Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Shule kuu ya Sheria kanyabuhinya@yahoo.co.uk Utangulizi na Historia Sheria zinazohusika na kulinda Hakimiliki Hakishiriki ni nini Umuhimu wa kulinda Hakimiliki Haki zinazolindwa Vigezo vya kazi zinazostahili kulindwa Muda wa ulinzi Mmiliki wa Hakimiliki ni nani? Jinsi ya kunufaika na hakimiliki Hakimiliki za kimila Vyama vya kulinda hakimiliki na wajibu wake Sheria za kimataifa Ukiukwaji na adhabu Umuhimu wa kurekebisha sheria zinazohusiana na hakimiliki Nini Kifanyike kuimarisha ulinzi wa kazi zenye hakimiliki Hakimiliki na hakishiriki ni moja sehemu ya sheria zinazohusu ulinzi wa kisheria wa miliki bunifu. Hakimiliki kwa upande wake hulinda kazi za ubunifu za kiuandishi na za wabunifu wa sanaa (literary and artistic works) Sheria huzuia kazi hizi zisinakiliwe, kuzalishwa au kusambazwa na mtu mwingine asiye mmiliki wa kazi husika. Sheria ya kwanza ya hakimiliki ilitungwa Tanganyika mwaka 1924 (The Copyright Ordinance) Sheria ya mwaka 1924 ilifutwa baada ya uhuru hapo mwaka 1966 na sheria namba 61 ya mwaka 1966. Mwaka 1999 bunge la Tanzania lilitunga sheria mpya ya Hakimiliki na hakishiriki (sura na 218) ambayo ndiyo inatumika mpaka sasa Hakimiliki ni haki ya msingi inayolindwa kisheria kwa kazi yoyote ya utunzi, ubunifu na uandishi wa kazi za maandishi na za kisanii. Hakishiriki ni haki muambata kwa hakimiliki apewayo mshiriki katika kazi inayolindwa na hakimiliki, mfano mtunzi wa mziki anakuwa mmiliki wa hakimiliki, wachezaji wa jukwaani wanastahili kutambuliwa kwa hakishiriki. Kujenga ari ya ubunifu kwa kuwafaidisha wabunifu kwa kazi zao Kusambaza kazi za ubunifu kwa watumiaji wengine Kufidia jasho na kazi za mbunifu-asiyefanya kazi na asile Kujenga utamaduni na jamii bunifu Kutekeleza mikataba ya kimataifa kuhusu ulinzi wa milikibunifu. Haki za kiuchumi na haki za haki za kiutamaduni/hadhi Haki za kiuchumi ni zile zinazomnufaisha mmiliki kiuchumi moja kwa moja –mfano ukiuza kazi, ukiikodisha, ukiiazimisha kwa malipo, ukimpa haki mwingine aitumie kwa malipo, kuionyesha katika umma, kuisambaza, kuitangza katika vyombo vya habari nk. Haki za kiutamaduni/hadhi hulinda hadhi na taswira ya mtunzi isichafuliwe machoni kwa jamii- mfano inazuia kuchana kazi ya mtu, kutumia kazi kwa kudhalilisha mtunzi nk. Mifano ni mingi: vitabu, muziki, filamu, sanaa, uchoraji, uchongaji, ramani, picha za sinema, mihadhara, hotuba, michoro, ramani za nyumba, mahubiri picha na katika nchi nyingine program za komputa. Kazi inalindwa kama mtunzi/mwandishi mtanzania, mkazi wa Tanzania au kama kazi imechapishwa kwa mara ya kwanza Tanzania. Kazi lazima liwe wazo halisi la mbunifu/mwandishi au mtunzi (original work of authorship) Sheria inalinda mawazo yaliyodadavuliwa (expressed) na siyo wazo tu (idea). Hakimiliki hulindwa kwa muda wa maisha yote ya mbunifu/mwandishi kujumlisha miaka hamusini baada ya kufariki. Kama ni kazi imebuniwa pamoja –ni baada miaka 50 ya maisha ya mbunifu wa mwisho kuishi. Kazi za video/muono-miaka 50 baada ya kutungwa au kutangazwa kwa umma-hii inahusu pia kazi amabayo mtunzi hajulikani. Mmiliki wa kwanza ni mbunifu/mwandishi (aliyeibuni kazi husika), Anaweza asiwe mmiliki kama ameuza kazi yake au alikodiwa/alilipwa kuibuni kazi hiyo kwa niaba ya mtu mwingine, Mbunifu hatakuwa mmiliki kama kazi hiyo ameifanya kama mwajiriwa kwa niaba ya mwajiri. Kazi inaweza hama umiliki kwenda kwa mwingine kwa njia ya leseni/kibali. Kama mmiliki una haki ya kipekee kuuza, kusambaza, kudurufu, kuzalisha nakala, kukodisha, kuionyesha/kuicheza sehemu za umma, kutafsiri, kuionyesha katika vyombo vya habari, kuitumia hadharani nk. Mtu mwingine yoyote amezuiliwa kufanya hayo bila kupata kibali cha mmiliki na mara nyingi kibali hutolewa baada ya malipo kwa mmiliki. Kuitumia bila kibali ukiwa si mmiliki ni kuvunja sheria na kuna adhabu zake. Kazi za uandishi na sanaa za kimila zimelindwa kisheria(folklore) Ni pamoja na nyimbo za kimila,vitendawili, misemo, methali, michoro, ufinyanzi, vinyago, mapambo ya mavazi, vifaa vya muziki vya kijadi nk. Sheria inamtaka yoyote anayetaka kutumia kazi hizi za kimila/kitamaduni kupata kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (National Arts Council) baada ya malipo yatakayotumika kukuza utamaduni. Ulinzi wa hakimiliki hauhitaji usajiri japo usajiri una faida nyingi. Chama kinachosajiri kazi zenye hakimiliki Tanzania bara kinaitwa The Copyright Society of Tanzania (COSOTA), kwa visiwani COSOZA Inashauriwa kusajiri kazi zenye hakimiliki kwa sababu usajiri una faida nyingi. Kurahishisha kuthibitisha umiliki wa hakimiliki ukitokea mgogoro Kurahisisha mtu yoyote kujua kazi yako ina hakimiliki na mmiliki Kukuwezesha kulipwa mirahaba kwa matumizi ya kazi zenye hakimiliki ndani na nje ya nchi Jaza fomu ya maombi COSOTA Kazi itachunguzwa kuona kama hakuna iliyosajiriwa inayofanana Ambatanisha nakala mbili za kazi husika, picha mbili za passport, vitambulisho Nakala ya mkataba au nyaraka nyigine kuthibitisha kazi ni yako au unaimiliki na wengine. Kwa badhi ya kazi viambatanisho zaidi vinaweza kuhitajika mfn kazi ya kwaya orodha ya wanakwaya wote. Kibali cha kumkodisha kazi yako mtu mmoja tu(ecxlusive licence) ni kama umeuza haki zako lazima ulipwe vizuri Kibali cha kukodisha wengi (no exclusive) kinakuacha huru kukodisha yoyote atakaye kuitumia kazi yako Mkataba wa Berne(WIPO) 1886 Mkataba wa TRIPS (WIPO) Mikataba hii inawezesha mmiliki wa hakimiliki mtanzania kulindwa katika nchi yoyote ambayo imeridhia mikataba hii Pia inaipa wajibu Tanzania kulinda kazi za wageni ambao nchi zao ni washirika katika mikataba hii. Haki za kiuchumi na za kihadhi tulizoziona hapo juu zikitumiwa na mtu mwingine bila ridhaa au kibali cha mmiliki basi ni ukiukwaji/ uvunjaji wa sheria. Mfano ni kunakili kazi ya mtu na kuiuza kama yako, au kuicheza sehemu za hadhara Unaweza kuthibitisha ukiukwaji kwa kulinganisha kazi mbili, iliyoibwa na inayotuhumiwa km kazi ya wizi. Ukiukwaji ni makosa ya jinai au ya madai Faini isiyozidi milioni 5 au kifungo kisichozidi miaka 3 au vyote kwa kosa la kwanza na km ukiukwaji ni wa kibiashara Faini isiyozidi milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka 5 au vyote kwa kosa la pili na kwa kiwango cha kibiashara Adhabu ya faini bila kifungo ni ndogo na mkiukwaji anaweza asijutie kutenda kosa Mdai anaweza kuomba amri ya zuio kuzuia uvunjifu kuendelea, kuharibu vifaa vinavyohusika na uhalifu, kuvikamata na kuvishikilia, nakala za kihalifu kuletwa kwa mdai, akadai fidia Matumizi ya kazi yanye hakimiliki kwa kazi zifuatazo hayatachukuliwa km ukiukwaji: -Kufundishia, utafiti, nukuu katika kuchapisha makala -Kuhabarisha -Kidini -Kwa matumizi ya maktaba Cha kuzingatia kusiwe na faida ya kibiashara Kuweka adhabu kali Kutambua hakimiliki kikatiba Kutambua hakimiliki kama mali nyingine Kuvipa meno na kuviwezesha vyama vya wamiliki wa hakimiliki kama COSOTA Kutekeleza sheria bila woga au kupuuza Kuruhusu vyama mbadala wa COSOTA kusajiriwa kuleta ushindani Kuelimisha wasanii na waandishi kuhusu haki zao Kufundisha somo la hakimiliki kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo vyote Msaada wa kisheria kwa wasanii/waandishi wasioweza kulipa gharama za wakili Wasanii/waandishi kutambua umuhimu wa wanasheria Vyama vya kutoa elimu kutambuliwa na kuwezeshwa. Asanteni kunisikiliza.
Hotuba Ya Mwenyekiti Wa Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba, Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, Akiwasilisha Rasimu Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Katika Bunge Maalum La Katiba, Machi 2014