kurithi ardhi ya ukoo yataendelea kusimamiwa
na sheria na desturi za kimila endapo hazikinzani na Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia haipingani na
kanuni za Haki Asili. Sambamba na misingi ya Sera ya Ardhi,
Sheria ya Ardhi ya Kijiji inatamka kwamba sheria za kimila
zitatumika kushughulikia haki za ardhi za kimila. Sehemu ya
kifungu husika inasema “sheria yoyote ya kimila au maamuzi
yaliyofikiwa kwenye umiliki wa kimila…lazima kuzingatia
mila, desturi, na mazoea ya jamii husika…” Angalizo pekee
ni kwamba sheria au mila hizo zisikinzane na sheria nyingine
zilizo andikwa ikiwa ni pamoja na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Kwa hiyo sheria yoyote ya kimila itakuwa batili na isiyo na
nguvu ya kisheria au kutekelezeka kama inanyima wanawake,
watoto au mtu yeyote mwenye ulemavu haki-sheria ya kupata,
kumiliki, kukalia, na kutumia ardhi.
7) Haki zote zilio katika ardhi na umilikaji wa ardhi kwa muda
mrefu unatambuliwa unafafanuliwa na kulindwa na sheria.
8) Kudhibiti kiasi cha ardhi ambacho mtu mmoja au taasisi
yaweza kumiliki na kutumia ardhi.
9) Kuzingatia kwamba maslahi yoyote katika ardhi yana thamani,
kana kwamba thamani hiyo inazingatiwa wakati wowote
katika mapatano yoyote yanayoathiri maslahi hayo.
10) Kuweka mfumo madhubuti, rahisi na wazi wa kusimamia
kwa ufanisi masuala ya ardhi.
11) Kuwezesha uendeshaji wa soko la ardhi.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 9


Tanzania women Lawyers Association

12) Kudhibiti uendeshaji wa soko za ardhi kwa madhumuni ya


kuhakikisha kuwa wakulima wadogo vijijini au mjini pamoja
na wafugaji hawawekwi katika hali ngumu ya kuwasababishia
hasara.
13) Kuweka kanuni za sheria ya ardhi ambazo zinapatikana kwa
urahisi na zinoeleweka kwa raia wote.
14) Kuanzisha mfumo ulio huru, unaofanya kazi kwa haraka
na wa haki kwa ajili ya kuamua migogoro ya ardhi, ambao
utasililiza na kuamua migogoro ya ardhi bila ya ucheleweshaji
usio wa lazima.
15) Kuhimiza usambazaji wa taarifa za usimamizi wa ardhi na
sheria ya ardhi kama ilivyofafanuliwa na Sheria hii, kwa
kupitia vipindi vya elimu ya uma na kwa watu wazima na
kwa kutumia njia mbalimbali za upashanaji habari.

10 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Pili
SHERIA YA ARDHI NA. 4 YA 1999

A. MGAWANYO WA ARDHI
Sheria hii mpya imeigawa ardhi yote ya Tanzania katika
Makundi matatu. Makundi hayo ni:-
i. ARDHI YA JUMLA
Ardhi ya jumla ni ile ardhi yote ambayo siyo ardhi ya
hifadhi au ardhi ya kijiji lakini ambayo inajumuisha
ardhi ya kijiji ambayo haikaliwi wala haitumiki.
ii. Ardhi ya Vijiji
Ardhi ya vijiji ni ile ambayo iko ndani ya mipaka ya vijiji
na ambayo imesajiliwa kwa kufuata sheria zilizoweka
kama vile sheria ya Serikali za Mitaa ya 1982 na sheria
mpya.
iii. Ardhi ya hifadhi
Ardhi ya hifadhi ni ardhi iliyotengwa kwa madhumuni
maalum. Ardhi ya hifadhi inajumuisha aina zifuatazo
za ardhi:-
• Maeneo ya hifadhi na misitu yanayotambulika
kisheria (sheria ya misitu)
• Mbuga za wanyama pori (sheria ya Hifadhi ya
mbuga za wanyama, sheria ya Hifadhi ya eneo la
Ngorongoro.
• Hifadhi za maji (bahari, mito , mabwawa makubwa
na maziwa n.k)
• Ardhi yenye majimaji (kama ile iliyo pembezoni
mwa mito na madimbwi)
• Hifadhi ya barabara
• Maeneo ya wazi (kama yale yaliyotengwa kwa ajili
ya kupumzikia, burudani, michezo na starehe)

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 11


Tanzania women Lawyers Association

• Maeneo yaliyotangazwa kuwa ni hatari kama


ilivyoelekezwa katika sheria Maeneo ya aina hiyo
ni kama yale ya mabondeni, kwenye miteremko
mikali, kingo za mito, maziwa na bahari, sehemu
zilizotengwa kwa kutupa taka,sehemu za mikoko
na miamba ya baharini

B. USIMAMIZI WA ARDHI CHINI YA SHERIA ZA


ARDHI ZA MWAKA 1999.
Kwa mujibu wa sheria za Ardhi (1999) zipo ngazi mbalimbali
za usimamizi na utekelezaji wa maasuala ya ardhi kama
inavyoonyeshwa hapa chini:-
I. Rais
II. Waziri wa Ardhi
III. Kamishna wa Ardhi
IV. Kamati za ugawaji Ardhi
V. Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi
VI. Halmashauri ya Wilaya
VII. Mkutano Mkuu wa kijiji
VIII. Halmashauri ya Kijiji
Majukumu ya usimamizi wa masuala ya ardhi ngazi ya Taifa
hadi Kijiji ni kama ifuatavyo:-

I. Rais
Rais ni msimamizi mkuu wa utawala wa ardhi lakini
anaweza kumteua mtu ambaye atashughulikia masuala
ya ardhi. Mtu huyo ni Waziri anayeshughulikia ardhi
na chini yake kuna Kamishna wa Ardhi ambaye
ndiye mtendaji na mshauri mkuu katika mambo yote
yanayohusu ardhi. Kwa maana hiyo Rais ana majukumu
yafuatayo;
o Udhamini wa ardhi yote ya Tanzania
o Kumteua waziri wa Ardhi
o Kumteua Kamishna wa Ardhi

12 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

o Kutoa maelekezo kwa waziri juu ya usimamizi na


utekelezaji wa sera na sheria za ardhi kwa ujumla
na pia kutoa maelekezo kwa kamishna kupitia
kwa waziri.
o Kubadili matumizi ya ardhi kutoka kundi moja
hadi jingine (mfano ardhi ya Kijiji kuwa ya hifadhi
na kinyume chake)
II. Waziri wa Ardhi
o Wajibu mkuu wa waziri ni kuunda sera ya ardhi
ya taifa na kusimamia utekelezaji wa sera hiyo.
Pia anatakiwa kusimamia utekelezaji wa sheria
za Ardhi ikiwa ni pamoja na kutamka tarehe ya
kuanza matumizi.
o Ana uwezo wa kuunda kamati za kugawa ardhi
na Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi.
o Kutoa ushauri na miongozo mbalimbali ya
utendaji kazi kwa maofisa wote wa Wizara.
III. Kamishna wa Ardhi
o Ndiye mtendaji na mshauiri mkuu wa serikali
katika masuala yote ya usimamizi na utekelezaji
wa sera na sheria za ardhi.
o Kutoa nyaraka, miongozo na maelekezo
mbalimbali juu ya utekelezaji wa sheria za ardhi.
o Kutayarisha ripoti ya mwaka juu ya utendaji
mzima wa masuala ya ardhi
o Kutunza rejesta inayoonyesha mipaka yote ya
ardhi ya vijiji.
IV. Kamati za Ugawaji wa Ardhi
o Kumshauri Kamishna katika masuala ya umilika
wa ardhi.
V. Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi.
o Kuangalia na kupitia upya masuala ya ardhi na
kumshauri waziri juu ya Sera ya Taifa ya Ardhi

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 13


Tanzania women Lawyers Association

kwa nia ya kutoa mapendekezo na kufanya


mabadiliko inapobidi.
o Kuangalia upya muundo wa kazi, mamlaka na
uongozi na kutoa ushauri kwa waziri kwa ajili ya
kuboresha utekelezaji wa masuala yote ya ardhi
nchini.
o Baraza la Taifa la Ushauri wa ardhi linatakiwa
kuwa na wajumbe wasiopungua saba na
wasiozidi kumi na moja walioteuliwa na waziri,
na Mwenyekiti wake atateuliwa na Rais. Katika
kuteua wajumbe hao sheria imeagiza kuzingatia
uwiano wa kuridhisha kati ya wanaume na
wanawake.
VI. Halmashauri ya Wilaya
o Jukumu kubwa la Halmashauri ya Wilaya ni kutoa
ushauri na mwongozo kwa kila Halmashauri ya
Ardhi ya kijiji iliyopo kwenye eneo la Halmashauri
hiyo juu ya usimamizi na uendeshaji wa kazi zake.
Hata hivyo ushauri na miongozo hiyo haitakiwi
itofautiane au kwenda kinyume na nyaraka au
maelekezo ya Kamishna wa Ardhi.
VII. Mkutano Mkuu wa Kijiji
o Kupitisha maombi juu ya utoaji na ugawaji wa
ardhi ya kijiji.
o Kutoa ushauri na mwongozo wa utendaji kwa
Halmashauri ya kijiji.
o Kuhakikisha kwamba Halmashauri ya kijiji
inatekeleza wajibu wake kwa kufuata sera na
sheria za ardhi nyinginezo zinazohusiana na ardhi
ya kijiji.
VIII. Halmashauri ya Kijiji
o Inawajibika katika masuala yote ya usimamizi,
ugawaji na utunzaji wa mipaka ya ardhi ya Kijiji.
o Inatakiwa kufuata ushauri na kusimamia masuala

14 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

yote ya ardhi ya kijiji kwa kufuata maamuzi na


amri zinazotolewa na uongozi uliopo juu yake.
o Imepewa mamlaka ya kuunda kamati ya
maamuzi ya kijiji na kutoa ushauri, mwongozo na
mapendekezo kwa kamati hiyo juu ya utekelezaji
wa kazi zake.
o Kabla ya kugawa au kutoa ardhi ya kijiji kwa mtu
yeyote ni lazima maombi hayo yapitishwe na
Mkutano Mkuu wa Kijiji.

C. KUMILIKI ARDHI
Nani mwenye haki ya kumiliki ardhi?
Mwenye haki ya kumiliki ardhi ni raia yeyote wa Tanzania.
Anaweza kumiliki ardhi kama mtu binafsi au kikundi cha
watu wawili ama zaidi. Watu wanaweza kumilikishwa ardhi
kwa njia zifuatazo:-
1. Kwa kupatiwa hati ya umilikaji kwa mujibu wa sheria
2. Kwa kuitwaa kwa kufuata taratibu za kimila/au kwa
kuikalia na kuitumia ardhi kwa muda mrefu kama vile
kwa miaka kumi na mbili au zaidi.
3. Kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji kwa lengo la
kutumia ardhi kwa uwekezaji.

MAANA YA UMILIKI WA MTU BINAFSI.


Umiliki huu unahususisha haki ya mtu binafsi kutumia ardhi akiwa
na uhuru wa kufanya maamuzi binafsi bila ya kumuhusisha mtu au
watu wengine. Umiliki wa aina hii unampa mtu uhuru wa kuuza,
kutoa zawadi au kuweka rehani ardhi husika bila kuomba idhini ya
mtu mwingine.

Maana ya umiliki wa pamoja:-


Umiliki huu unahusisha haki ya mtu zaidi ya mmoja kutumia
ardhi kwa pamoja. Umiliki huu haumruhusu mtu binafsi kufanya
maamuzi binafsi bila ya kumuhusisha mwenzake au wenzake.
Maamuzi yatakayofanywa na mtu mmoja bilaya kumuhusisha

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 15


Tanzania women Lawyers Association

mwenzake au wenzake juu ya kuuza, kutoa zawadi au kuweka


rehani ardhi husika yanakuwa batili.

Ieleweke kwamba kila mmilikaji wa pamoja atapewa hati yake


ya umiliki ardhi wa pamoja. Kwa hiyo kila mmiliki wa pamoja
awe mwanamke au mwanaume ahakikishe kuwa anapata hati ya
umiliki. Wanawake wanaomiliki ardhi pamoja na wanaume (kwa
mfano katika ndoa) ahakikishe kwamba wanapata hati ya umiliki
wa pamoja

Umiliki wa pamoja upo wa aina mbili:-


a) Umiliki wa pamoja wa mafungu yasiyogawanyika
b) Umiliki wa pamoja wa mafungu yanayogawanyika.
a) Umiliki wa pamoja wa mafungu usiogawanyika.
o Umiliki huu utawahusu wanandoa tu, wakipnda,
kwa wengine lazima kwanza kipatikane kibali cha
Mahakama.
o Umiliki wa aina hii huandikishwa kwa msajili wa hati ya
umiliki wa ardhi.
o Utoaji wa ardhi ni lazima ufanyike kwa makubaliano ya
wamiliki wote.
o Mmoja wa wamiliki akifa maslahi yake yote yatarithiwa
na mmiliki au wamiliki waliobaki.
b) Umiliki wa ardhi wa pamoja katika mafungu
yanayogawanyika
Umiliki wa pamoja wenye maslahi yanayotambulika kwa hisa
za kila mmilikaji.
o Wamiliki, wanamiliki ardhi yote kwa ujumla
o Utoaji wa ardhi au ubadilishaji wa umiliki hufanyika
kwa kibali cha wamiliki wote
o Pale inapoteokea kifo cha mmili mmojawapo, fungu
lake kurithiwa na warithi wake
o Umiliki huu pia huandikishwa kwa msajili.

16 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

c) Umiliki wa pamoja baina ya Wanandoa


Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 inaeleza kuwa wanandoa
wanaweza kumiliki ardhi katika mafungu yanayogawanyika
au katika mafungu yasiyogawanyika.
Ieleweke pia kwamba kama mwanandoa mmoja anamiliki ardhi
kwa jina lake pekee lakini baadaye mwanandoa mwenzake
akachangia katika kuiendeleza ardhi hiyo, mwanandoa Yule
aliyechangia atakuwa amepata haki ya kumiliki ile ardhi kwa
hisa(share)zisizogawanyika wakichangia umilikaji huo na
yule mwanandoa aliyepewa kwanza haki ya kumiliki ardhi.

ANGALIZO: Utaratibu huu ni mzuri unawahakikishia


wanawake haki yao ya kumiliki ardhi ukilinganisha
na sheria za mirathi za kimila ambazo zinawanyima
wanawake haki yao ya kurithi ardhi ikiwa ni njia
mojawapo ya kupata na kumiliki ardhi.

Hati ya kumiliki Ardhi.


Mwenye uwezo wa kutoa hati ya kumiliki ardhi kwa mujibu wa
sheria ya ardhi ya 1999, ni Kamishna wa Ardhi.

Ieleweke kwamba serikali za mitaa, kwa mujibu wa sheria za ardhi


za 1999, hazina mamlaka ya kutoa au kugawa ardhi kama toleo
(offer),bali kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sheria hizo za ardhi.

Umuhimu wa Hati au Cheti cha kumiliki Ardhi


1. Ukiwa na hati au cheti cha kumiliki ardhi una uhakika wa
usalama wa ardhi yako unayomiliki, nyumba au maendeleo
yoyote uliyoyafanya katika ardhi hiyo.
2. Hati au cheti kinaweza kutumika katika kuomba mkopo benki
ikitumika kama rehani.
3. Hati au cheti kinaweza kutumika kama dhamana Mahakamani,
polisi n.k.
4. Hati au cheti kinasaidia kuhamisha umiliki wa ardh kiuhalalai
na kwa uhakika.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 17


Tanzania women Lawyers Association

Taratibu za kufuata:
Sheria hii inaeleza taratibu zifuatazo:
1. Maombi yawekwe na kuwasilishwa kwenye fomu maalum
inayoambatanishwa na picha ya mwombaji. Maombi hayo
yawasilishwe wilayani ama wizarani kwa kadri ya sheria na
taratibu zinavyoelekeza.
2. Maombi yaambatanishwe na ada kama inavyoelezwa kwenye
sheria.
3. Fomu isainiwe na mwombaji, mwakilishi au wakala wa
mwombaji.
4. Maombi yaeleze ama yaambatanishe taarifa inaotakiwa
ambayo kamishna ataiomba kwa maandishi.
5. Maombi yaambatanishwe na tamko la mali nyingine
zinazohusiana na ardhi anazomiliki mwombaji kwa wakati
huo.
6. Endapo sheria inahitaji idhini ya mamlaka ya serikali ya
mahali ama mamlaka ya chombo chochote kabla ya kutoa
idhini ya kumiliki ardhi, hatua hizo zifanyike na nyaraka hizo
zisainiwe na mamlaka husika. Mfano kama mashirika ya dini
yatatakiwa kuidhinishwa na kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali.
7. Kama ombi ni la mgeni ama kampuni ya kigeni liambatanishwe
na cheti cha kuidhininishwa na kitengo cha mwekezaji
kulingana na sheria ya uwekezaji ya 1997 au nyaraka nyingine
zitakazohitajika.
8. Kama ombi ni la mgeni ama kampuni ya kigeni na linahusu
haki ya miliki ya makazi, matumizi ya ardhi yalingane na yale
yaliyoidhinishwa na sheria ya uwekezaji.
9. Baada ya kupokea nyaraka na maelezo yote yanayohitajika,
Kamishna ataanza kushughulikia ombi la haki miliki kwa
kufuata sheria inavyoagiza. Hatua ya kwanza ni kusajili ombi
hilo katika kitabu cha usajili wa maombi ya ardhi. Hii inasaidia
kuondoa usumbufu kwa umma kwa visingizio mbalimbali.

18 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Mwananchi yeyote anayo nafasi ya kupeleka malalamiko kwa


Kamishna kabla kamishna hajatoa uamuzi kwa kutoa hati miliki
mfano mwanaume akituma maoni kwa kumgandamiza mwanamke;
basi mwanamke ataweza kupeleka malalamiko yake kwa kamishna
ili mwanaume anyimwe hati hiyo.

Baada ya kamishna kuridhika na mombi ya haki ya kumiliki ardhi,


ataandaa fomu ya ahadi kwa maandishi ikiwa katika fomu maalum.

Fomu ya ahadi (offer)


Fomu ya ahadi ni taarifa ya maandishi inayotolewa na Kamishna
kwenda kwa mwombaji ikieleza kuwa ombi lake limekubaliwa na
kueleza nini cha kufanya kama inayYoelezwa hapa chini.
Fomu ya ahadi ina mambo yafuatavyo.
1. Ina maelezo ya yote ya umilikaji.
2. Imesainiwa na Kamishna ama ofisa aliye na mamlaka,na
inaonesha tarehe ambayo hati iliandikwa.
3. Imepigwa muhuri wa ofisi ya ardhi mahali ardhi ilipo.
4. Iwasilishwe ama itumwe kwa mwombaji kwa njia
zinazoaminika.
5. Inaeleza matumizi ya ardhi
6. Muda wa kuanza na kumaliza kumiliki.
7. Malipo ya ada na kodi zote husika na jinsi ya kuzilipa, kwa
mfano kama ni kwa awamu au mafungu n.k
8. Ukubwa wa eneo la ardhi inayozungumziwa katika fomu ya
ahadi ikieleza nambari ya kiwanja/shamba, kitalu na mahali
yaani mji au mtaa ama kijiji.
Hata hivyo katika mazingira fulani fulani kamishna anaweza
kuifuta fomu ya ahadi na kumlipa mwombaji fidia ya gharama
zilizotokana na kufutwa kwa fomu hiyo. Vinginevyo,gharama
hizo hazitarejeshwa endapo kamishna atampatia mwombaji fomu
nyingine ya ahadi kwa ajili ya kiwanja kingine ambacho kwa
kadri inavyowezekana kinafanana na kile cha kwanza. Jambo hili
linapaswa kufanyika ndani ya kipindi cha siku kumi na nne (14).

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 19


Tanzania women Lawyers Association

Kwa mujibu wa sheria, malipo yaliyokwishalipwa yatahamishiwa


katika ardhi nyingine anayopatiwa.

Kukubali fomu ya ahadi (offer)


Hatua inayofuata ni kukubali fomu ya ahadi ambapo mwombaji
anapopokea fomu hiyo anapaswa;
1. Kuikubali kwa maandishi na kulipa ada zote zinazotakiwa
kwa kutumia fomu maalum.
2. Fomu iambatanishwe na nakala za stakabadhi za malipo/ ada
yaliyoelezwa.
3. Fomu isainiwe na mwombaji au mwakilishi anayekubalika
ama wakala wake
4. Pia kulingana na taratibu zilizopo mwombaji anapaswa
kuwasilisha picha zake nne za siku za karibu na zinazofanana.

ieleweke wazi kuwa hatua muhimu katika kuikubali fomu


ya ahadi ni kulipa ada na kodi zilizotajwa,na hii inapaswa
kufanyika ndani ya siku thelathini (30) toka tarehe
ilipotolewa fomu ya ahadi.

Ada zinazozungumziwa hapa ni ada ya:-


1. Utayarishaji wa hati ya kumiliki ardhi
2. Usajili wa hati ya kumiliki ardhi
3. Upimaji iwapo kiwanja au shamba limepimwa na idara ya
upimaji ya serikali
4. Hati ya ramani ya sehemu lilipo shamba au kiwanja
5. Ushuru wa serikali
6. Kodi ya kiwanja au shamba
7. Fedha ya tahadhari (premium) inapolazimu
Malipo yote yaambatanishwe na stakabadhi.

20 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Upatikanaji wa hati ya kumiliki ardhi


Kamishna anaweza kutoa hati ya kumiliki ardhi kwa:
o Mwombaji aliyekubali fomu ya ahadi na kufanya malipo ya
awali, kama alivyoelekezwa kwenye fomu ya ahadi au kama
kamishna atakavyokuwa anaelekeza mara kwa mara,
o Anayeendelea kutumia ardhi husika,
o Anayestahili kupata hati miliki kulingana na sheria.

Usajili wa Hati ya Miliki ya Ardhi.


o Usajili hufanyika baada ya maandalizi yote ya utayarishaji wa
hati kukamilika ikiwa ni pamoja na mmiliki kuweka sahihi
yake mbele ya shahidi anayekubalika kisheria, kwa mfano
Wakili, Hakimu ama (Muhuri maalum/muhuri wa moto) ya
serikali. Hati ya kumiliki ardhi huweza kusajiliwa na Msajili
wa hati hizo kabla ya kumkabidhi mhusika nakala yake.
o Baada ya usajili wa Hati ya kumiliki ardhi kukamilika katika
ofisi ya Msajili wa Hati, mmiliki atakabidhiwa nakala yake.
Idadi ya nakala za hati miliki na hati ya ramani hutayarishwa
kulingana na mahitaji ya usajili.

MASHARTI YA MATUMIZI NA MABADILIKO YA


HATI YA KUMILIKI ARDHI.
Masharti ya Hati ya kumiliki ardhi.
Sheria inampa Waziri wa Ardhi uwezo wa kumtaka mtu yeyote
mwenye hati ya kumiliki ardhi kulipa fedha ya tahadhari. Malipo
ya tahadhari yatalipwa mara moja ama kwa awamu kama
itakavyoelekezwa na Waziri.
Kiwango cha fedha ya tahadhari kitakachoelekezwa kitapangwa na
waziri kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1. Matumizi ya ardhi yaliyoruhusiwa
2. Thamani ya ardhi inayotokana na ada ya mauzo au upangishaji
n.k kama ilivyoelekezwa na sheria.
3. Thamani ya ardhi kama inavyooneshwa na bei iliyopatikana
katika mnada uliofanywa na /au kwa niaba ya serikali

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 21


Tanzania women Lawyers Association

4. Thamani ya ardhi ilithibitika katika zabuni ambapo bei ya juu


iliyotajwa ndiyo inathaminisha ardhi hiyo.
5. Maendeleo yaliyopo.
6. Ushauri wa thamani uliotolewa na mthamini anayetambulika
katika mazingira ya soko huria.
Sheria inaainisha masharti yanayoambatana na kumilikishwa ardhi,
ambayo ni pamoja na:-
1. Gharama zilizotumika juu ya ardhi husika kwa mfano kuweka
huduma muhimu kama vile barabara, maji, mtaro, ama
mifereji ya maji taka, umeme n.k
2. Muda wa kumiliki unatolewa kwa kipindi au kwa vipindi
tofauti tofauti ambapo kwa ujumla hautazidi miaka tisini
na tisa. Vile vile miliki inaweza kutolewa kwa kipindi cha
mwaka hadi mwaka ama kwa muda mfupi zaidi kama
itakavyoelekezwa na Kamishna , na kwa vyovyote vile vipindi
hivyovisizidi miaka minne.

Muda wa Kumiliki Ardhi.


Hati maalum ya kumiliki ardhi iliyotolewa na kamishna muda wake
hautapunguzwa mpaka makubaliano yafikiwe na mmiliki (zingatia
kifungu cha 32 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999).

Baada ya muda wa umiliki kuisha na endapo mmiliki atakuwa


amezingatia masharti ya umiliki kwa kadiri inavyowezekana
anaweza akapewa nafasi ya kumiliki tena kwa masharti ambayo
kamishna ataamua kabla hati ya umiliki mpya haijatolewa kwa mtu
mwingine yoyote.

Baada ya muda wa umiliki kuisha na kamishna ameona si vyema


kummilikisha mmiliki ambaye muda wake umekwisha kwa kipindi
kingine licha ya maendelezo ambayo yamekwisha fanyika mmiliki
hatalipwa fidia yoyote.

22 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Uhamisho wa Hati ya Kumiliki Ardhi.


Uhamisho wa hati ya kumiliki toka mmiliki mmoja kwenda
mmiliki mwengine unapaswa upate kibali cha kamishna au afisa
mteule. Utaratibu huu umewekwa ili kuhakikisha kwamba wakati
wa uhamisho huo masuala kama vile kuuza, kuweka rehani au
kupangisha lazma kuzingayia sheria ya ardhi na nyinginezo husika
zinazingatiwa.

Mauziano ya Hati ya Kumiliki Ardhi.


Pale ambapo masharti yanayoambatana na miliki yametekelezwa
na kama kamishna hatakuwa na kipingamizi kingine basi haki
miliki inaweza kuuzwa baada ya Kamishna kutoa kibali ambacho
huombwa na mmiliki. Kwa vile kuuza haki ya kumiliki ni mambo
yanayohusu mkataba ikiwa mmojawapo wa wahusika atashindwa
kutimiza masharti ya mkataba wanaweza kutafuta njia ya ufumbuzi
ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani kutafuta suluhu.

Iwapo mwenye hati ya kumiliki ardhi au nyumba atataka


kukodisha au kuhamisha (au kuuza) hati yake kwa mtu mwingine,
yule atakayehamishiwa au kupewa ile ardhi atakuwa na wajibu
vilevile wa kuuliza iwapo kibali cha mke/mume wake kimetolewa
kufuatana na Sheria ya Ndoa ya 1971 na sheria za ardhi. Sect 167.

Kinyume cha hilo umiliki wa mtuamiaji mpya unaweza


kubatilishwa endapo mwanandoa mmojawapo ataweka pingamizi
au kulalamika. Aidha, mwanandoa atakayegundulika kutoa habari
za uongo kimaandishi au kwa mdomo kuhusiana na ugawaji/
uhamishaji wa ardhi au shughuli yoyote inayohusu ardhi au jambo
lolote linalohusiana na sheria hii ya ardhi, atakuwa ametend akosa
la jinai. Iwapo itabainika kuwa ametenda kosa hilo, atahukumiwa
kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini isiyozidi milioni moja au
vyote faini na kifungo kwa pamoja.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 23


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Tatu
SHERIA YA ARDHI YA KIJIJI
NA.5 YA 1999
Lengo la sheria hii nikuweka masharti ya usimamizi na uendeshaji
wa maswala ya ardhi na vijiji na mambo mengine yanayo husiana
na hayo.

Ardhi ya Kijiji ni Ipi?


Sheria hii imefafanua kwa kina kuhusu maswala mbalimbali yanayo
husu ardhi ya kijiji. Ardhi yaa kijiji ni ile ambayo inasifa zifuatazo:-
1. Ardhi iliyo ndani ya mipaka ya vijiji vilivya sajiliwa chini
ya sheria ya serikali za mitaa (mamlaka za wilaya1982), na
vijijivilivyohusishwa chini ya sheria ya makazi 1965
2. Ardhi ambayo imemilikiwa na wanakijiji kwamuda wa miaka
12 au zaidi kabla ya sheria ya ardhi ya mwaka 1999
3. Ardhi ambayo raisi ameibadilisha kutoka kuwa ardhi ya jumla
au ya hifadhi na kuwa adrhi ya kijiji. Rais hufanya h ivyo
kwa kumuelekeza waziri muhusika kutangaza na kuitaarifu
halmashauri ya kijiji.

Mgawanyo wa Ardhi ya Kijiji.


Sheria hii imegawanya ardhi ya kijiji katika Makundi yaufatayo:-

24 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Jedwali Na. 1

Ardhi ya
Ardhi ARDHI pamoja
iliyokaliwa ambayo
na kutumiwa halmashauri
na mtu, ya kijiji
itapendekeza
familia au YA kwa kupitia
kikundi cha mkutano
watu kwa wa kijiji
mujibu wa maeneo na
sheria za KIJIJI makusudio
kimila ya maeneo
hayo

Ardhi ya makazi au matumizi


ya jumuiya ambayo inaweza
kutolewa kwa njia ya mgao na
halmashauli ya kijiji

Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji


Mamlaka zilizopewa majukumu ya kushughulikia masuala ya ardhi
ya kijiji ni hizi zifuatazo:-

Mkutano mkuu wa kijiji-ambao huishauri Halmashauri ya kijiji


kuhusu masuala ya ardhi na kuhakikisha kwamba Halmashauri
hiyo inazingatia sera na sheria za ardhi mkutano mkuu pia hupitisha
maombi ya ardhi ya kijiji.
1. Halmashauri ya kijiji inaweza kuunda kamati maalum za
kushauri katika masuala ya usimamizi wa ardhi ya kijiji.
2. Baraza la ardhi la kijiji-ambalo kazi yake kubwa ni kutatua
migogoro yote ya ardhi kijijini inayohusiana na ardhi.
3. Kamati ya maamuzi ya ardhi ya kijiji-ambayo ina jukumu la
kuitambua ardhi ya kijiji na mipaka yake.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 25


Tanzania women Lawyers Association

Nani Anaweza Kumiliki Ardhi ya Kijiji?


Kwa mujibu wa sheria hii wafuatao wanaweza kuomba haki ya
kumiliki ardhi ya kijiji:-
1. Mwanakijiji yoyote (mwanaume/mwanamke) anaweza
kuomba hati ya kumiliki ardhi ya kijiji
2. Mtu yeyote ambaye ni mtalaka na na mwanandoa mwenzake
alikua mwanakijiji kabla ya kufunga ndoa, wote wakiwa raia
wa Tanzania, anaweza kuomba haki ya kumiliki ardhi ya kijiji
3. Mtu yeyote au familia yoyote au kikundi kinacho tambulika
chini ya sheria au mila ambacho kimejiunga kama chama cha
ushirika
4. Mtu au kundi la watu ambao kwakawaida sio wakazi wa kijiji
hicho anaweza/wanaweza kuomba kupewa hati ya kumiliki
ardhi ilimradi tu waambatanishe maelezo kuusu mipango
yao ya kuweka makazi ya kudumu katika kijiji hicho ndani
ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kupata hati ya kumiliki
ardhi kimila.

Utaratibu wa Kuomba Hati ya Kumiliki Ardhi Kimila


Katika Kijiji
Hati ya kumiliki ardhi kimila inaweza kutolewa kwa mtu, familia
au kikundi kwa kufuata hatua zifuatazo:-
1. Muombaji au waombaji watajaZa fomu na kuisaini. Ombi hilo
liambatanishwe na tamko kuhusu ardhi nyingine ambayo
muombaji anamiliki hapa nchini. kama muombaji ni familia
isainiwa na wanafamilia wasiopungua wawili.
2. Muombaji au waombaji, watoe maelezo au nyaraka nyingine
zozote zitakazohitajika na Halmashauri ya kijiji. Kama ni
kikundi cha watu wanao tambulika chini ya sheria za kimila
isainiwe na watu wasiopungua wawili wanaotambulika chini
ya sheria za kimila na isainiwe na watu wasiopungua wawili
wanaotambulika kama viongozi wakuu wa kikundi hicho.
Kama ni kikundi kilichoundwa kama umoja ama ushirika

26 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

chini ya chombo kinacho tambulika kisheria wasaini maofisa


wake wasiopungua wawili.
3. Maombi na malipo pia yaambatanishwe. Malipo yote yapatiwe
stakabadhi halali za malipo
4. Muombaji au waombaji wasio wenyeji wa kijiji hicho
waambatanishe maelezo kuusu mipango yao ya ujenzi ndani
ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kupata haki ya kumiliki
ardhi kimilafomu yake au yao isainiwe na wanakijiji wasio
pungua watano na wasio husiana kabisa na muombaji
5. Maombi hayo yawasilishwe kwa Halmashauri ya kijiji au afisa
mwenye mamlaka.
Hata hivyo taarifa muhimu zinaweza kuombwa ili kutosheleza
maelezo yaliyo wekwa hapo awali ili kusaidia katika kufikiwa kwa
uamuzi sahihi. Endapo maelezo zaidi yanayoombwa hayawezi
kupatikana basi mwombaji atoe sababu.

Baada ya kukamilisha na kukabidhi maelezo yote yanayohitajika


uamuzi wa kumpatia muombaji hati ya kumiliki ardhi kimila
unaweza kutolewa ndani ya siku tisini. Katika kufikia uamuzi
Halmashauri ya kijiji itazingatia yafuatayo:-
o Maamuzi yaliyo fikiwa na kamati ama chombo kingine chenye
hadhi kisheria ndani ya eneo ardhi ilipo.
o Maelezo yoyote ya kamishina wa ardhi kuhusiana na ombi la
raia au kikundi cha raia ambao sio wenyeji wa kijiji husika
o Suala zima la usawa kwa raia wote kama kuwatendea haki
wote bila ubaguzi wa kijinsia
o Kama ombi ni la kikundi ambacho ni cha raia lakini si
wenyeji wa kijiji Halmashuri ya kijiji itaomba maelekezo kwa
kamishina wa ardhia mbapo naye atazingatia yafuatayo:-
- ushauri wa awali uliotolewa na mwombaji toka
Halmashairi ya wilaya au chombo kingine kilicho na
mamlaka kisheria juu ya kijiji ardhi ilipo
- mchango wa kikundi ambacho si wenyeji ambao
umekwisha tolewa ama utatolewa na kikundi hicho

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 27


Tanzania women Lawyers Association

kusaidia maendeleo na ustawi wa kijiji na wana kijiji.


- mchango wa kikundi kwa maendeleo ya taifa.
- kama eneo linaloombwa na wageni ni kubwa ama lipo
katika eneo ambapo litaathiri shughuri za ki uchumi,
kijamii na hata tamaduni za wenyeji wa hapo kijijini
Iwapo muombaji/ waombaji ni raia na mwenyeji, basi mambo
yafuatayo yazingatiwe;
a. Iwapo mwombaji analo eneo jingine la ardhi analo miliki hapo
kijijini chini ya sheria ya kimila maombi ya ardhi anayoomba
yataangaliwa ili kuzingatia ukubwa wa ardhi inayoruhusiwa
mtu kumiliki katika eneo hilo.
b. Iwapo mwombaji anamiliki eneo lingine katika kijiji itaangaliwa
iwapo ametimiza kikamilifu masharti na madhumuni aliyo
kuwa ameombea ardhi husika
c. Iwapo mwombaji ana uwezo wa kiufundi, kiutaalam na kiujuzi
ama uwezo wa kiuchumi unaohitajika kuendeleza eneo kwa
faida zilizokusudiwa
d. Kiwango na namna muombaji anavyotarajia kumilikisha
wategemezi wake baada ya kufa
e. Suala lolote ambalo lina weza kuhitajika na halmashauri ya
kijiji mfano, uwezo wa kifedha kuendesha shughuli zilizo
kusudiwa
Baada ya maelezo hayo kukamilika, halmashauri ya kijiji inaweza
kutoa hati ya kumiliki ardhi kimila.

ZINGATIA: Endapo maombi ya kumiliki ardhi kimila


yatakataliwa, halmashauli ya kijiji italazimika kutoa
maelezo na sababu za kukataa kwake kama mwombaji
atataka maelezo hayo.

Endapo maombi yatakubalika, Halmashauri ya kijiji itampatia


mwombaji fomu ya ahadi iliyosainiwa na mwenyekiti na katibu,
ikiwa katika fomu maalumu inayo elezea masharti ya haki ya
umiliki wake mwombaji an anapokea fomu ya ahadi anatakiwa

28 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

kujibu kwa maandishi ndani ya siku tisini kama anaikubali au


anaikataa. Endapo atakubali, mwombaji atatakiwa kulipa ada zote
zinazotakiwa kisheria.

Baada a kukamisha taratibu zote, Halmashauri ya kijiji inatakiwa


kumpatiya mwombaji hati ya kumiliki ardhi kimila katika muda
usiozidi siku tisini (90). Iwapo mwombaji amekubali hati ya ahadi
na kuzingatia masharti yanayoambatana nayo na siku mia moja
themanini (180) zimepita bila kupatiwa Hati ya kumiliki ardhi
sheria inatambua hati ya ahadi kama hati halali ya kumiliki ardhi
kimila na itasajiliwa hivyo mpaka hapo hati ya kumiliki ardhi kimila
itakapopatikana.

Hati ya kumiliki ardhi Kimila hutolewa;


1. Katika Fomu maalum
2. Ikiwa na sahihi ya Mwenyekiti na Katibu wa Halmashauri ya
kijiji.
3. Ikiwa na sahihi ama alama ya dole mmiliki kwa mfano dole
gumba la mkono wa kushoto au kulia chini ya kila ukurasa wa
hati ya kumiliki ardhi. Sahihi ionyeshe dole gumba la mkono
gani limetumika.
4. Vile vile itasainiwa, itawekwa lakiri (muhuri maalum/muhuri
wa moto) na kusajiliwa na Afisa Ardhi wa Wilaya ambamo
kijiji kipo.

Malipo na muda wa Hati miliki ardhi kimila


Hati ya kumiliki ardhi kimila inaweza kutolewa kwa raia kwa
kipinidi kisicho na kikomo au kwa kipindi kisichozidi miaka tisini
na tisa (99) kadri serikali ya kijiji itakavyoona inafaa.

Kurejesha, Kugawa na kuhamisha Haki miliki ya Ardhi


Kijijini.
Kwa mujibu wa kufungu cha 35 cha Sheria ya ardhi namba 5
urejeshaji wa ardhi unaweza kufanywa na mwanakijiji yeyote
au kikundi kinachomiliki ardhi. Ikiwa mwenye haki ya kumiliki

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 29


Tanzania women Lawyers Association

ardhi kijijini anataka kurejesha, kugawa au kuhamisha miliki ya


ardhi anayomiliki atapeleka maombi kwenye Halmashauri ya Kijiji.
Endapo anayerejesha ardhi ni mwanandoa basi Halmashauri ya
kijiji itawasiliana na mwanandoa wa anayetaka kurejesha, kugawa
au kuhamisha haki ya kumiliki ardhi ili kuhakikisha kwamba
mrejeshaji huyo hafanyi hivyo kwa nia ya kumdhulumu mwenzi
wake.

Iwapo anayerejesha ardhi ya miliki ya kimila anao watu


wanaomtegemea, kwa mfano kama ni mwanamke, mume
anamtegemea na kama ni mwanamme, mke anamtegemea,
Halmashauri ya Kijiji katika kutoa milki mpya itatoa kipaumbele
kwa mke au mme – mwenza wa ndoa. Kama hana mke /mume basi
kipaumbele kitakuwa kwa watu wengine wanaomtegemea.

Hata hivyo urejeshaji wa ardhi inayomilikiwa chini ya hati miliki ya


kimila ambao utaashiria yafuatayo;
1. Kumnyang’anya au kumzuia mwanamke asimiliki ardhi au
2. Mrejeshaji ana nia ya ubadhirifu, utovu wa uaminifu au
dhuluma, urejeshaji huo hautakuwa halali na hautakubaliwa.
Ieleweke kwamba mrejeshaji wa ardhi atatakiwa kuendea kulipia
1. Kodi
2. Riba ya mkopo iliyochukuliwa kama dhamana ya hati miliki
ya kimila.
3. Kodi,ada na ushuru unaodaiwa na ule unaostahili kulipwa
siku ya kurejeshwa kwa haki miliki ya kimila.
Ikiwa mrejeshaji anarejesha ardhi kwa sababu za umri, ugonjwa
ulemavu, umasikini, Halmashauri ya Kijiji itachukuwa jukumu la
kulipia madeni hayo.

Kama ardhi inayorejeshwa inakaliwa na mtu, Halmashauri ya Kijiji


itaendelea kutoza kodi ya pango toka kwa mtu huyo. Mtu yeyote
anayerejesha haki miliki ya kimila ataendelea kuhusika na makosa
ya ukiukwaji wa masharti ya kumiliki ardhi uliotokea wakati akiishi
kwenye ardhi hiyo.

30 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Nne
SHERIA YA FEDHA NA REHANI
Sheria ya fedha na rehani imeweka mazingira kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba kwa kutoa hakikisho la kuwalinda wakopeshaji.

Sheria ya umiliki wa sehemu ya jengo umefungua mwanya kwa ajili


ya umiliki wa pamoja kati ya wenzi au mke na mume pia. Wenzi
hawa Wanapomiliki sehemu ya jengo kwa umoja wanaweza kuuza,
kuweka reheni au kupangisha.

Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za uwajibikaji kisheria pale


endapo wenzi wanaomiliki kwa pamoja wamechukuwa mkopo na
wakashindwa kurejesha basi mkopeshaji atawashtaki kwa pamoja
au kuwashitaki mmoja mmoja.

Kama shitaka ya kushitakiwa kwa pamoja halitotosheleza (ushahidi)


basi mume au mke ambaye amekopa atashitakiwa peke yake.

Mtizamo wa kina wa vifungu vya sheria ya mikopo ya nyumba


unatoa taswira ya athari zinazoweza kuwakabili wanawake kwenye
umikili wa mali kutokana na vifungu vya sheria hiyo.

Kama ilivyoelezewa hapo awali, sheria ya mikopo ya nyumba


haijitegemei peke yake. Sheria hiyo kwa kuwa ni sehemu ya sheria
kuu ya ardhi (1999) basi sheria hizi mbili zitasomwa kwa pamoja
kwa kuwa inarekebisha vifungu vingi vya sehemu ya Kumi (10) ya
Sheria ya Ardhi inayohusu rehani.

pia imerekebisha utaratibu wa kuomba kugawiwa ardhi kwa


kuondoa barua ya kusudio ambayo ilikuwa utaratibu muhimu
kwenye maombi ya haki ya kugawiwa. Barua ya kusudio haikutoa
tu unafuu kwa mwombaji wa haki ya kugawiwa bali ilikuwa
sehemu ya utaratibu muhimu katika uhusiano wa mgawaji (grantor)
na mgawiwaji. Barua hiyo ilifuata utaratibu wa kawaida kwenye
sheria za mikataba ambao ni muhimu kujenga mahusiano ya pande
zilizoingia mkataba.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 31


Tanzania women Lawyers Association

Taratibu za uombaji
Sheria hii inatoa mwanya kwa mwombaji kujua asili, masharti
na muda wa haki kusudiwa kabla ya kukubali. Mara mwombaji
anapokuwa amekubaliana na masharti yaliyoainishwa alitakiwa
kusaini barua hiyo ya kukubaliwa na kulipa malipo yanayotakiwa.

Kutokea hapo Serikali ingeweza kuandaa taratibu za kukamilisha


ugawaji na kama serikali ikabadilisha kusudio lake ilibidi kutoa fidia
kwa mwombaji kwa hasara yoyote atakayokuwa ameingia kutokana
na kuondoa barua hiyo ya kusudio au kutafuta eneo lingine ikiwa
masharti na sifa za eneo la awali kama barua ya kusudio ilivyokuwa
inaainisha.

Endapo hati ya umiliki wa kugawiwa haikutolewa kwa muda wa


siku 180, aliyegawiwa anaweza kusajili barua ya kusudio chini ya
Sheria ya usajili wa Nyaraka (Registration of Documents Act Cap
117). Usajili huo chini ya vifungu vya Sura ya 117 uliifanya barua ya
kusudio kuwa na sifa ama hati ya umiliki.

Usajili huo pia uliweka ashirio la notisi ya umiliki unao subiriwa.

Barua hii ilimpa mwombaji (offeree) haki inayofanana na ya mmiliki


na aliweza kuweka rehani hiyo ardhi. Mfumo wa barua ya kusudio
ulitoa nafasi kuwa kwanza kuomba ndiye anayepewa. Lakini baada
ya kufutwa kwa mfumo huo inawezekana kamishna wa ardhi kutoa
upendeleo kwa maombi ya nyuma akiacha yaliyotangulia.

Kufutwa kwa vifungu hivyo kunaweza kuwa kichaka cha mazalia


ya ubadhilifu wa madaraka, rushwa na matendo yanayofanana na
hayo. Matajiri wanaweza kukanyang’anya haki za wanyonge kama
wanawake walio na maisha magumu kwa kigezo cha uendelezaji
makazi.

ANGALIZO: Sheria pia imefuta na kubadilisha kanuni


za rehani za 2005 pamoja na fomu mbalimbali na kuweka
kanuni mpya (2009) na fomu mpya.

32 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

WAJIBU WA MKOPESHAJI NA MKOPWESHAJI


Marekebisho yameweka ulazima kwa mkopaji kusaini hati ya kiapo kwamba
hana mwenzi au ridhaa ya mwenzi imetafutwa na kupatikana. kifungu na.
8 cha sheria ya marekebisho ambayo ilibadilisha kifungu na.114(2)
cha sheria ya ardhi.

Wajibu pekee wa mkopeshaji ni kuhakikisha kuna hati ya kiapo


au waraka wa kimaandishi ambapo mwombaji anatamka kwamba
kuna mwenzi/wenzi au watu wengine wenye maslahi kwenye
ardhi ya rehani.

Kama ilivyoainisha katika kifungu na. 8 cha marekebisho ambacho


kimeongezwa katika sheria ya ardhi kifungu na. 114(3).

TATIZO LA KUKIUKA MASHARTI KWA MKOPAJI


i. Endapo itagundulika baadaye kwamba mkopaji alitoa taarifa
za uongo au zisizo sahihi kuhusiana na hadhi ya kindoa basi
ataweza kushtakiwa na kama akihukumiwa kwa kosa hilo
atapaswa kulipa faini isiyopungua nusu ya thamani ya mkopo
au kifungo kisishopungua miezi kumi na miwili (12).
ii. Kwahiyo sheria inahamisha jukumu la kuthibitisha usahihi
wa taarifa kwenda kwa mkopaji na hata familia yake maana
kama sio sahihi familia itaathirika).
iii. Pia inajenga mazingira ya mashaka kwa watoto na mwenzi /
wenzi wa mkopaji. Endapo mkopaji ni mume na akahukumiwa,
familia yote itapata tabu itokanayo na adhabu iliyotolewa.
iv. Kutokana na uwezekano wa mkopo kuchukuliwa bila mke
kujua, familia inaweza kujikuta inaadhibiwa kwa makosa
yasiyowahusu na hata kwa mkopo ambao haukuwa na
maslahi kwao.
v. Hata kama mali ya familia haitauzwa familia itataabika kulipa
deni vilevile. Katika mazingira haya, wale watakaoathirika
zaidi na sheria hii watakuwa ni wanawake na watoto.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 33


Tanzania women Lawyers Association

MAPUNGUFU YA SHERIA
1. Kifungu hiki kimeegemea zaidi upande mmoja pasipo
kuangalia upande wa familia ya mkopaji lakini pia
kutokuzingatia uwezekano wa hati ya kiapo kugushiwa.
2. Ilipaswa kubaki kuwa jukumu la mkopeshaji kuthibitisha
taarifa zilizo tolewa na mkopaji endapo ni sahihi kabla ya
kutoa mkopo.
3. Pia, marekebisho yameruhusu kubadilishwa kwa kiwango cha
riba kwa mkopeshaji kuandika notisi kwenda kwa mkopaji;
hii inamweka mkopaji katika hali ya mashaka endapo ataweza
kulipa deni pale riba inapopandishwa.
4. Vilevile kama inavyoonekana kigezo kikubwa cha kubadilisha
kiwango cha riba ni kuangalia faida ya soko na sio hali ya
kichumi ya mkopaji.
5. Pia uamuzi wa kupandisha riba ni wa upande mmoja wakati
mkataba wa mkopo ulikuwa wa pande mbili. Mkopaji hana
fursa ya kutoa mtizamo wake.
6. Hata baada ya nyongeza ya kiwango cha riba endapo mkopaji
akashindwa kulipa mali yake inaweza kuchukuliwa na
kuuzwa kulipia deni na kuwaacha mke na watoto wakiteseka.
Wakati inajulikana kwamba mkopaji anaweza kuweka rehani nyumba
ya kuishi ambayo kuna watu ndani au shamba linalotumiwa kwa
ajili ya kilimo, marekebisho yameweka wazi kwamba mkopeshaji
anaweza kuuza ardhi kama mkopaji atashindwa au kuchelewa
kulipa deni kwa wakati. Mauzo yanaweza kufanyika kwa njia
ya mkataba na kwa muda mfupi au mnada wa hadhara ambapo
mkopaji na watu wengine wenye maslahi watapewa notisi ya siku
kumi. Hii kwa vyovyote itaathiri wanawake na watoto inapokuja
kwenye swala la lazima kuondoka kwenye nyumba.

Mnunuzi wa nyumba iliyowekwa rehani chini ya marekesbisho ya


sheria anaweza kuingia kwenye nyumba mara tu baada ya kushinda
mnada wa mauzo au mkataba wa mauzo. Mwanya huu hauzingatii
changamoto zinazoweza kuikabili familia wakati wa utekelezaji wa

34 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

mauzo. Mwanya huu pia unabaki kuwa mlango wazi kwa ajili ya
soko kukanyaga haki za wanyonge hasa wanawake na watoto.

Wajibu ya Mahakama Katika Kesi za Rehani


Pale haki za mkopaji na wategemezi zinapokuwa zimevunjwa
suluhisho pekee ni kwenda mahakamani. Mahakama ina uwezo
kama mkopaji alikuwa na uweza wa kulipa ndani ya kipindi cha
wastani kuahirisha tarehe ya kuondoka na kukabidhi nyumba.

Hata hivyo, chini ya marekebisho yaliyoletwa na sheria ya mikopo


ya nyumba mahakama lazima zihakikishe kwamba upo uhakika wa
kiwango cha juu kwamba mkopeshaji hatapata hasara.

Pia nguvu ya kuahirisha tarehe ya kukaza hukumu, ua kuahirisha


tarehe ya kuachilia nyumba iliyowekwa rehani kwa mkopaji mmoja
inaruhusiwa mara moja tu na ahirisho hilo lisizidi miezi sita.

Hii inaminya nguvu ya mahakama katika kutoa maamuzi na


kuathiri pia ustawi wa familia na wategemezi wa mkopaji isipokuwa
mkopeshaji.

Katika kurahisisha mazingira zaidi kwa wakopeshaji marekebisho


ya sheria yameweka nadharia inayopingika kwamba mkopeshaji
hajajihusisha na udanganyifu, uongo kuhusiana na masharti ya
mkataba wa mkopo. Kwa nadharia hii ni wajibu wa mkopaji
kuthibitisha kwamba mkopeshaji alipata ridhaa ya mkopaji kwa
ushawishi pamoja na kumuingiza kwenye masharti husika ya
mkataba ambao sio jambo rahisi kwa mtu wa kipato cha chini.

Katika kugongelea msumari wa mwisho sheria ikafanya marekebisho


kwenye sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai sehemu ya
XXXV kwa kupunguza aina za utetezi ambazo mkopaji angeweza
kuzitumia mahakamani.

Mkopaji au mwombaji anayefanya kwa niaba atachukuliwa kuwa


ametii masharti na kutimiza wajibu wake katika mkataba wa
mkopo kama akaunti yake itaonyesha kwamba deni limeshalipwa
au hakuchukua mkopo.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 35


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Tano
SHERIA YA UMILIKI WA VIPANDE

UTANGULIZI:
Sheria ya umiliki wa vipande ya mwaka 2008, ni Sheria inayoweka
mfumo wa kisheria kwa ajili ya utekelezaji wa mfumo wa umiliki
pacha Tanzania. Sheria hii japo inalenga kupunguza changamoto za
makazi ambazo ni pamoja na mpangilio hafifu, vikwazo vya kisheria,
kukosekana mikopo ya nyumba ya muda mrefu, udhaifu wa sheria
za ardhi, kuongezeka na kupanuka kwa miji na kukosekana kwa
fedha za kununua au kujenga makazi bora.

Kwa hiyo sheria ya umiliki wa vipande imelenga kuwezesha


mikopo ya nyumba, kusimamia mfumo wa umiliki pacha wa
majengo yanayofanania kusimamia wadau wa mfumo huu,
kuboresha ustawi wa makazi ya mijini, kuzuia usambazaji wa miji,
kutoa uhawilishaji wa nyumba kwa wakati na wa umakini mijini na
kupunguza gharama za safari za mijini.

Sheria hii imefungua mwanya kwa ajili ya umiliki wa umoja kati ya


wenzi au mke au mume pia. Wanapomiliki sehemu ya jengo kwa
umoja wanaweza kuuza, kuweka rehani au kupangisha. Hata hivyo
kwa mujibu wa kanuni za uwajibikaji kisheria (liability) wajibu chini
ya umiliki wa umoja (joint occupancy) kama wenzi wamechukua
mkopo na wakashindwa kurejesha ni kushtakiwa kwa pamoja
na au kushtakiwa mmoja mmoja. Hivyo mume na mke anaweza
kushtakiwa kivyake kama shtaka la pamoja halikutosheleza kulipia
deni.

ANGALIZO: Sheria hii inakwenda sambamba na sheria


za ardhi za mwaka 1999 na sheria ya ndoa ya mwaka 1971
kwa kumpa mwanamke haki ya kumiliki ardhi/jengo
kama mali yake binafsi. Kwa mantiki hiyo mwanamke ana
haki ya kumiliki, kuuza sehemu ya jengo na kurithisha
kwa kufata taratibu zilizowekwa na sheria hii.

36 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Sifa za umiliki pacha.


o Ni lazima jengo liwe na sehemu /eneo ambalo linamilikiwa na
mtu mmoja mmoja kwa matumizi yake mwenyewe na baadhi
ya maeneo yanayomilikiwa na wamiliki wa sehemu kwa
pamoja kwa matumizi ya pamoja.
o Zile sehemu (eneo) linalomilikiwa na mtu mmoja mmoja kama
eneo binafsi linaitwa kisehemu (unit). Maeneo ya jengo yanayo
milikiwa na wamiliki wa visehemu kwa faida na matumizi ya
jumla yanaitwa maeneo ya jumla (common areas). Maeneo ya
jumla yanasimamiwa na chama cha wamiliki wa visehemu
(unit owners’ association) ambacho uanachama wake ni wa
lazima kwa wamiliki wote wa visehemu.
Mchoro Ufuatao Unaelezea Mfumo wa Umiliki Pacha

Kisehemu Eneo la Kisehemu


binafsi Jumla binafsi

Chama cha Wamiliki wa Sehemu

Taswira ya Sheria ya Umiliki wa Sehemu ya jengo


Sheria ya umiliki wa vipande inalenga kusimamia majengo ya
visehemu, nyumba zilizo katika mkusanyiko (clusters) magorofa
(blocks) na hata sehemu zinazomilikiwa kibinafsi. Pia inaweka
mfumo wa utoaji wa hati kwa wamiliki wa visehemu. Ili kuhakikisha
kwamba upo ulinzi wa kutosha na usimamizi wa maeneo ya
jumla, sheria imeanzisha mfumo wa kitaasisi kusimamia majengo
yanayoangukia chini ya sheria hiyo ikiwa ni pamoja na mfumo
wa utatuzi wa migogoro inayotokana na umiliki pacha. Chini ya

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 37


Tanzania women Lawyers Association

sheria hii usimamizi majengo ya visehemu unajumuisha chama


cha wamiliki, wakala wa kusimamia majengo (Estate agents),
sheria ndogo ndogo za wamiliki wa visehemu, katiba ya chama cha
wamiliki na mikataba na wakala wa kusimamia jengo.

Haki za wamiliki wa sehemu ya jengo


• Kila mmiliki wa sehemu ya vipande atakuwa na haki ya
kumiliki maeneo ya matumizi ya pamoja kwa usawa bila
kugawa sehemu za haki ambazo hazigawanyiki.
• Maeneo ya matumizi ya pamoja yatahusisha ardhi, uwa,
veranda, ubaraza wa gorofani, sehemu ya kuegesha magari,
sehemu ya kupumzika, bustani, njia, ngazi, lifti, kumbi na
sehemu za matumizi ya pamoja kama choo, stoo, misingi ya
nyumba na kuta za pamoja, vitu vya matumizi ya pamoja na
vifaa kama tanuru, mfumo wa kiyoyozi, mfumo wa mabomba
pamoja na mfumo wa umeme.
• Mmiliki ana haki ya kutumia ipasavyo vitu vyovyote
ambavyo haviingiliani na mmiliki mwenza labda tu sheria
itakavyoelekeza vingine.
• Mmiliki ana haki ya kupewa cheti cha umiliki baada ya kusajili
mpango wa kumiliki ardhi ya vipande kwa mujibu wa sheria.
• Mmiliki baada ya kupewa cheti cha umiliki atakuwa na haki
zote ikiwa ni pamoja na kuuza, kubadili umiliki, kukodisha,
kutoza gharama au vinginevyo ilivyo kwa mujibu wa sheria.
• Wamiliki wana haki ya kutumia ardhi ya vipande na maeneo
ya pamoja kwa matumizi binafsi na pia kwa matumizi ya
kifamilia na nyumbani.
• Mmiliki ana haki ya kuuza, kuweka rehani, kuhamisha,
kugawa,kupangisha, kuweka chini ya uwangalizi.
• Pale ambapo kampuni itakuwa ni mojawapo ya wamiliki
wenza wa kipande mwakilishi wa kampuni anaruhusiwa
kuwa mwakilishi wa wamiliki wa kipande katika ushirika.

38 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Uuzaji wa vipande
• Sheria inaelekeza yakuwa eneo la matumizi ya pamoja
halitauzwa au kutozwa gharama yoyote labda tu kama
linamilikiwa na mtu mmoja.
• Mmiliki ana haki ya kumpa mtu yeyote sehemu yake kwa njia
ya kuuza ,kupangisha, kuzawadia, kurithisha, kuweka rehani
au kwa namna nyingine yoyote iliyoidhinishwa kisheria.

Upangishaji.
• Mmiliki ana haki ya kupangisha kipande chake.
• Mmiliki anayepangisha kipande chake atawajibika kuweka
fedha ya tahadhari chini ya uangalizi wa ushirika na kulipia
gharama zozote za matengenezo, upotevu na manunuzi ya
vitu vitakavyoharibiwa.
• Mmiliki wa sehemu ya vipande ana wajibu kisheria kujulisha
ushirika juu upangishaji wa sehemu yake kwa maandishi
yenye maelezo muhimu na jina la mpangaji ndani ya siku
saba.
Urithishwaji.
• Mmiliki wa sehemu ya vipande anaweza kurithisha sehemu
yake kwa kufata taratibu zilizoainishwa katika sheria ya Usajili
wa Ardhi, sura ya 334.

Rehani.
• Sheria inaruhusu mmiliki kuweka rehani sehemu ya jengo lake
kwa kufuata taratibu zilizoainishwa katika sheria ya Ardhi ya
mwaka 1999 (sura ya 113) ambayo imerekebishwa na sheria
Na 2 ya mwaka 2004 na sheria Na 17 ya mwaka 2008.
• Ushirika unawajibu kisheria kulinda sehemu ya jengo ya
ushirika ilyowekwa rehani kwa kuzingatia taratibu ya Sheria
ya umiliki wa sehemu ya jengo na 16 ya mwaka 2008.

Usimamiaji wa sehemu ya vipande.


Ushirika utakaoanzishwa na wamiliki wa vipande zaidi ya watano
watatakiwa kuusajili kwa msajili na utakuwa na kazi zifuatazo:

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 39


Tanzania women Lawyers Association

• Kusimamia sehemu ya matumizi ya pamoja katika hali nzuri.


• Kulinda na kusimamia fungu kwa ajili ya gharama za
uendeshaji.
• Kusimamia uendeshaji na utawala wa mali za matumizi ya
pamoja.
• Ulipwaji wa gharama za bima, kodi na mgawanyo wa
majukumu yoyote ya ushirika.
• Kupanga na kuamua kila gharama za matumizi ya pamoja.
• Kusimamia upatikanaji wa pesa kwa kuchangisha kulingana
na sehemu ya umiliki vipande kwa ajili ya gharama za ushirika.
• Kuhakikisha na kuweka majengo pamoja na kuchukua jitihada
za makusudi kuzuia ajali za moto katika majengo hayo.
• Kuyawekea bima majengo hayo kwa mujibu wa sheria ya
vipande ama watakayoona inafaa.
• Kulipa gharama za bima kulingana na mkataba wa bima
unavyoelekeza.
• Kusimamia wajibu wote uliowekwa na sheria hii.

Utatuzi wa Migogoro na mbinu za utekelezaji wa sheria.


• Migogoro yote ya ambayo itatokea kati ya wanachama wa
ushirika itafikishwa katika ushirika kwa ajili ya usuluhishi,
kama usuluhishi utashindikana mgogoro huo utapelekwa
katika mahakama kuu na mahakama kuu kitengo cha ardhi
kwa hatua zaidi au baraza la nyumba na ardhi la wilaya ikiwa
hakuna mahakama kuu kitengo cha ardhi katika eneo husika.

Ubadilishaji wa vipande vya ardhi.


• Mabadiliko ya umiliki wa ardhi ya vipande yatapaswa
kuwasilishwa kwa msajili kwa usajili yakiambatanishwa na
hati yenye uthibitisho wa chama kueleza bayana kwamba
makubaliano ni hakika na ruhusa imetolewa na wahusika
kuwa ardhi hiyo yaweza kubadilishwa.
• Msajili atawajibika kuwezesha mabadiliko ya umiliki wa ardhi
hiyo kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
• Wamiliki wana haki ya kuhamisha ardhi ya vipande kwa mtu

40 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

mwingine kwa njia ya kuuza, kupangisha, kutoa zawadi au


kukabidhi warithi .

Utaratibu wa kuomba Umiliki wa Ardhi ya vipande


• Mmiliki au mwendendelezaji wa ardhi ya vipande anaweza
akagawa jengo katika vipande viwili au zaidi kwa kusajiliwa
kwa mpango wa vipande kwa msajili wa ardhi kwa mujibu
wa sheria hii. Baada ya kusajili atawasilisha nakala tano za
mpango huo kwa usajili na atapaswa kuonyesha idadi ya
vipande ndani ya vipande alivyogawa na wakati anawasilisha
mpango huo kwa msajili anaweza kuonyesha kama maendeleo
yaliyoonyeshwa kwenye eneo yatafanyika mara moja au kwa
nyakati tofauti.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 41


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Sita
SHERIA NYNGINEZO ZINAZOHUSIANA NA
UMILIKAJI WA ARDHI
SHERIA YA NDOA.
Nyumba ya ndoa katika sheria ya ndoa
o Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mume na mke wanaishi
wakati wa ndoa inawezekana ikawa mali binafsi ya mke au
mume au nyumba ya kupanga .
o Mke au mume hanaruhusiwi kuuza nyumba hiyo, kuweka
rehani au kumpa mtu mwingine kama zawadi bila makubaliano
ya wanandoa.
o Kama mmoja wa wanandoa anataka kuuza nyumba hiyo bila
kukubaliana na mwenzi wake Yule mwenzi ambaye hakutoa
idhini anaweza kuweka pingamizi (caveat-buyer be aware)
ambayo kimsingi inatahadhalisha mtu yeyote atakaye taka
kujihusisha na mali au ardhi hiyo mfano kwa kununua kuwa
kuna mtu mwingine mwenye maslahi katika ardhi au mali
hiyo.

Mali ya Ndoa ni ipi?


Ni ile mali iliyopatikana kutokana na nguvu za pamoja za wanandoa
wakati ndoa inaendelea. Mali ya ndoa inaweza ikawa nyumba au
shamba. Mali hiyo itahesabika kuwa imepatikana kwa juhudi za
pamoja za wanandoa. Hivyo basi mwanamke ana haki sawa na
mwanaume pale ndoa inapovunjika na kupata mali ya kutumia.
Isipokuwa pale tu mume au mke atakapo kanusha ukweli huo.

Je uchangiaji wa mwanandoa katika uendelezaji au upatikanaji wa


ardhi unatambulika kisheria?

Sheria ya ardhi ya vijiji sheria, inaeleza kuwa, pale ambapo


mwanandoa anapata ardhi chini ya miliki ya kimila haki miliki
kwa matumizi ya wanandoa wote wawili, au pale penye mke

42 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

zaidi ya mmoja kwa ajili ya wanandoa wote , kutakuwepo na


dhana kuwa wanandoa watamiliki kwa pamoja katika mafungu
yanayogawanyika.

Dhana hii inaweza kubatilishwa pale ambapo mwanandoa


anayeomba ardhi ataeleza bayana kuwa anachukua hati ya umiliki
kwa jina lake mwenyewe au anachukuwa ardhi na mwanandoa au
wanandoa wenzake katika mafungu yasiyogawanyika.

Iwapo mwombaji wa ardhi hataweka wazi suala la umiliki


kama ilivyoelezwa hapo juu, basi msajili wa hati atalazimika
kuwasajili wanandoa hao kama wamiliki wa pamoja wa mafungu
yanayogawanyika.

Sheria ya ardhi ya 1999 inaeleza pia kuwa iwapo hati ya umiliki


ardhi ipo kwa jina la mwanandoa mmoja tu lakini wanandoa au
mwanandoa wengine wamechangia nguvu zao katika kuzalisha,
kutunza na kuendeleza ardhih iyo, mwanandoa au wanandoa hao
watatambulika kutokana na nguvu zao kwamba wana maslahi
ndani ya ardhi hiyo katika misingi ya umiliki wa pamoja wa ardhi
wa mafungu yanayogawanyika katika ile ardhi ambayo jina la
mwanandoa limesajiliwa katika hati ya umiliki wa ardhi au cheti
cha umiliki wa ardhi kimila.

Je mke au mume wanapoachana nani ana haki ya


kuendelea kumiliki ardhi yao?
Suala la kuachana yaani talaka linashughulikiwa na sheria ya ndoa
Na 5 ya mwaka 1971 ambayo imefanyiwa marekebisho na kuwa
sheria mwaka 2002 (CAP 29 R.E.2002)

Kifungu cha sheria ya ndoa cha 114 kinaelezea kuwa mahakama


ina uwezo wa kutoa amri ya kugawanya mali iliyochumwa kwa
pamoja baina ya mke na mume au kutoa amri ya kuuza mali hiyo
na kugawanya fedha iliyopatikana.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 43


Tanzania women Lawyers Association

Katika kutumia uwezo wake, wa kugawanya mali ya ndoa,


mahakama inatakiwa kuzingatia:-
a) Desturi na maisha ya wanandoa waliyokuwa wanatumia.
b) Kiasi cha mchango uliofanywa na kila mtu (mke na mume)
katika upatikanaji wa mali hiyo. Mchango unaweza kuwa wa
fedha, mali au kazi (nguvu) iliyofanywa katika kupata mali
iyo.
c) Madeni yaliyopo ambayo yanatokana na mwanandoa mmoja
au wote kwa ajili ya faida ya wanandoa wote (mke na mume).
d) Mahitaji ya watoto wadogo wa ndoa.
e) Kwa vile mchango wa mwanandoa unaweza kuwa si wa
fedha bali wa kazi au nguvu anazozifanya za nyumbani
na shambani ardhi itagawanywa kwa mke na mume kwa
kuzingatia kiwango cha uchangiaji wa fedha au nguvu ya kila
mwanandoa.

SHERIA ZA MIRATHI
Mirathi ni Nini?
Ni masuala yanayohusu kukusanya kulipa na kugawa mali pamoja
na kulipa madeni yaliyoachwa na marehemu. Mojawapo ya mali ni
ardhi, nyumba na vinginevyo ambayo marehemu alikuwa anamiliki,

Kuna Sheria Ngapi za Mirathi?


Tofauti na sheria ya ndoa, mirathi inalindwa na sheria tatu tofauti,
nazo ni:-
• Sheria ya kiserikali tuliyoipokea kutoka India ya Mwaka 1865
• Sheria za mirathi za kimila GN NO.436 ya 1963
• Sheria za mirathi za kidini (kiislamu, kihindu)

Zingatia: Sheria hizi hutumika pale tu ambapo


marehemu hakuacha wosia. Kama ameacha wosia, basi
mirathi yake / mali zake itagawiwa kwa mujibu wa
wosia aliouacha marehemu.

44 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

I. Sheria ya kimila
Sheria hii diyo inayodhaniwa kutumiwa kwa wazawa wote
isipokuwa pale ambapo alikuwa afati mila na desturi husika za
kiafrika.

ANGALIZO: Wazawa inamaanisha watu wenye asili ya


hapa hapa Tanzania ambao siyo wahamiaji au waliopata
uraia. Sheria ya kimila haitatumika itakapothibitishwa
kuwa marehemu tayari alishaachana na desturi za
kabila yake.

Mgawanyo ukoje katika sheria za kimila?


Kanuni hizi zimo katika kanuni za urithi, tangazo la Serikali Na.
436 la 1963. Sheria hii imegawa urithi katika madaraja matatu kama
ifuatavyo:-
I. Daraja la kwanza
Mtoto wa kwanza wa kiume wa mke mkubwa ( wa kwanza)
au kama hakuna, basi wa kwanza yeyote wa kiume kwa mke
mwingine atapata fungu kubwa zaidi.
II. Daraja la pili
Watoto wote wa kiume waliosalia katika nyumba zote
watapata fungu kubwa kidogo.
III. Daraja la tatu
Hili ni la watoto wote wa kike wa marehemu ambao
watapata fungu dogo zaidi kuliko wote. Watoto hawa wa
kike hawaruhusiwi kurithi ardhi ya ukoo bali kuitumia
tu wakati wa uhai wao. Iwapo hakutakuwa na watoto wa
kiume watoto wa kike wanaweza kurithi lakini hawataweza
kuirithisha ardhi hiyo. Watoto hawa wa kike wanaweza kuuza
ardhi iwapo watakuwa na mahitaji ya msingi ya kuwafanya
wahitaji kufanya hivyo lakini watatakiwa kutangaza kwanza
kwa wanaukoo kama yupo mwenye kuhitai kuuza ardhi
hiyo. Iwapo hakutakuwa na mwanaukoo mwenye kuhitaji
na kumudu gharama ya kununua ardhi au nyumba hii

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 45


Tanzania women Lawyers Association

watoto hawa wataweza kuiuza ardhi au nyumba hiyo kwa


mtu mwingine wan je ya ukoo. Masharti haya kuhusiana na
kuuza ardhi au nyumba ya ukoo yanatumika vilevile hata kwa
warithi wa kiume.

Hata Hivyo Ikumbukwe Kuwa:


Katika Tanzania Mahakama Kuu imeishatamka kwamba sheria
ya mila inayombagua mwanamke ni batili. Hii iliamuliwa na
Mahakama kuu ya Tanzania katika kesi ya BERNADO EPHRAIM
DHIDI YA HOLARIA PASTORY iliyoamriwa mwaka 1989.

Watoto wa marehemu waliozaliwa nje ya ndoa hawaruhusiwi


kurithi chochote ila wanaweza tu kurithi iwapo walihalalishwa na
marehemu kabla ya kufa kwa kuzingatia mila na desturi za kabila la
marehemu. Hata hivyo sheria ya karibuni zaidi yaani Sheria ya Mtoto
ya mwaka 2009 inakataza vitendo vyote vya ubaguzi dhidi ya mtoto.
Sheria inakataza ubaguzi kwa mtoto unaotokana na kigezo cha jinsi,
umri, mila, dini n.k. Pia sheria inasema mtoto hatanyimwa kufurahia
mali iliyoachwa na marehemu mzazi wake katika kifungu cha kumi.
Japo kuwa kifungu hiki kakiko kinagaubaga katika kulinda haki
za watoto za kurithi kama ilivyochanganuliwa hapo juu, kifungu
hiki cha kumi kikisomwa pamoja na kifungu cha tano kinachozuia
ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya watoto tunaweza kusema mtoto
akiwemo hata mtoto wan je ya ndoa ana haki ya kurithi mali ya
marehemu wazazi wake. Pamoja na hayo sheria ya ndoa inatafsiri
mtoto kuwa ni mtu yeyote aliye chini ya miaka kumi na nane. Kwa
maana hiyo watoto wa marehemu walio chini ya miaka kumi na
nane hawatahusika na sheria hii.

Nini Haki ya Mjane / Mgumba?


Mjane ambaye hana watoto kwa mujibu wa Sheria ya Hali ya Watu
atabaki katika nyumba ya marehemu na kupewa asilimia ishirini
(20) ya nusu ya mali ya marehemu kuitumia wakati wa uhai wake.
Akifa au akiolewa mali hiyo na nyumba aliyokuwa akikaa hugawiwa
warithi halali wa marehemu mume wake.

46 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Sheria inaeleza wazi kuwa, mjane ana haki ya kubakia ndani ya


nyumba ya marehemu mume wake mpaka hapo atakapoolewa na
mtu mwingine au mpaka atakapokufa.
II. Sheri ya Kiislamu
• Sheria hii hutumika kwa wale waislamu wanaofuata
dini ya kiislamu ipasavyo yaani waislamu safi.
• Warithi wakuu katika sheria hii ni mke, watoto, baba na
mama wa marehemu.
Mgawanyo katika Sheria ya Kiislamu
• Wajane wote, (wasiozidi wanne) hupata 1/8 (sehemu moja ya
nane) ya mali yote ya marehemu kama ameacha watoto na
kama hajaacha watoto basi, mjane/wajane hupata 1/3 Ya mali
ya marehemu.
• Wazazi wa marehemu hupata moja ya sita (1/6) ya mali ya
marehemu.
• Watoto wa kiume wa marehemu hugawana 2/3 ya mali
inayobakia na wale wa kike 1/3.
• Ikumbukwe kuwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa kwa sheria
ya kiislamu hawarithi mali ya marehemu muislamu baba yao
hata kama ni waisilamu.

III. Sheria ya Kiserikali


Sheria hii hutumika na watu ambao si wazawa na wazawa wachache
walioachana na mila na desturi na ambao hawafuati maadili ya dini
ya kiislamu. Hata hivyo ili kufuata sheria hii inabidi uthibitisho
wa kuachana na mila utolewe mahakamani kwa wale wazawa
wanaodai kuachana na mila.

Mgawanyo ukoje katika sheria ya kiserikali.


Kama marehemu ameacha mke na watoto basi mjane atapata 1/3 na
kama mali inayobakia hugawanywa kwa watoto wote sawa sawa.
Kama marehemu hakuacha watoto, mjane atapata nusu ya mali ya
marehemu na inayo bakia wanagawiwa wazazi na ndugu wa damu
wa marehemu.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 47


Tanzania women Lawyers Association

Pale itakapothibitika kuwa marehemu aliachana na mila na desturi,


basi sheria ya kiserikali itatumika. Mfano katika kesi ya Re Innocent
Mbilinyi.

Katika kesi ya Innocent Mbilinyi ya 1969 mjane wa marehemu


aliweza kuithibitishia Mahakama kwamba mumewe alikuwa
ameachana na mila na desturi hivyo sheria ya kiserikali ilitumika
katika mirathi.

Kwa mujibu wa sheria hii ya kiserikali watoto wa nje ya ndoa


hawana haki ya kurithi mali ya marehemu baba yao pia kama ilivyo
kwa Sheria ya kiislamu.

TARATIBU ZIPI NA NI NANI ANAWEZA KUOMBA


USIMAMIZI WA MIRATHI
Taratibu za kufuata kabla ya kuomba usimamizi wa mirathi
• Mtu yeyote anapofariki jambo la muhimu kabisa la kufanya
ni kuandikisha kifo cha marehemu ili uweze kupata cheti
kitakachothibitisha kuwa mtu huyo kweli amefariki.

I. Ni wakati gani na wapi kifo kiandikishwe?


a) Ndani ya siku 30 tangu kifo kilipootokea, unatakiwa
uende ukaandikishe kifo kwa msajili wa vizazi na vifo
wa Wilaya ambaye ofisi yake ipo katika ofisi ya Mkuu
wa Wilaya.
b) Wakati wa kwenda kuandikisha hakikisha kuwa unalo
tangazo la kifo / kibali cha mazishi kutoka hospitali kifo
kilipotokea.
c) Kama alifia nyumbani lazima mwombaji awe na barua
kutoka kwa Afisa mtendaji wa Kata au Aafisa Mtendaji
wa Kijiji.
II. Cheti cha kifo kikipatikana wanandugu waje kujadili masuala
ya mirathi na kuteua mtu atakayeomba usimamizi wa mirathi
pale ambapo marehemu hakuacha wosia. Hatimaye mwombaji
wa usimamizi wa mirathi aende mahakamani akiwa na cheti

48 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

cha kifo pamoja na muhtasari wa kikao cha wanandugu.


Hili hufanyika pale ambapo hamna wosia, Kabidhi wasii
Mkuu (Msajili Mkuu) wa vizazi na vifo, pia anaweza kuomba
usimamizi wa mirathi pale ambapo:-
a. Marehemu aliacha wosia na akamteua Kabidhi Wasii
Mkuu awe msimamizi wa mirathi
b. Pale ambapo kuna mgogoro mkubwa baina ya warithi,
na mali zilizoachwa ni nyingi na za thamani, basi
mahakama kwa maombi ya warithi inaweza kutoa amri
kabidhi Wasii mkuu awe msimamizi wa mirathi
c. Warithi kwa hiari yao wanaweza kuomba kabidhi
Wasii Mkuu awe msimamizi, pale ambapo marehemu
hakuacha mke, watoto wala ndugu.

ANGALIZO: Iwapo Kabidhi Wasii Mkuu atakuwa


msimamizi ijulikane huwa atalipwa gharama za usafiri
na posho.

III. Nani aombe usimamizi wa mirathi?


Mtu yeyote mwenye uhusiano na marehemu, awe mwanamume
au mwanamke mwenye akili timamu na aliyetimiza miaka 18
anaweza kuomba kuwa msimamizi wa mirathi. Pia kabidhi
Wasii Mkuu anaweza kuomba kuwa msimamizi wa mirathi.
IV. Maombi ya simamizi yafanyike wapi?
Kwa mujibu wa taratibu za kisheria masuala ya mirathi
ambayo yatatumia sheria ya kimila au kiislamu, maombi
yafanyike katika mahakama ya Mwanzo iliokaribu na pale
ambapo marehemu amefia/ alipoishi au pale penye mali zake.
Hii italeta urahisi kwa mahakama ikitaka kutembelea eneo,
warithi pamoja na msimamizi katika ufuatiliaji wa mali za
marehemu.
V. Maombi ya usimamizi yaonyeshe nini?
a) Jina la mwombaji
b) Mahali anapoishi

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 49


Tanzania women Lawyers Association

c) Jina la marehemu, dini yake, tarehe na mahali alipofia


d) Majina ya warithi na uhusiano wao na marehemu
e) Mali za marehemu au mahali zilipo
VI. Nani atachagua sheria ipi itumike?
Si msimamizi wala ndugu wa marehemu watakaochagua
sheria ipi itumike bali maisha aliyokuwa anaishi marehemu
na nia yake ndivyo vitakavyoashiria sheria ipi itumike.
VII. Nini kazi ya msimamizi wa mirathi?
Mara nyingi wasimamizi wamedhani kuwa wao ni warithi,
la hasha! Wasimamizi wana kazi kubwa na ngumu, na iwapo
utaratibu utafuatwa hawawezi kunufaika kwa chochote kile
kwa kazi hiyo.

Kazi na wajibu wa msimamizi wa mirathi ni nini?


a) Kukusanya mali na madeni ya marehemu
b) Kulipa madeni kama yapo.
c) Kuwagawia warithi mali iliyosalia kwa kuzingatia sheria
husika katika mirathi hiyo.
d) Kutayarisha taarifa ya namna alivyogawa mirathi na
kuwakililsha mahakamani.

Msimamizi afanye nini baada ya kugawa mali za


marehemu?
Atoe taarifa jinsi alivyogawa mali za marehemu.

Msimamizi wa mirathi anatakiwa kupeleka mahakamani taarifa ya


namna alivyogawa mali za marehemu (inventory) ili mahakama
iweze kufunga jalada hilo la mirathi.

Kazi hii ikamilike baada ya muda gani?


Sheria inamtaka msimamizi awe amekamilisha kazi yake ndani ya
miezi sita tangu siku aliyopewa usimamizi wa mirathi.

50 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Akishindwa kukamilisha afanye nini?


Msimamizi wa mirathi akishindwa kukamilisha kazi yake ndani ya
miezi sita atatakiwa aiombe mahakama ile ile iliyompa usimamizi
imuongezee muda ili aweze kukamilisha kazi yake ya usimamizi.
Hapa atatakiwa atoe sababu zilizomfanya ashindwe kukamisha
kazi hiyo katika muda unaotakiwa ili kuiridhisha mahakama na
hivyo kumuongezea muda.

Je msimamizi wa mirathi aweza kuwa mrithi?


Ndiyo, msimamizi aweza kuwa mmoja wa warithi ili mradi asifuje
mali za marehemu.

Nini kifanyike msimamizi anapofuja mali za marehemu


Pale msimamizi anapofanya kazi kinyume na utaratibu ulioelezwa
hapo juu, basi nenda kwenye mahakama ile ile iliyompa usimamizi
upeleke maombi ya kuomba afutiwe usimamizi. Utakapoenda
mahakamani eleza sababu zilizokupelekea kufanya hivyo.

Pamoja na kuomba afutiwe usimamizi wa mirathi, unaweza pia


kumfungulia kesi ya madai ukieleza mali alizofuja na hivyo kuiomba
mahakama imuamuru azirudishe au azilipe mali hizo pamoja na
gharama za kuendesha shauri la madai.

ANGALIZO: Ieleweke pia kuwa ni kosa la jinai kwa


msimamizi kufuja mali za marehemu

Je mjane afanye nini ili msimamizi asifuje mali na


kudhulumu mali za marehemu?
Iwapo mke wa marehemu utakuwa na mashaka na msimamizi wa
mirathi, mara tu msimamizi anapoteuliwa nenda mahakamani,
fungua kesi ya kuomba ugawiwe nusu ya mali aliyoacha marehemu
mume wako, hapo hapo omba mahakama itoe amri kuwa mali ya
marehemu isigawiwe mpaka hapo kesi yako itakapomalizika.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 51


Tanzania women Lawyers Association

Watoto wanalindwaje dhidi ya msimamizi mbadhilifu?


Sheria inaeleza wazi kuwa kama marehemu ameacha mtoto au
watoto wadogo wa chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) lazima
mahakama iteue wasimamizi wa mirathi wasiopungua wawili.
Hata kama marehemu hakuacha mtoto mdogo vile vile sheria hiyo
inasema kama marehemu ameacha mrithi ambaye ni mlemavu
basi mahakama lazima iteue wasimamizi wa mirathi wasiopungua
wawili.

Je kuna sheria inayolazimisha kutoa tangazo la miezi mitatu (3)


kabla ya kumteua msimamizi wa mirathi?

Hakuna sheria ya namna hiyo hata kidogo, huo ni utaratibu


uliowekwa na mahakama.

ANGALIZO: kesi zote za mirathi ambazo ni za kimila


na za kidini ( kiislamu) zitatakiwa kufunguliwa katika
mahakama za mwanzo. Kesi zote za mirathi ambazo ziko
chini ya sheria ya serikali au kikristo zitatakiwa kufungulia
katika mahakama ya wilaya au ya hakimu mkazi. Kesi
ambazo i azikufunguliwa baada ya muda wa mwaka kupita
zitafunguliwa katika mahakama kuu.

WOSIA
Wosia ni kitu muhimu sana kwani unaondoa migogoro mingi katika
familia na kuwapunguzia matatizo wale wanaobaki, baada ya mtoa
wosia kufariki hasa kwa wale ambao ni warithi.

Wosia ni tamko linalofanywa na mtu yeyote kwa mdomo au kwa


maandishi likionyesha jinsi anavyotaka mali yake igawanywe au
isimamiwe baada ya kifo chake, na jinsi mazishi yake yatakavyokuwa.
Ni muhimu kila mtu mwenye miaka kumi na nane au zaidi ajue
jinsi ya kuandika wosia na aandike, bila kujali mila zisemazo mtoto
mwenye baba hata kama mtoto huyo ni mtu mzima kabisa mwenye
mke au mume na watoto na mali haruhusiwi kuandika wosia wakati
baba yake angali/ akiwa hai.

52 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Wosia katika sheria za kimila

Kuna aina mbili za wosia katika sheria za kimila nazo ni :-


• Wosia wa maneno
• Wasia wa maandishi

Wosia wa maneno
Wosia huu unapaswa kushuhudiwa na mashaidi wasiopungua
wanne na wawili kati ya hao lazima wawe ni wanaukoo wa huyo
mwosia. Wosia wa aina hii unaweza kufutwa kwa wosia mwingine
wa mdomo au wa maandishi.

Wosia wa maandishi
Wosia wa maandishi unatakiwa uandikwe kwa kalamu isiyofutika
au upigwe chapa. Ni muhimu na lazima wosia huu uwe na tarehe.

Wosia wa maandishi ni lazima ushuhudiwe na watu wawili


wanaojua kuandika na kusoma. Kama anayetoa wosia hajui kusoma
na kuandika basi atatia sahihi ya kidole gumba cha mkono wake
wa kulia na wosia wake utashuhudiwa na watu wanne wanaojua
kusoma na kuandika.

Mashahidi wote kwa pamoja lazima wawepo kwa wakati mmoja


mwosia anapotia sahihi katika wosia wake na wote lazima watie
sahihi katika wosia huo.

Mambo ya kuzingatia katika wosia


Mtu anayeandika wosia anatakiwa awarithishe warithi wa malli
zake na mtu mwingine yeyote anayetaka mweneyewe kumrithisha
mali zake, lakini anatakiwa asirithishe rafiki sehemu kubwa kuliko
ile ya warithi halali kisheria.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 53


Tanzania women Lawyers Association

Je mwosia anaweza kumnyima mrithi halali urithi?


Katika hali ya kawaida mwosia anatakiwa amrithishe kila mrithi
halali mali zake isipokuwa kama:-
• Mrithi amezini na mke wa mwosia.
• Mrithi amejaribu kumuua, kumshambulia au kumdhuru
vibaya mwosia au kumtendea mama wa mwosia mambo
mabaya yaliyotajwa hapo juu.
• Bila sababu ya kuridhisha Yule anayestahili kurithi kushindwa
kumtunza mwosia wakati wa shida ya maradhi au njaa.
Iwapo mwosia ataamua kutomrithisha mrithi halali kutokana na
sababu yoyote hapo juu, atatakiwa kutaja sababu za kutofanya
hivyo katika wosia wake.

Wosia katika sheria ya kiserikali


Wosia katika sheria za kiserikali hauna tofauti na wosia katika sheria
za kimila, ule wa aina ya maandishi. Vipengele vyote vya wosia wa
maandishi vinatumika.

Mwosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa


kuandika maandishi mengine (codicil) ambayo yatasomwa pamoja
na yale ya awali. Maandishi haya lazima yazingatie uandikaji wa
wosia na ni lazima yawe na tarehe.

Kumbuka: Ni vizuri mtu akaandika wosia ili kuepusha


mgogoro kwenye mirathi.Ukiandika wosia mbele ya Wakili/
hakimu bila kuwa na mashahidi waliotajwa hapo juu basi
wosia wako utakuwa batili.

Mume au mke anapokufa, nani anarithi ardhi?


Suala la urithi, hapa Tanzania lina shughulikiwa na sheria tofauti
ambazo ni sheria za kimila, sheria za kiislamu na sheria ya kiserikali.

Sheria za kimila hutumika kwa watanzania wote wazawa wasio na


asili ya kiasia , kizungu au kisomali. Hata hivyo endapo mahakama

54 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

itadhirika kuwa mzawa huyo aliacha kabisa mila na desturi za


kabila lake, mahakama inaweza kutumia sheria ya kiserikali.

Sheria ya kiislamu inawahusu watanzania ambao mahakama


itaridhika kuwa waliacha mila zao na ambao uislamu huwaongoza
katika Nyanja na desturi zote za maisha.

Sheria ya nchi (Indian Succession Act 1865), hutumiwa na watanzania


ambao wameridhika kuwa wameacha mila na desturi zao na ambao
ni wakristo.

Ni vyema watu wakajenga tabia ya kutafuta ushauri wa kuandika


wosia unaokubalika kisheria ili kukidhi na kulinda matakwa.

Sheria za ardhi zinaruhusu mke na mke na mume kuandikisha


ardhi yao katika mafungu yasiyogawanyika.(joint occupiers). Iwapo
wanandoa watafanya hivyo, basi pale anapofariki mume, mke
atarithi ardhi au pale atakapofariki mke mume anarithi ardhi.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 55


Tanzania women Lawyers Association

Ufuatao ni mfano mmojawapo wa wosia wa Maandishi

Mimi………………………………………ninayeishi (taja mahali)


S.L.P………………………, nikiwa na akili timamu nabatilisha
wosia amabazo niliwahi kutamka au kuandika kabla ya tarehe
ya leo na kutangaza huu ndiyo wosia wangu wa mwisho.

Tarehe………………………

Na kwa wosia huu namrithisha:-


1 ………………………………………mke wangu, nyumba
iliyopo………………………..
2 ………………………motto wangu wa kwanza wa kike
nyumba Na. ……………….. iliyopo…………….
3 ………………………..mtoto wetu wa kiume nyumba na
shamba lililoko……………………………………n.k
Kwa wosia huu ninamteua……………………………………..kuwa
msimamizi na muamana wa wosia huu. Kwa kushuhudia hayo
yaliyoelezwa ninaweka sahihi yangu katika siku ya mwaka
ulioelezwa hapo juu.

Imewekwa sahihi na mwosia

Hapa…………….siku ya…..….…….mwezi wa……….mwaka 200…..

Mbele yetu sisi wawili kwa wakati mmoja katika muda huu
kutokana na matakwa yake mwenyewe nasi tunaweka majina
na sahihi zetu hapa chini kama mashahidi:-
1. Jina la shahidi……….. 2. Jina la shahidi…………
Sahihi………………….. Sahihi …………………….
Kazi………………….…. Kazi……………………….

Tarehe………..………. Tarehe…………………….

56 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

  Sura ya Saba   Tanzania  women  Lawyers  Association  


 
 
UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI
UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI
UTARATIBU WA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA
UTARATIBU WA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA VYOMBO VYA SHERIA
VYOMBO VYA SHERIA
MAHAKAMA YA RUFAA
Itashughulikia rufaa toka Mahakama
Kuu kitengo cha ardhi  

MAHAKAMA KUU – MAHAKAMA KUU


KITENGO CHA ARDHI Mahakama hii ina uwezo
Itashulikia rufaa za sawa na mahakama kuu –
maamuzi ya Baraza la kitengo cha ardhi. Kwa iyo
Inashulikia rufaa za maamuzi
Ardhi na Nyumba la Wilaya
ya Baraza la Ardhi na
na mashauri yatakayokua
Nyumba la Wilaya na
na uwezo wa kusikiliza na
mashauri yatakayokua na
mahakama hii.  
uwezo wa kusikiliza na
mahakama hii.  

BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA


WILAYA
Wajumbe wake na kazi zake
huanishwa na sheria husika  

BARAZA LA KATA
Wajumbe wasiopungua 6 wala kuzidi 8
Kazi:- Kutatua migogoro ya ardhi
katika kata husika
Kupokea rufaa toka baraza la ardhi la
kijiji  

BARAZA LA KIJIJI
Wajumbe 7 kwa ujumla na kati yao
wanawake wawe watatu au zaidi
Kazi:- Kusuluhisha migogoro ya ardhi
  katika eneo la kijiji husika
- Kupokea rufaa toka maamuzi ya  
Mwongozo
Mwongozo wa Taratibu
wa Taratibu za KisheriazaKatika
Kisheria
kamati Umiliki Katika
wa Ardhi
ya ardhi
Umiliki wa Ardhi  
ya kijiji   57
41
Tanzania women Lawyers Association

Katika shughuli za kugawa, kumiliki au kurithi au kurithi ardhi,


mara nyingi watu hutofautiana kimawazo na kiutendaji na hivyo
kusababisha migogoro. Katika Migogoro kama hiyo mwenye haki
yake kuhusu kumiliki au kurithi ardhi inayogombewa itapatikana
tu kwa kutumia sheria. Kama ilivyoelezwa hapo juu, tume ya rais
ya ardhi iliona tatizo hili na kupendekeza kuwa kuwepo na mfumo
unaoeleweka utakaoshughurikia utatuzi wa migogoro inayotokana
na umiliki na ugawaji wa ardhi. Sheria za ardhi zimezingatia msingi
huu na zimeweka vyombo na utaratibu wa kusuluhisha na kutatua
migogoro hiyo huku sheria hizo zikitoa mwanya kwa wanawake
kudhiriki katika mabaraza mbali mbali ya utatuzi wa migogoro ya
ardhi.

Kwa mujibu wa sheria za ardhi mahakama na mabaraza yafuatayo


ndio yatashughulikia utatuzi wa migogoro hiyo:-
• Mahakama ya Rufaa
• Mahakama Kuu na Mahakama Kuu – Kitengo cha Ardhi
• Baraza la Ardhi na nyumba la Wilaya
• Baraza la Kata
• Baraza la Ardhi la Kijiji
• Kamati ya maamuzi ya ardhi ya Kijiji (Kamati hii inaundwa
pale tu ambapo kutaonekana na haja ya kamati hiyo kuundwa)

Kamati ya Maamuzi ya Kijiji


Kamati hii ina wajumbe wasiozidi 9 ambapo wajumbe wasiopungua
4 watakuwa ni wanawake. Wajumbe hawa watatumikia kwa kipindi
cha miaka mitatu. Kikao hiki pia kitakuwa iwapo tu kitakuwa na
wajumbe wasiopungua 5. Kikao halali cha kamati pia lazima kiwe
na wanawake. I wapo wanawake watakuwa pungufu ya wawili
kikao hakitakuwa halali.

Kazi za Kamati ya Maamuzi ya Kijiji


- Kutambua ardhi ya Kijiji na mipaka yake
- Kutenga au kuweka akiba ya ardhi au kutoa mipaka ya haki

58 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

ya njia na haki zingine za kutumia njia ambazo itaziona ni


muhumu kwa umiliki bora wa ardhi.
- Kulinda maslahi ya wanawake, watoto, walemavu na
wanakijiji wasiokuwepo kijijini kwa nyakati fulani kwa
sababu maalum mfano wafungwa, wanakijiji wanaofanya kazi
sehemu nyingine n.k

Rufani
Kwa mtu ambaye atakuwa hajaridhika na uamuzi wa kamati
ataweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo kwenye baraza la
ardhi la kijiji ndani ya siku thelathini (30) baada ya kutolewa kwa
kumbukumbu.

Baraza la Ardhi la Kijiji


Kwa mujibu wa Sheria ya Vijiji, Baraza la Ardhi la Kijiji linaundwa
na wajumbe 7 na kati yao ni lazima wawepo wajumbe wanawake
wasiopungua watatu. Wajumba hawa watatumikia kwa kipindi cha
miaka mitatu. Kikao halali cha kamati hii kitakuwa na wajumbe 4
na lazima kiwe na wajumbe wanawake wasiopungua wawili.

Sifa za wajumbe.
Mtu hatateuliwa kuwa mjumbe kama:-
a. Si mkazi mwenyeji wa kijiji ambacho Halmashauri inaendesha
kazi zake;
b. Ni mbunge
c. Ni hakimu mwenye mamlaka kwenye Wilaya ambayo ndimo
ilimo Halshauri ya kijiji itakayoendesha shughuli
d. Ni mtu aliye chini ya miaka kumi na nane
e. Ni mtu mwenye matatizo ya akili
f. Ni mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kuhusiana
na kukosa uaminifu au kukosa maadili
g. Mtu asiye raia wa chi hii

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 59


Tanzania women Lawyers Association

Kazi za Baraza la Ardhi la Kijiji.


1. Kupokea malalamiko juu ya masuala ya ardhi
2. Kuitisha kikao ili kisikiliza malalamiko juu ya migogoro ya
ardhi.
3. Kusuluhisha na kusaidia pande zote mbili zinazohusika na
mgogoro wa ardhi kufikia maafikiano kindugu ndani ya eneo
ambalo baraza husika lina mamlaka

Baraza la ardhi la kijiji litafanya shughuli zake za


usuluishaji kwa kuzingatia-
1. Misingi yoyote ya kimila ya usuluishaji
2. Haki ya asili kadri inavyo wezekana iwapo misingi ya
usuluishaji wa kimila haitoshi;
3. Misingi yoyote na uzoefu wa usuluishi unao tokana na
mafunzo ambayo wajumbe wamekwisha pata.
Jukumu kubwa la Baraza la Ardhi la kijiji ni kutatua migogoro yote
kijijini inayohusiana na maswala ya ardhi.

Rufani
Kwa mtu ambaye atakuwa hajaridhika na uamuzi wa Baraza la
Ardhi la Kijiji ataweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo kwenye
baraza la kata.

BARAZA LA ARDHI LA KATA


Baraza la kata linaundwa na wajumbe wasio pungua wa 4 na wasio
zidi 8. Kati ya hao lazima wawepo wanawake wasiopungua wa 3.
Kikao halali cha baraza la kata kitakua na wajumbe 3 wakiwemo
wanawake wasiopungua mjumbe mmoja.

Sifa za wajumbe hawa zinapatikana kwenye kifungu cha 5 na 6 cha


sheria ya mabaraza ya kata. Mtu hata teuliwa kuwa mjumbe kama :-
1. Ni mbunge
2. Ni mbunge wa armashauri wa kijiji au kamati ya kata

60 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

3. Ni mtumishi wa serikari
4. Ni mwanasheria au mtu yeyote aliye ajiriwa katika idara ya
mahakama
5. Ni mtu ambaye haja timiza umri wa mmiaka 18
6. Ni mtu ambaye ametiwa hatiania kwa kosa la kukosa uaminifu
7. Ni mtu ambaye si raia wa Tanzania

Kazi, Mamlaka na Taratibu za Baraza la Kata.


Baraza la Kata lita pokea rufaa kutoka baraza la Ardhi la kijiji na
kutolea maamuzi

Kwa ujumla kazi ya Baraza la Kata itakua ni kuhakikisha kuna


amani na usalama katika kata husika kwa kusuruisha migogoro ya
ardhi na kuwasaidia wahusika wa migogoro kufikia muafaka unao
ubaliwa na pande zote mbili zilizo na mgogoro.

Baraza la Kata lina mamlaka ya kuchunguza na kutoa maamuzi juu


ya maswala yote yatokanayo na sheria za ardhi za mwaka 1999.

Baraza katika kusuruisha migogoro litazingatia misingi ya usuluishi


ya kimila, haki asilia pale mbapo misingi ya kimila haitumiki na
misingi yoyote ya usuluishi ambyo wajumbe wamepewa mafunzo
kwayo.

Baraza la Kata litafikia uamuzi kwa kusuluisha na linaweza


kuahilisha kikao cha baraza pale ambapo litaona kuwa kwakufanya
hivyo litaweza kufikia maamuzi ya kidugu.

Uwezo na Uwakilishi katika Balaza la Kata


Baraza la kata lina uwezo wa kusikiliza na kusuluhisha migogoro ya
ardhi au mali (mfano nyumba) yenye thamani isiyo zidi milioni 3.

Mawakili hawaruhusiwi kuwakilisha watu wenye migogoro ya


ardhi katika Baraza la Kata. Sheria imetoa mwanya kwa ndugu wa
karibu au mtu wa familia moja kumwakilisha mtu mwenye mgogoro
wa ardhi katika Baraza la Kata endapo tu ataliomba Baraza kwamba
mtu huyo amuwakilishe

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 61


Tanzania women Lawyers Association

Rufani
Kwa mtu ambaye atakua hajaridhika na uamuzi wa Baraza la Kata
ataweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo kwenye Baraza la Ardhi
na nyumba la Wilaya.

BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYA


Lugha inayo tumika katika Balaza hili ni Kiingereza au Kiswahili

Baraza hili linaundwa na Mwenyekiti na wazee wa Baraza 2.


Kikao halali cha Baraza hili kina jumuisha Mwenye kiti na wazee
2 wa Baraza. Katika kutoa maamuzi mwenyekiti atazingatia
maoni ya wazee wa baraza lakini halazimiki kufuata maoni hayo
kama hakubaliani nayo na atatoa sababu zake iwapo ataamua
kutokukubaliana nao.

Mwenyekiti wa Baraza atateuliwa na Waziri wa Ardhi. Sifa ya


mwenyekiti ni lazima awe Mwanasheria na ata shika wadhifa huo
kwa kipindi cha miaka 3.

Waziri atateuwa wazee wa Baraza si zaidi ya 7 baada ya kushauriana


na Mkuu wa Mkoa husika na kati ya hao wazee lazima kuwe na
wanawake wasiopungua 3.

Wazee wa Baraza watakua na wadhifa huu kwa kipindi cha miaka 3


lakini wanaweza wakateuriwa tena kwa kipindi kingine.

Sifa za wazee wa Baraza:-


1. Awe mkazi wa Wilaya husika
2. Asiwe Mbunge, Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya,
Halmashauri ya Kijiji, Baraza la Ardhi la Kijiji, Kamati ya
Maamuzi ya Ardhi ya kijiji.
3. Awe na akili timamu
4. Asiwe mtu ambaye amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai
au kwa kosa la uaminifu.
5. Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

62 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Kazi, Mamlaka na Taratibu za Baraza la Ardhi na


Nyumba la Wilaya
Baraza hili litapokea rufaa kutoka Baraza la Kata.
Baraza hili lina uwezo wa kusikiliza na kutoa maamuzi ya migogoro
ya ardhi au mali (mfano nyumba) yenye thamani isiyopungua milioni
hamsini (50) kwa mali isiyo hamishika na kwa inayohamishika
milioni arobaini,(40).

Baraza litaweza kuita shauri toka Baraza la kata kwa ajili ya kupitia
mwenendo mzima wa shauri husika ili kujiridhisha kama uamuzi
wa Baraza la Kata haujakiuka sheria zilizopitishwa na Bunge ama
sheria ndogo. Pia Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya linaweza
kufanya hivyo ili kutazama kama maamuzi ya Baraza la Kata
halijakiuka haki asili au kama uamuzi ulitolewa na Kikao halali.
Pia Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya laweza kufanya hivyo
ili kujiridhisha kama Baraza la Kata halikusikiliza mgogoro ambao
haupo chini ya mamlaka yake.

Uwakilishi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.


Mtu mwenye mgogoro wa ardhi anaweza kusimama mwenyewe
kujitetea mbele ya Baraza ua kuwakilishwa na Wakili ama ndugu
wa karibu au mtu wa familia.

Rufani
Kwa mtu ambaye atakua ajaridhika na uamuzi wa Baraza hili
ataweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo kwenye mahakama
kuu kitengo cha ardhi ndani ya siku 60 toka siku uamuzi huo
ulipotolewa.

MAHAKAMA KUU NA MAHAKAMA KUU -


KITENNGO CHA ARDHI
Mahakama kuu kitengo cha ardhi Iliundwa na kuanza kazi mwaka
2003.
Kikao halali cha mahakama hii ni Jaji mmoja na wazee wa Baraza
wawili. Lakini kuanzia mwaka 2011 mahakama kuu ya Tanzania

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 63


Tanzania women Lawyers Association

ilirudishiwa uwezo tena wa kusikiliza mashauri ya ardhi kutokana


na kuzidiwa kwa kitengo cha mahakama kuu kitengo cha ardhi.

Uwezo na Mamlaka ya Mahakama Kuu hizi


Mahakama hizi zina uwezo wa:-
1. Kupokea rufaa kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
na kuitolea maamuzi.
2. Kusikiliza na kutoa maamuzi ya migogogro ardhi au mali
(mfano nyumba) yenye thamani inayo zidi milioni hamsini
kwa mali isiyo hamishika na kwa inayo amishika inayo zidi
milioni arobaini
3. Kusikiliza kesi zote chini ya sheria ya Uwekezaji ya mwaka
1997, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na Sheria ya utaifishaji
wa Ardhi kwenye kesi ambazo serikari inahusika.
4. Kusikiliza kesi zote zinazo husisha Mashirika ya Umma na
kesi nyingine ambazo umma una maslahi.
5. Kusikiliza kesi zote za ardhi zitokanazo na sheria nyingine
ambazo haziko chini ya mamlaka ya Baraza au mahakama.

Mahakama hii inayo mamlaka ya:


1. Kuitisha na kukagua mienendo ya kesi ya Mabaraza yote
ya ardhi ya Wilaya muda wowote, na kutoa maagizo kama
itakavyo onekana inafaa ili haki itendeke na mabaraza yote ya
Wilaya yatalazimika kufuata maagizo hayo.
2. Kuita mashauri toka mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya
kwaajili ya kupitia mwenendo mzima wa mashauri hayo
kuona kama mabaraza yametoa uwamuzi unao toa haki. Kama
itaonekana kulikuwepo makosa ambayo yamesababisha haki
isitendeke mahakama itabadilisha uamuzi huo, jinsi itakavyo
ona inafaa.

Rufani
Kwa mtu ambaye atakua hajaridhika na uamuzi wa Mahakama hii
ataweza kukata rufani dhidi ya uwamuzi huo kwenye Mahakama
Kuu ya Rufani na taratibu za kukata rufaa kwenye Mahakama ya

64 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

Rufaa zitakua ni zile za sheria ya Mahakama ya Rufaa za mwaka


1979. Ni utaratibu uleule unao fuatwa kwenye kesi nyingine zisizo
za ardhi. Mahaka ya Rufaa ndio Mahakama ya juu kabisa na mtu
ambaye hataridhika na uamuzi huo utakaotolewa hapa hatakua na
mahali pengine pa kukata rufaa.

MAKOSA YA JINAI YALIYO HAINISHWA NA


SHERIA YA ARDHI
Kwakuwa ardhi ni swala nyeti kwa jamii hasa kwaajili ya kilimo na
ujenzi, wapo watu ambao wangetaka kujinufaisha pasipo kuwa na
haki katika utaratibu mzima wa upatikanaji wa ardhi. Hivyo katika
kuhakikisha kuwa matendo maovu yanadhibitiwa Sheria za ardhi
zimefafanua matendo mbalimbali ambayo yatahesabiwa kama
makosa ya jinai katika masuala ya ardhi

1) Ni kosa la jinai kwa mtu:-


Kutoa matamko ya uwongo kwa maneno au maandishi, akijua kuwa
ni uwongo, kuhusiana na ardhi au maswala mengineyo yaliyo chini
ya sheria hii au akiwa anafahamu atatoa taarifa ya uongo au kutoa
matamko ya uongo aidha kwa maneno au maandishi kuhusiana
na uchunguzi wowote kuhusu kosa lolote chini ya sheria hii.Kwa
udanganyifu kujipatia Usajiri au kupatia haki yoyote ya hakimiliki,
hakimiliki ya kimila au kwa waraka wowote au hawala yoyote
inayo husu ardhi.

Kuingiziwa tarakimu au idhini au jambo lolote kwenye nyaraka


kama hizo au hawala iliyo tajwa hapa juu au kufuata au kurekebisha
chochote kati ya nyaraka zilizo tajwa hapo juu ya hawala au maingizo
au idhini kwa udanganyifu ikibadili, kuongeza, kufuta, kuvuruga,
kukatakata au kuaribu nyaraka zozote au nyaraka zinazo husiana na
ardhi au maingizo au idhinisho kwenye nyaraka au hawala;Kuzuia
au kuficha waraka wowote muhimu, ukweli au jambo lolote au
kusaidia au kuchochea vitendo kama hivyo kwa kamishna, msajiri,
Afisa yeyote aliye idhinishwa au Afisa wa Halmashauri ya kijiji
mwenye mamlakma kwa mujibu wa sheria hii.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 65


Tanzania women Lawyers Association

Adhabu:-
Mtu atakayetenda makosa yaliyoainishwa hapo juu atahukumiwa
adhabu ya faini isiyo zidi shilingi milioni moja au kifungo cha muda
usio zidi miaka mitatu jela au adhabu zote mbili, yaani faini na
kifungo.

2) Ni kosa la jinai
Kwa mtu bila sababu ya kuridhisha kushindwa kutoa waraka
wowote kama inavyo hitajika chini ya sheria hii.

Adhabu
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa hili ata hukumiwa adhabu ya
faini isiyozidi shilingi hamsini elfu au kifungo kisichozidi miaka
mitatu au vyoteiwili.

3) Nikosa la jinai
Kwa mtu kukalia ardhi kinyume cha sheria.

Adhabu
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa hili atahukumiwa faini isiyozidi
shilling za kitanzania miatan o kila siku atakayo endelea kufanya
kosa.

4) Nikosa la jinai
Kwa mtu yeyote kwa makusudi kuzuia au kuingilia haki ya njia kwa
Umma, na akashindwa kuondoa kizuizi hicho au kuacha kuingilia
haki hiyo ya Umma ndani ya wakati unao ainishwa katika notisi
yoyote aliyo pelekewa.

Adhabu
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa hilo ataukumiwa faini isiyo
zidi shilingi elfu kumi au kama ataendelea kutenda kosa hili
atapata adhabu ya faini isiyo pungua shilingi mia mbili kila siku
atakayoendelea kutenda kosa hili.

66 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

5) Nikosa la jinai
Kwa mtu yeyote kwa makusudi atakawiza kuzuia, kuziba,
kuogopesha, au kumpinga mtu yeyote aliye idhinishwa chini ya
sheria hii kuingia na kukagua ardhi kwa zoezi halali la mamlaka
aliyo pewa.

Adhabu
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa hilo atahukumiwa faini
isiyopungua shilingi laki moja au kifungo kisicho pungua muda wa
mwaka mmoja au vyote viwili, faini na kifungo.

6) Ni kosa la jinai
Iwapo mtu yeyote ama katika hali ya kawaida au katika kutekeleza
jukumu maalumu au vinginevyo ataingia isivyo halali au kwa
nguvu kwenye ardhi au wakati akikalia ardhi hiyo au kuharibu kitu
chochote cha hasili kwenye ardhi hiyo au kinacho milikiwa na mtu
yeyote anaye tumia ardhi hiyo au kuharibu madhao yaaliyooteshwa
au majengo yaliyoko kwenye ardhi, mtu huyo atakuwa ametenda
kosa la jinai.

Adhabu
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa lililotajwa hapo juu atahukumiwa
faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo kisicho zidi miezi
mitatu au vyote viwili, faini na kifungo.

Chini ya kifungu cha 63 cha Sheria ya Ardhi ya kijiji mtu akitiwa


hatiani na ikaonekana kuwa alikwisha faidika kimasilahi kwa
kukalia ardhi isivyo halali, mahakama itakuwa na uwezo wakutoa
hadhabu ya ziada na itatoa agizo kuhusu maslahi yaliyo patikana
kushikiliwa Ili kuhakikisha kuwa mtu hafaidiki kutokana na makosa
yake.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 67


Tanzania women Lawyers Association

Sura ya Nane
ULINZI WA MWANAMKE DHIDI YA
VIPENGELE VYA KUBAGULIWA
Ni muhimu pia kutambua kwamba haki za kijamii, kiuchumi
na kisiasa zimetambuliwa na kulindwa na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Inatakiwa wakati wa kuangalia haki za
wanawake kwenye maswala ya ardhi kuzingatia katiba ya nchi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inatambua haki
ya wanawake kwenye ardhi kwa kuzuia ubaguzi na kutilia mkazo
usawa wa watu wote. Kwenye

Ibara ya 12; Bniadamu wote ni sawa.

Ibara ya 13(i), inaeleza kwamba “watu wote ni sawa mbele ya sheria


na wanastahili pasipo ubaguzi wa aina yoyote usawa na ulinzi
mbele za sheria”.

Ibara ya 24(1), ni mahususi kwenye haki ya kumiliki mali kwamba


“kila mtu ana haki ya kumiliki mali”.

Endapo mali hiyo itanyang’anywa au kuchukuliwa mwathirika


atastahili fidia ya haki, kamili na halali. Kwa ujumla vifungu hivi
vinaweka bayana haki ya mtu kumiliki mali pasipo ubaguzi wala
upendeleo wa kijinsia nk.

Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi ya Bernado Ephrahim vs.


Holaria Pastory and Gervazi Kazirege Civil Appeal No. 70/1989
iliamua kwamba mila za kibaguzi zinakinzana na Katiba.

MIKATABA YA KIMATAIFA
Tanzania kama mjumbe wa Umoja wa Mataifa (UN) inawajibu
kutoa haki sawa kwa wanawake na wanaume kama ilivyoainishwa
kwenye Katiba ya Umoja huo (UN Charter) na Tamko la Haki za
Binadamu (UDHR)). Mkataba wa kuzuia aina zote za ubaguzi dhidi

68 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

ya wanawake (CEDAW)) na Mkataba wa Africa wa nyongeza wa


Haki za Wanawake (APRW)) pia unatoa ulinzi wa jumla dhidi ya
ubaguzi na ulinzi wa kipekee kwenye mageuzi yanayohusu sekta
ya ardhi.

Mali ya Familia
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 pia inatamka kwamba ridhaa ya
mwenzi lazima ipatikane kwenye uhawilishaji wa ardhi kama vile
kuuza, kukodisha, kupangisha au kuweka rehani.

Kwa mujibu wa sheria hii, ridhaa ya mke lazima ipatikane pale


nyumba ya familia inapohitajika kuuzwa, kuwekwa rehani au
kuhawilishwa kwa namna nyingine.

Kama ridhaa hiyo haijapatikana mauziano hayo yanaweza kuwa


batili.

Kwa mujibu wa sheria hii ya ndoa, mwanamke aliyeolewa ana


haki ya kujipatia kushikilia au kuuza mali inayohamishika au
isiyohamishika wakati wa kipindi cha ndoa na haki ya kugawa
mali waliyoichuma kwa pamoja kati ya mke na mume pale ndoa
itakapovunjika.

Sheria ya ndoa imeeleza kuwa wanandoa wana haki ya kumiliki


mali binafsi.

Pale panapokuwa wake wawili au zaidi, wote wanakuwa na haki


sawa katika nyumba na mali ya familia.

Mali ya familia (wanandoa) inaweza kugawanywa endapo


mwanandoa anaweza kuthibitisha thamani aliyoweka katika
mali hiyo. Wakati huo huo, katika kipindi cha ndoa, pale mali
inapoandikwa kwa jina la mume au mke, inachukuliwa kwamba
mali hiyo ni Yule ambaye jina lake limeandikishwa peke yake. Pale
wanandoa wanaposajili mali ya familia kwa pamoja kwa majina yao
ndipo wanakuwa na haki na maslahi sawa katika mali hiyo (ardhi/
nyumba).

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 69


Tanzania women Lawyers Association

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi mahakama zinatakiwa kuangalia


jinsi mwanamke atakavyoathirika pale inapokusudia kutoa amri ya
kusitisha upangaji au nafuu nyingine chini ya amri hiyo.

Sheria hii ya ardhi inatamka bayana kuwa mmiliki wa ardhi mwenye


hati ya kugawiwa pamoja na wapangaji wa muda mrefu anaweza
kuweka rehani haki yake au sehemu ya haki kwa ajili ya mkopo au
deni lililopo. Ridhaa ya wanandoa wote kabla mali ya wanandoa
haijawekwa rehani inahitajika. Wategemezi wa mkopaji ambaye
ardhi yake inaelekea kunyang’anywa wanaweza kupeleka maombi
mahakamani kwamba masharti ya mkopo yalilenga kuwaingiza
kwenye matatizo. Kwa vyovyote hii inapaswa kujumuisha pia
maswala ya jinsia.

KIMILA
Mali ya wanandoa iliyoko chini ya hati ya kimila ambayo imeingia
kwenye hatari ya kuchukuliwa na mkopeshaji inalindwa na
sheria. Hati ina maana zaidi kwa wanawake kwa jinsi inavyotoa
ulinzi wa baadaye hata pale ambapo haki ya mwanamke kutoa
ridhaa haikuzingatiwa pale awali. Lakini hata pale mali ilipokuwa
inamilikiwa na mwanamke na anaona kwamba masharti hayakuwa
ya haki au wazi wakati wa kuingia kwenye makubaliano anaweza
kupata msaada wa baraza la ardhi la kijiji kuhakikisha kwamba
mali (ardhi/nyumba) haichukuliwi kirahisi. Hata kama ulinzi huu
ulilenga kulinda ardhi ya kijiji na sio mali ya familia ulinzi huo kwa
vyovyote vile utamnufaisha mmiliki wa ardhi familia au mali ya
wanandoa.

Maslahi ya Wanawake kwenye Umiliki-Pamoja


Sheria ya Ardhi inaruhusu umiliki wa pamoja wa ardhi ambapo
mwanamke anaweza kumiliki ardhi kwa umoja au kwa pamoja Pale
ambapo ardhi inamilikiwa kwa umoja, uhawilishaji wake unaweza
kufanywa tu endapo wamiliki wote watahusika; pale mmojawapo
anapo fariki, haki au maslahi yake kwenye ile mali itachukuliwa
na yule mmiliki aliyebaki hai au wamiliki waliobaki hai. Mmiliki
wa umoja anaweza kuhamisha haki yake kwenda kwa wamiliki

70 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

wengine tu na sio mtu mwingine, jaribio lolote la kuhamisha haki


yake kwenda kwa mtu nje ya umoja huo ni batili. Sheria imetamka
bayana kwamba umiliki pekee wa umoja ni kati ya mke na mume.
Huu ni ulinzi wa kisheria wa dhahiri wa mali ya wanandoa na hivyo
kuwaleta pamoja wanandoa kusimamia mali ya familia.

Pale mwanandoa (mwenzi) anapopata ardhi chini ya haki ya


umili kwa ajili ya umiliki wa pamoja au kwa matumizi ya wenzi
(wanandoa), na pale kunapokuwepo na mke zaidi ya mmoja au wenzi,
kunakuwepo na nadharia kwamba wenzi hao wata miliki ardhi
hiyo chini ya umiliki wa pamoja. Endapo nadharia (presumption)
hiyo haijaweza kupingwa basi msajili atapaswa kusajili wenzi hao
kama wamiliki wa pamoja. Tofauti ni pale tu ambapo kuna kifungu
kwenye hati ya umiliki (certificate of occupancy) au hati miliki ya
kimila (certificate of customary right of occupancy) kinacho bainisha
kwamba mwenzi anamiliki haki hiyo ya umiliki peke yake au wenzi
wanamiliki haki hiyo kwa pamoja. Pale ambapo ardhi iliyoko chini
ya haki ya umiliki inamilikiwa kwa jina la mwenzi mmoja lakini
mwenzi mwingine au wengine wamechangia kwa nguvu kazi yao
kwenye uzalishaji, utunzaji na uendelezaji wa ardhi, wenzi hao
watakuwa wamepata haki ya kuwafanya wamiliki wa pamoja kwa
nguvu kazi yao.

Pia, mwenzi anayemiliki ardhi kwa jina lake mwenyewe na


akataka kuuza ardhi au nyumba ya kuishi ni lazima achukue
hatua kadhaa kuthibitisha kwamba hakuna wenzi wengine. Kama
kuhawilishaji ni uwekaji rehani, mkopeshaji lazima aulize maswali
kujua kama mwenzi/wenzi wa mkopaji wameridhia mkopo huo.
Kama uhawilishaji unajumuisha uuzaji wa ardhi, mnunuzi lazima
amuulize muuzaji kujua kama ana mke /mwenzi na kama ameridhia
uuzaji huo.

Endapo mwenzi anayetaka kufanya uhawilishaji ametoka taarifa


zisizo sahihi uuzaji unabaki kuwa batili , endapo mwenzi ambaye
ridhaa yake haikupatikana ataamua kuchukua hatua za kisheria.
Hii ni muhimu kwa kuwa kuna uwezekano wa mwanaume kuweka
rehani mali ya familia bila taarifa ya mke /mwenzi.

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 71


Tanzania women Lawyers Association

Sheria pia imetoa mamlaka kwa Msajili pale anapopokea maombi


ya amri ya kugawanya (partition) ardhi inayomilikiwa kwa pamoja.
Baada ya kusikiliza pande husika kabla hajafanya maamuzi ya
kugawa ardhi lazima azingatie vigezo vingine kama thamani ya
mchango uliotolewa na mmiliki kwenye umiliki huo wa pamoja
kwenye gharama za utunzaji au uendelezaji wa ardhi au jingo
linalokaliwa kwa pamoja. Hapa endapo mwenzi ambaye haki au
maslahi yake inayoelekea kuathirika ni mwanamke atatakiwa
kutathmini ni kwa kiasi gani mwanamke ataathiriwa na ugawanyaji
huo. Kwa maneno mengine ni lazima aweke katika uwiano kile
ambacho kitawanufaisha wamiliki wote na sio mmoja peke yake.
Pale ambapo wamiliki wa pamoja ni wenzi (mke na mume) au
wale wamiliki wa pamoja ambao hawakubaliani na ugawanyaji
ni wategemezi (dependants) au wana uhusiano na hao wamiliki wa
pamoja, ni lazima atathmini endapo maslahi ya hao wawili ambao
hawakubaliani na ombi la ugawanyaji wanaweza kupata stahili yao
katika ugawanyaji huo. Hapa, kama mwenzi au wategemezi wa
mmiliki kwenye umiliki wa pamoja ambaye ameomba ugawanyaji
wa mali hataachwa / hawataachwa bila makazi baada ya mgawanyo.

Pia ni lazima msajili ahakikishe kwamba anazingatia maslahi ya


mwenzi au wategemezi wa mmiliki ambaye hisa yake kwenye
umiliki wa pamoja inatarajia kuuzwa kutekeleza amri ya mahakama
endapo haki yake imetiliwa maanani na hasa mwezi au wategemezi
wake hawataachwa bila makazi baada ya mauzo.

Haki ya Wanawake Kwenye Utatuzi wa Migogoro


Ili kuhakikisha usawa wa kijinsi kwenye usimamizi wa ardhi
ushiriki wa wanawake kwenye utatuzi wa migogoro katika ngazi
ya kata na kijiji umefanywa kuwa wa lazima. Sheria ya Ardhi ya
Kijiji, na Sheria ya Mahakama za Ardhi ya mwaka 2002 inataka kati
ya wajumbe saba wa baraza la ardhi la kijiji wanawake wasipungue
watatu na kati ya wajumbe 5 hadi 8 wanawake wasipungue watatu.
Hapa kuna kusudio la dhahiri la kuwainua na kuwajengea uwezo
wanawake kwa kuhitaji ushiriki wa wanawake katika vyombo vya
maamuzi ya ardhi ikiwa ni pamoja na usuluhishi wa migogoro,

72 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi


Tanzania women Lawyers Association

kamati za usuluhishi na mabaraza ya ardhi. Kwenye Halmashauri ya


Kijiji yenye wajumbe 25 angalau robo yao lazima wawe wanawake.
Halmashauri ya kijiji ndio msimamizi mkuu wa ardhi ya kijiji.
Pamoja na vifungu vyote vya kisheria, vinavyotoa uhakikisho wa
nafasi ya mwanamke kumiliki ardhi hali ilivyo ni tofauti kwa jinsi
wanawake wanavyobaguliwa na kunyimwa haki zao.

Kwa mfano, wanawake walio wengi wanaweza kupata ardhi kupitia


kwa waume zao au ndugu zao wakiume lakini sio umiliki. Wanawake
ambao hawajaolewa, wajane na wanawake waliotalakishwa bado
wanakabiliwa na unyanyapaa, ubaguzi na unyanyasaji kutoka
kwa ndugu wa kiume. Mara nyingine waume wametuhumiwa
kutumia hati za viwanja kuchukulia mikopo bila kupata kwanza
ridhaa ya wake zao na kusababisha kufukuzwa au kupoteza mali
ya familia kwa kushindwa kulipa deni. Kwenye maswala ya urithi
kumekuwepo na ugawanyaji usio lingana kati ya wanaume na
wanawake ambapo wanawake wamekuwa wakichukuliwa kuwa
daraja la pili na la tatu katika daraja la tatu.

Kwa kuwa ndoa za kimila hazisajiliwi, wanawake wanakuwa katika


hatari kwa kuwa wakati wa talaka au kifo cha mume wanajikuta
wakipoteza karibia kila kitu ikiwa ni pamoja na ardhi.

2.8 Hitimisho
Inaweza kuonekana kwamba kinadharia mfumo wa kisheria uliopo
umeweka nyenzo zinazohitajika kuhakikisha kwamba haki ya
wanawake kwenye ardhi inalindwa. Inapaswa kuwepo na jitihadi
za dhati kuhakikisha kuna utekelezaji wa sheria zilizopo. Vikundi
vyenye kutetea maslahi ya umma vinapaswa kusimama, kutetea na
kuhakikisha kwamba maudhui ya sheria hizi yanatiliwa mkazo na
kutekelezwa

Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi 73


Tanzania women Lawyers Association

74 Mwongozo wa Taratibu za Kisheria Katika Umiliki wa Ardhi

You might also like