Mgina Agri-Business company limited iko kwenye Facebook.
Ili kuunganisha kwa
Mgina Agri-Business company limited, jiunge kwenye Facebook leo.
Jiunge
au
Ingia
Mgina Agri-Business company limited
8 Aprili 2019 saa 17:42 ·
FAIDA ZA STRAWBERRY MWILINI
Matunda haya ya strawberry yana faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja nafaida za kiafya. Faida hizo ni kama ifuatavyo Hutunza ngozi ya mwili ( anti-aging skin) Huimarisha mifupa ( bone care) Hupunguza madhara ya presha ya kupanda na kushuka( hype – tension) Ina madini yanayohitajika kwa mama wajawazito na ukuaji wa mimba ( natal care) Kinga na afya ya mzunguko wa damu Kinga ya baadhi ya saratani Inasaidia kuponya jeraha kwa haraka Inasaidia kupunguza uzito kwa wale wenye uzito mkubwa Inasaidia kuongeza kumbukumbu Inasaidia kuongeza nguvu na muamko wa kufanya mapenzi strawberry zina madini ya zink kwa wingi ambayo husaidia zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanaume. Hivyo, katika bustani yako unaweza kupanda miche kadhaa kwa ajili ya afya yako na familia yako pia. Mbali na faida kwa mfumo wa uzazi, berries vitamini C huongeza nguvu wa mfumo wa kinga na magonjwa, kuimarisha mwili. Ni matunda muhimu sio tu kwa wanaume, bali pia kwa wanawake. Wakati wa ujauzito, MATUMIZI: Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo. Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na: Kuliwa kama tunda. Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula. Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi. Kutengeneza marashi n.k. UKIITAJI KITABU CHA KILIMO BORA CHA STRAWBERRY WASILIANA NASI 0657420067 AU 0688468809 HARDCOPY SH 15000 SOFTCOPY SH 5000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP PIA TUNAZALISHA MICHE YA STRAWBERRY MCHE MMOJA SH 1500 BY FRANK E MGINA 0657420067 Mgina Agri-Business company limited iko kwenye Facebook. Ili kuunganisha kwa Mgina Agri-Business company limited, jiunge kwenye Facebook leo.
Jiunge
au
Ingia
Chapisho la Hivi karibuni kwa Ukurasa
Mgina Agri-Business company limited
Jana saa 12:46 ·
KUUNGANISHA MICHE YA PARACHICHI NA MATUNZO YAKE
MCHE ULIOUNGANISHWA Sehemu mbili za mimea ya jamii moja (muembe kwa muembe, mparachichi kwa mparachichi) au miche ya aina tofauti kidogo ila jamii moja (mchungwa kwa mlimao) ndiyo inayoweza kuunganishwa au kubebeshwa. Hii huusisha sehemu muhimu mbili: Sehemu ya shina (mche shina) ambayo hutokana na kuotesha mbegu za mmea ulichaguliwa kuwa mmea shina. Sehemu ya tawi (kikonyo) huchukuliwa kutoka mti mama wenye sifa za kuzaa matunda mengi na yaliyo bora, ambayo ndiyo yanayotakiwa kama zao. FAIDA ZA KUUNGANISHA/KUBEBESHA MICHE Mche uliyounganishwa kwa kutumia kikonyo au kitawi kilichochukuliwa kutoka kwa mche mama uliokwisha zaa, utazaa matunda mapema. Kwa mfano parachichi hutumia miaka 2 na nusu had 3 kuaanza kuzaa matunda badala ya miaka 8 had kumi kwa miti ya kienyeji. Mche uliounganishwa unadumisha/endeleza sifa halisi ya mmea mama ambao kikonyo chake kimetumika kwenye kuunganisha. Kuunganisha mche kunatoa nafasi ya kutumia mimea shina ambayo inauwezo kwa mfano wa kuvumilia ukame, magonjwa na ama hali ya udongo ambayo mmea tawi usingeweza kuvumilia Mimea inaweza kuunganishwa kwa sababu mbalimbali zingine. Kwa mfano kuna aina ya mimea ambayo haina uwezo wa kutoa mbegu (ndimu zisizo na mbegu, machungwa yasiyo na mbegu). Miche inaweza kuunganishwa kwa sababu za kudhibiti magonjwa au wadudu, Pia miti iliyounganishwa itakuwa na umbile dogo endapo mmea shina una asili ya kuwa na umbile dogo. NJIA ZA KUUNGANISHA MICHE Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika katika kuunganisha miche. Njia hizi zimegawanya kufuatana na aina ya kikonyo kinachotumika katika uunganishaji.
Kuunganisha kwa kutumia kijicho (budding)
Kuunganisha kwa kutumia kitawi / kikonyo (grafting). Njia hizi zote zinaweza kuwa bora lakini ubora utategemea zaidi aina ya miche inayounganishwa. Kwa mfano katika hali ya kawaida miche ya jamii ya michungwa inashika vizuri unapotumia kijicho kuliko kitawi, wakati uunganishaji ITAENDELEAAA............ UKIITAJI KITABU CHA KILIMO BORA CHA PARACHICHI WASILIANA NASI 0784161464 AU WHATSAPP NO 0657420067 HARDCOPY SH 10000 SOFTCOPY SH 5000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP