You are on page 1of 2

MRADI WA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA TANZANIA

The Rabbit bliss Limited (Tanzania) ambayo kwa Kenya inafaamika kama The Rabbit republic limited ni
kampuni inayotoa huduma ya mafunzo na msaada wa kitaalamu kuhusu mambo yote yanayohusiana na
mnyororo mzima wa thamani kwenye ufugaji wa sungura kibiashara,ikiwemo uzalishaji na usindikaji wa
nyama nyeupe ya sungura kwa soko la ndani na la kimataifa.

Tunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura, kwa gharama ya Tshs 68,400/= tu kwa kimoja
cha ukubwa wa 2.5futi3 , chenye uwezo wa kufugia Sungura mmoja mkubwa wakuzalisha pamoja na
watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda
cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu. Tunashauri ujenzi wa
vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada
ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.

Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko
letu, na tunawauzia kwa gharama ya Tshs 95,000/= kwa kila jike aliyetayari kubeba mimba na Tshs
47,500/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.

Tuna mafunzo mara kwa mara pia, na zaidi kuhusu ujezi wa mabanda bora, Utunzaji na ufugaji kwa
ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.

Tuna saini mkataba wa miaka 6 na mkulima/mfugaji (kwa ada ya Tshs 95,000/= kila mwaka) ambao
utamuhakikishia mfugaji/mkulima soko kwa kipindi chote cha mkataba pale sungura wake wanapokuwa
tayari kwa kuuzwa

Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri
anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs 7,600/=.
Tafadhali tembelea ofisi zetu kwa maelezo zaidi.

Tafadhali zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya muhimu
sana na ni sehemu ya mambo ya msingi unapoanza mradi nasi , utagharimia nauli yake na atafundishwa
na rabbit bliss limited kwa vitendo kwenye mabanda ya Sungura wetu na nadharia ofisini kwetu,.

Gharama ya kumlisha sungura ni gramu 100 kwa siku, hivyo kwa mwezi sungura atatumia kilo 3 tu,
Kumbuka sungura wanapofikia umri wa wiki 6 ndipo huanza kujitegemea wanakula 30gkila mmoja, kwa
muda wa wiki 2; kwahiyo ni sawa na 30g x 14siku= 420g - mpaka kufikia umri wa miezi 2.Wakifikia umri
wa miezi 2, kila mmoja anakula 50g, kwa hiyo ni saw na 50g x 30siku= 1500g mpaka kufikia umri wa
miezi 3.Wakifikia umri wa miezi 3 kila mmoja anakula 8og, kwa hiyo ni sawa na 80g x 30siku= 2400g
mpaka kufikia umri wa miezi 4.Na hatimaye , wakifikia umri wa miezi 4 kila mmoja anakula 100g. kwa
hiyo ni sawa na 100g x 30siku= 3000g.

Hivyo 420g + 1500g + 2400g + 3000g= 7320g- 7320/1000g ni sawa na kilo 7.3 , kwahiyo sungura mmoja
atakula wastani jumla ya kilo 7.5 mpaka kufikia kuuzwa.
Kilo 1 ya pellets ni Tshs 850, Hivyo, kilo 7.5 x Tsh 850= Tshs 6375 ambayo ni gharama ya kumlisha
sungura mmoja mpaka anapokuwa tayari kuuzwa.

Ikiwa atafikia uzito wa chini kilo 3 utamuuza kwa Tsh 22,800 (kilo 3 x Tsh 7,600=).Kwahiyo bei ya kuuza
22,800 ukitoa Tsh 6,500(ambayo ni gharama ya kumlisha) na gharama nyingine za dharura kila sungura
achangie Tshs 2,000/=, Utabaki na Tsh 14,300 (22800-8500) kwa sungura mmoja,kama faida baada ya
kutoa gharama za uendeshaji mradi, tokea hapo utazidisha na idadi ya sungura unaotegemea kuzalisha
kila mwezi kupata kipato chako cha mwezi. Matarajio ya chini ya faida utakayopata kwa jike mmoja ni
wastani wa Tshs 30,000/= hadi Tshs 57,000/= kwa mwezi ambayo ni sawa na wastani wa kuanzia Tshs
360,000/= hadi Tshs 684,000/= kwa mwaka (Kutegemeana na utunzaji (kg) na idadi ya watoto), baada ya
watoto kukuzwaa na kuuzwa kwa bei tuliyokuhakikishia katika mkataba. Na kumbuka jike huyo
atakuzalishia kwa wastani wa miaka 3-5 ndipo naye utakapomuuza pia na Kumbuka unaweza kufuga
idadi kubwa uwezavyo ili kuongeza faida/pato lako.

CHINI NI MAKISIO YA GHARAMA YA KUANZIA KWA KIFURUSHI KIDOGO CHA JIKE 5 NA DUME 1

BEI YA BEI YA JUMLA KWA


IDADI BIDHAA/MAELEZO MOJA (KSH) MOJA(TSH) TSH
5 Jike aliyepevuka 5,000 95,000 475,000
1 Dume aliyepevuka 2,500 47,500 47,500
1 Mfuko wa chakula (pellets) 50kg 2,200 42,000 42,000
1 Kisanduku cha madawa(startup kit) 3,000 57,000 57,000
12 Vyungu vya kulishia. 100 1,900 22,800
1 Mafunzo kwa mtunzaji (siku 1) 10,000 60,000 60,000
1 Ada ya mkataba 5,000 95,000 95,000
Taratibu na usafirishaji 190,000
989,300/=
JUMLA NDOGO YA MRADI
16 Ujenzi vibanda (Material + ufundi) 3,600 68,400 1,094,400
2,083,700/=
JUMLA KUU
Kumbuka: kwa kila majike nane yatahitaji
dume moja kuwahudumia.
Changamoto.

Changamoto kubwa tunayokutana nayo katika ufugaji wa sungura ni wakulima kushindwa kuzingatia
maelekezo wanayopewa na kuweka kwenye matendo yale wanayojifunza kwenye mafunzo ya ufugaji
bora. N a tatizo jingine ni kutozingatia usafi na utumiaji wa madawa ya matibabu ya sungura kama
wanavyoelekezwa na madaktari wa mifugo.

Kwa sasa bado tunashughulikia kutoa toleo la Kiswahili la kitabu chetu cha (THE RABBIT BLISS) na
kipeperushi vyakiswahili vitapatikana hivi karibuni.

Kwa maelezo zaidi na namna yakuanza mradi huu hapa Tanzania, Tafadhali wasiliana na nasi:

The rabbit bliss LTD AU Positive eye Co. Ltd, Kwa mawasiliano tajwa hapo juu na tovuti zetu

Web: www.positiveeye.net au www.rabbitrepublic.co.ke

You might also like