You are on page 1of 68

Mwongozo

wa Madereva
Wanafunzi

Kwa wale wanaojifunza


magari madogo na magari
mengine ya kawaida
©Wizara ya Miundombinu
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Julai 2009

ISBN 978 9987 9171 2 9

ii
Yaliyomo

Dibaji ................................................................................. 1
Utanguluzi ......................................................................... 3
Mambo gani yanayomfanya dereva kuwa mzuri?............... 5
Jukumu lako ktika mfumo wa barabara ............................. 6
Sheria na madereva wanafunzi.......................................... 6
Kujua kuhusu gari lako na jinsi kulidumisha...................... 7
Vijenzi vya msingi........................................................................8
Kulikagua gari ........................................................................... 12
Ushauri kwa madereva wa magari yenye nguvu ya magurudumu ya
mbele na ya nyuma ................................................................... 14
Kuwa katika hali nzuri ya kuendesha............................... 14
Uwezo wa kuona ....................................................................... 14
Uchovu..................................................................................... 15
Kunywa pombe ......................................................................... 16
Kutumia dawa na kuendesha....................................................... 17
Hali na ugonjwa......................................................................... 17
Jinsi ya kuanza, kunyonga, kusimama na kurudi nyuma.. 18
Utangulizi ................................................................................. 18
Kuwasha injini........................................................................... 20
Kunyonga ................................................................................. 21
Kuondoka ................................................................................. 22
Kubadili gia............................................................................... 22
Kuendelea kulidhibiti gari............................................................ 23
Kufunga breki ........................................................................... 24
Kurudi nyuma ........................................................................... 25
Kuliacha gari ............................................................................. 26
Uendeshaji salama barabarani......................................... 27
Kuendesha barabarani................................................................ 27
Mwendo.................................................................................... 31
Kulipita gari jingine .................................................................... 32
Makutano ................................................................................. 36
Ushauri maalumu kwa madereva kwenye sehemu zenye mzunguko. 41
Uendeshaji wa usiku au kwenye hali mbaya ya hewa ..................... 42
Kurudi nyuma ........................................................................... 43
Kuwajali watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara
wanaoweza kuathirika ................................................................ 44
Kurudi ulikotoka ........................................................................ 46
Reli Inayokatisha ....................................................................... 47

iii
Kuegesha......................................................................... 48
Uegeshaji wa 900 ....................................................................... 49
Uegeshaji sambamba ................................................................. 50
Uegeshaji wa mshazari ............................................................... 50
Kuegesha kilimani...................................................................... 51
Alama za barabarani ........................................................ 52
Jaribio la udereva ............................................................ 53
Maombi ya kufanya jaribio la udereva .......................................... 53
Kujiandaa kwa jaribio................................................................. 53
Yaliyomo kwenye jaribio ............................................................. 54
Jaribio ...................................................................................... 54
Baada ya jaribio ........................................................................ 56
Kuharibika ....................................................................... 57
Iwapo kuna ajali.............................................................. 58
Muhtasari wa mafunzo ya madereva wa magari madogo
(Leseni za Daraja B & D) ................................................. 59

iv
Dibaji

Mwongozo wa Madereva Wanafunzi unajumuisha taarifa na maelekezo


kwa wale wanaojifunza kuendesha magari madogo na magari mengine
ya kawaida. Umeweka viwango kwa ajili ya programu za mafunzo ya
udereva, na wafundishaji wote wa udereva lazima wawafundishe
wanafunzi wao ujuzi na maarifa yaliyoelezwa humu. Watu wengi sana
wamekuwa wakiuawa na kujeruhiwa bila sababu kwenye barabara zetu,
na sababu kuu ni makosa ya dereva. Kila siku tunaona mifano ya tabia
za hatari za madereva, ambao ama hawajui sheria au wasiojali kuhusu
usalama wa wengine.

Ni matumaini yetu kuwa Mwongozo huu utasaidia uzalishaji kizazi kipya


cha madereva bora, salama. Iwapo utausoma Mwongozo vizuri, utapata
maelekezo mazuri – bora, na daima jaribu kujiendeleza, uwe na malengo
marefu na salama ya udereva mbele yako.

1
2
Utanguluzi

Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi ni mwongozo rasmi kwa


wanaojifunza kuendesha magari madogo na magari mengine ya kawaida.

Uendeshaji gari mzuri na salama kwenye barabara zetu huhitaji ujuzi


unaofaa, uzoefu, na tahadhari. Lazima ujue:
• Namna ya kuvitumia vidhibiti vya gari lako
• Namna ya kuliweka gari lako katika hali nzuri barabarani
• Wakati unapokuwa katika hali isiyo nzuri kwa kuendesha gari
• Namna ya kuliendesha gari lako kwa usalama
• Sheria za barabarani na maana ya alama na michoro ya barabarani
• Nini cha kufanya katika tukio la gari kuharibika au ajali.

Seti hii yenye stadi mbalimbali ngumu si kitu unachoweza kujifunza kwa
urahisi kutoka kwa marafiki na ndugu – lazima upate maelezo ya
kitaalamu kutoka kwenye shule ya udereva yenye kibali.

Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi umeandikwa ili kuzipatia shule


za udereva miongozo ya maudhui ya programu zao za ufundishaji
madereva. Wana wajibu wa kuwafundisha wanafunzi kwenye nyanja zote
za udereva si jinsi ya kulidhibiti gari tu. Mwongozo unaonyesha kile
ambacho mwanafunzi anapaswa kufundishwa. Baadhi ya ushauri
umechukuliwa kutoka kwenye Kanuni za Barabara, lakini wanafunzi
wanatakiwa kuzipata nakala zao za Kanuni za Barabarani, kwani zina
taarifa za alama zote za barabarani, na taarifa nyingine muhimu.

Utakapoona maneno LAZIMA au SI LAZIMA maana yake ni kuwa


unatakiwa kisheria kufuata maelekezo haya. Iwapo hutafuata moja kati
ya maelekezo haya umevunja sheria, na iwapo utakamatwa na
kuthibitika, unaweza kutozwa faini na kuondolewa kutoka kwenye
udereva. Pia unaweza kupelekwa jela mpaka miaka mitano. Sheria za
Barabarani zitabadilika katika miaka ijayo na uwasiliane na polisi wa
eneo lako iwapo una shaka yoyote kuhusu sheria za sasa.

Mwongozo wa Madereva Wanafunzi unajaribu kuelezea mambo kwa


lugha rahisi, lakini baadhi ya istilahi zilizotumika zinaweza kuwa ngeni
kwako au zenye maana tofauti kidogo na ile unayoifahamu. Mwongozo
mfupi umetolewa hapo chini:

3
“Dereva” maana yake ni mtu yeyote anayeendesha gari au vitu vingine
(pamoja na baiskeli) au anayechunga wanyama barabarani

“Njia mbili” maana yake ni barabara ambazo zinapishana na


kutenganishwa kati au na kizuizi

“Achia njia” maana yake ni kuwa dereva asiendelee, iwapo kufanya


hivyo kutawalazimisha madereva wa magari mengine kubadili mwendo
au mwelekeo kwa haraka

“Njia” maana yake sehemu ya barabara ambayo imeonyeshwa kwa ajili


ya mstari mmoja wa magari yanayokwenda

“Mtumiaji wa barabara” maana yake mtu yeyote anayesafiri, au


aliyemo barabarani, au ndani ya gari barabarani

“Magari barabarani” maana yake magari yanayotembea

“Gari” maana yake mashine yoyote inayoendeshwa barabarani kwa


nishati yoyote, na ikijumuisha uzungukaji pedeli, mikokoteni ya
kusukumwa kwa mikono na mikokoteni ya kuvutwa na wanyama

“Alama za pundamilia” maana yake alama za kivuko cha watembea


kwa miguu inayoonyeshwa na mistari myeupe sambamba na mwelekeo
wa barabara.

Mwongozo huu wa Madereva Wanafunzi umetolewa na Kitengo cha


Usalama Barabarani cha Wizara ya Miundombinu kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi Tanzania. Kazi hii ilisaidiwa na Shirika la Kimataifa la
Misaada ya Maendeleo la Denmark. Waandishi wanashukuru kwa
matumizi ya maelezo kutoka Mwongozo wa madereva Wanafunzi wa
SATCC, na Kanuni za Barabarani za nchi nyingine ikiwa ni pamoja na
Uganda. Vielelezo vingi vimetolewa kwa hisani ya Wizara ya Ujenzi,
Nyumba na Mawasiliano, Jamhuri ya Uganda. Maelezo mengi
yamechukuliwa kutoka kwenye toleo la mwanzo la Mwongozo
lililoandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa msaada wa fedha
kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway.

4
Mambo gani yanayomfanya dereva kuwa mzuri?

Dereva mzuri anahitaji ustadi na uzoefu, na mtazamo sahihi. Mwalimu


wako wa udereva atakufundisha ustadi na utauendeleza kwa kutenda.
Uzoefu utakuja kadiri unavyoendesha mara nyingi na kukabiliana na
mazingira mengi. Ubora unaochangia kuwa na mtazamo sahihi wa
udereva ni kama ufuatao:

Uwajibikaji –kuwafikiria wengine. Gari ni mashine ambayo inaweza


kuuwa kwa urahisi, kwa hiyo lazima uzingatie usalama wako, usalama
wa abiria wako, na usalama wa kila mtumiaji mwingine, hususan
watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na watumiaji wengine wa
barabara wanaoweza kudhurika. Daima lazima uzingatie usalama na
kamwe usifanye jambo ambalo linaweza kuwaingiza wengine hatarini.
Wakati wote kumbuka kuchukua tahadhari zaidi, kwa sababu kosa dogo
linaweza kusababisha ajali inayoweza kuua mtu.

Umakini. Pamoja na uwajibikaji kuna umakini katika kazi ya udereva.


Lazima uwe makini wakati wote iwapo unataka kuendana na hali
inayojitokeza barabarani. Usiendeshe ukiwa umechoka,
umechanganyikiwa au kuumwa. Usiwaruhusu abiria wakusumbue na
maongezi yao, na usitumie simu yako ya mkononi.

Matarajio. Umakini husaidia kutarajia kitakachotokea. Unatakiwa daima


kuangalia kile ambacho watumiaji wengine wa barabara wanafanya, na
tumia busara yako kupima kile ambacho kitatokea baadaye. Kwa njia hii
utakuwa tayari na kuweza kuendana na kuitikia kwa usalama katika hali
yoyote ambayo itatokea.

Uvumilivu. Iwapo utapoteza uvumilivu pale dereva mwingine


anapofanya kitu kibaya au unapokabiliwa na foleni ndefu ya magari,
utakuwa unaelekea kupata ajali. Endelea kuwa mtulivu na idhibiti hasira
yako. Fuata sheria za barabarani.

Kujiamini. Unahitaji kujiamini ili kuendesha vizuri katika mazingira ya


kisasa ya barabara. Madereva wapya bila shaka hawatajiamini, lakini
kujiamini kutakuja kutokana na kukua kwa ujuzi na uzoefu. Hata hivyo,
usijiamini kupita kiasi, kwani hili linaweza kukusababishia uendeshaji wa
hatari. Daima dhibiti uendeshaji wako na jaribu kurekebisha makosa
yoyote yatakayojitokeza.

5
Jukumu lako ktika mfumo wa barabara

Wakati unatumia barabara unaweza kujifikiria kama unafuata mfumo


unaojumuisha vitu vinne:

Magari – Magari madogo (la kwako na mengine), malori, mabasi,


baiskeli, n.k.
Watumiaji barabara – madereva wa magari (wewe na wengine) na
watumiaji barabara wanaoweza kudhurika (watembea kwa miguu,
waendesha baiskeli na pikipiki)
Mazingira ya barabarani – barabara na sehemu zake, pamoja na
alama na michoro ya barabarani
Sheria za barabarani (Katika Sheria za Barabarani na Kanuni za
Barabarani) – zinazodhibiti mwingiliano kati ya watumiaji wa barabara
(pamoja na wewe) magari na mazingira ya barabara.

Kwa pamoja, mambo haya manne yanaunda mfumo wa barabara. Ili


mfumo ufanye kazi vizuri mambo haya manne lazima yafuatwe vizuri
kwa kila moja na kila moja litumike bila ya makosa. Mazingira ya
barabarani yamekuwa yakiboreshwa taratibu, na sheria za barabarani
zimetungwa (ingawa si kila mmoja anazifahamu). Wajibu wako ni kuona
kuwa wewe na gari lako mnaenda bila makosa.

Sheria na madereva wanafunzi

Leseni za madereva wanafunzi. Madereva Wanafunzi lazima wawe na


leseni za madereva wanafunzi kabla ya kuendesha gari kwenye barabara
za umma. Leseni hizi huombwa kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA). Leseni hii hudumu kwa miezi mitatu, lakini inaweza
kuombwa upya kwa kipindi cha miezi mitatu mingine kwa wakati mmoja.
Leseni haiwezi kuombwa upya zaidi ya miezi 15 isipokuwa kama
umefanya na kushindwa jaribio la udereva katika kipindi hicho.

Unaweza kuomba leseni ya kuendesha baiskeli moto mara tu ufikishapo


umri wa miaka kumi na sita. Unatakiwa kuwa na angalau miaka 18 kabla
hujaruhusiwa kuendesha gari dogo, pikipiki au magari mengine ya
kawaida. Unaweza kutakiwa kuthibitisha umri wako.

Unapoomba leseni ya madereva wanafunzi unaweza kutakiwa kuonyesha


kuwa umefanya mipango ya kupata mafunzo kutoka kwenye shule yenye

6
kibali cha mafunzo ya udereva. Lazima uonyeshe kasoro zozote au
ulemavu mwilini wakati unaomba leseni ya dereva mwanafunzi.

Wanafunzi lazima waendeshe chini ya usimamizi wa Mwalimu wa


udereva aliyesajiliwa. Usiendeshe bila ya mwalimu wako kwenye kiti
cha mbele cha abiria. Hata hivyo madereva wa pikipiki wanafunzi
wanaweza kuendesha peke yao.

Kiwekwe “kibao cha L” Gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi


lazima liwekwe “Vibao vya L” mbele na nyuma.

Jaribio la udereva. Dereva mwanafunzi anaweza kuomba polisi afanye


jaribio la udereva pindi atakapokuwa ameendesha kwa angalau mwezi
mmoja baada ya kutolewa kwa leseni ya dereva mwanafunzi. Iwapo
atafaulu jaribio, atapatiwa cheti cha kufuzu, na hiki kitamuwezesha
kuomba leseni kamili ya udereva. Angalia vifungu vingine mbele kwa
taarifa zaidi kuhusu jaribio la udereva.

Gari. Gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi lazima liwe na nyaraka


halisi za usajili, leseni ya barabara, na sera ya bima ya gari. Pia lazima
liwe na hali nzuri kutembea barabarani.

Kujua kuhusu gari lako na jinsi kulidumisha

Ni vizuri kuwa na maarifa ya msingi ya jinsi gari lako linavyofanya kazi.


Lazima ujue kazi za vyombo mbalimbali vya gari na sehemu vilipo.
Maarifa haya yatakusaidia kuliweka gari katika hali nzuri ya kutembea
barabarani.

Hali ya kiufundi ya gari lako lazima iendane na kanuni za gari. Fundi


mchundo mwenye ujuzi anaweza kuchunguza iwapo gari lako linakidhi
viwango vinavyotakiwa. Iwapo gari lako litahitaji matengenezo
inashauriwa kutumia karakana zenye uzoefu na zinazoaminika. Epuka
kutumia vipuri vyenye ubora mdogo au vya kughushi, ukidhani unaokoa
fedha unaponunua vipuri vya bei rahisi. Daima huweza kuwa hatari kwa
kuvunjika ghafla au kuchakaa haraka.

“Kitabu cha Mwongozo” kwa ajili ya gari lako ni chanzo kizuri sana cha
ushauri wa namna ya kulitumia gari na kulifanya lidumu katika hali nzuri.
Fuata maelekezo haya kwa makini. Kumbuka kuwa gari linalotunzwa

7
vizuri halitakugharimu sana kulitumia, halitaharibika mara kwa mara na
litakuwa salama.

Vijenzi vya msingi


Injini. Injini ni mashine inayolifanya gari kutembea. Nishati huhamishwa
kupitia kwenye klachi kwenda kwenye giaboksi na hatimaye kwenye
magurudumu. Injini za petroli ni nyingi lakini baadhi ya magari madogo
na magari mengi ya magurudumu manne na magari madogo ya mizigo
yamewekwa injini za dizeli.

Ulainishaji. Injini lazima ilainishwe kwa mafuta/vilainishi ili iweze


kufanya kazi vizuri na bila kuharibika. Vilainishi vya Injini huchafuka na
huhitaji kubadilsihwa, kwa kawaida kila baada ya km 5,000 au kila baada
ya miezi sita (yoyote itakayotangulia). Pima kiasi cha oili kila wiki. Iwapo
taa ya tahadhari ya oili itawaka kwenye chombo cha kuonyeshea wakati
unaendesha simama na kupima kiasi cha oili. Ni jambo zuri kuwa na
dumu la oili ya injini kwenye gari lako.

Uwashaji. Mfumo wa uwashaji hupatia injini ya petroli kichocheo


ambacho huifanya petroli kulipuka na kuzalisha nishati kwenye silinda.
Plagi lazima ziwe safi na kufungwa vizuri, ili zitoe kichocheo kikubwa.
Injini za dizeli hazina mfumo huu wa uwashaji.

Mfumo wa upozaji. Injini hupata moto sana kwa hiyo lazima kuwe na
mfumo wa kuipoza. Mfumo huu kwa kawaida hufanya kazi kwa kupeleka
maji (kipozeo) kuzunguka injini kupitia mipira na mirija. Angalia kiasi cha
maji kwenye tangi kila wiki na angalia uvujaji kwenye mirija ya maji.
Iwapo mshale kwenye kipimo unaonyesha kuwa joto la injini ni la juu
sana lazima uzime injini kuepuka uharibifu. Maji yatakuwa moto sana na
yanaweza kukuunguza – hivyo, kama unahitaji kujaza tena, subiri hadi
injini ipoe.

Mfumo wa mafuta. Mafuta hunyonywa kutoka kwenye tangi la


mafuta/vilainishi na pampu na kisha huchanganywa na hewa na
kusukumwa kwenye injini. Injini inaweza kuharakishwa kufanya kazi kwa
kubonyeza kwenye pedeli ya kichapuzi ambayo hurekebisha
mchanganyiko wa mafuta/hewa.

Giaboksi. Giaboksi husafirisha nishati kutoka kwenye injini kwenda


kwenye magurudumu hivyo nishati ya kutosha kuendesha gari
8
inakuwepo kwenye mwendo tofauti. Magari mengine yana giaboksi za
mikono. Magari haya yana gia 4 au 5 za kwenda mbele zinazoitwa ya
kwanza, ya pili, ya tatu ya nne na ya tano, na gia moja ya kurudi nyuma.
Wakati mwingine mpangilio huonyeshwa kwenye sehemu ya gia yenye
muundo wa “H” – angalia kielelezo.

Mpangilio halisi wa giaboksi

1 3 5 1 3 R 1 3

Nyutro Nyutro
Mpango wa pedeli 2 4 2 4 R 2 4
R

R maana yake gia ya kurudi nyuma

Klachi Breki Kichapuzi

Kwa kawaida unatumia gia ya kwanza kulifanya gari lianze kutembea na


kisha polepole endelea na gia zinazofuata kadiri mwendo
unavyoongezeka. Kanyaga pedeli ya klachi kutenganisha injini na
giaboksi wakati unabadili gia na wenzo wa gia.

Magari mengine yamewekwa mfumo wa otomatiki ambao hubadili gia


kwa ajili yako – unachotakiwa kufanya kabla ya kuondoka ni kukanyaga
pedeli ya breki, kuondoa kichaguzi cha gia kutoka kwenye “kuegesha”
kupeleka mbele au “kurudi nyuma”, kisha kuachia pedeli za breki.

Mfumo wa otomatiki:
Mpango wa pedeli
Wenzo wa kichaguzi

Kuegesha
Kurudi nyuma
Nyutro
Kuendesha
2 Breki
L Kichapuzi

9
Breki. Gari lina mfumo wa breki ambao unatumia mafuta ya haidroliki
(kilainishi/mafuta ya breki) kuendesha pedi ambazo hubana
magurudumu na kuyapunguza mwendo. Pedi hizi huweza kuchakaa na
huhitaji kubadilishwa kila baada ya wakati fulani. Breki hufanya kazi kwa
kukanyaga pedeli za breki. Ni muhimu kuangalia kiasi cha
kilainishi/mafuta ya breki kwenye akiba kila wiki. Daima tumia
kilainishi/mafuta halisi ya breki, si mengine ya bei rahisi yasiyo halisi. Ni
muhimu sana kwa usalama wako na kwa usalama wa watumiaji wengine
wa barabara breki kuwa katika hali nzuri, iwapo hazifanyi kazi vizuri na
kwa ubora (gari huenda upande, breki hupiga kelele, au pedeli za breki
kuwa laini na kubonyea) lazima ziangaliwe haraka. Matengenezo ya
mfumo wa breki yafanywe na karakana yenye ujuzi.

Magari yote madogo yana breki ya mkono, ambazo lazima zitumiwe


wakati wa kuegesha. Lazima iwe na uwezo wa kulifanya gari liendelee
kusimama hata kwenye kilima kikali.

Usukani na Viangiko. Magari mengi sasa yamewekwa nishati ya


usukani ambayo huufanya usukani kunyongwa kirahisi. Unyongaji wa
usukani lazima uhamishe mzunguko wa usukani kwenye magurudumu
taratibu na kwa ufanisi. Kusiwe na nguvu nyingi kwenye unyongaji.
Chunguza jambo hili kwa kuzungusha usukani mpaka upate kizuizi halisi
– Iwapo unaweza kunyonga usukani zaidi ya sm 2-3 kuna kudorora
kwingi. Uchunguze usukani kwa kukata kona kali katika mwendo mdogo
– iwapo kuna kelele zisizo za kawaida au usukani haufanyi kazi vizuri,
lipeleke gari kwenye karakana yenye ujuzi kwa kukaguliwa kwa makini
na matengenezo.

Mfumo wa viangiko (springi na shokomzoba) hudhibiti uendaji juu na


chini wa magurudumu ili uendeshaji uendelee kuwa mzuri. Mfumo huu ni
muhimu zaidi kwa usalama; unayaweka magurudumu katika
kukandamiza vizuri barabara, hususan wakati wa kufunga breki.
Shokomzoba zina kazi ngumu na huhitaji kubadilishwa mara kwa mara.
Wakati wa kubadili shokomzoba badili pande zote, kuepuka kutokuwepo
uwiano.

Matairi na magurudumu. Matairi ni sehemu ambayo hulifanya gari


lako likae barabarani, na eneo la kukanyaga kwa kila tairi kwa wastani ni
kubwa kama mkono wako. Iwapo utahitaji kufunga breki au kupinda
ghafla utendaji wa eneo hili dogo la tairi unaweza kuwa mkubwa kwa
usalama wako, hivyo, ni muhimu sana kuwa na matairi mazuri. Matairi:
10
• Yaenee vizuri kwenye magurudumu
• Yawe na sehemu ya kukanyagia yenye kina cha kutosha – mm3 ni
kina cha chini kinachopendekezwa
• Yawe na upepo sahihi
• Yakae vizuri ndani, kuepuka kukatika, kuvimba au maeneo ambayo
umbo la ndani linaonekana
• Yote yawe ya aina na utengenezaji mmoja.

Fuata ushauri wa mtengenezaji juu ya wakati gani wa kubadili matairi.


Usijaribu kutengeneza matairi yaliyoharibika vibaya. Matairi
yaliyotengenezwa yanaweza kukupa matatizo na yanaweza yasiwe
salama. Iwapo utafunga matairi yenye ubora na kuyatunza utapunguza
hatari ya tairi kupasuka wakati unaendesha. Upasukaji wa matairi
husababisha ajali za mara kwa mara.

Pancha inaweza kutokea wakati wowote. Daima uwe na tairi la akiba


kwenye gari, pamoja na jeki ya kulinyanyua gari, na spana ya kufungulia
nati za gurudumu. Hakikisha kuwa tairi la akiba liko katika hali nzuri na
kujaza upepo sahihi. Fanya mazoezi ya namna ya kubadilisha matairi.

Betri na mfumo wa umeme. Betri inatoa nishati kwenye stata na


huhifadhi nishati ya ziada inayotoka kwenye altaneta. Hakikisha altaneta
ina chaji betri wakati injini inafanya kazi (magari mengine yana taa ya
kuashiria kwenye dashibodi). Iweke betri katika hali nzuri – aina nyingine
huhitaji kujazwa tena maji ya betri mara kwa mara. Hakikisha kuwa kebo
zimefungwa vizuri kwenye betri, kwani mara nyingi zikilegea zinafanya
umeme usipite.

Taa, indiketa na viakisi. Lazima uhakikishe kuwa na:


• Taa mbili nyeupe za mbele ambazo zinaweza kuteremshwa (yaani
kumulika chini)
• Taa mbili nyeupe mbele na taa mbili nyekundu nyuma
• Indiketa za njano mbili mbele na mbili nyuma
• Taa mbili nyekundu nyuma za kusimamia ambazo huwaka wakati
breki ikifungwa.
• Angalau kiashiria kimoja nyuma.

Hakikisha kuwa taa za mbele zimerekebishwa ili wakati zikiteremshwa


mwanga uende chini na kushoto. Ziangalie taa zako mara kwa mara – ni
kinyume cha sheria kuendesha wakati moja au zaidi ya taa hizi haifanyi
kazi.
11
Mfumo wa ekzosi. Huu huitoa gesi iliyoungua kutoka kwenye injini na
kuisukuma kupitia kwenye sailensa kabla ya kuitoa nje kupitia kwenye
bomba la ekzosi. Usiuache mfumo wa ekzosi kuwa katika hali mbaya kwa
sababu hili litasababisha kelele, na gesi ya ekzosi inaweza kuambaa
kwenye gari.

Dashibodi. Mpango wa dashibodi hutofautiana kulingana na


mtengenezaji na aina ya gari, lakini kielelezo kinaonyesha mpango halisi.
Angalia “Kitabu cha Mwongozo” iwapo kuna taa zozote au vipimia
ambavyo huna uhakika navyo.

Taa za mbele
Indiketa ya kushoto Indiketa ya kulia

80 100 P
FUEL TEMP
H
60 120 F
R
40 140 N
160 D
20 2
0 180 L
km/h E C

Kuendesha
Kipimia joto
Kipimia mwendo
Mahali pa Kipimia Mahali pa
taa ya tahadhari mafuta taa ya tahadhari

Kulikagua gari
Ni muhimu gari lako kufanyiwa matengenezo ya kawaida ya mara kwa
mara na karakana yenye ujuzi, lakini vitu vinaweza kuharibika baada na
kabla ya matengenezo mengine, hivyo ni lazima uendelee kulikagua
mwenyewe.

Kabla ya kila safari angalia kuwa:


• Hakuna tairi lisilo na upepo
• Chungulia uvunguni mwa gari kuona iwapo kuna kuvuja kokote,
wanyama, watoto n.k.
• Kioo chako cha mbele na madirisha ni safi
• Vioo vyako vya pembeni viko mahali sahihi ili uone vizuri.
• Hakuna taa yoyote ya tahadhari inayowaka kwenye dashibodi

12
Vitu ambavyo unapaswa kuvichukua kwenye gari:
• Leseni ya biashara, waraka wa usajili wa gari, stika ya leseni ya
barabara, na stika ya bima (vibandikwe ndani kwenye kioo cha
mbele)
• Kisanduku cha huduma ya kwanza
• Tairi la akiba- lijazwe upepo sahihi
• Spana ya gurudumu
• Vibao viwili vya tahadhari vya Pembetatu vyekundu (hivi huhitajika
kisheria)
• Tochi.

Vingine muhimu ni:


• Mfuko wa Spana na bisisbisi
• Utepe
• Pampu ya mguu
• Mkanda wa feni wa akiba
• Oili ya injini
• Mafuta ya breki
• Kipozeo cha akiba
• Kamba ya kuvutia
• Fyuzi za akiba kwa ajili ya mfumo wa umeme
• Kebo kwa ajili ya kuchajia betri
• Poda kavu ya kuzimia moto isiyo pungufu kg 1.

Kila wiki lazima uangalie:


• Uchakaaji wa matairi na upepo
• Nati za magurudumu
• Kiasi cha oili
• Kiasi cha mafuta ya breki
• Kiwango cha upozaji
• Indiketa na taa ni safi na zinafanya kazi
• Honi inafanya kazi
• Kiasi cha betri na kukaza kwa vifungo vya betri
• Weipa za kioo cha mbele zinafanya kazi na chupa ya kuzioshea imejaa
maji
• Kioo chote ni safi ndani na nje, na kuwa vioo na viashiria ni safi
• Funua boneti kuona kama kuna kitu chochote chenye matatizo
• Chunguza kelele zisizo za kawaida wakati injini inaunguruma.

13
Iwapo unaendesha umbali mrefu kila siku, au gari lako limechakaa,
fanya uchunguzi wa yaliyoandikwa hapo juu mara kwa mara badala ya
mara moja kwa wiki.

Kila mwezi chunguza:


• Kukaza kwa mkanda wa feni
• Kuvuja kwa mipira ya maji.

Ushauri kwa madereva wa magari yenye nguvu ya


magurudumu ya mbele na ya nyuma
Magari yenye nguvu ya magurudumu ya mbele na nyuma yana faida
kubwa kuliko magari madogo kwani yanaweza kupita kwa urahisi kwenye
barabara mbaya na vilima vikali. Hata hivyo utendaji wake wa usalama
umechanganywa. Mahali pa uendeshaji ni pazuri na panaonekana
kumlinda vizuri dereva na abiria ajalini, kwa sababu ya ukubwa wake.
Lakini yana kitovu cha mvutano mkubwa ambao huyafanya kuelekea
kupinduka. Uwe mwangalifu kunyonga na kufunga breki taratibu,
hususan wakati unaendesha kwa mwendo wa kasi, au iwapo tairi la
mbele litapasuka. Pia ukumbuke kuwa ukimgonga mtembea kwa miguu,
mwendesha baiskeli au pikipiki kwa magari ya namna hii yana
uwezekano mkubwa wa kupata ajali mbaya, hivyo uwe makini zaidi
viwapo karibu. Kuendesha gari kubwa hakukupi haki ya kuwasukuma
wengine walio karibu na wewe – unatakiwa kujali wakati wote.

Kuwa katika hali nzuri ya kuendesha

Kuendesha gari ni kazi ngumu inayoendelea kwa hali ambayo si ya


kawaida kwa binadamu. Matukio yasiyotarajiwa hutokea ambayo
yanakuhitaji kutenda haraka. Hivyo, unahitaji kuwa na uwezo mzuri wa
kuona, kutenda upesi, na kuwa na tahadhari na kuwa makini. Iwapo
utakuwa umechoka au kunywa pombe au kutumia dawa fulani unaweza
usiwe katika hali nzuri ya kuendesha.

Uwezo wa kuona
Taarifa nyingi anazohitaji dereva humfikia kupitia macho yake. Kwa hiyo
uwezo wa kuona vizuri ni muhimu kwa uendeshaji salama. Lazima uweze
kusoma kibao cha namba za gari kutoka umbali wa kiasi cha mita 20
katika mwanga mzuri wa mchana. Iwapo unahitaji kuvaa miwani (au
lenzi zilizobandikwa kwenye mboni) kuona, lazima uvivae wakati wote

14
unapoendesha. Wakati unaomba leseni ya udereva utatakiwa kuonyesha
cheti kinachoonyesha kuwa uwezo wako wa kuona uko katika viwango
vinavyotakiwa.

Kadiri watu wanavyozeeka na uwezo wao wa kuona hupungua. Wakati


mwingine mabadiliko huwa ya polepole kiasi cha kutoyagundua. Upimaji
wa mara kwa mara wa macho ni muhimu.
Upunguaji wa uwezo wa kuona
Uonaji wa kawaida pembeni baada ya kunywa
pombe au kwenda kwa mwendo
wa kasi

Vitu ambavyo moja kwa moja viko mbele yako vinaweza kuonekana kwa
uwazi zaidi, lakini uonaji wako wa pembeni kwa kawaida ni mzuri
kugundua mienendo ya eneo pana kuelekea kwako. Uonaji huu wa
pembeni ni muhimu, kwa sababu unahitaji kuona kitu chochote haraka
(magari, watembea kwa miguu) vinavyokuja kwako kutoka pembeni.
Wakati unaendesha kwa kasi hutaweza kutumia vioo vyako vya pembeni
kikamilifu. Hii inamaanisha kuwa utaikaribia hatari kubwa kabla
hujaweza kuigundua. Kitu kama hicho hutokea pindi ukinywa pombe –
vioo vyako vya pembeni hutiwa ukungu na kuwa vidogo.

Uchovu
Kuendesha kunaweza kukufanya ujisikie usingizi, na hili kwa kiasi
kikubwa hukuongezea hatari ya kupata ajali. Unaweza kuepuka usingizi
kwa kuhakikisha kuwa kuna hewa nzuri ndani ya gari, na umekaa
sehemu nzuri ya kuendeshea. Kitu chochote kinachosababisha ugumu
katika uendeshaji, mfano uchafu kwenye kioo cha mbele, vitakuchosha
kwenye safari ndefu.

15
Inashauriwa kuwa upumzike kwa dakika 30 kila baada ya saa 3 za
kuendesha. Epuka kuanza safari ndefu usiku sana au baada ya saa za
kazi. Usiendeshe kwa zaidi ya saa 9 kwa siku. Madereva wa magari ya
biashara lazima wafuate kanuni za saa za madereva.

Iwapo unajisikia kuchoka tafuta sehemu salama usimame na kupumzika.


Toka ndani ya gari na utembee kidogo. Unywaji wa vikombe viwili vya
kahawa unaweza kukusaidia. Usitumie dawa ili usilale.

Kunywa pombe
Kamwe usinywe pombe kabla ya kuendesha. Pombe hupunguza uwezo
wa mfumo wa akili yako, kupunguza utendaji wako, kuathiri uamuzi
wako wa mwendo unaofaa, umbali sahihi na hatari itakayotokea, na
kukupa hisia zisizo sahihi za kujiamini.

USIENDESHE gari iwapo umekunwya pombe nyingi kiasi cha kushindwa


kuimudu. Hairuhusiwi kuendesha ukiwa na kiasi cha pombe kwenye
damu cha juu zaidi ya mg 80/ml 100, lakini uendeshaji wako unaweza
kuathiriwa kabla hata ya kufikia kikomo hiki. Kwa hiyo, ni vizuri
kutokunywa kabisa kilevi chochote kabla ya kuendesha.

Kumbuka kuwa inachukua muda kwa kwa kilevi kuondoka mwilini


mwako, hivyo unaweza kutokuwa katika hali nzuri ya kuendesha jioni
baada ya kunywa pombe wakati wa chakula cha mchana.

Pombe ni sababu ya ajali nyingi za barabarani, hususan zile zinazotokea


usiku. Hivyo, kuendesha ukiwa na pombe kwenye damu ni kosa kubwa,
na iwapo utakamatwa, adhabu inaweza kuwa kali sana, ikiwa ni pamoja
na faini, kufukuzwa udereva, na kufungwa. Iwapo polisi
watakusimamisha kwa kukuhisi kunywa pombe wanaweza kupima
haraka kiwango cha pombe kwenye damu yako kwa kukutaka kupumua
kwenye kifaa kiitwacho kipimaulevi (alcometer).

16
Pombe na hatari ya ajali
Hatari kubwa ya Watu wanaoathiriwa
ajali baada ya zaidi na pombe
kunywa pombe
Wanaoathirika
MARA 15 zaidi
KIKOMO Wanaoathirika
KISHERIA kidogo

MARA 5

Hatari ya ajali
bila pombe
0 10 50 80 100 150 200

Mchanganyiko wa damu na pombe


(mg za pombe kwa 100 ml za damu)

Chanzo: kulingana na matokeo ya tafiti Marekani na Canada.

Kutumia dawa na kuendesha


Kutumia dawa kunaweza kuathiri uwezo wako wa kuendesha katika
namna nyingi. USIENDESHE gari kama umekunywa dawa
zitakazokufanya kushindwa kulidhibiti gari vizuri. Dawa nyingi zina athari
mbaya, mfano kukufanya kulala kuliko kawaida, hivyo kuwa makini na
hili na ikibidi acha kuendesha. Daktari au mfamasia wako akushauri
iwapo ni salama kuendesha. Utumiaji wa vichocheo, dawa za kubadili
akili, na vitu vingine haramu inaweza kuwa hatari, hasa vikienda pamoja
na pombe.

Hali na ugonjwa
Usiendeshe wakati una hasira, ukiwa na furaha zaidi au kuchanganyikiwa
sana kuhusu jambo fulani. Usiendeshe kama hujisikii vizuri. Iwapo una
tatizo la kiafya litakalokufanya kuelekea kuzimia au kifafa, au kupata
ulemavu wa mwilini lazima umuulize daktari wako iwapo ni salama
kwako kuendelea kuendesha. Iwapo daktari wako atakuambia uache
kuendesha, ipeleke leseni yako Polisi. Fanya hivyo hivyo iwapo uwezo
wako wa kuona utaathirika na kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa.

17
Jinsi ya kuanza, kunyonga, kusimama na kurudi
nyuma

Utangulizi
Kabla hujaliendea gari lako ili uendeshe ni muhimu kuwa na tabia ya
kupanga safari yako. Unajua kwa uhakika unakokwenda na namna ya
kufika kule? – Kama hujui, angalia kwenye ramani au pata ushauri
kutoka kwa mtu anayelijua eneo hilo. Unapopanga safari yako fikiria
kuhusu msongamano wa magari, matengenezo ya barabara, hali mbaya
ya barabara, au matatizo mengine.

Unapolielekea gari lako anza kufanya uchunguzi wa awali kabla ya safari:


• Hakuna tairi lolote linaloonekana kutojaa (au kujaa sana)
• Hakuna uvujaji wowote chini ya gari
• Kioo chako cha mbele na madirisha ni safi
• Hakuna vizuizi vinavyokuzuia kuondoka
• Kama una mafuta ya kutosha kwa safari
• Kiti chako kimerekebishwa vizuri – angalia chini kwa taarifa zaidi
• Mkanda wa kiti umeshikizwa vizuri – na abiria wako wote wamefunga
mikanda yao (sheria inaagiza wewe na abiria wako wa kiti cha mbele
LAZIMA mjifunge mikanda)
• Kizuizi chako cha kichwa kimerekebishwa ili sehemu yake ya juu iwe
sawa na sehemu ya juu ya kichwa chako na kuna pengo dogo au
hakuna pengo kwenye sehemu hiyo na sehemu ya nyuma ya kichwa
chako-pia angalia vizuizi vya vichwa vya abiria wako
• Milango imebanwa na kufungwa vizuri
• Kuwa hakuna vitu vilivyozagaa vinavyoweza kukuchanganya wakati
unaendesha au vitu vinavyoweza kuruka ajali ikitokea
• Kuwa vifurushi vyovyote au vitu vingine vilivyobebwa vimefungwa
kiusalama
• Hakuna taa yoyote ya tahadhari inayowaka kwenye dashibodi
• Una leseni yako ya udereva, waraka wa usajili wa gari, stika ya leseni
ya barabara, na stika ya bima (stika zibandikwe ndani ya kioo cha
mbele).

Urekebishaji kiti ili kupata sehemu nzuri ya kuendeshea. Shika


usukani kwa mkono mmoja wakati unatumia mkono mwingine kulegeza
kizuizi cha mahali pa kiti. Sukuma kiti mbele au nyuma hadi pale
ambapo mguu wako wa kulia utakapokanyaga vizuri pedeli ya breki huku
ukiwa umepinda kidogo, si kunyooka. Ni muhimu kuweza kudhibiti pedeli
18
vizuri lakini kwa msukumo mzuri inapohitajika. Mikono yako iwe
imepinda kidogo kwenye kiwiko, ili uweze kuufikia usukani vizuri – usiwe
mbali sana kiasi cha kukufanya ujinyooshe ili kuufikia, wala mikono yako
isiwe karibu sana kiasi cha kupinda sana ili kuukamata usukani. Nyuma
ya kiti kuwe katika hali ya wima na si kunyooka. Lazima uweze kuona
vizuri juu ya usukani. Iwapo wewe ni mfupi unaweza kuinua kiti – la
sivyo, tumia mto thabiti.

Kurekebisha vioo vyako. Unahitaji kutumia vioo vyako sana wakati wa


kuendesha. Ni muhimu virekebishwe ili uweze kuviona kirahisi, na
vionyeshe vizuri eneo la nyuma.
Kioo cha ndani kionyeshacho nyuma - bila ya kuondoa kichwa chako
kutoka mahali pa kuendeshea, kishike kioo hicho na kukirekebisha ili
uweze kuliona dirisha la nyuma kwa ukingo wa kulia wa kioo ulioungana
na ukingo wa kulia wa dirisha la nyuma – lazima uone vizuri nyuma na
nyuma kulia kwa gari.
Kioo cha nje cha upande wa kulia – Geuza kichwa chako kidogo kutoka
mahali pa kuendeshea na kirekebishe kioo hiki ili uweze kuona pembeni
kidogo ya gari – kioo kitaonyesha upande wa nyuma kulia kwa gari.
Kioo cha nje upande wa kushoto - geuza kichwa chako kidogo upande wa
kushoto na rekebisha kioo kionyeshe upande wa nyuma wa kushoto wa
gari.

Kumbuka kuangalia ukaaji wa vioo vyako wakati wote wa kuondoka.


Kumbuka pia kuwa vioo vingine ni vya mbinuko na kuwa vitu
vinavyoonekana kuwa karibu kuliko ilivyo katika hali ya kawaida.

Maeneo yaliyofichika. Pamoja na ukweli kuwa umevirekebisha vioo


vyako kiusahihi kuna
maeneo mengi karibu na
gari lako ambayo huwezi
kuyaona – haya huitwa
“maeneo fiche”. Maeneo
haya yako upande wa
nyuma kushoto na kulia
kwa gari nje ya eneo
linaloonekana kwa vioo
vyako. Wakati wowote
unapohitaji kubadili
uelekeo wa gari lako,
kwanza angalia vioo vyako na kisha haraka geuza kichwa chako
19
kuangalia eneo fiche kwenye upande unaohitaji kwenda. Jizoeshe
kufanya hivi ili uweze kufanya haraka na bila taabu. Epuka kuendesha
kwenye maeneo fiche ya wengine – rudi nyuma polepole au endesha
mahali ambapo dereva mwingine anaweza kukuona kwa urahisi zaidi.

Kuwasha injini
Kabla ya kuwasha injini, hakikisha kuwa breki ya mkono imewekwa na
kuwa gari haliko kwenye gia – Angali kuwa wenzo uko kwenye
“KUEGESHA” (kwa otomatiki) au NYUTRO ( kwa manyu gia boksi). Pia
angalia kuwa hakuna aliyesimama mbele au nyuma ya gari. Weka
ufunguo kwenye swichi ya kuwashia na iwashe (mahali penye ON) –
dashibodi itaanza kufanya kazi. Zungusha ufunguo wa kuwashia mahali
pa kuwashia na sikiliza sauti ya injini – mara ukishasikia injini imeanza
kuunguruma achia swichi (angalia Kitabu cha Mwongozo kwa ushauri
wowote maalumu wa kutumia pedeli ya kichapuzi wakati wa kuwasha).
Iwapo una gari lenye injini ya dizeli lazima usubiri taa ya indiketa ya
PLAGI INAYONG’AA (kwa kawaida ni ya rangi ya chungwa) lazima kabla
ya kunyonga ufunguo kutoka ON, hadi START.

Kamwe usiendelee na stata kwa zaidi ya sekunde 10 – iwapo injini


haitawaka, achia swichi na subiri kwa dakika 5 hadi, 10, kisha jaribu
tena.

Wakati injini inafanya kazi angalia taa za indiketa na vipimia. Vionyeshe


kuwa kila kitu kiko sawa.

Iwapo umekuwa ukijaribu kuwasha injini ya petroli kwa muda fulani,


huenda labda ukawa umeijaza injini petroli. Iwapo hili litatokea kanyaga
pedeli ya kichapuzi hadi chini na acha hapohapo wakati unazungusha
swichi ya kuwashia ili kuwasha (START). Jaribu tena kama haifanyikazi
kama mwanzo. Mara injini itakapowaka, achia pedeli ya kichapuzi
haraka.

Angalia Kitabu cha Mwongozo kwa maelezo zaidi ya namna ya kutatua


tatizo la ugumu wakati wa kuwasha.

20
Kunyonga
Mwazoni ni changamoto kufanya vitendo vichache mfano kupinda, na hili
litahitaji umakini wako mkubwa. Kwa kufanya mazoezi na baada ya
muda, utakuwa na uwezo wa kuliongoza gari kirahisi na kwa kujiamini.
Kuzungusha usukani kulia hulifanya gari lako lipinde kulia na kuzungusha
usukani kushoto hulifanya gari lako kupinda kushoto.

Usijaribu kupinda usukani wakati gari limesimama, kwani hii husababisha


kuharibika mapema kwa matairi na mfumo wa usukani. Daima gari liwe
kwenye mwendo, hata kama ni polepole, wakati
unanyonga usukani shika usukani kama
inavyoonyeshwa
kwenye kielelezo –
Iwapo utauchukulia
usukani kama saa,
mikono yako itakuwa
kwenye saa 3.15 au
4.10.

Iwapo utaanza kwenye sehemu ya kawaida ya


kuendeshea na unataka kukata kona kali
kushoto, anza kwa kushika juu ya usukani kwa
mkono wako wa kushoto na kuvuta chini. Kisha
shika chini ya usukani kwa mkono wako wa kulia
na kupeleka juu. Shika juu ya usukani kwa
mkono wa kushoto tena na kusukuma chini.
Iwapo kona ni kali sana unaweza kurudia
kusukuma huku kwa mkono wako wa kulia na
kusukuma kwa mkono wako wa kushoto mara nyingi.

Unapotaka kwenda moja kwa moja tena unaweza kunyonga usukani


nyuma kwa mikono kwa kutumia njia ileile kwa kurudisha tofauti na
mwanzo (kuvuta kwa mkono wa kulia na kuvuta kwa kushoto). Hata
hivyo, wakati unaendesha kwa kasi ya kawaida ni rahisi kuuacha usukani
kuzunguka kurudi upande ulikotoka kwenye mikono yako wakati
unaendesha polepole. Uwe tayari kuushika usukani tena kurekebisha
mwelekeo wa mwisho wa gari.

Kamwe usipinde usukani sana wakati unaendesha kwa mwendo mkali –


gari linaweza kuteleza au kupinduka.
21
Kuondoka
Baada ya kuwa umewasha injini kwenye gari kwa kutumia gia boksi ya
manyu, kanyaga klachi, na ingiza gia ya kwanza. Kisha achia breki ya
mkono. Taratibu achia pedeli ya klachi mpaka sauti ya injini
itakapobadilika wakati gari linajaribu kuondoka – tumia nguvu kidogo
kwenye kichapuzi, na kisha polepole achia pedeli ya Klachi wakati huo
huo ukianza kukanyaga kwa nguvu kichapuzi. Gari litaanza kwenda, na
kadiri nishati zaidi inapopelekwa kwenye magurudumu mwendo
utaongezeka taratibu. Baadaye itakulazimu kubadili kuwa gia ya pili.

Kuondoka wakati gari lako limesimama juu ya kilima, tumia breki


ya mkono. Kanyaga pedeli ya klachi, ingiza gia ya kwanza, na kanyaga
kidogo kwenye kichapuzi. Kisha polepole achia klachi hadi utakaposikia
sauti ya injini inabadilika – ukiachia breki ya mkono gari litasimama na
kutulia – na, iwapo utakanyaga kichapuzi kidogo zaidi na polepole
ukaachia klachi moja kwa moja, gari litaanza kupanda kwenda mbele juu
ya kilima.

Kwa gari la mfumo wa otomatiki, kanyaga pedeli ya breki na hamisha


mahali pa kichaguzi kutoka kuegesha kwenda kuendesha. Kisha kanyaga
kichapuzi kidogo, achia breki ya mkono na kisha pedeli ya breki – gari
litaanza kupanda kwenda mbele. Taratibu za kuanza kilimani ni sawa na
giaboksi ya mkono, isipokuwa unaachia pedeli ya breki badala ya klachi.

Kubadili gia
Maelekezo haya yametumika tu unapokuwa unatumia giaboksi ya
manyu. Kubadili gia bila shida inaweza ikakuchukua muda mrefu
kujifunza.

Kubadili gia (juu). Ili kuongeza mwendo wa gari bila ya kuongeza zaidi
mzunguko wa injini unahitaji kubadili gia. Isikilize injini na usikie wakati
inaanza kuzunguka zaidi; huu ni wakati wa kubadili gia. Hatua ni:
• Kanyaga pedeli ya klachi chini wakati unaachia kichapuzi - klachi
ikanyagwe kwa kiasi cha sekunde kabla ya kuachia kichapuzi (siri ya
kwanza ya kubadilisha gia vizuri).
• Sogeza sehemu ya gia kutoka ilipo hadi kwenye gia mpya (mwanzoni
wakati wa mafunzo hili hasa litahusisha kutoka gia ya kwanza kwenda
ya pili – kupitia nyutro)- usilazimishe mahali pa gia – uweze
kuhamisha taratibu kwenda mahali papya kwa nguvu za wastani.

22
• Iache pedeli ya klachi ipande polepole, na wakati huohuo (au muda
mfupi baadaye) polepole kanyaga pedeli ya kichapuzi kwenda chini
(siri ya pili ya ubadilishaji gia vizuri).

Kubadili gia (chini)


• Achia kichapuzi na funga breki, hadi gari liende kwa mwendo
unaotakiwa
• Kanyaga klachi
• Peleka wenzo wa gia panapotakiwa gea ya chini
• Achia klachi polepole na ongeza moto kwenye kichapuzi.

Unaweza kurekebisha mwendo wako vizuri kwa kutumia moto wa


wastani kwenye kichapuzi na kusukuma klachi kiasi cha kutosha
kuachanisha kidogo injini. Njia hii ni nzuri wakati unataka kwenda
mwendo mdogo, mfano wakati unaegesha au kuendesha kwenye foleni.
Usiitumie mara kwa mara kwani utaharibu haraka klachi.

Kumbuka kuwa gari lazima lisimame kabisa kabla ya kuweka gia ya


kurudi nyuma.

Kuendelea kulidhibiti gari


Lazima daima ulidhibiti vilivyo gari. Kuwa makini na mwendo wako na
urekebishe kuendana na barabara na hali ya magari ilivyo mbele yako.
Uwe na tahadhari na tabiri kila ambacho wengine watafanya, ili
usilazimike kufunga breki ghafla au kukwepa ili kuepuka kugongana.
Iwapo utaona hatari mbele yako, mfano kona kali, punguza mwendo
kabla ya kupinda, na kisha endesha polepole kupita hapo – hili
litakuwezesha kulidhibiti gari vizuri kadiri ya mwelekeo wa gari.

Kamwe usiendeshe gari kwa gia ya nyutro au klachi ikiwa imekanyagwa.


Kwa hakika hupunguza udhibiti ulionao wa gari – iwapo unashuka
kilimani, gari litaongeza mwendo haraka na utatumia breki mara nyingi
kuendelea kulidhibiti gari. Kabla ya kushuka kilima kikali, chagua gia ya
chini, ili injini iweze kukusaidia kulizuia gari kwenda mwendo wa kasi
zaidi.

Kuwa makini zaidi kwenye barabara zisizo na lami, kwani matairi yako
yatakuwa yakikamata barabara kidogo, na kukufanya uwe na uwezekano
mkubwa wa kuteleza ikiwa utajaribu kwenda kwa kasi. Mwendo wako
uwe chini ya km 80kwa saa na nyonga usukani taratibu.
23
Kufunga breki
Iwapo unataka kupunguza mwendo wako fanya taratibu, ondoa mguu
wako kwenye kichapuzi. Hii itakufanya upunguze kasi yako. Wakati
unataka kupunguza mwendo haraka funga breki. Wakati mwendo
unapungua unatakiwa urudi kwenye gia za chini.

Umbali unaohitajika kusimamisha gari hutegemea hasa mwendo gani


unaokwenda – angalia kielelezo. Tambua kuwa kadiri unavyoongeza kasi
yako mara dufu umbali wako wa kusimama huongezeka mara tatu.
Iwapo unaendesha kwenye majimaji au barabara isiyo na lami matairi
yako yatakuwa na mgandamizo mdogo, hivyo umbali wako wa kusimama
unaweza kuwa mara mbili ya umbali ulioonyeshwa hapa. Iwapo gari lako
limejaza litakwenda pia mbali kabla ya kusimama. Kumbuka pia kuwa
magari makubwa na pikipiki daima huchukua muda kusimama kuliko
magari madogo.

Wakati unajua kuwa utasimama, punguza mwendo polepole.


Usisubiri hadi mwisho kufunga breki. Kanyaga pedeli ya breki polepole
kwanza na kisha kwa nguvu zaidi wakati umeanza kusimama. Achia
moto kabla ya gari kusimama, ili usimame bila taabu na vizuri. Kanyaga
pedeli ya klachi kabla ya kwenda kusimama, ili injini isishindwe
kuendelea. Iwapo utafunga breki kwa nguvu matairi yatajibana
(yataacha kuzunguka) na kuteleza kwenye ardhi – utashindwa kuudhibiti
usukani na umbali wako wa kusimama utaongezeka. Iwapo utateleza,
nyonga kwenye mwelekeo ambao sehemu ya nyuma ya gari inaelekea
na ondoa mguu wako kwenye pedeli ya breki hadi utakapolidhibiti tena
gari.

Iwapo utasimama ghafla (usimamaji wa dharura) Kanyaga pedeli


za breki kwa nguvu (lakini si nguvu sana kiasi cha kuyazuia matairi) na
wakati huohuo kanyaga klachi. Kitendo hiki hufanya injini izizuie breki,
na husaidia kuyazuia matairi kutokwenda. Pia hujirahisisha kwenye injini.

24
Umbali Halisi wa Kusimama
km 30 kwa saa
Umbali wa
mita 12 kufikiria
au urefu wa magari 3
Umbali wa kufunga
km 50 kwa saa breki

mita 23
au urefu wa magari 6

km 80 kwa saa
mita 53
au urefa wa magari 13

km 100 kwa saa

mita 73
Wastani wa urefu wa gari = mita 4 au urefu wa magari 18

Kurudi nyuma
Kurudi nyuma ni hatari zaidi ya kwenda mbele, hivyo usirudi nyuma zaidi
ya inavyotakiwa. Wakati unataka kurudi nyuma kwanza ingiza gia ya
kurudi nyuma – kamwe usifanye hivi mpaka gari lisimame kabisa. Kisha
weka mkono wako wa kulia kwenye usukani mahali ambapo ni sawa na
saa 6 kamili kwenye saa na geuza kichwa chako na sehemu ya juu ya
mwili wako kushoto. Hili litakuwezesha kuangalia kupitia begani kwako
na kupitia kwenye dirisha la mwisho-angalia kielelezo. Endesha polepole
wakati unarudi nyuma. Ikibidi dhibiti mwendo wako kwa kukanyaga
vizuri pedeli ya klachi.

Kabla ya kuanza kurudi nyuma lazima


uhakikishe kuwa hakuna mtu – labda

25
mtoto - aliyejificha kwenye eneo fiche. Angalia kwenye mwelekeo wako
lakini angalia pia pande nyingine. Ni vizuri kumpata mtu kusimama
nyuma ya gari kukuongoza. Hili ni muhimu hasa kama unaendesha gari
la mizigo au gari lolote ambalo kuna ugumu dereva kuona eneo la nyuma
ya gari.

Kumbuka kuwa, kama unapinda wakati unarudi nyuma, sehemu ya


mbele ya gari itakwenda upande tofauti wa mwelekeo. Kuwa makini
kuona kuwa sehemu ya mbele haigongi kitu chochote wakati wa kupinda.

Kuliacha gari
Pindi gari lako likisimama weka breki ya mkono. Kwa gari lenye mfumo
wa otomatiki sogeza wenzo wa kichaguzi kwenye kuegesha. Kwa gari la
giaboksi ya manyu peleka wenzo wa gia kwenye nyutro (madereva
wengine hupenda kuyaacha magari yao kwenye gia ya kwanza au ya
kurudi nyuma). Kisha zima injini yako.

Zima taa zote, vifuasi, kiyoyozi n.k. na funga madirisha. Zungusha


funguo za kuwashia kwenye sehemu ya kuzimia na kutoa funguo.
Angalia kupitia bega lako la kulia na iwapo hakuna gari linalokuja, fungua
mlango na kutoka nje. Hakikisha unalifunga gari. Tembea kupitia upande
wa nyuma wa gari unaoangalia barabara na kisha vuka barabara.
Waeleze abiria wako kushuka kwenye gari kwa upande wa kushoto
ambako kuna uwezekano mdogo wa wao kugongwa na magari
yanayopita.

26
Uendeshaji salama barabarani

Kuendesha barabarani
Endesha kwa usalama. Sheria inasema USIENDESHE kwa hatari au
kwa uzembe. Hii huelezwa kama tabia ambayo dereva mwenye ujuzi
ataichukulia kama hatari – mfano kulipita gari jingine mahali ambapo
pana kona kali kiasi kuwa huwezi kuona vizuri mbele.

Endesha kwa makini. Sheria inasema USIENDESHE bila kujali. Lazima


uwe macho na uchukue tahadhari wakati wote. Ni kutokuwa makini
kuruhusu kusumbuliwa wakati unaendesha au kutoangalia vizuri kuona
kama barabara haina kikwazo kabla ya kuiingia.

Wathamini wengine. Usiendeshe kama vile uko kwenye mashindano


na madereva wengine. Endesha kwa utulivu na kuwa mvumilivu iwapo
wengine watafanya makosa. Usiyaruhusu magari madogo kutoka kwenye
njia yako.

Kuwa mwangalifu – usisumbuliwe. Epuka kuzungumza au kubishana


na abiria. Usile, usinywe, usisome au kuvuta sigara wakati unaendesha –
hata kama una kifaa cha kuifanya mikono isiwe na kazi. Tafuta sehemu
nzuri usimame, na kisha tumia simu yako.

Endelea kutazama
sehemu zote. Usiangalie
sehemu moja kwa zaidi ya
sekunde 2 – endelea
kuhamisha macho yako
sehemu zote kuhakikisha
kuwa hukosi kuona kitu
chochote – angalia mbele
zaidi na kushoto na kulia –
na kila sekunde 5 angalia
kwenye vioo vyako, hata
kama unadhani hakuna magari karibu.

Jifunze Uendeshaji wa Kujihami. Angalia nje kwa uwezekano wa


matatizo mbele, mfano mtoto anayecheza mpira, au gari linakuja kwa
kasi pembeni mwa barabara. Iwapo kuna gari pembeni mwa barabara
lenye dereva ndani, tegemea litaingia mbele yako ghafla. Iwapo basi
27
limesimama mbele yako, jitayarishe kwa abiria kuvuka barabara kutoka
nyuma yake. Iwapo utaona uwezekano wa tatizo kama hili punguza
mwendo na jiandae kuchukua hatua kuepuka kugongana.

Tumia ishara kuwaonya na kuwaarifu watumiaji wengine wa


barabara. TUMIA viashiria vya
Ishara kwa watumiaji mwelekeo au ishara ya mkono kabla
wengine wa barabara ya kubadili mwendo au mwelekeo,
kusimama au kuondoka. Toa ishara
Kupinda kulia inayoeleweka kwa muda wa kutosha
(sekunde 5-10 kabla ya kitendo), na
kumbuka kuacha baada ya kutenda
kitendo.

Tumia honi tu iwapo ni lazima


uwaonye watumiaji wengine wa
Kupinda kushoto barabara kuwa uko pale. Iwapo
madereva watatumia honi kupita
kiasi, watumiaji wa barabara
hawatasikiliza. Usitumie honi
“kusalimia” au kuonyesha
umekasirishwa na mtu, au kumueleza
dereva aliye mbele kuharakisha na
kuongeza mwendo. Usitumie honi nje
Kupunguza mwendo ya hospitali, mahakamani na shuleni,
au kati ya saa 5 usiku na saa 12
asubuhi mjini. Epuka kutumia honi
kwenye Hifadhi za Taifa na Mbuga za
Wanyama.

Washa taa zako tu pale utakapotaka


kuwajulisha watumiaji wengine wa
barabara kuwepo kwako, katika
mazingira ambayo honi inaweza kutosikika au mjini wakati wa usiku.
Usiwashe taa zako ghafla kuonyesha kuwa umekasirika au kujaribu au
kuomba haki ya njia. Iwapo dereva mwingine atakuwashia taa ghafla,
usiichukulie kuwa ni ishara ya kukuruhusu kupita.

Fuata alama za barabarani. LAZIMA ufuate alama zote za barabarani,


na ishara na michoro ya barabarani. Hakikisha kuwa unajua na kutenda
kulingana na alama na michoro yote mingine ya barabarani. (Angalia
28
Kanuni za Barabara kwa ufahamu zaidi wa alama za barabarani) LAZIMA
pia ufuate ishara zinazotolewa na maofisa wenye sare za polisi na watu
wengine wenye mamlaka. Ishara zao zinazidi alama na michoro yote
mingine.

Alama za maofisi wa Polisi au watu wengine


wenye mamlaka

SIMAMA Askari wa barabarani SIMAMA Askari wa barabarani


anayeashiria kwa mbele anayeashiria kwa nyuma

SIMAMA Askari wa barabarani SIMAMA Askari wa barabarani


anayeashiria mbele na nyuma anayeashiria kwa upande mmoja

PITA PITA

29
Kuondoka. Kabla ya kuondoka, daima tumia vioo vyako, toa ishara na
tazama nyuma ya mabega yako kuona kuwa barabara haina kikwazo.
Ondoka iwapo umejiridhisha kuwa ni salama kufanya hivyo.

Pita kushoto. LAZIMA uendeshe upande wa kushoto wa barabara.


Vyombo vinavyokwenda polepole (baiskeli, mikokoteni inayokokotwa na
ng’ombe kwa mikono na matrekta, n.k.) lazima vipite upande wa
kushoto na kuruhusu magari yaendayo kasi kuvipita.

USIENDESHE kwenye njia ya watembea kwa miguu au maeneo ya


watembea kwa miguu.

Vioo – alama – kitendo. Tumia vioo vyako daima ili wakati wote ujue
kilichoko nyuma na pembeni yako. Tumia vioo vyako vizuri kabla ya
kupinda au kubadili njia, na kisha toa ishara ifaayo.

Chunguza
katika kioo,
pima, amua

Toa ishara
sahihi

Fanya tendo

Waendesha pikipiki wanashauriwa kuangalia nyuma yao kabla ya kubadili


njia na kupinda kulia.

30
Usiweke msururu wa magari nyuma yako. USIENDESHE taratibu bila
sababu. Iwapo unaendesha gari kubwa au linalokwenda polepole na kuna
foleni ya magari nyuma yako, LAZIMA utafute sehemu ya kuingilia kwa
usalama na ruhusu magari mengine yakupite.

Foleni ya magari. Iwapo kuna msururu wa magari mbele, ingia nyuma


yake. Usiuruke msururu huo. Kuwa mvumilivu. Daima simamisha gari
lako ili uweze kuyaona matairi ya nyuma ya gari la mbele – linaweza
kurudi nyuma kidogo wakati linaanza kuondoka. Iwapo utafika kwenye
alama za pundamilia wakati uko kwenye foleni, usisimame juu ya alama
hizo za kuvukia– ziache wazi ili watembea kwa miguu wazitumie.

Endesha kwenye njia. Pale penye njia zaidi ya moja zenye mwelekeo
mmoja, tumia njia ya kushoto kwenda mbele na nyingine kwa ajili ya
kuvipita vyombo vingine, kupinda kulia, au kuyapita magari
yaliyosimama. Usibaki kwenye njia ya kulia muda mrefu zaidi ya
unaohitajika. Wakati wa kubadili njia kumbuka vioo – ishara - kitendo.

Mwendo
Endesha kwa mwendo salama. USIENDESHE kwa mwendo ambao
unaweza kuwa wa hatari kwa wengine. Daima rekebisha mwendo wako
kulingana na mazingira. Kwa mfano, punguza mwendo kama unakaribia
kona, daraja jembamba, au makutano, au eneo lenye watembea kwa
miguu wengi. Chagua gia itakayokuwezesha kulidhibiti gari zaidi.
Endesha polepole zaidi iwapo barabara ina majimaji, au huwezi kuona
vizuri. Endesha polepole zaidi usiku, kwa kuwa ni vigumu kuwaona
watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wanyama, na magari
yaliyoegeshwa au kuharibika.

Kuendesha kwenye barabara zisizo na lami. Daima endesha


polepole zaidi kwenye barabara zisizo na lami, nyonga usukani polepole,
na epuka kufunga breki kwa nguvu. Barabara zisizo na lami zina ardhi
inayoteleza zaidi ya zenye lami, na matairi yako yana pungufu ya
asilimia 50 ya kiwango cha ubanaji.

Endesha katika namna ya kusimama wakati wote kuepuka


kugonga kitu chochote. Endesha katika mwendo utakaokuruhusu
kusimama vizuri katika umbali unaouona kukufaa. Usiendeshe kwa kasi
kwenye kona au juu ya kilele cha mlima – itakuwaje iwapo gari
litaharibika mahali ambapo huoni vizuri?
31
Kumbuka kuwa, ukiongeza maradufu mwendo wako, umbali wako wa
kusimama unaongezeka mara tatu – angalia mchoro. Umbali wa
kusimama utakuwa mrefu zaidi ya huu kwenye barabara zenye majimaji
zisizo na lami. Magari makubwa na pikipiki daima huchukua muda mrefu
kusimama kuliko magari madogo.

Kama sheria/kanuni ya jumla daima acha pengo la sekunde – 2 kati ya


gari lako na lililo mbele yako. Moja ya njia inayotumika kupima pengo hili
wakati wa kuendesha ni kuhesabu “elfu moja na moja, elifu moja na
mbili” wakati gari lililo mbele yako litakapopita sehemu iliyowekwa.
Iwapo utapita mahali palipowekwa kabla ya kumaliza hesabu yako, uko
karibu mno.

Fuata ukomo wa mwendo. USIPITISHE mwendo wa kiwango cha juu


kilichoruhusiwa cha gari lako. Kwa sasa ukomo wa kisheria ni:

Km 50 kwa saa kwa magari yote kwenye maeneo ya makazi (hata


kama hakuna alama ya barabarani)
Km 80 kwa saa kwa magari makubwa ya mizigo (> uzito halisi wa gari
wa kg 3500) na magari ya huduma za umma (mabasi, mabasi ya safari
ndefu, lakini si teksi) nje ya maeneo ya makazi
Km 100 kwa saa ni mwendo unaoshauriwa wa juu kwa magari madogo
na magari mengine ya wastani nje ya eneo la makazi.

Ukomo huu wa mwendo unaweza kutofautiana kwa mwendo wa vijijini


unaoonyeshwa na alama za udhibiti za barabarani. USIZIDISHE mwendo
wa mwisho wa juu zaidi unaoonyeshwa kwenye alama. Kumbuka kuwa
ukomo wa mwendo haumaanishi kuwa daima itakuwa salama
kuendesha katika mwendo huo. Lazima uendeshe katika mwendo
ambao ni salama kwa barabara hiyo, vyombo vingine vya usafiri na hali
ya hewa.

Kulipita gari jingine


Kabla ya kulipita gari jingine LAZIMA uhakikishe kuwa:
• barabara haina vikwazo vyovyote
• gari lililo nyuma halijaanza kulipita gari lako
• gari la mbele halijaanza kulipita gari jingine
• kuna upenyo mkubwa wa kutosha mbele ya gari unalotaka kulipita

32
Usilipite gari jingine isipokuwa kama una uhakika unaweza kufanya hivyo
bila ya kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa barabara au kwako
mwenyewe. Iwapo una mashaka usilipite gari jingine.

Usilipite gari linalotembea au lililoegeshwa:


• iwapo gari linakaribia kutoka upande mwingine – isipokuwa kama una
uhakika unaweza kufanya hivyo bila ya kulilazimisha gari hilo
kupunguza mwendo au kupinda ghafla ili kukuepuka
• pale gari linalohitajika kupitwa linaashiria kupinda kulia
• pale ambapo huwezi kuona umbali wa kutosha mbele, mfano kwenye
kona au karibu ya kilele cha kilima
• kwenye makutano
• kwenye alama za pundamilia au karibu na alama hizo au mahali
pengine wanapovuka watembea kwa miguu
• kwenye reli au karibu na reli
• ambapo unatakiwa kuingia kwenye njia iliyo maalum kwa mabasi au
waendesha baiskeli
• ambapo unatakiwa kupita kwenye eneo lenye mistari ya mshazari au
ya umbo la V
• ambapo kulipita gari jingine hakuruhusiwi kwa alama ya “Hakuna
kulipita gari jingine” au michoro ya barabarani.

Michoro ya barabarani ambayo inakuonyesha mahali ambapo


unaweza kulipita gari jingine. Iwapo mstari mweupe wa katikati ya
barabara unachorwa kwa kukatikakatika (----) unaweza kuvuka ili
kulipita gari jingine, kama ni salama kufanya hivyo. Iwapo mstari
mweupe wa katikati ya barabara haujakatikakatika ( ____ ), USIVUKE
mstari huo, isipokuwa kama ni muhimu kulipita gari lililosimama au
kupinda kwenye barabara ya upande mwingine. Pale ambapo pana
mistari miwili mstari ulio karibu na wewe ndio utakaoutumia.

Unaweza kuvuka
mstari wa katikati
USIVUKE mstari USIVUKE mstari kama ni salama
wa katikati wa katikati kufanya hivyo

33
Sehemu zisizo salama kulipita gari jingine

Alama za pundamilia Karibu na


makutano

Karibu na kilele cha Kwenya kona kali


kilima

Kwenye kona isiyo na michiro Mahali reli inapokatisha


ya kuruhusu kulipita gari barabara
jingine

34
Utaratibu wa msingi wa kulipita gari jingine. Kabla hujaanza kulipita
gari hakikisha kuwa barabara haina vikwazo mbele kukuwezesha kulipita
gari na kurudi kushoto bila ya
kulilazimisha gari jingine
kupunguza mwendo au kupinda
haraka ili kukukwepa.
Kama una shaka – usilipite gari
jingine. Tumia vioo vyako
kuona kuwa hakuna gari
linalokupita. Toa ishara kabla
ya kuanza kutoka [1]. Kuwa
mwangalifu zaidi usiku na
kwenye ukungu au mvua kubwa
wakati inapokuwa vigumu
kuamua kuhusu mwendo na
umbali. Kumbuka: vioo -
ishara - kitendo

Iwapo huna hakika na kile


ambacho dereva wa gari la
mbele atafanya, piga honi.

Unapokuwa umeanza kulipita


gari jingine, [2] nenda haraka
kulipita gari hilo na liache kwa
umbali fulani. Unapozipita
baiskeli au pikipiki vipatie
angalau umbali zaidi kuliko ule wa gari. Rudi upande wa kushoto wa
barabara haraka iwezekanavyo, [3] lakini usirudi haraka kiasi kuwa gari
unalolipita kulazimika kufunga breki au kupinda haraka ili kukukwepa.
Fanya hivi kwa kuliangalia gari kwenye kioo chako.

Iwapo gari lingine litakuwa linakupita. Usiongeze mwendo wako


unapokuwa unapitwa. Sogea kushoto kama unaweza kufanya hivyo kwa
usalama. Punguza mwendo ikibidi kuliacha gari linalokupita lipite haraka
na kwa usalama.

Lipite gari lingine upande wa kulia. Daima lipite gari jingine upande
wa kulia, isipokuwa kama:

35
• gari la mbele yako linaonyesha ishara ya kupinda kulia, na kuna nafasi
ya kulipita kwa usalama kushoto (usiendeshe kwenye njia ya waendao
kwa miguu)
• magari yanakwenda polepole kwenye njia, na magari kwenye njia ya
kulia yanakwenda polepole zaidi yako.

Pale wengine watakapokuashiria upite. Wakati mwingine dereva wa


gari la mbele yako anaweza kukuashiria kuwa barabara haina vikwazo
kwako kupita. Usidhani kuwa dereva yuko sahihi. Lipite gari hilo tu pale
utakapoona kuwa barabara haina kikwazo chochote.

Iwapo gari unalolipita litaongeza mwendo au kuonyesha kukataa


kwa namna yoyote, acha kujaribu kulipita. Usishindane kamwe na dereva
mwingine.

Makutano
Kukaribia makutano ya barabara. Kugongana kwingi hutokea kwenye
makutano, hivyo chukua tahadhari zaidi. Angalia makutano yaliyo mbele
yako, na fikiria hatua ipi ya kuchukua, iwapo utatakiwa kufanya hivyo.
Hakikisha kuwa gari lako liko mahali sahihi kwa hatua unayotaka
kuichukua na kuwa unaendesha kwa mwendo unaofaa.

Kaa kwenye njia au mahali


sahihi. Iwapo barabara itakuwa na
alama za njia, ingia kwenye njia sahihi
kwa wakati mzuri. Fuata mishale
inayoonyesha njia ipi ni ya mwelekeo
upi. Usibadili njia bila sababu ya msingi. Usiivuke
Iwapo kuna foleni ya magari mbele yako, foleni
usijaribu kuivuka foleni hiyo – kuwa
mvumilivu.

Fuata kanuni za kipaumbele. Kwenye


makutano yenye alama ya “SIMAMA” (pia itakuwa na mstari mweupe
usiokatikakatika wa “SIMAMA” kukata barabara) LAZIMA usimame kabisa
kwenye mstari huo. Angalia kwa makini kuona kama kuna gari lolote
linalokuja. Subiri upate upenyo salama kabla ya kupita.

Kwenye makutano yenye alama au mchoro wa “KURUHUSU” (mstari


mweupe uliokatikatika kukata barabara) LAZIMA uyaruhusu magari ya
36
kwenye barabara nyingine. Subiri upate upenyo salama, kabla ya kupita
– usiyalazimishe magari mengine kupunguza mwendo haraka au
kukukwepa ghafla.

Pale ambapo hakuna alama na mchoro wowote, daima kumbuka


kuyaruhusu magari yanayotoka kulia.

Haki za msingi za njia

SIMAMA

Simama
na subiri

RUHUSU GARI LIPITE

Simama
na subiri

Angalia vizuri. Usitupe macho tu kuona kama kuna kitu kinakuja –


angalia vizuri – angalia waendesha pikipiki na baiskeli. Iwapo utatumia
zaidi ya sekunde 2 kuangalia mwelekeo mmoja, kisha lazima uangalie
tena mwelekeo mwingine kuona kama bado hakuna vikwazo.

Pale ambapo una haki ya kupita, nenda mbele kwa tahadhari na uwe
tayari ikibidi kupunguza mwendo na kusimama kuepuka kugongana.

Usiingie kwenye makutano mpaka njia iwe salama. Usisababishe


msongamano bila sababu. Subiri na ruhusu magari mengine yapite
37
mbele yako. Kama madereva watakuwa wavumilivu na kutumia maarifa
yao ya kawaida, kila mmoja atafika anakokwenda kwa haraka zaidi.

Kupinda kulia
1. Hakikisha usalama kabla ya kupinda kulia, tumia vioo vyako kuona
kuwa magari yaliyo nyuma yako yapo umbali salama
2. Onyesha ishara ya kupinda kulia na anza kwenda polepole
3. Nenda kwenye sehemu ya kushoto ya katikati ya barabara
4. Mara tu panapokuwa na upenyo salama wa magari yanayokuja
mbele yako pinda kulia-usipite njia ya mkato.

Angalia waendesha baiskeli, pikipiki watembea kwa miguu – iwapo kuna


watembea kwa miguu wanaovuka barabara kwenye sehemu unayoelekea
kupinda, lazima usimame na kuwaacha wapite.

Waangalie watumiaji wengine wa barabara, hususan waendesha


pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu, na wajulishe kile unachotaka
kufanya kwa kuonyesha ishara vizuri.

Yaruhusu magari marefu kupinda. Yanaweza kutumia upana wote wa


barabara ili kupinda.

38
Kupinda kushoto
1. Hakikisha usalama kabla ya kupinda kushoto, tumia vioo vyako
kuona kuwa hakuna gari linalokuja nyuma yako upande wa kushoto
2. Onyesha ishara ya kupinda kushoto na anza kwenda polepole
3. Kama barabara haina vikwazo pinda huku ukiwa karibu na ukingo wa
upande wa kushoto wa barabara (madereva wa magari marefu
wanaweza kuhitaji kwenda katikati ya barabara ili kuweza kupinda).
Kuwa makini na waendesha baiskeli na pikipiki ambao wanaweza
kutokea kwa upande wako wa kushoto - waache wakupite na angalia
usalama kabla ya kupinda. Kuwa makini na watembea kwa miguu -
iwapo kuna watembea kwa miguu wanaovuka barabara upande
unaopindia, lazima usimame na kuwaacha wavuke.

KAMWE usilipite gari lingine na kisha kupinda kushoto mbele ya gari hilo.

Angalia kwenye
kioo chako kuona
kama pikipiki au
baiskeli zinakuja
upande wako wa
kushoto

Kupinda kwenye barabara mbili zinazokwenda upande mmoja.


Wakati unapita au unapinda kulia kwenye barabara mbili za upande
mmoja, angalia ili uone iwapo nafasi kati ya barabara hizo mbili (kati)
ina upana wa kutosha kumudu urefu wote wa gari lako. Iwapo hivyo
ndivyo, pita kwa usalama kwenda katikati na kisha subiri pale hadi
upatikane upenyo salama wa magari kwenye barabara ya pili. Iwapo
39
eneo la katikati halina upana wa kutosha, lazima usubiri hadi pale
utakapoweza kuvuka njia zote mbili kwa pamoja.

Kupinda kulia kwenye makutano ya barabara mbili wakati gari


linalokuja pia linapinda
kulia. Utaratibu wa
kawaida ni kupinda kulia
mbele ya gari jingine
(angalia kielelezo hapo
chini). Gari jingine
linaweza kukuziba kuona
magari yanayokuja, hivyo
endelea kwa tahadhari na
usipinde mpaka uwe na
uhakika kuwa njia iko
salama.

Fuata ishara ya taa za barabarani. LAZIMA usimame nyuma ya


mstari mweupe wa “SIMAMA” isipokuwa kama ishara ni ya kijani. Kama
taa za njano zitawaka unaweza kupita iwapo tu umeupita mstari wa
simama au uko karibu nao sana kiasi kuwa kusimama kunaweza
kusababisha kugongana. Elekea kwenye taa kwa mwendo ambao
utakuwezesha kusimama haraka iwapo taa zitabadilika kuwa njano.

Nenda mbele tu wakati taa za kijani zitakapowaka, iwapo njia yako haina
vikwazo, au unajiandaa kupinda kulia.

Iwapo taa za barabarani hazifanyi kazi, na hakuna ofisa wa polisi


anayeongoza magari, nenda mbele kwa makini, na toa kipaumbele kwa
magari yanayotoka kulia kwako.

Kuendesha kwa kujihami. Kwa mfano, wakati unasubiri kupinda


kwenda barabara kuu kutoka kwenye barabara za pembeni hakikisha
kuwa gari linalotoka kulia na kuashiria kwenda kushoto linaanza kupinda
kabla hujaendelea - ikiwa dereva mwingine hana lengo la kupinda
kushoto, lakini amesahau kuondoa ishara baada ya kupinda kwa
mwanzo.

40
Ushauri maalumu kwa madereva kwenye sehemu zenye
mzunguko
Kabla hujafika kwenye kiplefti hakikisha unapunguza mwendo wako,
amua ni njia ipi unahitaji kupitia, angalia kioo chako, na ingia kwenye
njia sahihi (angalia ushauri hapo chini) ukifika kwenye kiplefti yaruhusu
magari ambayo tayari yako kwenye mzunguko yapite. Angalia kwa
makini waendesha baiskeli na pikipiki, ambao inaweza kuwa vigumu
kuwaona iwapo kuna magari mengi. Kumbuka kuwa pia kunaweza kuwa
na watembea kwa miguu wanaovuka barabara - kutoka kushoto na pia
kulia.

Wakati unapinda kushoto:


1. Ashiria kupinda kushoto
2. Pita kwenye njia ya kushoto
3. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko
4. Pita kushoto kwenye mzunguko
5. Endelea sehemu ya kutokea, ukiwa bado unaendelea kuashiria
kushoto.

Njia sahihi ya kuitumia kwenye mzunguko

Wakati unakwenda mbele moja kwa moja:


1. Pita kwenye njia ya kushoto (isipokuwa kam njia ya kushoto
imeonyeshwa kwa ajili ya magari yanayopinda kushoto tu) –
usionyeshe ishara
2. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko yapite
3. Ungana na magari, yaliyo kwenye njia ya kushoto

41
4. Onyesha ishara ya kwenda kushoto baada ya kupita njia ya kutokea
kabla ya ile unayohitaji
5. Endelea kwenye njia yako ya kutokea, ukiwa bado unaonyesha ishara
ya kwenda kushoto.

Wakati wa kupinda kulia au kuzunguka:


1. Onyesha ishara ya kwenda kulia
2. Pita kwenye njia ya kulia
3. Yaruhusu magari yaliyo kwenye mzunguko
4. Jiunge na msururu, pita kulia
5. Endelea kuashiria kwenda kulia hadi upite barabara ya kwanza ya
kutokea kabla ya ile unayohitaji, kisha onyesha ishara ya kwenda
kushoto
6. Endelea sehemu ya kutokea.

KAMWE usisimame au kuegesha gari kwenye mzunguko. Wakati uko


kwenye mzunguko usilipite gari refu – linaweza kukugonga.

Uendeshaji wa usiku au kwenye hali mbaya ya hewa


Endesha kwa mwendo ambao utakuruhusu kusimama katika
umbali unaouona unafaa. Iwapo utashusha taa zako (yaani kuzifanya
zimulike chini), au kumulikwa na taa za magari yanayokuja lazima
upunguze mwendo – mbele gizani kunaweza kuwa na gari bovu au
mwendesha baiskeli.

LAZIMA utumie taa usiku (adhuhuri hadi alasiri) au mchana ambapo


ni vigumu kuona kwa sababu ya moshi, ukungu, mavunde au mvua
kubwa. Kwa mwongozo wa jumla washa taa zako unapokuwa huwezi
kuona vizuri kwa zaidi ya mita 100. Usichelewe kuziwasha-zinakufanya
uonekane zaidi kwa wengine.

Angalia taa zako za mbele kuwa ni safi, zinafanya kazi na


zimerekebishwa vizuri. Taa lazima ziwekwe kiusahihi ili zitoe mwanga
wa kawaida bila ya kuwaathiri madereva wengine - fundi wa magari
mwenye ujuzi anaweza kukusaidia kuangalia.

Tumia taa zinazomulika chini:


• Wakati magari yanakuja mbele yako
• Wakati unaendesha nyuma ya gari, au unalipita gari jingine
• Wakati unaendesha mijini ambako kuna mwanga wa kutosha mtaani.

42
Usiwafanye watumiaji wengine wa barabaraa kutoona vizuri. Usiwashe
taa za mavunde au taa nyingine isipokuwa kama kuna mavunde sana au
ukungu.

Mulika taa zako chini kwa ajili ya gari linalokuja

Mulika taa zako chini wakati unalifuata gari jingine

Kurudi nyuma
USIRUDI nyuma zaidi ya inavyotakiwa.

Kabla ya kurudi nyuma hakikisha kuwa hakuna watembea kwa miguu au


vitu kwenye barabara nyuma yako-kumbuka kuwa watoto wadogo
wanaweza kuzibwa na sehemu ya nyuma ya gari. Rudi nyuma kwa
makini na kamwe isiwe zaidi ya inavyotakiwa. Kama hutaweza kuona
vizuri, mtafute mtu akuongoze. Mtu huyu pia anaweza kuwatahadharisha
watumiaji wengine wa barabara kupisha. Tumia taa za kurudia nyuma
kuwafanya wengine wajue wakati wa mchana, na kuona vizuri wakati wa
usiku. Usihangaike barabarani – liweke gari lako mbali kidogo na ukingo
wa barabara.

Kuwa makini hasa wakati unarudi nyuma ili utoke kwenye jengo, uzio,
kiwanja cha nyumba – ukuta au uzio unaweza kuwaziba watembea kwa
miguu ambao wanakaribia kupita sehemu ya kutokea gari. Ikiwezekana,
geuzia ndani, ili uweze kutoka nje kwa mbele.

43
Usirudi nyuma
kamwe kwenye
barabara ndogo
pembeni mwa
barabara kuu. Usirudi
nyuma kamwe
kwenye makutano
makuu. Usirudi
nyuma kamwe
mahali wavukapo
watembea kwa
miguu, au mahali reli
inapokatisha
barabara.

Kuwajali watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa


barabara wanaoweza kuathirika
Kuwa makini na watembea kwa miguu. Watembea kwa miguu wako
katika hatari kubwa pindi wanapogongwa na magari. Na watembea kwa
miguu wengi, hususan wale wa maeneo ya vijijini, hawajazoea barabara
zenye magari na hawajui jinsi barabara ilivyo hatari. Endesha kwa makini
sana na punguza mwendo hadi km 50 kwa saa au chini ya hapo iwapo
kuna watembea kwa miguu mahali hapo, hususan katikati ya miji yenye
watu wengi, kwenye masoko na karibu na vituo vya mabasi. Kuwa
makini na watembea kwa miguu wanaovuka barabara ghafla kutoka
nyuma ya gari lililoegesha au kusimama (labda basi).

44
Kuwa makini sana kama watoto wako karibu, na wakati unaendesha
karibu na shule. Usiwategemee watoto kutenda kama watu wazima.
Uwezo wao wa kuona na kusikia una ukomo na hawawezi kutambua
mwendo vizuri. Hawako makini, na wanapokuwa hatarini wanaweza
kusimama tuli kwa hofu, badala ya kuondoka mahali hapo. Mahali
ambapo pana watoto punguza mwendo na kuwa makini sana.

Wasaidie wazee na walemavu


pindi inapokuwa vigumu kwao
kuvuka barabara. Waache
wavuke kama ni salama
kufanya hivyo. Daima punguza
mwendo unapokuwa karibu na
shule na hospitali.

Iwapo kuna watembea kwa


miguu wanaovuka barabara
mahali ambapo unapinda
kuelekea huko, simama na kuwaacha wavuke mbele yako.

Alama za Pundamilia. Unapofika kwenye mahali pa kuvukia waenda


kwa miguu penye alama za mistari myeupe (“alama za pundamilia”) uwe
tayari kupunguza mwendo na kusimama kuwaacha watu wawavuke.
LAZIMA usimame kama mtu yeyote anavuka au anakaribia kuvuka.
USILIPITE gari lolote ambalo limesimama kuruhusu watembea kwa
miguu kuvuka. Na USIEGESHE gari lako kwenye kivuko cha waendao
kwa miguu – au ndani ya eneo la umbali wa mita 5 kutoka alama hizo.

45
Ishara zinazoongoza kuvuka kwa watembea kwa miguu. Sehemu
nyingine za kuvukia zinaongozwa na taa za barabarani. Fuata ishara za
taa za barabarani. Watembea kwa miguu wanaweza kuvuka barabara
mbele yako, taa NYEKUNDU ikiwa inawaka.

Kuwa makini na wandesha pikipiki na baiskeli. Vyombo vyenye


magurudumu mawili ni vigumu zaidi kusimama ukilinganisha na magari
makubwa. Daima viangalie vyombo hivyo unapoingia na kutoka kwenye
makutano. Waachie nafasi ya kutosha waendesha pikipiki na baiskeli
wakati unawapita, hususan iwapo unaendesha gari refu au gari linalovuta
tela. Kamwe usiwapite na kupinda karibu mbele yao. Kadhalika wapite
kwa uangalifu waendesha mikokoteni.

Kurudi ulikotoka

Wakati mwingine utahitaji kurudi kwenye mwelekeo uliotokea. Mjini


fanya hivi kwa kupinda kushoto (au kulia) na kuzunguka mitaa hadi
urudi kwenye barabara uliyotoka – hili hukuepusha kurudi nyuma
ulikotoka. Pia unaweza kutumia mzunguko kwa usalama kubadili
mwelekeo. Pia unaweza kurudi ulikotoka kwa kutumia sehemu ya
kuegeshea au eneo la wazi ambapo unaweza kuzunguka kwa usalama
nje ya barabara yenye magari yanayopita.

Iwapo huwezi kufanya moja ya haya utatakiwa kupinda katika umbo la U


au kugeuza kwa kurudi nyuma. Iwapo barabara ni pana vya kutosha
unaweza kugeuza gari katika umbo la U, lakini zingatia kuwa kugeuza
kwa U aghalabu hukatazwa kwenye barabara pana na barabara mbili
(angalia alama za kudhibiti za barabarani) kwani huvuruga kasi ya
magari na si salama. Katika mazingira haya toka nje ya barabara kuu
kwenye upande wa barabara usio na magari mengi na geuza gari lako
kwenye barabara hiyo.

Iwapo utatakiwa kugeuza kwa


kurudi nyuma chagua mahali
ambapo unaweza kuona mbali
mbele na nyuma. Ikiwezekana
tumia upande wa kushoto
pembeni ya barabara, kisha
pinda kulia kubadili mwelekeo –
angalia kielelezo. Usifanye hivi
iwapo kuna magari mengi
46
upande huo wa barabara – tafuta barabara isiyo na magari mengi.

Katika barabara isiyo na magari mengi unaweza kugeuza katika hatua


tatu. Anza kwa kuendesha upande wa kushoto sana. Kisha nyonga
usukani kulia kabisa na kuvuka barabara. Halafu, nyonga usukani
kushoto na kurudi nyuma upande mwingine wa barabara. Kumbuka
usinyonge usukani wakati gari limesimama. Kisha vuka na endesha
kwenye mwelekeo sahihi.
Ama utageuza kwa U au
kugeuza kwa kurudi nyuma,
kumbuka kuwa hiki ni
kitendo cha ujanja ambacho
kinapaswa kufanywa kwa
uangalifu mkubwa. Chagua
sehemu yako ya kugeuzia
kwa makini, tumia viashiria
vyako, na angalia magari
mengine.

Reli Inayokatisha
Kwenye reli inayokatisha bila vizuizi, ishara au mtu yeyote anayeongoza
magari, punguza mwendo kabla ya kuingia kwenye reli ili kuchunguza
kama magarimoshi yanakuja. Madereva wa mabasi, na magari
yanayobeba vitu vinavyoweza kuwaka moto, LAZIMA wasimame na
kuangalia kabla ya kuendelea. Sikiliza king’ora cha garimoshi. Kamwe
usishindane na magarimoshi – mara zote yana haki ya kupita. Hakikisha
ni salama kabla ya kuvuka, na uwe makini zaidi pale penye njia za reli
zaidi ya moja.

Pale ambapo reli inayokatisha inaongozwa na vizuizi, ishara au mtu


mwenye mamlaka hayo, LAZIMA uvifuate. Kamwe usijaribu kuongeza
mwendo ili upite haraka wakati vizuizi vinashushwa chini. Kamwe
usiondoke hadi alama za taa zinapozima na vizuizi vimefunguliwa kabisa.
Waache watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wapite kwanza.

Kamwe usiendeshe kwenye reli inayokatisha hadi pale barabara


itakapokuwa wazi upande mwingine, na usilikaribie sana gari la mbele
yako. Kamwe usisimame au kuegesha kwenye reli au karibu na reli.
Iwapo gari lako litaharibika kwenye reli, watu watoke ndani ya gari
47
haraka na kukaa mbali na hatari. Mwarifu msimamizi wa reli, kama yupo,
na fuata maelekezo yake. Vinginevyo, piga simu polisi. Iwapo hakuna
garimoshi linalokuja omba msaada wa kulisukuma gari kutoka kwenye
reli. Iwapo utalisikia au kuliona garimoshi likija ondoka kwenye reli
haraka, jaribu kumuonya dereva wa garimoshi bila ya kujiweka hatarini.

Kuegesha

Wakati unataka kusimama au kuegesha, kumbuka vioo-ishara-


kitendo. Toka nje ya barabara ikiwezekana kwenda kwenye eneo
linalofaa kuegesha. Iwapo itakubidi usimame barabarani, simama karibu
kadiri iwezekanavyo na upande wa kushoto. Daima angalia iwapo ni
salama kuegesha gari na iwapo inaruhusiwa kuegesha mahali hapo.
Kabla ya wewe au abiria wako kufungua mlango, hakikisha hautamgonga
mtu yeyote anayepita barabarani au kwenye njia ya waendao kwa miguu
– angalia kwa makini waendesha baiskeli na pikipiki. Kumbuka kuwa ni
salama kushuka kwenye gari upande wa kushoto karibu na ukingo wa
barabara.

USIEGESHE gari:
• bila ya kujali na kuwafikiria wengine
• kwenye alama za pundamilia au mita 5 karibu na alama hizo
• mita 5 ndani ya makutano au mahali reli inapokatisha barabara
• kwenye kituo cha basi au mita 15 toka pande zote za alama ya “kituo
cha basi”
• kwenye njia ya waendao kwa miguu
• mbele ya sehemu ya kuingilia magari
• kwenye barabara yenye mistari myeupe miwili ya katikati, hata kama
moja ya mistari hiyo umekatikakatika
• ambapo haparuhusiwi kuegesha gari kwenye alama ya USIEGESHE
na/au mistari ya njano kwenye ukingo wa barabara.

Usiegeshe mahali popote ambapo itakuwa hatari au kusababisha


matatizo kwa watumiaji wengine wa barabara, kwa mfano:
• Karibu na geti la shule
• Karibu na kilele cha kilima
• Kwenye kona kali
• Upande mwingine wa gari lililoegeshwa (uegeshaji wa magari mawili)
• Mkabala na kizingwa
• Pale ambapo gari lako litakiziba kituo cha teksi

48
• Pale ambapo gari lako litaziba alama au ishara ya barabarani.

Usiegeshe usiku kwenye barabara zenye magari mengi au mahali


ambapo magari yanakwenda kwa kasi. Iwapo huwezi kuepuka kufanya
hivi, washa taa za kuegeshea. Wakati wa usiku egesha upande wa
kushoto wa barabara tu.

Egesha gari lako kwa unadhifu, kwa uzuri na usalama. Unahitaji udhibtii
mzuri wa mwendo wako na usukani na pia uamuzi sahihi wa nafasi.
Chagua sehemu yako ya kuegesha kwa makini –
• kuna sehemu ya kutosha?
• ardhi inafaa – kuna vikwazo vyovyote?
• gari lako litakuwa salama?

Kumbuka daima kuendesha gari polepole wakati unanyoosha usukani –


usinyonge usukani wakati gari limesimama. Kunyonga usukani ili gari
lirudi nyuma huhitaji umakini, lakini usisahau kuangalia magari na
watembea kwa miguu nje. Kumbuka kuwa kadiri upande wa nyuma ya
gari lako unapopinda upande wa mbele utakwenda kwenye mwelekeo
mwingine. Tumia viashiria vyako kuwaeleza madereva wengine
unachokifanya.

Uegeshaji wa 900
Jaribu na egesha pale ambapo
unaweza kuendesha mbele na
kutoka kwenye maegesho.
Hata hivyo, katika maegesho
mengi utatakiwa kurudi nyuma
- ama mahali pa maegesho au
nje ya hapo. Kwa kawaida ni
vizuri kurudi nyuma kwenye
maegesho, kwa sababu hili
litakuwezesha kwenda mbele wakati unatoka – hali itakayokuwezesha
kuona vizuri magari na watembea kwa miguu. Usiliweke gari lako karibu
sana na gari la jirani kwani dereva wake au abiria atapata taabu kuingia
kwenye gari hilo. Usiegeshe kwenye maeneo yaliyoachwa kwa ajili ya
walemavu isipokuwa kama una uhalali wa kuyatumia.

49
Uegeshaji sambamba
Lazima uwe na uwezo wa kuegesha gari lako kwenye mstari wa wengine
sambamba na ukingo wa barabara – huu huitwa uegeshaji sambamba,
na ni wa kawaida mijini. Angalia nafasi ya kiasi cha mara moja na nusu
ya urefu wa gari lako. Ni vizuri kuingia kwa kurudi nyuma, isipokuwa
kama eneo lenyewe ni refu vya kutosha. Endesha ukipita sehemu tupu
na simama upande wa gari la kwanza baada ya eneo hilo – kiasi cha mita
moja (1) kutoka kwenye gari hilo.

Kisha rudi nyuma polepole


hadi sehemu ya nyuma ya
gari lako itakapoipita
sehemu ile ya gari la mbele
yako, kisha pinda kushoto
kabisa na endelea kusogea
nyuma. Pale tairi lako la
upande wa kushoto
litakapokuwa karibu na
ukingo wa barabara na
katika pembe ya 45º kutoka
hapo, nyonga usukani kulia kabisa, na endelea kwenda polepole nyuma
hadi gari lako litakapokuwa sambamba na ukingo kisha unaweza kuhitaji
kwenda mbele kidogo kuliweka gari katikati ya mahali hapo.

Usiyaguse kamwe magari mengine kwa gari lako. Wakati unarudi nyuma
kwenye maegesho upande wa kulia wa barabara fuata taratibu zilezile za
msingi.

Uegeshaji wa mshazari
Ziko sehemu ambazo utatakiwa kuegesha mshazari kwenye kingo za
barabara. Kuendesha kwenda kwenye maegesho hayo ni rahisi: angalia
vioo vyako na maeneo fiche, ashiria kwenda kushoto, punguza mwendo
taratibu, na kisha nyonga kwa nguvu kuingia eneo hilo. Yanyooshe
matairi na simama pamoja na gari la mbele kwenye ukingo wa barabara.
Kuacha sehemu si kitu rahisi, kwa sababu utatakiwa kurudi nyuma, na
magari mengine yaliyoegesha yanaweza kukukinga kuona magari
yanayokuja. Jaribu kumtafuta mtu wa kusimama nyuma ya gari na
kukuongoza utoke. Rudi nyuma taratibu sana na angalia wakati wote
magari – pindi sehemu ya mbele ya gari lako itakapokuwa sawa na
sehemu ya nyuma ya gari lililoegeshwa kando yako, anza kupinda kwa
50
nguvu – angalia kuwa sehemu ya mbele ya gari lako iwe inapita kwenye
sehemu ya nyuma ya gari la jirani upande mwingine – kisha nyoosha na
simama – kisha utakuwa tayari kuondoka.

Kuegesha kilimani
Unapoegesha kilimani liache gari likiwa matairi ya mbele yamegeuzwa
kwenye upande wa barabara. Iwapo breki za mkono zitashindwa kufanya
kazi gari litakwenda nje ya barabara. Iwapo gari lako linatumia giaboksi
ya manyu liache gari kwenye gia ya kwanza au gia ya kurudi nyuma. Hii
itasaidia kulizuia gari lisitembee iwapo breki za mkono zitashindwa
kufanya kazi.

51
Alama za barabarani

Alama za barabarani zinasaidia kutoa tahadhari, kudhibiti, kuongoza na


kuwapa taarifa watumiaji wa barabara. Zinajumuisha ishara za
barabarani za nguzo za wima, taa za barabarani, na michoro ya
barabarani.

Kuna makundi manne ya alama za barabarani:


Alama za udhibiti kuwaambia madereva kipi lazima wafanye na kipi
wasifanye
Alama za tahadhari kuwatahadharisha madereva juu ya hatari au
ugumu wa barabara mbele
Alama za taarifa kuwasaidia madereva kuangalia huduma na
maeneo wanayoyataka
Alama za mwongozo kuwasaidia madereva kuona njia
wanakokwenda.

Alama za makundi mengine


zina umbo maalum na rangi Alama za
kuwasaidia madereva mviringo zinatoa
maelekezo
kuzitambua haraka. Alama
mbili muhimu sana ni alama
za “Simama” na “Ruhusu,” Alama za
zina maumbo yake maalum. pembetatu
zinatoa tahadhari
Ambapo pana haja ya Alama za mraba
kupambanua au kupanua au mstatili -
taarifa ya kwenye alama kuu alama ya kijani
taarifa ya ziada inatoa taarifa;
imejumuishwa kwenye kibao alama ya bluu
inatoa maelekezo
chini ya alama kuu.

Ishara za barabarani zinatumika kudhibiti magari na watembea kwa


miguu kwenye makutano na kwenye alama za pundamilia.

Michoro ya barabarani inagawanywa kwenye michoro ya udhibiti,


tahadhari na mwongozo.

Rejea kwenye Kanuni za Barabarani kwa maelezo ya kina ya alama


zote za barabarani.

52
Jaribio la udereva

Maombi ya kufanya jaribio la udereva


Kama unafikiri kuwa uko tayari kufanya jaribio la udereva lazima:
• Upate cheti kutoka kwenye shule ya udereva yenye leseni kuonyesha
kuwa umemaliza kozi ya maelekezo
• Uwe na leseni halali ya dereva mwanafunzi
• Upate fomu ya maombi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania na
kulipa ada ya jaribio
• Andika barua ya maombi kwa polisi wa usalama barabarani
ukionyesha siku ambayo unataka kujaribiwa; ambatisha nakala za
cheti kutoka kwenye shule yako ya udereva, leseni yako ya dereva
mwanafunzi, na cheti cha kipimo cha macho/kuona kutoka kwenye
kituo cha vipimo vya macho kinachotambulika
• Kuwe na barabara inayofaa, gari lililothibitishwa la aina sahihi la leseni
unayoiomba.

Kujiandaa kwa jaribio

Kama dereva mpya unahitaji maelekezo sahihi kabla ya kwenda kwenye


jaribio. Kama umejiandaa kikamilifu unaweza kufaulu jaribio baada ya
kujaribu kwa mara ya kwanza.

Iwapo unajifunza kuendesha LAZIMA upate mafunzo kutoka kwa


mwalimu wa udereva aliyesajiliwa anayefanya kazi kwenye shule ya
udereva yenye kibali. Wakati unachagua shule ya udereva, jaribu kupata
mapendekezo kutoka kwa wanafunzi waliopita, angalia hali ya gari la
mafunzo, na angalia wanafunzi wangapi wengine watakuwa wanachangia
gari na wewe. Baadhi ya shule zinatoa kozi ambazo zimethibtiishwa na
serikali. Shule lazima ikufundishe nyanja zote za uendeshaji salama, na
si tu jinsi ya kufaulu jaribio la udereva.

Gari ambalo utalitumia kufanyia majaribio lazima liwe safi na linalofaa,


na liwe limesajiliwa vizuri, lenye leseni na kuthibitishwa. Pia lazima liwe
na giaboksi ya manyu - hutaruhusiwa kufanya jaribio kwenye gari lenye
mfumo wa otomatiki. Viti vya mbele lazima viwe na mikanda ambayo
inafanya kazi.

53
Yaliyomo kwenye jaribio

Lengo la jaribio hili ni kuona kama unaweza kuendesha vizuri. Ni lazima


umridhishe mtahini wa udereva kuwa unaweza kulidhibiti gari lako kwa
usalama, onyesha uungwana na kuwajali watumiaji wengine wa
barabara, na fuata Kanuni za Barabarani. Pia lazima uwe na ufahamu wa
Sheria ya Barabarani [Ibara ya 168 R.E ya 2002) na alama zote za
barabarani na michoro iliyoelezwa kwenye Kanuni za Barabarani.

Sheria ya Barabarani inaeleza kuwa jaribio ni kwa ajili ya kuangalia


uwezo wako wa:
• Kulidhibiti gari barabarani
• Kulisimamisha gari kutoka kwenye mwendo wa kawaida
• Kukata kona kwenye barabara kuu, kukatisha barabara, na kupinda
kutoka kwenye barabara ndogo kuingia barabara kuu
• Kuyapita magari mengine barabarani
• Kurudisha gari nyuma kwenye barabara iliyonyooka na yenye kona
• Kupinda barabarani
• Kuelewa na kufuata Sheria na ushauri wa Kanuni za Barabarani.

Jaribio

Jaribio limeandaliwa ili kuona kama una uwezo mkubwa wa kuendesha


na iwapo unajua Sheria za Barabarani na alama za barabarani. Liko
kwenye sehemu mbili: nadharia, na jaribio la vitendo.

Jaribio la nadharia linaweza kuwa la mdomo au kuandika. Maswali


yatachukua nyanja zote za udereva, pamoja na mbinu za msingi za
udereva, alama za barabarani, michoro, Kanuni za Barabarani, na Sheria
za Barabarani. Mtahini atasahihisha majibu yako, na iwapo 70% au zaidi
ni sahihi, utakuwa umefaulu jaribio.

Iwapo utafaulu jaribio utaruhusiwa kufanya jaribio la vitendo. Hili


hufanywa barabarani., huku mtahini akiwa amekaa mbele kwenye kiti
cha abiria. Mtahini atakuwa anaangalia kuona kuwa:
• Unatumia vizuri vioo
• Unaonyesha ishara za lazima kwa usahihi na kwa wakati unaofaa
• Unachukua hatua inayofaa papo hapo kwa alama zote za barabarani,
ishara, na michoro
• Unadhibiti mwendo wako ili daima uwe wa salama na unaofaa katika
mazingira uliyopo na namna unavyoendesha

54
• Unakuwa mwangalifu nakuangalia vizuri kabla ya kuingia, au
kukatisha makutano yoyote
• Unaonyesha ufahamu na matarajio kwa vitendo vya watembea kwa
miguu, waendesha baiskeli, na madereva wengine
• Liweke gari lako kwenye njia sahihi barabarani – wakati unaendesha
moja kwa moja na wakati unapinda kwenye makutano.

Jaribio la vitendo husahihishwa kwa njia ya kupunguza alama. Unaanza


na alama 100 na mtahini atakuwa anapunguza alama kwa kila kosa
unalofanya. Idadi ya alama zinazopunguzwa hutegemea na ukubwa wa
kosa – alama 10 kwa kila kosa kubwa na alama 5 kwa kila kosa dogo.
Kama bado utakuwa na alama 70 au zaidi mwishoni mwa jaribio utakuwa
umefaulu.

Ni kawaida kuwa na wasiwasi wakati wa kufanya jaribio, lakini kadiri


unavyofanya mazoezi zaidi ndivyo utakavyojiamini zaidi. Kwa kawaida
jaribu kuendesha kwa jinsi ulivyofundishwa.

Ukijiona umefanya kosa, usiogope kuhusu kosa hilo. Mtahini hatasema


bila sababu wakati unaendesha kwa sababu hili linaweza
kukuchanganya. Hakikisha kuwa umejifunga vizuri mkanda wako wakati
unaendesha.

Iwapo una ulemavu wa viungo mtahini ataelewa matatizo yako na


kukusaidia kadiri awezavyo. Unaweza kuchagua mtahini wako
azungumze Kiswahili au Kiingereza. Haishauriwi kutumia wakalimani.

Ni muhimu kuonyesha kwa mtahini kuwa unajiamini (lakini si kujiamini


kupita kiasi) katika kuendesha barabarani. Endesha vizuri na si kwa
kusitasita sana, au kutoweza kutumia upenyo salama barabarani wakati
wa kupinda. Usiwe mpole sana kiasi cha kuyaruhusu magari yapite bila
sababu – hili linaweza kusababisha kujichanganya na unaweza kuyazuia
magari ya nyuma yako bila sababu. Kamwe usiwaashirie watembea kwa
miguu kuvuka barabara mbele yako – unaweza kuwasababishia hatari
kutoka kwenye magari mengine.

Mtu yeyote anayetoa zawadi au fedha au kishawishi kingine kwa mtahini


kwa lengo la kuathiri uamuzi wake anaweza kushitakiwa kwa kosa kubwa
la ‘kujaribu kutoa rushwa.'

55
Baada ya jaribio

Iwapo umefaulu. Kwa kufaulu mtihani utakuwa umeonyesha kuwa


wewe kimsingi ni dereva mzuri. Hata hivyo, bado huna uzoefu, na una
mengi ya kujifunza. Jaribu kuendelea kuboresha ujuzi wote wa udereva
kwa uzoefu zaidi na umakini zaidi wa mbinu zako za udereva. Hili
liendelee wakati wote wa maisha yako ya udereva- daima kuna
mawanda kuendelea zaidi.

Iwapo utashindwa. Utashindwa tu iwapo utafanya makosa mengi ya


udereva au kuwa na maarifa madogo ya udereva. Mtahini atakupa taarifa
ya kushindwa ambapo ataonyesha vipengele vya udereva wako
vinavyohitaji umakini zaidi. Makosa yatakayoonyeshwa yatakuwa ni yale
yaliyokusababisha kushindwa jaribio, lakini yanaweza kuwako mengine,
ambayo ni madogo. Hivyo, wakati taarifa ya kushindwa ikusaidie wewe
na mwalimu wako kurekebisha makosa haya makubwa, jaribu kuboresha
nyanja zote za udereva wako.

Iwapo utashindwa lazima usubiri kwa kiasi cha wiki nne kabla ya
kujaribiwa tena. Mtahini anaweza kuongeza kipindi hiki hadi wiki tisa (9)
kama ataona kuwa unahitaji muda zaidi wa kuboresha udereva wako.

56
Kuharibika

Iwapo gari lako litaharibika, au kupata pancha, jaribu kulisogeza gari


lako nje ya barabara. Kama hili haliwezekani liweke gari karibu na ukingo
wa kushoto wa barabara na mbali ya makutano, madaraja, kona na
sehemu nyingine za hatari.

Iwapo huwezi kuepuka


kusimama barabarani
LAZIMA utoe tahadhari kwa
magari mengine kwa
kuweka kiashiria chekundu
cha pembetatu karibu na
ukingo wa barabara si chini
ya mita thelathini (30)
nyuma ya gari-pamoja na
kiashiria kingine cha
pembetatu katika umbali
uleule mbele ya gari. Pia lazima utumie taa zako za tahadhari ya hatari
(indiketa mbili-zote zikiwaka kwa pamoja). Iwapo umesimama kwenye
kona au karibu ya kilele cha kilima tafuta mtu mmoja arudi nyuma
barabarani kuyatahadharisha magari yanayokuja.

LAZIMA ujaribu na kuliondoa gari haraka iwezekanavyo. Ofisa wa polisi


ana mamlaka ya kupanga namna ya kuliondoa gari lolote iwapo ataona
linahatarisha usalama. Utapaswa kulipa gharama za kuliondoa.

Jaribu kutosimama au kutoshughulika na gari mahali ambapo utakuwa


katika hatari ya kugongwa na magari yanayopita. Unapolitengeneza gari
usimwage dizeli au kilainishi kingine barabarani, kwani inaathiri
barabara.

Fanya kila jitihada kulitengeneza gari au kuliondoa barabarani, kabla ya


giza kuingia. Iwapo utalazimika kuliacha gari bovu barabarani usiku,
washa taa za kuegeshea na hakikisha kuwa kuna vibao vya tahadhari
vya pembetatu barabarani mbele na nyuma ya gari kuwatahadharisha
madereva wengine. Waarifu polisi.

Hakikisha kuwa mawe uliyotumia kuzuia matairi ya gari yameondolewa


barabarani wakati unapoondoa gari.

57
Iwapo kuna ajali

Iwapo umehusika kwenye ajali au umesimama kusaidia:


• wape tahadhari madereva wa magari mengine kwa kuwasha taa zako
za tahadhari ya hatari (indiketa mbili) na, ikibidi, waashirie madereva
wengine wapunguze mwendo. Dhibiti magari ili kuepuka ajali nyingine.
Waombe madereva wengine na wanakijiji wakusaidie.
• waombe madereva kuzima injini zao na kutokuwa na sigara zozote
• wasiliana na polisi mara moja – waeleze eneo hasa la ajali na idadi ya
magari na watu waliojeruhiwa – waombe watu wengine kufanya hivi ili
kuhakikisha kuwa ujumbe umefika
• jiandae kutoa huduma ya kwanza
• iwapo majeruhi wameumia sana, na kuna matumaini madogo ya
kupata msaada haraka, fanya utaratibu wa kuwapeleka majeruhi
kwenye hospitali ya karibu
• wahudumie walioathirika na tunza mali zao – na mshawishi kila mmoja
kufanya hivyo.

Ukiyaona magari yamesimama mbele, punguza mwendo na uwe tayari


kusimama. Iwapo ukiona tayari kuna watu wa kutosha wanaotoa msaada
usisimame na kusababisha kizuizi. Wakati unapita mahali penye ajali
usibabaike – kuwa makini na barabara mbele yako. Fuata amri za
maofisa wa polisi walio kwenye tukio, na kuwa mvumilivu iwapo
kutakuwa na kukaa kwa muda mrefu.

Iwapo umehusika kwenye ajali ambapo mtu amejeruhiwa LAZIMA utoe


jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa gari, kama ni
tofauti) kwa mtu yeyote aliyehusika na ajali na LAZIMA utoe taarifa ya
ajali kwenye kituo cha polisi cha karibu au kwa ofisa wa polisi haraka
iwezekanavyo.

LAZIMA usimame na kuwasaidia watu waliojeruhiwa kwenye ajali,


isipokuwa kama unahofia usalama wako. Iwapo umehusika kwenye ajali
ya barabarani ambapo hakuna aliyejeruhiwa huhitaji kutoa taarifa polisi,
lakini LAZIMA utoe jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa
gari, kama ni tofauti) na namba ya usajili ya gari lako kwa mtu mwingine
yeyote aliyehusika.

58
Muhtasari wa mafunzo ya madereva wa magari
madogo (Leseni za Daraja B & D)

1. Gari
Mwanafunzi lazima:
a) Awe na uelewa wa msingi wa jinsi gari inavyofanya kazi
b) Ajue matumizi na kazi za vidhibiti vya gari (mf. Usukani, breki na
gia) injini, mwako na sehemu nyingine za kiufundi
c) Aweze kusoma na kuelewa vifaa vya gari (mf. Spindometa) na
umuhimu wake
d) Kutambua hatari zinazotokana na kushindwa kufanya kazi kwa
sehemu mbalimbali za gari na jinsi ya kugundua hitilafu,
e) Ajue jinsi ya kufanya safari za awali, ukaguzi wa kila wiki na kila
mwezi,
f) Awe na uelewa wa jinsi aina mbalimbali za magari madogo (mf.
Magari madogo ya kawaida, pikapu, magari yenye kutumia
magurudumu yote manne) yanavyokuwa yakiendeshwa na jinsi ya
kuyaendesha kwa usalama.

2. Kufaa kuendesha
Mwanafunzi lazima:
a) Awe na mtazamo sahihi wa uendeshaji:- kuwajibika, kuwa makini,
matarajio, uvumilivu na kujiamini
b) Aelewe jinsi pombe inavyoathiri uwezo wa kuendesha gari, ajue
sheria inasemaje kuhusu kunywa pombe na kuendesha gari na jinsi
sheria inavyotekelezwa
c) Aelewe umuhimu wa kutoendesha gari wakati amechoka na ajue
miongozo kuhusu ni mara ngapi anatakiwa kupumzika
anapoendesha gari
d) Aelewe kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuathiri uwezo wa
kuendesha gari na ajue jinsi ya kuzitambua
e) Aelewe jinsi ya kubadilikabadilika na ugonjwa kunavyoathiri uwezo
wa kuendesha gari
f) Aelewe umuhimu wa kuona vizuri na jinsi ya kutambua hali ya
macho.

3. Dereva na Gari
Mwanafunzi lazima:
a) Ajue nafasi inayotaiwa kuendeshea na jinsi ya kuingia sehemu hiyo

59
b) Ajue jinsi ya kurekebisha vioo, kujua ukomo wake na kujua kuhusu
maeneo yasiyo mazuri (“blind zone”)
c) Ajue jinsi ya kurekebisha udhibiti wa kichwa vizuri
d) Aelewe umuhimu wa kufunga mikanda, jinsi ya kuifunga vizuri na
sheria inayohusika
e) Ajue namna nzuri ya kubeba watoto kwa usalama
f) Ajue jinsi ya kubeba mizigo na wanyama kwa usalama.

4. Dereva na Sheria
Mwanafunzi lazima:
a) Ajue sheria muhimu, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu kusababisha
ajali kutokana na kuendesha gari vibaya na kwa uzembe, kuendesha
wakati mtu amekunywa pombe na dawa za kulevya, kuendesha kwa
kasi n.ik..
b) Awe na uelewa wa msingi wa masharti ya gari kuwa zima
c) Ajue masharti ya leseni ya udereva, ikiwa ni pamoja na yale
yanayowahusu madereva wanafunzi
d) Ajue majukumu ya kisheria ya kuhusu kugongana
e) Ajue masharti ya bima ya gari na umuhimu wa kukata bima inayofaa
f) Awe na uelewa wa msingi wa jinsi sheria za usalama barabarani
zinavyotekelezwa (ikiwa ni pamoja na faini za papo hapo) na adhabu
za makosa ya uendeshaji gari.

5. Udhibiti na uratibu
Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kuwasha injini, kuondoka na gari, kuongeza mwendo,
kubadilisha gia, kurudi nyuma, kuendesha kwenye kupanda mlima
na kushuka na kukata kona, na kufunga breki kusimama kwa
usalama bila taratibu na kiumahiri
b) Aweze kusimama na kuondoka kwenye mlima bila tatizo na bila ya
kurudi nyuma
c) Ajue jinsi mtindo wa uendeshaji unavyoathiri matumizi ya mafuta,
starehe na usalama wa abiria.

6. Uendeshaji salama katika foleni


Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kuednesha katika hali inayoonyesha kujali kuzingatia na
uvumulivu
b) Ajue umuhimu wa kuwa makini katika kazi ya kuendesha na
kuepuka kuwa sehemu nyingine kimawazo na kujua ni vitu gain
vinaweza kumchanganya dereva
60
c) Aweze kuendelea kuchunguza barabara kwa mbele na pembeni (kwa
kutumia vizuri vioo) na kutazamia hali fulani itakavyojitokeza na
kuchukua hatua sahihi waendeshaji magari wengine na mazingira ya
hatari
d) Atumie mchakato wa hatua katika ishara ya kioo
e) Aweze kupita magari yaliyosimama na vizuizi kwa usalama
f) Ajue ni jinsi gain na wakati gain wa kutoa ishara kwa kutumia
indiketa na ishara za mkono
g) Ajue nani mwenye kipaumbele wakati magari yanapokutana kwenye
mzunguko au hali ya kupitana
h) Aliweke gari vizuri barabarani na akae kwenye mkondo wake
i) Ajue jinsi ya kuamua umbali gain ni salama kutoka kwenye gari iliyo
mbele na aweze kukaa katika umbali huo kwenye foleni
j) Ajue jinsi ya kutumia njia mbili kwenye barabara yenye njia nyingine
k) Aelewe kwa nini tabia zinazoonekana kuwa ni mbaya, kama vile
kuondoka kwenye foleni, na kuendesha pembeni mwa barabara
kwenye eneo la watembea kwa miguu, ni hatari na haifai.

7. Mwendo kasi
Mwanafunzi lazima:
a) Ajue kuwa hatari ya kugongana inaongezeka kadri mwendo
unavyoongezeka
b) Aweze kuendesha kwa mwendo salama katika mazingira
c) Ajue vizuri jinsi ya kuepuka kuteleza na afanye nini utelezi
unapotokea
d) Awe na uelewa wa jumla wa umbali wa kusimama na jinsi
unavyotofautiana kulingana na mazingira ya barabara na mambo
mengine
e) Ajue mipaka ya mwendo kasi wan chi wa eneo, umuhimu wake na
jinsi inavyotekelezwa
f) Ajue kwamba kikomo cha mwendo kasi hakina maana na kwamba
wakati wote itakuwa ni salama kuendesha katika mwendo huo.

8. Kupita gari
Mwanafunzi lazima:
a) Ajue wakati gain ni salama kulipita gari
b) Ajue maeneo ambayo si salama kulipita gari – na wapi alama za
barabara zinaonyesha ni kosa kulipita gari
c) Aweze kulipita gari jingine katika hali ya usalama na umahiri, bila
kusababisha gari linalotoka katika mwelekeo tofauti kupunguza
mwendo au kubadili uelekeo ili kuepuka kugongana.
61
9. Makutano (tofauti na mzunguko)
Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kuendesha gari kwa kupita katika aina zote za makutano
katika hali ya usalama na umakini, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo
katika barabara iliyogawanywa sehemu mbili, mitaa ya njia moja na
zile zinazoongozwa na alama za barabarani
b) Ajue umuhimu wa kukaribia makutano kwa mwendo unaofaa,
kuingia katika njia na nafasi sahihi, kutii sheria muhimu kuangalia
vizuri na kutozuia misururu mingine ya magari kutembea
c) Atumie vizuri ishara.

10. Mizunguko
Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kupita kwenye mizunguko katika hali ya usalama na umahiri
b) Ajue ni njia gani ya kutumia anapoingia na kukata kona na
kuondoka kwenye mzunguko
c) Atumie vizuri ishara
d) Ajue nani mwenye kipaumbele.

11. Vivuko vya watembea kwa miguu


Mwanafunzi lazima:
a) Ajue aina mbalimbali za vivuko vya watembea kwa miguu – sehemu
ya katikati ya kuvukia kwa waendao kwa miguu, vivuko vya
pundamilia, taa za barabarani na jinsi alama zinavyofanya kazi
b) Ajue sheria kwa matumizi ya kila aina ya kivuko cha watembea kwa
miguu
c) Aelewe umuhimu wa kutolipita gari au kuegesha karibu na alama za
pundamilia za kuvuka barabara
d) Ajue muda wenye hatari zaidi na sehemu zenye hatari kubwa.

12. Kuendesha gari usiku na katika hali mbaya ya hewa


Mwanafunzi lazima:
a) Aelewe umuhimu wa kuendesha katika mwendo ambao utamruhusu
kusimama katika umbali ambao anaweza kuona vizuri
b) Ajue ni wakati gani wa kuwasha taa za mbele zenye mwanga mkali
c) Ajue ni wakati gani wa kutumia taa za mbele zenye mwanga hafifu
d) Aelewe jinsi hali ya unyevunyevu itakavyoathiri umbali wa kusimama
e) Ajue jinsi ya kukabiliana na mvua kubwa, mafuriko, ukungu, barafu
na upepo mkali.

62
13. Kuharibika na dharura
Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kutumia breki na gia ili kuweza kusimamisha gari haraka bila
ya kuteleza na bila ya kuzima injini
b) Ajue atafanya nini kama atahusika katika kugongana au kusimama
kutoa msaada
c) Ajue atafanya nini kama ataharibikiwa gari barabarani na hususan
jinsi ya kuepuka kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa
barabara.

14. Kutambua hatari


Mwanafunzi lazima:
a) Ajue muda, mahali na hali ya hewa ambapo hatari ya kugongana ni
kubwa kuliko kawaida
b) Ajue aina za kugongana zinazotokea sana na kwa nini zinatokea
c) Ajue hatari mahsusi zinazomkabili dereva wakati analipita basi
lililosimama; anapoingia kwenye mzunguko ambapo kuna magari
mawili, anakata kushoto ambako kuna magari mawili; anaingia
barabara kuu wakati upeo wa kuona pembeni ni mdogo anakata
kulia kwenye barabara yenye njia mbili zinazotumiwa na watu;
analipita gari kubwa/refu kwenye mzunguko; anageuza gari kutoka
kwenye jengo au kwenye geti katika ukuta anakaribia njia ya reli
inayokatisha; kuna watoto wadodo pembeni mwa barabara.

15. Kugeuza gari kwa kuzunguka barabarani


Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kujua kama ni salama ni sheria na ni busara kugeuza gari
kwa kuzunguka barabarani
b) Ajue wakati gani wa kugeuka kwa mzunguko wa U, kugeuzia kwenye
njia ya pembeni na kutumia ugeukaji wa point i– 3
c) Aweze kugeuka alikotoka kwa hali ya usalama na umakini, kwa
usimamizi mzuri, kutumia usukani kwa usahihi na kuwaangalia vizuri
watumiaji wengine wa barabara.

16. Maegesho
Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kuamua kama ni salama ni sheria na ni busara kuegesha
sehemu yoyote
b) Aweze kuegesha sambamba, maegesho ya 90º, na maegesho
mshazari katika hali ya usalama na umahili kwa usimamizi mzuri,
uelekeo sahihi na uzuiaji mdogo wa magari mengine
63
c) Kuweza kuegesha kwa usalama kwenye mteremko (mwinuko na
mteremko).

17. Kurudi nyuma


Mwanafunzi lazima:
a) Aweze kujua kama ni salama ni sheria na busara kurudi nyuma
b) Aweze kurudi nyuma katika hali ya usalama na umakini katika
mstari ulionyooka, katika kona ya kushoro na kulia na katika
barabara zilizo tambarare na katika miteremko.

18. Alama ishara na michoro ya barabara


Mwanafunzi lazima:
a) Ajue makundi makuu manne ya alama za barabarani na sifa za
maumbo yake na rangi
b) Ajue alama zote za udhibiti, ishara na alama za usalama barabarani
na jinsi ya kuzifuata
c) Aweze kutambua vizuri 80% ya alama na ishara nyingine
d) Ajue ishara zinazotolewa na maofisa wa polisi na watu wengine
walioidhinishwa na jinsi ya kuzifuata.
19. Mfumo wa barabara
Mwanafunzi lazima:
a) Awe na uelewa wa jumla wa barabara zipi ziko chini ya Mamlaka ya
Taifa ya Barabara Tanzania (TANROADS), ambazo ni mali ya
Halmashauri za wilaya na ambazo ni binafsi
b) Ajue umuhimu wa kutozuia trafiki kwenye barabara au kuharibu
barabara zetu au kuiba au kuuza au kuharibu alama au vifaa vingine
vya barabarani.

20. Huduma ya Kwanza


Mwanafunzi lazima:
a) Ajue utaratibu hatari–mwitikio–njia ya hewa–kupumua-mzunguko
b) Ajue jinsi ya kuzuia upotevu mkubwa wa damu (bila kujiweka
mwenyewe hatarini)
c) Ajue jinsi ya kuwashughulikia waathirika wa mshtuko
d) Ajue jinsi ya kupata msaada
e) Ajue jinsi ya kumweka majeruhi katika sehemu atakapopata nafuu.

21. Kujitayarisha kwa jaribio la udereva


Mwanafunzi lazima:
a) Ajue jinsi ya kuomba kufanyiwa jaribio la udereva na mahitaji yake
b) Ajue muundo wa upimaji wa udereva na jinsi atakavyopewa alama.

64

You might also like