You are on page 1of 165

YALIYOMO

YALIYOMO ................................................................................................................................................ 1

VIFUPISHO VYA MANENO ................................................................................................................... 6

SHUKRANI ................................................................................................................................................ 9

ANGALIZO............................................................................................................................................... 12

UTANGULIZI .......................................................................................................................................... 13

MFUMUKO WA BEI NA MAISHA YAKO (INFLATION) ............................................................................................ 14

SEHEMU YA KWANZA ......................................................................................................................... 16

MFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA NI NINI? ..................................................................................................... 16

AINA ZA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA .................................................................................................... 16

KIPANDE NI NINI? ................................................................................................................................................ 17

UTT AMIS NI NINI................................................................................................................................................. 18

JINSI UTT AMIS INAVYOFANYA KAZI .................................................................................................................... 18

FAIDA ZA KUWEKEZA UTT AMIS........................................................................................................................... 19

MREJESHO WA UWEKEZAJI (RETURN ON INVESTMENT) (ROI) ............................................................................. 25

UNAPATAJE FAIDA KUWEKEZA UTT AMIS ............................................................................................................ 27

SEHEMU YA PILI ................................................................................................................................... 29

MIFUKO YA UTT AMIS .......................................................................................................................................... 29

HATARI ZA UWEKEZAJI KATIKA MIFUKO YA UTT AMIS ........................................................................................ 29

MAANA YA MANENO MUHIMU ........................................................................................................................... 33

MFUKO WA UMOJA ............................................................................................................................................. 35


UTANGULIZI .............................................................................................................................................................35
MFUMO WA UWEKEZAJI .........................................................................................................................................35
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................35
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................36
KIASI CHA CHINI CHA UWEKEZAJI...........................................................................................................................36
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................36
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................37
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................37
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................37
KUUZA VIPANDE ......................................................................................................................................................37
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................38
HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI YA MFUKO WA UMOJA .........................................................................38
KUHAMISHA VIPANDE AU KUVITUMIA KAMA DHAMANA......................................................................................38

WEKEZA MAISHA ................................................................................................................................................. 39


UTANGULIZI .............................................................................................................................................................39
MPANGO WA UCHANGIAJI .....................................................................................................................................40
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................41
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................41
JINSI YA KUWEKEZA KATIKA MFUKO HUU ..............................................................................................................41
KIASI CHA FEDHA YA KUWEKEZA ............................................................................................................................45
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................45
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................46
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................46
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................46
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................47
FAIDA YA BIMA YA MFUKO WA WEKEZA MAISHA ..................................................................................................47
KUHAMISHA VIPANDE AU KUTUMIA KAMA DHAMANA .........................................................................................51
KUSITISHWA UANACHAMA KATIKA MPANGO WA UWEKEZAJI ..............................................................................51
KUSITISHWA UANACHAMA KWA SABABU YA KUTOCHANGIA................................................................................52
KUFUFUA UANACHAMA ..........................................................................................................................................52

MFUKO WA WATOTO .......................................................................................................................................... 53


UTANGULIZI .............................................................................................................................................................53
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................53
NAMNA FAIDA INAVYOWEZA KUMFIKIA MTOTO ...................................................................................................53
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................55
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................56
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................57
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................57
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................58
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................58
VIPANDE VINAWEZA KUTUMIKA KAMA DHAMANA ...............................................................................................59
KUHAMA MFUKO ....................................................................................................................................................59

MFUKO WA JIKIMU.............................................................................................................................................. 60
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................60
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................60
KIASI CHA CHINI CHA KUWEKEZA ............................................................................................................................61
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................61
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................62
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................62
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................62
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................62
MPANGO WA GAWIO KATIKA MFUKO WA JIKIMU .................................................................................................63

MFUKO WA UKWASI............................................................................................................................................ 66
UTANGULIZI .............................................................................................................................................................66
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................67
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................67
KIASI CHA CHINI CHA KUANZA KUWEKEZA .............................................................................................................67
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................67
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................68
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................68
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................68
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................68
HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA UKWASI .......................................................................69

MFUKO WA HATI FUNGANI (BOND FUND) ........................................................................................................... 70


UTANGULIZI .............................................................................................................................................................70
SERA YA UWEKEZAJI KATIKA MFUKO ......................................................................................................................70
MPANGO WA KUPATA FAIDA ..................................................................................................................................70
MPANGO WA UWEKEZAJI .......................................................................................................................................71
MPANGO WA GAWIO..............................................................................................................................................71
GAWIO .....................................................................................................................................................................71
ANAYESTAHILI KUWEKEZA ......................................................................................................................................72
KIASI CHA CHINI CHA KUANZA KUWEKEZA .............................................................................................................72
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO ..........................................................................................................................73
GHARAMA YA UNUNUZI..........................................................................................................................................73
GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD) ..........................................................................................................73
MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD) .........................................................................................................................73
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI ........................................................................................74
HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA HATI FUNGANI ............................................................74
UNAFUU WA KODI ..................................................................................................................................................74

SEHEMU YA TATU ................................................................................................................................ 76

JINSI YA KUTENGENEZA GAWIO LAKO ................................................................................................................. 76


SABABU ZA KUTAKA GAWIO KUTOKA MIFUKO YA UTT ..........................................................................................77
JINSI YA KUTENGENEZA GAWIO LAKO KWENYE MFUKO WAKO .............................................................................78
GAWIO KWA MWAKA KULINGANA NA UTENDAJI WA KAMPUNI ...........................................................................82

JINSI YA KUTUMIA KIKOKOTOZI (CALCULATOR) ILIYO KATIKA TOVUTI YA UTT AMIS ........................................... 83
KIKOKOTOZI CHA UWEKEZAJI WA MWEZI (MONTHLY INVESTMENT CALCULATOR) ..............................................85
MPANGO WA KUWEKEZA KILA MWEZI (MONTHLY INVESTMENT PLAN) ...............................................................90
UTT AMIS NA HATI FUNGANI KIPI KINA MREJESHO MKUBWA ........................................................................... 106

SEHEMU YA NNE................................................................................................................................ 109

MAMBO UNAYOHITAJI KUJUA KABLA NA BAADA YA KUWEKEZA UTT AMIS ..................................................... 109
MIPANGO NA MIKAKATI YA UWEKEZAJI ...............................................................................................................109
MUDA WA UWEKEZAJI ..........................................................................................................................................110
MATARAJIO YA MAPATO YAUWEKEZAJI ...............................................................................................................110
NIDHAMU YAKO YA UWEKEZAJI ............................................................................................................................111
HALI YA UCHUMI YA MUWEKEZAJI .......................................................................................................................111

KUMBUKUMBU ZA MANUNUZI YA VIPANDE ..................................................................................................... 112

MPANGO WA KUWEKEZA MARA MOJA NA MPANGO WA KUWEKEZA MARA KWA MARA ............................... 112

MAAJABU YA RIBA YA KAMPAUNDI .................................................................................................................. 121

MREJESHO WA MIFUKO YENYE HISA NA MIFUKO ISIYO NA HISA ...................................................................... 123


MFUKO WA UKWASI VS MFUKO WA UMOJA .......................................................................................................127

RIBA YA KAMPAUNDI KATIKA MFUKO UNAOTOA GAWIO NA AMBAO HAUTOI ................................................ 128

JINSI YA KUTENGENEZA PENSHENI YAKO NA UTT AMIS ..................................................................................... 132


KUSTAAFU NI NINI .................................................................................................................................................133
AINA ZA WATUA AMBAO WANASTAAFU ..............................................................................................................134
MAKOSA AMBAYO WASTAAFU WENGI WANAYAFANYA ......................................................................................134

HATUA ZA KUFUATA ZA KUTENGENEZA PESHENI YAKO ..................................................................................... 137

SEHEMU YA TANO ............................................................................................................................ 147

JINSI BEI YA KIPANDE INAVYOKOKOTOLEWA .................................................................................................... 147

VITU MUHIMU VYA KUKUMBUKA ..................................................................................................................... 149

KUSHUKA KWA BEI YA KIPANDE ........................................................................................................................ 150

KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA VIPANDE VYA UTT AMIS ............................................................................ 150
(i) Maeneo ambayo UTT AMIS imewekeza .......................................................................................................151
(ii) Riba kutoka katika hati fungani ....................................................................................................................151
(iii) Gawio kutoka katika hisa .........................................................................................................................153
(iv) Kukua kwa thamani ya hisa ambazo mfuko umewekeza .........................................................................153

JINSI UTT AMIS INAVYOFANYA KAZI .................................................................................................................. 154


(i) Uwekezaji mseto ..........................................................................................................................................155
(ii) Maswali yanayoulizwa mara kwa mara ........................................................................................................156
HATARI ZA JUMLA ZA UWEKEZAJI KATIKA MIFUKO ........................................................................................... 156

SEHEMU YA SITA ............................................................................................................................... 159

SAIKOLOJIA NA UWEKEZAJI ............................................................................................................................... 159


JE MIAKA 30 NI MINGI KUWEKEZA........................................................................................................................159

SEHEMU YA SABA ............................................................................................................................. 161

MADA YA ZIADA KUTOKA KATIKA KITABU CHA NAMNA BORA YA KUWEKEZA KATIKA SOKO LA HISA .............. 161

JIFUNZE KUJILIPA WEWE KWANZA .................................................................................................................... 161

JINSI YA KUANZA KUWEKEZA UTT AMIS ............................................................................................................ 163


VIFUPISHO VYA MANENO
DSE - Dar Es Salaam stock exchange (Soko la Hisa la DSM)

DSM - Dar Es Salaam

MLN- Milioni

NICOL – National Investment Company Limited

ROI - Mrejesho wa uwekezaji (return on investment)

TSH - Shilingi ya Tanzania

UTT AMIS - Mfuko wa pamoja wa uwekezaji


©Maombi A. Chagamba

Simu: +255713999596
WhatsApp: +255713999596
Email wiseinvestorr@gmail.com
@January, 2022

Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili, kurudufu au kutumia kitabu hiki au sehemu ya
kitabu hiki kwa namna isiyokubalika kiuandishi. Mwandishi ametoa kitabu hiki kwa lengo la
kuelimisha na kinapaswa kutumiwa kwa lengo hilo tu na si vinginevyo.
Kwa ajili ya

Wize investors wote popote walipo nchini Tanzania na nje ya


Tanzania
SHUKRANI
Ni jambo la kumshuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kheri zake tangu

nilipoanza kujifunza kuhusu uwekezaji, kuanza kuwekeza na hata kuona

mafanikio ya kuwekeza katika eneo la mifuko ya pamoja. Ni kutoka na safari hiyo,

nimeweza kuandika kitabu hiki ili kuwanufaisha watu wengi zaidi na maarifa

kuhusu uwekezaji katika mifuko ya pamoja ya uwekezaji, hususani UTT Amis.

Pili, ninatoa shukrani za pekee kwa wazazi wangu kwa kunilea vyema na kunipa

msingi imara wa elimu. Tatu, natoa shukrani kwa mdogo wangu Chagamba Abel

ambaye alinipa ushauri wa kitaalam kwenye uandishi wa kitabu hiki lakini pia

amekuwa akinipa ushauri kwenye masuala mbalimbali ya kimaisha.

Maarifa yaliyowasilishwa kwenye kitabu hiki yametokana na kusoma, kusikiliza

na kujifunza kutoka kwa watu na wanazuoni mbalimbali wa masuala ya

uwekezaji, kiukweli si rahisi kuwataja wote lakini kwa uchache tu niwashukuru

wataalam na wafanyakazi wa mfuko wa UTT pamoja na soko la hisa la Dar Es

Salaam (DSE). Mengi yaliyoandikwa humu ni zao la elimu wanayoitoa na baadhi

ya taarifa zimetokana na taarifa halisi za utendaji wa mfuko wa UTT.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, ninatoa shukrani kwa Joseph E. Gamba

aliyehusika katika kuhariri kitabu hiki.


VITABU VINGINE

Kila kitabu hapo kinauzwa TSH 5000/= na viko katika mfumo wa E BOOK
(PDF), FALSAFA YA UWEKEZAJI (page 54), JINSI YA KUSOMA RIPOTI
ZA FEDHA (page 63).
JINSI YA KUTUMIA KITABU HIKI

Kitabu hiki kimesheheni elimu ya uwekezaji katika mifuko ya pamoja ya


uwekezaji hasa mfuko wa uwekezaji unaoendeshwa hapa nyumbani TANZANIA
wa UTT Amis. Kitabu hiki kimetolewa na kusambazwa katika mfumo wa nakala
laini (softcopy) inayoweza kusomwa kwa kutumia program ya PDF (Portable data
file).

Kama unatumia pdf reader au WPS OFFICE basi upande wa kushoto kwenye
bookmarks/table of contents utaona yaliyomo na unaweza kubonyeza mada
yoyote ile na itafunguka.

Ili kupata maarifa kama ilivyolengwa na mwandishi, inashauriwa msomaji aweze


kusoma kuanzia mwanzo na kuendelea kwa mada zinazofuata kwani mada
zilizowasilishwa kwenye kitabu hiki zinategemeana.
ANGALIZO
Kitabu hiki kimetolewa kwa lengo la kutoa uelewa wa masuala ya uwekezaji
katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa UTT AMIS. Mwandishi
ameandika haya aliyoyawasilisha kwenye kitabu hii kutokana na uelewa wake
juu ya masuala ya uwekezaji katika mfuko wa Pamoja wa UTT AMIS na
uwekezaji katika masoko ya mitaji. Uelewa na elimu aliyoiwasilisha katika
kitabu hiki imetokana na kujifunza kupitia kusoma, semina na kuwekeza
kwenye mifuko mbalimbali iliyo chini ya UTT AMIS lakini pia kwenye vyanzo
vingine vya mapato vilivyo kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam.

Mwandishi sio mshauri wa masuala ya fedha au uwekezaji isipokuwa ni


mwekezaji na mtu aliye na ufahamu kuhusu masuala ya uwekezaji ambapo
kwa upendo ameamua kuandika kitabu hiki ili kutoa uelewa huu kwa jamii
kubwa zaidi duniani. Hivyo, kama msomaji atahitaji kuwekeza sehemu yoyote
iliyoelezwa kwenye kitabu hiki, anashauriwa awaone wataalamu wa masuala
ya fedha na uwekezaji kwa ajili ya kupata ushauri mahsusi kabla ya kuwekeza.

Mwandishi hatahusika na kitendo chochote ambacho kitachukuliwa na


msomaji kutokana na taarifa zilizopo katika kitabu hiki, ieleweke kuwa
kilichoandikwa humu ni maoni ya mwandishi na wala hayahusiani na UTT
AMIS wala chombo chochote kilichotajwa katika kitabu hiki. Pia mwandishi
sio mfanyakazi wa UTT AMIS na wala hana mahusiano yoyote na mifuko hii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu UTT AMIS unaweza kuwasiliana na mfuko wa
UTT AMIS kupitia ofisi zake ambazo zimetapakaa sehemu mbalimbali nchini
Tanzania.
UTANGULIZI
Chukulia ungekuwa umewekeza katika mfuko wa umoja wakati unaanzishwa
mwaka 2005, bei ya kipande kwa wakati huo ilikuwa TSH 70/= tukija leo hii
mpaka disemba 29 mwaka 2021 bei ya kipande ilikuwa 776 ina maana kama
ulikuwa umewekeza kipindi kile mrejesho wako wa uwekezaji ungekuwa
1008.6% ndani ya miaka 16 tu, ambayo ukipiga hesabu ni sawa na wastani wa
mrejesho wa uwekezaji wa 63% kila mwaka, kama wewe ni muwekezaji na
unafahamu maana ya mrejesho wa uwekezaji basi utaona kuwa uwekezaji kuwa
na mrejesho wa wastani wa 63% kwa mwaka ni uwekezaji bora wa kiwango cha
juu. Aidha, uwekezaji katika eneo hili unabeba hatari ndogo za uwekezaji.

Kama haufahamu maana ya mrejesho wa uwekezaji basi usihofu hapo chini


nitakuelekeza jinsi gani muwekezaji anavyoweza kupata mrejesho wa uwekezaji
katika uwekezaji wowote ule. Mathalani, kama muwekezaji angewekeza TSH 10
milioni kipindi cha mwaka 2005 ambapo mfuko wa Umoja ulikuwa unauza
kipande kwa TSH 70, mwezi disemba mwaka 2021, hiyo milioni 10 yake ingekuwa
TSH 110 milioni ambayo ni sawa na mrejesho wa uwekezaji wa 1000%.

Mfano mwingine wa mrejesho wa uwekezaji ni kuhusu mfuko wa wekeza Maisha


ambao ulianzishwa mwaka 2007. Wakati huo, bei ya kipande ilikuwa 100 tukija
mpaka disemba 29 mwaka 2021 bei ya kipande ilikuwa 659/= ambayo ni sawa
mrejesho wa 559% asilimia, ambayo ni sawa na wastani wa 39.9/= kwa mwaka.
Haya, tuendelee kwa kuangalia mfuko wa ukwasi (liquid fund) ulioanzishwa
mwaka 2013. Wakati huo bei ya kipande ilikuwa TSH 100/= mpaka kufikia
disemba 29 mwaka 2021 bei ya kipande ilikuwa 302/= ambayo ni sawa na mrejesho
wa uwekezaji wa 202% ndani ya miaka 8 ambayo ni sawa na wastani wa mrejesho
wa 25.25% kwa mwaka, kwa muwekezaji yoyote ambaye amekwisha kuwekeza
katika masoko ya fedha na mitaji basi utajua kuwa wastani wa mrejesho wa 25%
ndani ya miaka 8 ni kitu ambacho wawekezaji wengi wanakitolea macho. Hebu
fikiria hati fungani ya miaka 25 ina mrejesho wa asilimia 15.95% kwa mwaka.

Sasa baada ya kuzungumza hayo huwa ninakutana na changamoto kutoka kwa


makundi mawili, kundi la kwanza hawa ni wawekezaji na wanakuwa na muda
mgumu sana kuamini kuwa kuna uwekezaji unaoweza kukupa mrejesho wa
asilimia 39% kama wastani kwa miaka 16, kwao wao mrejesho ambao
wanaukubali ni mrejesho wa asilimia 12% au 15% kwa mwaka.

Kundi la pili huwa wanaona kuwekeza kwa miaka 16 ni mtihani ambao hakuna
anayeweza kuufaulu.

Kama wewe ni mmoja wapo wa watu walio katika kundi mojawapo kati ya hayo
yaliyo juu ungana nami ili nikuonyeshe kuwa ina wezekana kuwa na uwekezaji
wenye mrejesho wa asilimia 39% na kwa kundi la pili wataona kuwa kuwekeza
miaka 16 sio kitu kigumu sana bali ni chepesi mno na wataona kuwa unaweza
kutengeneza utajiri wa kudumu kupitia uwekezaji wa pamoja.

MFUMUKO WA BEI NA MAISHA YAKO (INFLATION)


Katika kitabu nilichokiandika cha namna bora ya kutengenza hela katika soko
la hisa nimeeleza sababu 6 za kwanini kila mtu lazima awe muwekezaji. Moja ya
sababu zilizoainishwa ni kuhusu mfumuko wa bei sitaelezea kila kitu ambacho
nimekisema katika kitabu kile bali nitakugusia kidogo kukuonyesha kuwa ni
muhimu uwe muwekezaji na sio muwekezaji tu bali uwe muwekezaji mwenye tija
ili kuepukana na madhara ya mfumko wa bei.

Mfumuko wa bei ni kuongezeka kwa bei za vitu au kwa maneno mengine


kupungua kwa nguvu ya ununuzi ya fedha. Unaposikia kuwa mfumuko wa bei ni
asilimia 4 kwa mwaka fulani ina maana kwa mwaka ule pesa imepungua uwezo
wake wa ununuzi kwa asilimia 4.
Nitoe mfano rahisi ili kujenga uelewa kwa watu wote kuhusu mfumuko wa bei.
Kama una mshahara wa 1000/= kwa mwaka na huu mshahara unatosha kabisa
matumizi yako bila kubaki, ikitokea mfumuko wa bei ukawa 5% ina maana nguvu
ya pesa imepungua kwa 5% kwa hiyo 1000/= haina tena nguvu ya kununua bidhaa
za 1000/= iliyokuwa ikinunua awali isipokuwa ina uwezo wa kununua bidhaa
zenye thamani ya shilingi 950/=. Ina maana mwaka unao fuata kama hautaongezwa
mshahara, utajikuta mshahara ule ule ulikuwa unapokea siku zote unashindwa
kukidhi mahitajiyako ya kila siku. Hivyo, ukitaka umshinde huyu jamaa anayeitwa
mfumuko wa bei ni lazima ujifunze kuwekeza tena kuwekeza sehemu ambazo
zina faida shindani.

Chukulia mfano mwingine bro chagamba yeye ni muwekezaji na amewekeza


shilingi 1000/= kwenye mfuko wa ukwasi na kwa mwaka huo mfuko wa ukwasi
ulikuwa na mrejesho wa asilimia 15%, hii ina maana pesa ya bro chagamba
imekuwa na kufikia 1150 ila mfumuko wa bei ulikuwa 5% ina maana na pesa ya
bro chagamba imepungua nguvu ya manunuzi kwa 5% na kubaki 1092.25/=.
Unadhani bro Chagamba na yule aliyetolewa mfano awali ni nani ataweza
kumudu gharama za maisha?

Kutokana na kuwa hakuna mafundisho mengi ya elimu ya kifedha kuna watu


hawajui kuwa nguvu ya mfumuko wa bei iko kinyume nao na kama hawatajifunza
kuwekeza basi watashindwa kumudu gharama za maisha miaka ijayo.
SEHEMU YA KWANZA

MFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA NI NINI?


Mfuko wa uwekezaji wa pamoja ni aina ya kampuni ambayo inajishughulisha na
uwekezaji ambapo kampuni inakusanya pesa kutoka kwa wawekezaji wakubwa
na wadogo na kuwekezwa kitaalamu chini ya uangalizi wa meneja wa kampuni
hiyo. Kampuni hii inakuwa chini ya meneja ambaye ni mtaalamu wa masuala ya
uwekezaji na fedha hasa kwenye eneo husika la uwekezaji. Kuna aina nyingi sana
za kampuni zinazofanya kazi kwa kutumia mfumo huu, mathalani, kuna kampuni
ambazo zinakusanya pesa kutoka kwa wawekezaji na zinawekeza katika hisa tu,
kuna kampuni ambazo zina mchanganyiko wa uwekezaji mfano hisa na hati
fungani au kuna kampuni ambazo zinajikita katika uwekezaji wa ardhi na mazao
yake (real estate). Kampuni hizi huwa zinaweza kuundwa kwa ajili ya kukidhi
hitaji fulani mahsusi, mfano ada ya watoto kama ilivyo kwa UTT AMIS mfuko wa
watoto. nk

AINA ZA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA


Mifuko ya uwekezaji wa pamoja (mutual fund) iko ya ina mbili

A. Mfuko ulio wazi (open ended mutual fund)


B. Mfuko ulifungwa (close ended)

MFUKO ULIO WAZI (OPEN ENDED MUTUAL FUND)

Mfuko huu unakuwa hauna idadi maalumu ya vipande (unit) ambavyo inaweza
kuwa nazo, ninacho maanisha ni kuwa vipande vya mfuko wa aina hii vinaweza
kuongezeka kutegemea na idadi ya watu wanaonunua au vikapungua kutegemea
na idadi ya watu ambao wanauza vipande vyao. Mfano wa kampuni ya namna ni
UTT AMIS. Muhimu kuhusu kampuni ya namna hii ni kuwa muda wowote
unaweza kununua vipande kama utahitaji na muda wowote unaweza kuuza
vipande kama utahitaji kufanya hivyo, kwa sababu hauna idadi maalumu ya
vipande ambavyo inaweza kuwa navyo.

Ukihitaji kununua vipande unatengenezewa vipande. Mfano kama kampuni ina


vipande 1000 na ukahitaji kununua vipande 300 basi utauziwa vipande 300 na
mfuko utakuwa na jumla ya vipande 1300 na kama akitokea mtu mwingine
akahitaji vipande 100 basi atauziwa vipande 100 na mfuko utakuwa na vipande
1400.

MFUKO ULIOFUGWA (CLOSE ENDED MUTUAL FUND)

Hii ni aina ya mfuko wa uwekezaji wa pamoja ambao una idadi kamili ya vipande
na haiongezeki kulingana na uhitaji au kupungua pale ambapo watu wanauza
vipande vyao, wakati mfuko huu unaanzishwa unakuwa na idadi maalumu ya
vipande na baada ya vipande vile kuuzwa basi kama ukihitaji kipande lazima
atokee mtu aliye nunua awali ndio akuuzie na kama akiwa hayupo basi hauwezi
kupata vipande,na kama unataka kuuza pia lazima apatikane mteja wa kununua
vipande vyako kama mteja hatapatikana basi hauwezi kuuza vipande vyako.
Mfano, kama mfuko unaanzishwa ulikuwa na vipande 1000 basi kama ukitaka
kununua vipande 100 basi lazima apatikane mtu akuuzie na baada ya kukuuzia
vipande vitabaki 1000. Mfano wa kampuni ya namna hii hapa nchini Tanzania ni
NICOL na TCIL ambazo ziko soko la hisa la DSE.

KIPANDE NI NINI?
Yamkini umekutana na neno kipande au vipande kwenye andiko hili na unajiuliza
kuwa kipande ni nini. Katika uwekezaji, kipande ni umiliki ulionao katika
uwekezaji ambao unafanywa na kampuni ya uwekezaji wa pamoja iliyo wazi
(open ended mutual fund). Mfano, kama mmekusanyika watu 4 na kununua
shamba la heka moja kwa gharama ya milioni moja sasa kutegemea na kila mmoja
amechangia kiasi gani kila mmoja atakuwa na kipande cha shamba kutegemea na
umiliki alio nao, mfano kama umechangia laki 5 basi kipande chako ni nusu na
kama mwingine amechangia laki mbili na nusu basi kipande chake ni robo.

Mfuko kama una ukubwa wa shilingi bilioni moja basi unagawaywa katika
vipande vidogo vidogo ambavyo kwa ujumla wake vinakuwa sawa na ukubwa wa
mfuko, hivi vipande vinauzwa kwa bei ndogo na unaponunua kipande kimoja basi
hiki kipande kinakuwa moja kati ya thamani ya mfuko. Nchini Tanzania tunao
mfuko wa uwekezaji wa Pamoja unaojulikana kwa jina la UTT Amis. Katika
kitabu hiki tutapata fursa ya kujifunza kwa pamoja namna ya kuwekeza kwenye
mfuko huu wa UTT Amis.

UTT AMIS NI NINI

UTT AMIS ni kifupi cha Unit Trust of Tanzania Asset Management and
Investor Services. UTT AMIS ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio wazi (open
ended mutual fund) ambao ulianzishwa mwaka 2003 kama UTT na baadae
mwaka 2013 ukaiitwa UTT AMIS. UTT AMIS ni taasisi ya serikali iliyo chini ya
Wizara ya fedha na Mipango.

JINSI UTT AMIS INAVYOFANYA KAZI


Kama nilivyoleza hapo juu ni kuwa UTT AMIS ni taasisi ya serikali iliyo chini ya
wizara ya fedha na mipango ambayo kazi yake ni kupokea fedha kutoka kwa
wawekezaji wakubwa na wadogo na kuziwekeza kitaalamu katika masoko ya
fedha na masoko ya mitaji. Nikupe mfano, chukulia mna kikundi cha watu 20 na
mna pesa wa ajiri ya kuwekeza basi mnaweza kuamua kumchagua mmoja wenu
kwa ajiri ya kusimamia uwekezaji wenu, huyu mtu ambaye mmemchagua ataenda
kuwekeza katika eneo husika na faida ikipatikana basi mtagawana kila mtu
kutegemea na kiasi ambacho amechangia katika mfuko wenu. UTT AMIS pia
inafanya kazi kwa mfumo huu, ambapo kupitia kukusanya fedha kutoka kwa
wawekezaji tofauti tofauti, inawekeza kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato
mathalani kwenye soko la fedha na mitaji (Hisa na hatifungani).

FAIDA ZA KUWEKEZA UTT AMIS


Kama una wasi was kuhusu kuwekeza UTT AMIS basi hizi ndizo faida za
kuwekeza na UTT AMIS.

FAIDA YA 1

MENEJA MWENYE UELEWA NA UWEKEZAJI

Kama ukitaka kuwekeza wewe mwenyewe katika hisa lazima uwe na uelewa na
masuala ya hisa, jinsi gani ya kuchagua kampuni ya kuwekeza na jinsi gani ya
kukabiliana na hatari za uwekezaji, muda gani sahihi wa kuwekeza na mambo
kadha wa kadha. Lakini kupitia UTT AMIS unapata nafasi ya kukutana na meneja
mwenye utaalamu wa masuala ya uwekezaji ambaye kazi yake kila siku ni
kusimamia pesa yako, kuhakikisha inawekezwa mahali sahihi na inakupa faida
shindani. Kwa kuwekeza UTT AMIS unaweza kuwekeza leo na ukaamua kwenda
safari ya miaka na ukirudi utakuta meneja amesimamia pesa zako vizuri.

FAIDA YA 2

UKWASI ((LIQUIDITY)
Moja kati ya vitu ambavyo utaipenda UTT AMIS ni urahisi wa kununua na kuuza
vipande, kama umewekeza katika hisa utafahamu ya kuwa ili uweze kununua hisa
lazima awepo mtu wa kukuuzia na kama hakuna mtu wa kukuuzia hisa basi
hauwezi kununua. Pili, kama unataka kuuza hisa lazima awepo mteja wa kununua
na mara kadhaa nimeona watu wanakaa na hisa miezi bila kupata mtu wa
kununua hisa zao ila UTT AMIS ni rahisi mno kununua na kuuza vipande kwani
pale ambapo unanunua vipande ni meneja wa mfuko ndio anakuuzia na kama
tulivyoona hapo juu mfuko ulio wazi (open ended mutual fund) hauna ukomo wa
vipande muda wowote unapohitaji vipande basi unaweza kuvipata. Aidha
kutokana na aina ya mfuko uliowekeza ndani ya UTT AMIS, pale ambapo unataka
kuuza vipande vyako, hauna haja ya kusubiri mpaka mteja apatikane kwani
meneja wa mfuko ndio anayenunua vipande vyako. Kuna baadhi ya mifuko ndani
ya UTT AMIS inakuwezesha kupata pesa yako ndani ya siku 10 za kazi baada ya
kujaza fomu ya kuomba kuuza na kuna mifuko kama mfuko wa ukwasi ni ndani
ya siku 3 za kazi unaipata pesa yako.

FAIDA YA 3

UWEKEZAJI MSETO

Uwekezaji mseto unapunguza hatari za uwekezaji kwani unakuta mfuko


umewekeza katika hisa mbali mbali na sio hisa tu bali katika hati fungani hivyo
hupunguza hasara ambayo inayoweza kujitokeza kama mfuko unakuwa
umewekeza sehemu moja au kwenye uwekezaji wa aina moja. Kama
unavyofahamu ili uwekezaji wa mseto uwe na tija basi lazima uwe na kiwango
kikubwa cha kuwekeza ila kupitia UTT AMIS unapata faida ya kuwekeza katika
mfuko ambao una uwekezaji wa mseto unaowekezwa kitaalamu na meneja wa
mfuko.
FAIDA YA 4

KIASI KIDOGO CHA MTAJI


Ukitaka kuwekeza katika hati fungani ya serikali ya muda mrefu kima cha chini
ambacho unatakiwa kuwa nacho ni TSH 1 milioni na kama unataka kuwekeza
katika hatifungani za muda mfupi basi kiasi ambacho unatakiwa kuwa nacho ni
laki tano za kitanzania ila kupitia UTT amis unaweza kuwekeza kwa kiasi kidogo
cha mtaji, kuna baadhi ya mifuko ukiwa na 5000/= unaweza kuanza kuwekeza na
kizuri ni kuwa hii mifuko imewekeza katika hati fungani na katika hisa maana
yake ni kuwa kwa kiasi kidogo tu unaweza kuanza kuwekeza katika hati fungani
na katika hisa kupitia mifuko ya UTT AMIS.

FAIDA YA 5

FAIDA SHINDANI (COMPETITIVE RETURN)

Ukitaka kuwekeza pesa benki ili upate riba ndani ya mwaka mmoja sio kitu cha
ajabu ukapokea riba ya 3% au kama utataka upate riba kubwa basi lazima uwe na
kiasi kikubwa cha pesa ila ukiwa na UTT AMIS kwa kiasi kidogo tu unaweza
kupata faida nzuri ambayo hauwezi kuipata benki huku ukiwa na uwekezaji
mdogo.

Ngoja nitoe mfano, kama una 100,000/= hauwezi kuwekeza katika hati fungani ya
miaka 25 (maana kiwango cha chini cha kuwekeza katika hati fungani ya muda
mrefu ni TSH 1milioni) ila kama ukikusanya rafiki zako 9 wenye laki moja
mnaweza kuwekeza hela yenu kwa pamoja na mkapata mrejesho wa asilimia
15.95% (mrejesho unaotolewa na hati fungani ya miaka 25) kwa mwaka, ambayo
mtagawana kila mmoja kulingana na kiasi chake alichoweka. UTT AMIS pia
inafanya kazi kwa mfumo huu ambapo unaweza kuwekeza katika hati fungani
kwa kiasi cha shilingi 50,000/= tu kupitia mfuko wa hati fungani (bond fund).

Mfano wa pili ni kama unahitaji kuweka pesa benki ili upewe riba kubwa lazima
uwe na kiwango kikubwa cha pesa lakini kupitia UTT AMIS unaweza kuwekeza
pesa kwa riba kubwa kwani pesa yako inakusanywa pamoja na wawekezaji
wengine na inawekezwa kwa pamoja kwa wingi wake.

FAIDA YA 6

MUDA MCHACHE KUFANYA UCHUNGUZI WA KABLA YA KUWEKEZA

Kufanya uchunguzi wa mifuko ya UTT AMIS ni rahisi mno ambavyo hata kama
sio mtaalamu wa uwekezaji unaweza kufuatilia jinsi mfuko unavyoenda bila shida
ikilinganishwa na kufanya uchunguzi wa kampuni ya kuwekeza kupitia soko la
hisa. Kiufupi ufuatiliaji wa uwekezaji wa UTT AMIS ni rahisi sana na hauchukui
muda.

FAIDA YA 7

RIBA YA KAMPAUNDI (COMPOUND INTEREST)


Kama uliwahi kumkopesha mtu kwa riba, au ulishawahi kukopa kwa riba basi
unaweza kuwa unafahamu maana ya riba, ila riba ambayo unaifahamu sio ambayo
tunaizungumzia hapa. Nianze na mfano ili kuweka urahisi wa kuelewa kile
tunachokizungumzia hapa, ukiwa na kikoba na ukaamua kukopa TSH 100,000/=
kwa riba ya asimilia 10 kwa wiki na ukakopa ndani ya wiki mbili ina maana wiki
ya kwanza utarudisha TSH 10000/= kama riba na wiki ya pili utarudisha riba ya
TSH 10000/=.Riba hii inaitwa riba rahisi (simple interest). Aina hii ya riba inafanya
kazi kwa namna iliyooneshwa hapo juu. Mfano wa pili wa riba rahisi ni uwekezaji
huu ambapo mwekezaji amewekeza fedha kiasi cha TSH 10,000/- benki kwa riba
ya 5% kwa miaka 5. Mapato ya mwekezaji huyu kwa miaka 5 yatakuwa kama
inavyoonekana kwenye jedwali namba 1 hapo chini:-

MWAKA RIBA

1 500
2 500
3 500
4 500
5 500

JUMLA 2500

Jedwali 1: Marejesho ya riba rahisi kwenye uwekezaji wa TSH 10,000

Hivyo kwa miaka mitano, mwekezaji huyu atapata faida iliyotokana na riba
iliyolipwa kwenye uwekezaji wake wa TSH 10,000/- kiasi cha TSH 2500. Mara
baada ya uwekezaji huu kukamilika, mwekezaji atarudishiwa shilingi 12500/-
ikiwa ni pamoja na fedha aliyoiwekeza. Hati fungani za serikali zinatumia riba
rahisi kulipa watu wanaoikopesha serikali.

Riba nyingine inaitwa riba ya kampaundi, usiombe mtu akukopeshe fedha kwa
riba ya kampaundi utaomba ardhi ipasuke au uwe na nguvu za kutoonekana ili
anayekudai akija asikuone. Wawekezaji makini wanapenda nguvu iliyo katika
riba ya kampaundi. Unaweza ukawa unajiuliza ni kwa nini wanaipenda sana hii
riba?, basi kupitia kitabu hiki tuone riba hii inafanyaje kazi.
Riba ya kampaundi inakuwa na utofauti na riba rahisi kwa kigezo cha kuwa
katika riba ya kampaundi baada ya kupokea riba mwaka wa kwanza ile riba
inakuwa sehemu ya mtaji nayo mwaka unaofuata inapokea riba, mfano wetu hapo
juu kama ungekuwa umeweka hela benki 10000/= kwa riba ya 5% ila ni riba ya
kampaundi ina maana mwaka wa kwanza ungepokea 500/= ila mwaka wa pili hii
500/= inaungana na 10000/= zote zinapokea 5%, kwa hiyo mwaka wa pili itakuwa
5% ya 10500/= ambayo riba yake itakuwa 525 kwa mwaka wa pili.

MWAKA RIBA
1 500
2 525
3 551.25
4 578.8
5 607.75
jumla 2762.8

Nadhani mpaka hapo umeona utofauti uliopo kati ya hizi riba mbili kwani
mwisho wa siku jumla ya hela yako inakuwa 12762.8 ambapo ni ongezeko la
262.8/= unaweza kusema 262.8 sio nyingi tukiongeza miaka 5 tena unaweza kuona
maajabu ya utofauti kwani kadri muda unavyoenda ndivyo tofauti inakuwa kubwa

UTT AMIS inatumia riba ya kampaundi katika mifuko yake na ndio moja ya kitu
ambacho kinafanya UTT AMIS iwe kipenzi cha wawekezaji wengi makini, hapo
mbele tutaona jinsi riba ya kampundi ya UTT AMIS ilivyo.
MREJESHO WA UWEKEZAJI (RETURN ON INVESTMENT) (ROI)
Sidhani kama kuna siku niliwahi kufundisha uwekezaji bila kugusia hii maana ni
muhimu sana, katika kitabu changu namna bora ya kutengeneza hela katika
soko la hisa nimeelezea hii kwa kirefu hapa nitatoa pointi chache tu.

Maana ya mrejesho wa uwekezaji (ROI) ni asimilia ya faida unayoipata


unapokuwa umewekeza katika uwekezaji Fulani. Mathalani, kama umenunua
kiwanja TSH 1 milioni na baada ya mwaka mmoja ukauza TSH 1.5 milioni, ili
kupata mrejesho wa uwekezaji unachukua faida kugawanya kwa mtaji. Kwa
mfano wetu hapo juu inakuwa kama ifuatavyo:-

Mrejesho wa uwekezaji = (Faida /mtaji) * 100

Faida 500000/=

Mtaji 1000000/=

Mrejesho wa uwekezaji = (500000/1000000)* 100 = 50%

Hivyo mrejesho wa uwekezaji (ROI) katika kiwanja hiki ni 50%

Mfano wa pili

Kuna mtu nilimpa swali nikamuuliza hivi mtu aliyenunua kipande kwa bei ya
TSH 1000/= na baada ya mwaka mmoja akauza kwa bei ya 2000 na mtu alinunua
kipande kwa bei ya 70 baada ya mwaka akauza kipande kwa bei ya 170 nani
amepata faida kuliko mwenzake? akajibu mtu wa kwanza nikajua huyu sio
muwekezaji, kwani wawekezaji tunafikiri tofauti kidogo hebu tuone mirejesho
yao
Mtu wa kwanza

Mtaji wake 1000/=

Bei aliyouza kipande = 2000/=

Faida aliyopata = 2000- 1000 = 1000/=

Mrejesho wa uwekezaji =( faida /mtaji)*100 = 1000/1000)*100= 100%

Kwa hiyo mtu wa kwanza alikuwa na mrejesho wa 100%

Mtu wa pili

Mtaji wake =70

Bei aliyouza kipande = 170

Faida aliyopata = 170-70= 100

Mrejesho wa uwekezaji =(faida /mtaji)*100 =100/70 = 142%

Mtu wa pili alipata mrejesho wa uwekezaji wa 142%

Kati ya 100% na 142% ipi kubwa, kama jibu lako ni 142% basi umeanza kufikiri
kama muwekezaji.

Kuna baadhi ya watu hawalijui hili yeye anachojua ni kuwa kipande kimepanda
bei tu, bila kujua faida yake ni shilingi ngapi, ila unatakiwa ujue kuwa japo
vipande vyote vinaweza kuwa vimepanda bei ila kuna vipande vimepanda bei
kubwa kuliko vipande vingine na unapojua mrejesho wa uwekezaji unakuweka
katika nafasi nzuri ya kujua wapi panakupa faida kubwa na wapi uwekeze ili
upate faida nzuri.

Kwa hiyo unaposikia kuwa mfuko una mrejesho wa 12% au 14% ina maana kuwa
asilimia 12% au 14% ndio inakurudia kama faida kwa mwaka huo, kama ulikuwa
umewekeza 100/= na mrejesho wa uwekezaji ukawa 12% ina maana faida yako ni
TSH 12/= kwa mwaka huo.

Kwa maelezo zaidi ya mrejesho wa uwekezaji unaweza kusoma pia kitabu changu
cha namna bora ya kutengeneza hela katika soko la hisa.

UNAPATAJE FAIDA KUWEKEZA UTT AMIS


Faida za kuwekeza UTT zinakuja kwa namna mbili:-

(i) Kupitia gawio (dividend)

Kuna baadhi ya mifuko kama mfuko wa HATI FUNGANI na mfuko wa JIKIMU


unatoa gawio katika vipindi tofauti tofauti, kwa hiyo unapata faida kupitia gawio.
Ukitaka kujua kuhusu gawio, soma kitabu nilichokiandika cha namna bora ya
kutengenza hela katika soko la hisa.

(ii) Kupitia ukuaji wa mtaji (capital gain)

Hii ni njia ya pili ambayo ina mnufaisha muwekezaji hii ni pale ambapo unanunua
kipande kwa bei ya chini na kukiuza kwa bei ya juu. Mfano umenunua kipande
kwa bei ya 100/- na baada ya muda bei ikapanda kufikia 200/= ukauza faida
ambayo umeipata ndio ukuaji wa mtaji na hata kama haujauza hiyo iliyoongezeka
ndio faida yako.
SEHEMU YA PILI

MIFUKO YA UTT AMIS

HATARI ZA UWEKEZAJI KATIKA MIFUKO YA UTT AMIS


Kabla hatujaanza kuuzungumzia mfuko kila mfuko ulio ndani ya UTT AMIS ngoja
tuzungumzie hatari za uwekezaji katika hii mifuko ya UTT AMIS.

Hatari za uwekezaji maana yake ni kuwa kile ambacho tunakitarajia kukipata


kinaweza kisije kama tulivyotegemea, mfano kama tunategemea msimu wa mvua
tulime mahindi na tupate gunia 10 ule uwezekano wa kuwa tulichokitarajia
kinaweza kisije kama tulivyokusudia ndio tunaita hatari za uwekezaji na huwa
tunaziweka katika makundi.

Katika mifuko ya UTT AMIS tumeigawanya katika makundi mawili kutegemea


sehemu ambapo mifuko hii imewekeza. Mgawanyo huo unahusisha mifuko iliyo
katika hatari za chini na ile iliyo katika hatari za wastani.

(i) Hatari za chini

Uwekezaji wowote ule una hatari za uwekezaji (risk), tunapozungumzia hatari za


chini maana yake mfuko umewekeza katika maeneo ya kuaminika au maeneo
ambayo yanaleta mrejesho ambao ni wa uhakika. Mfano, kama mfuko umewekeza
katika hati fungani pekee unakuwa na uhakika wa mapato kwa asilimia kubwa
kuliko mfuko ambao umewekeza katika hisa ambako mapato yake siyo ya
kutabirika. Mfuko ukiwekeza katika hati fungani mathalani ya miaka 25 yenye
mrejesho wa uwekezaji wa 15.95% kutokana na mkataba wenu maana yake ni
kuwa serikali itaendelea kukulipa asilimia 15.95% kila mwaka kwa hati fungani
uliyonayo. Kwa hiyo unakuwa na uhakika kwa asilimia fulani kuwa mwaka ujao
mapato yangu yatakuwa kiasi fulani na hivyo hivyo kwa miaka inayofuata.

Mfano mwingine ni kama umewekeza katika hisa, bei ya hisa inaendeshwa na


uhitaji na usambazaji (demand and supply) kitu ambacho wewe kama
muwekezaji hauna mamlaka nacho na hauwezi kujua kama mwaka huu bei ya hisa
itapanda au itashuka pia upande wa gawio, inategemeana na ufanisi wa utendaji
wa kampuni ili kupata faida. Pamoja na kampuni kupata faida, bado wanahisa
wanaweza wasikubali kampuni itoe gawio au menejimenti ikaona sio vyema kutoa
gawio kwa mwaka huo. Kwa hiyo utaona kuwa mapato ya Hisa si ya kuaminika
ikilinganishwa na mapato yatokanayo na hati fungani. Hii ni kusema kuwa ikiwa
mfuko wa uwekezaji wa pamoja umewekeza kwenye hisa tu basi hatari za
uwekezaji zinakuwa juu kuliko mfuko uliowekeza kwenye hati fungani.

Kwa hiyo tunaposema mfuko umewekeza katika hati fungani au amana za benki
basi mapato yake yana uhakika kwa asilimia kubwa kwa hiyo mfuko huo una
hatari za chini za uwekezaji, na tutaona chini kuwa mifuko hii haina mabadilko
makubwa sana ya mrejesho wake mwaka kwa mwaka.

Kwa hiyo ninapoanza kuielezea mfuko mmoja baada ya mwingine ninaposema


mfuko huu una hatari za uwekezaji za chini basi ujue mfuko huu umewekeza
katika mapato ya kuaminika pekee.

(ii) Hatari za wastani

Nadhani nimetoa maelezo ya kutosha hapo juu kuhusu namna tunavyoigawa


mifuko katika makundi mawili kundi lenye hatari za uwekezaji za juu na kundi
lenye hatari za uwekezaji za wastani, sasa hapa kuna kundi la mifuko ambayo
imewekeza katika hisa na pia imewekeza katika mapato ya kuaminika. Kama
tulivyosema awali kuwa, mapato ya kuaminika ina maana mfuko huo una hatari za
chini na mapato kutoka kwenye hisa una hatari za juu basi mfuko uliowekeza
kiasi katika hisa na kiasi katika mapato ya kuaminkia una hatari za wastani. Uzuri
wa mifuko ambayo imewekeza asilimia kadhaa katika hisa na kiasi kwenye
sehemu zingine zilizo na hatari za chini tutaona kuwa imewekeza kwa njia ya
mseto maana yake ni kuwa haijawekeza katika hisa za kampuni moja bali katika
kampuni tofauti tofauti

Katika kitabu changu cha hisa nimezungumzia namna ambavyo uwekezaji mseto
unasaidai kupunguza hatari za uwekezaji.

Kwa hiyo mifuko ya UTT AMIS imegawanyika katika makundi mawili kulingana
na hatari za uwekezaji: hatari za chini kwa mifuko iliyowekeza katika mapato ya
kuaminika na hatari za wastani kwa mifuko iliyowekeza katika hisa na pia katika
mapato ya kuamika. Ukisikia mfuko una hatari za wastani basi ujue una hisa
ndani yake na mfuko ambao una hatari za chini hauna hisa ndani yake.

Aidha, kwenye uwekezaji katika mfuko wa UTT AMIS, kuna mipango ya aina
mbili inayotofautisha vipande vyake. Kuna mpango wa gawio na mpango wa
kukuza mtaji. Mpango wa gawio una maana ya kuwa mifuko iliyo chini ya mpango
huu inalipa gawio kwa wawekezaji wakati mifuko iliyo kwenye mpango wa
kukuza mtaji yenyewe hailipi gawio isipokuwa uwekezaji wake unaongezeka
kutokana na kukua kwa mtaji wa mwekezaji kutokana na bei ya vipande katika
mfuko kupanda. Ikiwa umeamua kuwekeza kwenye mifuko inayopatikana chini
ya UTT AMIS ni dhahiri utakutana sana na maeno haya ya mpango wa gawio na
mpango wa kukuza mtaji, hivyo nitaeleza kwa undani kidogo na kwa mifano
kuhusu hii mipango:-
Mpango wa gawio

Kama mfuko una mpango wa gawio ina maana mfuko una utaratibu wa kulipa
gawio, kwani katika mifuko ya UTT AMIS kuna mifuko miwili ambayo inatoa
gawio na kuna mifuko ambayo haitoi gawio, kwa hiyo ukisikia mfuko una mpango
wa gawio katika maelezo hapo chini basi ujue mfuko huo una toa gawio.

Mpango wa kukuza mtaji

Katika mfuko wa UTT AMIS mpaka wakati kitabu hiki kinaandikwa, kuna
mifuko minne ambayo hailipi gawio ila muwekezaji anapata faida kwa njia ya
kukua kwa mtaji. Mtu mmoja akaniuliza kukua mtaji maana yake nini, iko hivi
unaponunua kipande kwa bei ya 100/= na baada ya kununua bei ikapanda kufikia
230/= ina maana hapo faida yako ni 130/=, hapa haujapewa gawio ila faida yako
unaipata pale ambapo kipande kinakuwa kimeongezeka thamani. Mtu mwingine
akauliza bro chagamba hapa sasa ina maana kama bei inakuwa imeshuka nakuwa
nimepata hasara jibu ni ndio ila tutaona mbele nitakapozungumzia kwa nini
kipande cha UTT AMIS kimekuwa kikipanda siku hadi siku utaona kwa nini
kipande hakiwezi kushuka na kukaa bei ile ile kwa miaka kama ilivyo hisa.

Mpango wa kukuza mtaji ni pale ambapo unanunua kipande kwa bei ya chini na
kinakuwa na kuongezeka thamani wewe unapata faida kwa ile tofauti, kama ilivyo
kwenye hisa kuwa unanunua kwa bei ya chini na unauza kwa bei ya juu.
MAANA YA MANENO MUHIMU
(i) Gharama ya kununua kipande

Hii ni gharama ambayo muwekezaji anaingia pale ambapo ananunua kipande.


Kwa lugha ya kiingereza gharama hii inajulikana kama “entry load”. Mfano, katika
soko la hisa la Dar Es Salaam, mwekezaji anapotaka kununua hisa anakwatwa
asilimia 2.366% ya manunuzi yake kama gharama ya ununuzi alioufanya, katika
vipande gharama kama hii inaitwa kwa jina la “entry load”. Lakini kwenye mifuko
iliyo chini ya UTT AMIS wao wamekuwa hawana hii gharama hivyo muwekezaji
anapata huduma hii bure anapohitaji.

(ii) Gharama ya kuuza kipande

Hii ni gharama ambayo unakatwa pale ambapo unauza kipande. Gharama hizi
zinajulikana kwa jina la kiingereza la “exit load”. Hii inakuwa ni asilimia kadhaa
ya mauzo yaliyofanyika. Kwa baadhi ya mifuko inatoza gharama hii endapo
muwekezaji atauza vipande vyake.

(iii) Repurchase

Hiki ni kitendo cha kuuza vipande, unapouza vipande ndio inaitwa repurchase,
hapa maana yake ni kuwa meneja wa mfuko ananunua vipande kutoka kwa
muwekezaji, pale unapouza vipande vyako meneja wa mfuko ndio anayenunua
vipande kutoka kwako na hiki kitendo ndio kinaitwa repurchase

(iv) Lock inn period (kipindi cha zuio)

Hiki ni Kipindi ambacho unazuiliwa kuuza vipande vyako, kipindi hiki kikiisha
unaruhusiwa kuuza vipande vyako, tutaona kuna mifuko ambayo unazuiliwa
kuuza vipande ndani ya muda fulani.
(v) Acceptance date

Hii ni siku ambayo oda yako ya kuuza vipande au oda yako ya kununua vipande
inapokelewa na meneja wa mfuko au wakala wa UTT AMIS

(vi) Muda wa kununua vipande

Una weza kununua vipande siku yoyote ya kazi, siku ambayo soko la hisa, benki
kuu na benki nyingine zinakuwa wazi ila siku ambazo sio za kazi na siku ambayo
UTT AMIS wanakuwa wanafunga vitabu vyao ambayo inatokea mara kadhaa na
inatangazwa hautaweza kununua vipande kwa siku hiyo.

Mara baada ya kueleza kinaga ubaga kuhusu hatari za uwekezaji katika uwekezaji
huu, mpango wa uwekezaji unaozingatiwa na mwekezaji na kujadili maneno
muhimu kwenye uwekezaji kwa njia hii, sasa twende kujadili mifuko mbalimbali
ya uwekezaji iliyo chini ya UTT AMIS ili mpendwa msomaji uweze kujua kila
mfuko kwa upana wake.
MFUKO WA UMOJA

UTANGULIZI
Huu ndio mfuko wa kwanza kuanzishwa kati ya mifuko yote ya UTT AMIS na
mfuko huu ulianzishwa mwaka 2005, mfuko huu ni mfuko wa wazi (open
endend) na wakati unaanzishwa ulianzishwa ukiwa na mpango wa gawio ila
mwaka 2006 ulibadilishwa na kuwa wa mpango wa kukuza mtaji, mfuko huu
wakati unaanzishwa bei ya kipande ilikuwa TSH 70 (hii ni kwa sababu serikali
ilitoa punguzo la bei ila thamani ya kipande ilikuwa TSH 100.

MFUMO WA UWEKEZAJI
Mfuko huu una uwekezaji katika hisa na katika hati fungani za serikali na za
makampuni binafsi. Uwekezaji katika hisa kwenye mfuko huu unatakiwa usizidi
50% ya uwekezaji wote wa mfuko na kiasi kingine kitawekezwa katika maeneo
mengine yenye mapato ya kuaminika.

MPANGO WA KUPATA FAIDA


Mfuko huu una mpango wa kukuza mtaji, kama nilivyozungumza hapo juu mfuko
huu hautoi gawio bali muwekezaji anapata faida pale ambapo thamani ya kipande
alichonunua inakua. Mfano, kama umenunua kipande kwa bei ya 200/= na bei
ikapanda mpaka kufikia 300/= faida yako ni 100/= sasa unaweza kuamua
kuichukua au ukaiacha iendelee kukua. Ieleweke kuwa, ili uweze kupata faida
yako mkononi lazima uuze kipande. Kuna mtu aliuuliza je ninaweza kuchukua hii
100/= na ikabaki 200/= ambayo niliweka kama mtaji, jibu ni kuwa hauwezi
kuchukua kwa mfumo huo ila nitakuonyesha njia ambayo inaweza kukuwezesha
kuchukua faida ukaacha mtaji. Ila kwa njia ya moja kwa moja lazima uuze kipande
ndio uipate faida yako mkononi.
ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Mfuko wa umoja unampa nafasi mtu yoyote (mtanzania mkazi na asiye mkazi) au
taasisi kuwekeza.

KIASI CHA CHINI CHA UWEKEZAJI


Mfuko huu unakuruhusu kuanza kuwekeza kwa kununua vipande kumi (10) hapa
ninachomaanisha ni kuwa kama ukitaka kuwekeza kwa mara ya kwanza katika
mfuko huu basi kima cha chini cha kuanzia ni vipande kumi na uwekezaji wa
nyongeza pia ni vipande kumi (10), kama unataka kuongeza uwekezaji.

HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO


Kama tulivyo zungumza hapo juu mifuko imegawanyika katika makundi mawili
kuna mifuko yenye hisa ambayo ina hatari za uwekezaji za wastani na mifuko
ambayo haina hisa ina hatari za chini za uwekezaji sasa mfuko huu una kiasi fulani
cha hisa ndani yake kwa hiyo hatari zake za uwekezaji ni za wastani

Mchoro Na. 1: Hali ya mgawanyo wa uwekezaji katika mfuko wa Umoja mpaka kufikia tarehe 30 June 2021
Kama unavyoona katika jedwali juu ni kuwa kiasi cha asilimia 41.2 kimewekezwa
katika hisa katika mfuko huu na 46.2% imewekezwa kwenye hatifungani za
serikali, 9% ziko kwenye hatifungani za makampuni binafsi na takribani 3.5%
zimewekezwa kwenye uwekezaji mwingine.

GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gaharama zozote ambazo
unakatwa, unauziwa kipande kwa bei ambayo iko sokoni.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Ukitaka kuuza vipande utakatwa kiasi cha 1% ya vipande ambavyo unataka
kuuza, lakini jumla ya hii gharama isiwe chini ya TSH 100 kwa kila muamala.
Maana yake ni kuwa, kama idadi ya vipande unavyotaka kuuza asilimia moja yake
ni chini ya TSH 100,utakatwa TSH 100. Mfano, kama una vipande 200 ambavyo
unataka kuuza kwa bei ya TSH 700/= ina maana jumla ya mauzo ni TSH 140,000/=
sasa hapa utakatwa 1% ambayo ni TSH 1400/=.

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Mfuko huu hauna muda wa zuio, maana yake unaruhusiwa kuuza au kunununua
siku yoyote ya kazi.

KUUZA VIPANDE
Unaruhusiwa kuuza vipande vyako siku yoyote ya kazi (isipokuwa siku za
mahesabu au siku ambayo UTT AMIS imetangaza kuwa mauzo hayatakuwepo) na
pesa yako utaipata ndani ya siku 10 za kazi. Kitu kingine ni kuwa, unaweza kuuza
vipande vyako nusu yake au vipande vyote ulivyonavyo, mfano kama una vipande
1000 unaweza kuuza vipande 100 na vipande vingine vikabaki au ukauza vipande
vyote 1000 au idadi yoyote unayoitaka.
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI
Mfuko huu hauna ukomo wa muda wala ukomo wa kiasi ambacho unaweza
kuwekeza. Maana yake ni kuwa unaweza kuwekeza mara nyingi uwezavyo na
kwa muda wote, kama tulivyoona kiasi cha chini cha kuwekeza ni vipande 10 ila
unaweza kuwa unaongeza kadri uwezavyo hakuna ukomo wa kiasi cha kuwekeza
kwenye mfuko huu.

HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI YA MFUKO WA UMOJA

Jedwali Na. 1: Historia ya mrejesho wa uwekezaji (ROI) wa mfuko wa Umoja mpaka Septemba 30, 2021

KUHAMISHA VIPANDE AU KUVITUMIA KAMA DHAMANA


Vipande vya mfuko wa umoja vinaweza kuhamishwa kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mtu mwingine na pia vipande vinaweza kutumika kama dhamana
pindi unapotaka kuomba mkopo katika taasisi ya fedha.
WEKEZA MAISHA

UTANGULIZI
Huu mfuko ulianzishwa mwaka 2007. Mfuko huu una mpango wa kuwekeza kwa
miaka 10 yaani baada ya miaka 10 uwekezaji wako unakuwa umefika kikomo na
unaweza kuchukua fedha yako yote lakini baada ya miaka 5 unaweza pia
kuchukua fedha yako hadi asilimia 75 ya hela uliyowekeza. Wakati mfuko
unaanzishwa bei ya kipande ilikuwa TSH 100.

`Mfuko huu una tabia zifuatazo:-

1) Uwekezaji
2) Bima (insurance)

BIMA

Kwa upande wa bima kuna vitu viwili, bima ya maisha (kifo au ulemavu wa
kudumu) na ajali binafsi (personal accident). UTT AMIS wanatoa bima hizi kwa
wawekezaji iwapo kifo, ulemavu au ajali binafsi itatokea kwa mwekezaji. UTT
AMIS wanatumia kampuni inayotoa huduma za bima inayoitwa Alliance
Insurance Corporation Limited.

Kwa kuwa uwekezaji kwenye mfuko huu ni wa miaka kumi (10) mpaka kuiva,
tangu mfuko huu uanzishwe mnamo mwaka 2007, uwekezaji wa kwanza uliiva
(kufika kikomo) mnamo mwaka 2017. Katika mfuko huu, mara baada ya
uwekezaji kuiva, mwekezaji anaweza kufanya lolote kati ya mambo haya
yafuatayo:-

1) Kuchukua fedha yako yote ukafanye mambo mengine;


2) Kufungua akaunti nyingine na kuanza uwekezaji upya kwa miaka 10
mingine; au
3) Kuwekeza katika mfuko mwingine wa UTT AMIS.

MPANGO WA UCHANGIAJI
Mfuko huu una mpango wa uchangiaji ambapo, mwekezaji anaainisha kiasi cha
fedha anachokuwa anachangia kwenye mfuko kwa miaka yote kumi (10).
Uainishaji wa kiwango cha uwekezaji unafanywa mwanzoni mwa
uwekezaji/wakati wa kufungua akaunti kwenye mfuko. Mfano, kama umepanga
kuwekeza TSH I milioni au kiwango chochote kile katika miaka yote kumi ndio
kiasi ambacho ninakizungumzia. Kiasi hiki mwekezaji anaweza kuamua
kukiwekeza chote kwa mara moja au akawekeza kiasi hiki kidogo kidogo ili mradi
mwisho wa miaka 10 hiki kiasi ambacho mwekezaji ameainisha kitimie. Kwenye
mfuko huu unaweza kuchagua kiasi chochote kile cha uwekezaji ila ni kwamba
kiasi hicho kisipungue TSH 1 milioni. Kiasi kinachowekezwa mara baada ya
shilingi milioni 1 kiwe katika ongezeko la Tsh 1000 na sio chini yake.

Angalizo

Baada ya kuanisha kiasi ambacho utawekeza kwa miaka yote 10 hauwezi


kukibadili aidha kupunguza au kuongeza ila unaweza kufungua akaunti nyingine
kwa jina lako na ukaanisha kiasi kingine, mfano kama umesema uwekezaji wako
utakuwa wa TSH 10 milioni kwa miaka yote kumi basi hauwezi kubadili tena ama
kuongeza au kupunguza.
MPANGO WA KUPATA FAIDA
Mfumo wa uwekezaji katika mfuko huu ni wa kukuza mtaji, mfuko wa wekeza
maisha hautoi gawio bali mwekezaji anapata faida pale ambapo kipande
alichonunua kinapanda thamani.

ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Katika mfuko huu mtu ambaye anaweza kuwekeza ni mtanzania (Resident
Individual Tanzanians) au mtanzania asiye mkazi (non resident individual
Tanzanians) mwenye umri wa miaka 18 mpaka 55.

JINSI YA KUWEKEZA KATIKA MFUKO HUU


Uwekezaji katika mfuko huu una ukomo wa muda ambao ni miaka 10, ina maana
baada ya miaka 10 uwekezaji wako unakuwa umeiva. Sasa uwekezaji hapa una
mipango miwili ambayo ni

1) Uwekezaji wa mara kwa mara; au


2) Uwekezaji wa mara moja

1) UWEKEZAJI WA MARA KWA MARA (REGULAR


CONTRIBUTION)

Hapa mwekezaji anachagua kiasi ambacho anataka kuwekeza katika miaka yote
10 na baada ya hapo unachagua kuwa utakuwa unachangia kila mwezi au kila
baada ya miezi sita au utakuwa unachangia kila mwaka mara moja, na baada ya
kujua muda ambao utakuwa unachangia unaangalia kiasi gani ambacho unatakiwa
uwe unachangia kwa muda ambao umeuchagua.

Tanbihi: Hakuna ukomo wa kiasi ambacho unaweza kuwekeza


Mfano

Tuangalie kama ukitaka kuwekeza TSH 1 milioni ndani ya miaka kumi katika
mpango wa kuchangia kila mwezi, miezi sita au mwaka inakuwaje, angalia jedwali
hapo chini.

Kiasi cha mpango Changia kila mwezi Kila baada ya miezi 6 Changia kila mwaka
1 milioni 8340 50,000/= 100,000/=

2 milioni 16670/= 100,000/= 200,000/=

3 milioni 25000/= 150,000/= 300,000/=

25 milioni 208,340 /= 1,250,000 /= 2,500,000 /=

100 milioni 833,340 /= 5,000,000/= 10,000,000/=

500 milioni 4,166,670 /= 25,000,000 /= 50,000,000 /=

1 bilioni 8,333,340/= 50,000,000 /= 100,000,000 /=

Maelezo ya Jendwali

Unapochagua kiasi ambacho unataka kuwekeza katika miaka 10 ya uwekezaji


wako na ukachagua utakuwa unachagia kila mwezi, miezi sita au mwaka hivyo
ndivyo inavyokuwa katika uchangiaji wako.

Mfano, kama umeamua kuwa katika uwekezaji wako unataka kuwekeza TSH 1
milioni (ndani ya miaka 10) basi kama utachagua mpango wa kuchangia kila
mwezi itakubidi kuchangia TSH 8340/= na kama utachagua kuchangia kila baada
ya miezi sita ina maana utakuwa unachangia TSH 50,000/= na kama utachagua
kuwa utakuwa unachangia kila mwaka basi itakubidi kuchangia TSH 100,000/=
kila mwaka kwa miaka 10, kusudi hapa ni kuwa baada ya miaka 10 kufika uwe
umechangia kiasi cha TSH 1 milioni kama ulivyoainisha katika mpango wako. Na
kama utachagua kiasi chochote kile basi mahesabu yatakuwa hivyo.
Mfano wa 2

Chakulia unataka kuwekeza TSH 1.5 milioni katika mpango wako wa miaka 10
(ina maana ndani ya miaka 10 uwe umechangia TSH 1.5 milioni) sasa kama
utachangia kila mwezi ina maana ndani ya miaka 10 kuna miezi 120, sasa
unachukua hii TSH 1.5 milioni unagawanya kwa miezi 120 kujua utakuwa
unachangia kiasi gani kila mwezi

1.5 milioni /120 = 12,500/=

Kwa hiyo itakubidi kuchangia 12,500/= kila mwezi ili kutimiza kiasi ambacho
unatakiwa kuchangia

Kama ukichagua kuchangia kila baada ya miezi sita

Kama utaamua kuchangia kila baada ya miezi sita ina maana katika miaka 10, kuna
jumla ya vipindi 20 vya miezi sita, hivyo itakuwa TSH 1.5 milioni kugawanya kwa
20 ambayo ni sawa TSH 75,000/= kila baada ya miezi sita.

Kama ukichagua kuchangia kwa mwaka mara moja

Hapa unachukua kiasi ambacho unataka kuwekeza kwa miaka yote kugawanya
kwa 10, ambayo ni TSH 1.5 milioni kugawanya kwa 10 ambayo ni sawa na TSH
150000/= kama utachagua kuwekeza mara moja kwa mwaka itakubidi uwekeze
kiasi hicho.
2) UCHANGIAJI WA MARA MOJA

Hapa muwekezaji anaweza kuchagua kuwekeza kiasi ambacho anataka kuwekeza


katika muda wote wa miaka 10 kwa mara moja kama pesa anayo. Mfano, kama
unataka kuwekeza TSH milioni 1 kwa kipindi cha miaka 10 na unaweza kuilipa
yote kwa mara moja basi unaweza kulipa au kama unataka kuwekeza TSH 10
milioni au kiasi chochote na unacho basi unaweza kuwekeza kwa mara moja.
Kumbuka kama umeainisha kuwa uwekezaji wako kwa miaka 10 utakuwa mfano
TSH 1 milioni na ukailipa yote kwa pamoja basi hautaruhusiwa kuongeza kiasi
kingine tena katika mpango huo labda kama utafungua mpango mwingine lakini
unaruhusiwa kuchagua kiasi chochote kile katika mpango wako.

NAMNA YA KUCHANGIA KWA MCHANGIAJI ALIYECHAGUA


MPANGO WA KULIPA MARA KWA MARA

Kuna namna tatu ambazo zinamuwezesha muwekezaji kuchangia katika mifuko


hii:-

1) Kuchangia moja kwa moja

Hapa muwekezaji analipa mwenyewe kiasi cha fedha ambacho anatakiwa kulipa
kutokana na mpango wa uchangiaji wake aliochagua. Mfano, kama umechagua
kuchangia kila mwezi basi unaweza kuwa kila mwezi unapeleka hela wewe
mwenyewe UTT AMIS au kupitia mawakala wake.

2) Uchangiaji kupitia benki ya muwekezaji

Hapa muwekezaji anaweza kuelekeza kuwa pesa itoke benki kwenda UTT AMIS,
na benki itafanya kama alivyoelekeza muwekezaji, Kwa hiyo, badala ya
muwekezaji kuwa anapeleka pesa UTT AMIS, basi benki yake inakuwa inafanya
hivyo kwa niaba yake.

3) Uchangiaji wa moja kwa moja kutoka kwa mwajiri

Kwa wale walioajiriwa, mwajiri anaweza kuwa anatumiwa kulipa moja kwa moja
fedha kwenda UTT AMIS.

Tanbihi: Muwekezaji atatakiwa kulipa pesa yake ya kuchangia ndani ya siku


kumi za kazi baada ya kuwa tarehe ambayo anatakiwa kulipa imefika ila pia
muwekezaji anaweza kulipa changio lake kabla ya muda wa kutoa changio lake
haujafika kama atataka kufanya hivyo.

KIASI CHA FEDHA YA KUWEKEZA


Kima cha chini ambacho muwekezaji anatakiwa kuwekeza katika mfuko huu ni
TSH 1 milioni kwa kipindi chote cha uwekezaji wake. Muwekezaji anaweza
kuchagua kama atawekeza hii milioni 1 kwa pamoja au atawekeza kila mwezi, au
kila baada ya miezi sita au mwaka mara mmoja, ni uhuru wa muwekezaji kuona
kipi kinamfaaa.

HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO


Mfuko huu una asilimia kadhaa umewekeza katika hisa na asilimia nyingine
katika mapato ya kuaminika kwa hiyo una hatari za uwekezaji za wastani. Kama
unavyoona katika jedwali hapo chini mpaka juni 2021 wekeza maisha ilikuwa na
25.7% ya mali imewekezwa katika hisa. Ifahamike kwamba mifuko ambayo
inawekeza katika hisa na mapato ya kuaminika asilimia ngapi iende kwenye hisa
na ngapi kwenye mapato mengine huwa inategemea na jinsi meneja wa mfuko
anavyoona ni sahihi, kwa hiyo asilimia hizi zinaweza kubadilika.
Mchoro Na. 2: Historia ya uwekezaji wa mfuko wa wekeza maisha mpaka kufikia June 30,
2021

GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gaharama zozote ambazo
unakatwa, hivyo kipande kinauzwa kwa bei ya soko kwa siku ambayo
muwekezaji ananunua kipande hicho.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Ukitaka kuuza vipande utakatwa kiasi cha 2% ya vipande ambavyo unataka
kuuza, hii gharama ya kuuza itakuwa kwa yule ambaye anataka kuuza vipande
baada ya muda wa zuio kuwa umeisha (baada ya zuio la miaka 5 unaruhusiwa
kuuza mpaka asilimia 75 ya mfuko wako. Maana yake ni kuwa, kiasi cha asilimia
25 lazima kibaki katika mfuko) ila kwa mtu atakaye subiri uwekezaji wake uive
yaani baada ya miaka 10 kuisha hatakatwa kiasi chochote kile. Malipo ya fedha
kwa vipande vilivyouzwa yanafanyika ndani ya siku kumi za kazi.

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Mfuko huu una muda wa zuio la muwekezaji kuuza vipande vyake. Mfuko una
zuio la muda wa miaka 10 uwekezaji kutouzwa na muwekezaji. Maana yake ni
kuwa, kama unawekeza pesa leo hauwezi kuichukua mpaka baada ya miaka 10.
Aidha, mfuko unatoa fursa ya muwekezaji kuuza mpaka asilimia 75 ya uwekezaji
wake baada ya miaka 5 ya uwekezaji. Hivyo, ikiwa unataka kufanya uwekezaji
wako kwa miaka mitano tu, huu mfuko hautakufaa. Muda wa zuio uliowekwa
kwenye mfuko huu ni moja ya sababu ya kuweka kikomo cha umri wa miaka 55,
maana kama utawekeza ukiwa na umri wa miaka 60 ina maana hautapata fedha
uliyowekeza mpaka ukiwa na umri wa miaka 70.

UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI


Kama tulivyoona katika utangulizi kuwa kuna ukomo wa muda wa kuwekeza
kwenye mfuko huu ambao ni miaka kumi. Aidha, mfuko huu hauna ukomo wa
kiasi cha fedha kinachoweza kuwekezwa, muwekezaji anaweza kuwekeza kwa
kiasi kikubwa atakacho ila kuna ukomo wa faida za bima ambazo unaweza
kupokea ambapo kiwango cha mwisho cha fidia za bima kinachoweza kutolewa
ni TSH 25 milioni.

HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA WEKEZA

Jedwali Na. 2: Historia ya rejesho la uwekezaji (ROI) ya mfuko hadi kufikia Septemba, 30, 2021

FAIDA YA BIMA YA MFUKO WA WEKEZA MAISHA


Kama tulivyoona awali kuwa mfuko huu unatoa bima kwa wawekezaji ukiachana
tu na faida zinazotokana na uwekezaji kwenye mfuko. Bima zinazotolewa na
mfuko huu ni ya maisha na ajali binafsi.
(i) BIMA YA MAISHA

Bima ya maisha inayotolewa na mfuko huu inahusisha kifo au ulemavu wa


kudumu kwa muwekezaji. Katika bima hii, ikiwa muwekezaji atafariki au kupata
ulemavu wa kudumu mfuko utatoa fidia kwake kwa kutegemea na mpango wa
uchangiaji aliouchagua.

a) Bima katika mpango wa kuwekeza mara kwa mara (regular contribution)

Kama muwekezaji amefariki au amepata ulemavu wa kudumu basi fidia


atakayopata ni sawa na kiasi ambacho bado hajachangia katika mpango wake.
Maana yake ni kuwa kama katika mpango wa muwekezaji ameainisha kuwa
atachangia milioni 10, basi kiasi ambacho muwekezaji atapewa kama fidia ni kiasi
ambacho bado muwekezaji hajachangia katika mpango wake. Mfano, kama
amechangia TSH 2 milioni na akapata tatizo basi fidia itakuwa TSH 8 milioni na
kuendelea kama ilivyo katika jedwali chini.

Mwaka wa tukio Kiasi ulichochangia Bima/kiasi ambacho bado kuchangia


1 1 milioni Hakuna (A*)
2 2 milioni 8 milioni
3 3 milioni 7 milioni
4 4 milioni 6 milioni
5 5 milioni 5 milioni
6 6 milioni 4 milioni
7 7 milioni 3 milioni
8 8 milioni 2 milioni
9 9 milioni 1 milioni
10 10 milioni Hakuna (*B)
A* Katika mwaka wa kwanza hakuna malipo kwa ulemavu wa kudumu au kifo kwa miezi 12 ya kwanza isipokuwa
pale ambapo kifo kimetokea kwa ajari hapa fidia itakuwa TSH 9 milioni;

B* Katika mwaka wa kumi pia hakuna malipo kama mpango wa uwekezaji ni wa mwaka ila kama ulikuwa na
mpango wa mwezi na kuna kiasi ambacho bado hakijalipwa basi hicho kiasi ndio kitakuwa kama fidia.
Tanbihi: Katika mpango huu wa kuwekeza mara kwa mara fidia ya bima ni kiasi
kile ambacho hakijalipwa katika mpango wako uliochagua ila kiasi cha bima
hakitazidi milioni 25. Hapa ina maana kuwa, kama mpango wako ni milioni 100 na
ukapata ulemavu wa kudumu au kufariki mwaka wa pili wa uchangiaji, basi bima
inayotakiwa kulipwa ni TSH 80 milioni, lakini kwa kuwa kiwango cha juu cha
bima ni TSH 25 milioni basi utapewa TSH 25 milioni kama fidia.

b) Bima katika mpango wa uwekezaji wa mara moja

Hapa muwekezaji atapata fidia sawa na kiasi alichowekeza katika mpango wake
ila kiasi cha juu ni TSH 25 milioni ina maana kama muwekezaji ameweka 10
milioni basi atalipwa 10 milioni kama fidia kwa miaka yote 10 ya uwekezaji wake
ila kama amewekeza kiasi zaidi ya 25 milioni basi fidia yake itakuwa milioni 25 tu.

Jedwali hapo chini linaonesha mfano wa bima inayolipwa kwa muwekezaji wa


mara moja aliyewekeza TSH 10 Milioni kwenye mfuko huu

Mwaka wa tukio Bima (fidia)


1 Hakuna (A*)
2 10 milioni
3 10 milioni
4 10 milioni
5 10 milioni
6 10 milioni
7 10 milioni
8 10 milioni
9 10 milioni
10 10 milioni

A* hapa muwekezaji kama atapata ulemavu wa kudumu au kifo hakuna fidia itakayotoka isipokuwa kifo au
ulemavu umesababishwa na ajari ambapo fidia itakuwa milioni 10.
Jedwali hapo chini linaonesha mfano wa bima inayolipwa kwa muwekezaji wa
mara moja aliyewekeza kiasi kinachozidi TSH 25 Milioni kwenye mfuko huu

Mwaka wa tukio Bima (fidia)


1 Hakuna (A*)
2 25 milioni
3 25 milioni
4 25 milioni
5 25 milioni
6 25 milioni
7 25 milioni
8 25 milioni
9 25milioni
10 25 milioni

Tanbihi: Katika mpango wa kuwekeza kwa mara moja (single contribution) fidia
ya bima inakuwa sawa na kiasi ambacho muwekezaji amechangia isipokuwa kwa
kiasi cha uwekezaji kilicho juu ya TSH 25milioni fidia itakayolipwa kwa
muwekezaji ni shilingi 25 Milioni.

(ii) BIMA YA AJARI BINAFSI

Hii inawahusu wawekezaji ambao ni wakazi wa Tanzania na inatolewa mpaka


kiasi cha 20% ya jumla ya pesa uliyoainisha katika mpango wako bila kujali una
mpango wa kuwekeza mara kwa mara au mpango wa kuwekeza mara moja. Kiasi
cha juu kabisa cha malipo ya bima hii kwa muwekezaji aliyeathiriwa na ajali ni
TSH 5 milioni.

Kuna bima ya msiba ila hii kutokana na maelezo ya kitabu cha ofa cha wekeza
maisha ni kwa ajili ya wawekezaji ambao walinunua vipande kwa mara ya kwanza
kabisa wakati mfuko unaanzishwa.
Hitimisho kuhusu Bima

Tukio Bima ya maisha Bima ya ajari binafsi mazishi


Kifo Ndiyo Ndiyo Ndiyo
Ulemavu wa kudumu kwa magonjwa au ajali Ndiyo Hapana A* Hapana
Kupoteza miguu au milango ya fahamu Hapana Ndiyo Hapana
A* hapa kwa kuwa bima ya maisha ni kubwa kuliko ya ajali, basi mdai atapewa fidia ya bima ya maisha na sio ya
ajali.

Maelezo zaidi kuhusu bima zinazotolewa na mfuko huu unaweza kuyapata


kupitia kusoma kitabu cha ofa cha wekeza maisha ukurasa wa 33 mpaka 37.

KUHAMISHA VIPANDE AU KUTUMIA KAMA DHAMANA


Kwa sababu vipande vya mfuko huu vimeunganishwa na bima haviwezi
kuhamishika au kutumiwa kama dhamana pale ambapo unataka mkopo.

KUSITISHWA UANACHAMA KATIKA MPANGO WA UWEKEZAJI


Kuna sababu 4 ambazo zinaweza kusababisha kusitishwa kwa mpango wa
uwekezaji wa muwekezaji aliyewekeza kwenye mfuko huu:-

a) Muda wako wa uwekezaji wako kuisha (baada ya kutimiza miaka 10)


b) Kifo au ulemavu wa kudumu wa mwanachama
c) Kama uanachama umesitishwa kwa sababu mwanachama ameshindwa
kutimiza uchangiaji wake katika uchangiaji wa mara kwa mara
d) Kama mwanachama amepoteza sifa za kuwa mwanachama kama kutoa
taarifa zisizo sahihi, kupoteza uraia nk.

Kama uanachama utasitishwa kwa sababu iliyoainishwa kwenye kipengele (a)


basi mwanachama atalipwa faida zote za kuwekeza; kama sababu ni (b),
mwanachama atalipwa bima na fidia nyingine; kama sababu ni (c), mwanachana
atalipwa pesa yake kulingana na thamani ya vipande kwa bei iliyopo sokoni na
kama vipande vitauzwa kipindi ya zuio basi muwekezaji atakatwa kiasi cha
gharama za uendeshaji kisichopungua 2% ya thamani ya vipande vyake.

KUSITISHWA UANACHAMA KWA SABABU YA KUTOCHANGIA


Uanachama utasitishwa pale ambapo mwanachama atashindwa kuchangia kiasi
anachotakiwa kuchangia. Ikiwa tarehe ya kuchangia inapofika, kwa mpango wa
kuwekeza kila mwezi na mwanachama asichangie kama inavyotarajiwa, basi
mfuko utasitisha uanachama endapo mwanachama hatachangia katika kipindi cha
miezi sita tangu tarehe aliyopaswa kuchangia. Ikiwa mwanachama atakuwa
kwenye mfumo wa uchangiaji wa miezi sita, uanachama utasitishwa endapo
atashindwa kuchangia kwa awamu mbili mfululizo na akiwa katika mfumo wa
uchangiaji wa mwaka mmoja, mwananchama ataondolewa uanachama wake
akishindwa kuchangia kwa mwaka mmoja.

KUFUFUA UANACHAMA
Mwanachama anaweza kufufua uanachama wake ndani ya mwaka mmoja toka
siku ambayo alishindwa kulipa kama atalipa michango yote iliyopita tangu
alipoishia. Mwanachama anaweza kutumia nafasi ya kufufua uanachama mara
mbili tu ndani ya kipindi chote cha uwekezaji wake kwenye mfuko. Hii
inamaanisha kuwa ndani ya miaka kumi (10) ya uwekezaji, mwekezaji anazo
nafasi mbili tu za kufufua uwekezaji wake ikiwa atashindwa kuweka mchango
wake kwa wakati.
MFUKO WA WATOTO

UTANGULIZI
Mfuko huu ulianzishwa mwaka oktoba mwaka 2008. Mfuko huu unalenga
kumsaidia mtoto wa kitanzania katika masomo yake. Bei ya kipande wakati
mfuko unaanzishwa ilikuwa TSH 100/=. mfuko huu ni wa wazi (open ended).

MPANGO WA KUPATA FAIDA


Mfuko huu pia hautoi gawio bali mpango wake wa kupata faida kwa muwekezaji
ni wa kukuza mtaji ninacho maanisha ni kuwa unapata faida pale ambapo
unanunua vipande kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu.

NAMNA FAIDA INAVYOWEZA KUMFIKIA MTOTO


Kuna namna mbili za jinsi ambavyo mtoto anaweza kupokea faida yake kutoka
katika mfuko huu

(i) Namna ya ufadhili wa kimasomo (scholarship)

Katika mpango huu, mtoto husika atalipiwa pesa mara mbili au mara moja kwa
mwaka kwa njia ya ufadhili wa masomo. Malipo hayo yanalipwa kwa awamu moja
au mbili kulingana na mwongozo wa wazazi au walezi wa mtoto husika. Malipo
haya yanafanywa baada ya mtoto kufikisha umri wa miaka 12. Katika mpango huu
mzazi au mlezi wa mtoto atakuwa na uhuru wa kuchagua kati ya vipindi vitatu
ambavyo mtoto atahitaji kulipiwa huu ufadhili wa kimasomo. Vipindi vitatu ni
wakati mtoto akiwa na miaka 12-18, 19-24, 12-24.

Kwenye skimu hii mzazi au mlezi anaweza kuchagua muda gani atahitaji ufadhili
huu uanze kulipwa kwa mtoto. Mfano, kama unajua kutoka miaka 12 mpaka 18
unaweza kuwa na uwezo wa kumlipia mwanao ada, ila ukahitaji kuwa akifikisha
miaka 19 ndio aanze kulipiwa basi UTT AMIS itafanya hivyo au kama utahitaji
kwa miaka yote yaani kuanzia miaka 12 mpaka 24 mtoto awe analipiwa basi UTT
AMIS itafanya hivyo.

Ili kupata fedha za kulipia mtoto ufadhili wa masomo, UTT AMIS wanauza
vipande ambavyo mwekezaji amewekeza. Hivyo, uchaguzi wa mpango wa
uchangiaji uliofanywa utaathiri kiasi na idadi ya muda wa ulipaji wa ada ya mtoto
husika.

Utofauti wa vipindi vya ufadhili Idadi ya vipindi pamoja na idadi ya ulipaji wa ufadhili
12-18 19-24 12-24
Ufadhili mara mbili kwa mwaka 14 12 26
Ufadhili mara moja kwa mwaka 7 6 13
Jedwali Na. 3: Jedwali linaonesha idadi ya vipindi na idadi ya ulipaji wa ufadhili

Jedwali hapo juu linaonesha namna ufadili unavyofanywa kwa vipindi tofauti
tofauti. Mathalani, kama umechagua kuwa kipindi cha ufadhili wa mwanao kiwe
pale anapotimiza miaka 12 mpaka 24 ina maana kama utachagua awe analipiwa
mara mbili kwa mwaka basi kutakuwa na vipindi 26 vya malipo na kama
utachagua kuwa awe analipiwa mara moja kwa mwaka basi kutakuwa na vipindi
13 vya malipo.

Mfano
Tuchukulie una mtoto ambaye umewekeza vipande 24,000 na ukachagua kipindi
chake cha kulipiwa ufadhili wa masomo kiwe kati ya miaka 19 mpaka 24, hapa ina
maana kuwa kwa mpango wa kulipiwa mara moja kwa mwaka atalipiwa mara 6
na kwa mpango wa kulipiwa mara mbili kwa mwaka atalipiwa mara 12.

Ufadhili wa kimasomo kwa mwaka mara mbili

Kwa kutumia idadi ya vipande vilivyoainishwa kwenye mfano hapo juu (24,000),
kwa hiyo 24,000 kugawanya kwa 12 ni sawa na 2000. Hivyo, kwa miaka yote, kila
baada ya miezi sita vipande 2000 vitakuwa vinauzwa ili mtoto aweze kulipiwa
ufadhili wa masomo.

Ufadhili wa kimasomo mara moja kwa mwaka

Hapa ukichukua vipande 24,000 kugawanya kwa miaka sita ina maana vipande
4000 vitakuwa vinauzwa kila mwaka ili kulipa ufadhili wa mara moja kwa
mwaka.

Kumbuka: Bei ya vipande inapanda na kushuka ila kanuni ya ukokotoaji wa


malipo ya udhamini ni kama ulivyoainishwa hapo juu. Aidha, malipo ya udhamini
yanategemea mpango wa uchangiaji uliochaguliwa na muwekezaji. Mathalani,
kama muwekezaji atachagua mpango wa kumlipia mtoto anapofikisha umri wa
miaka 12 mpaka 24 basi idadi ya vipande vitakavyouzwa itakuwa tofauti.

Aidha, katika mfuko huu, kiwango cha chini cha udhamini wa masomo ni TSH
20000/=. Hii inamaana kuwa, kama muwekezaji atachagua mpango wa udhamini
wa masomo kwa mwaka mara 2 basi kiwango cha chini ambacho kinatakiwa
kulipwa kwa kila udhamini ni 20000/= chini ya hapo utahamishiwa kwenye
mpango wa kukuza mtaji.

(ii) Mpango wa ukuaji

Hapa mtoto hatalipiwa kitu chochote na mfuko ila atapata faida kwa ukuaji wa
kipande.

ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Anayepata faida katika kuwekeza katika mfuko huu ni mtoto wa kitanzania
mkazi au asiye mkazi mwenye umri chini ya miaka 18. Mzazi au mlezi anawekeza
kwa niaba ya mtoto ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18. Mtoto anaweza
kuwekezewa pesa na wazazi wake au walezi au taasisi yoyote ya kiserikali au
isiyo ya kiserikali. Ili kuondoa mashaka yoyote, lazima utambulisho wa mtoto
ambaye ni mnufaika wa uwekezaji huu uwekwe wazi na mtu anayetuma maombi
ya kufungua akaunti kwa ajili ya mtoto.

KIASI CHA FEDHA CHA KUWEKEZA

Kiasi cha chini cha kuwekeza katika mfuko huu ni TSH 10,000/= na uwekezaji wa
nyongeza ni TSH 5,000/=. Tunapozungumzia uwekezaji wa nyongeza maana yake
ni kama unataka kuongeza kuwekeza baada ya kuwekeza kwa mara ya kwanza,
kima cha chini cha kuongeza ni TSH 5000/= ila hakuna ukomo wa kiasi ambacho
unaweza kuongeza kuwekeza.

HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO


Kama nilivyo eleza awali katika eneo la hatari za uwekezaji wa mifuko ni kuwa
mifuko iliyowekeza katika hisa na katika mapato ya kuaminika ina hatari za
uwekezaji za wastani. Mfuko wa watoto umewekeza katika hisa na vyanzo
vingine hivyo hatari zake za uwekezaji ni za wastani. Jedwali hapo chini
linaonesha hali ya uwekezaji wa mfuko mpaka kufikia Juni 2021. Mpaka kufikia
mwezi Juni, 2021, mfuko ulikuwa na asilimia 28.3% ya mali zake katika uwekezaji
wa hisa wakati 68.8% ya uwekezaji wa mfuko huu uko kwenye hati fungani za
serikali. Hati fungani ni moja ya eneo lililo salama sana katika uwekezaji hivyo
kufanya mfuko huu kuwa na uwekezaji mkubwa katika sehemu salama zaidi.
Mchoro Na. 3: Mchoro unaoesha mgawanyo wa uwekezaji ulofanywa na mfuko wa watoto hadi
kufikia Juni 30, 2021

GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gharama zozote ambazo
unakatwa. Unauziwa kipande kwa bei ambayo iko sokoni. Kama unataka kuuza
vipande basi kiwango cha chini ambacho kinatakiwa kubaki katika akaunti yako
ni vipande 10 kama utafanya mauzo na kiwango ambacho kinaonekana kitabaki ni
chini ya vipande kumi basi uwekezaji wako wote utauzwa na akaunti itafungwa.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Kama muwekezaji atahitaji kuuza uwekezaji wake ndani ya kipindi cha miaka
mitatu (3) tangu alipowekeza, anakatwa asilimia moja (1%) ya bei ya kipande
lakini baada ya miaka 3 hautakatwa chochote. Hapa pia kuna unafuu wa watoto
wenye ulemavu au watoto ambao ni yatima, kwa makundi haya mawili hakuna
makato ya aina yoyote pale ambapo wanataka kuuza vipande vyao. Ili watoto
watoto kupata faida hii lazima vitambulisho vinavyothibitisha hali za hawa
watoto vitolewe. Kiwango cha chini cha gharama ya kuuza kinatakiwa kuwa 500/=
hapa ina maana kuwa kama utataka kuuza vipande na jumla ya gharama ya mauzo
(1%) ni chini ya 500/= basi itakatwa 500/= ambayo ni kima cha chini.

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Huu mfuko pia una muda wa zuio wa mpaka mtoto atakapofikisha miaka 12.
Mfano, kama ukianza kumuwekezea mtoto akiwa na umri wa mwaka mmoja basi
hautaruhusiwa kutoa hela mpaka afikishe miaka 12 ila kama kuna sababu za
lazima au mtoto akiwa mgonjwa anahitaji matibabu unaruhusiwa kutoa hela
yako hata kama mtoto hajafikisha umri wa miaka 12. Baada ya mtoto kutimiza
miaka 12 unaruhusiwa kuuza vipande vyako vyote au baadhi.

UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI


Hapa uwekezaji una kikomo pale ambapo mtoto atafikisha umri wa miaka 24 basi
ndio uwekezaji wake utakuwa umefikia kikomo kama kuna pesa imebaki katika
mfuko wake atapatiwa au anaweza kuwekeza katika amfuko mwingine. Pia
hakuna kikomo cha pesa ambayo unaweza kuwekeza katika mfuko huu.

Baada ya kuwa uwekezaji umefikia kikomo hapa ina maana mtoto ametimiza
miaka 24 basi anaweza kufanya yafuatayo kwa pesa iliyopo katika akauti yake:-

(i) Kuchukua pesa yake yote kwa kuuza vipande

Hapa baada ya mtoto kufikisha miaka 24 ambapo uwekezaji wake unakuwa


umekomaa mtoto anaweza kuamua kuchukua pesa yake kwa kuuza vipande na
hapa hakuna makato ambayo atakatwa (exit load) pale anapouza vipande vyake.

(ii) Kuwekeza kwa niaba ya mtoto mwingine

Mtoto ambaye uwekezaji wake umekomaa anaweza kuamua kuwekeza pesa yake
kwa mtoto mwingine ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18 na huyu ambaye
uwekezaje wake umekomaa anaweza kuwa kama mlezi wa huyu mtoto mwingine.
(iii) Kuhamia mfuko mwingine

Kama amekidhi vigezo huyu mtoto ambaye sasa uwekezaji wake umekomaa
anaweza kuhamia mfuko mwingine wowote wa UTT AMIS kama amekidhi vigezo
vya mfuko anaohamia.

Ikiwa atashindwa kufanya maamuzi ndani ya miezi mitatu baada ya uwekezaji


wake kukomaa basi atahamishwa moja kwa moja kwenye mfuko wa kwanza wa
UTT AMIS (mfuko wa umoja).

HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA WATOTO

Jedwali Na. 4: Linaonesha mrejesho wa uwekezaji (ROI) wa mfuko wa watoto mpaka kufikia Septemba, 30
2021

VIPANDE VINAWEZA KUTUMIKA KAMA DHAMANA


Vipande vya mfuko huu vinaweza kutumika kama dhamana pale ambapo
unahitajika mkopo ila huu mkopo uwe ni kwa faida ya mtoto husika.

KUHAMA MFUKO
Unaruhusiwa kuhama kutoka mfuko huu kwenda katika mfuko mwingine endapo
umekidhi vigezo vya mfuko unaohamia. Uhamaji huu unafanyika bila gharama
yoyote. Lakini unapohama kutoka mfuko huu na kwenda katika mfuko mwingine
basi unapoteza haki na faida zote ambazo zinaendana na mfuko wa huu.
MFUKO WA JIKIMU
Mfuko huu ulianzishwa mwaka 2008 na mfuko huu unalenga kumuwezesha
mtanzania kupata faida ya mara kwa mara, mfuko huu unalipa gawio kwa
wawekezaji wake. Mfuko wa jikimu uko wazi kama ilivyo mifuko mingine. Mfuko
wa jikimu wakati unaanzishwa mwaka 2008, bei ya kipande katika mfuko huu
ilikuwa ni TSH 100/=. Mpango wa uwekezaji wa mfuko huu ni 0-100% kwenye
mapato ya kuaminika kama hati fungani, na 0- 35% katika hisa. Mpango huu
unaweza kubadilika pale ambapo meneja anaona ni sahihi kwa ajili ya manufaa ya
wawekezaji.

MPANGO WA KUPATA FAIDA


Mfuko huu una mipango miwili ya kupata faida

(i) Kutoa gawio


ii. Mpango wa ukuaji wa mtaji (annual reinvestment plan)

Katika mpango wa gawio kuna mipango miwili pia

(a) Gawio kila baada ya miezi 3


(b) Gawio kila mwaka

Maana yake ni kuwa katika faida ambayo inapatikana kuna baadhi itaenda kwa
wawekezaji kama gawio na kiasi kingine kitabaki kwa ajili ya kukuza mtaji maana
kuna watu wanadhani kuwa kama akichukua gawio basi hakuna faida nyingine
zaidi ya hiyo.

ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Mfuko huu uko wazi kuwekeza kwa wawekezaji wote binafsi au taasisi na watoto
pia.
KIASI CHA CHINI CHA KUWEKEZA
Kiasi cha chini cha kuwekeza katika mfuko huu kinategemea na mpango
uliouchagua kwa mpango wa gawio kwa miezi mitatu kiwango cha chini cha
kuwekeza ni TSH 2 milioni. katika mpango wa gawio la mwaka kiwango cha chini
cha kuwekeza ni TSH 1 milioni na baada ya hapo kwa mipango ya gawio unaweza
kuwa unawekeza kuanzia 15,000/= kama nyongeza ila haina ukomo, kwa mpango
wa kuwekezewa gawio (annual reinvestment) kiwango cha chini cha kuanza
kuwekeza ni TSH elfu tano(5000/= )na baada ya hapo unaweza kuwa unaongeza
sh 5000/= kama nyongeza

HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO


Mfuko huu una hatari za uwekezaji za wastani kwani sehemu ya mali yake
imewekezwa katika hisa, kama inavyoonyesha katika mchoro hapo chini ambapo
mpaka kufikia Juni, 30 mwaka 2021, mfuko huu ulikuwa na uwekezaji kwenye
hisa kwa kiwango cha asilimia 26.1% ya mfuko.

Mchoro Na. 4: Mgawanyo wa uwekezaji katika mfuko wa Jikimu mpaka


kufikia June 30, 2021
GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gharama zozote ambazo
unakatwa, unauziwa kipande kwa bei ambayo iko sokoni.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Kama utahitaji kutoa hela yako ambayo umeiweka ndani ya mwaka mmoja basi
utakatwa 2% ya bei ya kipande maana yake ni kuwa kama umewekeza Januari na
ukauza kabla ya Disemba 31 ya mwaka huo huo.

Kama utauza baada ya mwaka mmoja lakini kabla ya mwaka wa pili kuisha
utakatwa 1.5% ya bei ya kipande maana yake kama utauza ndani ya mwaka wa
pili.

Kama utauza baada ya mwaka wa pili ila kabla ya mwaka wa 3 kuisha utakatwa
1% lakini baada ya miaka 3 hautakatwa chochote. Kiwango cha chini ambacho
kitakatwa kama gharama ya kuuza ni TSH 500/=

MIAKA MAKATO
1 2%
2 1.5%
3 1%
Baada ya miak 3 Hakuna makato

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Mfuko huu hauna muda wa zuio.

UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI


Katika mfuko huu hakuna ukomo wa muda wa kuwekeza wala kikomo cha kiasi
cha juu ambacho unaweza kuwekeza unaweza kuwekeza mara nyingi uwezavyo
na kwa kiasi kikubwa uwezavyo. Aidha, muwekezaji anaweza kuhama kutoka
mfuko huu kwenda mfuko mwingine kama amekidhi vigezo vya mfuko
anaohamia.

HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA JIKIMU

Jedwali Na. 5: Historia ya mrejesho wa uwekezaji (ROI) ya mfuko wa jikimu hadi kufikia Septemba, 30, 2021

Vipande vya mfuko huu vinaweza kutumika kama dhamana pale ambapo unataka
kuomba mkopo katika taasisi ya kifedha.

MPANGO WA GAWIO KATIKA MFUKO WA JIKIMU


Hapo awali tumezungumizia kuwa moja kati ya faida ambayo unaipata katika
mfuko huu ni gawio, sasa gawio linakuwa katika mipango yote mitatu ila kuna
utofauti kidogo tutaona hapo chini. Lengo la UTT AMIS ni kutoa gawio katika
mfuko huu ila kutokana na hali ya kiuchumi na utendaji wa mfuko gawio linaweza
kuwa kidogo au lisilipwe mara kwa mara kutokana na utendaji wa mfuko huu.

(i) GAWIO KILA BAADA YA MIEZI 3


Watu ambao wako katika mpango wa gawio kila miezi mitatu na watakaosajiriwa
katika siku ya usajili ndio tu watakaopewa gawio mkononi yaani pesa keshi.

Kalenda ya ugawaji gawio katika mpango huu

Kila siku ya mwisho ya mwezi wa tatu wa mpango huu ambayo ni siku ya kazi
ndio siku ambayo ina rekodiwa watu ambao wanastahili kupata gawio. Hii
inamaanisha kuwa katika mwaka kuna vipindi vine vya miezi 3, sasa siku ya
mwisho ya kazi ya mwezi Machi, Juni, Septemba na mwezi Disemba ndio siku ya
kurekodi watu ambao wanastahili kupata gawio. Baada ya kurekodi ndani ya siku
kumi za kazi baada ya siku hii ya kurekodi ndio gawio linatoka. Maana yake ni
kuwa kwa kipindi cha Januari mpaka Machi siku ya kurekodi ni siku ya mwisho
ya kazi ya mwezi Machi na baada ya hii siku gawio linatoka ndani ya siku kumi za
kazi.

Kwa kipindi cha mwezi Aprili mpaka Juni siku ya kurekodi ni siku ya mwisho ya
kazi ya mwezi juni na baada ya kurekodi watu wanaostahili kupata gawio. Gawio
linatoka ndani ya siku kumi za kazi.

Kwa kipindi cha mwezi Juni hadi September tarehe ya mwisho ya kurekodi ni
tarehe ya mwisho ya kazi ya mwezi Septemba na baada ya hii tarehe gawio
linatoka ndani ya siku kumi za kazi, hivyo hivyo kwa kipindi cha mwisho
ambacho ni Oktoba mpaka Disemba.

(ii) GAWIO KWA MWAKA MARA MOJA


Mwaka wa UTT AMIS huwa unaisha Juni 30, kwa hiyo kwa wenye mpango wa
gawio kila mwaka siku yao ya kurekodi ni juni 30 na gawio linalipwa ndani ya
siku kumi za kazi ila kuna utofauti kidogo hapa.

JINSI GAWIO LA MWAKA LINAVYOKUWA

Wawekezaji walio katika mpango wa gawio kwa mwaka hawatapokea gawio kwa
vipindi vitatu vya miezi mitatu kama walio katika gawio baada ya miezi mitatu ila
gawio litakalokuwa linatoka katika kipindi litatumika kuwanunulia wawekezaji
vipande kwa bei iliyopo sokoni na baada ya vipindi vyote vinne kuisha hivi
vipande vilivyonunuliwa vitakatwa (cancleled) na pesa itakayopatikana ndio
itakayotumika kuwapa gawio hawa wawekezaji wa gawio kwa mwaka mara moja.
MPANGO WA KUWEKEZEWA GAWIO(ANNUAL REINVESTMENT)

Hapa katika mpango huu wawekezaji hawatapokea gawio kwa kipindi cha miezi
yote 12 ila gawio ambalo litakuwa linatoka litatumika kuwanunulia wawekezaji
vipande tena.

Kama ilivyo katika mfuko wa hati fungani kuwa sio kwamba ukiweka TSH 2
milioni basi utawekwa katika mpango wa gawio moja kwa moja hapana bali
unaweza kuweka TSH 2 milioni au zaidi ila ukachagua mpango wa kuwekezewa
gawio ni uchaguzi wako.

Pia unaruhusiwa kubadili mpango kutoka katika mpango wa gawio kwenda


katika mpango wa kuwekezewa gawio au kutoka katika mpango wa kuwekezewa
gawio kwenda katika mpango wa gawio bila gharama yoyote.
MFUKO WA UKWASI

UTANGULIZI
Mfuko huu wa ukwasi (liquid fund) ulianzishwa 2013 ukiwa na malengo makuu
matatu ambayo ni:-

(i) Kulinda mtaji wako;


(ii) Kutoa ukwasi (liquidity); na
(iii) Kutoa mrejesho shindani kulinganisha na maeneo mengine ambayo
unaweza kuweka hela kwa muda mfupi
Mfuko huu unampa muwekezaji uwezo wa kuweka hela zake kwa muda mfupi au
mrefu. Mfano, kama muwekezaji amepata fedha ya ghafla au ambayo bado hana
malengo nayo kwa wakati huo. Muwekezaji anaweza kuiweka kwenye mfuko
huu wakati anafikiri nini cha kufanya na fedha yake ikawa inapata faida ya
ongezeko la kiasi cha pesa yake wakati hakatwi makato ya aina yoyote.

Kuna maeneo mengi mtu anaweza kuweka fedha yake kwa muda mfupi ila kipindi
anapoitoa kuna uwezekano wa fedha hiyo kupungua kutokana na makato Fulani
Fulani lakini mfuko wa ukwasi unaweza kukupa msaada sana hapa kwani utatuza
fedha zako pasipo kupungua kwa fedha yako wakati wa kuichukua. Mathalani,
unaweza kuwa mkulima wa msimu (unategemea mvua) baada ya kuvuna na
kuuza mazao pesa yako ya mtaji ambayo utatumia kwa ajiri ya kilimo mwaka ujao
unaweza kuiweka katika mfuko huu wakati unasubiri msimu hapa utapata faida
ya ongezeko la mtaji bila kupoteza chochote.

Mfuko huu ni wa wazi kama mifuko mingine na wakati unaanzishwa bei ya


kipande ilikuwa 100/=, mpaka kufikia juni 2021 mfuko ulikuwa na thamani ya
215.9 bilioni
MPANGO WA KUPATA FAIDA
Mfuko huu uko kati ya ile mifuko minne isiyotoa gawio na mpango wa kupata
faida katika mfuko huu ni wa KUKUZA MTAJI (CAPITAL GAIN), yaani ukuaji
wa thamani ya kipande. Mfano, umenunua kipande TSH 200/= ukauza kwa bei ya
juu ndio jinsi unavyopata faida.

ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Mfuko huu uko wazi kuwekeza kwa wawekezaji binafsi na wawekezaji wasio
binafsi, maana yake mtu wa kawaida au kampuni inaweza kuwekeza katika
mfuko huu. Mtu, kikundi, kampuni au taasisi yoyote inaruhusiwa kuwekeza
katika mfuko huu. Mfuko huu unaruhusu hata watoto kuwekeza, hivyo ndugu
muwekezaji kama una mtoto au mdogo wako badala ya kuwa unamnunulia Pipi
na vitu vya hulka hiyo, unaweza kuamua kumfundisha kuwekeza kupitia mfuko
huu.

KIASI CHA CHINI CHA KUANZA KUWEKEZA


kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza katika mfuko huu ni laki moja
(100,000/=) na uwekezaji wa nyongeza ni wa kuanzia TSH 10,000/= na kuendelea,
hakuna kikomo cha kuwekeza unaweza kuwekeza mara nyingi uwezavyo na kwa
kiasi ulicho nacho ili mradi kisipungue 10000/= kwa kila uwekezaji.

HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO


Mfuko huu haujawekeza katika hisa hivyo katika orodha yetu huu ndio mfuko wa
kwanza kuwa na hatari za uwekezaji za chini kuliko mifuko mingine iliyo chini ya
UTT AMIS. Kama inavyoonyesha katika mchoro hapo chini, inaonesha 94.2% ya
uwekezaji wa mfuko huu umefanywa kwenye hati fungani za serikali na kiasi
kilichobakia (5.8%) imewekwa kwenye akaunti maalum inayo uwezesha mfuko
kufanya manunuzi ya vipande kutoka kwa watu ambao wanauza vipande vyao.
Mchoro Na. 5: Mgawanyo wa uwekezaji uliofanywa na mfuko wa ukwasi mpaka kuishia Juni, 30 mwaka 2021

GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gharama zozote ambazo
unakatwa, unauziwa kipande kwa bei ambayo iko sokoni.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Katika mfuko huu, hakuna makato ya aina yoyote unapotaka kuuza vipande
vyako. Mfuko huu ni moja ya mifuko inayopendwa sana na wawekezaji
wanaowekeza ndani ya UTT AMIS, hii inatokana na kutokuwa na gharama zozote
pale ambapo unataka kuuza kipande.

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Mfuko huu hauna muda wa zuio.

UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI


Katika mfuko huu hakuna ukomo wa muda wa kuwekeza wala kikomo cha kiasi
cha juu ambacho unaweza kuwekeza unaweza kuwekeza mara nyingi uwezavyo
na kwa kiasi kingi uwezavyo.
HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA UKWASI

Jedwali Na. 6: Hali ya mrejesho wa uwekezaji uliofanywa na mfuko wa ukwasi mpaka kufikia Septemba, 30
mwaka 2021

Unaweza kuhama mfuko wa ukwasi kuelekea mfuko wa hati fungani na sio


mifuko mingine iliyobakia.
MFUKO WA HATI FUNGANI (BOND FUND)

UTANGULIZI
Ulishawahi kutamani kuwekeza kwenye hati fungani ila hauna TSH 1 milioni ya
kuwekeza kwani kima cha chini cha kuwekeza kwenye hati fungani za muda
mrefu za serikali ni shilingi milioni moja?. Ikiwa ndiyo, basi UTT AMIS ipo kwa
ajili yako. UTT AMIS wameanzisha mfuko wa uwekezaji wa hati fungani (Bond
fund). Mfuko huu umeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kukusanya mitaji kutoka
kwa wawekezaji wengi wadogo kwa wakubwa na kuziwekeza kwenye hati
fungani za serikali. Mfuko huu unaruhusu muwekezaji kuwekeza kwa kiwango
cha kuanzia shilingi 50000/= na kuendelea. Huu ndiyo mfuko mchanga kuliko
mifuko yote iliyo chini ya UTT AMIS kwani mfuko huu umeanzishwa mwaka
2019. Wakati mfuko unaanzishwa bei ya kipande ilikuwa TSH 100/=, ukubwa wa
mfuko mpaka kufikia Juni 2021 ilikuwa ni TSH 94 bilioni.

SERA YA UWEKEZAJI KATIKA MFUKO


Sera ya kuwekeza ya mfuko huu ni kuwa asilimia 90 itawekezwa katika hati
fungani za serikali na hati fungani za makampuni binafsi zenye muda tofauti wa
kuiva (maturity), na asilimia 10 itawekezwa kwenye mali zenye ukwasi (liquid
assests) kwa ajili ya kufanya mfuko uwe na uwezo wa kununua vipande kutoka
kwa wawekezaji wanaotaka kuuza.

MPANGO WA KUPATA FAIDA


Mfuko huu una mipango miwili ya kupata faida mpango wa gawio na mpango wa
kukuza mtaji. Yaani ukiwekeza katika mfuko huu unakuwa unapata faida kupitia
gawio na kuongezeka kwa thamani ya kipande (capital gain). Mfano kwa mwaka
2021 mfuko wa hati fungani ulitoa TSH 12 kama gawio kwa kila kipande na kwa
mwaka huo huo kutoka Juni 30 2020 mpaka Juni 30 2021 bei ya kipande ilikua
kutoka TSH 104.4/= mpaka TSH 109.7/=. Kwa hiyo utaona kuwa kama ulikuwa
umewekeza katika mfuko huu sio tu ulipokea gawio bali pia ulipata faida kwa
ongezeko la mtaji.

1) Mpango wa gawio
2) Mpango wa kukua kwa mtaji
MPANGO WA UWEKEZAJI
Mfuko unatoa fursa za kuwekeza katika mipango mitatu

1) Mpango wa gawio kila mwezi;


2) Mpango wa gawio kila baada ya miezi sita; na
3) Mpango wa kuwekezewa gawio tena (re investment)

Mpango wa kuwekezewa gawio hapa ina maana utapokea gawio kama mipango
mingine ya gawio ila gawio lako hautalipokea bali litaenda kuwekezwa kwa
kukununulia vipande kwa bei iliyopo. Mfano, kama gawio kwa kila kipande ni
TSH 12 na wewe una vipande 1000 ina maana utapokea gawio la 12000/= hii pesa
hautapewa mkononi bali itaenda kukununulia vipande tena.

MPANGO WA GAWIO
Mpango wa gawio umegawanyika mara mbili

a) Gawio kila mwezi


b) Gawio kila baada ya miezi 6

GAWIO
Katika mipango yote mitatu, muwekezaji anapokea gawio ila utofauti ni kuwa
gawio ambalo anapokea mtu aliyewekeza katika mpango wa kuwekezewa gawio
hapewi mkononi bali gawio lake linatumika kumnunulia vipande kwa bei
iliyopo,wakati hiyo mipango miwili iliyobaki gawio wanapewa.

Gawio kila baada ya miezi sita maana yake kila baada ya miezi sita utapokea
gawio na mtu wa gawio kila mwezi atapokea gawio kila mwezi.

Gawio kwa mwaka 2020, 2021 lilikuwa ni TSH 12 kwa kila kipande. Ieleweke
kuwa gawio linaweza kupungua au kuongezea kutegemea na utendaji wa mfuko
kwa mwaka husika. Katika mipango yote hiyo muwekezaji anaweza kuuza baadhi
au vipande vyake vyote.

ANAYESTAHILI KUWEKEZA
Mfuko huu uko wazi kuwekeza kwa wawekezaji binafsi na wawekezaji wasio
binafsi, maana yake mtu wa kawaida au kampuni au taasisi au kikundi cha watu
wote wanaweza kuwekeza katika mfuko huu.

KIASI CHA CHINI CHA KUANZA KUWEKEZA


Kiasi cha chini cha kuanza kuwekeza kinategemea na mpango ambao muwekezaji
ameuchagua. Muwekezaji ambaye anataka kupokea gawio kila mwezi kiwango
cha chini cha uwekezaji ni kuanzia ni TSH 10milioni na wale wanaotaka gawio
kila baada ya miezi 6 kiwango cha chini ni TSH 5milioni. Aidha kuna wanataka
kuwa katika mpango wa kuwekezewa gawio, hawa wanawekeza kuanzia shilingi
50,000/= na uwekezaji wa nyongeza katika mipango yote ni sh 5000/= hiki ni
kiwango cha chini kuanzia ila hakuna ukomo unaweza kuwekeza kadri
uwezavyo. Hapa haimaanishi kuwa ukiwekeza TSH 10 milioni basi utakuwa
unapokea gawio moja kwa moja hapana, unaweza kuamua kuwekeza TSH 10
milioni au zaidi ila ukachagua mpango wa kukuza mtaji. Muwekezaji pia
anaweza kuwekeza katika mipango yote mitatu kama atapenda kufanya hivyo.

Ikitokea katika kuuza vipande vyako, thamani ya uwekezaji wako ikawa


imeshuka chini ya kiwango cha chini cha mpango ulipo sasa, basi utahamishwa na
kupelekwa katika mpango wa kuwekezewa gawio, mfano kiwango cha chini
kuwekeza ili kupokea gawio kila mwezi ni TSH 10 milioni, sasa ikitokea ukauza
vipande vyako na mfuko wako ukabakiwa na TSH 900000/= basi utahamishwa
mpango na kupelekwa mpango wa kuwekezewa gawio.
HATARI ZA UWEKEZAJI ZA MFUKO
Mfuko huu pia haujawekeza katika hisa hivyo hatari zake za uwekezaji ni za
chini. Moja ya sharti muhimu katika mfuko huu ni kutokuwa na kiasi cha fedha
kinachowekezwa kwenye hisa. Jedwali hapo chini linaonyesha hali ya uwekezaji
wa mfuko kwenye vyanzo vyake vya mapato.

Mchoro Na. 6: Hali ya uwekezaji kwenye mfuko wa hati fungani ulio chini ya UTT AMIS mpaka Juni, 30, 2021

GHARAMA YA UNUNUZI
Unavyonunua kipande katika mfuko huu hakuna gharama zozote ambazo
unakatwa, unauziwa kipande kwa bei ambayo iko sokoni.

GHARAMA YA KUUZA KIPANDE (EXIT LOAD)


Hapa hakuna makato ya aina yoyote unapotaka kuuza vipande vyako.Na mauzo
yatafanyiwa kazi ndani ya siku 10 za kazi.

MUDA WA ZUIO (LOCK IN PERIOD)


Mfuko huu una zuio la miezi 3, kwa mpango wa gawio kila mwezi ina maana ili
uanze kupata gawio basi itakubidi ukae katika uwekezaji wako kwa miezi 3
ukiwa na kiwango kinachostahili kupewa gawio. Hapa ina maana kama umejiunga
na mfuko mwezi wa kumi basi ni baada ya miezi mitatu ndio utastahili kulipwa
gawio, na miezi 3 inaisha Disemba na baada ya hapo utastahili kulipwa gawio la
mwezi wa kwanza ambalo litalipwa ndani ya siku 10 za kazi za mwezi Februari.
UKOMO WA UWEKEZAJI NA NYONGEZA YA UWEKEZAJI
Katika mfuko huu hakuna ukomo wa muda wa kuwekeza wala kikomo cha kiasi
cha juu ambacho unaweza kuwekeza. Muwekezaji anaweza kuwekeza mara
nyingi awezavyo na kwa kiasi kikubwa kwa kadri awezavyo.

HISTORIA YA MREJESHO WA UWEKEZAJI WA MFUKO WA HATI


FUNGANI

Jedwali Na. 7: Mrejesho wa uwekezaji kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa mfuko huu

UNAFUU WA KODI
Katika mipango yote kiwango ambacho unapokea kama gawio hakina makato ya
kodi ya mapato katika mikono ya muwekezaji. Tunafahamu kuwa unapopokea
gawio kutoka katika kampuni ambayo iko soko la hisa unakatwa 5% kama kodi ya
zuio lakini gawio unalopokea kutoka katika mfuko huu halina makato ya aina
yoyote ya kodi.

Aidha, muwekezaji anaweza kuhama mfuko huu kuelekea mfuko wa ukwasi(na


sio vinginevyo) yaani hauwezi kuhama kutoka mfuko huu kuelekea mfuko wa
umoja au mifuko iliyobaki.
Ukurasa umeachwa wazi
SEHEMU YA TATU

JINSI YA KUTENGENEZA GAWIO LAKO


Kama nilivyoeleza katika sehemu ya pili kuwa kuna mifuko miwili ambayo inalipa
gawio, ambayo ni mfuko wa jikimu na mfuko wa hati fungani. Sasa ukichunguza
kwa makini utaona kuwa gawio ambalo linatoka katika hii mifuko lina masharti
ya kima cha chini ili upate gawio;- mfano ili upate gawio kila mwezi kwa mfuko
wa hati fungani ni lazima uwe na kima cha chini cha uwekezaji cha TSH 10 milioni
na kama unataka gawio kila baada ya miezi sita basi inabidi uwe umewekeza kiasi
cha TSH 5 milioni, aidha mfuko wa jikimu una mpango wa gawio kwa mwaka na
mpango wa gawio kwa miezi 3, ila ili muwekezaji apate gawio kila baada ya miezi
3 basi ni lazima awe amewekeza milioni 2 na ili upate gawio kila mwaka lazima
awe amewekeza shilingi milioni 1.

Sasa mpaka hapo nadhani umeshaona kuna changamoto mbili

1) UTT AMIS ina mifuko sita ila ni mifuko miwili tu ndio inayolipa gawio; na
2) Sio watu wengi nchini wanaweza kuwa na fedha ya kuwekeza shilingi
milioni 1 au zaidi ili waweze kupata gawio la kila mwezi.

Ila usijali kwa sababu nahodha wako nipo nitakupa njia ya kutengeneza gawio
lako hata kama hela yako ni kidogo. Ujue gawio ambalo wanatoa UTT AMIS
halina maajabu kabisa (vijana wa mtaani wanasema) kama wewe ni muwekezaji
mwenye nidhamu na unayetunza kumbukumbu zako za uwekezaji unaweza
kutengeneza gawio lako bila wasiwasi. Ngoja nikuoneshe namna ya kufanya hilo;
SABABU ZA KUTAKA GAWIO KUTOKA MIFUKO YA UTT
Kuna sababu nyingi za kwa nini wewe kama muwekezaji unaweza kuhitaji gawio
kutoka katika mfuko mwingine tofauti na mifuko ambayo UTT AMIS imepanga
kuwa ndiyo inayotoa gawio:

(i) Masharti mazuri katika baadhi ya mifuko

Mimi napenda sana mfuko wa ukwasi kwa sababu ya masharti yake kuliko mfuko
wa hati fungani na kwa kuwa mifuko hii ina uwekezaji wa aina moja maana yake
ni kwamba imewekeza katika mapato ya kufanana ila changamoto inaweza kuwa
mfuko wa ukwasi hauna gawio kama ilivyo mfuko wa hati fungani. Muwekezaji
anaweza kuamua kutengeneza gawio lake mwenyewe kwenye mfuko wa ukwasi
kama ambavyo inalipwa kwenye mfuko wa hati fungani.

Kitu kingine angalia mfuko wa jikimu unaolipa gawio ni mfuko ambao


umewekeza katika hisa na katika mapato ya kuaminika kama ulivyo mfuko wa
umoja ila mfuko wa umoja una masharti nafuu kama mtu anataka kuuza vipande
vyake. Mfano, kama unataka kuuza vipande katika mfuko wa umoja utakatwa 1%
ya thamani ya vipande unavyotaka kuuza ila kama unataka kuuza vipande katika
mfuko wa jikimu utakatwa 2% kama unauza ndani ya mwaka mmoja ulionunulia
na utakatwa 1.5% kama utauza baada ya mwaka mmoja ila kabla ya miaka 2 na
kuendelea kwa hiyo ninaweza kuwa ninapenda mfuko wa umoja kuliko jikimu ila
tatizo ni kuwa mfuko wa umoja haulipi gawio kwa hiyo nikaamua kujitengenezea
gawio la kwangu.

(ii) Mfuko kuwa na mrejesho mzuri

Sio kwa sababu mfuko unatoa gawio basi mrejesho wake wa uwekezaji utakuwa
mkubwa hapana, kuna mifuko ambayo haitoi gawio ila ina mrejesho wa uwekezaji
mkubwa kuliko mifuko ambayo inatoa gawio. Hivyo, muwekezaji anaweza
kuchagua mfuko ambao hauna gawio ila una mrejesho mkubwa na akatengeneza
gawio lake kwenye mfuko husika.

(iii) Kima cha chini cha uwekezaji kwa baadhi ya vyanzo kuwa
kikubwa

Unaweza kuwa huna millioni 10 ya kuwekeza katika mfuko wa hati fungani ila
unataka gawio kutokana na uwekezaji wako, unaweza kuwekeza kiasi cha fedha
ulicho nacho katika mfuko wa ukwasi kwani unafanana sana na mfuko wa hati
fungani na ukatengneza gawio lako mwenyewe.

JINSI YA KUTENGENEZA GAWIO LAKO KWENYE MFUKO WAKO


Kwanza nianze kwa kusema kwa mifuko ambayo ina zuio la muda inaweza kuwa
ngumu kutengeneza gawio lako mwenyewe ndani ya muda ule wa zuio, baada ya
hayo tuangalie jinsi ya kutengeneza gawio. Gawio unaweza kulitengeneza kwa
njia nyingi kutegemea na mfuko ambao umewekeza ila hapa nitazungumzia
namna mbili tu.

(i) Gawio kwa mwezi


Hapa unaweza kuamua mwenyewe gawio lako uwe unachukua lini na kwa namna
gani na inakuwa vizuri unapotumia mfuko kama wa ukwasi kwani katika mfuko
huu unapouza vipande haukatwi chochote. Sasa hapa unachofanya ni rahisi sana,
mfano tunajua kihistoria mfuko wa ukwasi una mrejesho wa kati ya asilimia 12-
15% kwa mwaka huwa inabadilika mwaka kwa mwaka ila kwa kila kipindi
inaweza kushuka au kupanda zaidi. Kwa wastani huwa inakuwa hapo, kwa hiyo
kila mwezi unauza vipande ambavyo ni sawa na asilimia 1 ya uwekezaji wako
kwenye mfuko husika.
Mfano, Jedwali hapo juu linaonesha mrejesho wa uwekezaji wa mfuko wa ukwasi
kama ilivyo kwenye ripoti ya fedha ya mfuko huo kwa mwaka 2021. Kupitia
jedwali hilo unaona kuwa tangu mfuko umeanzishwa 2013 una mrejesho wa
wastani wa 13.5% kwa mwaka. Sasa, tuchukulie una pesa ambayo haitoshi
kuwekeza kwenye mfuko wa hati fungani kwa hiyo unaamua kuwekeza katika
mfuko wa ukwasi kwa gawio la asilimia moja kila mwezi. Ikiwa mfuko huu
unakua kwa asilimia 1.125% (nimechukua wastani 13.5 gawanya kwa miezi 12 ya
mwaka) basi hesabu au mbinu yetu tunaiwasilisha kwa mfano huu hapa chini.

Mfano:

UWEKEZAJI KWA MWAKA WA 1

Wekeza 500,000 mwaka wa 1

Miezi Ukuaji Gawio baki


1 505625 5056.25 568.75
2 505625 5056.25 568.75
3 505625 5056.25 568.75
4 505625 5056.25 568.75
5 505625 5056.25 568.75
6 505625 5056.25 568.75
7 505625 5056.25 568.75
8 505625 5056.25 568.75
9 505625 5056.25 568.75
10 505625 5056.25 568.75
11 505625 5056.25 568.75
12 505625 5056.25 568.75
jumla 60675 6825
Kwa hiyo kinachotokea ni kuwa ijapokuwa umekuwa ukiuza vipande vyenye
thamani ya asilimia 1% ya mfuko wako kila mwezi fedha yako uliyowekeza
inabaki pale pale na kama mfuko utaendela kupata mrejesho kama huu ina maana
utatoa pesa kila mwaka na hautaathiri mtaji wako.

Mtaji wako utakuwa unakuwa japokuwa kwa kasi ndogo ila utakuwa unapata
gawio kila mwezi kwa mwaka mzima bila shida na kama tulivyo ona baada ya
kuchukua gawio bado utabakiwa na kiasi cha mtaji wa 6825/= ambacho hiki
kitaenda kuongezeka mwenye mtaji na kufanya mtaji wako kukua na kuwa
506825/=. Hii ina maana mwaka unaofuata utakuwa na gawio kubwa kwani mtaji
wako sasa umekua kiasi.

Kwa maelezo mafupi ni kwamba, ikiwa ukuaji wa mfuko wako kwa mwaka ni
13.5% ina maana kila mwezi mfuko wako unakuwa kwa asilimia 1.125% sasa
ukiamua kuchukua 1% kama gawio kila mwezi, na hii unaipata kupitia kuuza
vipande vyenye thamani ya 1% ya mfuko wako kila mwezi kitakachotokea ni kuwa
utakuwa umechukua faida na mtaji unabaki pale pale na kunakuwa na ongezeko
kidogo la mtaji kwa mwaka. Na hapa unaweza kuamua kuuza asilimia yoyote ile
ya faida kwa muda unaotaka, mtu mwingine anaweza kuamua kuuza asilimia 6
kila baada ya miezi sita au akaamua kuuza asimilia 3 kila baada ya miezi 3.
Kikubwa ni kuwa unauza vipande vyako kulingana na kiasi ambacho unataka
kiwe kama gawio.

Mwaka ambao mfuko utakuwa na mrejesho mkubwa unaweza kuongeza gawio


ule mwezi wa mwisho au ukaamua kuacha ili lile ongezeko liende kwenye mtaji na
mwaka unaofuata uwe na gawio kubwa. Sasa hili gawio unaweza kuamua
kuliwekeza katika uwekezaji mwingine mfano pesa unayoipata kila mwezi kama
gawio ukaamua kuwa unanunua hisa kutoka soko la hisa na mitaji la Dar es
Salaam na masoko mengine duniani. Suala unalokuwa unalifanya ni uwekezaji
mseto ambao kimsingi una faida nyingi kwa muwekezaji ikiwa kutatokea
mitikisiko kwenye uchumi na/au maeneo tuliyowekeza.

MWAKA WA 2

(Tunachukulia mfuko unakua kwa 13.5% kwa mwaka)

Kumbuka hapa mtaji wetu umekua na sasa ni 506,825/=

Sasa huu mwaka wa pili unaweza kuamua kuchukua 2% kama gawio, hapa
utabaki na mtaji wako wa kwanza kabisa na faida kidogo au ukaamua kuchukua
1% ya mtaji wa pili wa 506,825/=

MIEZI MTAJI GAWIO BAKI


1 512526.8. 5125.3 576.5
2 512526.8. 5125.3 576.5
3 512526.8. 5125.3 576.5
4 512526.8. 5125.3 576.5
5 512526.8. 5125.3 576.5
6 512526.8. 5125.3 576.5
7 512526.8. 5125.3 576.5
8 512526.8. 5125.3 576.5
9 512526.8. 5125.3 576.5
10 512526.8. 5125.3 576.5
11 512526.8. 5125.3 576.5
512526.8 5125.3 576.5
Jumla 61503.6 6918

Kwa mwaka unaona gawio limeongezeka na kama ungeamua kuchukua gawio


la 2% ya fedha yako ya mwanzoni pia ingekuwa vizuri, sasa kanuni ya
kampaundi imeshaanza kufanya kazi hapa gawio lako litaendelea kukua na
pia mtaji wako utaendelea kuongezeka ijapokuwa kwa kasi ndogo.
GAWIO KWA MWAKA KULINGANA NA UTENDAJI WA KAMPUNI
Hii ya pili pia inapendeza sana, ngoja nikuoneshe kwa ufupi gawio kwa mwaka
kulingana na utendaji wa kampuni linakuwaje?. Mathalani, nimewekeza katika
hisa na huwa zinatoa gawio mara baada ya kampuni kupata faida kwa mwaka
husika. Sehemu ya faida ya kampuni ndiyo inayoelekezwa kwenda kwa
muwekezaji kama gawio. Hivyo, gawio hili huwa linatokana na utendaji wa
kampuni maana ikiwa imetengeneza hasara haiwezi kutoa gawio au faida ikiwa
ndogo basi gawio linaweza kuwa dogo au kutokuwepo kabisa. Aidha, katika
utoaji wa gawio, baadhi ya kampuni zinaamua kutoa asilimia kadhaa mfano 30%
ya faida baada ya kodi na nyingine mpaka 100%.

Sasa kwa UTT AMIS hasa kwa mifuko ambayo imewekeza katika hisa na baada ya
mwaka kuisha huwa wanafanya ukokotoaji wa faida ambayo kampuni
imetengeneza kwa mwaka huo na baada ya kufanya hivyo, muwekezaji ndiyo
anachagua gawio lake liwe kiasi gani kwa mwaka.

Mfano, mfuko wa umoja kwa mwaka 2021 umekuwa kwa 16.9% sasa wewe
unaweza kuamua uchukue asilimia ngapi kama gawio, unaweza kuamua
kuchukua 6%,9%,10%,12% au 16% kutegemea na mapenzi yako

Sasa unachofanya ni kuuza vipande vinavyolingana na asilimia unayotaka


kuchukua. Kama ulinunua kipande kimoja mwanzoni mwa mwaka kwa bei ya
200/= na baada ya ripoti ya mwisho mwaka kutoka ikaonyesha kuwa mfuko wa
umoja umekua kwa asilimia 16.9% ina maana kipande chako sasa kina thamani ya
233.8. Faida hapa ni 33.8 kwa hiyo unaweza kuchukua gawio la 6% kati ya 16.9%
maana yake unauza asilimia 6 ya faida wako ambayo ni 14.028 na iliyobaki
unaiacha kama mtaji, kwa maneno mengine kati ya hii 33.8/= ambayo ni faida
unachukua TSH 14.O28/=.
Mimi nadhani mpango wa kujitengenezea gawio ni bora kuliko mipango ambayo
imetolewa na UTT AMIS, kwani mpango wa kujitengenezea gawio unakupa
uwezo wa kuchukua gawio hata kama una pesa kidogo na unaweza kuchagua
mfuko uupendao wewe na gawio kwa muda uupendao.

Mfano halisi

Tuchukue mfano nina vipande 2000 vya umoja nimenunua mwanzoni mwa
mwaka kwa bei ya shilingi 100/= ina maana mfuko wangu una thamani ya
200,000/= na mwisho wa mwaka mfuko wa umoja umekuwa kwa asilimia 20% ina
maana thamani ya mfuko wangu imekuwa kwa 40,000/= sasa kama nitaamua
kuchukua gawio la 10% ambayo ni sawa 20,000/= ina maana nitauza vipande 166.6
kutoka katika mfuko wangu na mfuko wangu utapungua na kubaki na thamani ya
220,000/=.

JINSI YA KUTUMIA KIKOKOTOZI (CALCULATOR) ILIYO KATIKA


TOVUTI YA UTT AMIS

Ukiachana na bei ya kipande, kikokotozi kilichopo kwenye tovuti ya UTT AMIS


ndio kitu cha pili kwa umuhimu katika tovuti ya UTT AMIS kwa maoni yangu,
kwani kikokotozi ni muhimu sana katika kumuwezesha muwekezaji katika hatua
za kupanga namna ambavyo atafikia malengo yake ya kifedha.

Kama unavyofahamu uwekezaji wowote ule ambao hauna mipango, huna tija na
nikupoteza muda na pia utashindwa kutumia fursa iliyoko mbele yako.

Katika kipengele hiki nitakufundisha jinsi gani unaweza kutumia kikokotozi hiki
ili kikusaidie katika kupanga uwekezaji wako na hata kukuonyesha ni kiasi gani
unategemea kukipata. Kwa hiyo hii ni moja kati ya kitu muhimu sana na katika
kipengele kinachofuata tutaanza kuangalia namna ambavyo unaweza kutumia
kikokotozi kupanga uwekezaji wako.

Tuanze na jinsi hiki kikokotozi kilivyo, muonekano wake ni kama jinsi unavyoona
hapo chini na kama unavyoona baada ya maneno INVESTMENT ASSUMPTION
CALCULATOR kuna viboksi 4 ambavyo vinaelezea mipango minne ambayo
unaweza kuichagua ambayo ni

1) Kikokotozi cha uwekezaji wa mwezi (monthly investment calculator)


2) Mpango wa kuwekeza kila mwezi ( monthly investment plan)
3) Kikokotozi cha uwekezaji wa mara moja (single sum investment
calculator)
4) Mpango wa uwekezaji wa mara moja (single sum investment plan)

Sasa nitaelezea mpango mmoja mmoja hapo juu kwa kina katika maelezo
yafuatayo:-

Unapobonyeza mojawapo ya kiboksi basi kikokotozi cha mpango husika


kinafunguka na unaweza kuanza mahesabu mara moja

Kumbuka

Kama wewe ni muwekezaji basi kikokotozi hiki ni muhimu sana kwako sio tu
kwa kupiga mahesabu ya uwekezaji wa UTT AMIS bali hata katika
uwekezaji mwingine ila kitu cha kukumbuka ni kuwa mahesabu ya
kikokotozi hiki ni ya RIBA YA KAMPAUNDI NA SIO RIBA RAHISI.
KIKOKOTOZI CHA UWEKEZAJI WA MWEZI (MONTHLY INVESTMENT
CALCULATOR)
Ukibonyeza kiboksi cha kwanza basi kikokotozi cha uwekezaji wa mwezi
kitafunguka na muonekano wake ni kama unavyoona hapo chini.

MATUMIZI YA HIKI KIKOKOTOZI


Hiki kikokotozi kinakuwezesha kupiga mahesabu mfano kama utakuwa
unawekeza kila mwezi kiasi fulani na katika mfuko wenye mrejesho wa asilimia
kadhaa baada ya miaka kadhaa utakuwa na kiasi gani? Hii inakusaidia kujua ni
kiasi gani unaweza kupata kama unakuwa umewekeza kwa mfumo huu. Kama
unavyoona kuna viboksi viko wazi na kuna maaelezo pia juu ya viboksi vilivyo
wazi tuangalie maana yake
(i) Monthly investment (TZS)

Hiki ni kiasi cha pesa ambacho utakuwa unawekeza kila mwezi, mfano kama
unataka uwe unawekeza 50,000/= kila mwezi basi hapa ndio utaiandika hii namba

(ii) Expected annual return (matarajio ya mrejesho wa uwekezaji)

Hapa unaandika kiasi ambacho unatarajia kupata kama mrejesho wa uwekezaji


katika miaka yote ya uwekezaji wako. Mfano kama matarajio yako ni kuwa mfuko
utakuwa unakuingizia 14% kwa mwaka basi hii namba utaiandika hapa.

(iii) Period (years) (miaka ya uwekezaji)

Hapa unaandika miaka ambayo utakuwa umewekeza katika mfuko huu, mfano
kama unataka kuwekeza kila mwezi 50,000/= katika mfuko wa ukwasi ambao una
wastani wa mrejesho wa uwekezaji wa 14% kwa mwaka na unataka kuwekeza
kwa miaka 30 basi hii miaka 30 utaiandika hapa.

Baada ya kujaza sehemu hizi tatu basi utabonyeza sehemu iliyoandika calculate.
Nabaada ya hapo majibu yatakuja upande wa kulia. Upande wa kulia pia una una
sehemu 3 ambazo zimeachwa wazi ambazo ni:-

(iv) Expected amount ( kiwango ambacho unatarajia)

Hapa kikokotozi kitakuletea pesa ambayo utaipata baada ya kuwa umewekeza


kwa miaka ambayo umeiandika. Hii ni pesa ambayo imekuja kama faida na pesa
ambayo umeiwekeza.

.
(v) Invested amount (TZS)

Hiki ni jumla ya kiasi ambacho utakuwa umewekeza kwa miaka yote ambayo
umefanya uwekezaji wako, maana hii ni jumla ya pesa ambayo umekuwa
ukichangia kwa miaka yote.

(vi) Wealth gain (TZS)

Hiki ni kiasi cha faida ambacho unakuwa umekipata baada ya kuwekeza kwa
miaka ambayo umeitaja.

Tuone mfano hapo chini

Tukuchukulie mfano unataka kuwekeza 50,000/= kila mwezi kwa miaka 25


kwenye mfuko ambao unakupa mrejesho wa uwekezaji wa 14% kwa mwaka, je
baada ya miaka 25 utakuwa na faida kiasi gani na utakuwa umewekeza kiasi gani?
Nadhani umeona matokeo yetu ni kuwa kama umewekeza 50,000/= kila mwezi
kwa miaka 25 kwenye mfuko ambao una mrejesho wa 14% kwa mwaka jumla ya
pesa utakayo pokea baada ya miaka 25 ni TSH 136 milioni na kiasi ambacho
unakuwa umechangia ni TSH 15 milioni na pesa ambayo ni kama faida ni TSH 121
milioni kwa hiyo utaona ni hela nzuri tu na kikubwa ni kuwa kupitia kikokotozi
hiki kinakupa picha ya nini ambacho utegemee.
MPANGO WA KUWEKEZA KILA MWEZI (MONTHLY INVESTMENT
PLAN)
Kikokotozi hiki kina tofauti na kikokotozi kilichopita kwani kikototozi
kilichopita kinakupa picha ambayo unaweza kuipata kama umewekeza.
Kikokotozi hiki kinaanzia mwisho kurudi mwanzo ili kukuweza kufanya
mipango. Mfano mimi ninaweza kuwa nahitaji milioni 100 baada ya miaka 14, sasa
kikokotozi hiki kinaniwezesha kujua ni kiasi gani niwe nawekeza kila mwezi ili
kufikia malengo yangu. Mchanguo umefanywa hapo chini kwa ajili ya wepesi wa
uelewa:-
Tuanze maelezo ya kila kipengele

(i) Expected amount (TZS)

hiki ni kiwango cha pesa ambachounakihitaji baada ya muda fulani, mfano kama
mimi nimepiga mahesabu kuwa ili nifikie uhuru wa kifedha basi nitahitaji milioni
150 baada ya miaka 20 ila sifahamu inanibidi niwekeze kiasi gani kwa mwezi ili
nifikie uhuru huo wa kifedha, hii pesa ndio ninaiweka hapa ili iniwezeshe kujua ni
kiasi gani ninatakiwa niwekeze kila mwezi

(ii) Expected annual return

Hiki ni kiasi cha mrejesho ambao unadhani uwekezaji wako unaweza kuwa
unarudisha kila mwaka, kama tulivyoona katika kikokotozi kilichopita, mfano
kama uwekezaji wako unakurudishia 14% kwa mwaka basi hii namba ndio
utaiweka hapa.

(iii) Period (years)

Hii ni idadi ya miaka ambayo unahitaji kuwekeza

Upande wa pili wa hiki kikokotozi una

(i) Monthly investment (TZS)

Hiki ni kiasi cha pesa ambacho kikokotozi kitakuelekeza kuwa unahitaji


kuwekeza kila mwezi ili ufikie malengo yako.

(ii) Invested amount (TZS)

hiki ni kiasi cha pesa cha jumla ambacho utakuwa umewekeza kwa miaka yote,
pesa ambayo ulitoa mfukoni na kuwekeza.

(iii) wealth gain (TZS)

hii ni jumla ya fedha ambayo imepatikana kama faida katika kipindi chote cha
uwekezaji.
Tuone mfano

Chukulia unahitaji milioni 150 ndani ya miaka 20 je ni kiwango gani cha fedha
unatakiwa kuwekeza kila mwezi ili uweze kufanikiwa katika malengo yako ikiwa
mfuko uliowekeza una mrejesho wa 14 kwa mwaka
Majibu yetu ndio hayo hapo juu, ni kuwa ili ufikie malengo yako ya kuwa na
milioni 150 ndani ya miaka 20 basi unatakiwa kuwekeza kila mwezi 113,952/= kila
mwezi na jumla ya fedha ambayo utakuwa umewekeza ni kiasi cha 27 milioni na
faida ni 122 milioni. Sio mbaya kama una nidhamu unaweza kutengeneza milioni
150 kirahisi mno na hapo chini nitakuelekeza njia ambayo unaweza kufikia lengo
lako kwa gharama nusu ya hiyo na pia kama nilivyosema tukipiga mahesabu
halisia unaweza kukuta faida inakuwa zaidi ya hiyo ngoja tutaona hapo chini pia .

Tuone mfano wa pili

Katika huu mfano tugeuze hesabu kidogo kama unakumbuka kwenya kikokotozi
cha uwekezaji wa mwezi tulipiga mahesabu ya kuwa tuna 50,000/= ya kuwekeza
katika mfano huu tugeuze tuseme tunahitaji milioni 136 ndani ya miaka 25 kwa
mrejesho wa 14% kwa mwaka tuone je itatuletea tuwekeze kiasi gani kwa mwezi.
Nadhani umeona utofauti wa hivi vikokotozi viwili, hapa tunaanzia mwisho
kurudi mwanzo na katika kikokotozi kilichopita tunaanzia mwanzo kwenda
mwisho. Nadhani umeona jibu la mfano wetu wa pili ya kwamba kama tunahitaji
milioni 136 kwa miaka 25 na mrejesho wa 14 basi itatubidi kuwekeza 50,000/= kwa
mwezi, sababu iliyofanya tukapata 49,867/= kwa mwezi ni kwa kuwa nimeandika
milioni 136 tu na zile pointi nyingine nikaziacha.

1) Kikokotozi cha uwekezaji wa mara moja (single sum investment


calculator)

Hiki kikokotozi kina utofauti na vikokotozi vilivyopita katika eneo hili.


Kikokotozi hiki kinapiga mahesabu ya uwekezaji endapo unakuwa umewekeza
mara moja tu na sio kila mwezi kama tulivyoona katika vikokotozi vilivyopita.
Mfano, unaweza kuwa umepata fedha ya mara moja na ukaamua kuiwekeza huku
ukiwa hauna matarajio ya kuwa unawekeza mara kwa mara kama tulivyoona
katika vikokotozi vilivyopita, kwani sio kila mtu anapendelea kuwekeza mara
kwa mara au kuna wengine hawana mapato ya kujirudia kwa hiyo kikokotozi hiki
ni kwa ajiri yao.

Kama kinavyoonekana katika picha hapo chini


Maelezo ya viboksi vilivyo kwenye mchoro hapo juu ni kama ifuatavyo:-

(i) Single sum investment (TZS)

Hiki ni kiasi ambacho unawekeza kwa mara moja, mfano kama pesa unayotaka
kuwekeza kwa mara moja ni 100,000/= basi hapa ndio unaweka hiyo pesa katika
kikokotozi hiki.

(ii) Expected annual return

Huu ni mrejesho wa uwekezaji ambao mfuko wako unatarajia kukurudishia kama


tulivyoona hapo juu. Mfano, kama mrejesho wa uwekezaji ni 12% au 14% au 20%
basi asilimia hizo zitaoneshwa kwenye eneo hili lililoandikwa “expected annual
return”.

(iii) Period (years)

Hii ni idadi ya miaka ambayo uwekezaji wako utachukua. Na hapa inaweza kuwa
miaka 2, 5, 10 na kuendelea kama unavyotaka kuwekeza

Kwa upande wa pili wa kikokotozi ambao ni upande wa majibu kuna

(i) Expected amount (TZS)

Hiki ni kiasi ambacho unategemea kupokea baada ya muda wako wa uwekezaji


na hapa ni jumla ya pesa uliyowekeza na faida yake.

(ii) Invested amount

Hiki ni kiasi cha fedha ambacho umewekeza katika muda wote wa uwekezaji.
Kwa kuwa hapa unawekeza mara moja basi kiasi hiki ni sawa na kile kiasi
ambacho ulikiandika pale mwanzo kwenye kipengele cha investment
(iii) wealth gain (TZS)

Hii ni faida ambayo unakuwa umeipata baada ya uwekezaji wako kuwa umeiva

Mfano,

Tuchukulie nina 100,000/= ya kuwekeza kwa pamoja na ninataka niwekeze kwa


muda wa miaka 15 na mfuko ninaotaka kuwekeza una mrejesho wa 15% kwa
mwaka. Je baada ya hii miaka 15 nitakuwa na kiasi gani?

Ngoja tufanye hesabu ili kuona ni kiasi gani kitapatikana kwenye uwekezaji huu:-
Matokeo ni kuwa baada ya miaka 15 ya kuwekeza TSH 100,000/= kwa mrejesho
wa 15% kwa mwaka pesa yetu imekuwa na kufikia TSH 813,706/= na katika kiasi
hiki faida ni TSH 713,706/=

(i) Mpango wa uwekezaji wa mara moja (single sum investment plan)

Kikokotozi hiki hakina tofauti na kikokotozi kilichopita ila utofauti ni kuwa


kikokotozi hiki kinaanzia mwisho kuja mwanzo yaani hapa unaanza na kiasi
ambacho unakihitaji mwisho wa uwekezaji wako na baada ya hapo kikokotozi
kinakuwezesha kujua ni kiasi gani unatakiwa kuwekeza kwa mara moja ili ufukie
malengo yako.

Kikokotozi ni kama kinavyoonekana katika jedwali hapo chini.


Maelezo

(i) Expected amount

Hiki ni kiasi ambacho unategemea kupokea mwisho wa uwekezji wako ikiwa


kama umewekeza kwa mara moja.

(ii) Expected annual return

Huu ni mrejesho wa uwekezaji wa mfuko husika ambao unautarajia

(iii) Period (years ) hii ni idadi ya miaka ambayo uwekezaji wako


utachukua

Upande wa pili wa kikokotozi kuna

(i) Single sum investment (TZS)

Hiki ni kiasi ambacho unatakiwa kuwekeza kwa mara moja ili uweze kufikia
malengo yako au kufikia pesa ambayo umeiainisha hapo juu

(ii) Wealth gain (TZS)

Hiki ni kiasi cha faida ambacho unakuwa umekipata baada ya miaka yako ya
uwekezaji wako kuisha

Mfano,

Tuchukulie una hitaji kiasi cha TSH 20 milioni baada ya miaka 10 kwenye mfuko
wenye mrejesho wa 15% kwa mwaka. Je ni kiasi gani utahitajika kuwekeza kwa
mara moja ili uweze kufikia malengo yako?
Kwa hiyo utaona ili uweze kupata TSH 20 milioni baada ya miaka 10 kwenye
mfuko wenye mrejesho wa 15% kwa mwaka basi itakubidi uwekeze TSH
4,943,694/= na faida ambayo utaipata ni kiasi cha TSH 15 milioni,

Nadhani mpaka kufikia hapo utakuwa umeona ni jinsi gani kikokotozi cha UTT
AMIS kinavyoweza kurahisisha upangaji wako wa mambo ya uwekezaji.

UTT AMIS NA HATI FUNGANI KIPI KINA MREJESHO MKUBWA


Kuna mtu nilimsikia siku moja anasema usiende kuwekeza UTT AMIS bali
wekeza moja kwa moja katika hati fungani za serikali kwani hata wao UTT AMIS
wanawekeza katika hati fungani za serikali.

Kama tulivyoona katika maelezo ya mifuko tumeona kuwa mifuko yote


imewekeza katika hatifungani kwa asilimia fulani ya mali zake. Kuna faida za
kuwekeza UTT AMIS ambazo hauwezi kuzipata kama unakuwa umewekeza
katika hati fungani moja kwa moja. Ukiachana na kuwa unahitaji kuwekeza kiasi
kidogo kama unawekeza UTT AMIS au ukwasi ambao upo katika mifuko ya UTT
AMIS. Suala ni kwamba sio kila hati fungani ya serikali ina mrejesho mkubwa
kuliko UTT AMIS nitoe mfano wa mfuko ambao umewekeza katika hati fungani
pekee na mrejesho wa hati fungani za serikali:
Huu ni mrejesho wa mfuko wa ukwasi na kama tunavyoona toka mfuko
unaanzishwa 2013 mfuko ulikuwa na mrejesho wa wastani wa 13.4% na kwa
miaka 5 iliyopita mfuko ulikuwa na mrejesho wa 14.2% sasa tuangalie baadhi ya
mrejesho ya hati fungani za serikali za muda mrefu.

MIAKA MREJESHO (%)


2 7.82
5 9.18
7 10.08
10 11.44
15 13.5
20 15.49
25 15.95

Sasa kabla hatujaendelea mbele, kuna kitu inabidi nikiseme hati fungani unaweza
kuinunua kwa bei ya chini ya thamani yake (at discount), maana yake mrejesho
wake unakua mkubwa zaidi ila hapa nimechukulia kuwa zinauzwa kwa bei halisi
(at par value) na kama umekuwa unafuatilia hati fungani siku hizi zimekuwa za
moto kwa upande wa bei.

Sasa kwa kuangalia utaona ni kuwa ni hati fungani mbili tu ndio zina mrejesho
mkubwa kuliko mfuko wa ukwasi. Hizi ni hati fungani ya miaka 20 na miaka 25
tu. Kitu kingine ambacho utaona kuwa ni bora kwa upande wa UTT AMIS ni
kuwa huu mrejesho ni wa mwaka mmoja ina maana tukichukulia mtu
anayewekeza katika hati fungani ya miaka 15 kushuka chini Hana mrejesho
mkubwa kuliko aliyewekeza UTT AMIS. Aidha, uwekezaji wa hati fungani ni wa
muda mrefu lakini wa UTT AMIS kama mnakuwa mmewekeza kwa miaka 2 na
baada ya hapo uwekezaji wenu unakuwa umeiva wewe ambaye umewekeza
katika mfuko wa ukwasi unakuwa na faida kuliko aliyewekeza katika hatifungani
ya miaka 2.
Jambo ninalolieleza hapa ni kuwa sio kwamba hati fungani ni bora kuliko
kuwekeza UTT AMIS, wala mtu anayewekeza UTT AMIS sio kwamba ni bora
kuliko anayewekeza katika hati fingani bali kila uwekezaji una ubora wake na
udhaifu wake kwa hiyo sio sahihi kutoa hitimisho la kuwa kwa kuwa UTT AMIS
imewekeza pia katika hati fungani basi ni bora kuwekeza katika hati fungani
kuliko UTT AMIS.
SEHEMU YA NNE

MAMBO UNAYOHITAJI KUJUA KABLA NA BAADA YA KUWEKEZA UTT


AMIS

MIPANGO NA MIKAKATI YA UWEKEZAJI


Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, uwekezaji wowote wenye tija
lazima uwe na mipango na mikakati, nimekutana na watu wengi ambao wanaishia
kununua vipande tu bila kuwa na mkakati au mipango ya vipande walivyonunua
viwafanyie nini mwisho wa siku. Katika kipengele cha jinsi ya kutumia kikokotozi
tumeona kuwa unapokuwa na mipango inakuwezesha kujua ni kiasi gani
uwekeze kila mwezi ili kufikia malengo yako. Embu fikiria yule mkulima ambaye
anatoka nyumbani kwenda shamba na jembe lakini hana mpango wa kuwa
analima nini, anaanza kupanda lini na analima shamba lenye ukubwa gani kwani
haya yote ndio yatakayo msaidia kujua analima shamba gani na analima vipi na
kama atahitaji nguvu ya ziada. Mfano shamba la mpunga lina utofauti sana na
shamba la mahindi kwa hiyo akijua ni nini anataka kupanda basi atachagua
shamba ambalo linamfaa kulima

Tumeona UTT AMIS ina mifuko mingi yenye sifa tofauti tofauti na malengo
tofauti, je wewe malengo yako ya kuwekeza ni yapi ili ujue mfuko ambao utakupa
faida zaidi kutokana na kile ambacho umekusudia kukipata. Kama unawekeza
kwa ajili ya mtoto au kwa ajii yako mwenyewe au kwa ajili ya shughuli fulani basi
ni vyema ukawa na picha kichwani nini unataka kwani uwezo wa UTT AMIS
kukusaidia unategema mahitaji uliyonayo. Kuna mtu anataka kuwekeza ili
akistaafu awe na chanzo cha mapato ambacho kitamuwezesha kukidhi mahitaji
yake pale ambapo anakuwa amestaafu.
MUDA WA UWEKEZAJI
Fikiria yule msafiri ambaye anaanza safari akiwa hajui wapi anaishia, yeye anaona
raha kusafiri ila hajui mwisho wa kituo chake ni upi. Huyu ni kama yule
muwekezaji ambaye anawekeza akiwa hajui kuwa uwekezaji wake unaiva lini
yeye anaona raha kuwekeza tu bila kujua ni lini uwekezaji wake utakuwa tayari,
kwani lengo kuu la kuwekeza ni kuwa mwisho wa siku uwekezaji wako
ukusaidie.

Kama unakumbuka wakati tunatumia kikokotozi moja kati ya kitu cha msingi
ambacho kilikuwa katika kile kikokotozi ni muda ambao utautumia katika
uwekezaji wako kwani huu pia utakuonyesha ni kiasi gani unatakiwa kuwekeza
ili ufanikishe malengo yako, lakini ukiwekeza tu bila kujua ni lini uwekezaji wako
unatakiwa uwe umeiva unakuwa hauna hekima ya kiuwekezaji na hauwezi
kupata faida kamili ya uwekezaji wako. Kitakuwa kitu cha ajabu una uhitaji hela
yako ndani ya miaka miwili halafu unaenda kuwekeza kwenye mfuko wa wekeza
maisha.

MATARAJIO YA MAPATO YAUWEKEZAJI


Ukitaka kupanga vizuri uwekezaji wako basi unatakiwa kujua pia ni kiasi gani
utahitaji baada ya muda wa uwekezaji wako kuwa umeiva, hii itakupa picha ni
kiasi gani unatakiwa uwekeze ili kufikia malengo yako, ukiwa kama muwekezaji
ni sawa na askari vitani lazima ujifunze kuwa na shabaha hauwezi kuwa vitani
halafu unapiga risasi tu bila mpangilio ila ukiwa na shabaha ni rahisi kumlenga
adui na kumshinda. Katika uwekezaji ukiwa na shabaha au lengo ambalo
umeliweka basi unakuwa katika nafasi nzuri ya kuwa na mikakati ya jinsi ya
kulifikia lengo lako. Usiwekeze tu vipande hapa vipande pale bali uwe na shabaha
kuwa baada ya muda fulani nahitaji kuwa na kiasi hiki cha fedha na ili nifikie kiasi
hiki cha fedha basi ninatakiwa kuwekeza katika mfuko huu na kwa kiasi hiki.
NIDHAMU YAKO YA UWEKEZAJI
Kama huna nidhamu ya kifedha basi kuna mifuko ambayo inabidi usiwekeze hasa
hasa ile ambayo inakufanya uachane na malengo yako, au kama unaweza kujenga
nidhamu ni vizuri kwa maisha yako ya sasa na ya baadae. Mfano, kama hauwezi
kujitawala mwenyewe na unataka kuwekeza kwa ajili ya mtoto wako basi ni
vyema usiwekeze katika mfuko kama wa ukwasi ambao unakupa nafasi ya kutoa
fedha kirahisi. Ni bora ukawekeza katika mfuko wa watoto ambao utakupa nafasi
ya kuweka hela tu mpaka mtoto atakapofikisha umri wa miaka 12 ndipo
utakaporuhusiwa kuitoa au kama una mahitaji mengine lakini hauwezi kujitawala
na jinsi ya kutoa fedha basi unaweza kuwekeza katika mfuko wa wekeza maisha
ambao una zuio muda.

HALI YA UCHUMI YA MUWEKEZAJI


Uzuri wa mifuko mingi ya UTT AMIS inakuwezesha kuwekeza kwa kiasi kidogo
sana na hivyo hata mtanzania wa kawaida anaweza kuwekeza ila hapa kuna kitu
ambacho pia nimekiona, unakuta mtu hana pesa ya matumizi ndani ya mwezi
ambayo inaweza kumsaidai kuendesha maisha yake lakini anaamua kuwekeza
kiasi kikubwa na anabaki hana kitu na anapopata shida basi inamlazima kuuza
uwekezaji wake kabla haujakomaa. Sasa unachotakiwa kufanya ni kuangalia
uwezo wako na kupima pia kiasi ambacho unaweza kuwekeza bila kuathiri
maisha yako ya kila siku ili kuepuka kuuza uwekezaji wako kabla ya muda wake.
KUMBUKUMBU ZA MANUNUZI YA VIPANDE
Moja kati ya vitu vinavyo mtofautisha muwekezaji anayefanikiwa na muwekezaji
ambaye hafanikiwi ni katika kutunza kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya
vipande. Ni vigumu kukumbuka bei ya kipande ambacho ulinunua miaka 3 au 5
iliyopita na hivyo ni ngumu kujua faida ambayo hicho kipande kimekuingizia kwa
hiyo ni vyema kujua kuwa una wekeza kiasi gani hii itakusaidia kujua ni faida
kiasi gani umepata na wapi ambako kuna shida ili uweze kurekebisha

MPANGO WA KUWEKEZA MARA MOJA NA MPANGO WA


KUWEKEZA MARA KWA MARA
Ukichukua kiasi kile kile ukakigawanya katika mipango miwili. Mpango wa
kwanza ni wa kuwekeza kwa mara moja na mpango mwingine ni wa kuwekeza
kidogo kidogo kwa mwezi au baada ya muda, tofauti ya kiasi ambacho
mtamalizanacho ni kubwa sana, kuna kipindi utofauti inaweza kuwa kubwa
mpaka ukashangaa nataka nitoe mfano mdogo tu hapa

Mfano

Chukulia watu wawili wenye milioni 100 za kuwekeza ndani ya miaka 20 mmoja
akasema nitawekeza hii milioni moja yote kwa kiasi kila mwezi kwa miaka yote
20 ambayo itakuwa TSH 417,000/= kwa mwezi na mwingine akasema nitawekeza
hii milioni 100 kwa pamoja. Jumla ya pesa ambayo imewekezwa na muwekezaji
wa kwanza na pili ni milioni 100 ila tofauti ni kwamba muwekezaji wa kwanza
amewekeza kiasi chote kidogo kidogo kila mwezi, na muwekezaji wa pili
amewekeza kiasi chote kwa pamoja tuchukulie mfuko walio wekeza una mrejesho
wa 14% kila mwaka.
Mrejesho wa muwekezaji wa kwanza

Turudi kwenye kikokotozi cha UTT AMIS tuone mahesabu yao yanakuwaje, huyu
muwekezaji amewekeza TSH 417,000/= kila mwezi kwa miaka 20 kwenye mfuko
wenye mrejesho wa 14% kwa mwaka.

Na haya ndio mahesabu yetu hapo chini


Kama utakuwa una kumbukumbu vizuri ya jinsi ya kusoma kikokotozi cha UTT
AMIS, utaona kuwa kwa muwekezaji wa kwanza kiasi ambacho amewekeza ni
takiribani milioni 100 na faida ambayo amepata kwa miaka 20 ni milioni 448 na
jumla ya pesa ambayo atapokea kwa miaka 20 ni milioni 548

Sio mbaya ila tuone muwekezaji wa pili ambaye alichagua kuwekeza 100 kwa
pamoja bila kuongeza pesa nyingine

Mrejesho wa muwekezaji wa pili

Muwekezaji huyu yeye aliwekeza milioni 100 yote kwa pamoja katika mfuko
wenye mrejesho wa uwekezaji wa 14% kwa miaka 20 tuone uwekezaji wake
umekuwaje
Matokeo ni kuwa muwekezaji aliyewekeza milioni 100 kwa pamoja amepata faida
ya 1.27 bilioni na jumla ya fedha ambayo ataipokea baada ya miaka 20 ni 1.374
bilioni.
Tuone taarifa fupi ya mrejesho wa wawekezaji hawa wawili

Kiasi walichowekeza Faida Jumla ya pesa


Muwekezaji wa kwanza 100 milioni 448 milioni 548 bilioni
Muwekezaji wa pili 100 milioni 1.27 bilioni 1.374 bilioni

Kwa hiyo utaona kuwa ingawa waliwekeza kiasi sawa kwa muda wote ila
muwekezaji wa pili alikuwa na faida mara tatu kumshinda muwekezaji wa
kwanza, wakati muwekezaji wa kwanza alikuwa na faida ya milioni 448
muwekezaji wa pili alikuwa na faida ya bilioni 1.27

Tuone wawekezaji wawili ambao wamewekeza katika mfuko wa wekeza maisha


kwa miaka 10 na kiwango walichonacho kuwekeza ni TSH 1 milioni lakini
muwekezaji wa kwanza alikuwa anawekeza kiasi kidogo kidogo kila mwezi na
muwekezaji wa pili akachagua kuwekeza pesa yote kwa mara moja. Tumeona kwa
wastani mfuko wa wekeza maisha umekuwa na mrejesho wa 14% kwa miaka
iliyopita japo hii inaweza kupanda au kushuka ila tutaitumia kwenye mahesabu
yetu.
Muwekezaji wa kwanza

Kwa TSH 1 milioni kwa mpango wa kuwekeza kila mwezi huyu muwekezaji
atawekeza 8,340/= kwa miaka yote kumi, turudi kwenye kikokotozi
Tumeona kuwa baada ya miaka 10 ya kuwekeza kila mwezi 8,340/= mwisho wa
siku jumla ya kiwango ambacho kimewekezwa ni TSH 1 milioni na faida baada ya
miaka ni 1.185 milioni na jumla ya pesa atakayopata baada ya miaka ni TSH 2.187
milioni.
Tuone muwekezaji wa pili
Muwekezaji wa pili

Muwekezaji wa pili amewekeza milioni 1 kwa pamoja kwa miaka yote 10 na


mrejesho wa uwekezaji ni 14%

Tuone matokeo
Kama uavyoona muwekezaji wa pili ana faida ya TSH 2.7 milioni na jumla ya pesa
ambayo ataipata kwa miaka yote ni 3.7 milioni kwa hiyo utaona kuwa muwekezaji
aliyewekeza kwa mara moja ana pesa nyingi kuliko muwekezaji wa kwanza faida
yake tu ni kubwa kuliko pesa yote ambayo muwekezaji wa kwanza kwa miaka 10
(jumla ya faida na mtaji).

Hitimisho

Kama tulivyoona kuwa kama unawekeza pesa yote kwa mara moja faida yako
inakuwa kubwa kuliko mtu ambaye anawekeza taratibu taratibu kama
mtawekeza jumla ya kiasi ambacho kinafanana na kama mrejesho wa uwekezaji ni
sawa.
Tanbihi

Kama kusoma matokeo ya kutoka kwenye kikokotozi yanakusumbua basi


unaweza kurudi kusoma jinsi ya kusoma kikokoktozi cha UTT AMIS hapo juu
MAAJABU YA RIBA YA KAMPAUNDI
Kuna watu ambao hawafahamu kuwa ili kupata faida zaidi ya riba ya kampaundi
lazima uwe umewekeza kwa muda mrefu zaidi, na jinsi unavyokaa kwa muda
mrefu katika uwekezaji wako ndio faida inakuwa kubwa zaidi.

Hebu tuangalie mfano hapa

Mfano

Tuchukulie kuna mfuko ambao unakua kwa asilimia 14% kwa mwaka na bei ya
kipande ni TSH 100/= tuone jinsi bei itakavyo kuwa kwa miaka 15 ijayo na tuone
jinsi riba ya kampaundi inavyokuwa na maajabu

Mwaka Bei ya kipande


1 114
2 129.96
3 148.15
4 168.89
5 192.52
6 219.47
7 250.19
8 285.21
9 325.13
10 370.64
11 422.52
12 481.67
13 548.5
14 625.29
15 712.83

Sasa tuangalie wawekezaji watatu ambao walinunua kipande kwa bei ya 100 ila
mmoja akauza mwaka wa 5 na wa pili akauza mwaka wa 10 na mwingine akauza
mwaka wa 20 tuone mrejesho wao unakuwaje:-

Muwekezaji wa kwanza

Huyu alinunua kipande kwa bei yaTSH 100/= na akauza mwaka wa tano kwa bei
ya TSH 192.52/= tuone mrejesho wake, kama unashida na jinsi ya kutafuta
mrejesho wa uwekezaji tafuta kitabu change cha namna bora ya kutengeneza
hela soko la hisa au soma jinsi ya kutafuta mrejesho wa uwekezaj katika kitabu
hiki

Mrejesho = 192.52- 100 = 92.52

Mrejesho = 92.52/100)* 100 = 92.52%

Lakini huu mrejesho ni kwa miaka 5, tukitaka kupata mrejesho wa wastani kwa
kila mwaka tunagawanya kwa tano

92.52/5 =18.504%

Kwa hiyo wastani wake ulikuwa ni 18.5% kwa kila mwaka

Muwekezaji wa pili

Huyu pia alinunua kipande kwa bei ya TSH 100/=na akauza mwaka wa kumi kwa
bei ya TSH 370.64/= tuone mrejesho wake

Mrejesho = 370.64 – 100) = 270.64

270.64/100)* 100 = 270.64% lakini huu ni mrejesho wa miaka 10 tukitaka kupata


mrejesho wa kila mwaka kwa miaka kumi

270.64%/10 =27.06%

Kwa hiyo utaona kuwa muwekezaji wa pili alikuwa na wastani wa 27.06% kama
mrejesho wa mwaka mmoja kwa miaka yote kumi.

Muwekezaji wa tatu

Huyu pia aliwekeza kwa bei ya TSH 100 na akauza vipande vyake mwaka wa 15
kwa bei ya TSH 712.83/= tuone mrejesho wake unakuwaje.
Mrejesho

712.83- 100 = 612.83

612.83/100)*100 = 612.83%

Ili kupata mrejesho wa miaka 15 = 612.83/15= 40.85%

Kwa hiyo kwa wastani miaka 15 mrejesho ulikuwa 40.85%

Hitimisho

Kama tilivyoona katika mfano wetu hapo juu, tumeona ijapokuwa kila mwaka
ongezeko la mfuko wetu lilikuwa 14% lakini kwa sababu ya riba ya kampaundi
mirejesho ya hawa watu imetofautiana na tumeona kuwa kadri unavyo endelea
kukaa katika uwekezaji basi ndivyo uwekekezaji wako unazidi kukupa faida
kubwa , sababu inayofanya mtu akikaa katika uwekezaji kwa muda mrefu awe na
mrejesho mkubwa kuliko wenzake ni kwa sababu pesa yake inachukua muda
mrefu kukampaundi na hivyo mrejesho wake unakuwa mkubwa pia.

Hivyo, ukitaka kufurahia uwekezaji wako katika mifuko ya UTT AMIS basi
unapowekeza wekeza kwa muda mrefu ndio unapata faida zaidi.

MREJESHO WA MIFUKO YENYE HISA NA MIFUKO ISIYO NA HISA


Kuna baadhi ya watu huwa ni waoga kuwekeza katika mifuko yenye hisa kwa
kigezo cha kuwa mifuko iliyowekeza katika hisa hatari zake za uwekezaji ni
kubwa na mrejesho wake ni mdogo au hautabiriki, ila ukichunguza kwa makini
utagundua kuwa kuwekeza katika mfuko wenye hisa sio kwamba ni duni kuliko
mtu aliyewekeza katika mfuko wenye hati fungani na amana za kibenki. Tutaona
kuwa mtu aliyewekeza katika mfuko wenye hisa pia ana nafasi nzuri ya
kutengeneza hela kuliko mtu ambaye amewekeza katika mfuko wa mapato
yanayotoka katika hati fungani na amana za kibenki. Tunapozungumzia mfuko
ambao umewekeza katika amana za kibenki na hati fungani ni mfuko wa hati
fungani (bond fund) na mfuko wa ukwasi (liquid fund). Mifuko ambayo
imewekeza katika hisa tunazungumzia mfuko wa umoja, wekeza maisha, mfuko
wa watoto na mfuko wa jikimu. Tuone kuwa mtu anayewekeza katika mfuko
wenye hisa ana nafasi pia ya kufanya vizuri.

Unapowekeza katika mfuko wenye hisa kuna uwezekano wa kuwa na


mrejesho mkubwa zaidi

Hapa nilichosema ni kuwa mtu anayewekeza katika mfuko wenye hisa kuna
uwezekano kuwa mfuko wake ukapanda sana kwa mwaka fulani kutokana na hali
ya bei ya hisa ilivyo na gawio linavyotoka kwa mwaka Fulani. Kitu ambacho ni
kigumu kukipata katika mifuko ambayo mapato yake ni ya kutabirika, kwa mfano
mfuko ambao umewekeza katika hati fungani za serikali za muda mrefu
unategemewa kwa mwaka unaweza kupokea 15.95% ambacho ndicho kiwango
cha juu cha riba ambacho kinatoka katika hati fungani za serikali. Hata kama pesa
ambayo itapatikana kwa ile miezi sita ya kwanza itawekezwa hatutegemei kuwa
mfuko utakuwa na 25% kama mrejesho kutoka katika hati fungani kwa mwaka
husika, ila katika mfuko wenye hisa uwezekano wa mfuko kukua kwa zaidi ya
25% kwa mwaka upo ijapokuwa uwezekano pia wa mfuko kushuka kwa kiwango
cha juu pia upo kitu ambacho si rahisi kukiona katika mifuko yenye mapato ya
kuaminika.

Hii uwezekano wa mfuko kuwa na mrejesho mkubwa kwa mwaka Fulani ni moja
kati ya faida za mifuko yenye hisa kwani ukijumlisha na riba ya kampaundi kwa
muwekezaji wa muda mrefu katika mifuko hii anaweza kuwa na mrejesho
mkubwa kuliko muwekezaji wa mifuko yenye mapato ya kuaminika.
Tuone mfano

Huu chini ni mrejesho wa mfuko wa umoja kwa miaka iliyopita tangu kuanzishwa
kwake mpaka mwaka 2020 na tukiongeza mwaka 2021 ambapo mfuko wa umoja
umekuwa na mrejesho wa 16.6%. Matokeo ni kama unavyoona hapo chini, kitu
ambacho nataka uone ni kuwa kwa mwaka 2014 mfuko ulikuwa na mrejesho wa
51% kitu ambacho ni kigumu kukipata katika mifuko mingine ambayo haina hisa
ndani yake.

Mfuko wa wekeza maisha


Mfuko wa watoto

Mfuko wa jikimu

Mfuko wa ukwasi
Hitimisho

Kitu kimoja nadhani utakuwa umekiona kuwa ijapokuwa mfuko wa ukwasi


ambao umewekeza katika mapato ya kuaminika ya hati fungani kuna baadhi ya
miaka mfuko huu haukuwa na mrejesho mkubwa kuliko mifuko yenye hisa.
Mrejesho wake haukupungua sana kwa miaka ya 2016 mpaka 2019 wakati mifuko
yenye hisa ilikuwa na mrejesho mdogo, aidha mfuko huu pia haukuwa na mrejesho
mkubwa kwa miaka 2014 na 2015 kama ilivyokuwa kwenye baadhi ya mifuko
yenye hisa. Kwa hiyo kitu cha msingi hapa ni kuwa mifuko yote ina ubora ambayo
imewekeza katika hisa na ambayo haijawekeza katika hisa.

Tuone mfano wa pili

Mfano huu tutachukua mfuko wa ukwasi na mifuko yenye hisa tuone mrejesho
wake ungekuwaje kama mfuko wa ukwasi nao ungeanzishwa kwa mwaka sawa
na mifuko ambayo ina hisa.

MFUKO WA UKWASI VS MFUKO WA UMOJA


Tumeona wastani wa mrejesho wa mfuko wa ukwasi toka 2013 mpaka 2021 ni
13.5% na tumeona bei ya kipande cha mfuko wa umoja wakati unaanzishwa
ilikuwa TSH 100/= na mwaka 2021 juni bei ya kipande ilikuwa TSH 740/= je tuone
kwa mfuko wa ukwasi kama na wenyewe ungeanzishwa mwaka 2005 kwa bei ya
100 je mwaka 2021 bei ingekuwa kiasi gani na je kama utofauti ni mkubwa au ni
bora kuwekeza mfuko wa ukwasi.

Mfano wa bei ya kipande ya mfuko wa ukwasi toka 2005 ukianza na bei TSH ya
100/= kwa mrejesho wa 13.5%
MWAKA BEI YA KIPANDE
2005 113.5
2006 128.82
2007 146.21
2008 165.95
2009 188.35
2010 213.77
2011 242.62
2012 275.37
2013 294.54
2014 334.30
2015 379.43
2016 430.65
2017 488.78
2018 554.76
2019 629.65
2020 714.65
2021 811.12

Hitimisho

Kwa mfano wetu tumeona kuwa endapo mfuko wa ukwasi ungeanzishwa mwaka
2005 na ungekuwa na mrejesho wa 13.5 kwa miaka yote basi bei ya kipande
ingekuwa 811.12/= kitu ambacho sio mbali sana na mfuko wa umoja ambao bei ya
kipande ni 740/=. Kwa hiyo utaona kuwa mfuko wenye hisa pia mrejesho wake ni
mzuri tu kama ilivyo mifuko ambayo haina hisa na kuna baadhi ya miaka mfuko
wa umoja ulikuwa na bei ya kipande kubwa kuliko mfuko wa ukwasi. Hapa
tumetoa mfano na sio mrejesho halisi wa mfuko wa ukwasi mrejesho halisi
ungeweza kuwa mkubwa, sawa au mdogo kuliko huu tuliouonesha hapa.

RIBA YA KAMPAUNDI KATIKA MFUKO UNAOTOA GAWIO NA AMBAO


HAUTOI
Kama tulivyoona katika kipengele cha jinsi ya kutengeneza gawio na kipengele
cha maajabu ya riba ya kampaundi tumeona kuwa ili riba ya kampaundi ifanye
kazi vizuri basi inakubidi uwe umewekeza kwa muda mrefu sasa unapochukua
gawio pesa yako inapungua na inapunguza kasi ya riba ya kampaundi.
Mfano

Tuchukulie watu wawili ambao wamewekeza katika mfuko mmoja wenye


mpango wa kulipa gawio na mpango wa kuwekezewa gawio. Tuchukulie kiasi
chote ambacho kinaongezeka kwa mwaka kinatolewa kama gawio, mfano kama
mfuko umekua kwa asilimia 10 basi yote inatoka kama gawio, tuangalie itakuwaje.
Muwekezaji wa kwanza anachukua gawio na muwekezaji wa pili hachukui gawio
bali gawio linawekezwa tena na mfuko unakuwa kwa asilimia 12% na bei ya
kipande ni TSH 100.

Muwekezaji wa kwanza
MWAKA GAWIO THAMANI YA
MFUKO WAKE
1 12 100/=
2 12 100/=
3 12 100/=
4 12 100/=
5 12 100/=
JUMLA 60

Huyu muwekezaji wa kwanza kama ataendelea kuchukua gawio na sio


kuliwekeza tena basi riba ya kampaundi inakuwa haina nguvu kwani ili riba ya
kampaundi iweze kufanya kazi basi inabidi kiwango ambacho kinakuja kama
faida kiwekezwe tena ili nacho kizae faida. Kama muwekezaji anataka kutatua hili
tatizo basi itambidi pesa ambayo anaipata aiwekeze tena sehemu nyingine kwa
mrejesho ule ule wa 12%. Hapo atakuwa ameiweka riba ya kamapundi katika
matendo. Mpaka mwaka wa 5 thamani ya mfuko wake itaendelea kuwa ile ile TSH
100/= na jumla ya faida itakuwa TSH 60/=
Muwekezaji wa pili
MWAKA GAWIO THAMANI YA
MFUKO WAKE
1 12 112
2 12 125.44
3 12 140.49
4 12 157.34
5 12 176.22
JUMLA 60 76.22

Nadhani umeona utofauti kati ya muwekezaji wa kwanza na wa pili kupitia


majedwali mawili hapo juu. Muwekezaji wa kwanza alipokea gawio na akalitumia
kwa ajili ya mahitaji yake mbalimbali, kwa hiyo halikuzaa tena. Aidha muwekezaji
wa pili yeye alipokea gawio na akaliwekeza tena kwa mrejesho ule ule sawa na
mfuko wake kwa hiyo mwisho wa siku jumla ya faida ambayo aliipata kwa miaka
5 ni 76.22/= ambayo ni zaidi ya pesa ambayo muwekezaji wa kwanza alipata, ila
kama muwekezaji wa kwanza angewekeza pesa yake pia kwa mrejesho wowote
pesa yake pia ingeongezeka.

Hii ni sawa na muwekezaji ambaye anawekeza UTT AMIS kwa mpango wa


gawio na mpango wa kuwekezewa gawio, ijapokuwa mfano wetu una utofauti
kidogo na UTT AMIS kwani unapowekeza kwa mpango wa gawio bado utapata
faida kidogo ya kukua kwa mtaji. Ila kanuni niliyotaka kuionyesha hapa ni kuwa
ukiwekeza kwa mpango wa gawio pesa yako haiwezi kukampaundi kama mtu
aliyewekeza kwa mpango wa kuwekezewa gawio ISIPOKUWA kama utaiwekeza
pesa yako ambayo umepokea gawio.

Hitimisho

Sio kwamba kuwekeza katika mpango wa kuwekezewa gawio ni bora kuliko


mpango wa kuchukua gawio, hapana, ina tegemea na mahitaji ya muwekezaji.
Mwekezaji mwingine anahitaji gawio kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila
siku na hivyo gawio kwao ni bora na kuna wengine wanawekeza kwa ajili ya
maisha yao ya baadae kwa hiyo kampaundi kwao ni bora zaidi. Kwa hiyo ubora wa
gawio unategemea mahitaji ya muwekezaji ila ambacho usisahau ni kuwa
ukichukua gawio pesa yako haiwezi kukampaundi kama mtu ambaye yuko
kwenye mpango wa kuwekezewa gawio.
JINSI YA KUTENGENEZA PENSHENI YAKO NA UTT AMIS
Kwa mtanzania wa kawaida ambaye sio mfanyakazi wa umma au binafsi, unaweza
kujitengenezea pensheni yako mwenyewe kwa ajili ya siku za uzeeni. Kupitia
UTT AMIS ni rahisi kwa wote mtumishi na asiye mtumishi kuwekeza kwa ajili ya
siku zake za uzeeni. Watanzania wengi hasa hasa wale ambao hawajaajiriwa
dhana ya kustaafu haipo kabisa kichwani mwao na wakati mwingine inawabidi
kufanya kazi mpaka siku yao ya mwisho hapa duniani ili kuendesha maisha au
kuwa wategemezi. Kupitia UTT AMIS kama tutatavyoona hapo chini unaweza
kutengeneza pensheni yako wewe mwenyewe na baada ya kustaafu ikakufaa sana
kwenye maisha yako.

Kwanza tuanze na vitu vya jumla kuhusu kustaafu

Muda wa kustaafu kwa wengi badala ya kuwa ni muda wa kupumzika na


kufurahia maisha baada ya miaka mingi ya kufanya kazi unakuwa ni muda wa
taabu na mateso kifedha kwa sababu wengi wanakuwa hawakujipanga na jinsi ya
kuishi pale ambapo wanakuwa wamestaafu. Hivyo, vyanzo vyao vya mapato
vinakuwa vimekatwa, unakuta wanakuwa na maisha magumu sana kifedha kwa
sababu hawakujipanga mapema. Kwa baadhi yao wanawageuza watoto wao kuwa
chanzo cha mapato pasi kujali uwezo wa watoto wao kubeba mzigo wa
kuwatunza na kujitunza wao binafsi.

Kwa wale wataofanikiwa kupata kusoma kitabu hiki, niwakumbushe kuwa tangu
siku uliyoanza kufanya kazi ndiyo ilikuwa siku sahihi ya kuanza kujiandaa
kifedha kwa ajili ya siku za kustaafu. Ikiwa bado hujafanya hivyo, nikutie moyo na
kukumbusha kuwa unapaswa kuanza sasa kwa kuwekeza kwenye fursa
mbalimbali zilizo nchini ikiwa ni pamoja na UTT AMIS. Kwa hiyo katika hili
andiko nitakufundisha ni jinsi gani ujiandae kwa siku zile ambazo utakuwa
umestaafu.
Ndugu msomaji, utakaposoma sehemu hii ninategemea utajifunza maana ya
kustaafu, aina za watu wanaostaafu, makossa wanayofanya wastaafu wengi na
umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya kustaafu.

KUSTAAFU NI NINI
Tunapozungumzia kustaafu kuna watu wengi wanadhani ni mpaka mtu afikishe
miaka 60 au 65 ili aweze kustaafu kufanya kazi kwa lengo la kuingiza kipato cha
kuishi. Kwa miaka hii ya hivi karibu na kutokana na serikali nyingi kuweka
mazingira bora ya kuwekeza, imekuwa kawaida ya watu wengi duniani kustaafu
kutenda kazi wakiwa na umri mdogo kabisa takribani miaka ishirini na tano ya
kuzaliwa. Watu wamekuwa wakistaafu kufanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato
ili waishi. Ikiwa wewe ni mfuatiliaji na unapenda kujifunza kupitia vyanzo
mbalimbali, ukienda kusoma mitandaoni kuhusu “FIRE MOVEMENT” utajua
namna ambavyo vijana wa zama hizi wanavyopambana kuhakikisha wanastaafu
mapema.

Kwa ufupi tu “FIRE” ni financial independence, retire early. Kwa tafsiri isiyo
rasmi ni kuwa kupata uhuru wa kifedha ili kustaafu mapema. Watu walio kwenye
imani hii wanahakikisha kuwa wanatunza na kuwekeza fedha zao kutoka kwenye
vyanzo vyao mbalimbali mapema kwa kadri wawezavyo ili waweze kustaafu
mapema. Njia hii inahusisha kutunza na kuwekeza fedha hadi kufikia asilimia
sabini (70%) kwa kipindi fulani ili kumfanya muwekezaji husika kutengeneza
vyao vya fedha vitakavyomfanya kuishi bila kutegemea kufanya kazi kwa maisha
yake yote.

Hivyo, utaona kuwa katika zama hizi, kustaafu hakutegemei kufikia umri
uliopangwa kisheria isipokuwa inategemea ni kwa kiasi gani umejiandaa kifedha
kwa ajili ya muda ule ambao utaishi bila kufanya kazi.
Hivyo kwa maana hiyo, kustaafu ni kile kipindi ambacho mtu anaacha kufanya
kazi za kila siku kwa ajili ya kujipatia kipato. Sasa basi kundi lolote lile ambalo
upo kati ya kundi la kustaafu kisheria au kustaafu mapema muhimu ni lazima
kuwa na mikakati maalum za kukuza kipato ili wakati wa kustaafu utakapofika
basi uwe na uwezo wa kuishi pasipo kuwa na matatizo ya kifedha.

Kwa vijana wengi ukimwambia suala la kujipanga kifedha kabla ya kustaafu


anakuwa hakuelewi na ndio maana wakishafikia umri wa kustaafu ambao
umepangwa na serikali huwa wanahisi kuchanganyikiwa, kwa sababu
hawakujipanga mapema. Epuka kuwa katika kundi hili, anza sasa kujiandaa
kustaafu.

AINA ZA WATUA AMBAO WANASTAAFU


Kuna aina 3 za watu ambao wanastaafu

i) Watu waliokuwa wameajiriwa na wamefikisha umri wa kustaafu;


ii) Watu ambao walikuwa wamejiajiri na aidha wamechoka au wameamua
kupumzika; na
iii) Vijana ambao wamepanga kustaafu mapema ili wafurahie maisha yao.

Kundi lolote ambalo utakuwa hapo juu kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifanya
ila kufanya siku zako za kustaafu kuwa njema kifedha.

MAKOSA AMBAYO WASTAAFU WENGI WANAYAFANYA


Baada ya kukutana na wastaafu wengi nimejifunza kuwa kuna makosa kadhaa
yanayohusu fedha ambayo wengi wao wanayafanya. Kitabu hiki kitaainisha
makossa hayo ili kukupa nafasi ya kuyafahamu.
(i) Kutokupanga ni jinsi gani wataishi baada ya kustaafu

Kuna baadhi ya nchi kama sikosei china ikiwa mojawapo, hii mifuko ya pesheni ya
kijamii (social security) ziliondolewa na isipokuwa mfanyakazi ana jukumu la
kupanga kiasi cha fedha ambacho atahitaji baada ya kustaafu. Hali iko tofauti kwa
nchi nyingi za Afrika, mifuko ya kijamii inawatunzia watumishi fedha na wakati
wa kustaafu wanawapatia fedha yote ili wakatumie au wakapange namna ya
kuzitumia. Suala hili limewaumiza wengi kwa sababu wanapokea fedha nyingi
bila kuwa na mipango sahihi iliyotafitiwa kwa lengo la kuwekeza isipokuwa fursa
yeyote inayojongea mbele ya macho ya mstaafu anaichukua na kuwekeza fedha
zake. Kutokana na kuingia kwenye biashara wasizozifahamu wanajikuta
wanapoteza fedha nyingi na kwa takribani miaka miwili ya kustaafu ya kwanza,
wastaafu wengi wanakuwa wamemaliza fedha zao zote. Kwa upande wa wasio
kwenye ajira rasmi ndio kabisa hata wazo la kupanga kuwa kuna siku watastaafu
hawana kabisa na hawa pia huwa hawabaki salama ndio kinachofanya mtu ana
miaka 70 lakini bado anaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha
kwa sababu hakupanga kuwa kuna kustaafu. Hivyo ni muhimu kupanga na kujua
kuwa siku moja kuna kustaafu kufanya kazi. Mipango hii ikianza mapema,
inasaidia kuweka unafuu katika miaka ya ustaafu.

(ii) Kuingia kwenye biashara na hela ya pensheni ilihali hawajui


biashara

Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya biashara 10 zinazoanzishwa ni mbili ndio


zinaweza kusimama na zingine zinafilisika au kufungwa, wastaafu wanapotea
sana hapa kwa sababu kuu mbili

Mosi, ili uweze kuendesha biashara na kufanikiwa unahitaji muda kwa ajili ya
kuijenga akili yako ili iwezi kufikiri kama mfanyabishara na pia uwe na ujuzi wa
kibiashara husika. Ujuzi hauwezi kutengenezwa kwa siku moja inahitaji muda.
Sasa unakuta mstaafu ana miaka 40 anafanya kazi kama muajiriwa ila akistaafu
anataka awe mfanyabiashara hapo hapo bila kujua kuwa anahitaji kuwa na ujuzi
ambao utamchukua muda kuujenga ili afanikiwe na ndio maana wengi sana
wanafeli

Pili, mara nyingi huwa inawachukua watu kupoteza biashara moja au mbili ili
kuweza kusimamisha biashara au unakuta biashara nyingi zina kaa miaka 2 au 3
kabla hazijaanza kutengeneza faida wakati huo mstaafu anategemea fedha hiyo
hiyo kujikimu hivyo anajikuta anashindwa kusimamisha biashara ipasavyo.

(iii) Kutumia Pesa ya pesheni kwa matumizi yasiyozalisha tu


Kuwa na Mtiririko chanya wa fedha ndio inamfanya mtu aweze kuwa na fedha ya
kutosha kujikimu na mahitaji ya kila siku. Sasa unakuta mtu anaweka hela ya
pesheni benki halafu ndio anakuwa anatumia kidogo kidogo na mwisho wake
inaisha, hata keki kama utakuwa unakula kidogo kidogo bila kutengeneza
nyingine itaisha tu. Kwa hiyo kuweka hela benki na kuanza kutumia kidogo
kidogo kutafanya uishiwe pesa mapema na ubaki unahangaika. Fedha inapaswa
iwe kwenye uwekezaji ambao utahakikisha upatikanaji wa kipato kwa wakati
wote wa kustaafu. Uwekezaji katika muda wa kustaafu unaendana na kufanya
tathmini ya hatari za uwekezaji unaofanya, inashauriwa katika muda wa kustaafu,
muwekezaji awekeze kwenye vyanzo vya mapato ambavyo vina hatari kidogo ya
kupoteza uwekezaji husika.
(iv) Kupeleka fedha kwenye matumizi yasiyolenga kuongeza kipato

Sio kitu cha kushangaza kuona msataafu anatumia fedha ya kustaafu kununua gari
la kutembelea, kuoa, kujenga nyumba ambayo haina sura ya kuingiza mapato
ambapo mwisho wa siku anaishiwa pesa. Matumizi yote ya pesa kuna matumizi
ya aina mbili yaani matumizi yenye lengo la kuingiza kipato na matumizi
yanayotoa fedha moja kwa moja kwenye mfuko wa mtumiaji. Mfano, unavyotumia
pesa kuwekeza hayo ni matumizi ila yana sura ya kukuingizia kipato siku za
mbeleni na unapotumia hela kunywa kinywaji basi hayo matumizi hayana sura ya
kukuingizia kipato. Kwa hiyo kama mstaafu unapojiingiza katika matumizi yasiyo
na sura ya kuingiza kipato kwa kiwango kikubwa huku akiwa hana vyanzo
vingine vya mapato, matokeo yake ni fedha itaisha baada ya muda fulani.

(v) Kustaafu maana yake ni kupumzika

Kuna watu ambao hawaelewi maana ya kustaafu, kustaafu ni kupumzika kwa


hiyo hawajipangi mapema ni jinsi gani wataendesha maisha yako katika kipindi
hicho cha mapumziko. Kwa hiyo unakuta wakati wa kustaafu ndio wananza
kukimbizana na kuanzisha biashara, kutafuta kazi tena ambayo itawapa kipato au
kuwa wategemezi wa watoto wao wakati kipindi hicho ndio wangekitumia
kutembea duniani maeneo mbali mbali ambayo hawakuwa na nafasi ya kwenda
kuyaona wakiwa kazini au kufanya kitu ambacho walikuwa wanakipenda. Kwa
wengi hapa ndio moto wa maisha unaanza, maisha yaanza kuwa magumu, na kwa
wale ambao wamejiajiri kuna ambao wanafanya kazi mpaka wanakufa.

HATUA ZA KUFUATA ZA KUTENGENEZA PESHENI YAKO


Hatua ya kwanza

Kabla haujapanga unahitaji kiasi gani ukisha staafu lazima ukae chini na kuanza
kupanga kila kitu ambacho unaweza kuwa unakihitaji katika muda wako wa
kustaafu. Hii itakupa picha ni kiasi gani unatakiwa kuwa nacho au fedha yako iwe
katika mfumo gani ili ikuwezeshe kufanikisha malengo yako.

Yafuatayo ni baadhi ya mahitaji ambayo mtu anaweza kuwa nayo kama atahitaji
kustaafu
(i) Matibabu

Unapostaafu hasahasa pale ambapo unakuwa umri umeenda utahitaji pesa au


huduma kwa ajili ya matibabu kwa hiyo ni vyema ukawa na kiasi cha fedha
ambacho unaweza kuwa unakihitaji kwa matibabu akati umesataafu au unaweza
kuwa na bima ambayo itakusaidia wakati unapokuwa na matatizo ya kiafya. Ujue
moja kati ya njia ambayo tunaweza kusaidia kupunguza matatizo mengi ya kijamii
yakiwemo umaskini na ufisadi katika nchi za kiafrika ni kupunguza idadi wa
watu tegemezi. Unakuta kijana anaaza kazi tu nyuma ana mzigo wa ukoo mzima
hata mjomba wake na mjomba wako akiugua wewe ndio unapigiwa simu utoe
fedha ya matibabu. La kushangaza ni kwamba unakuta hawa wote walikuwa
wafanyakazi ila kwa wakati wakifanya kazi hawakupanga wataishije wakistaafu.
SIO LAZIMA UKISTAAFU UWE TEGEMEZI WA WATOTO WAKO KWA
SABABU WAO NAO WANA MAISHA YA KUPAMBANA NAYO KWA HIYO
JIPANGE MWENYEWE ILI KUWAPUNGUZIA MZIGO.

(ii) Chakula

Unaweza kuamua kuyaendesha maisha yako unavyotaka na sio maisha yako


yendeshwe tu kama bendera. Kwa hiyo moja ya vitu ambavyo unahitaji kuviweka
katika mahesabu ni chakula.

(iii) Starehe

Tukija kwenye suala la kutalii huo muda sisi hatuna, unakuta tuko busy
kukimbizana na maisha kwa kiwango ambacho inafikia mtu anakuwa kama
amezaliwa ili afanye kazi hana muda wa kupumzika na akistaafu ndio kabisa hana
hata senti ya kutembea hata vituo vya utalii vya nchi yake. Kwa hiyo kama una
pendelea kutembea lazima hili pia liwe katika bajeti yako kwa sababu litakusaidia
kujua ni kiasi gani unahitaji ukistaafu.
(iv) Kutimiza ndoto

Chukulia ulitaka kuwa mchoraji au mwanamuziki ukiwa mdogo ila maisha


yakakupeleka kusiko na unatamani ukistaafu ufanye kile kitu ambacho ulikuwa
unakipenda, basi unahitaji kuwa na bajeti hii pia.

Kadri siku zinavyosogea utaona kuwa mahitaji yako yanabadilika hivyo utakuwa
unabadilisha ratiba yako kadri unavyoona mahitaji yanatokea hiyo hapo juu
nimetoa kama picha tu ambayo inaweza kukusaidia katika upangaji

Mfano halisi

tuchukulie wewe ni kijana na una umri wa miaka 30 na unategemea kustaafu


ukiwa na miaka 60. kwa hiyo una miaka 30 mbele ili uweze kustaafu, sasa umekaa
chini na kupiga mahesabu na ukaona kuwa ukishastaafu utakuwa unahitaji
shilingi TSH 1 milioni kwa mwezi ili kuendesha miasha yako. Sasa unaweza
kuanzia hapa katika kupanga pesheni yako na ukajua ni kiasi gani unatakiwa
kuwekeza ili ufikie malengo yako. Huu ndio mfano tutakao tumia katika hiki
kipande cha jinsi ya kutengeza pesheni yako.

Hatua ya pili

Hapa katika hatua ya pili unafanya uchaguzi wa kuwa pesa ambayo itakuwezesha
kujikimu kwa miaka yako ya kusataafu itatoka wapi. Ngoja nikupe mifano miwili
Watu wawili wanaweza kuwa wamepokea TSH 100 Milioni kutoka kwenye
pensheni na mtu wa kwanza akaamua kuiwekeza hii 100 milioni katika uwekezaji
ambao unampa mrejesho wa 12% kwa mwaka na malengo yake ni kuwa atakuwa
anatumia 1 milioni kwa mwezi kwa miaka yote ya baada ya kusataafu. Hapa ina
maana kiasi ambacho atakuwa anatumia kwa mwaka ni kutoka katika faida na
mtaji wake wa 100 milioni utabaki palepale. Na mtu wa pili akaamua mimi pesa
yangu sita iwekeza bali nitaweka benki na nitakuwa nachukua kiasi cha milioni
12 kwa mwaka, au anaweza kuiwekeza pia ila akaamua kuwa atakuwa anachukua
faida na sehemu ya mtaji. Mfano faida kwa mwaka ni 12 milioni yeye anaweza
kuchukua milioni 13 kwa mwaka au zaidi ni uchaguzi wako.

Ila kwa sisi ambao bado tunapanga pensheni yetu ni vyema tukawaza kuwa pesa
ambayo tutakuwa tunaitumia ni faida tu na sio mtaji kwani haujui utaishi miaka
mingapi baada ya kustaafu unaweza kudhani kuwa utaondoka duniani mapema na
hivyo utumie mtaji pamoja na faida ukakuta unaishi miaka mingi zaidi ya ambavyo
umetegemea, hivyo ni bora kuwaza kuchukua faida tu na sio mtaji

Hatua ya tatu

Jua ni kiasi gani unatakiwa kuwekeza

Turudi kwenye mfano wetu, tumeona kuwa huyu kijana ambaye ana miaka 30 ya
kuwekeza katika mahesabu yake ni kuwa kwa mwaka atakuwa anahitaji TSH 12
milioni ili kuendesha mahitaji yake, sasa tukichukulia kwa mrejesho maarufu wa
uwekezaji ni 10% ina maana ili huyu kijana awe na uweze wa kutumia 12 milioni
kwa mwaka ambayo ni faida basi itambidi awekeze milioni 120 wakati wa
kustaafu au awe na milioni 120 wakati wa kustaafu ili kwamba 10% ambayo ndio
mrejesho wa uwekezaji umuwezeshe kupata milioni 12 kila mwaka bila kuathiri
mtaji wake.

Hatua ya nne

Hatua ya nne ni kujua hii milioni 120 tunaipataje ndani ya miaka 30 ijayo

Sasa kuna njia mbili ambazo tunaweza kuzitumia ili kupata hii milioni 120 baada
ya miaka 30 ambayo ndiyo itatuwezesha kupata milioni 12 ambayo tunaihitaji kwa
ajiri ya kuendesha maisha baada ya kustaafu, njia zenyewe ni kama ifuatavyo
(i) Kuwekeza taratibu taratibu

kama tulivyoona wakati tunajifunza kutumia kikokotozi cha UTT AMIS, kuwa
unaweza kuwa unawekeza kidogo kidogo kutokana na uwezo ulionao na baada ya
miaka 30 ukatimiza hii milioni 120. Tuone mfano

Kwa mfuko wenye mrejesho wa12% kwa mwaka itambidi huyu muwekezaji
awekeze 33,995/= kwa mwezi kwa miaka yote 30 ili baada ya hiyo miaka awe na
milioni 120
Kwa mfuko wenye mrejesho wa 13% itambidi awekeze 27,134/= kila mwezi kwa
miaka 30
Kwa mfuko wenye mrejesho wa 10% itambidi awekeze 52,647/= kwa mwezi ili
kufanikisha lengo lake
(ii) Kuwekeza kwa mara moja

Namna ya pili ni ya kuwekeza kwa mara moja, hapa kama una kiasi cha kuwekeza
kwa mara moja unaweza kuwekeza katika mfuko na ukaendelea na mambo
mengine huku uwekezaji wako unakua, tukirudi katika kikokotozi cha UTT
AMIS tunaweza kupata majibu.
Kwa hiyo kwa mfuko ambao una mrejesho wa 13% kwa mwaka itamuhitaji
awekeze milioni 3 na elfu sitini na saba (3,067,806/=)
Hatua ya tano

Kujua muda ambao unao wa kuwekeza

Kutokana na umri ulio nao na muda ambao unahitaji kustaafu basi unaweza kujua
ni muda gani uliobaki kwa ajili ya kufanya uwekezaji wako na hii itakusaidia
katika kupanga ni jinsi gani uwekeze, katika mfano wetu hapo juu tumeona kuwa
muwekezaji ana miaka 30 na anahitaji kustaafu akiwa na miaka 60 kwa hiyo muda
alio nao kuwekeza ni miaka 30.

Hatua ya mwisho

Hapa ni kuchagua mfuko au uwekezaji ambao unaweza kukutimizia malengo


uliyonayo, hapa utaangalia mfuko unaokufaa kwa upande wa mrejesho wa
masharti ya mfuko.

NENO KUTOKA KWA MWANDISHI

Mahesabu ambayo tumeyapiga katika huu mfano ni ya kufikirika na uhalisia


unaweza kuwa tofauti na mahesabu ambayo tumeyapiga ila kanuni nyuma ya
pazia ni ile ile ya jinsi ambavyo tumefikia katika jawabu letu na ukumbuke kuwa
mrejesho huwa unabadilika kulikana na hali ya uchumi na jinsi sehemu ambapo
UTT AMIS imewekeza inavyofanya kazi.
SEHEMU YA TANO

JINSI BEI YA KIPANDE INAVYOKOKOTOLEWA


Kuna mtu akauliza swali tunajua jinsi bei ya hisa inavyokuwa, je bei ya kipande
kama UTT AMIS ni nani anapanga au wanajuaje leo iwe bei fulani. Ok majibu ni
mepesi sana.Kuna vitu sio lazima kuvijua ili upate faida UTT AMIS ila kama wewe
ni muwekezaji makini kuna vitu ambavyo ni lazima kuvifahamu kwani
vitakuongezea uwanja wa kufanya maamuzi.

Ili kujua bei ya kipande inapigwaje tuanze kwa kutengeneza kampuni yetu
kwanza ya uwekezaji kama UTT AMIS kampuni yetu inaitwa WISE INVESTOR
INVESTMENT COMPANY na inaanza na mtaji wa 1 milioni ambao tunanunua
vipande 1000. Kwa haraka haraka mtaji wa TSH 1 na vipande 1000 ina maana
thamani ya kila kipande ni 1000 na kampuni yetu haina deni

Bei ya kipande ya mwanzoni = 1 MLN/1000 = 1000

Kwa hiyo kampuni yetu inaanza na mtaji wa 1MLN (TSH) na idadi ya vipande ni
1000 na thamani ya kila kipande ni 1000 sasa meneja wa mfuko ambaye ni bro
chagamba anaenda kuwekeza hii hela katika soko la hisa (DSE) na akifika kule
ananunua hisa za CRDB peke yake kwa bei ya 100/= kwa kila hisa na anapata hisa
10000

Kwa hiyo mfuko wetu una hisa 10000 za CRDB na baada ya hapo siku hiyo hiyo
bei ya hisa ya CRDB inapanda kutoka 100/= kwenda 120/= kwa hiyo unaona mfuko
wetu umepanda thamani

Kumbuka hisa zetu tulinunua kwa bei ya 100 na tukawa na hisa 10000 sasa bei
hisa imepanda thamani ina maana mfuko wetu umekua kutoka 1MLN kwenda 1.2
MLN sasa bei mpya ya kipande inakuwaje? inakuwa ni sawa na thamani ya mfuko
kugawanya kwa idadi ya vipande

Bei mpya ya kipande = thamani ya mfuko/ idadi ya vipande

Bei mpya = 1.2 MLN/1000 = 1200/=

Kwa hiyo bei mpya ya sasa ya kipande ni 1200/=, baada ya hapo kesho yake bei ya
hisa ya CRDB inapanda tena inatoka 120/= kwenda 130/=, hapo mfuko wetu
umekua tena kwani hisa zetu zimepanda bei kutoka kutoka 120/= kwenda 130/=

Kwa hiyo jumla ya thamani ya mfuko inakuwa 130/= kuzidisha kwa hisa 10000
ambapo thamani mpya ya mfuko ni 1.3 MLN

Bei mpya ya kipande = 1.3/1000= 1300/=

Baada ya muda CRDB inatoa gawio la 22 kwa kila hisa, na sisi tunapokea gawio
kwa hisa zetu 10000/=

Gawio letu linakuwa 220,000/= ila kumbuka kuna kodi ya zuio tunalipa ya 5%
kwa gawio letu kwa hiyo baada ya kulipa tunabakiwa na 209,000/=

Kwa hiyo mfuko wetu unakua tena kwani tumepata 209,000/= kutoka kwenye
gawio

Thamani ya mfuko wetu inakuwa 1.3 MLN + 209000= 1.509 MLN

Kwa hiyo bei mpya ya kipande inakuwa 1.509 MLN /1000 = 1509/=

Hivi ndivyo bei ya kipande inapigwa sasa hili gawio ambalo tumepokea tunaweza
kuliwekeza tena.
VITU MUHIMU VYA KUKUMBUKA
(i) Bei unayoiona leo sio ya leo bali ni ya jana

Kama una kumbukumbu vizuri bei ambayo tumekuwa tunaitumia kufanya hesabu
ni bei baada ya soko kufungwa. Kwa hiyo bei ya leo ndio utaiona kesho ila bei ya
kesho itapigwa jioni baada ya soko kufungwa na itatolewa kesho kutwa. Maana
kuna watu wanadhani wakiomba kununua leo basi bei wakakayo nunulia ni bei ya
leo hapana, bei utakayonunulia ni ile ambayo itatolewa kesho inayoitwa kwa jina
la kiingereza la FORWARD PRICING

(ii) Baadhi ya pesa inaenda kwenye matumizi

Kama unavyojua kampuni huwa ina matumizi kwa hiyo baadhi ya pesa ambayo
inapatikana kwenye uwekezaji inaenda kwenye matumizi, kwa hiyo usidhani
kama kampuni imepokea gawio basi gawio lote litaenda kuwa thamani ya
kipande, baadhi ya pesa inaweza kupunguzwa na kwenda kwenye matumizi hii
haitaonekan katika thamani ya mfuko

(iii) Ikiwa mfuko una deni basi thamani yake inapungua

katika kupiga mahesabu ya kipande kama mfuko una deni basi tunachukua mali
na kutoa madeni ili kupata mali halizi za mfuko na hizi ndio tunagawanya kwa
idadi ya vipande ili kujua bei ya kipande.
KUSHUKA KWA BEI YA KIPANDE
Kama tulivyoona katika jinsi bei ya kipande inavyopigwa,kama ikitokea katika
mfuko wetu kuna hisa ambayo imeshuka bei basi kinachotokea ni kuwa thamani
ya mfuko inapungua na ikipungua tunavyokuja kupiga hesabu za bei mpya ya
kipande basi utaona kipande kimeshuka thamani mfano

Kama bei ya hisa ya CRDB ilikuwa 130 na thamani ya mfuko ilikuwa 1.3 MLN
ikitokea bei imeshuka mpaka 125 basi na mfuko wetu utapungua thamani kutoka
1.3 MLN kwenda 1.25 MLN kwa hiyo bei mpya ya kipande ni

Bei ya kipande ni 1.25 MLN/1000= 1250/=

Utaona kipande chetu kimesshuka bei kutoka 1300/= kwenda 1250/=

Hii ni moja kati ya sababu inayopelekea kipande kishuke

KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA VIPANDE VYA UTT AMIS


Moja kati ya swali la msingi ambalo huwa nakutana nalo pale ambapo
ninawafundisha watu kuhusu kuwekeza UTT AMIS linakuwa hivi bro chagamba
wewe unatuelekeza kuwekeza UTT AMIS na sisi tunajua mifuko mingi haitoi
gawio sasa ikitokea kipande kimeshuka bei na kikawa na bei ile ile kwa muda
mrefu ninafanyaje?

Kwanza nafahamu huyu mtu ametoa uelewa huu kwenye hisa, kwani katika hisa
kuna kipindi bei ya hisa inaweza kupanda mwaka huu na mwaka ujao ikashuka
zaidi au ikabaki pale pale kwa Muda mrefu. Kwa hiyo mtu wa namna hii
ukimuelekeza kuwekeza UTT AMIS ambako anapata faida kwa ukuaji wa bei ya
kipande anakuwa muoga. Baada ya kufanya uchunguzi nimegundua kuwa bei ya
kipande cha UTT AMIS ijapokuwa inaweza kuwa na kipindi ambacho inashuka
kwa muda ila muelekeo wa jumla ni kuwa bei ya kipande inapanda juu tu haishuki
kama ilivyo katika hisa na hivi ndivyo nilivyofikia katika hitimisho langu.

Kuna sababu 3 ambazo ninadhani zitafanya kipande kiendelee kukua siku hadi
siku:-

1) Maeneo ambayo UTT AMIS imewekeza


2) Jinsi UTT AMIS inavyofanya kazi
3) Uwekezaji mseto

(i) Maeneo ambayo UTT AMIS imewekeza


Kama tulivyoona katika kipengele cha maelezo ya mifuko tumeona hakuna mfuko
ambao una sheria ya kuwekeza katika hisa peke yake bali inawekeza katika hisa
na katika mapato ya kuaminika kama hati fungani za serikali. Kwa hiyo kama jinsi
tulivyoona namna inayochangia bei ya kipande kushuka au kupanda
kunachangiwa na sababu kuu 3 ambazo ni

(ii) Riba kutoka katika hati fungani


Kama tunavyofahamu hati fungani zinalipa riba ya kuaminika na kama tulivyoona
mifuko mingi ina hati fungani za serikali kwa hiyo kila baada ya miezi sita mfuko
unapokea riba na kama tulivyoona mfuko unapopokea riba unaongezeka ukubwa
na hivyo bei ya kipande inaongezeka na kwa muda wote ambao mfuko unakuwa
umewekeza katika hati fungani basi utaendelea kupokea riba na utaendelea na
kukua na hivyo bei ya kipande itaendelea kukua tu siku hadi siku. Mifuko yote ina
sheria ya kuwekeza katika hati fungani kwa hivyo ina uhakika wa kupokea
mapato katika hati fungani na mapato yanavyokuja ndivyo mfuko unaongezeka
ukubwa na bei ya kipande pia inakua tuangalie mfano halisi.
Tuchukulie mfuko ambao umewekeza katika hati fungani pekee na umewekeze
hati fungani ya miaka 25 yenye riba ya 15.95% kwa mwaka. Mfuko huu una TSH 1
milioni ya kuwekeza na una vipande 10,000 na kila kipande kina thamani ya TSH
100 (Hapo tumechukua milioni moja kugawanya kwa vipande 10,000).

Kwa hati fungani ya TSH 1 yenye riba ya 15.95% ina maana kila mwaka mfuko
utakuwa unapokea TSH 159,500/= na hivi ndivyo mfuko wetu utakavyokuwa kwa
miaka 5 ya kwanza kama ilivyo katika jedwali hapo chini, kwa jinsi bei ya kipande
inavyopigwa rejea hapo juu. Hapa inakuwa hivi mwaka wa kwanza mfuko
utapokea 159,500/= na mfuko utakuwa umekua na kuwa na kiasi chaTSH 1,159,500
(milioni moja tuliyoanza nayo na hii ambayo tumeppokea kama riba) sasa bei
mpya ya kipande tunaipata kwa kuchukua thamani mpya ya mfuko kugawanya
kwa idadi ya vipande 10,000 ambapo kwa mwaka wa kwanza bei ya kiapande
inakuwa TSH 115.95/=.

Mwaka Thamani ya mfuko Riba kwa mwaka Bei mpya ya kipande

1 1159500 159500 115.95


2 1319000 159500 131.9
3 1478500 159500 147.85
4 1638000 159500 163.8
5 1797500 159500 179.75

Kama ambavyo umeona ni kupitia jedwali na maelezo hapo juu, mfuko


unapokuwa unapokea mapato ndivyo unavyoongezeka na ukiongezeka bei ya
kipande pia inaongezeka na kwa sababu mifuko imewekeza katika hati fungani
ambazo zinalipa riba yenye uhakika basi tunakuwa na ujasiri wa kusema kuwa
mfuko utaendelea kukua siku hadi siku. Mfano wetu huo ni mfano rahisi kwani
mfuko huwa una matumizi yake pia kwa hiyo sio kila unachokipokea kinaenda
moja kwa moja kwenye kukuza kipande bali kuna sehemu inatumika ili kukidhi
mahitaji ya kila siku ya mfuko kama mishahara ya wafanyakazi na mengineyo.
Hapa tumechukulia miaka 5 lakini kwa kuwa hati fungani ni ya miaka 25 basi
tutaendelea kupokea riba na kukuza mfuko kwa miaka 25. Lakini katika hisa
mambo ni tofauti kwani bei inapangwa na nguvu ya usambazi na ugawanyaji
(demand and supply).

(iii) Gawio kutoka katika hisa


Hiki pia ni chanzo cha mapato kwa mifuko, tuchukulie mfuko uliowekeza katika
hisa za CRDB kwa miaka miwili iliyopita. Kwa mwaka 2019, benki ya CRDB ilitoa
gawio la TSH 17 kwa hisa na kwa mwaka 2020 benki ilitoa gawio la TSH 22 kwa
hisa, maana yake mfuko kwa miaka hii miwili imepokea gawio na gawio
linapopokelewa pia linaongeza ukubwa wa mfuko na ukubwa wa mfuko
unapelekea kuongezeka kwa bei ya kipande. Kwa hiyo, kama kampuni mfuko
utaendelea kuwekeza katika hisa na kupokea gawio basi bei ya kipande itazidi
kuongezeka.

(iv) Kukua kwa thamani ya hisa ambazo mfuko umewekeza


Bei ya hisa inapoongezeka pia thamani ya mfuko inaongezeka na hivyo kufanya bei
ya kipande pia kuongezeka,na hii ndio moja kati ya sababu za mifuko yenye hisa
kuwa inashuka bei pale ambapo bei ya hisa ambayo mfuko umewekeza unashuka.
Lakini hii pia inachangia kukua kwa kipande pale ambapo bei ya hisa
inaongezeka. Kwa hiyo ukichangana vyanzo hivi vya mapato sio kitu kigumu
kuona ni kwa nini mfumo wa bei ya kipande na hisa ni tofauti na ijapokuwa kuna
kipindi bei ya kipande inashuka lakini haiwezi kuwa kama hisa.

Hivyo hata kama UTT AMIS hailipi gawio unaweza kupata faida na pia
unashauriwa uwekeze ukiwa na malengo ya muda mrefu kwani bei ya kipande
inaweza kushuka mwaka huu ila kiujumla bei ya vipande inapanda siku hadi siku
ukiangalia utendaji wa mifuko hii toka inaanzishwa utagundua kuwa
ninachokisema ni sahihi na hii ni sababu moja ngoja tuangalie sababu nyingine.
JINSI UTT AMIS INAVYOFANYA KAZI
Ukifahamu jinsi UTT AMIS inavyofanya kazi basi hofu ya kuwa kipande
kitashuka kama ilivyo kwenye hisa na utapata hasara inapungua. Tumeona katika
kipengele kilichopita cha mapato ya UTT AMIS kuwa ina sehemu ambayo
inapokea mapato ya kuaminika kama riba ya hati fungani na gawio sasa kitu
kinachoongezeka hapa ni kuwa pesa inayopokelewa pia inawekezwa na hivyo
kufanya mfuko kukua kwa kasi zaidi kwani wanatumia riba ya kampaundi. Ngoja
nitoe mfano wa mfuko ambao unapokea riba na gawio uone kwa nini kwa mjengo
huu wa ufanyaji kazi basi bei ya kipande itaendelea kukua siku hadi siku:-

Mfano

Tuchukulie mfuko ambao umewekeza katika hati fungani kwa mwaka 2019 na
2020. Mfuko huu una ukubwa wa TSH 2 milioni na idadi ya vipande ni 10,000 na
bei ya kipande TSH 200/=. Milioni moja imewekezwa katika hisa za CRDB kwa
bei ya 100 ambapo mfuko utakuwa na hisa 1,000,000/= na nyingine katika hati
fungani ya miaka 25 yenye riba ya 15.95%.

Kwa mwaka 2019 CRDB ilitoa gawio la 17 kwa hisa ambapo kwa hisa 10,000
mfuko ulipata 170,000/= kutoka katika hati fungani mfuko ulipokea 159,500/=.
Jumla ya thamni mpya ya mfuko itakuwa 2,329,500/= na bei mpya ya kipande
itakuwa TSH 232.95/= sasa kinachokuja kuweka utofauti ni kuwa hii pesa
iliyopatikana inawekezwa tena ili mwaka unaokuja faida iwe kubwa zaidi na
hivyo kufanya mfuko uwe na faida ya riba ya kampaundi.

Tuchukulie faida ya mwaka 2019 ilitumika kununua hisa za CRDB kwa bei ya 100,
hivyo mfuko sasa utakuwa na hisa 13,295. Mwaka 2020 CRDB ilitoa gawio la TSH
22/= kwa kila hisa hivyo mfuko ulipokea TSH 292,490/= na kutoka katika hati
fungani, mfuko ulipokea TSH 159,500//= kwa hiyo mfuko utakuwa na kuwa na
thamani ya TSH 2,451,990/= na hivyo kufanya bei ya kipande kuwa TSH 245.199/=

Sasa huu mtindo wa kuwekeza hela ambayo inapatikana kila mwaka ni moja kati
ya sababu ambazo zinafanya mfuko ukuze thamani ya kipande kwa siku hadi siku.

(i) Uwekezaji mseto


Kupanda na kushuka kwa bei ya hisa ni moja kati ya sababu inayofanya bei ya
kipande kuwa inashuka na kupanda mara kwa mara, sasa UTT AMIS huwa
inatumia uwekezaji mseto kwa maana hiyo. Madhara ambayo yanayoweza
kufanywa na kushuka kwa bei ya hisa moja yanaweza kumezwa na hisa nyingine
ambayo imepanda bei na hivyo kufanya bei ya kipande kutoshua sana. uwekezaji
mseto ni moja kati ya vitu ambavyo vinapunguza uwezekano wa bei ya kipande
kushuka kama jinsi bei ya hisa husika inavyoshuka.

Ukichukua sababu hizo tatu ni rahisi kuona kuwa bei ya kipande haiwezi
kushuka na kukaa hapo hapo kwa miaka kadhaa kwani mapato mengine kama
hati fungani na gawio la hisa yanasaidia kukuza bei ya kipande na hata kama bei
ya hisa ambayo mfuko umewekeza inaweza kushuka. Kama tulivyoona
mchanganuo wa sehemu ambayo mifuko hii imewekeza utaoa hisa haina asilimia
kubwa sana na hivyo kufanya kinachotokea katika hisa kutokuwa na madhara
makubwa kwenye bei ya kipande. Ukiangalia muenendo wa bei za vipande kwa
miaka iliyopita unaweza kuona ya kuwa hili ni sahihi.

Angalizo

Kuna miaka bei ya kipande inashuka katika baadhi ya mifuko kutokana na hali ya
uchumi kwa hiyo kama muwekezaji unatakiwa kulifahamu hili.
(ii) Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Swali: Je ninaweza kuwa na akaunti katika mifuko zaidi ya mmoja, yaani nikawa
na umoja, jikimu na liquid au mfuko mwingine

Jibu: NDIYO, ila kila mfuko utakuwa na akaunti yake, siyo kama hisa kuwa
akaunti moja ya DSE inakuwa na hisa zaidi ya moja, hapa ukitaka kuwa na mfuko
mwingine unafungua akaunti ya mfuko husika.

Swali: Katika hisa mtu anapata faida pale ambapo ananunua hisa kwa bei ya chini
na kuuza bei inapopanda je kwa vipande vya UTT AMIS ikoje

Jibu: Unaweza kununua pale ambapo bei ya kipande imeshuka, hasa hasa kwenye
mifuko yenye hisa ila kutokana na masharti ya mifuko na pia uendeshwaji wa
mifuko ni ngumu sana kuona poromoko la bei ya vipande kama ilivyo hisa na pia
kama tulivyoona bei ya kipande kwa asilimia kubwa inapanda mwaka kwa
mwaka hivyo sio rahisi kununua bei ikiwa chini na kuuza tena kama ilivyo katika
hisa ijapokuwa bei ya kipande kuna kipindi inashuka

HATARI ZA JUMLA ZA UWEKEZAJI KATIKA MIFUKO


Hizi ni hatari za uwekezaji ambazo unaweza kukutana nazo endapo unakuwa
umewekeza katika mifuko hii ya uwekezaji wa pamoja

a) Bei ya hisa ambazo mfuko unamiliki zinaweza kupanda au kushuka


thamani

hii ni kwa mifuko ambayo imewekeza katika hisa ya kuwa bei ya hisa inaweza
kupanda au kushuka na hivyo kuathiri thamni ya mfuko

b) Ukwasi wa hisa ambazo mfuko umewekeza unaweza kuwa mdogo


Kama umewekeza katika hisa utafahamu ya kuwa kuna kipindi baadhii ya hisa
zinakuwa na ukwasi mdogo sana na hivyo inaweza kuathiri mfuko pale ambapo
mfuko unataka kuuza hisa ambazo unamiliki

c) Badiliko la kodi

Kuna faida nyingi ambazo UTT AMIS inazipata kwenye upande wa kodi kwanza
katika sehemu ambazo imewekeza na pili kwa wawekezaji ambao wamewekeza
UTT AMIS, ukiwekeza katika soko la hisa kwa sheria za sasa ni kwamba gawio
utakalopokea litakatwa kodi ya 5% ambayo ni unafuu kwa makampuni yaliyoko
soko la hisa ikitokea serikali ikabadilisha sheria ya kodi itaathiri mapato ya mfuko
na pia katika hati fungani za serikali za muda mrefu kuna unafuu wa kodi kama
sheria itabadilika basi na mapato ya mfuko yatabadilika. Kitu kingine ni kodi kwa
upande wa muwekezaji wa UTT AMIS, kwa sasa hakuna kodi anayotoa ila sheria
zinaweza kubadilika siku zijazo.

d) Riba ambayo inapokelewa na mfuko kutokakatika hati fungani na


amana nyingine zinaweza kubadilika

Hapa tunazungumzia hati fungani na amana za kibenki, kwa kuwa sehemu ya


mapato ya mifuko yanatoka katika hati fungani ikitokea riba inayotolewa na hati
fungani ikapungua basin a mapato ya mfuko yatapungua pia

e) Sababu nyingine ambazo zinaweza kuathiri uwekezaji wa mifuko hii na


hivyo kuathiri bei ya kipande
Sehemu hii imeachwa wazi
SEHEMU YA SITA

SAIKOLOJIA NA UWEKEZAJI

JE MIAKA 30 NI MINGI KUWEKEZA

Nimekutana na awatu ambao ukiwaambia kuwa wewekeze na kuvuna uwekezaji


wao kwa miaka 30 wanaona kama ni kitu ambacho hakiwezekani kwani miaka 30
inaonekana ni mingi mno. Kitu ambacho wanashindwa kujua ni kuwa mika 30
ijayo kama utakuwa hai itafika tu, bali kitu cha msingi ni kuwa itakukuta katika
hali gani.

Kama ni mchunguzi ukiangalia nyuma muda ambao umeshakaa duniani umepita


bila hata wewe kuwa na taarifa na ghafla ukajikuta una miaka 20 au 30 au 50 na
ukae ukijua kuwa miaka 30 ijayo itapita kwa namna hiyo hiyo.

Watu wengi wanatamani sana kuwa na pesa nyingi kwa haraka zaidi kitu
ambacho sio kibaya ila sio watu wengi wenye njia ambazo zinaweza kuwafanya
wakapata pesa nyingi kwa haraka ila njia ambazo zinawafaa kutokana na maisha
yao ni njia kama hizi za kuwekeza kwa muda mrefu ila wengi huwa hawazitilii
mkazo na miaka inaenda na kurudi na mwisho wa siku wanakosa ile pesa nyingi
ambao walidhani wangeipata kwa haraka na wanakosa hii pesa nyingi ambayo
ingekuja taratibu.

Kwa hiyo wewe uwe na hekima, ukipata njia ya kukuwezesha kupata hela kwa
haraka ni vizuri ila ukiwa na nafasi ya kuwekeza taratibu hii pia ni njema, kwani
njia zote zitakuletea fedha na pesa ikipatikana siku zote itapata matumizi hata
kama itakuja nyingi kiasi gani.
Tumeona kuwa kupitia UTT AMIS unaweza kuwa unawekeza kidogo kidogo
kwa siku nyingi na ukaja kupata milioni 100 mpaka bilioni, kuna watu watapuuzia
kwa kusema miaka 30 ni mingi sana ila ninakuhakikishia kuna wengi ambao
wanasoma kitabu hiki ambao watafika miaka 30 ijayo na bado watashindwa kuwa
na milioni 100 ambayo kama wangewekeza UTT AMIS wangeipata.

Miaka 30 sio mingi kwani ukianglia hata hii pensheni ambayo wastaafu wanapata
unakuta wameichangia kwa miaka 30 au zaidi sasa kwa nini ushindwe kuwekeza
wewe mwenyewe.
SEHEMU YA SABA

MADA YA ZIADA KUTOKA KATIKA KITABU CHA NAMNA BORA YA


KUWEKEZA KATIKA SOKO LA HISA

JIFUNZE KUJILIPA WEWE KWANZA


Moja kati ya vitu ambavyo nilijifunza ambavyo vilibadilisha maisha yangu ni
kujifunza kujilipa mimi kwanza. Nimekutana na watu wengi ambao ukimwambia
kuwekeza anakuona kama wewe ni mshamba au anakwambia mimi sina hela ya
kuwekeza. Nikueleze kuwa kuna umuhimu wa watu wote kujua umuhimu wa
kujilipa wenyewe kabla ya kulipa watu wengine kwanza. Suala la kujilipa
mwenyewe linafanyika kwa kuwa na kiasi fulani cha fedha unachokitenga kutoka
kwenye kipato chako ili kuwekeza kwa ajili yako kwa siku za baadae. Suala hili
litakusaidia kupambana na umaskini au kuondokana na umaskini katika siku za
mbeleni.

Nitatoa mfano huu unaokaribiana na ukweli kuhusu umuhimu wa kujilipa


mwenyewe. Chukulia mfano wa watu wawili waliotoka nyumbani au ndani kwa
ajili ya kwenda kuteka maji katika bomba la maji. Ikatokea mmoja ana ndoo au
chombo cha kutekea maji kilicho na matundu mengi na mmoja akiwa na chombo
chake kilicho kizima. Wote wanateka maji bombani, lakini mmoja anateka maji
kwenye ndoo mbovu na hivyo maji yanakuwa yakimwagika chini. Baada ya muda
utaona yule mwenye chombo kizima taratibu kikiwa kinajaa wakati mwenye
chombo kibovu anakuwa hajazi au haongezi maji kwa kiasi. Hii inaibua swali, je
ikitookea maji yakakatika, je ni nani atabakia na maji?
Unapopokea au kupata fedha kutoka kwenye mshahara au chanzo chochote cha
pesa na unaitumia kwa matumizi ya kula na matumizi mengine ya kawaida
ambayo ni muhimu baada ya hapo pesa inaisha unasubiri wakati mwingine kupata
kipato kingine tena. Hii unakuwa unajitengenezea umasikini kwani ili uweze
kuendelea kuishi lazima chanzo hicho kiendelee kuwepo siku hadi siku. Ikitokea
kwa sababu yoyote ile chanzo hicho kika katika basi hapo ndio mwanzo wa
matatizo ya kifedha yanaweza kukukumba.

Ngoja nikupe mfano mwingine ambao unaweza kuuelewa, umejifunza kusoma


ripoti ya hali ya fedha na ripoti ya mapato na matumizi. Unapotoa pesa mfukoni
kuitumia kununua chochote hiyo pesa inakuwa katika fungu la matumizi sasa
tuchukulie una shilingi 1000/= hii pesa mtu mmoja akaamua kununua soda kubwa
ya 1000/= hii pesa inatoka mfukoni mwake inaenda kwa muuzaji wa soda na
inaondoka jumla hairudi tena mfukoni mwako.

Kama huyu mtu ataamua kununu hisa za 1000/= hii pia itakuwa kama matumizi ila
utofauti wake ni kuwa hii pesa haijatoka mfukoni mwake bali inaenda kuwa
MALI ambayo utaikuta katika ripoti ya hali ya fedha na kama unavyojua mali
huwa ndio inazalisha mapato. Sasa utofauti wa watu hawa wawili ni kuwa
aliyenunua soda amemtajirisha muuza soda ila aliyenunua hisa amejitajirisha
mwenyewe kwani hizi hisa zitaendelea kuwa kwake na kuendelea kuzaa pesa
zaidi na kama akifanya hivi kwa miaka 10 atafika kipindi cha kuwa na vyanzo
viwili vya mapato kimoja ni kile cha kila siku na kingine ni hisa ambazo
ametengeneza ila yule ambaye alikuwa anakunywa soda ni muuza soda tu ndio
anakuwa ametajirika.

Kwa hiyo unavyojenga utaratibu wa kujilipa kwanza wewe kwa kununua


uwekezaji iwe hisa au kitu kingine, unakuwa umejenga tabia ya kujitajirisha
mwenyewe lakini kama hauna utaratibu wa namna hii, basi utaendelea kuwa na
chanzo hicho kimoja tu.

Sijasema usitumie pesa kwenye matumizi mengine ila jifunze kujilipa kwanza na
hiyo iwe ndio aina ya maisha unayoishi. Utatengeneza utajiri bila jasho. Mtu
anayetumia hela kununua uwekezaji hana utofauti na mtu ambaye amechukua
fedha mfuko wa kushoto na kuiwekza mfuko wa kulia ambapo inaweza kuzaa
tena.

JINSI YA KUANZA KUWEKEZA UTT AMIS


Jinsi ya kuanza kuwekeza UTT AMIS ni rahisi mno, na unaweza kuanza
kuwekeza kwa njia zifuatazo

(i) Kwa njia ya simu

Kama una simu unaweza kubonyeza *150*82# na baada ya hapo utafuata


maelekezo ya kufungua akaunti kwa mfuko wowote unaoupenda na utafungua na
kupewa akaunti namba ambayo unaweza luanza kuwekeza mara moja

(ii) Kutembelea tawi lolote la CRDB benki au mawakala wake

Ukitembelea tawi lolote la benki ya CRDB popote Tanzania utapata huduma ya


kufungua akaunti na pia kama unataka kununua vipande unaweza kuanza
kununua vipande moja kwa moja.

(iii) Kupitia mawakala wa soko la hisa la DSE

Mwakala wote wa soko la hisa la DSE wanaweza kukufungulia akaunti na


ukaanza kuwekeza moja kwa moja.

(iv) Tembelea ofisi yoyote ya UTT AMIS


Huduma ya kufungua akaunti na kuwekeza unaweza kuipata katika ofisi za UTT
AMIS popote zilipo

Tanbihi

Unapofungua akaunti kwa njia ya simu itakuruhusu kuwekeza tu kwani unakuwa


haujakamilisha usajiri, ukitaka kukamilisha usajiri itakubidi upakue fomu ya
kukamilisha usajiri na uijaze na kuituma UTT AMIS au unaweza kuwaona
mawakala wak soko la DSE, tawi lolote la CRDB au ofisi za utt amis kwa ajili ya
kukamilisha usajiri. Baada ya kukamilisha usajiri utaruhusiwa kuuza vipande
vyako, ila kama utasajili kwa njia ya simu pasipo kukamilisha usajiri utaruhusiwa
kununua vipande tu na sio kuuza vipande.

HITIMISHO

Natumaini umejifunza mambo mengi sana katika kitabu hiki sasa ni wakati wa
kuyafanyia kazi yote uliyojifunza nikutakie kila la heri katika safari yako ya
uwekezaji na mafaniko katika uwekezaji wako

You might also like