You are on page 1of 3

Home ▼

MAHITAJI YA MTAJI WA MRADI


WA KUKU WA NYAMA (200)
1.VIFARANGA
  Manunuzi ya vifaranga mia mbili (200) X 1300= Tshs. 260,000/=       
2.CHAKULA
MUDA (WIKI)                                     KIASI CHA ULAJI              JUMLA
Siku 1 - wiki 1 (siku7)                       25g X siku 7                         175g
 Wiki 1 - wiki 2 (siku7)                     50g X siku 7                        350g
Wiki 2 - wiki 3 (siku 7)                     65g X siku 7                        455g
                                                  Jumla  980g

Hivyo, kwa kuku wote 200 zitahitajika  980g x kuku 200 = 196000g (196Kg)
ambazo ni sawa wastani wa mifuko 4 ya ujazo wa kilogramu 50 kwa gharama
ya: = Mifuko 4 x Tshs. 38,000 (bei ya mfuko mmoja)/= =Tshs.152,000/= 
Kuanzia wiki ya tatu mpaka ya wiki ya 6 (siku 21),  watapewa chakula cha Broiler
Finisher kama ifuatavyo:
MUDA (WIKI)                                    KIASI CHA ULAJI                               JUMLA
Wiki 3 - 4 (siku7)                               80g X siku 7                        560g
Wiki 4 - 5 (siku7)                               110g X siku 7                       770g
 Wiki 5 - 6 (siku 7)                             130g X siku 7                      910g
 Jumla 2240g

Hivyo kwa kuku wote 200 zitahitajika  2240g x kuku 200 =448,000g (448Kg)
sawa na mifuko 9 ya 50Kg,
kwa gharama ya: Mifuko 9 x Tshs 38,000(bei ya mfuko mmoja)/=Tshs.
342,000/=

3.MFANYAKAZI
Wastani wa juu wa gharama za mfanyakazi kwa mwezi ni Tshs. 40,000/=. Hivyo
kwa kipindi chote cha ufugaji ni sawa na  Tshs. 40,000/= X mwezi 1.5 = Tshs.
60,000
4.MADAWA NA CHANJO
 Wastani wa gharama za madawa na chanjo ni  Tshs. 50,000/= kwa kipindi chote
cha wiki sita kwa kuku wote.

5.BANDA
Kiutaalam, katika eneo la 16m2 wanatakiwa kukaa kuku 200 na gharama za
banda/nyumba inakadiriwa kuwa ni Tshs. 5000/= kwa mwezi.  Hivyo kwa kipindi
chote cha ufugaji (wiki 6/mwezi 1.5) ni sawa na Tshs.5000/= X mwezi 1.5 =
Tshs. 7,500/=
4.NISHATI YA MWANGA NA JOTO
Ikiwa gharama za juu za unit moja ya umeme ni Tshs 250/= na zitahitajika  balbu
4 kwa muda wa siku 14 za kwanza.  Hivyo gharama za umeme ni  Tshs. 250 X
balbu 4 X siku 14 =Tshs. 14,000/=.
Wastani wa gharama za mkaa kwa siku 14 za mwanzo ni  gunia 2 X Tshs.
20,000/=(bei ya gunia moja) ambayo ni sawa na Tshs. 40,000/= kwa kuku wote
200.
5.MAJI
 Wastani wa kiasi cha maji kwa kuku wote 200 kwa siku ni ndoo 5 (lita 100), na
wastani wa ndoo moja ya maji ni Tshs. 50/=.  Hivyo kwa kipindi chote cha
ufugaji (wiki 6) ni sawa na  Ndoo 5 X wiki 6 (siku42) X Tshs.50/= ni sawa na
Tshs. 10,500/= kwa kuku wote 200.
6.MATANDIKO
Wastani wa gharama za matandiko kwa kipindi chote cha ufugaji ni :
Tshs.10,000 X mwezi 1.5 = Tsh 15,000/=
7.JUMLA YA MATUMIZI YOTE
  Manunuzi ya vifaranga mia mbili (200)                        Tshs. 260,000/=
 Gharama za chakula kwa Broiler Starter                      Tshs. 152,000/=
 Gharama za chakula kwa Broiler Finisher                    Tshs. 342,000/=
Gharama za mfanyakazi                                                  Tshs. 60,000/=
Gharama za madawa na chanjo                                      Tshs. 50,000/=
 Gharama za umeme                                          Tshs. 14,000/=
 Gharama za maji                                                                 Tshs. 10,500/=
Gharama za mkaa                                                 Tshs. 40,000/=
Gharama za matandiko                                                    Tshs. 15,000/=
Gharama za banda/pango                                              Tshs. 7,500/=
 JUMLA                                                                                     Tshs. 951,000/= 

KUMBUKA: CHANJO NA USAFI NI MUHIMU SANA KWA MATOKEO BORA KWA


UFUGAJI WA FAIDA

8. MAPATO YA MAUZO
 Wastani wa chini wa mauzo ya kuku ni Tshs.6,500/= (Kila kuku akiwa na uzito
wa wastani wa kilo 1.3) kwa kuku, hivyo kwa kuku wote 200 ni sawa na Tshs.
6,500 x kuku 200 = Tshs. 1,300,000/=
 Mauzo ya mbolea itakayopatikana yanakadiriwa kuwa Mifuko/viroba 26 na
ikiwa wastani wa bei ya kiroba kimoja ni Tshs. 2000/= hivyo jumla ya mauzo ya
mbolea ni  Mifuko/viroba 26 X Tshs. 3000/ = Tshs. 78,000/=
9.FAIDA
Faida  itakayopatikana ni : Tshs. 1,378,000 – Tshs. 951,000 = Tshs. 427,000/=
kwa muda wa wiki sita tu, ukitoa gharama zote.
Hivyo, jumla ya mapato yote ni Tshs. 1,378,000/=
          
MAMBO MUHIMU: 
• Matokeo bora ya ufugaji wa faida unaanzia kwenye mazingira/mabanda na sio
kwa kuku mwenyewe, hivyo zingatia vipimo vya banda kwa kutambua idadi
kamili ya kuku wanaohitajika. (1m2= Broilers 9 – 12) 
• Zingatia usafi wa banda kila baada ya kuchafuka au kila baada ya kutokea
mlipuko wa ugonjwa. 
• Fuatilia ratiba za chanjo bila kukosa kwa kutumia chanjo iliyo salama. 
• Ni vyema kufanya matibabu mara tu dalili za ugonjwa zinapoonekana na
kuwatenga kuku walioathirika katika kundi. 
• Magonjwa karibu yote ya kuku husambaa kwa kinyesi, hivyo epuka mazingira
ya kuingiza kinyesi cha kuku mgonjwa bandani kwa kuwa makini kwenye
chakula, matandiko, vyombo, n.k.
          
MAPENDEKEZO 
 Ni vyema kwa mfugaji kununua chakula kilichotengenezwa  kiutaalamu kwa
sababu zifuatazo:
a. Kudhibiti magonjwa kwa kuku.
 b. Kudhibiti sumu kwa kuku (poisoning i.e mycotixins).
 c. Kuepuka uchanganyaji mbaya wa viinilishe kwa kundi husika la kuku.
 d. Kuokoa muda na kuongeza jitihada zaidi kwenye uzalishaji.
  Hakikisha unakuwa na kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi.
  Hakikisha unakuwa karibu na Afisa Mifugo aliye karibu nawe kwa msaada
zaidi.
   Nunua vifaranga kwenye mashamba yaliyo salama kwa kushirikiana na
wataalamu (free from diseases).
 Zingatia : Kiwango kizuri cha joto kinachohitajika kwa ufugaji bora wa kuku
ambayo ni kati ya 60°F – 90°F (15.6°C – 32 °C).
I POULTRY CARE I
POULTRY CARE itakusaidia mfugaji katika upatikanaji wa soko la uhakika la kuku
na ndege wote ufugao(“poultry”).

Wasiliana nasi:

POULTRY CARE . Email : poultrycaretz@gmail.com,  Website    :


www.poultrycare.blogspot.com, www.facebook.com/poultrycare , www.instagra
m.com/poultry_care/ ©poultrycare 2015

poultry care

Share

‹ Home ›
View web version

Powered by Blogger.

You might also like