You are on page 1of 3

http://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/69559-kilimo-cha-vitunguu-saumu-na-majiushauri-na-masoko-2.

html
T444ZZZ444
keni10000@yahoo.com
MCHANGANUO WA KILIMO CHA UFUTA/ SESAME CULTIVATION BUSINESS PLAN
1. MUHTASARI WA KILIMO BORA CHA UFUTA
Ufuta (sesamum indicum) ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwa
ra, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma,
Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa aj
ili ya chakula na biashara.
Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.
Kwa sasa soko la ufuta Tanzania ni zaidi ya mara tatu ya uzalishaji wake, kwa ma
ntiki hiyo zao hili lina soko kubwa sana.
Uzalishaji wake unafanyika kwa kiasi kidogo kwa sababu wakulima wamekuwa wakili
ma zao hili la ufuta kwa mazoea na kutumia
mazao yake kama nafaka ya kutengeza vyakula mbalimbali kama kashata. Lakini kam
a utalima kibiashara ni zao ambalo linaweza kukomboa
jamii yetu kutoka katika dimbwi la umasikini.
2. UZALISHAJI WA ZAO LA UFUTA
MBEGU
Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya
magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.
Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotev
u wa zao shambani.
Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.
Mbegu bora ya ufuta inayopendekezwa ni LINDI 02, mbegu ambayo imefanyiwa utafiti
na chuo cha utafiti NALIENDELE.
Kwa wastani mbegu hii hutoa kati ya gunia 10 mpaka 15 ukifuata kanuni za kilimo
bora. Mbegu hii hukomaa ndani ya siku mia (100) mpaka mia na kumi(110).
Aina hii ya ufuta ina asilimia 55 ya mafuta. Hii ni habari njema kwa wakulima ku
toka kwa watafiti wetu wa Kilimo kutoka kituo cha Utafiti Naliendele, Mtwara.
UPANDAJI
Panda mbegu nusu inchi chini ya udongo, inchi sita umbali wa mbegu na mbegu na f
uti mbili nafasi ya msitari na msitari, kabla ya kupanda hakikisha ardhi
imelowana vya kutosha na upande mbegu masaa mawili au matatu baadae.
MBOLEA
Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba
ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapo
bidi.
PALIZI
Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutub
ishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta.
MAGONJWA
Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upu
ngufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua
na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi, c
hukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA
Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa. Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na m
inne tangu kupanda kutegemea aina. Aina ya ufuta usiokuwa na matawi
hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi. Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufut
a kupukutikia shambani.

DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI


Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya manjano na hatimaye
kudondoka. Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya kahawia.
VIFAA VYA KUVUNIA
Tumia kamba, siko na panga kipindi cha kuvuna.
VIFAA VYA KUKAUSHIA
Hakikisha Sehemu ya kukaushia ni safi na yenye Sakafu ya saruji na pamefunikwa v
izuri. Waweza tumia maturubai kufunika sehemu ya kukaushia.
USAFIRI
Mikokoteni
Matela ya matrekta
Magari
KUVUNA
Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana na kuanza kupasuka na kuachia punje.
Mapodo ya ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na upepo hupasuka
na kuachia mbegu, hali inayosababisha upotevu mkubwa. Mbegu za ufuta ni ndogo n
a zikidondoka chini ni vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni vigumu
kuzitenganisha na uchafu.
Uvunaji wa ufuta huhusisha ukataji wa mimea yenye mapodo kwa kutumia vyombo vya
mkono kama panga kwa kukata mashina. Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka
,
uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili kuepuka upotevu wa mbegu.
Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala jua kali. Baada ya kukata mashin
a yafunge katika mizigo midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha kama vile
mikokoteni, matela au magari hadi sehemu ya kukaushia. Panga mizigo midogo kwa k
usimamisha katika malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye sehemu safi za
kukaushia.
KUKAUSHA
Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa ku
egeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea
hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa p
unje kutokana na kupasuka kwa mapodo.
KUPURA
Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye sakafu safi.Vitita hupigwa tar
atibu kwa kutumia mti au hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili
kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu safi au turubai.
KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa takataka kama vile mawe, vipande vya m
apodo,vijiti na vumbi.Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa kutumia mikono.
Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa kiasi cha kilo mbili hadi tatu. U
futa hurushwa hewani kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na upepo.
KUFUNGASHA
Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye vifungashio kama vile magunia madogo y
a aina ya juti ya ujazo wa kilo 50. Fungasha mbegu za ufuta kwenye
magunia yenye uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha mbegu zimeka
uka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.
KUHIFADHI
Panga magunia ya ufuta juu ya chaga. Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguk
o wa hewa kati ya magunia na magunia yako tiyari kupeleka sokoni.
3. GHARAMA ZA UZALISHAJI NA FAIDA KWA HEKA
Jedwali hapo chini linaonesha mchanganuo gharama na faida ya kilimo cha ufuta kw
a maeneo ya Mbeya (Namkukwe katika wilaya ya chunya). Gharama hizo
zinaweza kupungua au kuongezeka na zinategemea eneo na msimu husika.
Na Shughuli Kiasi
1 Kuandaa shamba 70,000
2 Kulima 30,000
3 Kupanda 20,000
4 Mbolea 100,000
5 Kupalilia 30,000

6 Kuvuna 50,000
7 Usafiri 50,000
8 Gharama zingine 50,000
9 Jumla 400,000
10 Mapato (Forecasts) gunia 10*50kg*3000 1,500,000
11 Faida 1,100,000
4. SOKO LA UFUTA
Soko la ufuta kwa Tanzania ni mara tatu zaidi ya uzalishaji wake. Kuna makampuni
mbalimbali Tanzania ya unuzi wa ufuta. Makampuni hayo hununua na kusafirisha
nje ya nchi kama India na China. Makampuni hayo ni kama vile OLAM, Export Trader
s n.k.
Katika msimu wa mwaka 2014 bei ya ufuta kwa kilo ilikuwa sh 3000 ambayo ni sawa
na sh 300,000 kwa gunia lenye ujazo wa kilo 100. Kwa maana hiyo uhakika wa soko
upo na ni mkubwa sana.
DISCLAIMER
Mchanganuo huu ni matokeo ya kiutafiti wa kibiashara, ambayo jitihada zimefanyik
a kuifanya iendane na hali ya kiuchumi ya sasa, hivyo haitaathiri au kuathiriwa
na tamko la wazi au la kiutendaji wa mabadiliko ya kila siku ya kiuchumi duniani
hasa ndani ya soko letu la Tanzania. Matokeo yoyote utakayoyapata mtumiaji au m
somaji yatakayokuathiri moja kwa moja au kimchakato, bila kikomo cha muda maalum
u mpaka kuathiri faida iliyopangwa, hatutakua tayari kutupiwa lawama ya aina yoy
ote ile.

You might also like