You are on page 1of 28

UTANGULIZI

Ufugaji wa mbuzi hapa ni fursa (opportunité) ambayo Wakongomani wengi hawajaiona. Ni


ufugaji ambao kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji
kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji
lazima awe na eneo pamoja na mtaji (capital) wa kuanzia. Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa
gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na
ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza
kuhudumiwa na familia yenye watu wa dogo na kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha
mfugaji kupata mbuzi/ kondoo wengi kwa kipindi kifupi. Ili mfugaji aweze kupata faida ni lazima
aheshimie kanuni (principe) fulani za ufugaji wa mbuzi kama vile Wafugwe kwenye banda
bora ,Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama/ maziwa. Walishwe chakula
sahihi kulingana na umri Kwa kufuata ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti
(prevenir) wa magonjwa. Kuweka kumbukumbu (registre) za uzalishaji. Mbuzi wana soko kubwa kila
mahali lakini si watu wengi wanaofuga mbuzi kibiashara. Kwa hiyo basi ni vizuri tukajifunza namana
nzuri ya kufuga mbuzi wa nyama kisasa. Kama unao tayari elimu hii itakusaidia kuboresha
(ameliorer), lakini kama bado, unaweza kushawishika kuanzisha mradi wa ufugaji mbuzi hata hapo
ulipo.

Ukiamua kufuga mbuzi kwa lengo la kibiashara unaweza kupata faida kubwa kwa sababu
kwa kawaida mbuzi anazaa mara mbili kwa mwaka. Anabeba mimba kwa miezi mitano (yaani siku
145 hadi 155) na wananyonyesha kwa miezi miwili. Wapo mbuzi ambao wanazaa mapacha, na kwa
hiyo unaweza kuongeza kundi lako katika muda mfupi. Kama unataka kuzalisha zaidi, basi unaweza
kuamua kuwauza madume na kubakiwa na majike ambayo yataendelea kuzaa na kuongeza kundi lako.
Faida za mbuzi ni nyingi sana, lakini mbali ya kuwauza wakiwa hai, ukiwachinja utapa nyama, ngozi,
kwato na pembe ambazo ni rasilimali (Procution) nyingine zinazoweza kuuzwa kwenye viwanda ili
kuzalisha bidhaa nyingine . Katika nchi nyingi, nyama ya mbuzi inapendwa sana kwa sababu ni tamu
na haina lehemu (cholesterol) wala mafuta mengi kulinganisha na nyama nyingine. Kitabu hiki
kitamsaidia mfugaji wa mbuzi kuweza kutambua mbinu (methode) zote muhimu za ufugaji wa
wanyama hawa ikiwa ni pamoja na kutambua namna bora ya ujenzi wa mambanda, lishe aina za
mbuzi wa kufugwa na mengineyo mengi za ngozi.

TABIA ZA JUMLA ZA MBUZI


Zifuatazo ni tabia za jumla za mbuzi:
(i) Mbuzi huweza kuwapiga pembe au kuwakumba watu wanaowasumbua.
(ii) Watakula kila mmea na iwapo wataachiwa kula majani na nyasi zote wanaweza
kusababisha mmomonyoko wa udongo.
(iii) Mbuzi dume wana harufu mbaya kutokana na dutu zinazoachiwa na tezi zilizoko
kwenye vichwa vyao.
(iv) Mbuzi wa asili ni wagumu na wana ukinzani zaidi kwa magonjwa, vimelezi na
mabadiliko ya tabianchi ukilinganisha na kondoo.
(v) Mbuzi huweza kuendelea kuzaa kwa kipindi cha miaka kumi.

SURA YA KWANZA: FAIDA ZA MBUZI

Mbuzi wana faida nyingi sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na


1. NYAMA : Hapa nchini mbuzi wa asili hufugwa, hasa, kwa ajili ya kujipatia nyama. Nyama ya
mbuzi ni nzuri na tamu kuliko ya aina nyingi za mifugo.
2. MAZIWA : Mbuzi wa maziwa hukamuliwa maziwa. Lakini, hapa nchini, kwa sasa ni wafugaji
wachache ambao hufuga mbuzi kwa lengo hiyo. Maziwa ya mbuzi ni bora kuliko ya ng’ombe
kwa sababu zifuatazo:
 Maziwa ya mbuzi yana protini na madini mengi zaidi kuliko maziwa ya ng’ombe.
 Maziwa ya mbuzi hayana viini vya ugonjwa wa kifua kikuu. Kwa hiyo, hayaambukizi
binadamu ugonjwa huu kama yafanyavyo maziwa ya ng’ombe yakinywewa bila kuchemshwa.
 Maziwa ya mbuzi humeng’enywa (digestion facile) upesi, na, kwa sababu hii , hutumika kwa
urahisi zaidi mwilini kuliko maziwa ya ng’ombe. Hii maana yake ni kuwa mara maziwa haya
yanywewapo hayakai muda mrefu maana huanza mara moja kutumiwa na mwili. Sifa hii
imetokana na mbuzi kula zaidi majani ya aina nyingi za miti na nyasi ambazo hazina asidi.
Kwa sababu hii, maziwa ya mbuzi yanafaa hasa kwa watoto wachanga na wagonjwa wenye
vidonda vya tumboni.
3. NGOZI: Ngozi ya mbuzi ni nzuri na hutumiwa kwa kutengenezea bidhaa mbalimbali(mfano viato)
4. MBOLEA: Mbolea inayotokana na kinyesi cha mbuzi ni nzuri na ni rahisi kuiandaa. Aidha, ni
bora kwa kurutubisha ardhi kuliko samadi ya ng’ombe.
5. MATUMIZI YA KIJAMII: Watu wengi hufuga mbuzi wa ajili ya kutolea mahari au kwa
shughuli za tambiko.
SURA YA PILI : UJENZI WA BANDA LA MBUZI

Mbuzi wanapenda kulala kwenye banda kavu, lililoinuliwa na kujengwa vizuri ili kuwakinga
na jua na mvua, lakini pia lililozungushiwa kuta (za udongo, mbao au manjanja) kuwakinga na upepo
mkali. Mwanga na hewa ya kutosha ni vitu muhimu sana. Banda la mbuzi siyo ghali, kwani linaweza
kujengwa kwa vyombo vinavyopatikana mahali ulipo – miti, manjanja, nyasi. Mbuzi/kondoo
wanaweza kufugwa katika mifumo ya huria (semi-intensif), shadidi (intensif) na kwa kutumia njia
zote mbili. Zizi hutumika katika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo huchungwa wakati wa mchana
na kurejeshwa zizini (bandani) wakati wa usiku.

SIFA ZA ZIZI BORA LA MBUZI

Lililo imara linaloweza kumkinga (proteger) mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na


wezi,
Lililojengwa mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,
Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo watengwe
kulingana na umri wao; na
Liruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.

Pale ambapo mbuzi/kondoo wanafugwa kwa mfumo wa intensif hufugwa katika banda wakati wote.

SIFA ZA BANDA BORA LA MBUZI


 Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano
jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari,
 Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
 Lijengwe sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Pia ujenzi uzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa kutoka bandani isiende kwenye makazi,
 Liwe na sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa banda la mbuzi),
 Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la chumvichumvi; na
 Liwe na vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo wanaokua,
wanaonenepeshwa na wanao gonjwa.

VIFAA VYA KUJENGEA NA VIPIMO VYA BANDA

Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo lako na kulinganana uwezo wa mfugaji.
Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwangaza na hewa ya kutosha. Mlango uwe na ukubwa wa
60X150 sentimeta. Sakafu (chini) iwe ya udongo/zege (ciment) ya kichanja unaweza kutumia
mabanzi(manjanja) /mianzi na iruhusu kinyesi (mavi) na mikojo ku angukia chini Ukubwa wa banda
utategemea idadi ya mbuzi/kondoo wanaofugwa humo na ukubwa wa umbo (taille/masse).
ENEO LA MBUZI/ KONDOO LINALOTAKIWA
Vitoto 0.3, Wasio na mimba 1.5, Wenye mimba 1.9, Dume 2.8, vipimo vyote ni kwa mita za
mraba na ni kwa mbuzi mmoja
Paa (toiture) lijengwe kwa kutumia vifaa kama miti, mbao, na kuezekwa kwa nyasi, majani
ya migomba, mabati (tôle) au hata vigae kwa kutegemea uwezo wa mfugaji.
SURA YA TATU AINA YA MBUZI WAFUGWAO KWA NYAMA

Inawezekana umesikia aina mbalimbali ya mbuzi, lakini hujajua ni wepi wanaofaa kufugwa
kwa ajili ya nyama. Ukumbuke kwamba, wapo mbuzi wanaofugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, na
nyuzi. Sasa hapa tunazungumzia mbuzi wa nyama.
1. BOER GOAT (MBUZI KABURU)

Mbuzi wanaofaa zaidi kwa nyama hasa unapofuga kibiashara ni jamii ya Boer (maarufu
kama Mbuzi Kaburu), ambao ni chotara (hybride) wanaokua kwa haraka, wana umbo(taille) kubwa,
nyama yao ni ya kiwango cha juu. Mbuzi hawa wana rangi nyeupe, kichwa chenye rangi ya udongo au
nyekundu, masikio makubwa na pembe ambazo zimepinda kwa nyuma na chini. Mbuzi jike mkubwa
wa jamii ya Boer ana uzito wa kilogramu kuanzia 68 hadi 102, wakati beberu mkubwa ana uzito wa
kilogramu 80 hadi 150.Unaweza kuona ni kwa jinsi gani mbuzi hao wanavyokuwa wakubwa na uzito
mkubwa sana.

2. KIKO

Kiko ni jamii ya mbuzi inayokuja kasi baada ya Boer hata katika utoaji wa nyama. Wana
uwezo wa kula nyasi na kuzibadili kuwa nyama, hivyo wananenepa haraka. Mbuzi hawa wanaweza
kuwa na rangi tofauti, ingawa wengi wao ni weupe. Pembe za beberu ni ndefu zilizojiviringa wakati
pembe za jike ni fupi. Jike ana uzito wa kilogramu 45 na beberu ana uzito wa kilogramu 80.

3. PYGMY (MBUZI MBILIKIMO)

Mbuzi jamii ya Pygmy ni wadogo kwa umbo lakini wenye miili imara na minene iliyojaa
minofu; miili yao ni mipana. Mbuzi hawa wana manyoya marefu. Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa
kati ya kilogramu 16 hadi 23, na beberu mkubwa ana kilogramu kati ya 20 hadi 32.
4. SPANISH

Kabla mbuzi jamii ya Boer na Kiko hawajawa maarufu, hususan Marekani, mbuzi wengi
waliofugwa kwa ajili ya nyama walikuwa wakiachwa kujitafutia wenyewe chakula kwenye mabonde
na vichakani Kusini na Kusini Magharibi mwa Marekani ili kusafisha mashamba yasiwe na vichaka na
nyasi – kama ilivyo kwa mbuzi wetu wa asili hapa Congo (Beni-Butembo). Mbuzi hao huko Marekani
waliitwa Spanish kwa sababu walipelekwa kwa mara ya kwanza na wapelelezi wa Kihispania na
wakaachwa huko ili wawafae kwa kitoweo wakati mwingine watakaporejea tena. Kwa vile mbuzi hao
wanatofautiana kwa maumbo na rangi, kwa hiyo jina la Spanish halimaanishi aina moja ya mbuzi.
Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa kilogramu kati ya 30 hadi 60 wakati beberu ana uzito wa kati ya
kilogramu 36 na 91.

5. SAN CLEMENTE

Katika miaka ya 1500, mbuzi wa Kihispania waliachwa kwenye Kisiwa cha San Clemente,
kutoka Pwani ya California jirani na San Diego. Mbuzi hao walizaliana na wameendelea kuzaliana
huko hivyo kupewa jina la San Clemente. Wakati fulani mbuzi walikuwa wengi mno kisiwani humo
kiasi kwamba walikaribia kuharibu mazingira ya kisiwa, hivyo ikabidi wapunguzwe. Mbuzi wa jamii
hii ni wadogo na wana nyama nzuri kuliko jamii nyingine ya mbuzi kutoka Hispania, na pembe zao
zinakuwa ndefu kwa kwenda juu. Mbuzi hawa wana rangi tofauti na mabaka ya rangi ya udongo au
nyeusi. Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa kati ya kilogramu 15 na 32 wakati bebeeru lina uzito kati ya
kilogramu 18 na 36.

6. MBUZI WA ASILI

Mbuzi wa asili ni mkusanyiko wa koo za mbuzi ambazo kwa karne na karne ya miaka
zimekuwa zikifugwa na makabila mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya nyama. Kwa sababu koo hizi za
mbuzi hufanana na koo za mbuzi wengine wa asili katika nchi za Afrika Mashariki, hujulikana kama
Mbuzi Wadogo wa Afrika Mashariki.
SIFA

1) Ni wadogo wa umbo. Wastani wa uzito ni kilo 22 kwa jike na kilo 25 kwa dume. Kwa hiyo, hutoa
nyama kidogo.
2) Hukua taratibu
3) Hutoa maziwa kidogo
4) Nyama yao ina ladha nzuri, hasa ikichomwa.
5) Huzaa kwa mara ya kwanza akiwa na wastani wa umri wa miezi 17.
6) Wana rangi mbalimbali (nyeupe, nyeusi, kahawia na mchanganyiko wa rangi).
7) Huweza kuishi katika mazingira mbalimbali, yakiwamo yenye mvua chache (chini ya milimita 750
kwa mwaka).
SURA YA INE UFUGAJI WA MBUZI WA MAZIWA

Sawa na ng’ombe wa maziwa hata mbuzi wa maziwa huhitaji utunzaji mwema. Mbuzi wa
maziwa wanatoa maziwa, lakini baada ya kuzaa. Hii maana yake ni kwamba lazima uwapandishe kwa
dume (breeding), hivyo unahitaji kuwa na beberu. Kama unazingatia ufugaji bora wa mbuzi, hakika
kipengele hiki ni muhimu sana kwako, vinginevyo itakuletea changamoto (shida) kubwa. Kuwalisha,
kuwanyweshwa na kuwatibu tu hakusaidii ikiwa utashindwa kuwaangalia katika masuala haya
muhimu ya kuanzia kuwapandisha, kuwazalisha na kuwatunza watoto wanapozaliwa. ufugaji wa
mbuzi wa maziwa ni fursa (opportunité) kubwa sana ambayo atu wengi bado haajaichangamkia
ukitaka kufuga mbuzi wa maziwa muhimu ni kufanya uchaguzi mzuri wa mbegu. utunzaji mbuzi wa
maziwa hazitofautiani na mbuzi wa nyama. Mbuzi wanao faa kwa maziwa ni:

 Anglo-nubian
 Toggenburg
 Alpines
 Saanen.

UTUNZAJI WA KIZAZI
Mbuzi wa kike anastahili kupewa mbegu ya uzalishaji akiwa na umri wa miezi 12 ili azae
akiwa wa umri miezi 18. Mbegu inastahili kutungwa masaa 12 baada ya dalili za joto kutambuliwa.
Kiwango cha juu cha uzalishaji wa mbuzi hufikiwa kati ya miaka 5 hadi 6 na hata utoaji wa maziwa ni
vivyo hivyo.

CHAKULA KWA MBUZI ANAYENYONYESHA


Mbuzi anayenyonyesha anastahili kupewa chakula kizuri hasa katika miezi 3 ya kwanza
baada ya kuzaa. Chakula hicho kinastahili kubadilishwa ili kutia hamu ya kula kingi. chakula kingi
wakati anapokuwa mja mzito hupelekea kula chakula kingi baada ya kuzaa. Virutubishi(supplements)
katika chakula viongezewe katika majuma 4 hadi 6 ya mwaanzo baada ya kuzaa lakini visizidi nusu
kilo.

MATATIZO YA UZALISHAJI
Mbuzi anaweza kupoteza mimba haraka zaidi kuliko wanyama wengine wowote wa
kufugwa. Mara nyingi mimba hupotea kati ya siku 90-110 za kipindi cha uja- uzito kutokana na
mfadhaiko. Kuavya mimba huko kunaweza kudhibitiwa(maitriser) kwa lishe bora na utunzaji
mwema.

KUWATUNZA WATOTO WA MBUZI


Wape maziwa ya mwanzo watoto wa mbuzi siku 3 za mwanzo baada ya kuzaliwa. Hii
huyasisimua matumbo ya mbuzi mtoto na kumpa vitamini iliyo na vikinga mwili inavyoweza kumpa
uwezo wa kujikinga kutokana na magonjwa. Baada ya siku 3 au 4 mpe lita 0.7 hadi 0.9 za maziwa kila
siku. Tumia chupa au bibero. Mpe maziwa haya kamili mara 3 hadi 5 kila siku.
Watoto wa kiume wasio wa kuzalisha wahasiriwe (castrer) muda mfupi baada ya kuzaliwa.

UTARATIBU WA KUFUATA KATIKA UKAMUAJI WA MBUZI WA MAZIWA

Kusudi ya ufugaji wa mbuzi/kondoo wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama


pamoja na mazao yatokanayo na maziwa. Mambo ya maana ya kufuata ni:
1) Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,
2) Mbuzi/kondoo awe na afya nzuri, msafi, na kiwele(nyongera) kioshwe kwa maji safi ya
uvuguvugu,
3) Mkamuaji asibadilishwe badilishwe awe msafi, mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya
kuambukiza,
4) Vyombo vya kukamulia viwe safi; na
5) Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili
kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
SURA YA TANO CHAKULA BORA KWA MBUZI

Ni muhimu kwa mfugaji kutambua kuwa chakula unachomlisha mbuzi wako ndicho
kinachotengeneza maziwa na nyama , hivyo basi ni muhimu kwa mfugaji:
a) Kumpa mbuzi chakula katika mahali palipo safi kwa sababu , mbuzi hula kila aina ya chakula
hivyo usiwaruhusu kula chakula kilicho na mchanga kwani huweza sababisha kuambukizwa
minyoo inayopatikana kwenye mchanga
b) Mbuzi wa maziwa mara nyingi hufugwa ndani hivyo basi kumbuka kuwatengenezea mahali pa
kulia chakula na kunywea maji (mangeoire + abreuvoir) ambapo panahitajika kuwa juu na mbali na
sehemu ya kulala ili wasikanyage au kuchafua chakula .
c) Mbuzi mwenye uzito wa moyenne huitaji kilo 500 za chakula kama vile nyasi zilizokauswa kwa
mwaka. Huku kiasi (quantité) cha kila siku kikiwa ni 5 had 7 % ya uzito wake
d) Majani kama vile majani ya mtama au mahindi, mboga zilizotumika, majani ya viazi yapaswa
kukatwa ili kupunguza uharibifu.
e) Ondoa chakula ambacho hakijatumika kutoka banda mara mbili kwa siku. Ikiwa mbuzi wako
hubakisha chakula kingi hii ni ishara kuwa chakula unachowapa hakiwafurahishe, ama wamepewa
chakula kingi kupita uwezo wao ama mbuzi wako hawana hamu ya kula basi watakua ni wagonjwa
f) Wape maji ya kunywa safi na kwa wingi kama lita 5 kwa mbuzi mmoja kwa siku
g) Waweza kuwapa mbuzi wako vyakula vya nafaka (cereale) kama njia ya kubadilisha chakula cha
kawaida lakini kumbuka kubadilisha polepole na sio kwa mara moja ili kuruhusu mbuzi kuzoea
chakula kipya bila kuwadhuru (stresser) Lakini tahadhari (Attehtion) kuwapa mbuzi nafaka peke
yake huweza kusababisha matatizo ya tumbo kwa mbuzi wako pia hakikisha kuwapa mbuzi
madini(Sel mineraux) muhimu kwa wakati sahihi.

UNENEPESHAJI WA MBUZI KWA AJILI YA NYAMA

Unenepeshaji wa mbuzi ni hatua ambayo mbuzi hutengwa (separer) na kuwekwa katika eneo
moja kisha kulishwa vyakula vya protini na nguvu kwa wingi kwa lengo la kupata nyama nyingi, safi
na bora pamoja na soko la uhakika. Hatua hii inayofanywa na mfugaji kabla ya kuuzisha mbuzi wake,
huchukua karibia miezi miwili mpaka minne kabla ya kuchinja ama kuuzisha mbuzi wake.

KWA NINI KUNENEPESHA MBUZI?

Tunanenepesha mbuzi kwa kusudi kubwa la kuongeza ubora wa nyama (upatikanaji wa


nyama nyingi zenye viwango) hasa kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa pamoja na
kupata nyama laini na yenye ladha (Bon goût).

JE, MBUZI WOTE WANAFAA KUNENEPESHWA ?

Mbuzi karibia wote wanafaa katika kunenepesha, kikubwa tu ni kuhakikisha unafuata


taratibu za unenepeshaji ikiwa ni pamoja kulenga (viser) kupata nyama na si kulisha mbuzi kupata
maziwa na nyama kwa wakati mmoja. Mbuzi wa kienyeji na mbuzi chotara (hybride) wanafaa
kunenepesha. Ni vizuri zaidi kunenepesha madume, na kutokuruhusu kupanda mbuzi jike. Mbuzi jike
anaweza kunenepeshwa pia kwa kutokumpandisha tena baada ya kuacha kunyonyesha na kukausha
maziwa ambapo atakuwa akilishwakwa ajili ya kupata nyama tu.
CHAKULA CHA KUENENEPESHEA MBUZI

Katika unenepeshaji wa mbuzi, vyakula vya kwenye makundi mawili makuu yaani protini
na vyakula vya kutia nguvu vinahitajika kwa wingi sana.
1. VYAKULA VYA PROTINI: Vyakula hivi ni pamoja na turto ya mapulunge, soya, mbegu
za kokodiko, majani ya kaliandra, nyasi, majani ya mahindi machanga, majani ya viazi vitamu, majani
ya maharagwe, majani ya njegere, na lusina.
2. VYAKULA VYA KUTIA NGUVU: Vyakula vya kutia nguvu ni pamoja na matete, ukoka,
majani ya tembo,.... Vyakula vya kutia nguvu pia vinaweza kutokana na aina zote za nafaka(cereale),
punje za ngano, au molasesi.
MAJI: Maji yanatakiwa yapatikane saa zote na yawe safi na piya ya kutosha.

MFANO WA CHAKULA CHA ZIADA

AINA YA CHAKULA KIASI/KILO


Pumba za mahindi (saut de maîs) 47
Mihindi iliyo pasuliwa 20
Tourteau ya mapulunge 20
Pumba za muchele (saut de riz)/drêche 10
Chokaa ya mifugo 2
Chumvi 1
Jumla 100

Mfugaji anatakiwa ku fanya yafuatayo ili kupata faida katika ufugaji: kulisha mchanganyiko
wa majani , na mchanganyiko wa vyakula hapo juu.
SURA YA SITA UTUNZAJI WA MBUZI WA UMRI MBALIMBALI UCHAGUZI
WA MBUZI/KONDOO WA KUFUGA

SIFA ZA JIKE BORA LA MBUZI


Kondoo/mbuzi jike wanaofaa kwa kuzalisha wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:
 Historia ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto vizuri,
 Umbo ya utoaji wa nyama nyingi; na
 Asiwe na ulemavu wa aina yoyote
 Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya
kiwele(Maziba);

SIFA ZA DUME BORA LA MBUZI :


Dume bora awe na sifa zifuatazo:
 Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu,
 Asiwe na ulemavu wa aina yoyote,
 Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda; na
 Mwenye kokwa(Testicule) mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana

UTUNZAJI WA VITOTO VYA MBUZI

Hakikisha kitoto kinapata maziwa ya mwanzo(dang’a)siku ya kwanza-3. Kama kinanywesha


kipewe lita 0.7-0.9 kwa siku maziwa haya ni bora kwa kuwa yana viinilishe na kinga dhidi ya
magonjwa Kama mama hatoi maziwa au amekufa kondoo au mbuzi mwingine anae nyonyesha
anaweza kusaidia kukinyonyesha. Kitoto kinyonye kwa wiki12-16 baada ya wiki2 kuzaliwa pamoja na
maziwa apewe chakula kingine kama nyasi ili akuze tumbo lake pia apewe maji ya kutosha.
Aachishwe kunyonya akifikisha miezi 3 Vipewe chanjo ya magonjwa kulingana na ushauri wa
mtaalam dactari wa mifugo.

MATUNZO MENGINE UTAMBUZI

Mbuzi huwekewa alama ili atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu
zake. Shughuli hii hufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni
pamoja na:
 Kuweka alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,
 Kumpa jina kwa wafugaji wenye mbuzi wachache,
 Kumvisha hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,
 Kumvalisha mkanda wenye namba shingoni

KUONDOA VISHINA VYA PEMBE

Mbuzi/kondoo aondolewe vishina vya pembe akiwa na umri kati ya siku 3 hadi 14.
Visipoondelewa hukomaa na kusababisha kuumizana na kuhitaji nafasi kubwa kwenye banda. Kazi hii
ifanywe na mtaalam wa mifugo.

KUHASI (CASTRER)

Vitoto vya mbuzi/kondoo ambavyo havitatumika kwa ajili ya kuendeleza kizazi vihasiwe
kabla ya kufikia umri wa miezi 3. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO WA MIEZI4-8

Mbuzi wa miezi 4 mpaka 8 ni wale ambao wameacha kunyonya mpaka umri wa


kupandishwa kwa mara ya kwanza. Mbuzi wa umri huu wana uwezo wa kula aina mbalimbali za
malisho kama nyasi, miti malisho na mabaki ya mazao wakati kondoo hupendelea zaidi nyasi fupi.
Wakati wa kiangazi huhitaji kupatiwa chakula cha ziada au kupewa pumba (saut) za nafaka(ceréale)
mbalimbali, tourteau ya kokodiko, tourteau ya mapulunge, majani, madini na vitamini. Katika ufugaji
huria (semi-intensif) ni vema kuzingatia hesabu ya mbuzi/kondoo inayoweza kuchungwa katika eneo,
aina na hali ya malisho. Ili mbuzi/kondoo aweze kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka
mapema, mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:
 Kumpatia vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 – 0.7 kwa siku
kuanzia anapoachishwa kunyonya,
 Kumpatia dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za magonjwa mengine
kama itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
 Kuchanja (vaccinner) na kuogesha ili kuzuia magonjwa mbalimbali,
 Kukata kwato mara zinapokuwa ndefu; na
 Kuhasi (castrer)madume yasiyotumika kuzalisha.

UMRI WA KUPANDISHA MBUZI/KONDOO

Mbuzi/kondoo wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na miezi 8 hadi 12 kwa


Hata hivyo, inashauriwa wapandishwe wanapofikia uzito wa kilo 12 au zaidi na wasipandishwe
mbuzi/kondoo wa ukoo (mama) mmoja.

DALILI ZA JOTO

Mfugaji anashauriwa asimpandishe jike kabla hajafikisha umri wa kupandwa wa miezi 8


hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili hata kama
ataonyesha dalili ya kuhitaji dume. Mbuzi/kondoo aliyezaa anaweza kupandishwa siku 30-60 baada ya
kuzaa. Mbuzi/kondoo aliyeko kwenye joto huonyesha dalili zifuatazo:
 Hutingisha/huchezesha mkia,
 Hupanda na kukubali kupandwa na wengine,
 Hutoa ute mweupe ukeni,
 Huhangaika mara kwa mara na kupiga kelele,
 Hufuata madume,
 Hamu ya kula hupungua,
 Hukojoa mara kwa mara,
 Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko ilivyo kawaida; na
 Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa.

Mbuzi/kondoo apelekwe kwa dume mara tu dalili za joto zinapoonekana kwani joto hudumu
kwa wastani wa siku 2 (saa 48). Chunguza tena dalili za joto baada ya siku 19 hadi 21 na kama dalili
hazitaonekana tena kuna uwezekano mkubwa kuwa mbuzi/kondoo amepata mimba. Mfugaji apange
msimu(Période) mzuri wa mbuzi/kondoo kuzaa. Msimu (période) mzuri ni mara baada ya mvua.

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO MWENYE MIMBA

Kwa kawaida mbuzi/kondoo hubeba mimba kwa muda wa miezi 5. Utunzaji


wambuzi/kondoo mwenye mimba ni muhimu kwani ndiyo chanzo cha kupata vitoto vyenye afya bora.
Mfugaji anashauriwa kufuata kanuni zifuatazo:

 Apatiwe vyakula vya ziada kilo 0.2 – 0.7 kwa siku ili kutosheleza mahitaji yake na kitoto
kinachokua tumboni,
 Apatiwe nyasi, miti malisho na mikunde mchanganyiko kilo 1.8 – 2.5 kwa siku.

DALILI ZA MBUZI/KONDOO ANAYEKARIBIA KUZAA

o Huhangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara,


o Sehemu ya nje ya uke hulegea,
o Hujitenga na kundi na hutafuta sehemu kavu na yenye kivuli,
o Hupiga kelele; na
o Hutokwa na ute mzito ukeni.

Mfugaji akiona dalili (signes) hizi anashauriwa asimruhusu mbuzi/kondoo kwenda


machungani, bali amtenge kwenye chumba maalum, ampatie maji ya kutosha na kumuandalia sehemu
ya kuzalia.

KUZAA

Siku chache kabla ya kuzaa, muweke mbuzi huyo kwenye banda safi la peke yake
ukimuwekea matandazo safi ya kulalia, maji, na nyasi nzuri. Usije ukashangaa wakati utakapoamka
asubuhi na kukuta mbuzi ana watoto wawili au watatu, hata kama hakuonyesha dalili. Ni jambo
muhimu sana kupanga kuwa karibu na mbuzi wako anapozaa – lakini kwanza lazima uanze kuwa
karibu naye kuanzia siku ya 140 baada ya kupandwa. Kuna dalili nyingi za kuangalia. Unaweza
kuwagusa watoto kwa mkono wakati mbuzi anapokuwa ametulia na wanaweza kuwa katika kila
upande wa tumbo. Kama utafanya hivyo mara mbili kwa siku utagundua kwamba ni wakati gani
huwagusi. Basi hapo tambua kwamba mbuzi huyo anaweza kuzaa ndani ya saa 12 zijazo. Wakati
mtoto wa kwanza anapokaribia kuzaliwa, mbuzi atalazimika kulala ubavu. Kadiri muda
unavyokaribia, mbuzi ataanza kulalamika. Anaweza kutoa ute wa manjano(jaune).
Wakati anapokuwa na utungu anaweza kukwangua sakafu na kulala na kusimama tena mara
nyingi huku akihangaika. Kama atakuwa na utungu kwa zaidi ya saa mbili au anaonekana kuwa na
matatizo, mwite mtu mwenye uzoefu na mifugo hata jirani, na kama wewe mwenyewe ni mzoefu, basi
ni jambo jema. Njia nzuri ya kujifunza kukabiliana na nyakati hizo ngumu ni kujifunza kwa
kumwangalia mtu mzoefu anavyofanya. Uzazi wa kawaida unaweza kudumu kwa saa nne au zaidi,
lakini ukiona kwamba kuna matatizo ya uzazi kwa mbuzi – kama kutokeza mguu mmoja ukiwa
umejikunja, au kitovu kikiwa kimejiviringa – na unataka kumsaidia mbuzi, hakikisha unanawa mikono
yako kwa sabuni yenye dawa (germicidal soap) na kupaka mikono mafuta yenye madini, kabla ya
kuingiza mikono yako kumsaidia. Kwa bahati nzuri, mambo kama haya yanaweza yasitokee mara ya
kwanza unapokuwa umejianza ufugaji wako, lakini ikiwa yatatokea wala usishangae. Ingiza mikono
yako, jaribu kuangalia mikono ya mbele na kichwa halafu saidi kuvivuta taratibu ukisubiri mbuzi
asukume kwanza. Ninazungumza haya kutokana na uzoefu na utaalamu wangu katika ufugaji, kwa
sababu nimekwishawahi kusaidia hata ng’ombe kuzaa. Kama una uzoefu na ujasiri ni jambo
linalowezekana. Hatua muhimu baada ya kuzaa ni kuondoa utando kwa watoto ili kuwafanya wapate
hewa (mama yao anaweza kufanya hivyo kwa kuwalamba kama wewe haupo), wawekee iodine
kwenye vitovu ili kuzuia maambukizi hasa ya bakteria na uwakaushe watoto.

Taratibu jaribu kukamua maziwa kutoka kila titi ili kujiridhisha kwamba linafanya kazi na
siyo limeziba. Safisha matandazo ya kulalia na weka mengine safi. Hakikisha kwamba watoto
wanapata maziwa ya kwanza (colostrum), ikibidi yakamue na uwanyweshe watoto kwa kutumia chupa
maalum yenye nyonyo kama zile za watoto. Maziwa hayo mazito ya njano yanayotoka katika siku za
kwanza ni muhimu kwa ukuaji wa watoto. Mbuzi huchukua muda wa siku kati ya 146 hadi 156 tangu
kupata mimba hadi kuzaa. Kwa wastani (en moyenne) tunaweza kusema kuwa mbuzi hushika mimba
kwa muda wa miezi mitano (5). Wiki mbili kabla ya kuzaa, anza kuandaa mahali pa Kuzalia.
Hakikisha kuwa mahali hapo ni safi, pakavu, pana mwanga na hewa ya kutosha, na pametandikwa
nyasi kavu ambazo hazijawahi kutumika. Hakikisha kuwa nyumbani kwako unayo dawa ya joto
(iodine) wembe mpya pamoja na kitambaa safi kwa ajili ya matumizi mara atakapozaa.

DALILI ZA KUZAA

Ibakiapo muda kati ya wiki 6 hadi 1 kabla ya kuzaa, kiwele cha mbuzi huonekana kikubwa
na kilichojaa. Utunzaji wa kumbukumbu za upandishaji itakusaidia kukumbuka tarehe uliyompandisha
mbuzi wako. Siku kadhaa kabla ya tarehe anayotarajiwa kuzaa, mhamishie mbuzi mahali ulipoandaa
kwa ajili ya kuzalia. Mpe malisho, vyakula vyenye protini na maji ya kunywa. Kwa tahadhari, baada
ya kumpa mbuzi wako maji hakikisha huachi ndoo (mbegeti) au chombo kingine cha maji mahali
hapo. Hii ni kwasababu ukiacha ndoo ya maji mahali hapo mbuzi anaweza kuzaa na mtoto
akatumbukia kwenye maji na kufa.

DALILI ZA KUZAA KWA MBUZI NI KAMA IFUATAVYO

1) Mbuzi hupoteza tabia ya utulivu na kuwa na wasiwasi.


2) Hutembetembea na mara nyingine husimama na kuparua nyasi za kulalia kwa kutumia miguu yake.
3) Sehemu ya nyuma karibu na mkia huonekana kuzama ndani kuliko kawaida.
4) Iwapo mbuzi huyo yuko kwenye kundi pamoja na wenzake atajitenga na kukaa peke yake.
5) Mbuzi huonyesha tabia ya upendo usio wa kawaida kwa binadamu aliye karibu naye. Kwa mfano,
ukisimama karibu naye ataonyesha tabia ya kujali kuwepo Kwako kwa kukulamba vidole.
6) Mbuzi hulala chini na kusimama mara kwa mara.
7) Mara nyingine anapokuwa amelala chini hutazama nyuma kupitia mabegani mwake na kutoa sauti
kama vile anaongea.
8) Mbuzi pia hutokwa na majimajiukeni.
9) Chupa ya uzazi hutokeza kutoka kwenye uke na hatimaye kupasuka na kumwaga maji yake.
10) Mtoto kuanza kujitokeza katika kipindi cha saa moja tangu chupa kupasuka.
11) Mbuzi huonyesha dalili za kusukuma ili mtoto aweze kutoka nje ya tumbo la uzazi.

MKAO WA KAWAIDA WA MTOTO WA MBUZI NDANI YA TUMBO LA UZAZI

Kwa kawaida wakati wa kuzaliwa mtoto wa mbuzi anaweza kutoka katika tumbo la uzazi
akiwa ametanguliza miguu ya mbele na kufuatiwa na pua katikati ya miguu hiyo.Mara nyingine ni
jambo la kawaida mtoto kutoka akiwa ametanguliza miguu ya nyuma. Inapotokea kuwa mbuzi anazaa
mapacha, ni kawaida kwa mtoto mmoja kuanza kutoka na kisha kufuatiwa na mwenzake. Kwa
kawaida pacha moja hutanguliza miguu ya mbele wakati mwenzake akitanguliza miguu ya nyuma.

KUTOA MSAADA KWA MBUZI WAKATI WA KUZAA

Inatakiwa mtoto awe amezaliwa katika kipindi cha saa moja tangu kupasuka kwa chupa ya
uzazi. Ikiwa katika kipindi hicho mbuzi atakuwa bado hajazaa, huenda akahitaji msaada wako.

1) Mbuzi atahitaji msaada kutegemeana na jinsi mtoto alivyokaa au anavyotoka kwenye njia ya uzazi.
2) Muoshe mbuzi sehemu ya nyuma kwa maji na sabuni na hakikisha kucha za mikono yako ni safi na
zimekatwa.
3) Ingiza mkono wako taratibu katika tumbo la uzazi na jaribu kupapasa na kupata ukweli juu ya
kinachoendelea ndani na ikiwezekana omba mtu mmoja akusaidie kumshika mbuzi huyo
4) Fanya marekebisho yanayostahili hadi mtoto wa mbuzi akae katika mkao ambao ni wa kawaida
kabla ya kuanza kumvuta nje taratibu kila mbuzi anaposukuma.
5) Ikiwa mtoto atakuwa anatoka akiwa ametanguliza mkia, jaribu kumgeuza mtoto huyo taratibu hadi
akae katika mkao wa kawaida. Katika hali ya namna hii, pengine mkao wa kawaida utakaokuwa
rahisi zaidi kuufanya ni ule wa kumgeuza mtoto taratibu hadi atangulize miguu ya nyuma.
6) Ikiwa mtoto atakuwa anatoka kwa kutanguliza miguu ya mbele lakini akiwa amekunja shingo na
kutazama nyuma, isukume miguu hiyo na kuirudisha ndani kisha ingiza mkono ndani zaidi ya
tumbo la uzazi na kukiweka kichwa cha mtoto kwenye kiganja. Kishike vizuri kichwa cha mtoto
wa mbuzi na kukivuta kiasi ili shingo inyooke na hivyo kichwa hicho kuwa katikati ya miguu
miwili ya mbele.

Katika mkao huu wa kawaida, mbuzi anaweza kuendelea kuzaa mwenyewe. Vinginevyo toa
msaada zaidi kwa kumvuta mtoto taratibu kila mara mbuzi anaposukuma. Ikiwa mtoto anatoka kwa
kutanguliza mguu mmoja tu wa mbele wakati mwingine umebakia nyuma, ingiza mkono kwenye njia
yauzazi kisha rudisha mguu huo kwenye tumbo la uzazi pamoja na kichwa kinachotangulia kutoka.
Ukianzia shingoni peleka mkono wako taratibu hadi kifuani na kisha kwenye goti la mguu wa mbele
wa mtoto. Zungusha kidole kwenye mguu huo uliobaki nyuma na kuuvuta taratibu ili kunyoosha
kuelekea nje ya tumbo la uzazi. Sasa miguu yote ya mbele itakuwa imenyooka na kichwa kikiwa
katikati yake. Katika mkao huu wa kawaida mbuzi anaweza kuendelea kuzaa mwenyewe na
ikishindikana toa msaada zaidi kwa kumvuta mtoto taratibu kila mara mbuzi anaposukuma Ikiwa
mtoto anatoka akiwa ametanguliza mguu mmoja wa mbele na huku akiwa amelala kwa mgongo,
rudisha ndani ya tumbo la uzazi kichwa pamoja na mguu unaotangulia kutoka. Ukianza shingoni,
peleka mkono wako taratibu hadi kifuani na kisha kwenye goti la mguu wa mbele wa mtoto. Zungusha
kidole kwenye mguu huo uliobaki nyuma na kuuvuta taratibu ili kuunyoosha kuelekea nje ya tumbo la
uzazi. Jaribu kumgeuza taratibu ili akae katika mkao wa kawaida na kutoka nje ya tumbo la uzazi kwa
kusukumwa na mama yake. Ikiwa watoto wawili watakuwa wakitoka kwa pamoja basi utalazimika
kuwa mwangalifu zaidi wakati wa kutoa msaada. Kwanza, sukuma na kurudisha ndani ya tumbo la
uzazi miguu yote itakayokuwa imeanza kutokeza nje. Chambua miguu miwili ya mtoto mmoja pamoja
na kichwa chake na hakikisha miguu pamoja na kichwa cha mtoto huyo vimetengana na kichwa
pamoja na miguu ya mtoto wa pili nahivyo kutokuwepo kwa kuingiliana. Msaidie mbuzi kutoa mtoto
wa kwanza kabla ya kuendelea kutoa mtoto wa pili.

MARA BAADA YA MTOTO WA MBUZI KUZALIWA HAKIKISHA UNAFANYA


YAFUATAYO

Mwangalie kama yuko hai na kata kitovu ili kumtenganisha mtoto :

1. Mtoe ute mdomoni, masikioni na puani kwa kutumia kidole safikisichokuwa na kucha ndefu
au kitambaa kisafi.
2. Kama ataonyesha tatizo la kushindwa kupumua, mshike miguu ya nyuma na kumning’iniza
kichwa chini huku ukimtikisa. Kama hapana budi, mwagie maji ya baridi ili kumshtua na
kumfanya aanze kupumua.
3. Mpake dawa ya joto ya (iodine) kwenye kitovu chake.
4. Mweke karibu na mama yake ili aendelee kumlamba.
5. Katika kipindi cha saa 1 hadi 2, hakikisha kuwa amesimama na kunyonya kwani maziwa ya
mwanzo yana viinilishe muhimu kwa ajili ya ukuwaji na kumwezesha mwili wake kujikinga
na maradhi.
6. Mruhusu mtoto wa mbuzi ashinde na mama yake kwa muda wa siku 3 hadi 4 tangu kuzaliwa.
Baada ya muda huo kupita unaweza kuanza kumtenga mbali kidogo na mama yake.

UTUNZAJI WA MBUZI/ KONDOO ANAYENYONYESHA

Mbuzi/kondoo anayenyonyesha huhitaji chakula kingi zaidi ili kukidhi (Satisfaire) mahitaji
ya mwili na kuzalisha maziwa kwa ajili ya kitoto/vitoto. Pamoja na nyasi, mikunde na majani ya miti
malisho kilo 1.8 – 2.5 kwa siku ni muhimu apewe chakula cha nyongeza kilo 0.3 – 0.8 kwa kila lita ya
maziwa inayoongezeka baada ya lita 2 na maji safi, salama na ya kutosha wakati wote. Ikitokea mama
hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza maziwa mbadala ya aina hiyo au kama kuna
mbuzi mwingine aliyezaa anaweza kusaidia kukinyonyesha kitoto hicho. Hata hivyo, wafugaji wengi
wa mbuzi wa maziwa huwaondoa watoto kwa mama yao mapema baada ya kuzaliwa na kuwapatia
maziwa kwa kuwakamulia. Watoto hao lazima walazwe kwenye sehemu safi, kavu na salama, na
ikiwezekana wawe mbali na mama yao. Kuwanywesha maziwa badala ya kunyonya kunahitaji
ustahimilivu na muda kwa sababu lazima uwafundishe watoto namna ya kunywa maziwa hayo.
Wafugaji wengi wanawanywesha watoto maziwa ya vugu vugu kulingana na joto la mama, mara tatu
au nne kwa siku. Wiki 2 baada ya kuzaliwa, pamoja na maziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama
nyasi laini na chakula cha ziada ili kusaidia kukua kwa tumbo. Uwaachishe watoto kwa kuangalia
uzito, siyo umri, na ni lazima wanapokuwa wamefikia uzito wa kilogramu9, bila kusahau kuvipatia
kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo. Lakini hakikisha kwamba
kitoto kinapewa maji wakati wote na vyombo vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote.
UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU

Dume bora la mbegu ni muhimu litunzwe ili liwe na uwezo wa kutoa mbegu bora, kupanda
na kuzalisha. Dume bora huanza kupanda akiwa na umri kati ya miezi.8 - 10 kwa mbuzi
walioboreshwa. Katika msimu wa kupandisha dume moja liruhusiwe kupanda majike 40 hadi 50.
Aidha, inashauriwa madume wenye umri wa miezi 8 – 9 waruhusiwe kupanda majike ambao ndio
mara ya kwanza kupandwa.

DUME APATIWE:

 Malisho ya kutosha na vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 0.2 – 0.7 kwa siku na maji ya
kutosha,
 Majani ya miti malisho, na nyasi mchanganyiko na mabaki ya mazao; na
 Kilo 0.45 hadi 0.9 za chakula cha ziada za nyongeza kwa siku kulingana na uzito wake na wingi wa
majike anayopanda.wiki 2 kabla na baada ya kuanza kupanda.

MATUNZO MENGINE KUKATA MKIA

Mara nyingine kondoo hukatwa mkia ili kuruhusu mtawanyiko mzuri wa mafuta katika
nyama mwilini. Pia kondoo aliyekatwa mkia huwa msafi. Kazi hii ifanywe kama itakavyoshauriwa na
mtaalam wa mifugo kwa kutumia vyombo maalum. Inashauriwa mkia ukatwe urefu wa sentimita 2.5 –
3.8 kutoka kwenye shina la mkia wakati kondoo akiwa na umri wa siku 3 mpaka mwezi 1.

KUMNYOA KONDOO WA SUFU

Sufu hunyolewa wakati kondoo akiwa hai au amechinjwa. Kwa kawaida hunyolewa miezi 6
hadi mwaka 1 ambapo sufu huwa imefikia urefu wa sentimita 15 – 20.Vifaa vinavyotumika ni pamoja
na mikasi au visu maalum. Uangalifu unahitajika wakati wa kunyoa ili ngozi ya kondoo isiharibike.
Unyoaji ufanyike wakati wa kiangazi na siyo wakati wa mvua, kondoo akiwa na mimba au kipindi cha
majani kutoa mbegu.
SURA YA SABA MAGONJWA MBALIMBALI YA MBUZI NA TIBA ZAKE

Magonjwa husababishwa na vimelea jamii ya virusi, bakteria, protozoa na riketsia.


Magonjwa mengine husababishwa na upungufu wa viinilishe, vitamini na protini.

DALILI ZA MBUZI/KONDOO MGONJWA NI PAMOJA NA:

o Manyoya husimama,
o Kuzubaa, kusinzia, kukohoa na kupiga chafya,
o Kukosa hamu ya kula na kunywa maji,
o Kujitenga na kundi,
o Kuvimba taya la chini,
o Kupumua kwa shida,
o Kutokwa na machozi na makamasi,
o Kuwa na upele au uvimbe kwenye sehemu ya mwili; na
o Kutupa mimba. Hatua za haraka za kumuona mtaalamu wa mifugo zichukuliwe iwapo baadhi ya
dalili hizi zitaonekana.

SIFA ZA MBUZI MWENYE AFYA

a) Mchangamfu wakati wote macho maang’avu huku mkia na masikio vikimsaidia kufukuza inzi
b) Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
c) Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi
d) Kutembea vizuri
e) Anastuka na kukimbia anapostuliwa na mnyama hatari anapomkaribia kamaa vile mbwa
mwitu, fisi, chui, simba.
f) Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha
kama vile maziwa.
g) Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukuna wanaongezeka uzito kwa
muda mfupi
h) Kwa mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto wake,kiwele
huwa kimejaamaziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka upande kwa ajili ya kujaa
maziwa ix.Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
i) Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto. Miili yao
hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake (yaani katikati ya
miguu)
j) Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
k) Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
l) Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka

VYANZO VYA MAGONJWA

Magonjwa mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa


damu na kusababisha homa na baadae madhara makubwa. Mangonjwa mengi ya mifugo
husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano mazingira machafu anayoishi
mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (Vitu vyenye ncha kali) husababisha vidonda ambapo
vimelea(parasites) vinaweza kukaa.Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali za ndani ya
mwili kama upungufu wa lishe, mfano: madini (sel minéraux) na magonjwa ya kurithi.
CHANJO NA KINGA

o Mbuzi na kondoo wachanjwe dhidi ya magonjwa ya homa ya maapafu. Ugonjwa huu ni hatari sana
na huenea kwa njia ya hewa na unaweza kusababisha vifo kati ya asilimia 60-100,
o Kila baada ya miezi 6 mifugo ipatiwe kinga dhidi ya ugonjwa wa miguu na midomo na magonjwa
mengine kama Kimeta, kutupa mimba na kambavu (BQ) zitolewe kulingana na ushauri wa
mtalaam wa mifugo,
o Kama kuna wanyama waliopata magonjwa watengwe kwenye kundi, wasisafirishwe au kuuzishwa,
o Mbuzi/kondoo wapatiwe dawa ya minyoo. Vitoto vya mbuzi/kondoo vipatiwe dawa ya minyoo
vinapofikia umri wa mwezi 1. viendelee kupatiwa dawa ya minyoo kila mwezi hadi vinapofikia
miezi 5 na baada ya hapo vipatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3 - 4; na
o Zingatia usafi wa banda ili kuwakinga na ugonjwa wa kuharisha na kuharisha damu na magonjwa
mbalimbali.

MAGONJWA YANAYOWAPATA MBUZI

Unaweza kuhakikisha kuwa unawachunguza mbuzi wako mara kwa mara na kuwapa chanjo
(vaccin) ili kuwakinga dhidi ya magonjwa,wadudu hatari na kuwalisha vyakula bora viliyvo na madini
(sel minéreaux) muhimu. Baadhi ya magonjwa yanayowasumbua mbuzi ni kama vile:

1. UGONJWA WA HEART WATER:

Huu ni ugonjwa wa bacteria unaosababishwa na kupe, Hata mbuzi wanaofanyiwa zero


grazing wanaweza kumbukizwa ugonjwa huu. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kufa kwa mbuzi
wengi haswa wachanga,kupoteza hamu ya kula chakula,matatizo ya kupumua,na mara nyingi mbuzi
huwa mnyonge (faible). Waoshe mbuzi wako mara kwa mara ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huu.
Ukiwa sehemu za Beni, Kabasha, Mataba, Mangina, ....... waoshe mbuzi mara ........; Ukiwa sehemu
za Lubero, Masereka, Luotu, Kyondo........ waoshe mbuzi wako mara ...... kwa ........; Ukiwa sehemu
za Butembo, Butuhe, Rwahwa, Masoyi, Mwenye osha mbuzi wako mara ................. kila ................

2. HOMA YA MAPAFU (pneumonia )

Ni ugonjwa wa kuambukiza mbuzi wakati mbuzi wenye afya nzuri wanapokaribiana na wale
wagonjwa Dalili (Symptômes) za pneumonia ni kama vile ongezeko la joto mwilini na matatizo ya
kupumua na vifo kwa wingi haswa katika maeneo ambao ugonjwa huu umeenea Wape chanjo mbuzi
wako mara kwa mara Zingatia marufuku ya kusafirisha mifugo maarufu kama karantine na uhakikishe
kuwa wanyama wamechunguzwa kabla ya kuwasafirisha ama kuhamishwa.

3. KUVIMBA KIWELE ( MASTITIS)

Ugonjwa wa kuvimba kiwele ni kawaida kwa mbuzi hasa wa maziwa. Ni uvimbe ambao
mara ya kwanza huonekana kama kiwele kimekua kigumu mfano wa jipu. Wakati mwingine huweza
kutoa maziwa yasiyo ya kawaida. Mbuzi hutoa maziwa yenye povu jingi ambalo sio la kawaida.
Ugonjwa huu mara nyingi hutokana na uzembe wa mfugaji kutofuata kanuni bora za ukamuaji wa
maziwa. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea kama STAPHYLOCOCCI, STEPTOCOCCI
DALILI ZA UGONJWA HUU:

i. Homa kali wakati uvimbe ni mkubwa


ii. Kiwele kinakua kikubwa sana na kigumu
iii. Maziwa yanakua na majimaji na povu jingi
iv. Maziwa yanakua na damudamu
v. Maziwa yanakua kidogo kuliko kiwango cha kawaida

MUHIMU kama maambukizi ni makubwa sana maziwa yanachachuka haraka, yanaganda na kutoa
harufu mbaya

KINGA : Osha kiwele kwa kutumia dawa maalumu ya majimaji ya KMNO4 solution na baada ya
kutumia kamua maziwa kwenye kiwele hicho Mwanzishie mbuzi dawa ya antibiotics acha kwa masaa
24 na rudia tena kwa siku 3 lakini mbuzi kila wakati wapimwe kama wana uvimbe kwenye kiwele

TIBA: Kwanza kabisa inahitajika kupimwa kwa kutumia kipimo cha RAPID MASTITIS TEST Kisha
mbuzi wanaweza kutibiwa kwa kutumia dawa kama vile TERRAMYCIN, ORBENIN L/A au
AUREOMYCIN 4.

SOTOKA/ NDIGANA ( RINDERPEST): Ugonjwa huu hushambulia sana mbuzi, ng'ombe na


kondoo. Kwa wafugaji wanauelewa ni ugonjwa hatari sana unaweza kumaliza ziziz lako lote mara
moja.

DALILI ZA UGONJWA HUU

i. Homa za kushitukiza
ii. Kuhara
iii. Sehemu ya haja kubwa huwa inakua imevimba au imechubuka.

KINGA/TIBA : Jitahidi kutoruhusu watu kuingia ovyo zizini na hata kwa wanaoingia chimba shimo
dogo kwenye mlango, weka maji na dawa maalumu ili kila anayeingia humo na kutoka lazima aingize
miguu yake humo kuua vijidudu. Kama kuna mnyama ameambukizwa mchome sindano ya RINDER
PEST VACCINE S/C

Lakini ni muhimu sana ukatoa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu yako maana
ugonjwa huu unaweza kusambaa.

4. COCCIDIOSIS

Ugonjwa huu unaweza kuwakumba hata mbuzi pia licha ya kuwa maarufu kwa kuku na
ndege wengine Dalili kubwa ni kuhara damu, upungufu wa damu udhaifu na kifo kwa watoto. Kwa
wale wanaokamuliwa kiwango cha utoaji wa maziwa hupungua na maziwa huwa na harufu kali.
KINGA/TIBA:
i. Lazima kipimo cha FAECAL kifanyike kwa mbuzi wako;
ii. Wapatiwe dawa ya SULPHAMEZATHINE kwa kuangalia uzito wao;
iii. Wapatiwe AMPROSOL 20% ya majimaji kulingana na uzito wa mnyama kwa siku 4 hadi 5 au
waweza kuwapatia ZOAQUIN

5. UGONJWA WA KLAMIDIA

Ugonjwa huu unasababishwa na bakteria aina ya Klamidia. Dalili zake kubwa ni pamoja na:

a) Homa ya mapafu

b) Wakati mwingine mbuzi huharisha

c) Mbuzi mwenye mimba anaweza kuharibu mimba

d) Kwa mbuzi wadogo wanaweza kuwa na kifua cha kukoroma

MUHIMU (N.B): Wakinge mbuzi wako kwa kuwachoma sindano ya PENICILLIN

6. COLLIBACILLOSIS /COLLISOPTICAEMIA

Huu ni ugonjwa unaowapata hasa mbuzi wadogo wenye umri chini ya mwezi mmoja. Dalili zake
kubwa ni pamoja na:

i. Homa kali
ii. Kuhara au kuhara damu
iii. Kukosa hamu ya kula
iv. Kuchachamaa kwa manyoya na ngozi kukauka katika hatua za baadae

KINGA/ TIBA

a) Puliza dawa ya kuuwa bakteia kwenye mazingira yote yanayozunguka banda na kwenye
banda la mbuzi kila wakati
b) Mbuzi wote wadogo wapatiwe dawa ya antibiotic
c) Dawa kama DARZIN yenye mchanganyiko wa neomein, chloromycetin, septran na quixallin
bolus hutumika zaidi.
7. CYSTITIS

Huu ni ugonjwa ambao dalili zake kubwa ni kuvimba kibofu, kutoa mkojo kidogo, kukosa
hamu ya kula na kusikia kiu sana TIBA Mtibu mnyama kwa kutumia antibiotic ukiichanganya na lita
2 za maji ya uvuguvugu na kijiko kimoja cha HIBITANE.

8. ANAEMIA

Huu ni upungufu wa damu ambao hutokea pia kwa mbuzi. Ngozi inaweza kupauka na
unaweza kuona kubadilika kwa ngozi katima macho, midomo, kiwele na sehemu zote zisizo na
manyoya Unaweza kuwatibu kwa kuwachoma sindano yenye madini joto kwa kiwango cha 5ml
DEXAVIN (PFIZER) au FERROFAX ( duphar).

9. KUHARIBU MIMBA

Kuharibu mimba hutokea mara nyingi wakati mbuzi wanapokuwa na mimba changa mpaka
miezi 3. Tiba ya kitaalamu inahitajika kwa wakati huo ili kuzuia jambo hilo. Tatizo hili huweza
kutokea pale mbuzi anapo kunywa maji yenye wadudu aina ya Salmonella typhinmurium, huweza
kutokea pia mbuzi anapolishwa chakula kisicho kizuri kwa kipindi ameshika mimba au mbuzi
aliyepandishwa kabla ya muda wake.
10. MINYOO NA WADUDU

Wadudu kama minyoo na kupe wanahitaji umakini wako kama mfugaji. Kumbuka kuwa
mbuzi wote wana minyoo lakini mfugaji wa mbuzi anaweza kuwadhibiti kwa kuwapatia mbuzi wako
dawa za minyoo kila wakati hasa kila baada ya miezi 3.

11. KETOSISI / ACETONEMIA:

Huu ni ugonjwa ambao hutokea kwa mbuzi wenye mimba hasa mwezi wa mwisho kabla ya
kuzaa. Mara nyingi huwatokea mbuzin wenye uzito mkubwa au ambao hawajalishwa vizuri na walio
kwenye mazingira hafifu Lakini ugonjwa huu unaweza kusababishwa na mazoezi makali kama
kufukuzwa na mbwa.

DALILI ZAKE

i. Mbuzi kuzubaa
ii. Anaweza kupatwa na kiharusi na kuharibu mimba

MUHIMU: Hata hivyo kumpatia kikombe cha molasses mara mbili kwa siku, mbuzi huyo ana
asilimia 50 kwa 50 za kupona .

12. NDUI YA MBUZI ( GOAT POX)

Ndui ya mbuzi inahusisha vivimbe ambavyo hubadilika na kutoa majimaji , kisha kunata na
majipu kwenye kiwele au sehemu ambazo hazina manyoya. Ndui ya mbuzi huweza kudhibitiwa kwa
utunzaji mzuri.

DALILI ZAKE

i. Homa
ii. Uvimbe na vidonda unaotokea kwenye sehemu zisizo na manyoya
iii. Kwa mbuzi wadogo jotokali hutokea lakini kifo huweza tokea kabla hata ngozi haijavimba.

KINGA :
Watenge mbuzi wagonjwa na kila siku waoshe kwa mchanganyiko wa hydrogen peroxide
dilute kwenye mchanganyiko wa maji ya vuguvugu Kuwapaka crem maalamu au waweza kuwapa
mafuta ya mgando Hakikisha mbuzi wenye ugonjwa wanakamuliwa mwishoni ili kuzuia kusambaa
kwa ugonjwa

14. BLOAT

Ugonjwa wa bloat unasababishwa na kuwa na gesi nyingi tumboni hasa kwenye utumbo
mpana na utumbo wa kati. Hii mara nyingi hutokea wakati mbuzi wanapoachiliwa kwenda malishoni
au wanapokula vyakula vingi vyenye kiwango kikubwa cha Succulents hasa nyasi aina ya Lucerne

DALILI ZAKE

 Mbuzi anakosa rahaa


 Mbuzi anakokota miguu chini
 Anakojoa mara kwa mara
 Anatembea kwa ukakamavu (marche difficile)
 Tumbo huwa limejaa gesi na kuwa gumu

Kama ilivyo kawaida kinga ni bora kuliko tiba , walishe mbuzi wako majani makavu kabla
hujawaachia kwenda kwenye malisho.

15. BRUCELLOSIS (BRUCELLA ORGANISMS)

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na vijidudu na unaweza kusumbua mbuzi wako. Ugonjwa


huu huweza kuwa na dalili (symptômes) zifuatazo :

i. Kuharibu mimba mwishoni kabisa wakati anakaribia kuzaa


ii. Maumivu kwenye placenta
iii. Kwa mbuzi dume kutokuwa na uwezo wa kurutubisha mimba na korodani kuvimba.

KINGA

Mbuzi ni lazima wawe wanapimwa mara kwa mara na walioambukizwa kuwatenga na


wengine unaweza kuwapatia dawa za antibiotics.
16. KICHA KIKUBWA

Ugonjwa huu wa kicha kikubwa hutokea wakati mbuzi anakuwa ameshambuliwa sana na
magonjwa hasa minyoo. Amabapo mbuzi hutoa sana ute, kuvimba kichwa na kupauka kwa ngozi.

17. KIMETA (GOAT ANTHRAX)

Kimeta ni ugonjwa hatari sana kuliko hata sokota, unaweza kufagia kundi zima la mifugo
katika muda mfupi na unaambukiza na baktera wanaoitwa Baccillus Anthracis

DALILI ZAKE

 Kupanda ghafla kwa joto kufika 108F


 Kukosa hamu ya kula
 Kutokwa kwa povu mdomoni
 Vifo vya ghafla
 Mbuzi anaweza kuishi kwa siku moja na kuanza kuhara damu kabla ya kufa

MUHIMU

Inashauriwa kuwa mnyama aliyekufa kwa kimeta afukiwe kwenye shimo kubwa au
kuchomwa moto kwani bakterria hao wanaweza kusambaa na kuambukiza wanyama wengine

KINGA/ TIBA

 Watenge wanyama walioshambuliwa,


 Hakikisha kila mwaka unawachanja wanyama wako hasa maeneo ambayo hutokea mara kwa
mara ugonjwa huu,
 Dozi kubwa ya PENICILLIN inaweza kuwatibu wanyama hao.

18. UVIMBE WA MAJIPU ( LYMPHADENTITIS)

Uvimbe wa majipu ni tatizo lingine linalojitokeza mara kwa mara kwenye ufugaji wa mbuzi.
Uvimbe huu au jipu hujitokeza mara kwa mara kwenye bega ingawa unaweza tokea sehemu nyingine
kama kwenye paja au mbavu. Mbuzi wengi sana hupatwa na uvimbe huu, na si ajabu katika mazingira
yetu ya kawaida ukakuta kundi la mbuzi limeenea na uvimbe huu. Baadhi ya watu hawapo makini na
uvimbe huu na huona ni jambo la kawaida tu. Inapotokea mmoja ana uvimbe huu ni lazima kumtenga
na wenzake. Kama mbuzi ni wa maziwa basi hata maziwa ya mbuzi huyo hayafai kunywewa. Uvimbe
huo hauwezi kumsumbua mbuzi lakini ni hatari kama ukitokea maeneo ya koo (gorge) kwani huweza
kukuaa na kusababisha kupitisha hewa na chakula kwa shida hivyo mnyama anaweza kufa.

NB Mtafute mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe uonapo dalili za ugonjwa huu kwa
mbuzi wako ili waweze kupata huduma ya kupasua uvimbe huo inayostaili.
19. RIFT VALLEY FEVER

Huu ni ugonjwa wa unaosababishwa na virusi vinavyosambazwa na mbu (Mouche)na


hutokea sana sana wakati wa mvua wakati mbu wanapozaana kwa wingi. Watu na mifugo wanaweza
kuambukizwa kwa kukanyaga kinyesi(fiante, escrement) ama mkojo wa wanyama wagonjwa na
kupitia kula ama kukanyaga nyama mbichi Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na homa ya ghafla,kukosa
hamu ya kula,kutoka kwa makamasi yaliyo na usaha puani,kutokwa na jasho jingi,kuhara,vifo visivyo
vya kawaida kwa wanyama wachanga na kutoka/kuharibika kwa .

Dalili hizi za ugonjwa huu hufanana na zile za magonjwa mengine na unapaswa kumwita
daktari wa mifugo ili akuthibitishie.

Ugonjwa huu unaweza kuzuilika kupitia chanjo na kuwazuia mbu Minyoo Hawa ni wadudu
wanaokaa kwenye tumbo la mbuzi.

Huathiri(menancer) uchangamufu wa mbuzi zaidi sana wale wadogo ambao hufa ikiwa
minyoo watakuwa wengi .

Wakati minyoo wanapozaana na kuwa wengine huamia kwenye mapafu na wanaweza


kusababisha matatizo ya kupumua.

Minyoo wanaweza kuzuiliwa kwa kuwapa mbuzi dawa ya kuua minyoo mara kwa mara
lakini ni muhimu kumshauri daktari wa mifugo kabla ya kuwapa dawa kwani dawa zingine huua aina
nyingi ya minyoo huku zingine zikiangamiza aina moja pekee. Kupe, Chawa, Viroboto.

Kupe huambukiza mbuzi magonjwa na ni vyema kuyazuia magonjwa haya oWadudu kama
vile viroboto,chawa hufyonza damu na kuwasumbua mbuzi.
SURA YA MUNANE : UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA MIFUGO

Kuweka kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua


gharama za utunzaji na faida. Pia, humsadia mfugaji kufanya maamuzi katika uendelezaji wa ufugaji
wake. Mtalaamu wa mifugo pia anaweza kutumia kumbukumbu hizi ili kumsaidia mfugaji kuboresha
ufugaji wake.

KUMBUKUMBU MUHIMU ZINAZOHITAJIKA KUTUNZWA NI:

o Kumbukumbu za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa mbuzi/kondoo kwa kila
mwezi ili kufuatilia ukuaji wake, tarehe ya kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa,
o Kumbukumbu ya uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi yake, aina (breed),
namba ya dume/jike, na uzito wa kuzaliwa,
o Kumbukumbu za upandishaji zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo anayepandwa, tarehe ya joto
na ya kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili kama atarudia na
tarehe ya kuzaa,
o Kumbukumbu za chanjo na matibabu zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya matibabu,
aina ya chanjo au ugonjwa, dawa iliyotumika, idadi ya waliokufa na waliopona na jina la mtaalam
aliye tibu,
o Kumbukumbu za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya kuzaa, kiasi cha
maziwa kwa siku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote cha kukamuliwa, tarehe ya kuacha
kukamua na idadi ya siku alizokamuliwa,
o Kumbukumbu za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au
kununuliwa kwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa nacho kila wakati, kiasi cha fedha unacho dai
na kudaiwa.

You might also like