Sehemu ya kwanza: Utangulizi UTANGULIZI Je wajua? • Kabichi imeanza kulimwa miaka 2500 iliyopita yaani kabla ya Yesu kuja ilikuwa inalimwa. • Inapatikana katika jamii moja na sukuma wiki, lettuce na cauliflower. • Asili yake ni Ulaya, ujerumani Aina za kabichi Kuna aina 3 kuu za kabichi, Lakini zilizo maarufu tz ni • Kabichi nyeupe • Kabichi nyekundu – Inavirutubisho mara mbili ya Kabichi nyeupe Je, ungependa kulima kabichi? • Faida • Ina soko la uhakika • Inaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu hivyo inaweza kusafirishwa kwa umbali mrefu • Ina madini na vitamini nyingi kama vile vitamini c. Changamoto • Changamoto kubwa ni magonjwa na wadudu Mfulizo huu utakusaidia • Kuchagua mbegu bora ya kabichi • Kutayarisha miche bora • Kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda mbegu • Utunzaji sahihi wa kabichi • Kukabiliana na wadudu na magonjwa ya kabichi • Uvunaji na utunzaji wa mavuno MAHITAJI YA HALI YA HEWA NA UDONGO KWA KABICHI Hali ya hewa • Jotoridi: –kwa uotaji wa mbegu 18-350 C – ukuaji 15-24 0 C • Lakini inauwezo wa kuhimili joto au baridi Udongo • Kama mazao mengi kabichi inahitaji udongo – Tifutifu – Wenye rutuba • Unaweza kupanda katika udongo wenye kichanga au mfinyanzi kwa kadri. Jambo la muhimu ni udongo usiotuamisha maji. Udongo…. • Inauwezo wa kustahimili chumvi kwenye udongo kwa kiasi . • Chumvi nyingi kwenye udongo huongeza uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa. • PH ya udongo 6.0-6.5 Sehemu inayofuata
Aina za kabichi (varieties)
• Baraka F1 • Globe Master F1 • Zawadi F1 • Haraka f1 • Victoria rock f1 • glory of • Green Coronet F1 enkhuizen Makala ijayo itazungumzia • Copenhagen kila aina , mikoa (maeneo) inayostawi, muda inayochukua hadi kuvunwa n.k Je, una maoni, ushauri au nyongeza kuhusu mada ya leo? Tutafurahi kupata maoni yako kupitia namba …..