You are on page 1of 2

RIPAMO & CO. ADVOCATES, P.O.

BOX 1081,
K.K.K.T BUILDING, GROUND FLOOR, ROOM NO. 06
INDIA STREET
+255717192671/+255742949604
mosharp8@gmail.com

13th January, 2021


RPM/ADV/L. 10/2021

KATIBU MKUU
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA,
DAYOSISI YA KASKAZINI KATI,
S.L.P 519, ARUSHA.
FAX: 2508039
Bwana Yesu Asifiwe,

YAH: OMBI LA KUPANGISHIWA CHUMBA NAMBA 07 NA KUFANYA UBORESHAJI


WA CHUMBA HICHO KWA KUWEKA MLANGO.

Husika na mada tajwa hapo juu

Sisi RIPAMO & CO. ADVOCATES ofisi ya sheria hapa Arusha, chumba namba 06
kwenye jengo la Kanisa (K.K.K.T) Dayosisi ya Kaskazini Kati sakafu ya kwanza;
tunaleta ombi kwako na kamati yako teule kuhusu kupangishiwa chumba namba 07
iliyopo karibu kabisa na chumba chetu (chumba namba 06) kwa kuwa ofisi yetu
imepanuka kwa uhitaji (chumba cha wakili mwandamizi, wakili msaidizi, katibu wa
ofisi, sehemu ya kabati la vitabu, sehemu ya shelves ya nyaraka mbalimbali na
majalada), chumba namba 06 imekuwa ndogo. Nasi tunapenda kuendelea kuwa
wapangaji katika jengo hili zuri.

Kutokana na uhitaji huo wa kuwa na sehemu kubwa zaidi tunaomba kupewa


chumba hicho. Maombi yetu ya kupewa chumba namba 07 yanaambatana na ombi
la kuweka mlango kati ya vyumba hivi viwili (06 na 07) ili kuunganisha ofisi yetu.
Ikiwa ombi letu litakubaliwa tutafanya hivyo kwa garama zetu wenyewe pasipo
kuhitaji kurudushiwa. Pia marekebisho hayo yatafanyika chini ya ushauri wa
wataalamu wa ujenzi.

Ni matumaini yetu kuwa ombi letu litapata kibali kwako; aidha tunatanguliza
shukrani zetu

Kwa niaba ya RIPAMO & CO. ADVOCATES

Wako mwaminifu

…………………………
RICHARD PATRICE MOSHA
(WAKILI)
RIPAMO & CO. ADVOCATES, P.O.BOX 1081,
K.K.K.T BUILDING, GROUND FLOOR, ROOM NO. 06
INDIA STREET
+255717192671/+255742949604
mosharp8@gmail.com

You might also like