You are on page 1of 1

TANGAZO LA UCHAGUZI

1. NAFASI ZA UONGOZI ZILIZOPO:


1. WAJUMBE WA BODI (Nafasi 9)
2. KAMATI YA USIMAMIZI (Nafasi 3)

2. HAJA YA UCHAGUZI:
Kufuatia Sheria ya Vyama Vya Ushirika; Sheria Namba 6 ya mwaka 2013, Vyama
Vyote vya Ushirika ikiwa ni pamoja na Chama chetu vinatakiwa kufanya Uchaguzi wa
Viongozi wake,Hivyo Bodi ya chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tanesco
Mbeya ;kinawatangazia wanachama wake kuwepo kwa nafasi za uongozi .

3. SIFA ZA WAGOMBEA
 Awe mwanachama hai(amelipia ADA, anachangia Hisa na AKIBA zake kila
mwezi) na awe mwadilifu na mwaminifu.
 Mwenye uwezo kushirikiana na kujitolea kufanya kazi za chama.
 Awe ana sifa zilizoainishwa katika kifungu namba 49 cha masharti ya chama.

4. Wanachama wenye SIFA na NIA ya kugombea nafasi hizo, mnashuriwa


kuchukuafomu za kuomba nafasi hizo zinazopatikana Ofisi ya chama iliy oko Mtaa
wa Sokomatola ,Jengo la Umati , ghorofa ya kwanza.

Fomu zitapatikana kuanzia tarehe 17 Februari 2020 na mwisho wa kurudisha fomu ni


tarehe 17 Machi 2020 saa 10:00 jioni katika ofisi za chama.

“TANESCO MBEYA SACCOS ITAJENGWA NA SISI WENYEWE”

KNY: TANESCO MBEYA SACCOS LTD

VENERANDA NOVATUS
MENEJA
Nakala: Afisa Ushirika Jiji– Mkoa wa Mbeya

TANGAZO HILI LIMETOLEWA LEO TAREHE 17/02/2020

You might also like