You are on page 1of 8

MRADI WA MBOGA YA MAJANI AINA YA TEMBLE

UTANGULIZI WA MBOGA ZA MAJINI KWA UJUMLA


Kilimo cha mboga za majani hutegemea sana utunzaji wake na inafaida nzuri. Mboga za majani
zipo za aina nyingi kama vile tembele, sukuma wiki, spinachi, mnafu, mchicha, chainizi na
nyingine nyingi. Katika aina hizi za mboga za majani, watu wengi hupendelea tembele, sukuma
wiki aina ya leshu pamoja na mnafu, mchicha na sukuma wiki aina ya koladi.

Uzalishaji wa mbogamboga hapa nchini Tanzania bado ni mdogo sana ukilinganisha na mazao
mengine kama vile nafaka na matunda. Hata hivyo mbogamboga nyingi zinazozalishwa ni kwaajili
ya soko la ndani ya nchi na haswa pale ambapo zinazalishwa. Mbogamboga husafirishwa kuunzwa
nje kwa kiasi kidogo sana.

Hata hivyo mboga za majani huzalishwa sana maeneo ya mwinuko na ukanda wa pwani na nyanda
za juu, haswa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Mbeya, Morogoro na Iringa. Mbogamboga
zinazozaliswa ili kusafirishwa nje ya nchi hufanywa na sekta binafasi haswa shirika la WIMBO
kupitia mashamba yao za uzalishaji. Mbogamboga zinazosafirishwa nje ya nchi na kampuni hiyo ni
Maharage ya kijani (Green beans, peas, courgettes chillies, baby corn, baby carrots and baby leeks.)
Kwa mfano kwa mwaka 2006/2007 waliweza kuzalisha na kusafirisha tani 1666.48 na 1500.

Mradi wa mbonga za majani utajikita zaidi katika uzalishaji wa tembele kwa wingi. Aina hii ya
mboga ya tembele zinasifa ya kukaa shambani kwa muda mrefu usiopungua miezi sita hadi nane
toka zianze kuchumwa.

AINA ZA MBOGAMBOGA
Mboga za majani zimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni;
i. Mizizi kama vile karoti, vitunguu nk
ii. Majani kama vile tembele, mchicha, sukuma wiki, nk
iii. Matunda kama vile biringanya, ngogwe na bamia.

Sehemu za mmea ambazo zinaweza kutumika kama mboga ni kama zifuatazo.


I. Majani: Mboga nyingi hutoka kwenye majani ya mimea. Mara nyingi haya majani huwa ya rangi
ya kijani kwasababu ya kutengeneza chakula cha mmea kutoka kwenye mionzi ya jua na huwa na
virutubisho vingi muhimu katika mwili wa binadamu kwa vile vitamin. Miongoni mwa majani
ambayo huliwa kama mboga ni tembele, Kabichi, Spinach, Chinese, Mchicha na figiri na nyingine
nyingi.

II. Mizizi: Mizizi ya baadhi ya mimea ni mboga nzuri na ina virutubisho kama vile vitamin A
ambayo huimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Miongoni mwa mizizi ambayo huliwa
kama mboga ni karoti.

III. Tunda: Tunda kwa maana ya kibustani ni sehemu ya mmea ambayo hubeba mbegu na inalika
ikiwa mbichi au imepikwa. Mfano wa mimea ambayo sehemu ya tunda ni mboga ni kama vile
nyanya, matango, bilinganya na bamia.

IV. Bulb (Tunguu): Hii ni sehemu ya mmea ambayo hukua chini ya ardhi kwa mfano vitunguu (maji
na swaumu). Mboga za aina hii ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwani husaidia
kusafisha damu na huongeza ladha na harufu nzuri katika chakula.

V. Tuber (Kiazi): Hii ni aina ya mboga ambayo ni mzizi unaohifadhi chakula cha mmea. Aina hii ya
mboga husaidia kujaza tumbo na kufanya usihisi njaa haraka. Mfano wake ni viazi (mviringo na
vitamu).
VI. Nyinginezo: Sehemu nyingine za mmea ambazo hutumika kama mboga ni pamoja na jicho la ua
(cauliflower), mbegu (kunde na maharage), shina (tangawizi), chipukizo/kimea (majani ya kunde,
soybean).

UMUHIMU WA VYAKULA VYA JAMII YA MBOGA MBOGA MWILINI HASWA


TEMBELE (KIAFYA)
Watu hushauriwa kula vyakula vya jamii ya mboga mboga kwa wingi. Sababu kubwa ni kutokana
na faida za kiafya ambazo huletwa kutoka kwenye mboga mboga ambazo haziwezi kupatikana
kutoka kwenye vyanzo vingine. Mboga zina vitamins na madini (minerals) kama vile potassium,
vitamin A & C hupatikana kwa wingi kwenye mboga mboga na huhitajika mwilini kila siku ili
kuusaidia kuwa na afya na kuweza kukinga au kuzuia maradhi. Virutubisho vingine husaidia
kukinga moyo na figo dhidi ya maradhi na huzuia kansa.
Mboga ya majani aina ya tembele inafaida kubwa sana kiafya kwani ni chanzo kizuri sana cha
kuongeza damu ambapo hushauriwa sana na wataalamu wa afya kwa wale wenye upungufu wa
damu na kina mama wajawazito. Pia kusaidia kupambana na magonjwa kwani zinaipa
chembechembe nyeupe nguvu.

FAIDA ZA TEMBELE KIAFYA


Kwa mujibu wa https://mabibosokoni.com/index.php/product/tembele/ tembele linafaida zifuatazo
kiafya;

i. Tembele husaidia kupunguza msukumo mdogo wa damu (Lowering Blood Pressure) hii ni
kutokana na uwepo wa kalshamu kwa wingi ambayo kiafya husaidia sana kupunguza shinikizo
dogo la damu.

ii. Husaidia kuimarisha mifupa na kuipa mifupa afya njema. Uwepo wa vitamin K husaidia
kuimarisha mifupa na kuiboresha mifupa. Husaidia kufyozwa kwa kalishim kwenye mifupa na
kuuimarisha na kupunguza kalishim kwenye mkojo.

iii. Husaidia kuimarisha ngozi na nywele. Tembele pia lina vitamin A kwa wingi ambayo husaidia
uzalishaji wa mafuta kwenye vitundu vya ngozi na vya vyele hivyo kuimarisha ngozi na nywele za
mtumiaji wa matembele ambapo huipa unyevunyevu ngozi na nywele.

iv. Husaidia kwenye umengenyaji wa chakula tumboni. Tembele limeshehena vinyuzinyuzi na maji
mengi ambayo huteleza. Vivyuzinyuzi hivyo pamoja na maji yake husaidia sana kwenye
mmengenyo wa chakula tumboni na kuondoa tatizo la choo kuwa kigumu (constipation). Hivyo
watu wengi hushauriwa kutumia tembele kwa kila mlo wanautumia kila siku.

Kiuchumi, mboga ya majani haswa tembele husaidia kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na
kusaidia kukuza uchumi wa mtu moja, familia hata uchumi wa taifa. Katika eneo la kilimanjaro na
baadhi ya mipaka ya nchi jirani kama vile Kenyea, mboga ya tembele imepata umaarufu mkubwa
kwani ni kati ya mboga zinanunuliwa sana na lina somo la uhakika.

MALENGO
Malengo makuu ya mradi huu wa uzalisha wa tembele ni kuongeza kipato pamoja na kuzalisha
tembele kwa kiwango cha hali ya juu bila kutumia madawa ya viwandani ili kuboresha afya za
walaji. Hata hivyo tembele halina wadudu wangi wanaolishambulia.

MAONO.
Maono ya uzalisha wa tembele ni kuhudumia jamii kubwa kwa mboga bora za tembele ili kukuza
afya ya jamii na kuongeza pato na hata kuuza nje ya nchi haswa Kenya. Hata hivyo kuwa na naona
ya kuwa na kampuni hapo baadae
MALENGO MAHUSUSI.
1. Kuzalisha aina ya mboga ya majani ambayo ni tembele kwa kiwango cha juu.
2. Kukuza pato la familia.
3. Kuhudumia jamii mboga ya majani ambayo ni tembele isizo na sumu wala kutumia viwatilifu
vya viwandani.
4. Kuwa na kampuni ya uzalishaji wa mboga za majani kanda ya kaskazini.

MUUNDO WA UZALISHAJI
Ninategemea kuwa na aina ifuatayo ya utawala pamoja na uongozi.
I. Meneja
II. Mshauri wa kilimo
III. Mshauri wa rasilimali fedha
IV. Wafanyakazi.

UMILIKI WA MRADI.
Mradi huu wa mboga ya tembele utamilikiwa na mimi mwenyewe kwa kuzingatia kanunu
nilizojiwekea ili kushirikiana na asasi nyingine kwaajili ya kutoa zao bora la kilimo cha tembele.
Hata hivyo, nategemea kuwa na kampuni yangu binafsi ambayo kwa baadae naweza kuipa jina la
“TEMBELE ONE”

MAELEZO YA MRADI.
Mradi huu wa uzalishaji wa mboga ya tembele ni wazo lilioanzia mbali kwa kuanza kununua na
kuzalisha tembele kwa kiwango kidogo. Hata hivyo niliweza kufanya tafiti za kujua faida za mboga
ya tembele kiafya na kiuchumi. Mrahi huu wa mboga ya temble ni kati ya miradi inayogharimu
mtaji wa fedha chache na una faida kubwa kiuchumi. Katika jamii inayotuzunguka ni bidhaa adimu
na inayohitajika kwa wingi. Hata hivyo mboga ya tembele zinatoa ajiria isiyo rasmi kwa mtu binafsi
kwani ninaweza kuzalisha mboba nyingi ya tembele na yenye viwango vya hali ya juu.

Zipo changamoto nyingi katika uzalisha wa mboga ya tembele. Kati changamoto nyingi kubwa ni
upatikanaji wa eneo la kudumu la kuzalisha mboga. Changamoto nyingine ni kutafuta soko la
uhakika la mboga ya tembele kwani baadhi ya wachuuzi huweza kuwakandamiza wauzaji kwa
kununua kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu. Hata hivyo kwa kufuata ushauri wa wataalamu
wa kilimo ninaweza kupambana na changamoto hizo, kwani kwa muda mrefu nimefanya biasha ya
kuuza tembele na nimekuwa na soko maeneo mengi haswa Kilimanjaro, Arusha, Tanga na hata nchi
jirani ya Kenya.

Mradi huu utatekelezwa kwa kushirikiana kwa pamoja na wataalamu wa kilimo ili kuufanikisha.
Hata hivyo, nategemea kupata fedha za mkopo kwenye taasisi za kukopesha kwa riba nafuu ama
bila riba, ili kunisaidia kuundesha mradi huu kwa urahisi. Mradi huu utatumia ghamara ndogo ama
za wastani ukilingalisha na faida itakayopatikana. Faida hutegemea sana uzingatiaji wa kanuni bora
za kilimo cha mboga za majani na haswa tembele na matumizi sahihi ya mbole pamoja na
kupambana na wadudu.

UTEKELEZAJI WA MRADI.
Mradi huu utakamilika kwa kukusanya vifaa vyote vinavyohitajika ili kuwa na uhakika wa
uzalishaji mzuri wa mboga ya tembele. Hapa ninategemea kutafuta fedha za kununulia vifaa
mbalimbali vinavyohitajika na fedha ya kuendesha mradi.

MATOKEO YA MRADI HUU.


Ninategemea baada ya miezi mitatu nitaanza kupata mazao ya kwanza. Nunagegemea kukusanya
mapato yote na kutoa gharama za uendeshaji na baada ya miezi mitatu (3) ya uzalishaji ama miezi
sita (6) baada ya kuanza mradi nitafanya tathmini ya hasara na faida. Tathmni hii itatusaidia kupata
mwelekeo wa mradi na kusaidia kuuboresha mradi huu wa mboga ya tembele kwaajili ya kuweza
kutoa bidhaa bora zaidi na kutengeneza faidi kubwa zaidi kwa kukuza soko la mboga ya tembele.
Hata hivyo ninategemea baada ya miezi sita (6) ya uzalishaji nitafanya hesabu na kuweza kurejesha
kidogo kidogo fedha niliyokopa na kuweza kugawa sehemu ya faida ya mradi huu kutumia ili
kupunguza makali ya maisha.

Katika mradi huu ninahitaji vifaa vya kutendea kazi na vitaainishwa katika bajeti ya mradi huu. Pia
nitakuwa na kitabu kidogo cha muongozo wa jinsi ya kutekeleza mradi huu ambacho pia kitaainisha
majukumu ya kila siku. Vile vile mradi huu utakuwa na urefu wa kipindi cha mwaka mmoja. Baada
ya mwaka nitakaa na kufanya tadhmini ya jumla kuangalia hasara na faida na kulipa fedha zote
nilizokopa na kugawana faida na kuhifadhi mtaji pamoja na kuboresha kwa mwaka mwingine kwa
kutumia mfumo wa vikao na makubaliano na taasisi zilizonikopesha fedha ya kuendesha mradi huu.
Pia kuingia kwenye mkataba wa muda mrefu na wenye mashamba ili kuongeza eneo la uzalishaji
kutoka heka moja kwenda heka mbili.

RASIMALI WATU.
Mradi huu unahitaji rasilimali watu wa aina nne;

I. Wafanyakazi wa bustani ambao watakuwa na kazi ya kulima shamba, kuandaaa matuta, kupanda
mboga ya tembele, kupiga dawa na huduma za kupalilia bustani zikiwemo shughuli zingine
zitakazojitokeza. Tunategemea kutafuta mtu mmoja mwenye uzoefu na uelewa wa kawaida wa
bustani na kumpa elimu kidogo juu ya utunzaji wa matembele.

II. Wataalam wa kilimo. Kundi hili tutasaidiana kwa pamoja na marafiki ambao ni mabwana
shamba pamoja na kusoma nyaraka kwenye mitandao ya intanet ili kufanisha kazi hii. Aidha
ninategemea uzoefu wangu ili kufanikisha mradi huu. Wataalamu wa kilimo watahitajika mara
mbilia au moja kwa mwezi. Wakati wa upandaji wa mbegu, wakati wa ukuzaji na wakati wa
uvunaji ili kuratibu ubora wa shamba na mazao yaliyopo shambani.

III. Wataalam wa masoko. Katika kundi hili nitashirikiana kwa pamoja na baadhi ya watu pamoja
na kutumia uzoefu wangu ili kujadili upatikanaji wa soko la uhakika na jinsi ya kusambaza mboga
za ya tembele kwa uhakika zaidi.

IV. Mtaalamu wa hesabu. Ninao uzoefu mdogo wa mambo ya utunzaji wa mahesabu. Hivyo basi,
kulingana na mradi wenyewe nitaweza kukokotoa hesabu ili kuwa na mfumo mzuri wa utunzaji wa
hesabu. Hata hivyo nitaweza pata ushauri toka kwa wataalam wa mahesabu ili kutengeneza jedwali
litakalonisaidia katika mapato na matumizi na fedha.

ENEO LA MRADI.
Mradi huu ninagegemea kuuendesha Marangu Rauya kwa kukodi ardi ya kiasi cha heka moja kwa
kuanzia.

MFANO WA SHAMBA LA TEMBELE


RASILIMALI FEDHA.
Rasilimali fedha nategemea kutumia fedha zangu mwenyewe ambazo nilizikusanya toka miradi
mingini kama mtaji wa kuwa na mradi huu. Pia nategemea kukopa kiasi toka kwa asasi za kifedha
zinazotoa mikopo ili kuwa na fedha za kutosha kwaajili ya kuendesha mradi huu.

UFUATILIAJI WA MRADI. (PROJECT MONITORING)


Mradi wa mboga aina ya tembele unaitaji ufuatiliaji wa karibu sana ili kuwa na faida. Kazi hii ili
iwe ya ufanisi mzuri katika kitabu kidogo cha muongozo wa uendeshaji wa mradi nitapata maelezo
jinsi ya kufuatilia hatua kwa hatua mradi huu pamoja na majukumu ya kila mmoja ma kila kundi
nitakaloshirikiano nalo.

BAJETI NA MAHITAJI YA MRADI.


No VIFAA @ KWA TSH./KIASI JUMLA
1. Ardhi kukodi heka 1 @ 300,000x 1 300,000/=
2. Maji (kisima kimoja) @ 500,000 x 1 500,000/=
3. Kuandaa shamba @ 80,000 x 1 80,000
4. Mbolea ya DAP Mfuko 2 @ 75,000 x 2 150,000/=
5. Urea mfuko 1 @ 50,000 x 1 75,000/=
6. Mbolea ya ng’ombe lori 6 @ 70,000 x 6 420,000/=
7. Mbegu ya tembele @ 40,000 x1 40,000/=
8. Pikipiki 1 @ 2,500,000 x 1 2,500,000/=
9. Mafuta ya pampu petroli @ 3,500 x 40/mwezi x 9 miezi 1,260,000/=
10. Majembe 3 @ 7,000 x 3 21,000/=
11. majembe madogo 4 @ 5,000 x 4 20,000/=
12. Reki kubwa 2 @ 4,000 x 2 8,000/=
13. Water ken 2 @ 12,000 x2 24,000/=
14. Mpira 3 inch 100 mita @ 150,000 150,000
15. Pampu ya mafuta 1 @ 350,0000 350,000
16. Mabuti ya mvua pea 4 @ 12,000 x 4 48,000/=
17. Fedha ya dharura 500,000x1 500,000/=
18. Bomba la kupigia dawa 1 kubwa la kisasa @ 48,000 x 1 48,000/=
19. Usafiri kwa wiki mafuta ya petroli @ 30,000 x 4 wiki =120,000 120,000x3meezi= 360,000
20. Posho ya wafanyakazi 3 kwa kila mwezi @ mwezi 240,000 x 3 720,000/=
21. Makoti ya shambani 3 rangi ya kijani @ 20,000 x 3 60,000/=
22. Super grow lita 10 @ 40,000 x 10 Tsh.400,000/=
23. Chakula kwa mwezi @ 38,000 x 3 miezi = 114,000/=
i. Mahindi debe 2 @ 15,000/=
ii. Dagaa sado 1 @ 15,000/=
iii. Maharage 10kg @ 2,500/=
iv. Mchele 10kg @ 2,700/=
v. sukari 10kg @ 2,800/=
jumla = 38,000/=
24. Afisi ugani @ mwezi 50,000/= 50,000 x 3 meizi = 150,000/=
25. Msimamizi mkuu @ mwezi 300,000 300,000 x 3 miezi = 900,000/=
Jumla kuu. 7,938,000

Shughuli zitakazotekelezwa.
Shughuli zitakazotekelezwa katika mradi huu wa shamba la migomba ni pamoja na;
 Ukodishaji wa shamba.
 Usafishaji wa shamba.
 Ulimaji wa shamba.
 Uchimbaji wa kisima cha maji.
 Uandaaji wa matuta ya kupandia tembele.
 Ununuzi wa miche ya tembele.
 Uwekaji wa mifumo ya umwagiliaji maji shambani.
 Upandaji wa tembele kwenye matuta

KUPAMBANA NA HASARA (RISK MANAGEMENT)


Katika mradi huu wa mboga za majani aina ya tembele hatutegemei kufanya uzembe wowote kwa
kila hatua ya uanzishaji wa mradi ili kufikia malengo. Yapo mambo ambayo yaweza kuwa nje ya
uwezo wetu kama vile;

1. Mafuriko. Endapo zitanyesha mvua nyingi kiwango cha kuvuka na kusababisha mafuriko huweza
kusababisha hasara kwa mradi huu. Kwa tathmini ya miaka mitano nyuma hatukuwa na mvua
ambazo zilisababisha mafuriko. Hata hivyo tunategemea kuanza mradi kipindi cha kiangazi na
ambapo hadi masika yafike tunaweza kumalize awamu ya kwanza ya mradi. Historia inatuonesha
pia eneo hilo kwa miaka 15 iliyopita halijawahi kukumbwa na mafuriko. Hata hivyo tutaendelea
kuchukua tahadhari zinazotakiwa kama watoavyo watabiri wa hali ya hewa na wataalamu wa
kilimo.

2. Ukame. Ukame husababishwa na ukosefu wa mvua kwa kipindi cha muda mrefu sana.
Tinategemea kutumia kilimo cha umwagiliaji kutoka kwenye visima vitakavyochimbwa shambani.
Hivyo hatutegemei kukauka kwa visima hivyo kwani tafiti zinaonesha eneo la mradi visima vingi
vilivyochimbwa vinauwezo wa kuhimili ukame kwani (water table) ipo juu na maji yake hutoka
kwenye maporomoko ya milima Kilimanjaro. Tunategemea kuwa na maji mwaka mzima.

3. Magonjwa sugu ya mboga ya tembele. Yapo magonjwa machache yanayoshambulia tembele,


kama vile ukungu, pia wapo wadudu wanaoshambulia kama vile fangazi (white fly), kimamba,
konokono na ndege na wanyama. Aidha wadudu hawa pamoja na magonjwa wanyama tutatumia
viwatilifu vya asili kupambana navyo ili kutoruhusu kushambulia kwa tembele na kutuingizia
hasara kwenye mradi huu. Uwezekano wa kupata magonjwa mabaya ni mdogo sana. Hataivyo
tutajitahidi sana kupambano na wadudu, wanyama na magonjwa ili kunusuru mradi huu kwa
kipindi chote cha uendeshaji wa mradi. Hata hivyo kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo
watatupa njia sahihi ya kuweza kupambambana na wadudu, magonjwa na wanyama.

SOKO LA MBOGA YA TEMBELE.


Soko kubwa la mboga za majani aina ya tembele ukanda huu wa maeneo ya – ni eneo la kwanza
soko la tembele lenyewe kwasababu ya uwepo wa wakaazi ambao ni wanunuzi. Hata hivyo Moshi
ni eneo lenye wateja wa tembele. Uwepo wa masoko makubwa matatu moshi mjini kama vile
mbuyuni, soko kuu, na soko la manyema ni eneo ambalo wakaazi wote wa Moshi na viunga vyake
ni wateja wazuri wa tembele.

Soko lingine ni Holili kwani ni mpaka wa Tanzania na Kenya. Soko hili ni la uhakikia sana kwani
wakenya ni kati ya wanunuzi wa tembele kwani hupeleka Mombosa. Maeneo ya Korogwe, Tanga
hadi Dar es Salaam pia kuna soko zuri la tembele. Maeneo haya yote tukiyatumia vizuri tunaweza
kupata soko la uhakika mwaka mzima kwani tembele ni kati ya mboga za maji zinazohitajika
mwaka mzima.
Katika mradi huu tunategemea kuwa na matuta 300 na zaido ya mboga ya tembele. Tuta moja
litakuwa na urefu wa mita 10 na upana wa mita 1. Tuta moja linakadiriwa kuwa na mafungu 10 ya
mboga kwa makadirio ya chini. Hivyo kwa kila tuta 1 tunaweza kutengeneza kiasi cha kati ya
Tsh5,000/= hadi Tsh.7,000/= Hivyo basi tukifanya Tsh5,000 X 300 = Tsh1,500,000/= kwa mchumo
mmoja. Tukichuma kila mwezi mara mbili tunafanya; 3,000,000X6 = Tsh18,000,000/= kwa makisio
ya chini sana kwa miezi sita.

RATIBA AU JEDWALI LA SHUGHULI BINAFSI ZINAZOHUSIANA NA MRADI.


Hayati Mwl. J.K.Nyerere aliwahi kusema katika hotuba yake kwamba, “Mbolea ya kwanza ya
shamba ni mkuu wako” Hivyo kwa kauli ya hayati Baba wa taifa, shughuli nyingi binafsi zitakuwa
zikihitaji kutembelewa mara kwa mara katika kuuendesha mradi huu wa mboga ya tembele.
Nategemea kuwa na ratibu ya kila wiki kama itakavyoonekana katika jedwale hapo chini ili
kuulinda, kuuboresha na kuufanya mradi huu ndiyo ofisi yangu. Hivyo basi shughuli kubwa za kila
siku zitakuwa katika kuuendesha na kuuboresha mradi huu siku baada ya siku.

JUMA SHUGHULI MUDA WA MUDA WA


KUANZA KUMALIZA
J.TATU Kukagua na kuanzisha shuli ya wili hii. 2:00 am 9:30 pm
J.NNE Kukagua ubora wa shughuli ya siku ya jana na 2:00 am 9:30 pm
kuendeleza shughuli hiyo.
J. TANO Kukagua ubora wa shughuli ya siku ya jana na 2:00 am 10:00 pm
kuendeleza shughuli ya siku hiyo. Pia kuratibu
mambo yote ya msingi ili kuboresha mradi haswa
pale mwanzo wa uandaaji wa shamba na upandaji
wa miche mipya ya tembele katika matuta.
A.HAMISI Kupitia mradi mizama wa siku tatu na kuufanyia 2:00 am 10:00 pm
tadhmini ili kuona kama unahitaji kuboreshwa ama
kuangaliwa kwanza kabla ya kuendeleza ama
kuanza hatua nyingine. Tathmini ya kina na ya
kitaalamu inahitajika ili kuimarisha mradi wa
tembele.
IJUMAA Kukagua mradi mzima na kuimarishi kwa mbolea, 2:00 am 8:30 pm
maji na kuona mapungufu ili kuyarekebisha.
J. MOSI Kupita maboresho na kurekebisha makosa 3:00 am 7:30 pm
madogomadogo. Pia ni siku ya kuandaa siku ya
Bwana yaani J. Pili.
J.PILI Ni siku ya ibada na kila mfanyakazi hupumzika na
kupata wasaa wa kumuabudi Mungu. Pia jioni
kama kutakuwa na haja jioni kwenda kuangalia
shamba kama kunauhitaji wa kunyesha ama
maandalizi ya J.tatu.

AINA ZA MASOKO
1. Uuzaji wa kila siku. Kuwa na watu maalum wa kununua mboga kutoka shambani kila siku.
Faida yake; wateja watakuwa na uhakika wa kupata huduma kutoka kwako mwaka mzima.

Hasara yake; mfumo huu unalazimu muuzaji kuwa shambani kila siku kusimamia mauzo, hata
hivyo ni lengo langu kufanya kazi hii kuwa ajira ya kila siku.
2. Wanunuzi wa jumla. Kupata wateja au mteja ambaye atanunua mboga zote shambani kwa mara
moja kila baada ya muda fulani kwa kipindi chote cha uzalishaji.

Faida yake. Hii inasaidia kuuza mzigo wote kwa mara moja na kupata fedha zako kwa mara moja.
Hata hivyo unaweza kupangilia fedha hivyo na kufanya shughuli nyingine. Hii haulazimiki kuwa
shambani muda wote bali kila baada ya kipindi fulani tu.

Hasara yeke. Mfumo huu utapoteza wateja kwa kukosa huduma kila wakati. Pia wateja wako
wanaweza kukosa imani na huduma yako.

3. Kuuza rejareja. Hii ni hatua nzuri kwani unakwenda shambani kwako na kuchumba tembele
kulingana na mahitaji sokoni. Kila siku unaweza kuwa na wateja ambao wanahitaji tembele. Hivyo
kila siku unaweza kuchuma tuta kadhaa za tembele na kusambaza.

Faida yake. Hii inasaidia kutafuta wateja wa rejareja na ina faida kubwa kama utaweza kufikia watu
wengi zaidi. Hata hivyo utaje huu unaweza kukupa imani kwa wateja wako.

Hasara yake. Hasara kubwa ya mbinu hii inakutegemea wewe au vijana wako kuwafikia wateja kwa
wakati. Hivyo ukishindwa kuwafikia kwa wakati au bidhaa zikipungua unaweza kupoteza wateja
wengi kwa mpigo. Hata hivyo mbinu hii inaweza kukunyima muda wa kukaa shambani kuendelea
kuhudumia tembele.

HITIMISHO.
Mradi huu wa kilimo cha mboga ya tembele ninategemea kuuanza September 2022 hati Desemba
2023. Mradi huu utasaidia kukuza ajira kwa watu wengi kwani kuna watu watapata kazi kwenye
maradi kama watunzaji wa bustani. Pia baadhi ya wateja watakuja na watu wa kuwasaidia na pia
kukuza vipato vya wachuuzi. Hata hivyo mradi huu wa mboga za majani utasaidia uanzishaji wa
kampuni ya kilimo cha mboga mboga hapo baadae.

You might also like