You are on page 1of 36

Mjadala wa pamoja

Maadili ni nini? nini?

Hii ni TANZANIA
Kwanini hali hii? Hali hii mpaka lini?

Tanzania kuna mambo


6

Barazani

Darasani
9

11

inaendelea
Ukaguzi wa kina ufanywe na Mkaguzi wa Halmashauri ya Manispaa. Viongozi wa Kijiji, Kata na Shule wasihusike kununua vifaa vya ujenzi badala yake watake taarifa na kutoa ushauri. Kamati ya Shule ndiyo ihusike na ununuzi wa vifaa vya ujenzi na kuhakiki ubora wa kazi ya ujenzi.

12

. Inaendelea ..
Kamati ya Shule ya Msingi Mkonoo A ivunjwe na Kamati nyingine iundwe. Uongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata uwe karibu sana na Kamati ya Shule kwa kutoa ushauri kuepusha ubadhilifu. Kuwekwe utaratibu wa kutunza vifaa vya ujenzi na taarifa ya matumizi itolewe kila siku.

13

. Inaendelea ..
Ulinzi wa Shule uimarishwe saa zote kuepuka upotevu wa vifaa vya shule. Elimu ya Kujitegemea ifufuliwe shuleni na iwe na usimamizi pia itoe taarifa kwenye mkutano wa wazazi.

14

Taarifa hii ilitolewa kwa Mkutano Mkuu wa Kijiji na kusambazwa kwa:Ofisi ya Serikali ya Kijiji Mkonoo Ofisi ya Kata Terrat Mratibu Elimu Kata Terrat Mh. Mbunge Jimbo la Arusha Mkurugenzi H/Manispaa Arusha Afisa Elimu H/Manispaa Arusha Ofisi ya MKUKUTA Kijiji cha Mkonoo
15

Katiba ya JMT na Maadili ya viongozi wa Umma


Ndilo chimbuko la la viongozi wa umma kutakiwa kuwa na maadili mema Katiba inaelekeza;
qkuundwa kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma qKutungwa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Na.13/1995 ilivyorekebishwa na Sheria Na. 5/2001)

Inaweka misingi ya Maadili ya Viongozi wa umma ikiwa ni pamoja na Kutoa mara kwa mara tamko la mapato, raslimali na madeni ya viongozi wa umma

Katiba ya JMT
Inawataka viongozi wasiwe na tabia ya udanganyifu, upendeleo, ukosefu wa uadilifu au tabia inayochochea rushwa wakati wanapotekeleza shughuli za umma Inawataka viongozi wa umma wawe waaminifu, wawazi, wenye kuutoa haki bila upendeleo, walinde fedha na mali ya umma Inaelekeza viongozi wa umma iwapo hawatekelezi majukumu yao wafukuzwe au kuondolewa madarakani.

Sheria za serikali za mitaa Na 7&8 za 1982


Zinampa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa uwezo wa kutunga Kanuni za Maadili ya Madiwani kwa lengo la kutekeleza maagizo ya Katiba ya JMT. Waziri alitunga Kanuni za Maadili ya Madiwani za Mwaka 2000

MAADILI MEMA YA MADIWANI


Ni sharti muhimu katika kujenga mahusiano mema kati ya Halmashauri, Wananchi na watendaji ili kujenga imani ya wananchi kwa viongozi wao wa umma na halamashauri zao Diwani ni kiongozi wa ngazi ya juu katika ngazi ya wilaya, kama kiongozi, wananchi wana haki ya kutegemea kuwa atatoa mfano wa kuigwa katika maisha yake ya kila siku na katika utekelezaji wa majukumu aliyokabidhiwa kwa mujibu wa sheria Wananchi huheshimu zaidi uongozi unaothibitishwa na matendo mema pamoja na mwenendo mzuri wa viongozi na watumishi wao badala ya ufasaha wa kauli au ahadi zitolewazo

Misingi ya Kanuni za maadili ya madiwani

Kujenga na kudumisha imani ya wananchi kwa viongozi wao Kuweka utaratibu mzuri wa uwazi na uwajibikaji Kujenga mazingira bora ya kuwavutia wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo Kupunguza migongano kati ya madiwani, watendaji na wananchi Kuweka bayana maadili yanayotegemewa kwa viongozi katika jamii ya watu Kuibua, kukuza na kudumisha demokrasia

Misingi, Misingi, taswira na malengo ya kanuni za maadili ya madiwani


Msingi mkuu ulio katika kanuni za maadili ni ule unaosisitiza
qUtumishi, qUwakilishi qKuweka mbele maslahi ya wananchi/umma badala ya maslahi binafsi

Kwa hiyo diwani anawajibika kuzingatia kiwango cha juu kabisa cha maadili yanayojumuisha tabia yake binafsi na mwenendo wa utendaji wa majukumu yake

Diwani anapaswa
Kuendesha shughuli zake kwa namna itakayojenga imani ya wananchi kwa halmashauri yao Kuheshimu na kuzingatia sheria na kuendesha shughuli zake kufuatana na dhamana aliyopewa na wananchi Kuisaidia Halamashauri yake kwa kadri iwezekanavyo kuhakikisha kuwa inatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia maslahi ya jamii nzima Kutotumia nafasi yake kama diwani kwa faida yake mwenyewe, familia yake, maslahi ya kifedha ya marafiki zake Kutotoa upendeleo wa aina yoyote wakati wa kutekeleza majukumu yake

Diwani anapaswa..
Kutojiweka katika hali inayowafanya wananchi kutilia shaka uadilifu wake Kuwajibika ipasavyo kwa wananchi walio kwenyewe eneo la halmashauri yake kutokana na maamuzi na matendo yake Kuwa muwazi katika matendo yake na katika kuchangia maoni yake ili kufikia uamuzi wa pamoja na kwamba ataunga mkono maamuzi hayo na kuyatolea maelezo kwa wadau wengine Kufanya maamuzi bila upendeleo na kulingana na stahili ya jambo bila kushawishiwa. Mfano katika masuala ya ajira Kutoshiriki katika majadiliano ama kupigia kura ktk jambo lolote ambalo ana maslahi nalo

Diwani anapaswa
Kuhakikisha kuwa habari/taarifa zote za siri zinazohusu watu zinahifadhiwa kwa mujibu wa sheria na kwa maslahi ya umma na kutozitumia habari hizp kwa maslahi yake binafsi Kutoa taarifa kwenye halmashauri au kamati ya halmashauri kuhusu maslahi yake binafsi katika jambo lolote linalohusu utekelezaji wa majukumu yake Kuheshimu nafasi na hadhi ya madiwani/watumishi wenzake kwa namna inatakayojenga hali ya kuheshimiana kati ya madiwani na watumishi wa halmashauri

Sifa za tabia binafsi


Kanuni Na. 8 hadi 11 zinaeleza sifa za binafsi ambazo kila diwani anapaswa kuwa nazo:
qKuwa mwadilifu na muwazi wakati wote (8) qKuzingatia kiwango cha juu cha uadilifu (9) qKutokuwa na uhusiano wa kimapenzi usiokubalika kati yake na madiwani wenzake na au watumishi wa halmashauri (10) qKutotumia vibaya dhamana na imani aliyonayo kwa umma (11)

Tabia ya Hadharani na Utekelezaji wa Majukumu ya Umma


Kama Mwakilishi na Mtumishi wa Umma, Diwani anatakiwa kuzingatia maadili yafuatayo (kanuni Na.12 18);
qKuzingatia sheria, kanuni na taratibu (12) qKuendeleza mashauriano na kuchochea maendeleo katika ngazi za chini za serikali za mitaa (13) qKuepuka migongano ya kimaslahi (14 16) qKutotumia nafasi yake ya udiwani kujinufaisha kifedha, kibiashara au kwa namna yoyote nyingine, au kutetea maslahi yake ama kikundi chochote na hivyo kuathiri jukumu lake la kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma kwa ujumla (17) qKutoomba na au kupokea hongo au zawadi kutoka kwa mtu anayemhudumia (18)

Mali, mapato na madeni


Kanuni ya 19 inasisitiza kila Diwani lazima awe na shughuli inayomwezesha kuendesha maisha yake inayompatia kipato cha kutosha. Kanuni ya 20 inamtaka kila Diwani atangaze mali aliyonayo yeyem m/wenzi wake wa ndoa na watoto wao walio chini ya umri wa utu uzima, na kuhakikisha kwamba matangazo hayo yanahifadhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri yake kwenye rejesta maalum itakayofunguliwa kwa minajili hiyo na ambayo itakuwa wazi kukaguliwa na wananchi bila malipo. Iwapo pana ma badiliko ktk hali ya mali, mapato na madeni yake, diwani atapaswa kufanya marekebishjo kwenye matamko ya awali kwa kutoa matamko ya nyongeza

Madaraka ya kisiasa, uwajibikaji , maslahi na kinga

Kanuni ya 21 inamtaka diwani


qAsitumie nafasi na uwezo wake kisiasa kujipatia fedha au huduma ambazo hazikuidhinishwa na kuwekwa katika bajeti ya halmashauri qAsishawishi madiwani wengine kufikia maamuzi kuhusu masuala yanayohusu watumishi qAsiwabague watu kwa sababu za kisiasa, dini, jinsia, rangi au kabila qAsifanye shughuli yoyote ya kisiasa itakayozorotesha ufanisi au kusababisha usimamizi na utendaji mbovu qKuzingatia haki na malengo yaliyowekwa na ataongozwa na ukweli wa mambo na ushauri wa kitaaluma utakaotolewa na menejimenti ya Halmashauri na ataepuka kusukumwa na itikadi pamoja na hisia zake binafsi wakati wa kujadili na kuamua masuala yanayohusu ustawi na maendeleo ya wananchi

Madaraka ya kisiasa
Mali ya halmashauri zilizo chini ya dhamana ya diwani zitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa (23) Uhuru wa kujieleza katika mikutano ya halmashauri na kamati zakke usivunje taratibu za mijadala zilivyofafanuliwa katika Kanuni za Kudumu (24)

Uhusiano baina ya madiwani na watumishi wa halmashauri (Na. 25 28) Maamuzi, maelekezo, amri na miongozo itatolewa katika vikao vya halmashauri na kuelekezwa kwa Mkurugenzi kwa utekelezaji Diwani akiwa peke yake hatatumia nafasi yake kama mjumbe kumzuia mtumishi au wakala wa halmashauri kutekeleza maamuzi ya halmashauri au maamuzi ya kamati ya halmahsuari (25) Madiwani na watumishi wa halmashauri watatakiwa kujenga uhusiano mzuri utakaohakikisha ufanisi na utendaji bora katika halmashauri, na kuepuka uhusiano wa karibu sana na watumishi wa halmashauri unaoweza kuathiri au kudhalilishanupande wa madiwani au upande wa watumishi wa halmashauri (26)

Uhusiano
Madiwani wasijihusisha na majukumu ya kitaaluma na kitaalam yanayohusu uendeshaji wa shughuli za halmashauri (27) Madiwani wasitoe taarifa za uongo au ushauri mbaya kwa halmashauri hasara (kanuni 28) na hatimaye kumfanya diwani awajibishwe kwa kulipa gharama ya hasara iliyopatikana

Utoaji wa taarifa
Diwani haruhusiwi kutoa taarifa za siri anazozipata kutokana na wadhifa wake ambazo hazitakiwi kutolewa kwa muhjibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 na kwa mujibu wa kanuni zilizotungwa chini ya sheria hiyo (29)

You might also like