You are on page 1of 69

MASWALI

NA
MAJIBU
Sheria za Tanzania

Toleo la 2

FAyaz A. Bhojani (Wakili)


BCom (McGill), LLB (London), LLM (Berkeley)

Gaudiosus Ishengoma (Wakili)


LLB (UDSM)

Toleo la 2 liliandaliwa na kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza (Questions and Answers on


Tanzanian Law) mnamo mwaka 2019. Chapisho hili la Kiswahili linatokana na tafsiri ya Toleo
hilo la Kiingereza iliyofanywa na Bw. Jaba Tumaini Shadrack (UDSM), na kuhaririwa na Dk.
Laurean Mussa (UDSM) akisaidiana na Bw. Rwekamwa Andrea Rweikiza (Wakili, FB Attorneys).

Dar es Salaam • Tanzania


Hairuhusiwi kunakili, kuhifadhi, kuchapisha kwa njia ya kielektroniki au mekaniki, kutoa vivuli
(kudurufu), kurekodi au kubadili sehemu yeyote ya kitabu hiki kwa njia, namna au mfumo
wowote bila idhini ya maandishi kutoka FB Attorneys. Maswali yoyote juu ya kitabu hiki
yatumwe FB Attorneys kwenye barua pepe: info@fbattorneys.co.tz

Angalizo: Maelezo yaliyomo katika kitabu hiki yanalenga kutoa mtazamo wa jumla wa kisheria.
Sio mbadala wa mshauri wako wa masuala ya kisheria. Ikiwa una changamoto za kisheria,
tunakusihi sana uwasiliane na mwanasheria wako. Tafadhali kumbuka na zingatia kuwa,
sheria ambazo ndio msingi wa majibu na hoja zetu hapa zinaweza kuwa zimebadilika kitambo.

Toleo la 2.
Kimechapishwa na Kusanifiwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ISBN 978-9976-5241-2-3
i

Kwa mama yangu Zainul, na baba yangu Amir.


FAyaz A. Bhojani

Kwa binti yangu Highness Ikamikile.


Gaudiosus Ishengoma
iii

Dibaji
Karibu kwenye toleo la pili la ‘Maswali & Majibu na FB Attorneys’ (Maswali na Majibu Kuhusu
Sheria za Tanzania).

Safu ya Maswali & Majibu na FB Attorneys ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009
katika gazeti la Daily News, na kuifanya kuwa safu ya kwanza ya maswali na majibu ya
kisheria katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kutokana na kupokelewa vyema na mrejesho
chanya wa Toleo la 1, FB Attorneys tumeamua kuandaa Toleo la 2, ambalo linajumuisha maswali
na majibu kutoka mwaka 2012 hadi 2014 juu ya Sheria za Tanzania na kimataifa. Kitabu hiki ni
mwongozo muhimu kwa wasomaji wa kawaida, wanafunzi, walimu, wanasheria na umma kwa
ujumla. Toleo la pili lina Sura 14 na linajumuisha mada za ziada kama vile Migogoro ya Biashara,
Sheria ya Uhamiaji, Mali isiyohamishika, Sheria ya Madini, Uhalifu wa Kibiashara, Sheria ya
Mazingira, Sheria ya Ushuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Kitabu kina lengo la kuwafikia wasomaji kutoka kila nyanja ya maisha na kuelimisha umma juu
ya sheria na madhara ya kuvunja sheria. Sheria inaweza kuchanganya, kukatisha tamaa na wakati
mwingine inaweza hata isiwe upande wako, lakini utaratibu ni kwamba inapaswa kufuatwa.
Kitabu hiki kitakuelimisha juu ya sheria, haki zako na mambo yote unayopaswa kufanya au
kutokufanya. Pamoja na kujibu maswali mazito juu ya sheria, kitabu hiki kina ucheshi ndani
yake na hivyo kufanya safu/makala hizi zinazochapishwa kila wiki kuwa ni somo zuri la Jumatatu
asubuhi huku ukiwa na kikombe cha kahawa pembeni.

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Daily News, gazeti la Kiingereza linaloongoza
nchini Tanzania, ambalo linachapisha safu ya Maswali & Majibu kila Jumatatu
(www.dailynews.co.tz). Kumekuwa na ushirikiano bora kati ya Daily News na FB Attorneys.

Tunatumaini utafurahia kusoma kitabu hiki.


iv

FB Attorneys
FB Attorneys ni kampuni ya kisheria iliyopo jijini Dar es Salaam na yenye uzoefu limbikizi wa
zaidi ya miaka sabini (70) katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tunashughulikia masuala yote
ya kisheria na tumebobea zaidi katika Mambo ya Mashirika na Biashara ikiwa ni pamoja na
Madini, Mafuta na Gesi, Kodi, Kesi za Madai, Mabenki, Ushindani, Mali zisizohamishika, Sheria ya
Haki Miliki na Sheria ya Ardhi, miongoni mwa mambo mengine mengi.

Tunaheshimiwa sana kwenye ukanda wetu na kimataifa. Sifa yetu imejengwa na umahiri wetu
katika kushughulikia kwa mafanikio changamoto ngumu za kibiashara ambazo zinahitaji
mbinu na ufanisi wa hali ya juu. Hutegemewa mara nyingi na wateja kama chaguo namba moja
miongoni mwa makampuni ya kisheria katika kesi za madai, FB Attorneys hutoa ushauri wa
kisheria wa kipekee katika masuala mbalimbali ya makampuni na ya kibiashara.

FB Attorneys tuna mahusiano ya muda mrefu na baadhi ya taasisi mashuhuri za kifedha,


mashirika ya Serikali, asasi za kiraia, na sekta nyingine maarufu za umma na binafsi katika ukanda
wa Afrika Mashariki.

FB Attorneys wanajivunia kuwa mwanachama wa LEX Africa ambao ni ushirika wa kampuni


kubwa za kisheria barani Afrika ambazo zimekuwa zikitoa huduma bora kwa zaidi ya miaka
20. Ushirika huu ulianzishwa mnamo mwaka 1993 na kuwa ushirika wa kwanza wa kisheria
unaolenga Afrika tu.
v

Kuhusu Waandishi
FAyaz A. Bhojani, Wakili.
BCom (McGill), LLB (London), LLM (Berkeley)
FAyaz Bhojani ni Mbia Mwendeshaji wa kampuni mwenye miaka 20 ya ujuzi katika masuala ya
sheria za kampuni na msimamiaji mwenza wa idara ya kesi. FAyaz ni mhitimu wa Shule maarufu
ya Sheria ya Berkeley, katika Chuo Kikuu cha California, inayoheshimika sana duniani. Katika
Shahada ya kwanza, FAyaz alisomea Sayansi ya Takwimu-Bima chini ya Taasisi ya Wataalam wa
Takwimu-Bima (Society of Actuaries - SOA), na hivyo kumjengea ujuzi thabiti wa hisabati.

Baada ya kuwa mshauri katika baadhi ya makampuni makubwa ya kimataifa, FAyaz hutumia
uzoefu huo wa kibiashara katika shughuli zake za kisheria na ameshiriki na kufanikisha
majadiliano mbalimbali ya mikataba mikubwa ya kibiashara katika sekta ya uchimbaji (madini,
mafuta na gesi). Utaalamu wake unajumuisha sekta muhimu za uchumi kama vile huduma za
kifedha, mawasiliano, nishati, madini, kodi, ushindani wa kibiashara, na Uunganishaji na Ununuzi
Mashirika. Anafahamika kwa uwezo wake wa kutatua masuala magumu/tata ya kibiashara na
migogoro ambayo inahitaji umakini mkubwa. Ni mbia ambaye anasimamia na kushiriki katika
majadiliano na kuandaa nyaraka za wateja, na mara zote huorodheshwa na Chamber & Partners,
IFLR 1000 na Legal 500 miongoni mwa wanasheria nguli na mahiri nchini Tanzania.
Gaudiosus Ishengoma, Wakili.
LLB (UDSM)
Baada ya kufanya kazi kama Mwanasheria wa Serikali kwa miaka minane, Ishengoma anaongoza
Idara ya Mashtaka Mahakamani na ana uzoefu mkubwa katika kusimamia migogoro nyeti na
masuala yote ya usuluhishi. Katika kazi zake za kisheria kwa muda wa miaka ishirini na sita (26),
amesimamia kesi ngumu na sehemu kubwa ya migogoro mbalimbali ya kibiashara katika nyanja
kama vile ardhi, sekta ya uchimbaji (madini, mafuta na gesi), fedha/mabenki, mawasiliano,
ushindani wa kibiashara na mikataba.

Amehusika katika kesi kubwa zilizofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania (Kitengo cha Ardhi
na Kitengo cha Biashara), na Mahakama ya Rufaa na kuwa na rekodi nzuri katika ufuatiliaji wa
madeni ya benki. Ishengoma alifundishwa mbinu za uendeshaji mashtaka na Baraza la Uingereza
(British Council) chini ya timu ya wataalamu kutoka Bunge la Mabwanyenye (House of Lords)
na ana uzoefu mkubwa kuhusu masuala ya ushindani wa kibiashara, migogoro ya wanahisa/
wabia, rufaa za kodi pia jinai ya kampuni (uhalifu wa kibiashara). Ameorodheshwa na Chamber
& Partners, IFLR 1000 na Legal 500 miongoni mwa wanasheria nguli na mahiri nchini Tanzania.
Yaliyomo
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali ...................................................................................1

Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka ................................................................................................15

Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki.........................................................................39

Haki za Walaji..................................................................................................................................................................59

Sheria za Makampuni na Kibenki, Migogoro ya Wanahisa/Wabia...........................................................89

Sheria za Madini, Biashara na Uwekezaji wa Kimataifa ............................................................................. 105

Migogoro baina ya Watu Binafsi ........................................................................................................................ 117

Sheria za Ajira na Uhamiaji.................................................................................................................................... 125

Sheria za Mazingira na Urithi wa Mali za Kale ............................................................................................... 149

Wanasheria, Tafsiri ya Sheria na Taratibu za Kimahakama ...................................................................... 157

Utakatishaji Fedha na Jinai ya Kampuni ......................................................................................................... 185

Hati ya Uwakilishi, Kifo, Mirathi na Wosia ...................................................................................................... 197

Sheria za Majengo, Ardhi na Mipango Miji .................................................................................................... 203

Sheria ya Kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ............................................................................ 211


Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 1

Migogoro ya Kibiashara
dhidi ya Viongozi wa
Serikali

Kila siku, na nchini kote, wafanyabiashara huwa na muingiliano na maafisa wengi wa serikali.
Ingawa muingiliano huo mara nyingi huwa ni wenye tija na kiungwana, siyo mara zote huwa
hivyo. Wakati mwingine maafisa wa serikali hutumia madaraka yao vibaya na hivyo kukiuka
sheria. Hakika, siyo maafisa wa serikali pekee, hata Mawaziri huweza kuvunja sheria.

Katika sura hii, tunatoa mifano kadhaa inayoonesha namna ambavyo maafisa wa serikali
wanapitiliza na kuvunja sheria, na namna ambayo wafanyabiashara wanaweza kudai haki zao.
Vilevile tunatoa mifano mahususi kuhusiana na idara ya uhamiaji ambapo maafisa wa serikali
wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ingawa hatua hizo huwa ni kero kwa
wafanyabiashara.

Sura hii pia inajumuisha mifano ya wahalifu wanaojifanya ni maafisa wa serikali au hata polisi
(vishoka/matapeli) ili kupata taarifa na kuingia mahala pa biashara. Tunawashauri wenye
kampuni kuchukua tahadhari na kuwakabili “maafisa” wanaowatilia mashaka.
2 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Mamlaka ya maafisa uhamiaji wako, inaonesha unalalamikia sana namna


ambavyo walikushtukiza na walivyowafanyia
Mimi ni mfanyabiashara Jijini Dar es Salaam wafanyakazi wako. Unaweza kutoa taarifa kwa
ambaye nina wafanyakazi wa ndani na Mkurugenzi wa Uhamiaji kuhusu kuvunjiwa
nje ya nchi. Kuna tukio lilitokea ambalo
heshima na yeye anaweza kulifanyia
liliathiri sana hadhi yangu na biashara kwa
uchunguzi tukio hilo.
ujumla. Maafisa Uhamiaji walivamia ofisi
Sehemu ya mwisho ya swali lako ni kuhusu
yangu mchana kweupe, wakaigeuza ofisi
mamlaka ya jumla ya maafisa uhamiaji.
yangu juu chini, wakatuweka chini ya ulinzi,
Kwa ajili hiyo, Tunanakili baadhi ya vifungu
wakiwemo wateja wangu, huku wakizuia
mtu yeyote kuingia wala kutoka. Hawakuwa muhimu vya sheria kwa ajili ya rejea yako.
na hati za upekuzi wala hawakutoa taarifa. Sheria inatamka kwamba afisa uhamiaji
Walinivamia kama wao ndiyo wamiliki wa yeyote anaweza (a) kumhoji au kukagua
ofisi na wakaondoka na nyaraka za siri. pasipoti ya mtu yeyote anayetaka kuingia
Wana mamlaka ya kufanya hivyo? Mamlaka au kuondoka nchini Tanzania au mtu yeyote
ya Maafisa Uhamiaji ni yapi? ambaye ataona ana sababu za msingi za
23 Januari 2012 kuamini kuwa ni mhamiaji haramu, na pale
anapokuwa na sababu za msingi za kuamini
Sheria za uhamiaji Tanzania zinaeleza kazi kwamba vifungu vya sheria hii au kanuni
na mamlaka ya maafisa uhamiaji kwa ujumla. zilizotungwa chini ya sheria hii zinavunjwa,
Sheria ya Uhamiaji inasema maafisa uhamiaji anaweza kumhoji au kukagua pasipoti ya
wana mamlaka ya kuingia jengo lolote kwa mtu yeyote ambaye anaamini kwamba
muda unaofaa na kukagua jengo hilo bila anaweza kutoa maelezo kuhusu uvunjifu
kuwa na hati ya upekuzi. Wana mamlaka ya huo; (b) kumtaka mtu yeyote aliyeingia au
kuchukua nyaraka zinazohusiana na masuala anayetaka kuingia au kuondoka Tanzania
ya uhamiaji ikiwemo kuzidai kutoka kwa mtu kujaza au kusaini fomu yoyote ya kukubali
ambaye wanaemuona ni mhamiaji, na ndiyo kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu; (c)
maana inashauriwa wale wenye vibali vya kazi kumtaka muongoza meli, rubani, dereva
wabebe vibali vyao vilivyothibitishwa. wa gari moshi au gari anayeingia au kutoka
Maafisa Uhamiaji pia wana mamlaka nje ya Tanzania kutoa nakala mbili za majina
ya kumkamata mtu ambaye hana nyaraka zilizosainiwa naye, wakala wake au mtu
zinazompa uhalali wa kukaa Tanzania. Na yeyote aliyeruhusiwa kufanya hivyo kwa
kama wakimkamata wanatakiwa wampeleke niaba yake majina ya watu wote wa kwenye
kwa hakimu aliyepo kwenye Mahakama meli, ndege, gari moshi au gari na kumpatia
yoyote iliyo karibu haraka iwezekanavyo. Hata maelezo yoyote ya ziada kama yatahitajika (d)
hivyo, kisheria hawatakiwi kutumia nguvu kama ana sababu za msingi kuhisi kwamba
kubwa kufanikisha hilo. Labda kama kuna mtu mtu yeyote anakiuka vifungu vya sheria
ameumizwa kutokana na matumizi ya nguvu hii au kanuni zake au uwepo wa mhamiaji
iliyopitiliza au amekamatwa bila kufikishwa haramu nchini Tanzania na kama anaona ili
Mahakamani haraka iwezekanavyo, au kuhakikisha haki inatendeka ni lazima mtu
walikuja muda usio muafaka, vinginevyo huyo akamatwe anaweza kumkamata mtu
sheria inawaruhusu kufanya hivyo huyo bila hati ya ukamataji na kumpeleka
walivyofanya walipokuja ofisini kwako. kwa hakimu haraka iwezekanavyo (e)
Yote kwa yote, ni lazima watende kwa kumtaka mtu kutoa uthibitisho au ushahidi
kuzingatia utu wa kila mtu. Kwa upande wa maandishi au wa mdomo ambao anaona
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 3

ni muhimu ili kuthibitisha maelezo yoyote ya Mahakamani. Nifanye nini?


maandishi au mdomo yaliyotolewa kwa ajili 6 Februari 2012
ya kuomba kibali, pasi ya kusafiria au ruhusa
nyingine ambazo zinatolewa chini ya vifungu Ingawa ushuru wa taka unaonekana kama
vya sheria hii (f) kuingia kwenye jengo lolote siyo jambo kubwa, kutokulipa ushuru huo ni
kwa muda unaofaa na kufanya upekuzi kosa la jinai. Viwango vya malipo ya ushuru
wa jambo linalohusiana na uhamiaji na (g) wa kukusanya taka vimeainishwa kwenye
kumtaka mtu yeyote kumpatia waraka ambao Sheria Ndogo za Makusanyo na Utupaji
mtu huyo amebeba. Taka za mwaka 1994 ambapo Nyongeza “C”
Kwa ajili ya kutekeleza kazi zilizoainishwa inahusu swali lako.
kwenye sheria hii, afisa uhamiaji anaweza, Chini ya sheri hizo, viwango vya malipo
bila kuwa na hati ya upekuzi, kusimamisha, vimeainishwa kulingana na idadi ya waajiriwa
kuingia na kukagua ndani ya ndege, treni, ulionao. Kwa mfano, biashara yenye waajiriwa
kati ya 76 hadi 100 inatakiwa kulipa Shilingi
gari, chombo, meli, jengo, ardhi, ghala,
150,000; hiyo Shilingi 7,500 ni kwa biashara
kontena, boti yoyote iliyopo nchini.
yenye waajiriwa 6 hadi 10. Tunaamini una
Kwa maelezo hayo, unaweza kuona kuwa
utetezi mzuri, kama idadi ya wafanyakazi
mamlaka ya maafisa uhamiaji ni makubwa.
wako haijaongezeka.
Hata hivyo, ni kawaida kwao kutumia vibaya
Katika hatua nyingine, kama tahadhari
mamlaka hayo. Kwa mfano, wanaweza tu
tu, unashauriwa kwenda Mahakamani na
kuchukua nyaraka zinazohusiana na uhamiaji
watu wawili ambao wanaweza kukuwekea
na siyo vinginevyo.
dhamana kama itahitajika.
Ni lazima uelewe kwamba Idara ya Uhamiaji
ina kazi kubwa ya kuweka mlinganyo/usawa Mhariri wa gazeti ameshtakiwa kwa
ili kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata uchochezi
ajira zisizohitaji ubobevu na wataalamu
kutoka nje. Nchi zote zina sera za namna hiyo Ninafanya kazi kama Mhariri Msaidizi
ili kulinda ajira za watu wake. Lakini pia kuna kwenye mojawapo ya magazeti
makampuni ambayo hayafuati sheria ambapo Tanzania. Kutokana na uhariri fulani
ambao uliichefua Serikali nimeshtakiwa
husababisha makampuni ambayo yanafuata
kwa uchochezi Mahakamani. Ni kweli
sheria kuvamiwa. Hata hivyo, tunakiri kuwa
niliandika chapisho/makala husika lakini
baadhi ya makampuni hayafanyi kazi kwa
ninaamini nilichoandika na sielewi kwa
kufuata sheria.
nini nikamatwe kwa kutoa maoni yangu.
Mahakamani kwa kushindwa kulipa Kwani wahariri si hawabanwi na kanuni
ushuru wa taka ya kuzingatia ‘ulali/ulinganifu wa habari’
kwa kuwa nilikuwa tu natoa maoni yangu.
Ofisi yangu ipo katikati ya jiji la Dar Nifanye nini?
es Salaam ambapo kwa miaka mingi 2 Aprili 2012
nimekuwa nikilipa Shilingi 7,500 kwa
mwezi kama ushuru wa kukusanya taka. Umeshtakiwa kwa mujibu wa Kanuni ya
Miezi michache iliyopita wazoa taka Adhabu, ambayo ni sheria ya jinai Tanzania.
walinidai Shilingi 150,000. Nilikataa kulipa Kifungu cha 55 (1) cha Kanuni ya Adhabu
kiasi kilichoongezeka na wao walikataa kinaelezea nia ya kufanya uchochezi kuwa
kuchukua kiasi nilichokuwa nalipa awali. ni nia ya (a) kuleta chuki au kudharau au
Kwa sasa nimeletewa wito wa kwenda kuchochea hali ya kutopendwa kwa mamlaka
4 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

halali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali unaweza kuandikwa tu vyovyote. Si hivyo.


yake; au (b) kuhamasisha wakazi wowote Maoni ya mhariri yanaweza kuwa ni ya
wa Jamhuri ya Muungano ili kuleta mageuzi, uchochezi. Ni kweli Katiba inakupa uhuru
kwa njia isiyo halali, juu ya jambo lolote wa kujieleza, lakini uhuru huo ni lazima uwe
lililowekwa na sheria katika Jamhuri ya ndani ya mipaka. Mwanasheria wako anaweza
Muungano; au (c) kuleta chuki au kudharau kukuongoza zaidi.
au hamasa ovu ya kuwafanya watu watende
kinyume na utawala wa sheria katika Jamhuri Taarifa katika tovuti za Serikali
ya Muungano; au (d) kupandisha hali ya
zimepitwa na wakati
kutoridhika au kudharau baina ya wakazi wa Mimi ni mshauri kutoka nje, nimegundua
Jamhuri ya Muungano; au (e) kukuza hisia za kuwa mara nyingi tarrifa zilizo katika tovuti
nia mbaya na chuki baina ya aina mbali mbali za idara za Serikali, wizara na pia bunge ama
za watu wa Jamhuri ya Muungano. hazijasahihishwa ama zina taarifa ambazo
Kifungu kidogo cha (2) cha Kanuni ya ni za zamani sana, hazihusiani na uhalisia
Adhabu kinaeleza kwamba kitendo, hotuba na siyo sahihi. Nikupe mfano wa tovuti moja
au tangazo halitahesabiwa kuwa ni la ambayo bado inasema Rais ni Benjamin
kichochezi kwa sababu tu linalenga katika Mkapa. Tovuti za Serikali bado zina majina
(a) kuonesha kwamba Serikali imepotoka au ya wizara za zamani. Mbaya zaidi baadhi ya
imekosea katika mwenendo wake wowote; au tovuti bado zina sheria za zamani na zingine
(b) kuonyesha makosa au mapungufu katika hata hazifunguki. Je, hakuna sheria ya
Serikali au Katiba ya Jamhuri ya Muungano tovuti ambayo inaharamisha kuweka taarifa
au kama ilivyowekwa na sheria, au katika za zamani? Huu ni mwaka 2012, uzembe wa
namna hiyo unapaswa kupingwa kwa kuwa
usimamiaji utoaji wa haki kwa lengo la
kuhudumia tovuti hakuhitaji bajeti kubwa
kurekebisha makosa hayo au upungufu huo;
zaidi ya nia tu. Je, suala hili linawezaje
au (c) kuwashawishi wakati wowote wakazi
kutatuliwa? Je, kama nilitumia taarifa za
wa Jamhuri ya Muungano kujaribu kwa njia
kwenye mojawapo ya tofauti hizi, ninaweza
ya halali kuleta mageuzi/mabadiliko ya jambo kuishtaki idara husika?
lolote katika Jamhuri ya Muungano kama
9 Julai 2012
ilivyowekwa na sheria; au (d) kuonyesha, kwa
nia ya kuyaondoa, mambo yoyote yanayoleta Kwa bahati mbaya hatujui sheria yoyote
au yenye mwelekeo wa kujenga hisia za nia inayoweka kosa kama hilo. Hata hivyo, kanuni
mbaya na uadui baina ya aina mbalimbali za utawala bora na hekima vinazilazimu
za watu wa Jamhuri ya Muungano. Kifungu idara, wizara, au wakala za serikali kuhuisha
kidogo cha (3) kinasema katika kuamua tovuti zao angalau kila siku au kila wiki.
endapo nia ya kitendo chochote kilifanywa Kwa kuwa unaonekana kufahamu idadi ya
au inayohusishwa na kitendo ilikuwa ya, tovuti hizo, ni vyema ukaziandikia kuwaeleza
maneno yoyote yatakayozungumzwa au kuhusu upungufu huu.
nyaraka yoyote itakayoandikwa itahesabiwa Upande wa pili wa swali lako hatuwezi
kuwa ni ya uchochezi, na mtu yeyote kulijibu bila kwanza kujua ulizitegemeaje
atahesabiwa kuwa alinuia matokeo ambayo taarifa hizo na vyanzo gani vingine ulikuwa
kwa hali ya kawaida yanatokana na kitendo navyo kabla ya kuzitegemea taarifa hizo.
chake kwa wakati na katika hali aliyoitenda Hata hivyo, kwa kawaida dai lako haliwezi
mwenyewe. kufanikiwa ikiwa ulikuwa na uelewa
Una imani isiyo sahihi kuwa uhariri kama ulivyoonesha kwamba tovuti hizo
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 5

hazijasahihishwa. Kama hivyo ndivyo, Hivi sasa, zabuni zinasimamiwa na Sheria


hatuamini kama unaweza kufanikiwa. ya Manunuzi ya Umma ya 2004 ambayo
Wanasheria wako wanaweza kukuongoza pia ina kanuni zake. Taarifa muhimu sana
baada ya kuwaeleza kila kitu. kwako ni kwamba bei siyo kigezo pekee
kinachoamua bali mambo mengine pia
Mfamasia mmoja sehemu mbili za kazi huzingatiwa.
Mimi ni Mfamasia ninayeendesha maduka Sheria ya Manunuzi ya Umma inaanzisha
mawili ya dawa ambapo nimeweka sifa nadharia ya “bei ya makadirio ya chini”
zangu. Nina wasaidizi sehemu zote mbili ambayo ina maana ya bei inayotolewa
lakini muda mwingi nautumia kwenye na muuzaji, mjenzi au mshauri ambayo
duka kubwa. Wakaguzi walikuja kwenye itaonekana kuwa ni ya chini zaidi baada ya
duka dogo na hawakunikuta. Kwa sasa kuzingatia mambo mengine yote husika na
nimeshtakiwa na kamati ya nidhamu kwa baada ya mahesabu mengine kwa kuzingatia
utovu wa maadili ya kazi kwa kumruhusu mambo hayo, isipokuwa kwamba mambo
mtu asiye na sifa kutoa huduma kinyume hayo ni lazima yawe yameelezwa kwenye
na Sheria ya Famasia. Je, nimevunja sheria? nyaraka za zabuni.
Niendeshaje biashara yangu? Baadhi ya zabuni zina gharama za ufundi
17 Septemba 2012 na gharama za kifedha ambapo asilimia fulani
inatolewa kwenye maeneo yote mawili na
Swali lako linaashiria jibu. Kama Mfamasia wastani wake unaunda bei ya makadirio ya
unaelewa wazi kwamba huwezi kuonesha chini. Kama haujaridhika na kutokuchaguliwa,
vyeti vyako kwenye duka moja la dawa na una haki ya kukata rufaa kwenda kwenye
kufanya kazi kwenye duka jingine. Ni kweli taasisi ya manunuzi na baadaye kwenye
kwamba hii ndiyo hali halisi mitaani kwa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni ambayo
sasa lakini tumearifiwa kwamba tabia hii hivi karibuni imebatilisha zabuni nyingi
inashughulikiwa. Mfamasia ni mtaalam ambazo zimefanyika bila kufuata taratibu.
anayetoa dawa za matibabu. Matibabu yasiyo Mwanasheria wako anaweza kuangalia njia hii
sahihi yanaweza kupelekea kifo. Unatakiwa na kukuongoza zaidi.
kuzingatia kazi yako kwa umakini mkubwa
Sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na
na utii Sheria ya Famasia ambayo inakutaka
sekta binafsi
ufanye kazi sehemu moja tu unayoweka cheti
chako cha usajili. Tunakushauri uache kufanya Nimesikia kuhusu Sheria ya Ubia kati ya
kazi sehemu mbili na uheshimu sheria. Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na kwamba
makampuni binafsi yatakuwa yanawatoza
Zabuni ya chini na bado si mshindi wananchi fedha kwa matumizi ya miundo
mbinu ya umma ikiwemo barabara.
Niliingia kwenye mchakato wa zabuni
Inawezekanaje Serikali kuuza barabara
kubwa ya ujenzi wa barabara. Uzabuni
zetu? Tafadhali nieleze kama nimeelewa
wangu ulikuwa ni wa chini na bado
vibaya.
sikupewa kazi. Baada ya kufuatilia
24 Desemba 2012
niliambiwa kwamba wenzangu walikuwa
na uzabuni bora zaidi. Je, sikustahili kupewa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na
kazi? Sekta Binafsi itaisaidia Serikali na sekta binafsi
17 Desemba 2012 kufanya kazi kwa pamoja kwa faida ya jamii
6 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

nzima. Serikali ya Tanzania inakusudia kufanya atawajibika kwa faini isiyopungua milioni
vitu vingi sana kwa ajili ya kuiendeleza nchi, moja au kifungo kisichozidi miezi sita au
yaani kujenga barabara, hospitali, vyuo n.k. vyote kwa pamoja.
Hata hivyo, siyo siri kwamba Serikali haina Sheria ya Utalii pia imeweka sifa ambazo
pesa za kutosha kugharamia miradi hiyo ni lazima mtu awe nazo ili aweze kusajiliwa
mingi kwa haraka. Sheria hii inakusudia kama muongoza watalii. Sifa hizo ni pamoja
kuzishirikisha sekta binafsi na makampuni na umri angalau miaka 21, elimu ya angalau
yenye uwezo wa kifedha kujenga miundo kidato cha nne, uwe na cheti cha huduma ya
mbinu hiyo na kurejesha faida pamoja na kwanza, ujuzi wa kutosha wa eneo husika na
gharama zao za ujenzi kwa kipindi fulani uelewa wa kutosha wa kazi yenyewe pamoja
na baadaye miundo mbinu hiyo inarudi na na kuwa na sifa nyingine ambazo waziri wa
kuwa mali ya Serikali. Ni kweli itahusisha utalii atazibainisha kwenye Gazeti la Serikali.
wanachi kulipa kiasi fulani cha pesa kwa ajili Kwa kuwa kaka yako anafanya kazi
ya matumizi ya miundo mbinu hiyo lakini ya kuongoza watalii kwa kukiuka sheria,
ni kwa maendeleo ya nchi. Sheria kama hizi kukamatwa kwake kulikuwa ni halali. Suala
zipo kwenye nchi nyingi ambapo sekta binafsi kwamba kujuana kwenu na mkubwa fulani
imekuwa mstari wa mbele kwenye miradi kulisaidia kuachiwa kwake kunaweza
hiyo. Umeelewa vibaya Serikali haiuzi nchi bali kusiwasaidie huko mbeleni kama mtaendelea
inafanya kazi ili kuleta maendeleo ya haraka. kufanya kazi ya kuongoza watalii bila
kusajiliwa.
Usajili wa waongoza watalii Mwisho, hata kama tungewaonea huruma
kiasi gani kwamba sheria haijazingatia
Nimekua kwenye kijiji kimoja kilichopo chini
uzoefu wenu wa toka enzi kwenye suala
ya Mlima Kilimanjaro. Tangu enzi na enzi,
la kuongoza watalii, bado tunapendekeza
familia yetu imekuwa ikijipatia kipato kwa
kufuata masharti yaliyowekwa na Sheria ya
shughuli za kuongoza watalii. Kwa kipindi
chote hicho hatujawahi kuingiliwa na mtu Utalii kwa kuwa ni sheria na ni lazima tuifuate.
yeyote na kazi hii tumeirithi kutoka vizazi Vinginevyo, unaweza kushawishi sheria
vingi vilivyopita. Hivi karibuni, kaka yangu ifanyiwe mabadiliko kwa kumwandikia barua
mkubwa alikamatwa kwa kuongoza watalii waziri wa utalii ili mahitaji yako yaingizwe
bila kusajiliwa. Tulifanikisha kuachiwa kwenye marekebisho ya sheria.
kwake kwa sababu tulikuwa tunajuana na
Kukataa kutoa nyaraka za mapato kwa
mkubwa fulani. Ninashangaa kwa nini sheria
afisa kazi
inatulazimisha kujisajili. Tumefanya kazi hii
kwa miaka mingi sasa na wengi wetu hatuna Mimi ni mwanamke mfanyabiashara, kwa
sifa za kufanya kazi nyingine. Je, sababu za sasa nimefungua ofisi zangu hapa jijini
kukamatwa kaka yangu zilikuwa ni sawa? Mwanza. Biashara yangu kuu ni uingizaji
Tafadhali nisaidie. na uuzaji bidhaa kutoka China. Nimeajiri
31 Desemba 2012 Watanzania saba kama wasaidizi wangu.
Hivi karibuni mtu ambaye alijitambulisha
Kwanza kabisa tunataka kukueleza kama afisa kazi alikuja ofisini kwangu na
kwamba kila mwongoza watalii anatakiwa kuomba vitabu na nyaraka mbalimbali.
kusajiliwa kwa mujibu wa maelekezo ya Sheria Alisema alikuja hapo ili kuhakikisha
ya Utalii Na. 29 ya 2008. Mtu anayekiuka kwamba tunafuata sheria za kazi. Nilimpa
sheria hii anatenda kosa na akikutwa na hatia nyaraka alizohitaji lakini nilikataa kumpa
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 7

vitabu vinavyoonesha mapato ya biashara. wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania. Ikiwa


Alisema atanichukulia hatua za kisheria. Je, una jina la afisa kazi, usione aibu kumripoti
sheria inasemaje? kwa Kamishna wa kazi. Wanasheria wako pia
28 Januari 2013 wanaweza kukuongoza zaidi.

Chini ya Sheria ya Taasisi za Kazi, sheria Maafisa wa Serikali wanachelewa


namba 7 ya mwaka 2004, kwa madhumuni wakati wote
ya usimamizi wa sheria za kazi, afisa kazi
Nimekuja Tanzania mara tano katika miaka
anaweza, kwa muda wowote unaofaa kuingia
miwili iliyopita na kila wakati ninapokuja
eneo lolote akiwa na cheti/kitambulisho
kuonana na Katibu Mkuu au Naibu Mawaziri
husika chenye kumhalalisha na kumtaka mtu
tunajikuta tukisubiri kwa saa ili tuonane.
yeyote mwenye udhibiti wa taarifa yoyote, Hawaombi msamaha na inanishangaza kwa
kitabu, hati au kitu, kukitoa na kuelezea nini hawawezi kusimamia muda wao vizuri.
chochote kilichomo kwenye taarifa, kitabu, Upotevu huo wa muda unaipotezea nchi hii
hati au kitu hicho. Mamlaka haya yametolewa mamilioni ya Dola kila siku. Kama ikitokea
chini ya Kifungu cha 45 cha Sheria ya Taasisi ya mara moja au mbili inaweza kueleweka,
Kazi na kimeenda zaidi na kutamka kwamba lakini hili inaonekana kuwa ni hali ya kila
anaweza kukamata, kutoa nakala ya taarifa siku. Hakuna afisa wa umma anaonekana
yoyote, kitabu, nyaraka au kitu chochote kujali muda. Kampuni yetu imetumia
halisia. maelfu ya Dola za ziada juu yangu kwa
Hata hivyo kwa ufafanuzi, sheria ya kuwa mara kwa mara nalazimika kuongeza
Taasisi za Kazi imesisitiza kwamba taarifa muda wa kuendelea kukaa Tanzania. Hivi
yoyote, kitabu au hati, sampuli au kitu karibuni mmoja wetu alitakiwa kwenda
halisia kitatumika tu katika utekelezaji na Dodoma ili kukutana na Waziri fulani kufika
usimamizi wa sheria ya kazi. Ikiwa madai ya kule akaambiwa na naibu wake kuwa usiku
afisa yalikuwa ya vitabu na taarifa ambazo uliopita Waziri alikuwa amesafiri kurudi Dar
hazihusiani na kazi, tunakubaliana kabisa kwa majukumu “ya kiofisi”. Kutupigia simu
tu ingetosha ili tuahirishe safari na hivyo
na wewe kwamba ulikuwa sawa kukataa
kuokoa fedha tulizotumia kwenda Dodoma.
kutoa vitabu vya mapato kwa afisa kazi huyo.
Tafadhali niongoze juu ya nini cha kufanya.
Hatuoni uhusiano wa vitabu vya mapato na
Je, hakuna mwongozo juu ya hili? Jinsi gani
utekelezaji na usimamizi wa sheria za ajira
na ni nani anaweza kulitatua hili?
labda kama haujatuambia ukweli wote.
6 Mei 2013
Hata kama ni kosa chini ya Sheria ya Taasisi
za Kazi kukataa kutoa nyaraka inayotakiwa Idara ya Utumishi wa Umma ina kanuni
na afisa kazi, kifungu cha 49 cha sheria hiyo zinazoitwa, Kanuni za Maadili ya Utendaji
hiyo pia kinatamka kwamba haitakuwa katika Utumishi wa Umma zilizotungwa na
kosa kukataa kujibu swali au kutoa taarifa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
yoyote, kitabu, nyaraka au kitu halisia ikiwa Utumishi wa Umma kwa mamlaka aliyopewa
kuna sababu za kisheria za kutofanya hivyo. na Kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa
Hatuoni uwezekano wowote wa hatua za Umma ya mwaka 2002 na Kanuni ya 65(1)
kisheria kuchukuliwa dhidi yako kwa sababu ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka
una sababu halali za kukataa kutoa vitabu vya 2003.
mapato kwa afisa kazi. Mambo yangekuwa Kanuni hizi zinaeleza kwa uwazi mambo
tofauti kama vitabu vingehitajika na viongozi yafuatayo: kutoa huduma bora, kutumia
8 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

misingi ya haki badala ya upendeleo katika Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania inatamka
utoaji wa huduma, kutimiza wajibu kwa wazi kwamba isipokuwa kwa idhini ya
kufanya kazi kwa ufanisi kwa kiwango cha juu maandishi ya Benki, hakuna benki itasajiliwa
na kuzikamilisha katika muda unaotakiwa, hapa nchini kwa masharti ya sheria yoyote,
isipokuwa kama imeruhusiwa vinginevyo, kwa jina ambalo linajumuisha maneno yoyote
watumishi wa umma wanapaswa kuwa kati ya haya: “Central”, “State”, “Government”
waaminifu na kutumia muda wao wa kazi and “Reserve”. Benki Kuu imefungwa na Sheria
kutekeleza wajibu wao. Hawaruhusiwi hii na hakuna uwezekano wa kuwakubalia
kutumia muda wa kazi kwa shughuli zao kusajili benki yenye jina lililo na neno “Central”
binafsi au kwa mapumziko isipokuwa kama ndani yake. Benki Kuu siyo kali bali inajaribu
wamepewa idhini ya kufanya hivyo. kuhakikisha kwamba, miongoni mwa mambo
Kutokana na maelezo hapo juu, unaweza mengine, hakuna mkanganyiko wa soko
kuona kwamba sheria inawataka maafisa unatokea.
wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa
kiwango fulani na kuzingatia misingi ya haki. Polisi bandia ofisini kwangu
Hivyo kutokujali muda ni kuvunja sheria Sekretari wangu alinitaarifu kwamba kuna
na unaweza ama kupeleka malalamiko polisi wawili wamekuja kunihoji kuhusu
rasmi kwa wakubwa zao ama kwa Waziri tuhuma fulani. Nikiamini kuwa ni polisi
anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi kweli, niliwaruhusu kuingia na wakaanza
wa Umma. kunitishia kuhusu kitu ambacho hata
Tunakubaliana na wewe kwamba sikijui. Hata gari waliyokuja nayo ilikuwa
kutokujali muda au kutokusimamia muda ni na namba ya polisi. Sikujua kwamba watu
tabia mbaya ambayo inafanywa na maafisa. hao walikuwa ni maafisa polisi ambao
Kimsingi, kwenye nchi nyingine kutunza walifukuzwa kazi na sasa wanazunguka
muda kwao ni muhimu na hata uchelewaji wakitapeli watu fedha kwa kujifanya
wa dakika tano tu, mchelewaji hulazimika kama bado wapo kazini. Je kuna sheria ya
kuomba msamaha. Wanasheria wako kuwaadhibu?
wanaweza kukuongoza zaidi. 8 Julai 2013

Benki Kuu ya Tanzania kukataa jina letu Chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa hili
ni kosa kubwa. Kifungu cha 6 cha Sheria hii
Sisi ni benki yenye kusifika kimataifa na
kinatamka kwamba mtu yeyote ambaye,
tumekuwa tukitumia jina letu ambalo pia
kwa malengo ya kuingia au kumsaidia mtu
lina neno “Central” ndani yake. Majadiliano
yetu yasiyo rasmi na Benki Kuu yameonesha mwingine kuingia sehemu inayolindwa au
kwamba Benki hiyo haifurahii matumizi ya kwa malengo mengine yanayohatarisha
neno ‘Central’ kwa sababu wakati mwingine usalama au maslahi ya Jamhuri ya Muungano
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaitwa (a) bila mamlaka halali anatumia au anavaa
“Central Bank”. Hata hivyo jina letu sio Benki sare za majeshi ya ulinzi au jeshi la polisi au
Kuu lakini neno ‘Central’ lipo ndani yake sare nyingine rasmi ya Jamhuri ya Muungano
na ni miongoni mwa maneno mengine. au zinazofanana sana kiasi cha kuonekana
Tunawezaje kuishawishi Benki Kuu? Kwa kupotosha, au anajifanya kuwa ni mtu
nini Benki Kuu inakuwa kali sana kwenye anayestahili kuvaa au kutumia sare hizo; (b)
suala hili? bila kibali halali anatumia gari ya Serikali au la
10 Juni 2013 ofisi yake, au gari yoyote ambayo kwa sababu
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 9

ya namba batili au sababu nyingine, au haki ya kutoa vitisho hivyo isipokuwa kama
anajifanya kuwa ni mtu anayestahili kutumia sheria inayoanzisha wakala huo au sheria
gari hiyo anatenda kosa na akikutwa na hatia nyingine yoyote inampa mamlaka mapana
atawajibika kwa kifungo kisichozidi miaka 20. namna hiyo. Tunatilia mashaka kama Waziri
Nenda katoe taarifa polisi, kama hujafanya ana mamlaka hiyo. Waziri anaweza kuwa
hivyo. ametoa maneno yake, na wewe unatakiwa
kumkumbusha matakwa ya mkataba wa ubia.
Ubia na Wakala wa Serikali Kama bei ya bidhaa unayosema
imeshuka na kupelekea hasara, na kushuka
Tumeingia kwenye ubia na Wakala wa
Serikali, ambao mtendaji wake mkuu huko hakujachangiwa na uzembe wenu,
yupo chini ya Wizara fulani. Ubia wetu upo hatuoni kwa nini kuwe na uvunjifu. Miradi
kwenye changamoto za kifedha kutokana inapoanzishwa, inaanzishwa kwa misingi ya
na kuongezeka kwa wazalishaji wa kigeni dhahania fulani, ambayo inabadilika kadiri
pamoja na kushuka kwa bei ya bidhaa muda unavyokwenda. Kama mkataba wa
tunazozalisha. Makadirio yetu ya faida ubia una kipengele cha usuluhishi na Waziri
hayajafikiwa na Waziri amesema kwamba anatishia kuvunja, tunawashauri mara
anakusudia kuvunja ubia. Tumewekeza moja muuwasilishe mgogoro huu kwenye
mamilioni ya Dola kwenye mradi na usuluhishi. Kama mtahitaji amri ya Mahakama
tumeshtushwa sana na kitisho hicho. Hata wakati usuluhishi unaendelea, mnaweza
mtendaji mkuu wa Wakala ameguswa na kupeleka maombi husika Mahakamani kwa
anasema Waziri ana mamlaka mapana ajili ya kupata nafuu ya zuio, wakati mkisubiri
kisheria ya kutusitishia hata kama kuna matokeo ya usuluhishi.
kipengele kwenye mkataba wa ubia Inaweza kuwa muhimu kumueleza Waziri
kinachotoa njia ya utatuzi wa mgogoro kwa na mshauri wake wa masuala ya sheria
njia ya usuluhishi. Tafadhali tuongoze kama Wizarani kwamba utaratibu wa kisheria ni
kuna sheria hiyo ambayo inampa Waziri lazima ufuatwe na kwamba kuvunja mkataba
mamlaka makubwa namna hiyo. kutakuwa ni kinyume cha sheria. Serikali
29 Julai 2013 imewawajibisha maafisa wengi tu wa ngazi
za juu kwa kushindwa kutekeleza masharti ya
Inakuwa ni vigumu sana kwetu mikataba ambayo maafisa hawa waliivunja
kujibu swali hili bila kujua huo uwakala kinyume na sheria kwa kisingizio cha jina la
unaouzungumzia ni upi na ni Wizara gani Serikali ambapo ilipelekea Serikali kupata
ambayo Wakala ipo. Wakala zote za Serikali hasara ya mabilioni na matrilioni ya Shilingi
zinaanzishwa chini ya sheria fulani ambayo kwenye usuluhishi. Mkataba ambao pande
ndiyo huanisha mamlaka ya wakala na wakati zinaingia ni lazima uheshimiwe kwa mapana
mwingine mamlaka ya Wizara husika. Hivyo yake; na lazima usomwe na sheria nyingine
tunajibu swali hili kwa ujumla na tunashauri za nchi.
utafute ushauri maalum.
Kwa kuanzia, mkataba wa ubia unatakiwa Duka la dawa lisilo la mfamasia
kueleza haki na wajibu wa pande zote ikiwemo Nilikuja Tanzania kama mtalii wa tamaduni
kipengele cha kuuvunja. Kutegemea na aina na nilishuhudia kwamba usambazaji wa
ya ukiukwaji, aina mbalimbali za kuvunja, madawa maeneo ya vijijini haukuwa wa
kurekebisha, kuponya n.k. zitaelezwa. Hivyo kuridhisha. Ninataka kuja na kufungua
Waziri anabanwa na mkataba wa ubia na hana biashara ya maduka ya dawa maeneo
10 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

ya vijijini na nimekwishaanza kufanya ya vijijini, inaweza kuwa ni changamoto.


uchunguzi wa awali juu ya jambo hili, Sheria haijatatua jambo hili na tunakushauri
ikiwamo kupata maoni juu ya muundo wa uwasiliane na Wizara ya sekta husika ili
biashara. Ninataka kuhakikisha madawa kujadiliana kuhusu jambo hili.
haya yanapatikana kirahisi na kwa bei
nafuu. Hata hivyo, nimearifiwa kwamba Mamlaka ya mji kukamata ng’ombe
kama sijasomea fani ya ufamasia siwezi wangu
kufanya biashara hiyo. Je, hii ni kweli?
Nitawashukuru sana kwa mwongozo wenu Nina ng’ombe na mbuzi wengi. Ili
kwenye jambo hili. kupunguza gharama ya kuwatunza huwa
ninawatelekeza mtaani karibu na nyumbani
28 Oktoba 2013
ili waweze kula majani na kitu kingine
Sheria ya ndani inayosimamia na kudhibiti chochote wanachokikuta/kilichojiotea.
fani ya famasia na taratibu zake ni Sheria Nimekuwa nikifanya hivyo kwa miaka
ya Famasia Na. 1 ya 2011. Ni sheria hii pia mingi, lakini pasipo mimi kujua hili wala lile,
mamlaka ya manispaa imekamata mbuzi na
ambayo imeanzisha Baraza la Wafamasia
ng’ombe wangu na kutaka nilipe faini. Zaidi,
ambalo ndilo lenye mamlaka pekee ya kusajili,
wameniamuru nisiwaachilie tena kama
kuandikisha na kuorodhesha wafamasia, nilivyokuwa ninafanya. Je, hii ni halali? Je,
wafamasia-mchundo (technicians) pamoja mtu asiwalishe ng’ombe na mbuzi wake kwa
na wasaidizi wa wafamasia. Chini ya Sheria amani kwenye majani yaliyojiotea kwenye
hii, ni kosa kwa mtu yeyote kufanya biashara ardhi ya nchi yangu ambayo mimi ni raia
ya famasi/duka la dawa isipokuwa kama wake? Ninataka kuiwajibisha manispaa.
mtu huyo ni mfamasia au amejiunga na Nifanye nini?
chama cha wafamasia. Sheria hii pia kwenye 13 Januari 2014
kifungu cha 43 inatamka kwamba siyo ruhusa
kwa mtu yeyote ambaye siyo mfamasia Tunaelewa manung’uniko yako na ni kweli
kutengeneza kwa kuuza, kusambaza au kutoa ni mazoea ya muda mrefu ya watu kuacha
dawa isipokuwa kwa usimamizi wa karibu wa mifugo yao ikizurura mitaani au barabarani.
mfamasia. Adhabu ya kukiuka masharti ya Hata hivyo, mazoea hayo yamezuiliwa na
kifungu hiki ni kulipa faini isiyopungua milioni sheria za manispaa pamoja na kanuni zake ili
moja au kifungo kisichozidi miezi sita au kuhakikisha kwamba jiji linakuwa safi, kuzuia
vyote kwa pamoja. Na kama mkosaji ni taasisi matatazo ya kiafya yasiyotarajiwa pamoja na
au kampuni, adhabu yake ni faini isiyopungua kuzuia ajali. Tunaamini manispaa imekuzuia
Shilingi milioni tano. kufanya jambo hilo kwa mujibu wa sheria.
Turudi kwenye swali lako, uwekezaji
Kuwa tu raia hakumaanishi kwamba
unaotarajia kuufanya unawezekana
unaweza kufanya chochote kwenye nchi yako.
isipokuwa unatakiwa ufanye biashara hiyo na
Kuna kanuni na sheria za kufuata ili watu wote
mfamasia ili kuendana na matakwa ya sheria,
na mfamasia huyo ni lazima awe amesajiliwa waishi kwa amani na utulivu. Hebu fikiria nini
nchini Tanzania. Kitu ambacho pengine kitatokea jijini Dar es Salaam iwapo kila mkazi
kitakupa changamoto zaidi ni kwamba kuna akaachia mbuzi na ng’ombe wake mitaani.
uhaba wa wafamasia nchini Tanzania na hivyo Tunakushauri uwasiliane na mwanasheria
kumpata mfamasia, achilia mbali maeneo wako.
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 11

Kuwajibika maafisa wa umma kuzingatia kiwango ambacho afisa huyo


amehusika katika upotevu, upungufu au
Nimekuwa nikifanya kazi na baadhi ya uharibifu husika. Katika Kifungu hiki, rejeo/
wahasibu kwenye ofisi za serikali ambao
maana ya neno afisa wa umma itahusisha pia
najua wanaisababishia serikali hasara
mtu ambaye aliwahi kuwa afisa wa umma.
kubwa kwa sababu ya uzembe wao. Si wezi,
Unaweza kuona, kutokana na maelezo
bali wanakosa umakini na muda wote huwa
hapo juu, kwamba kuna sheria maalum
na haraka ya kwenda nyumbani. Ni tatizo
kubwa ambalo linahitaji utatuzi. Je, hakuna ambayo inairuhusu serikali kudai fidia
sheria ambayo inayoadhibu tabia kama kutokana na hasara iliyosababishwa na
hizi ambazo zinaisababishia serikali hasara maafisa wa umma. Wahasibu wengi hawakijui
kubwa? kifungu hiki cha sheria.
24 Februari 2014 Wanadiplomasia hawagusiki
Kifungu cha 10 cha Sheria ya Fedha za Kwa nini wanadiplomasia hawagusiki nchini
Umma kinatamka wazi kwamba: Tanzania? Sisi ni legelege sana kwenye
Iwapo itatokea hasara au upungufu wa suala hili. Tunawezaje kubadili hali hii?
fedha za umma au fedha nyingine zilizotolewa Nimeshtushwa.
au zilizokuwa chini ya usimamizi wa afisa 17 Machi 2014
wa serikali au iwapo hasara au uharibifu wa
mali ya serikali au mali nyingine unatokea Hatujui unamaanisha nini unaposema
wakati mali hiyo ikiwa chini ya uangalizi wa tunawezaje kubadili. Sisi ni wanachama
afisa wa umma na ikiwa Waziri ameridhika wa Mkataba wa Kimataifa wa Vienna, na
baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwamba wanadiplomasia wetu wanapewa upendeleo
uzembe au mwenendo mbovu wa afisa ndio huo huo kwenye nchi nyingine.
uliosababisha au kuchangia kupatikana Unapaswa kutambua kwamba tunafaidika
kwa hasara au upungufu huo; (a) Kiasi hicho pia na mahusiano mazuri ya kidiplomasia
kilichopotea au kupungua; au (b) thamani tuliyonayo nchini Tanzania, ni wazi
ya mali iliyopotea au kuharibika; au (c) umepotoka na maoni yako hayakubaliki. Kwa
gharama za kurudishia au kutengeneza mali kukuongezea mshtuko zaidi, Mkataba wa
iliyoharibika, kama itakavyokuwa, litakuwa Vienna unaeleza yafuatayo: katika Ibara ya 9,
ni deni la serikali na linaweza kurudishwa nchi mwenyeji (wa ubalozi) inaweza wakati
na afisa huyo kwa mujibu wa Sheria ya wowote na kwa sababu yoyote kutangaza
Watumishi wa Umma (Malipo ya Madeni) ya kuwa haimhitaji/haimtaki mwanadiplomasia
mwaka 1970. yoyote. Nchi husika iliyomtuma ni lazima
Iwapo uzembe au utendaji mbovu wa imrudishe/imuondoe afisa huyo ndani
afisa wa umma haukuwa ni sababu pekee ya muda muafaka, vinginevyo afisa huyo
iliyochangia hasara, upungufu au uharibifu atapoteza kinga yake ya kidiplomasia.
unaotokana na kitendo kilichotajwa chini ya Ibara ya 22: Nchi mwenyeji haiwezi
Kifungu kidogo cha (3), kiasi kitakacholipwa kufanya upekuzi, wala kuchukua nyaraka
na afisa huyo kitakuwa ni kile tu ambacho au mali za ubalozi. Ibara ya 30 inapanua
gharama za kukirudisha au kukitengeneza, wigo wa kifungu hiki hadi kwenye makazi
kupotea au kuharibika kama Waziri binafsi ya wanadiplomasia, na ndiyo maana
atakavyoona, baada ya kufanya uchunguzi unaona kwamba katika jiji la Dar, makazi
wa kina, kitakuwa ni cha haki na sawa kwa binafsi ya wanadiplomasia yanajipambanua
12 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

wazi. Ibara ya 27: Nchi mwenyeji ni lazima ya bodi. (3) Kwa madhumuni ya kufanya
iruhusu na kulinda mawasiliano baina maamuzi ya Bodi chini ya kifungu kidogo (2)
ya wanadiplomasia/ubalozi na nchi zao. kuhusu mwanabodi aliyeeleza maslahi yake
Ibara ya 29: Hairuhusiwi kuwakamata wala chini ya kifungu kidogo (1), (a) hatakuwepo
kuwafunga wanadiplomasia. Wana kinga wakati wa majadiliano na katika kutoa
dhidi ya mashtaka ya madai na jinai, ingawa maamuzi ya Bodi; au (b) hatamshawishi
nchi iliyomtuma inaweza kuondoa kinga mwanabodi yeyote wala kushiriki katika
hii chini ya Ibara ya 32. Chini ya Ibara ya 34, kuifanya Bodi kutoa maamuzi. (4) Iwapo
wanadiplomasia wana msamaha wa kodi akidi ya kikao haitatimia kwa sababu ya
mbalimbali, mathalani chini ya Ibara ya 36 mwanabodi kuondolewa kwenye majadiliano
wamesamehewa kulipia ushuru wa forodha. juu ya jambo ambalo ameeleza kuwa na
Ibara ya 31(1)(c) inahusu mambo ambayo maslahi nalo, wanabodi waliobaki wanaweza
hayakingwi na kinga ya kidiplomasia; (a) kuahirisha majadiliano juu ya jambo hilo
shughuli ya kitaalam nje ya shughuli mpaka akidi itimie bila mwanabodi husika; au
rasmi za kidiplomasia, na ndiyo maana (b) kuendelea kujadili na kutoa maamuzi juu
wanadiplomasia wengi hawafanyi kazi yoyote ya jambo hilo kana kwamba akidi imetimia.
nje ya kazi za kidiplomasia. Kwa hiyo, mwanabodi wa TRA ambaye
anamaslahi binafsi ni lazima afichue maslahi
Mgongano wa maslahi kwenye bodi husika, na ikiwa hatofanya hivyo, atakuwa
ya TRA amekiuka Sheria. Adhabu ya juu kabisa ya
Miongoni mwa mambo mengine, kukiuka Sheria hii ni kufungwa jela kwa miaka
nimegundua kwamba kuna wanabodi wa miwili.
TRA ambao wana mgongano wa kimaslahi
Kuishtaki serikali
kwenye masuala ya manunuzi/ugavi. Je,
hakuna Sheria inayowazuia kuwa sehemu Kwa nini nisubiri siku 90 kuishtaki serikali?
ya wafanya maamuzi kwenye manunuzi Au mwanasheria wangu ananichukulia
husika? mbumbumbu? Nini kitatokea kama idara
23 Juni 2014 ninayoishtaki haitoi utetezi wake? Kitu gani
zaidi unaweza kunishauri?
Jedwali la 2 aya ya 4 ya Sheria ya Mamlaka
18 Agosti 2014
ya Mapato inajibu swali lako. Sheria hii
inaeleza kama ifuatavyo: 4(1) Mwanabodi Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya
ambaye anamaslahi ya moja kwa moja Serikali inaeleza wazi katika Kifungu cha 6
ama yasiyo ya moja kwa moja katika jambo kwamba (1) bila kujali masharti ya vifungu
linalojadiliwa au linalotaka kujadiliwa, baada vingine kwenye Sheria hii, kesi za madai
ya kufahamu jambo husika, atapaswa kuweka zinaweza kufuguliwa dhidi ya serikali kwa
wazi maslahi hayo haraka iwezekanavyo. masharti ya kifungu hiki. (2) Hakuna kesi dhidi
(2) Maslahi yaliyoelezwa chini ya kifungu ya serikali itakayo funguliwa na kusikilizwa
kidogo (1) yatarekodiwa kwenye muhtasari isipokuwa pale tu mlalamikaji atakuwa
wa kikao cha Bodi, na mwanabodi aliyefichua amewasilisha kabla kwenye wizara ya serikali,
maslahi yake, isipokuwa kama Bodi itaamua idara au afisa anayehusika notisi siyo chini ya
vinginevyo kuhusu suala hilo (a) hatahudhuria siku tisini juu ya nia yake ya kuishtaki serikali,
kwenye majadiliano yoyote ya Bodi kuhusu ikieleza msingi wa dai lake dhidi ya serikali na
jambo hilo; (b) hatakuwa sehemu ya maamuzi atatuma nakala ya dai lake kwa Mwanasheria
Migogoro ya Kibiashara dhidi ya Viongozi wa Serikali • 13

Mkuu wa Serikali. (3) Kesi zote dhidi ya Mkurugenzi Mkuu atampa ofisa wa Taasisi
serikali, baada ya kuwasilishwa kwa taarifa kitambulisho ambacho kitakuwa ni ushahidi
zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa utumishi wake kwenye Taasisi (2) Kila
wa Serikali, na nakala ya hati ya mashtaka ofisa wa Taasisi atapaswa kumuonesha mtu
ipelekwe kwenye wizara husika, idara au afisa atakayehitaji kitambulisho chake cha kazi
ambaye anatuhumiwa kutenda kosa hilo (3) Ofisa wa Taasisi anayefanya upelelezi wa
ambalo ni msingi wa shtaka la madai. (4) Kesi kosa linaloshukiwa kufanywa kwa mujibu wa
zote dhidi ya serikali zitafunguliwa Mahakama Sheria hii au Sheria nyingine zinazohusiana
Kuu kwenye Kitengo cha Mahakama Kuu na rushwa anaweza kumuomba msaada ofisa
katika eneo ambalo dai limetokea. (5) Bila yeyote wa umma kwa kuzingatia matumizi
kujali masharti ya kifungu kidogo cha (3), yanayofaa ya mamlaka yake au utekelezaji wa
Mwanasheria Mkuu anaweza, isipokuwa majukumu yake kwa mujibu wa sheria hii.
kama mtu mwingine anastahili kushtakiwa, Kifungu cha 12 kinahusu upekuzi ambapo
kushtakiwa au kuunganishwa kama kinaeleza: (1) Mkurugenzi Mkuu anaweza,
mshtakiwa mwenza/pacha, kwenye kesi kwa maandishi, kumuidhinisha ofisa yeyote
yoyote dhidi ya serikali. (6) Vifungu vya Sheria kumpekua mtu yeyote iwapo, kwa sababu
ya Watumishi wa Umma (Malipo ya Madeni) za msingi, itashukiwa kuwa mtu anayehusika
vitatumika kwa afisa yeyote aliyeisababishia anamiliki mali iliyopatikana kwa njia ya
serikali hasara, gharama na fidia kutokana rushwa au kwa njia nyingine yoyote haramu
na kushindwa kwake kupata uwakilishi wa au kupekua mahali popote, chombo cha
kisheria katika kesi husika. usafiri, boti/meli, ndege au gari lingine lolote
Ingawa haihusiani, iwapo idara ya serikali iwapo kuna sababu za msingi za kuamini
ikishtakiwa na haijajitetea kwa kupeleka kuwa mali yeyote iliyopatikana kwa njia
utetezi, basi kesi itaendelea upande mmoja ya rushwa au kwa njia haramu imewekwa,
na inawezekana ukafanikiwa katika madai imetunzwa au kufichwa humo.
yako. Hata hivyo, mkuu wa idara ambaye Hivyo, ingawa upekuzi wa majengo
ameshindwa kupeleka utetezi dhidi ya kesi unaruhusiwa chini ya sheria, kama maafisa
anaweza kuwajibishwa yeye mwenyewe waliopo hawataki kuonesha utambulisho
kwa kiasi cha fedha hizo chini ya Sheria ya wao, watakuwa hawatoki TAKUKURU na
Watumishi wa Umma (Malipo ya Madeni). inawezekana ulikuwa unashughulika
na waharifu hasa ukizingatia kwamba
Mamlaka ya TAKUKURU kufanya walilazimisha kuingia ndani.
upekuzi
Zabuni kufunguliwa kabla ya muda
Maafisa wa TAKUKURU walikuja kufanya
mwafaka
upekuzi kwenye eneo letu. Tuliwasihi
wajitambulishe, lakini walikataa na Kampuni yetu iliomba zabuni kubwa
kulazimisha kuingia. Je, hii inaruhusiwa? ya ujenzi wa barabara. Wakati zabuni
15 Septemba 2014 zinafunguliwa tuligundua kwamba lakiri
ya zabuni ilikuwa imechezewa na bahasha
Hujatuambia nini kilitokea baada ya wao imefunguliwa. Je, hili siyo tatizo kubwa?
kulazimisha kuingia. Tunaona jambo hili ni
22 Septemba 2014
kinyume cha sheria kwa sababu Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa inaeleza Ikiwa lakiri ya zabuni ilifunguliwa, zabuni
yafuatayo kwenye Kifungu cha 11(1)-(1) inaweza kufutwa. Hata hivyo hii itategemea
14 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

na mazingira na ushahidi ambao utatolewa.


Ikiwa upo sahihi, mtu aliyefungua lakiri
ana hatia kama ilivyoelezwa chini ya Kifungu
cha 104 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma
ya mwaka 2011 ambayo inasema kwamba
mtu anayefungua zabuni yoyote ambayo
bado ina lakiri, ikiwa ni pamoja na zabuni
zinazoweza kukusanywa kupitia mfumo wa
kielektroniki na nyaraka yoyote inayotakiwa
kufungwa, au kufungua na kuona yaliyomo
kabla ya muda rasmi uliowekwa kwa ajili ya
ufunguzi kwa umma wa nyaraka za zabuni,
atakuwa ametenda kosa na akikutwa na
hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua
Shilingi milioni kumi au kifungo kwa
muda usiopungua miaka saba au vyote
kwa pamoja, na kwa kuongezea, adhabu
iliyotolewa chini ya kifungu hiki, mahakama
itaagiza kiasi cha hasara aliyopata mlalamikaji
afidiwe, ikishindikana mahakama itatoa
amri ya kupokonywa mali binafsi ya mtu
aliyehukumiwa ili kufidia hasara husika.
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 15

Watoto, Mahusiano,
Sheria za Ndoa na
Talaka

Ndoa, talaka, na masuala yanayohusu ustawi wa watoto yanaweza kupelekea migogoro


mizito ya kisheria. Je, unaweza kudai zawadi ulizoahidiwa kabla ya harusi, kumpa jina
mwanao, au kutoa talaka kwa mwenzi wako kwa sababu ya unene uliopitiliza au kufuga
ndevu? Haya ni baadhi tu ya maswali yaliyoulizwa na wasomaji wa safu yetu.
16 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Stahiki baada ya talaka Kwa kawaida, mgawo haujali kama mali zipo
kwa jina la mmeo au la kwako.
Niliolewa miaka kumi iliyopita, Mmeo anadhani anaweza tu kukufukuza.
nimemchoka mume wangu na ninataka
Hiyo siyo kweli na sheria inakulinda. Mmeo
talaka. Nimekuwa mama wa nyumbani na
anapaswa kusoma baadhi ya kesi maarufu
sikuwa na mchango wa moja kwa moja
za talaka ambapo wanaume wamekuwa
wa kifedha kwenye kununua mali ambazo
masikini zaidi kwa sababu ya talaka kama
mume wangu alizichuma wakati wa ndoa
yetu. Mara zote amekuwa akiniambia ilivyo kwa kesi ya mwandishi maarufu Rupert
nimekuwa baraka kwake, kwa kuwa tangu Murdoch, aliyekuwa mcheza kikapu maarufu
amenioa ameingiza pesa nyingi sana. na nyota Michael Jordan, aliyekuwa mcheza
Anajua ninataka takala lakini ameniambia gofu maarufu, Tiger Woods, muongoza filamu
wazi kuwa kama nikifungua kesi kudai Steven Spielberg, muigizaji Harrison Ford na
talaka nitaishia mtaani na hatonipatia muimbaji Lionel Richie ambapo wote hao
pesa ya matunzo wala kunilipa (kifuta talaka ziliwagharimu mabilioni.
jasho) chochote. Na anasisitiza kuwa mali Tunakuonya pia kuwa kama wakati
zote ni za kwake na wanafamilia yake. Ni wowote uliwahi kutumia mali za familia vibaya
kweli sijaleta pesa taslimu nyumbani lakini kwa mfano kununua vito vya thamani visivyo
nimemsaidia kusimamia biashara zake zote. vya lazima au ulitumia pesa kwa anasa, pesa
Hivi, ni kweli sistahili chochote? Nifanyeje? hizo zitakatwa kwenye kiasi unachostahili
Kusema kweli, sitaweza kuishi hata kidogo kupewa. Ushauri wetu hapa ni kwa ajili ya
kwenye dunia hii kama mume wangu kukuongoza tu na siyo kuharibu au kuvunja
dhalimu atanifukuza bila kunipa chochote. uhusiano wenu. Unaweza kumtafuta mshauri
6 Februari 2012 wa masuala ya ndoa kwa ushauri zaidi.
Hujatuambia kwa nini unataka talaka. Mke anataka talaka
Nchini Tanzania, hamuwezi tu kukubaliana
kupeana talaka. Sheria ya ndoa inatoa Mimi na mke wangu tulioana na kuishi
sababu maalum kama vile uzinzi, ukatili, au kwa furaha hadi siku za hivi karibuni
kutelekezwa ambazo ni lazima uzieleze ili alipoanza kuibua barua-pepe za kabla ya
uweze kupata talaka. Mahakama pia, kabla ndoa yetu ambapo alikuta zenye ujumbe
ya kutoa amri ya talaka, ni lazima ijiridhishe wa mapenzi kutoka kwa mpenzi wangu wa
kwamba ndoa yenu imevunjika kabisa na zamani. Anasema ningemwambia kuhusu
uhusiano huo kabla ya ndoa. Nilimjibu
kwamba haiwezi kurekebishika kabla ya
kuwa hakuniuliza na sijawahi kuwasiliana
kutoa amri ya talaka.
na mpenzi huyo baada ya ndoa. Hata yeye
Iwapo utaamua kuomba talaka
alikuwa na wapenzi wake ambao taarifa zao
Mahakamani, kuna maamuzi mengi ya
sikuwahi kuzifuatilia kwa kuamini kwamba
Mahakama, ikiwemo kesi maarufu ya ya kale yamepita. Mke wangu anataka
Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambayo talaka. Nifanyeje?
iliamua kwamba kazi za nyumbani zina
20 Februari 2012
mchango katika kuchuma mali za ndoa.
Kwa kuwa umemsaidia mmeo kuangalia Sheria ya Ndoa ya Tanzania ina vifungu
nyumba yenu, pale anapokuwa mbali, pamoja mahususi ambavyo vinaeleza sababu
na kusimamia mali za familia, unastahili zinazoweza kutolewa wakati wa kuomba
mgawo sawa kwa mali mlizozichuma pamoja. talaka. Kwa mfano, mtu hawezi tu kupewa
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 17

talaka Tanzania kwa makubaliano yake na akichunguliwa wakati akichukua sampuli ya


mume wake. Baadhi ya sababu za msingi mkojo.
ni ukatili, uzinzi na utelekezaji. Ni wazi Ni lazima tukueleze kwamba, jibu letu
kuwa haupo kwenye kundi la uzinzi, kama kuhusu suala lako linaweza lisikidhi matakwa
tutachukulia kuwa ulichotuambia kina ukweli yako kwa sababu katiba yetu haitumiki
ndani yake kwamba hujawahi kuonana nchini Afrika Kusini. Unaweza kuwasiliana
na mpenzi wako baada ya ndoa. Inatuwia na mwanasheria wa huko (Afrika Kusini) kwa
vigumu kuamini kwamba kutoka tu hewani mwongozo zaidi.
mkeo ameamua kuangalia barua-pepe zako
Kutelekeza mtoto na kukataa kumpa
za miaka mingi iliyopita. Kama kuna kitu
chakula
unatuficha tafadhali puuza jibu letu. Hata
hivyo, tunajaribu kujibu swali lako tukiamini Nimekutana na mwanamke mmoja jijini
hujatuficha chochote. Dar es Salaam ambaye hatoi mahitaji kwa
Sababu nyingine ya kawaida ya talaka ni watoto wake wadogo. Anasema ni yeye
kutelekeza ambayo pia tunaamini haihusiki ndiye anayeamua juu ya ustawi wa watoto
kwenye kesi yako. Ukatili ni sababu mojawapo wake na siyo mtu mwingine. Hawajali japo
lakini ni ya mbali sana. Kwa mfano, hivi ana uwezo wa kufanya hivyo. Je, hilo siyo
mkeo anaweza kudai umekuwa mkatili kwa kosa?
kutokumtambulisha kwake mpenzi wako wa 19 Machi 2012
zamani? Tuna mashaka kuna mazingira yasiyo Mtu yeyote ambaye ni mzazi, mlezi au
ya kawaida ambayo hatuyajui. mtu mwingine ambaye ni mwangalizi halali
Yote kwa yote, hatuoni namna kesi ya au aliyepewa jukumu la kumlea mtoto
mkeo itafanikiwa kwa sababu ulizotueleza ana wajibu wa kutoa mahitaji ya msingi ya
kwenye swali lako. Tunapendekeza maisha kama vile chakula, mavazi, malazi
mumtafute mshauri maana inaonesha kuna na kadhalika kwa ustawi bora wa mtoto.
jambo unatuficha. Kumwacha mtoto bila msaada ni kosa la
kutelekeza ambalo linaadhibiwa kisheria. Kwa
Kuvunja haki ya faragha kuongezea, kukataa kutoa mahitaji ya msingi
Nimempeleka kijana wangu wa kiume kiasi cha kudhohofisha afya ya mtoto pia ni
kosa. Makosa haya adhabu yake ni kifungo
wa miaka 14 nchini Afrika Kusini kwenye
cha miaka miwili jela, faini au vyote viwili kwa
shule ya michezo kwa ajili ya majaribio.
Kabla hawajampokea, walimsindikiza pamoja.
bafuni na kumpima mkojo. Nilipinga, Kumlazimisha mwenza kupima VVU
lakini waliniambia ni lazima apimwe. Je,
kitendo hicho si kuvunja haki yake ya Mimi na mpenzi wangu/rafiki wa kiume
faragha kikatiba? tupo kwenye mahusiano kwa miezi sita na
27 Februari 2012 tunakusudia kuoana. Nakubaliana na sharti
lake lakini nina sharti kwamba wote wawili
Suala hili limekuwa na mjadala kwa nchi ni lazima tukapime VVU/UKIMWI kwanza
nyingi na utafiti wetu unaonesha kwamba kabla ya kuendelea. Jambo la kushangaza,
mara nyingi chuo kinachofanya vipimo amekataa anasema yeye ana afya na
huwa kinashinda. Wakati mwanao alipoenda haoni haja ya kwenda kupima. Nioane
kupima mkojo, inawezekana alisindikizwa nae? Nifanyeje?
lakini hakuna uwezekano kwamba alikuwa 30 Aprili 2012
18 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Sheria za Tanzania hazilazimishi upimaji wa kumuoa mtoto wake mwenyewe au mtoto


VVU, isipokuwa kwa hiari ya mtu anayepimwa. wa mwenzi wake wa awali. Mmeo anaweza
Hata hivyo yapo mazingira ambayo upimaji kujenga hoja kwamba binti anayetembea naye
wa VVU hauhitaji hiari kama vile: kwa amri kwa sasa siyo mwanao kwa sababu ulimuasili.
ya Mahakama, uchangiaji wa viungo vya Lakini sheria inamtambua kama mwanao na
binadamu na makosa ya kingono. Mpenzi hivyo kwenye sheria zetu hawezi kumuoa.
wako haangukii kwenye lolote kati ya hayo na Chini ya Kanuni ya Adhabu mwanamume
hivyo huwezi kumlazimisha kwenda kupima. yeyote ambaye amekatazwa kufanya ngono na
Katika hali nyingine, ni vizuri kumfahamisha mwanamke yeyote ambaye anamjua kuwa ni
mpenzi wako kwamba ni kosa la jinai nchini mjukuu wake, binti yake, dada yake au mama
kwetu kusambaza VVU kwa makusudi kwa mtu yake, mwanamume huyo atakuwa amekosa
mwingine. Kosa hilo adhabu yake ni jela kati ya na akipatikana na hatia atastahili adhabu.
miaka 5 hadi 10. Kuwa na afya hakumaanishi Iwapo mwanamke ana umri wa chini ya
kwamba hauna VVU/UKIMWI, tunawashauri miaka kumi na nane, mwanamume huyo
mpate ushauri kutoka kwa mshauri wa atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka
masuala ya VVU/UKIMWI. Iwapo uolewe au thelathini, na iwapo mwanamke ana umri wa
usiolewe, kwa bahati mbaya kama wanasheria miaka kumi na nane au zaidi, mwanamume
hatuna sifa za kujibu swali hilo. huyo atahukumiwa kifungo kisichopungua
miaka ishirini. Haitakuwa na utetezi kwamba
Mume wangu kumuoa mwanangu wa
kitendo cha ngono kilifanywa kwa idhini ya
kuasili
mwanamke huyo.
Nilikuwa kwenya ndoa kwa zaidi ya miaka Mwanao anafanya uhalifu. Sheria inatamka
20 na ndoa yetu haikubarikiwa mtoto kwamba mwanamke yeyote mwenye umri wa
yeyote. Tuliasili mtoto ambaye tumemlea zaidi ya miaka kumi na nane ambaye anaridhia
kwa miaka mingi. Mume wangu alifariki kwa na anamruhusu babu yake, baba yake, kaka
ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na yake au mtoto wake wa kiume kujamiiana
fahamu, kwa kiingereza ‘Alzheimer’, miaka
naye (akijua kwamba huyo ni babu, baba,
mitano iliyopita. Hivi karibuni nilikutana
kaka au mtoto wake vyovyote itakavyokuwa)
na kijana mzuri na tukaoana na baadaye
nikagundua kuwa ana mahusiano ya atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa
kimapenzi na mwanagu wa kuasili. Sikuwa adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo
na jinsi zaidi ya kudai talaka na mwishowe kisichopungua miaka thelathini na pia anaweza
nikagundua kwamba mume wangu anataka kuamriwa kulipa fidia ya kiasi kitakachoamriwa
kufunga ndoa na binti yangu wa kuasili. na Mahakama kwa yule aliyetendewa kosa hilo.
Wanasheria wangu wananiambia ni ngumu Kunaweza kutokea mjadala wa iwapo mume
kuzuia wasioane kwa sababu ndoa ni uliyeachana naye ni baba wa mtoto wa binti
mkataba wa watu wawili na kwa hiyo siwezi yako lakini yote kwa yote mume uliyeachana
kuingilia. Nifanye nini?
naye atakuwa ametenda kosa la uharimu.
30 Aprili 2012
Unaweza kuweka pingamizi kanisani
Wanasheria wako, wako sahihi kwamba ambako ndoa itafanyikia au unaweza kuomba
ndoa ni mkataba. Lakini iwapo unaweza kuzuia Mahakamani. Unaweza pia kutoa taarifa kituo
ndoa hiyo, tunaamini unaweza. Kwa mujibu wa cha polisi kwa kitendo hicho, kwani kitendo cha
Sheria ya Ndoa ya Tanzania, baba amezuiliwa uharimu ni kosa la jinai.
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 19

Mke ananinyima penzi/unyumba mimba za mara kwa mara. Siamini katika


matumizi ya kondom na iko nje ya uwezo
Tangu nilipomuoa, mke wangu hajawahi wangu kwani Mungu ametutunukia watoto
kuniruhusu hata kumgusa. Anasema wengi. Mwanasheria ameniandikia barua
hayuko tayari kwa hilo. Nimechanganyikiwa kwamba kuna Kanuni fulani ambazo
na sijui nifanye nini. Naweza kupata amri ya zinataka familia lazima itumie uzazi wa
Mahakama ya kumlazimisha ashiriki nami? mpango vinginevyo kuwe na ukomo wa
Bado nampenda. idadi ya watoto ambayo mtu anatakiwa
7 Mei 2012 kuwa nao. Je, hii ni kweli?
4 Juni 2012
Unaposema hakuruhusu kumgusa,
tunachukulia kwamba anakunyima unyumba, Kwa uzoefu wetu wa miaka mingi,
yaani anakunyima haki ya ndoa. Ndoa ni hatujawahi kuona sheria inayomlazimisha
mkataba na moja ya masharti ya mkataba mtu kutumia uzazi wa mpango. Pia, hakuna
ni kwamba mtaishi kama mke na mume sheria ambayo inaelezea idadi ya juu ya
na kwamba hautanyimwa tendo la ndoa. watoto ambayo mtu anatakiwa kuwa nao.
Umenyimwa haki zako hizi kwa sababu mkeo Ingawa mwanasheria pamoja na baba mkwe
hayuko tayari. Labda ungetamani akuambie wako wanakupotosha, siyo wazo baya kuanza
hili mapema kabla hamjaoana lakini sasa kufikiria kutumia njia za asili za kuzuia ujauzito
umechelewa sana. Kwa hiyo swali lako ni kwa sababu kudhibiti uzazi, baada ya kuwa
iwapo unaweza kupata amri ya Mahakama ya na idadi fulani ya watoto, kunaweza kuwa na
kumlazimisha ashiriki tendo la ndoa. faida. Hilo nalo linategemea, na ni wazo letu
Kutaka amri ya Mahakama kushinikiza tu. Kama wanasheria, hatuna ujuzi kuhusu
tendo la ndoa ni kitendo cha kizamani, na siyo njia za asili za uzazi wa mpango. Tunakushauri
chaguo sahihi nyakati hizi. Kwa hiyo, hauna kuwasiliana na mshauri wa masuala ya jinsia
chaguo hilo, labda muendelee kuishi hivyo na uzazi.
mpaka yeye atakapokuwa tayari au umpe
Nataka kuoa msichana mwenye umri
talaka. Kunyimwa tendo la ndoa ni sababu
wa miaka 16
mojawapo ambayo unaweza kuitumia
kuomba talaka. Tafadhali elewa kwamba Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu. Ninaishi
usimlazimishe kufanya mapenzi. Ingawa ni Dodoma na nipo kwenye mapenzi na
wanandoa na bado mpo kwenye mahusiano, msichana wa miaka 16. Sote tunapendana
mkeo anayo haki ya kusema hapana, na sana na tunataka kuoana. Wazazi wa
ikiwa utaendelea kumlazimisha unaweza msichana wamekataa kutupatia baraka za
kushtakiwa kwa kosa kubwa la ubakaji. Katika kuoana. Nimefanya kila linalowezekana
hali nyingine, unaweza kutafuta kujua sababu kuwashawishi watupe baraka zao lakini
haijazaa matunda. Ni mwanya gani
ya kukukatalia. Unaweza pia kufikiria kupata
mwingine ninao?
ushauri kutoka kwa mshauri wa ndoa.
18 Juni 2012
Idadi ya juu ya watoto
Sheria ilivyo kwa sasa inamtaka
Baba mkwe wangu amekuwa akiingilia mwanamke ambaye hajafikisha umri wa
ndoa yangu kwa miaka kadhaa sasa. miaka kumi na nane kupata idhini ya wazazi
Anasema kwamba nampa sana mwanae na kama hakuna wazazi basi mlezi kabla
msongo wa mawazo kwa kumbebesha hajaolewa. Hata hivyo, kifungu cha 17 cha
20 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Sheria ya Ndoa ya 1971 kinasema kwamba Kushika ujauzito kwa kawaida ni baraka
kama idhini imekataliwa unaweza kuomba na siyo laana na kama ulivyosema siyo kosa
Mahakamani ambayo baada ya kuridhika kisheria. Sheria ya Mtoto inamruhusu mama
kwamba idhini imekataliwa bila sababu za anaetarajia kujifungua kupeleka maombi
msingi, inaweza kutoa idhini hiyo ambayo ya matunzo Mahakamani na kama itaona
itakuwa sawa na idhini inayotolewa na wazazi sababu za msingi za kuamini kwamba
au mlezi kutegemea na aliyepo. mwanamume anaedhaniwa kuwa ni baba
Hata hivyo, inashauriwa kuoa/kuolewa wa mtoto kweli ndiye na kwamba maombi
katika umri mkubwa zaidi baada ya msichana ya matunzo yameletwa kwa nia njema na
kupata elimu ya juu zaidi. Ulimbwende wa siyo kwa malengo ya kutishia au kwa shari,
msichana unaweza ukaishia miaka 20, lakini maombi yako yanaweza kufanikiwa. Hivyo
elimu yake itabakia; na inawezekana hicho una hiari ya kufungua maombi Mahakamani
ndicho wazazi wake wanafikiria, na sisi ukiomba amri ya matunzo kwa kipindi cha
tunadhani siyo vibaya kuwa na fikra hizo. ujauzito. Kwa msaada zaidi tafadhali wasiliana
Lazima pia tulilete suala hili moja kubwa na mwanasheria wako.
kwenye akili yako. Tunachukulia kwamba
unashiriki ngono na huyo msichana. Tafadhali Uhalali wa ndoa
elewa kwamba kifungu cha 130(2) (e) cha Mimi ni Mkatoliki ambaye niliolewa miaka
Kanuni ya Adhabu kinatamka kwamba mtu minne iliyopita na kubarikiwa kupata
wa jinsia ya kiume atakuwa ametenda kosa watoto wawili. Hivi karibuni nimegundua
la kubaka kama atakuwa amefanya tendo kwamba mume wangu ana mke mwingine
la ndoa na msichana au mwanamke kwa Dar es Salaam ambaye alimuoa kwa ndoa
idhini au bila ya idhini akiwa chini ya umri ya kikristo. Baada ya kufuatilia kwa karibu,
wa miaka kumi na nane, isipokuwa kama nimegundua kwamba alimtelekeza mke
mwanamke ni mke wake ambaye ana na familia yake kwa ajili yangu na hakuna
umri wa miaka kumi na tano au zaidi na talaka iliyotolewa. Je, inawezekana mume
hajatengana na mumewe. wangu kuoa wake wawili?
Kutokana na maelezo hapo juu unaweza 2 Julai 2012
kuona kwamba hata kama mpenzi wako
anaridhia kufanya ngono na wewe, kwa umri Sheria ya ndoa ya Tanzania inatambua
wake, siku akitoa taarifa hii polisi, unaweza ndoa kama ni muungano wa mume na mke
kushtakiwa kwa ubakaji ambalo ni kosa ambayo inakusudia kudumu mpaka mwisho
kubwa sana. wa maisha yao. Pia sheria inatambua ndoa
ya kikristo kuwa ni doa ya mke mmoja. Ndoa
Kuhudumia ujauzito ya mke mmoja ni ndoa kati ya mke mmoja
Mimi ni mtu mzima na nimepata ujauzito na mume mmoja tu. Pia sheria inatambua
na najua siyo kosa kisheria. Mpenzi njia zifuatazo ambazo zinaweza kufanya
wangu ambaye alinipa ujauzito, hana tena ndoa kufika mwisho; (a) kifo cha mmoja
mapenzi na mimi kwa sababu ananiona wa wanandoa (b) amri/tuzo ya Mahakama
ati ni mkubwa na sivutii tena. Anashindwa inayotangaza kuwa mmoja wa wanandoa
kunisaidia na kusahau kuwa na yeye ana anadhaniwa kuwa amefariki; (c) amri/tuzo
mama ambaye pia aliubeba ujauzito wake. ya Mahakama ya kubatilisha ndoa; (d) amri/
Nifanye nini? tuzo ya talaka; au (e) kwa talaka iliyotolewa na
25 Juni 2012 Mahakama nje ya Tanzania.
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 21

Kwa kuwa mume wako hakupata talaka hutaki kumsajili mwanao kwa sababu ana
kabla ya kukuoa, ndoa yake ya kwanza ni uwezo wa kipekee haitambuliki kwenye
halali na bado ipo. Sheria pia inazuia mtu sheria zetu. Hakuna uwezekano kwamba
mwenye ndoa ya mke mmoja kuingia uwezo huo utapotea kwa kumsajili mwanao.
kwenye ndoa nyingine. Kifungu cha 15 cha
Sheria ya Ndoa kinasema kwamba hakuna Kuolewa tena
mwanamume, akiwa kwenye ndoa ya mke Nilikuwa kwenye ndoa kwa miaka 10 kabla
mmoja, kufunga ndoa nyingine. Wakati mume ya mume wangu kufariki miaka miwili
wako alipokuoa, alikuwa hana sifa za kufanya iliyopita. Wakati wa ndoa yetu tulichuma
hivyo, na ndoa yako inaweza kuwa batili. mali kwa pamoja kwa sababu sote
Tunakushauri uwasiliane na mwanasheria tulikuwa na kazi nzuri. Nimekutana na mtu
wako kwa muongozo zaidi. ambaye ananipenda na tunataka kuoana.
Ndugu wa mume wa zamani wanajaribu
Kusajili uzazi/mtoto aliyezaliwa kunizuia kuolewa tena wakisema kwamba
Mimi na mke wangu tuna mtoto mzuri wa hairuhusiwi na kama nikifanya hivyo moja
kiume ambaye mke wangu alizalishwa kwa moja wao watachukua mali zangu.
nyumbani na mkunga wa jadi kijijini Tafadhali naomba muongozo.
kwetu. Ninaamini mwanangu ana uwezo 6 Agosti 2012
wa kipekee na sitaki kumsajili kama mtoto
Kifungu cha 68 cha Sheria ya Ndoa
aliyezaliwa. Nifanye nini? Je, ni lazima
hakimkatazi mwanamke kuolewa tena na
nimsajili?
kinaeleza kwamba bila kujali mila zozote
9 Julai 2012
zinazoenda kinyume, mwanamke aliyefiwa
Sheria ya Uandikishaji Vizazi na Vifo na mume atakuwa huru (a) kwenda kuishi
inakulazimisha kumsajili mtoto wako mahala popote apendapo; na (b) kukaa
aliyezaliwa. Sheria inatamka wazi kwamba bila mume au kuolewa na mume yeyote
kila mtoto aliyezaliwa hai baada ya kuanza atakayeridhika naye kwa kuzingatia masharti
kutumika Sheria hii na ambaye usajili wake ya kifungu cha 17; Isipokuwa, kama aliolewa
ni wa lazima, itakuwa ni jukumu la baba au katika ndoa ya kiislamu, mjane huyo
mama, na kama baba au mama wakishindwa, hatakuwa na haki ya kuolewa tena mpaka
mkazi wa nyumba ambaye kwa uelewa pale kipindi cha eda kitakapokwisha.
wake, mtoto huyo amezaliwa, na kila mmoja Kuhusiana na ndugu wa upande wa mume
aliyekuwepo wakati mtoto anazaliwa, wako, kama mlimiliki mali hizo kama wamiliki-
kumsajili mtoto huyo ndani ya miezi mitatu wenza (joint occupiers), basi umiliki wa mali
tangu kuzaliwa. hizo moja kwa moja unahamia kwako kama
Chini ya Sheria hii, kama mtu mwenye mmiliki mwenza uliyesalia baada ya kifo cha
wajibu wa kusajili kizazi au kifo cha mtoto mume wako. Lakini kama umiliki wa mali
anashindwa kufanya hivyo atawajibika kulipa hizo ulikuwa ni umiliki-shirika (occupiers
faini isiyozidi Shilingi laki tano au kifungo in common), basi sehemu yako katika
kisichozidi mwezi mmoja au vyote kwa umiliki itabaki kwako na sehemu ya mume
pamoja. wako itahamishiwa kwa yeyote (mshirika
Hivyo, kumsajili mtoto wako ni lazima na mwingine) aliyetajwa kwenye wosia. Utofauti
kuna kifungo ikiwa utakiuka. Sababu kwamba kati ya umiliki-wenza na umiliki-shirika ni
22 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

muhimu na watu wengi hawajui kutofautisha maisha yangu. Anauvunja moyo wangu kitu
haya. ambacho ni sawa na kosa la jinai. Je, siwezi
kupata zuio, kumzuia kutoka na mpenzi
Zawadi kwa msichana mzuri wangu? Ninawezaje kumrudisha mpenzi
wangu kisheria? Tafadhali niongoze.
Nilikutana na msichana mzuri na tulianza
mahusiano. Baada ya kumshawishi na 27 Agosti 2012
yeye kukubali kuhusu kuoana, na ili Ingawa tunasononeka sana moyo
kumfanya aridhike, nilimpatia zawadi wako kuvunjika, tafadhali elewa kwamba
nyingi sana, mojawapo ikiwa ni gari langu. mwanamume unayetembea naye ni mpenzi
Hivi karibuni nimeshtuka kuona kwamba
tu na siyo mume wako. Ingawa kimaadili
ana mwanamume mwingine ambaye
inaweza isiwe sahihi kwake kutembea na
alikuwa anajifanya kama ni dereva wake
nyie wote wawili, hakuna sheria inayomzuia
na yupo kwenye mahusiano naye na
kutembea na mwanamke mwingine. Sheria
tayari amekwisha toa mahari. Anakataa
ni tofauti na maadili, kwa bahati mbaya sana,
kunirudishia zawadi nilizomnunulia,
hatujawahi kuona sheria inayozuia jambo hili.
likiwemo gari langu. Nifanye nini?
Tabia za rafiki yako zinaweza kuwa
13 Agosti 2012
za kikatili, zisizo na maadili na pengine
Zawadi zilizotolewa wakati wa uchumba zisikubalike; lakini siyo kinyume cha sheria
zinaweza kurudishwa kisheria kama uchumba na hivyo haiwezekani kushtaki. Sisi kama
huo usipozaa ndoa. Kifungu cha 71 cha Sheria wanasheria hatuna utaalamu na masuala ya
ya Ndoa kinamruhusu mtu kufungua shauri mahusiano na hivyo unaweza kufikiria kupata
Mahakamani ili kurudisha zawadi zilizotolewa ushauri kuhusu mpenzi wako kama unaona
wakati wa kusubiria ndoa ambayo hata hivyo anaweza kubadili tabia zake. Kinyume na
haikufanikiwa, na inaweza kurudishwa kama hapo, huna jinsi, zaidi ya kuachana naye na
Mahakama itajiridhisha kwamba zawadi hizo kutafuta rafiki na mpenzi mwingine.
zilitolewa kwa sharti kwamba ndoa ifanyike na Zuio haliwezi kutolewa kwa sababu
siyo vinginevyo. Wanasheria wako wanaweza ulizoziainisha hapo juu. Rafiki yako havunji
kukuongoza zaidi. sheria kwa kutembea na mpenzi wako.
Tuchukulie mpenzi wako na rafiki yako
Rafiki yangu anatembea na mpenzi wanashiriki mapenzi, hakuna sheria
wangu inayomzuia yeye wala mtu mwingine yeyote
kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi,
Mimi ni msichana mrembo na niliyeelimika.
Nina mpenzi ambaye tupo kwenye ilimradi tu kama kuna idhini, wapenzi wana
mahusiano kwa miaka mitatu. Hivi karibuni umri sahihi, na hakuna kitu kingine kisicho
kuna mtu amenidokeza kwamba rafiki cha kawaida kwenye mahusiano hayo ya
yangu wa karibu anatoka kimapenzi na kimapenzi.
mpenzi wangu. Ninakumbuka kipindi Mama hawatunzi/kawatelekeza watoto
cha nyuma rafiki yangu alikuwa akimsifia
mpenzi wangu na kumtamani. Kuna ujumbe Kuna mwanamke mmoja ambaye ana
wa kufurahisha ambao alikuwa anamtumia watoto wanne lakini hawatunzi Wanao-
mpenzi wangu ukionyesha kwamba kuna nekana kuzurura na kulala maeneo ya
kitu kinaendelea. Nataka nimfundishe Gymkhana. Je hakuna sheria inayowalinda
rafiki yangu kwa kumshtaki kwa kuingilia watoto hao bila kujali kwamba ni mama yao
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 23

ambaye anawatesa? mrefu na mwanamke ambaye tuliachana


15 Oktoba 2012 hivi karibuni. Ili asimwambie yeyote kuhusu
mahusiano yetu ikiwemo mke wangu,
Sheria ya Mtoto ina Vifungu ambavyo tuliingia mkataba kupitia mwanasheria
vinamtetea mtoto. Sheria hii ina muelezea kwamba nimlipe milioni 2.2 kila mwezi na
mtoto kama ni mtu yeyote mwenye umri chini kumlipia gharama za bima za matibabu.
ya miaka kumi na nane na inaeleza kwamba Makubaliano yalikuwa mwanamke huyo
maslahi ya mtoto yatakuwa ni zingatio la afunge mdomo wake na kwenda kuishi
msingi katika masuala yote yanayohusiana kwenye mji mwingine. Nimemlipa pesa
na mtoto yanayosimamiwa na taasisi za hizo kwa miaka minne na sasa nipo kwenye
umma au taasisi binafsi za ustawi wa jamii, hali mbaya ya kifedha, anasema nimevunja
Mahakama au mamlaka za kiutawala. mkataba kwa kutokumlipa na anakusudia
Sheria inatamka wazi kwamba mtoto kunishtaki. Ninawezaje kukabiliana na hili.
atakuwa na haki ya kuishi na wazazi wake Je sijamzidishia malipo?
au walezi na kwamba mtu hatazuia haki ya 29 Oktoba 2012
mtoto kuishi na wazazi wake, walezi au familia
na kukua katika mazingira salama isipokuwa Jibu letu litajikita kwenye utekelezaji
kama itaamliwa na Mahakama kwamba kwa wa mkataba ambao mliingia na siyo iwapo
kuishi na wazazi au familia (a) kutasababisha ukishtakiwa mke wako atajua na hasa
madhara kwa mtoto; (b) kutamfanya mtoto ndiyo sababu kubwa iliyokufanya uingie
apate manyanyaso makubwa; au (c) kutakiuka
makubaliano hayo. Inaonesha ulitishwa na
maslahi mapana ya mtoto. Kwa kuzingatia
ulikuwa kwenye hali ya uoga wakati unaingia
masharti ya kifungu hapo juu pale ambapo
mamlaka husika yenye uhalali au Mahakama kwenye makubaliano hayo. Haijalishi kama
imeamua kwa mujibu wa sheria na taratibu wanasheria wako walihusika. Haijalishi pia
husika kwamba ni kwa masilahi ya mtoto kama umemlipa miaka kadhaa nyuma.
kumtenganisha kutoka kwa wazazi wake, Maoni yetu ni kwamba mkataba huo ni
mtoto atapewa matunzo/hifadhi/malezi bora batili kwa sababu unaenda kinyume na sera
mbadala yaliyopo. ya umma na uliingiwa kwa uoga baada ya
Sheria pia inaeleza kwamba itakuwa ni kutishwa. Tukichukulia kwamba hujatuficha
wajibu wa mzazi, mlezi au mtu mwingine kitu, uwezekano wa mwanamke kushinda
yeyote anayemlea mtoto kumtunza mtoto ni mdogo sana. Kama akikushtaki na wewe
huyo na jukumu hilo linampa mtoto haki
ufungue shtaka kinzani dhidi yake ukidai pesa
ya chakula, malazi, mavazi, huduma ya afya
zote ulizomlipa kwa miaka yote ya mkataba. Ili
pamoja na kinga, elimu na muongozo, uhuru,
usije kuaibika, unaweza kufikiria kumJulaisha
na haki ya kucheza na kupumzika. Kutokana
na maelezo hayo, tuna shauri utoe taarifa kwa mkeo. Ila hilo ni hiari yako na pengine
afisa ustawi wa jamii wa eneo husika ili afanye unaweza kufikiria kuonana na mshauri wa
uchunguzi husika na kupeleka maombi ndoa kabla hujamuambia mkeo.
Mahakamani kwa maamuzi stahiki. Hakuna suala la kutosheleza kwa thamani,
kwani tunaamini kwamba makubaliano hayo
Nyumba-ndogo/Kimada anataka pesa yalikuwa ni batili tangu mwanzo. Hivyo,
yangu
Mahakama haitakwenda kwenye utoshelevu
Nilikuwa kwenye mahusiano kwa muda wa malipo.
24 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Ghiliba ya ndoa hivi sasa tumetengana na mimi ninaishi


kwenye moja wapo ya nyumba tulizojenga.
Nilikuwa na mpenzi kwa miaka minne Nimeshauriwa na rafiki yangu wa karibu
lakini baadaye tuligombana na kila kushtaki ili kupata talaka, mgawanyo wa
mmoja alikwenda njia yake kutokana na mali pamoja na matunzo ya watoto. Hata
tofauti kubwa tuliyokuwa nayo. Baadaye hivyo watu wengine wanasema sitapata
alipata ugonjwa wa akili na hivyo niliamua hata Shilingi kwa sababu hatukuwa na doa
kumtibia kwa sababu familia yake si rasmi. Tafadhali nishauri.
wakazi wa Dar. Baada ya kupona, nilijikuta
26 Novemba 2012
nimempenda tena, na kwa sababu hakuwa
na kumbukumbu za iwapo nilichosema Sheria ya Ndoa inatamka kwamba ikiwa
kilikuwa ni kweli ama la, akaendelea kuishi mwanamke na mwanamume wameishi
na mimi baada kumwambia kwamba pamoja kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili
tumeoana. Tumezaa watoto lakini sasa na kwa kipindi hicho wameishi kama mke
tumeanza tena matatizo. Siku moja baada na mume, kutakuwa na dhana inayoweza
ya mabishano nikamwambia ukweli na kukanushwa kwamba wameoana na hivyo
nikamfukuza nyumbani. Aliniripoti polisi na kama mume wako wa zamani hana ndoa
sasa nina kesi ya jinai. Inawezekanaje suala nyingine halali na jamii inayowazunguka
la mgogoro wa ndoa kama huu kuwa ni kesi
inawachukulia kama mke na mume, kanuni
ya jinai? Hivi polisi hawana kitu kingine cha
ya ndoa-dhahania itatumika kwenye kesi
kufanya?
yako. Unachotakiwa ni kuiridhisha Mahakama
19 Novemba 2012
yenye mamlaka kwamba mmekuwa kwenye
Suala lako ni la kipekee sana, amini mahusiano kwa zaidi ya miaka miwili, watu
usiamini, limeelezwa kwenye Kanuni ya walikuwa wanawachukulia kama mke na
Adhabu ambayo inatamka wazi kwamba mume na kwamba mlichuma mali hizo kwa
mtu yeyote ambaye kwa makusudi na pamoja.
kwa kulaghai anamfanya mwanamke yeyote Kwenye dhana ya ndoa-dhahania,
ambaye hakuolewa kihalali na yeye aamini mwanamke atachukuliwa kama mke halali
kwamba ameolewa naye kihalali na akakaa isipokuwa tu hataweza kupeleka maombi ya
naye kinyumba au akamwingilia mwanamke talaka au kutengana. Hivyo huwezi kupeleka
huyo huku akiamini kuwa ni mume wake maombi ya talaka au kutengana Mahakamani
amekosa na atawajibika kwa adhabu ya kwa sababu muunganiko wenu ulikuwa ni wa
kifungo cha miaka kumi. Tunakushauri upate kidhahania tu. Hata hivyo sheria inakupa haki
msaada wa kisheria kwa sababu suala lako ya kuomba matunzo kwa ajili yako na mtoto.
siyo jepesi kama unavyolifikria. Una haki pia ya kuomba malezi/matunzo ya
watoto mliowapata katika mahusiano yenu
Haki ya mwanamke kwenye ndoa- na nafuu nyinginezo, ikiwemo kugawana mali
dhahania mlizochuma pamoja. Tunakushauri uwasiliane
Sikuwahi kuwa na ndoa rasmi lakini niliishi na mwanasheria wako kwa mwongozo zaidi.
kwa furaha na mwanamume fulani kama Gari aina ya Mercedes-Benz S-Class kwa
mume wangu kwa miaka mitano hadi siku ajili ya mke
za hivi karibuni tulipoachana. Kipindi cha
uhusiano wetu tulizaa watoto watatu na Mimi ni mwanamke mlimbwende sana,
tulichuma mali kadhaa. Kwa masikitiko, wengi wananitamani. Wanawake wengi
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 25

wanapinga ukweli huu, lakini nitakueleza pande zote wakati wa ndoa walikua na imani
wazi kwamba niliamua kuolewa na mtu moja na ambapo kwa mujibu wa sheria za
tajiri. Kabla ya ndoa, aliahidi kuninunulia imani hiyo, kubadilisha dini kunafuta ndoa au
gari jipya aina ya Mercedes-Benz S-Class ni moja ya misingi ya kutengua ndoa.
la mwaka 2011, gari ambalo hajaninunulia Kutokana na maelezo hapo juu, ni
mpaka sasa. Anasema “amefulia”, ingawa dhahiri kwamba kukosa kwako Mercedes
najua sio kweli, pengine anatumia faida hakujitoshelezi kuingia kwenye vigezo
ya kuwa tayari ameshanioa kutokutimiza vilivyoainishwa hapo juu. Hakika
ahadi yake. Je, ninaweza kufungua madai kutokununuliwa Mercedes Benz hakuwezi
ya talaka kwa kuwa sitaki kuishi na kuchukuliwa kuwa ni ukatili. Ikiwa unaomba
mwanamume asiye mwaminifu? Naamini tu talaka kwa sababu ya kutokununuliwa
sheria inataka wanawake warembo kama Benz, tunadhani huenda usifanikiwe kupata
mimi kuhudumiwa vizuri. talaka hiyo. Tukudokezee tu kwamba katika
7 Januari 2013 nchi nyingine, tofauti na Tanzania, madai
Sheria ya Ndoa ya Tanzania inatoa vigezo ya talaka yanaweza kufunguliwa kwa idhini
ambavyo vinapaswa kuzingatiwa katika ya pande zote. Kwa Tanzania, hali ni tofauti
kudai talaka pale ambapo ndoa inapokuwa kwa kuwa hamuwezi kukubaliana kwenda
imevunjika bila uwezekano wa kurekebishika. Mahakamani kuomba talaka. Ni kweli Sheria
Sababu zifuatazo zimetolewa: (a) uzinzi ya Ndoa ipo nyuma ya wakati, lakini bado
uliofanywa na mmoja wa wanandoa, hasa inabaki kuwa ni sheria nzuri hata leo. Mwisho,
kama tendo la uzinzi limefanyika zaidi sheria haitofautishi wanawake wazuri na
wanawake wabaya - kwanza uzuri wa mtu
ya mara moja au kutokoma kwa tabia hii
upo machoni pa mtazamaji. Mwanasheria
licha ya kuonywa; (b) tabia ya uzinzi kwa
wako anaweza kukuongoza zaidi.
upande wa mlalamikiwa; (c) ukatili, uwe
wa kiakili au wa kimwili, unaosababishwa Harusi/Ndoa ya siri na kutokutoa taarifa
na mlalamikiwa kwa mlalamikaji au kwa
watoto; (d) kupuuzwa kwa makusudi kwa Ninataka kuoa lakini nataka harusi/ndoa ya
mlalamikiwa; (e) mlalamikiwa kumtelekeza faragha sana. Sitaki kuujuza umma kuhusu
mlalamikaji kwa kipindi cha angalau miaka nia yangu ya kutaka kuoa na sitaki mtu
mitatu, na Mahakama imethibitisha kwamba yeyote kuhudhuria ibada ya ndoa. Mimi
ni mtu msiri sana na hivyo ningependa
ni kwa makusudi; (f) kutengana kwa hiari au
kujua kama sheria za Tanzania zinaruhusu
kwa amri ya Mahakama, ambapo utengano
sherehe hizo.
huo umeendelea kwa angalau miaka mitatu;
7 Januari 2013
(g) kifungo cha maisha kwa mlalamikiwa au
kipindi kisichopungua miaka mitano, kwa Sheria ya Ndoa inatamka bayana
kuzingatia urefu wa muda wa kifungo na kwamba pale mwanamume na mwanamke
hali ya kosa ambalo alihukumiwa nalo; (h) wanapotaka kuoana, watatoa taarifa
ugonjwa wa akili kwa mlalamikiwa, ambapo angalau siku ishirini na moja kabla ya siku
angalau madaktari wawili, mmoja wao awe wanayopendekeza kufunga ndoa. Hata
aliyehitimu au awe na uzoefu wa ugonjwa wa hivyo, Msajili Mkuu anaweza, kwa leseni na
akili, kuwe na uhakikaa kuwa hakuna tumaini kwa fomu maalum, kuondoa sharti la utoaji
la kutibika au kupona kwa mlalamikiwa; (i) taarifa, kama inavyotakiwa chini ya sheria
kubadilisha dini kwa mlalamikiwa, ambapo ikiwa, tu, ameridhika kwamba watu hao
26 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

hawako kwenye mahusiano yaliyozuiliwa, wakati mwingine ajali, na wakati mwingine


hakuna kipingamizi cha ndoa nyingine, watu mizimu. Njozi nyingi si za kweli, hivyo ndivyo
hao hawako chini ya umri wa ndoa na ikiwa tunavyoamini. Unaweza kumpa faida ya
ni chini ya umri, basi idhini inayohitajika shaka na kujadili hili na mshauri wa ndoa.
imepatikana na Msajili Mkuu lazima Kwa vyovyote vile, katika maandalizi yako ya
ajiridhishe kwamba, kuna sababu nzuri, na za kudai talaka, ambayo unaonekana kusisitiza,
kutosha kufanya hivyo. unapaswa kushauriana na wanasheria wako.
Kwa hiyo inawezekana kuondokana na
suala la kutoa taarifa kama inavyotakiwa Ndoa ya jino la dhahabu
chini ya sheria iwapo tu umetimiza masharti Nilimuoa msichana ambaye nilimpa jino la
yanayotakiwa na pia Msajili Mkuu ameondoa dhahabu. Ili kuonesha upendo wetu, jino
sharti hilo la kutoa taarifa. Hata hivyo, sheria lake moja liliondolewa na kubadilishwa
iko wazi kwamba mtu yeyote anaweza ili kuweka jino la dhahabu. Wakwe zetu
kuhudhuria sherehe ya ndoa ya kiserikali, wameharibu ndoa yetu na tumekuwa na
hivyo hatuamini kama unaweza kuwa na ugomvi kila siku. Anataka talaka na nipo
sherehe ya ndoa binafsi; hata hivyo unaweza tayari kumpa lakini kwa sharti kwamba
kufanya harusi ya faragha na idadi ndogo ya anipe jino langu la dhahabu au alinunue
watu au unaweza kuamua kutokukaribisha kutoka kwangu. Unawezaje kunisaidia?
mtu yeyote kwenye harusi yako na kufurahia
1 Aprili 2013
wewe mwenyewe.
Jino ulilompatia ilikuwa ni kama zawadi
Mume anataja majina ya vimada wake
ya ndoa na harusi kwa mke wako na likawa ni
ndotoni
kama sehemu ya mali zake binafsi, na hivyo
Nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka 12 hivi hakuna uwezekano wa kurudishiwa. Hata
sasa na kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita kama unaweza, itamaanisha kuling’oa kutoka
nimekuwa na shaka kwamba mume kinywani mwa mkeo, kwa sababu kwa sasa
wangu amekuwa kwenye mahusiano na limeshakuwa sehemu ya mwili wake. Kuna
mwanamke fulani aliyekuwa akifanya mamia ya kesi za kigeni ambazo zimewahi
nae kazi huko nyuma. Imekuwa vigumu kuhoji iwapo jino la bandia ni sehemu ya
kuthibitisha hili na daima amekuwa mwili au la, na nyingi zake zimeamua kwamba
akikanusha. Wiki chache zilizopita, wakati jino bandia ni sehemu ya mwili wako baada
amechoka sana kutokana na safari ya ya kuwekwa.
ughaibuni, mume wangu alitamka jina la
Kwa kuzingatia hili, kuondolewa kwa jino
mwanamke karibu mara tatu hivi akiwa
ni kinyume na sera ya umma na tunaamini
usingizini. Nataka kudai talaka. Nifanye
hakuna uwezekano kwamba unaweza
nini?
kurudishiwa jino lako. Iwapo kama linaweza
4 Machi 2013
kuondolewa kwa urahisi, ulimpa kwa masharti
Sababu za kuomba talaka ni pamoja na gani, ikiwa ni pamoja na jino lake lililotolewa
ukatili na uzinzi ambazo husababisha ndoa (ikiwa utashinda kesi dhidi yake) na kadhalika.
kuvunjika pasipo kurekebishika. Kumtuhumu Yote kwa yote, inaonekana una kesi ngumu
tu mmeo kwa kutaja jina la mwanamke dhidi ya mkeo. Labda kama unaweza kumpa
mwingine usingizini siyo uzinzi. Ndoto ni punguzo na anaweza kununua, vinginevyo
ndoto - wakati mwingine upata njozi za kifo, itakuwa vita kubwa ya kisheria Mahakamani.
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 27

Ugomvi juu ya malezi ya watoto uhusiano ambao watu wanapaswa kuingia


kwa hiari yao wenyewe. Kwa hiyo sababu
Mimi ni mwanamke ninayeishi Dar es kwamba haujaolewa na baba wa mtoto wako
Salaam. Miaka miwili iliyopita nilizaa haitoshelezi kukunyima haki yako ya kumlea
mtoto wa kike ambaye baba yake mzazi
mwanao. Mwanasheria wako anaweza
ni mwalimu anayeishi Mwanza. Miezi
kukuongoza zaidi.
nane baada ya kumzaa mtoto huyu
nilisafiri nje ya nchi kibiashara. Nilimwacha Uthibitisho wa baba wa mtoto
mwanangu na bibi yake (mama wa baba
wa mtoto) anayeishi Morogoro. Baada ya Ninakabiliwa na hali isiyo ya kawaida
kurudi Tanzania nilikwenda kumchukua ambayo inaniondolea furaha yangu.
mtoto wangu lakini bibi amekataa kabisa Nimekuwa na uhusiano wa kimapenzi
kuniruhusu kumchukua mtoto wangu. Jibu na mwanamke mmoja kwa muda mrefu,
analonipa ni kwamba, kulingana na mila na baadaye alipata ujauzito. Kwa bahati
zao siwezi kuishi na mtoto mpaka niolewe. mbaya, alifariki wakati wa kujifungua.
Binafsi sina nia ya kuolewa kwa sababu Bahati nzuri mtoto alipona. Baada ya
huko nyuma niliwahi kuwa katika ndoa mazishi, mwanamume mwingine alijitokeza
mbaya. Nifanye nini? na kudai kuwa yeye ndiye baba halisi
8 Aprili 2013 wa mtoto na ule ujauzito wa marehemu
ulikuwa ni wake. Ninaamini mimi ndiye
Kisheria mtoto ana haki ya kuishi na nilikuwa mwanamume pekee kwake,
wazazi wake. Haki hii imetolewa wazi chini ya na ndiye pekee niliyekuwepo wakati
Sheria ya Mtoto, Na. 21 ya 2009. Vivyo hivyo, akijifungua. Kila mmoja wetu anadai
kama mzazi pia una haki ya kumlea mwanao. kuwa ndiye baba, na ninaamini huyu
Ikiwa bibi hataki kukuruhusu kumchukua mwanamume aliyejitokeza amepandikizwa
mtoto wako tunakushauri kupeleka maombi tu. Je, sheria inasemaje kwenye hali kama
Mahakamani ili kupata malezi ya mtoto. Chini hiyo? Vipi kuhusu gharama nilizotoa wakati
ya Sheria ya Mtoto kuna dhana inayoweza wa ujauzito, ninawezaje kurudishiwa
kubatilishwa kwamba inafaa mtoto aliye gharama zangu iwapo itabainika kuwa
chini ya umri wa miaka saba kulelewa na mtoto siyo wangu? Ninaweza kuruhusiwa
mama yake, ili kuamua iwapo dhana hiyo kumtunza mtoto?
itumike kwenye mazingira fulani, itategemea 13 Mei 2013
na maelezo ya kesi husika lakini Mahakama Masuala yanayohusu baba mzazi na
itazingatia haja ya kutokumsumbua mtoto matunzo ya watoto yanashughulikiwa na
kwa kubadilisha mlezi. Sheria ya Mtoto, Na. 21 ya 2009. Sheria hii
Kwa kuwa hakuna mazingira ya usumbufu inatoa fursa kwa mtoto, mzazi, mlezi, afisa
huo kwa malezi bora ya mwanao, tunadhani ustawi wa jamii au mtu yeyote mwenye
Mahakama itatumia dhana hiyo na kuamuru maslahi na mtoto, kwa ruhusa maalum ya
mtoto alelewe na mama yake. Mila ambazo Mahakama, kupeleka maombi mahakamani
bibi yake anazizungumzia hazipaswi kukuzuia ili kuthibitisha baba wa mtoto.
kumlea mtoto wako. Unabaki kuwa mama Sheria hii pia inaeleza namna ambavyo
mzazi wa mtoto labda kama kuna sababu maombi haya yanatakiwa kufanywa.
nyingine ambazo hujatushirikisha, unastahili Inaruhusu maombi hayo kufanyika kabla
kupata matunzo ya mtoto (kutoka kwa mtoto hajazaliwa, baada ya kifo cha baba
baba). Zaidi ya hayo, ndoa kama taasisi ni au mama wa mtoto, kabla mtoto hajafikia
28 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

umri wa miaka 18, au kwa ruksa maalum ya huku nikimwambia Msajili tatizo lililopo.
Mahakama, baada ya mtoto kufikisha umri wa Nina maswali mawili; moja inawezekana
miaka 18. mwanamke mzee kama yule akamrubuni
Kuhusu kurudishiwa gharama za wakati mtoto huyu wa miaka 20? Mbili, kwa kuwa
wa ujauzito, na mama wa mtoto akiwa hati zilichanwa na hivyo hakuna ushahidi
amekwishafariki, hatuna uhakika utamshtaki wa ndoa, je ndoa hii bado ni halali?
nani ili akurudishie gharama hizo. Hakuna 24 Juni 2013
uwezekano wa shtaka lako kufanikiwa dhidi
Kwa kuanzia, mwanao yupo juu ya umri
ya baba halisi wa mtoto, lakini wanasheria
wa kisheria wa kuoa, hivyo wewe ujue au
wako wanaweza kukuongoza zaidi.
usijue, bado yeye anaweza kuoa. Hata hivyo,
Swali kuhusu malezi ya mtoto linahitaji
tunaelewa hisia zako kwamba kwa umri wake
umakini zaidi. Lengo kuu la sheria ni
anaweza kuwa bado ni mdogo na hasa kuwa
kuhakikisha kwamba maslahi bora ya mtoto
katika ndoa na mwanamke ambaye amemzidi
yanazingatiwa. Kama mtoto ni wa kwako
sana umri. Ndoa ilifanyika pale walipokwenda
kweli, uwezekano ni mkubwa wa kuruhusiwa
kwa Msajili na kusaini hati zilizowekwa mbele
kumlea mtoto, baada ya kuzingatia uwezo
wako wa kumtunza na kumlea, uwezo wa yao na tunachukulia hati hizo zilishuhudiwa
kifedha, n.k. vyema. Inaonekana hilo lilifanyika hivyo
Inafahamika kwamba mtoto anaweza wakati unaingia chumbani, mwanao alikuwa
kulelewa vizuri zaidi na mwanamke kuliko tayari ameshaoa. Kuchana tu hati za ndoa
mwanamume. Hivyo, uwepo wa mama yako hakumaanishi kwamba ndoa imebatilishwa
au mwanamke mwingine kwenye familia au haikufungwa. Ndoa bado ipo na namna
yako mwenye uwezo wa kutoa mwongozo pekee mwanao anaweza kutoka kwenye ndoa
wa malezi au msaada stahiki, itasaidia sana hiyo ni kufungua talaka. Hivyo kama mwanao
iwapo kutakuwa na mgogoro juu ya malezi ya atatoa au anahitaji talaka ni uamuzi wake
mtoto. na siyo wako. Wanasheria wako wanaweza
kukuongoza zaidi.
Kuchanwa kwa hati za ndoa
Hadhi ya ndoa ya kimila
Bila mimi kujua, mwanangu wa kiume
wa miaka 20 alikuwa anatembea na Mimi na mchumba wangu ni wakristo
mwanamke ambaye anamzidi kama miaka lakini mchumba wangu anataka kwanza
15 hivi. Mwanamke huyo alifanikiwa tufunge ndoa ya kitamaduni kabla ya
kumshawishi mwanangu amuoe na ndoa ya kanisani. Je, hilo linawezekana?
walikwenda kufunga ndoa ya Serikali jijini Madhara yake ni yapi? Je, ndoa ya kimila
Dar es Salaam. Kwa bahati nzuri, dreva inatambulika Tanzania?
wangu ambaye nimekuwa nae kwa miaka 1 Julai 2013
30, ndiye aliyemwendesha mwanangu
mpaka sehemu ambayo walitakiwa kusaini Sheria ya Ndoa inatambua ndoa za
hati za ndoa. Alihisi kuna kitu hakiendi kimila, kidini na kiserikali. Ndoa za kimila
sawa na hivyo akanipigia simu. Kwa haraka ndiyo hizo unazoziita ndoa za kitamaduni;
nilikwenda na kuingia kwenye ofisi ambayo ndoa za kidini ni zile zinazofungwa kidini,
zoezi la kutia saini lilikuwa likifanyika na yaani, kiislamu, kikristo, kihindi n.k. Ndoa za
sikuamini kumbe walikuwa wameshasaini. kiserikali ni zile zinazofungwa na maafisa wa
Nilichukua hati zile na kuzichanachana Serikali walioruhusiwa. Tanzana inatambua
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 29

ndoa za kimila na zina hadhi sawa na ndoa kwamba taarifa hizo ni za siri na hawawezi
nyingine zozote yaani, za kiserikali na kidini. kuzidukua/kuzivujisha kwangu. Ninawezaje
Unatakiwa kufahamu kwamba ndoa za kupata taarifa hizo kutoka kampuni ya
kimila zinachukuliwa kama ni ndoa za wake simu? Tafadhali elewa, ninahitaji kuzipata
wengi na hivyo anaweza kuoa mke zaidi bila yeye kujua. Napenda kuuliza pia, je
ya mmoja na hivyo hivyo wewe unaweza kupiga busu ni uzinzi? Je, inawezekana mtu
usiwe mke pekee. Sheria ya Ndoa inatamka anayezini na mke wangu kuunganishwa
kwamba ndoa iliyofungwa Tanganyika kwenye kesi ya talaka?
(Tanzania Bara) inaweza kubadilishwa, kama 16 Septemba 2013
mwanamume alikuwa na mke mmoja, kutoka
Kanuni za Mawasiliano (Ulinzi kwa
ndoa ya mke mmoja kwenda wake wengi,
Mtumiaji) zinatamka mwenye leseni
kwa tamko maalum lililotolewa na mume na
kutofuatilia wala kutoa maudhui ya taarifa
mke, kwamba wote kwa hiari yao wenyewe
zozote za mteja zinazopitia kwenye
wamekubali mabadiliko hayo. Tamko hilo
mfumo uliopewa leseni, isipokuwa kama
litatolewa mbele ya Jaji, Hakimu Mkazi au
inavyotakiwa na kuruhusiwa na sheria
Hakimu wa Wilaya na litakuwa la maandishi,
litasainiwa na mke na mume na mbele ya mtu inayotumika. Hivyo kampuni ya simu ipo
anayeshuhudia wakati wa kulitoa. sahihi kukuzuia kupata kumbukumbu za
Unatakiwa uelewe kwamba, hakuna ndoa simu za mke wako.
inayoweza kubadilishwa, kutoka mke mmoja Unatakiwa pia kuelewa kwamba haki ya
kwenda wake wengi na kutoka wake wengi faragha inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya
kwenda mke mmoja kwa namna nyingine Muungano wa Tanzania. Kisheria, kampuni
zaidi ya njia ya tamko kama ilivyoelezwa hapo za mawasiliano zitawajibika kutoa taarifa hizo
juu. Hivyo kama mtaoana kwa ndoa ya kimila, kama mwenye namba ataziomba au kwa
ni lazima muibadilishe kuwa ndoa ya mke amri ya Mahakama yenye mamlaka husika
mmoja kwanza ndipo muendelee kuoana au kama polisi wanazihitaji kwa malengo ya
kanisani isipokuwa kwamba mmeo hatakiwi kiuchunguzi.
kuwa na mke mwingine kwa sababu kubadili Kama unaona ni lazima kwako kuthibitisha
kwenda ndoa ya mke mmoja hakutakuwa iwapo mke wako ni mwaminifu au siyo,
halali kama mmeo atakuwa na mke zaidi tunakushauri uwasiliane na mkeo ili aiombe
ya mmoja. Kama mtaoana kwa ndoa ya kampuni ya mawasiliano impatie taarifa
kikristo wakati ana mke mwingine, ndoa ya zake za mawasiliano ambazo unaweza
kikristo haitakuwa halali kwa sababu ndoa kuziangalia, vinginevyo, hakuna uwezekano
ya kimila itakuwa juu ya ndoa ya kikristo. kwamba Mahakama itatoa amri hiyo kwa
Tunapendekeza umuulize kwa nini anataka sababu za udanganyifu pekee. Maelezo yako
kwanza ndoa ya kimila. Pia tunashauri nyote yanayofuata ni kwamba mke wako ambaye
mumtafute mtaalam wa masuala ya ndoa. siyo mwaminifu (au mume kwa maana hiyo)
hatoi ushirikiano kwa mwenzi wake. Hilo ni
Kupata taarifa za simu kweli na kwa bahati mbaya mke na mume
Nadhani mke wangu anafanya udanganyifu wanachukuliwa tofauti pale linapokuja suala
kwa sababu wakati wote ametingwa sana la faragha.
na simu yake. Nilijaribu kupata meseji na Kuhusu swali lako la pili, iwapo kubusu
historia ya miito kutoka kampuni ya simu ni uzinzi. Kwa bahati nzuri au mbaya,
anayotumia lakini walikataa kwa sababu uzinzi haujafafanuliwa kwenye Sheria ya
30 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Ndoa ya Tanzania. Kupiga busu nako pia Ni kweli Sheria ya Ndoa ya Tanzania
hakujafafanuliwa kwa sababu unaweza kuwa imepitwa na wakati na hairuhusu talaka ya
na busu la mdomo, shavuni na aina nyingine maridhiano. Sheria inataka kwamba ni lazima
za busu, na baadhi yake zinategemea na aina kuwe na sababu, miongoni mwazo ni , uzinzi,
ya mila na desturi za mahala ambapo mtu tabia za kingono zisizokubalika n.k. ili uwe na
anaishi. Wakati mwingine zinaweza kuwa kitu sababu halali za kuomba talaka. Muonekano
cha kawaida bila kuchukuliwa kama ni uzinzi. au mabadiliko ya muonekano, kama ilivyo
Kwa mfano pale busu la mdomo linapochukua kwa kesi yako hapa, siyo sababu ya msingi ya
muda mrefu kidogo inaweza kuchukuliwa ni kuomba talaka na haiwezi kutolewa chini ya
dalili za wazi kwamba mahusiano ya kiuzinzi
sheria zetu.
yapo, wakati busu la shavu ni la kawaida
Kwa kuwa ndoa yako ipo chini ya miaka
siku hizi. Ni ngumu kukujibu swali lako bila
miwili, isipokuwa kama unaweza kuthibitisha
kujua aina ya busu, muda, mara ngapi, watu
ugumu wa kipekee, sheria inazuia talaka
wanaohusika n.k. Mara nyingi, ngono ya aina
yoyote huchuliwa kama uzinzi. ndani ya muda huo. Kuna kama kipindi cha
Mwisho, ni iwapo mtu anayehisiwa kupoa/mpito ambacho, kwa miaka ya sasa,
kutembea na mkeo anaweza kuunganishwa kimsingi kimepitwa na wakati.
kwenye maombi ya talaka, jibu ni ndiyo lakini Ziko juhudi za kubadilisha sheria yetu
kwa maelekezo ya Mahakama husika unaweza ya ndoa lakini kwa sasa huo ndiyo ukweli.
kumuunganisha mtu huyo kama mdaiwa Tunakushauri uwasiliane na mshauri wa ndoa
mwenza. Unaweza pia kudai fidia kutoka ili aweze kuzungumza na nyote wawili juu ya
kwa mtu huyo. Tunakushauri uwasiliane na jambo hili. Tunakutakia kila la heri.
mwanasheria wako kwa mwongozo zaidi.
Picha za harusi magazetini
Mume anafuga ndevu na kuvaa hereni
Mimi ni mtu maarufu sana na nilifunga ndoa
mbili
na kufanya harusi ya kifahari. Wakati wa
Nimeolewa na mwanamume ambaye harusi, baadhi ya mapaparazi/wapiga picha
nimekuwa kwenye mahusiano naye kwa walijipenyeza na kunipiga picha. Nilitokea
zaidi ya miaka kumi. Tulioana mwaka kwenye magazeti yote makubwa/maarufu
jana na ghafla ameamua kufuga ndefu na sasa mpenzi wangu/kimada amekasirika
na kuvaa hereni mbili, kitendo ambacho kuhusu ndoa yangu na mwanamke huyu
kinamwondolea mvuto na hivyo mpya. Je, mnaweza kunisaidia? Ninaweza
kunikera. Mwanzoni nilidhani ni utani, kuwashtaki wenye magazeti?
sasa chaguo liko wazi kati ya ndevu zake 10 Machi 2014
na talaka. Jambo hili ni la kushangaza
lakini ndiyo ukweli wenyewe. Nimekubali Hatujui ni msaada gani unahitaji kutoka
matokeo na sitaki kuendelea tena. Hata kwetu. Kinachotuchanganya zaidi ni kwamba
hivyo mwanasheria wangu anasema umeoa na bado unaendeleza mahusiano na
kupata talaka kwa sasa na kwa sababu mpenzi wako/kimada, ikiwa na maana kuwa
hizo haiwezekani. Hata hivyo, huyu ni una mahusiano ya kizinzi nje ya ndoa. Bila
mwanasheria yule yule ambaye mume kujali kama wewe ni maarufu na kama hujui,
wangu anamtumia na anaweza kuwa na uzinzi ni sababu mojawapo ya talaka na
maslahi binafsi. Je, ushauri wa mwanasheria anayepaswa kukasirika ni mke wako na siyo
huyu ni wa kweli? Tafadhali niongoze. mpenzi wako. Unatakiwa kukumbuka kiapo
9 Desemba 2013 chako kwenye ndoa na unahitaji kuonana
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 31

na mshauri wa masuala ya ndoa na siyo ukumbi wa mkutano, Skype au kutuma


wanasheria. karatasi zako. Ndoa ni tendo takatifu na
Kuhusu wapiga picha/mapaparazi, kwa Sheria ya Ndoa inaeleza kwa uwazi kwamba
taarifa chache tulizonazo kukuhusu, hatujui ni lazima uwepo na inatamka kwamba
iwapo umekashfiwa au haki yako ya faragha ndoa itakuwa batili iwapo pande zote mbili
imeingiliwa. Inavyoonesha, lalamiko lako hazitakuwepo zenyewe wakati wa ndoa.
kubwa ni kwamba mpenzi wako hana furaha Hatujawahi kusikia nchi inayoruhusu ndoa ya
na ndoa yako hiyo, jambo ambalo halikupi uwakilishi au masafa marefu.
haki ya kuwashtaki wenye magazeti. Vile vile Kuhusu kaka yako kuhudhuria ndoa,
unadai kwamba wewe ni maarufu na kama tafadhali elewa kwamba huwezi kumpa kaka
ni kweli wewe ni maarufu kama unavyofikiria yako hati ya uwakilishi kusaini vyeti vya ndoa.
pia itakuwa ni ngumu kwako kuwashtaki Kwa jinsi tunavyojua, iwapo atasaini, ataishia
wenye magazeti kwa shtaka la kukashfu. kuwa mume wa mchumba/mpenzi wako.
Watu maarufu wapo kwenye macho ya umma Hata hivyo, wanasheria wako wanaweza
na ni lazima utegemee mambo kama haya kukuongoza zaidi.
kutokea. Tunakushauri uwasiliane na mshauri
wa ndoa na pengine Mchungaji. Unahitaji
Uhanithi na ndoa
kuelewa maana hasa ya kuwa kwenye ndoa. Niliolewa na mwanamume kwa ndoa
Wanasheria wanaweza wasiwe na msaada ya kutafutiwa mume, lakini nimekuja
mkubwa katika hili lakini unaweza kuwajaribu kung’amua kwamba ni hanithi. Ingawa
pia. ninatamani sana kumsaidia, lakini jambo
hili haliwezekani kwa sababu hali yake
Kumwakilisha mtu kwenye ndoa haitibiki. Je, ndoa hii inaweza kusimama/
Mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi na kuendelea?
ninafanya kazi kwenye kampuni kubwa 24 Machi 2014
sana nje ya Tanzania. Mchumba wangu
Kwa ujumla uhanithi ni hali ya kimwili
anasisitiza tuoane chini ya sheria za
au kisaikolojia ambayo inamfanya mwenza
Tanzania, kwangu ni vigumu sana kupata
muda huo. Ninaweza kujaza fomu zangu kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Hata
za ndoa na kuzituma kwa Msajili Jijini Dar hivyo, kukataa kufanya mapenzi na mwenzi
es Salaam na hivyo kutufungisha ndoa? wako siyo uhanithi, wala kushindwa kuzaa pia
Ninajua nchi nyingine zinaruhusu aina hizo siyo uhanithi.
za ndoa ambapo huhitaji kuwepo moja kwa Kwa ujumla, iwapo utapeleka maombi ya
moja. Katika namna nyingine, je kaka yangu talaka dhidi ya mpenzi wako kwa sababu za
anaweza kuhudhuria na kusaini cheti cha uhanithi, utahitaji kuthibitisha. Jambo hilo
ndoa kwa niaba yangu kwa kutumia hati litakutaka uiombe Mahakama kumlazimisha
ya uwakilishi. Ninawezaje kuoa bila kufika mwenzi wako kufanyiwa uchunguzi wa
Tanzania?
kimwili na kisaikolojia na wataalamu wa afya
24 Machi 2014
waje kuthibitisha. Kifungu cha 39 cha Sheria
Ingawa tunafurahi kwamba una shughuli ya Ndoa nchini Tanzania kinatamka kwamba
nyingi na unafanya kazi kwenye kampuni kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 97 na
kubwa, ni lazima uwepo kwenye chumba cha 98, ndoa itakuwa batili iwapo: (a) wakati wa/
kusaini vyeti vya ndoa. Huwezi kuwa kwenye baada ya ndoa (i) upande wowote kushindwa
32 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

kushiriki tendo la ndoa; au (ii) upande Kifungu cha 20 cha Sheria ya Ndoa
wowote unaugua ugonjwa wa akili au kifafa; kinazungumzia hali kama yako. Kifungu hicho
au (iii) mmoja wa wanandoa kudhihirika kinatamka kwamba iwapo mwanamume
kuwa alikuwa na ugonjwa wa zinaa; au aliyefunga ndoa ya wake wengi/mitala
(iv) mwanamke kudhihirika kuwa alikuwa anatoa tangazo la kusudio la kufunga ndoa,
na mimba ya mwanamume mwingine; mke wake, au kama ana mke zaidi ya mmoja,
au (b) mwanandoa mmoja kukataa kwa yeyote kati ya wake zake anaweza kuweka
makusudi kushiriki tendo la ndoa tangu ndoa pingamizi kwa Msajili au afisa msajili ambaye
ilipofungwa; au (c) mwanamke hajatimiza tangazo la kufunga ndoa limetolewa kwa
misingi kwamba kwa kuzingatia hali ya kipato
umri wa miaka 18 na ridhaa iliyotakiwa
cha mume, kuoa mke mwingine kunaweza
kutolewa chini ya kifungu cha 17 haijatolewa
kupelekea ugumu wa maisha usiomithilika
na Mahakama inaona kuna sababu nzuri za
kwa mke au wake zake wa sasa na watoto
kutengua ndoa. Kifungu cha 40, ndoa batilifu
kama wapo; au mwanamke anayekusudia
itaendelea kuwa ndoa halali hadi hapo
kumuoa ni mwenye tabia mbaya au anaugua
Mahakama itakapoitengua. magonjwa ya kuambukiza au ya zinaa au
Kutokana na maelezo hapo juu, anaweza kuleta ugomvi/kutoweka utulivu.
unaweza kuona kwamba kwa kuwa mume Mara pingamizi linapotolewa kwa Msajili au
ameshindwa kushiriki tendo la ndoa, ndoa afisa msajili, ndoa hiyo haitafungwa mpaka
itakuwa batilifu, yaani, inaweza kutenguliwa pingamizi hilo litakapoamuliwa na Baraza la
na hivyo unaweza kuomba talaka. Sheria Usuluhishi wa Ndoa.
haisemi kwamba ndoa hiyo ni batili, yaani Tunashauri wewe na mke mwenzio
haipo tokea mwanzo, ikiwa na maana kufuata njia iliyoelezwa hapo juu. Hili pia
kwamba huwezi kuomba talaka. Wanasheria linaweza kutatuliwa na wazee kwenye ukoo
wako wanaweza kukuongoza zaidi. wako. Vinginevyo unaweza kuwasiliana na
mshauri wa masuala ya sheria za familia kwa
Kukataa kuongeza mke mwingine hatua stahiki.
katika ndoa ya mitala
Ndoa za jinsia moja nchini Tanzania
Mimi ni mmoja wa wake wawili wa
mwanamume fulani. Mume anatutegemea Tumefunga ndoa ya jinsia moja na tunataka
sana ili kuweza kuishi. Mimi mwenyewe kutembelea Tanzania wakati wa siku za
nafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya familia mapumziko. Ninataka kujua, je ndoa za
yetu. Cha kushangaza, mume wetu anataka jinsia moja zinaruhusiwa nchini Tazania?
kuongeza mke mwingine. Tumemkatalia 31 Machi 2014
lakini anasisitiza kwamba sisi sote
tumeolewa kwenye ndoa ya mitala na Ndoa za jinsia moja haziruhusiwi
hivyo hatuwezi kumzuia. Nina hofu juu ya kabisa nchini Tanzania. Sheria ya Ndoa
ndoa yake mpya kwa sababu mwanamke inatambua ndoa kama ni muunganiko
anayetaka kumuoa afya yake inatiliwa wa mwanamke na mwanamume na siyo
mashaka. Tumetonywa kwamba tangazo mwanamume na mwanamume mwingine.
la kusudio la kufunga ndoa limeshatolewa Jambo hilo pia ni geni kwenye tamaduni
kwenye ofisi ya Msajili. Je, kuna namna ya za kitanzania na linachukuliwa kuwa ni
kuepuka au kuzuia ndoa hii? utovu/ukosefu wa maadili. Mahusiano kama
31 Machi 2014 hayo ya mwanamume na mwanamume
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 33

yanaadhibiwa vikali chini ya Sheria ya Kanuni nyumba yangu. Hata hivyo, benki inataka
ya Adhabu. ridhaa ya mke wangu na haitaki kuelewa
Ingawa hauzuiliwi kuja nchini Tanzania, kwamba mimi na mke wangu tumetengana.
lakini tunakushauri kuwa makini na tabia Nahitaji sana mkopo huu. Nifanye nini?
na vitendo vyako. Unaweza kuwasiliana na 12 Mei 2014
mwanasheria wako kuhusu nini cha kufanya
Sheria ya Ndoa inatambua kwamba
na cha kutokufanya.
ingawa mali inaweza kuwa kwa jina la
Akaunti ya pamoja ya mke na mume mwenza mmoja, mwenza mwingine anaweza
kuwa na mchango katika kupatikana,
Mimi na mume wangu tumefungua akaunti kusimamia na/au kulinda mali hiyo ingawa
ya pamoja benki Jijini Dar. Mimi pekee maslahi yake kwenye mali hiyo yanaweza
ndiye ninayefanya kazi kwenye familia yasiwe yamesajiliwa. Kuna kesi moja maarufu
na mume wangu hafanyi kazi yoyote na ambapo Mahakama ilikuwa na maoni
anatumia muda wake mwingi kuangalia
kwamba hata kazi za ndani/nyumbani
televisheni. Kwa bahati mbaya nimekuwa
zinazofanywa na mke zinachukuliwa/
nikiweka fedha kwenye akaunti ya pamoja
zinahesabika kama mchango wake katika
kwa muda wa miaka 7 na sasa ninahitaji
kupatikana na kusimamia mali ya familia.
kuchukua fedha zangu. Mume wangu
Sheria ya Ardhi inazitaka taasisi za fedha
anakataa kusaini fomu ya kuchukua fedha
kupata ridhaa ya mwenza kabla ya kukubali
iwapo sitampatia nusu ya fedha hizo. Benki
haitaki kutoa fedha kwangu peke yangu. mali ya ndoa kuwa dhamana ili kulinda
Ninaweza kuishtaki benki? maslahi ya mwenza mwingine. Sheria ya Ndoa
inatambua kwamba wanandoa wanaweza
21 Aprili 2014
kuwa wametengana, ama kwa amri ya
Upo kwenye hali tatanishi sana. Umeweka Mahakama au kwa hiari yao wenyewe. Hata
fedha zako ulizozipata kwa shida kwenye hivyo, kutengana siyo kuachana na wakati
akaunti ya pamoja. Kisheria, akaunti ya wanandoa wanapokuwa wametengana,
pamoja ni deni la wamiliki wote wa akaunti hakuna mgawanyo wa mali unaofanyika,
ya pamoja. Kuna kesi moja iliwahi kuamuliwa ikiwa na maana kwamba, haki za mke wako,
kwamba sababu tu kwamba mmoja wa kama zipo, kwenye nyumba yenu bado zipo.
wamiliki wa akaunti hachangii hakumzuii mtu Isipokuwa kama umepata talaka, hakuna
huyo kunufaika. Benki ipo sahihi kwamba namna yoyote halali ya kutatua jambo hili
fedha zinamilikiwa kwa pamoja na haziwezi isipokuwa kwa kumtafuta mke wako na
kutolewa kwako peke yako. Hatuoni namna kupata ridhaa yake kwa ajili ya kuweka
ya kufanikiwa iwapo utaishtaki benki. Hata dhamana nyumba yako. Kama hana maslahi
hivyo unaweza kuwasiliana na wanasheria yoyote kwenye mali, hatuoni kwa nini akatae
wako kwa mwongozo zaidi. kutoa ridhaa. Namna nyingine ni kutafuta
dhamana nyingine kama vile mali binafsi au
Idhini ya mwenza wakati wa kutengana dhamana ya mtu mwingine. Mwanasheria
Nilikwenda benki kuomba mkopo na wako anaweza kukuongoza zaidi.
niliulizwa iwapo nimeoa. Niliwaarifu Daktari anaruhusu uzinzi
nimeona lakini tumetengana kwa miaka
minne sasa. Benki ilikubali kunipa mkopo Daktari wangu anasema kwamba nina
kwa sharti kwamba niweke dhamana moyo dhaifu na kwamba ili afya yangu
34 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

iimarike (hasa moyo wangu), ninahitaji Mume kupewa uraia wa kurithisha/


kushiriki mapenzi na mwanamke mwingine, kuhamisha
ingawa nipo kwenye ndoa ya mke mmoja.
Daktari anasema hii itaniongeza maisha Mimi ni mwanamke Mtanzania ambaye
marefu. Si haki yangu ya kufanya mapenzi nimeolewa na mwanamume wa nje na
na mwanamke mwingine ambayo tumekubaliana kuishi na kuanzisha familia
itapelekea kuimarisha kwa afya yangu yetu nchini Tanzania. Hata hivyo, inanikera
inalindwa na Katiba? Nimesikia Sheria ya kwa sababu mume wangu anatakiwa
Ndoa inakataza uzinzi lakini inawezekanaje kuomba na kupata kibali cha ukaazi
Sheria ya Ndoa ikiuke Katiba ya nchi? Je, kutoka Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania.
hakuna upekee kwenye uzinzi? Amejaribu kuomba uraia kupitia uraia
wangu lakini imekuwa ni ngumu kutokana
2 Juni 2014
na sababu nisizozijua. Kuomba na kupata
Unaonekana kuchukulia kwamba daktari kibali cha ukaazi imekuwa ni kama jinamizi
wako amekuruhusu kufanya mapenzi na kwa kuwa hatuwezi kuishi siku zote
mwanamke mwingine ili kuendelea kuwa tukiomba kibali. Tafadhali tushauri hatua za
kufuata ili aweze kupata uraia wa Tanzania
na afya nzuri. Tuna mashaka sana na daktari
kupitia ndoa yetu.
uliyemuona na unaweza kupata ushauri
28 Julai 2014
zaidi kwingine. Ingawa sisi siyo madaktari,
hii ni mara yetu ya kwanza kusikia kwamba Sheria inayozungumzia uraia nchini
mapenzi nje ya ndoa yanaweza kuimarisha Tanzania ni Sheria ya Uraia ya mwaka 1995
moyo wako. Kimsingi, kwa elimu ndogo ambayo inatamka kwamba mwanamke
tuliyonayo kuhusu moyo, tuna uhakika aliyeolewa na mwanamume raia wa Jamhuri
kwamba kama utazidisha mapenzi ya nje ya Muungano, wakati wowote wa uhai wa
ya ndoa, unaweza kupata ugonjwa wa mume wake atakuwa na haki, baada ya
shambulio la moyo. kufanya maombi kwenye fomu maalum, ya
Sheria haizungumzi mapenzi kwa namna kurithishwa uraia wa Jamhuri ya Muungano.
uliyosema. Kwa kuwa umekubali mwenyewe Kutokana na kifungu hiki, ni mwanamume
kwamba wewe upo kwenye mahusiano ya ndiye anayeweza ‘kuhamisha’ uraia wa
mwanamke mgeni.
mke mmoja, hauwezi kurudi na dawa mpya
Kwa bahati mbaya Sheria ya Uraia haina
ya kufanya mapenzi nje ya ndoa yako. Haki
kifungu kama hicho kwa mwanamke
zako za kikatiba zinalindwa, ziko juu ya
Mtanzania aliyeolewa na mwanamume wa
sheria nyingine zote za nchi, lakini tafsiri yako
kigeni. Hii ni bahati mbaya sana na mtu
kinadharia na kisheria haipo sahihi.
mwingine anaweza kusema ni ubaguzi dhidi
Tuna uhakika mke wako pia hawezi ya wanawake.
kukubali matibabu kama hayo, kama Mume wako anaweza kuomba uraia (wa
ambavyo wewe hutakubali ushauri wa aina kujiandikisha/tajnisi) lakini ni lazima afanye
hiyo kutoka kwa daktari wake. Tunakusihi sana hivyo kama mhamiaji mwingine anayetaka
upate ushauri mwingine na umuone mshauri kupata uraia wa Tanzania kwa kuwa na sifa
wa ndoa. Kuna mahali kitu hakijaenda sawa. zilizoelezwa kwenye sheria kama ifuatavyo: (a)
Na mwisho ni kweli, kama utafuata njia ya awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano
daktari wako, mke wako atakuwa na haki zote miezi kumi na mbili mfululizo kabla ya tarehe
za kukupa talaka. ya maombi; na (b) kwa kipindi cha miaka kumi
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 35

kabla ya miezi 12 ya maombi awe ameishi Kuhusu talaka, Sheria ya Ndoa hairuhusu
ndani Jamhuri ya Muungano kwa muda talaka bila sababu za msingi. Kwa bahati
ambao ni wastani wa miaka isiyopungua mbaya kupoteza kwako mvuto wa mapenzi
saba; na (c) anajua vizuri lugha ya Kiswahili au kwa mume wako siyo moja ya sababu
Kiingereza; na (d) ni mtu mwenye tabia nzuri; iliyoelezwa na sheria. Kunenepa na kuzeeka
(c) kwa kuzingatia historia yake, anaonesha siyo sababu za kuzitumia pia. Kama ingekuwa
kuwa na nafasi ya kuwa na mchango mkubwa ni uzinzi, kushindwa kufanya mapenzi/ngono
kwa maendeleo ya taifa katika nyanja ya au ukatili, hapo sheria ingekuruhusu kuomba
uchumi na sayansi. talaka. Tunakushauri kuwasiliana na mshauri
wa ndoa ili kuokoa ndoa yako.
Kupoteza mvuto wa mapenzi Unatakiwa kufikiri zaidi hatua zako kwa
Niliolewa na mwanamume mwenye mvuto sababu inawezekana wakati huu ndiyo
kwa kadri mwanamume anatakiwa kuwa. mume wako anakuhitaji zaidi kuliko wakati
Kwa bahati mbaya benki anayofanyia kazi mwingine wowote. Isije kuonekana kama
inamfanyisha kazi mpaka usiku sana, eti tunahubiri, usisahahu viapo vyenu vya ndoa,
vitabu vya benki vinatakiwa kufungwa ndo na usisahahu pia kwamba hata wanawake
aondoke. Hivi sasa mume wangu ana kilo nao mara nyingi wanaongezeka uzito.
zaidi ya 150, mara mbili ya uzito wa awali,
na hanivutii tena. Nimepoteza mvuto wa Mume analazimisha kumpa mtoto jina
mapenzi naye. Ninawezaje kumpa talaka Mimi nimeolewa na ninaishi Dar. Mimi na
haraka mume wangu kwa sababu simuoni mume wangu ni wasomi na tunafanya
akipungua uzito? Amejaribu mara nyingi kazi Serikalini. Mungu ametubariki kupata
lakini ameshindwa. Benki inapata faida watoto watatu na hivi karibuni tunatarajia
kubwa, mume wangu hapati kitu, wakati mtoto wetu wa nne, kwa kuwa ni mjamzito.
wafanyakazi wengine wa benki wanapata Kwa bahati mbaya mume wangu ndiye
ujira mnono. Je, ninaweza kuishtaki benki pekee aliyewapa watoto wetu majina
pia? na amekuwa akiwapatia majina ya ukoo
11 Agosti 2014 wake. Ameshamchagulia jina hata mtoto
tunayemtarajia, na kupelekea kubishana
Tunaanza na benki na tunaamini kwamba
kwa kuwa na nami nataka kumpatia jina
haki yako ya kuishtaki benki ipo mbali sana
mtoto huyu. Je, kuna sheria inayosimamia
na hivyo huwezi kuishtaki. Hata hivyo, mume watoto kupewa majina? Tafadhali niongoze.
wako anaweza kuishtaki ila anatakiwa kuwa
29 Septemba 2014
na sababu za msingi sana za kuegemea. Kwa
mfano, je analipwa malipo ya muda wa ziada Sheria ya Mtoto, Na. 21 ya 2009 chini
kwa kazi anazozifanya mpaka saa za usiku? ya kifungu cha 6 inaeleza kwamba mtoto
Anafanya kazi kwenye mazingira salama? Je, atakuwa na haki ya kupewa jina, utaifa na
benki inamjali kwa mujibu wa mkataba wa kuwafahamu wazazi wake wa kumzaa na
ajira? Je, kuna mazingira ya ndani ya benki ndugu/jamaa wengine wa ukoo/familia
ambayo yanachangia kuongezeka uzito kwa tandaa. Inaeleza zaidi kwamba, mtu
mfano kuwapatia wafanyakazi vyakula visivyo hatamnyima mtoto haki yake ya jina, utaifa
bora? Unahitaji kuwa na uelewa wa haya na kufahamu wazazi wake wa kumzaa na
yote ili kuweza kuelewa haki ya mume wako ndugu zake wengine kwa kuzingatia masharti
kushtaki. ya sheria nyingine. Pia, kila mzazi au mlezi
36 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

atakuwa na wajibu wa kusajili kuzaliwa kwa wa ahadi ya ndoa/kulazimisha ndoa.”


mtoto wake kwa Msajili Mkuu. Kwa hiyo Sheria ya Ndoa inaruhusu
Kwa bahati mbaya hakuna sheria madai juu ya hasara ambayo mtu anaipata
inayolazimisha iwapo baba au mama kwa kuvunja ahadi ya ndoa. Katika kesi
atoe jina la mtoto. Pia hatuna kesi yoyote yako, inategemea na maelezo zaidi ambayo
ya kutuwezesha kukuongoza juu ya unaweza kuwapatia wanasheria wako, fidia
hili. Unaweza kuutatua mgogoro huu inaweza kudaiwa lakini hatuamini kama una
Mahakamani, lakini mfumo wa Mahakama kesi nzuri. Kitu ambacho tuna uhakika nacho
umezidiwa na mrundikano wa kesi na
ni kwamba kama mwanamke huyu amebadili
huenda mpaka mgogoro unatatuliwa
mawazo juu yako, basi itabidi uanze kutafuta
utakuwa tayari umejifungua.
tena. Haijalishi kama wewe ni tajiri na mwenye
Mkataba wa ndoa mamlaka – ni mwanamke ndiye atakayeamua
iwapo aolewa na wewe au la.
Nilipokuwa Chuo Kikuu miaka tisa iliyopita,
niliingia mkataba na rafiki yangu wa kike Kushikiliwa kwa mali za ndoa/familia
kuwa ikiwa wote wawili tutatimiza miaka
30 na hatupo kwenye ndoa au kuwa na Mume wangu amekuwa akifanya kazi
mahusiano imara na mtu mwingine, basi kwenye shirika la umma na wakati wa
tutaoana. Mwezi uliopita wote wawili ndoa yetu tumeweza kuanzisha vitega
tulitimiza miaka 30 na alinihakikishia uchumi vya familia ikiwa ni pamoja na
kwamba hajaolewa na wala hayupo baa, supamaketi na saluni mbili zisizojali
katika uhusiano wowote imara, anadai jinsia. Tumeweza pia kujenga nyumba
havutiwi tena na mimi, ingawa mimi nzuri ambayo hivi sasa tunaishi. Ninakiri
ni tajiri na mwenye mamlaka. Huku ni kwamba mume wangu amechangia
kukiuka makubaliano, nataka kumpeleka sehemu kubwa ya mtaji ingawa na mimi
Mahakamani ili alazimishwe kuolewa na nimechangia sehemu kwa mkopo niliopata
mimi. Bado ninamhitaji. kutoka taasisi ya mikopo midogo iliyopo
29 Septemba 2014 Dar es Salaam. Mimi pia sijui ikiwa mapato/
mchango wa mume wangu umetoka
Mkataba wa ndoa si kama mkataba kwenye vyanzo vingine au mshahara wake
mwingine wowote. Hatima yake inaongozwa mnono na marupurupu tu. Kwa bahati
na upendo wa pande zote mbili. Unaweza mbaya, hivi sasa mume wangu na wenzake
kuwa bado unamuhitaji, lakini yeye hakuhitaji. wameshtakiwa kwa makosa ya rushwa/
Hata kama Mahakama itamshinikiza kuolewa ufisadi kutokana na madai ya ubadhirifu
wa fedha ofisini kwao. Sasa nimeambiwa
na wewe, kitu ambacho haiwezi, basi kusudio
na rafiki yangu kwamba ikiwa mume
kuu la ndoa litakuwa limekiukwa.
wangu atakutwa na hatia, mali/uwekezaji
Sheria ya Ndoa inaeleza kwamba, “kesi
wetu wote, ikiwa ni pamoja na nyumba
inaweza kufunguliwa kudai fidia ya kukiuka tunayoishi, vitataifishwa na Serikali. Nataka
ahadi ya ndoa iliyotolewa Tanganyika bila kujua kama hii inawezekana. Je, ninaweza
kujali ukiukwaji huo ulifanyika Tanganyika kufanya chochote kupinga jambo hili?
au kwingineko, na mdai, iwapo mdai/ Kwani ninahisi kuwa litanipotezea haki
upande huo haujafikisha miaka kumi na zangu kwa kuwa na mimi nimechangia
nane, na mzazi wake au mlezi. Hakuna kesi kwenye uwekezaji huu.
itakayoletwa kwa ajili ya utekelezaji maalum 24 Novemba 2014
Watoto, Mahusiano, Sheria za Ndoa na Talaka • 37

Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Wilaya inavyoruhusu. Zaidi ya hilo, muumini


Rushwa, Namba 11 ya 2007 inazungumzia yeyote wa dini ambayo ndoa hiyo inafungwa
hali inayokukabili na inasema kwamba anaweza kuhudhuria ndoa hiyo. Vile vile,
TAKUKURU inaweza, kwa kushirikiana na mwananchi yeyote anayehusiana na pande
ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, kurejesha zote au upande mmoja wapo wa ndoa
mapato yatokanayo na rushwa kwa kutaifisha inayofungwa kwa imani ya kiislamu au kimila
na kuwa mali ya Serikali. anaweza kuhudhuria.
Sheria hii inaeleza zaidi kwamba pale Kutokana na maelezo hapo juu, hakuna
ambapo mtu anapatikana na hatia ya kosa ndoa inayoweza kufungwa kwa siri kwa
sheria za Tanzania. Kitu pekee unachoweza
la rushwa chini ya Sheria hii, Mkurugenzi
kuomba ni kwamba mtu yeyote asijitokeze/
wa Mashtaka anaweza kuiomba Mahakama
asihudhurie wakati wa ndoa ama kwenye
iliyomtia hatiani, au Mahakama nyingine
ofisi ya msajili wa ndoa au kwenye nyumba ya
yoyote inayofaa katika kipindi kisichozidi
ibada, au popote unapotaka kufungia ndoa.
miezi sita baada ya mtu huyo kutiwa Kuhusu suala la fungate, tumeangalia
hatiani, kutoa amri ya kutaifisha mali yote sheria zetu na hatujaliona popote neno hili.
iliyopatikana kwa njia ya rushwa. Kuhusu Na kwa hakika siyo sharti la baada ya ndoa.
mapato ya rushwa, sheria imetoa maana Utafiti wetu umegundua kwamba fungate ni
kuwa ni mali yoyote ambayo inatokana na/ likizo ya kitamaduni wanayopewa wanandoa
au inapatikana na hatia ya makosa ya rushwa. baada ya kuoana ili kusherehekea ndoa
Hivyo, madhara ya sheria yaliyoelezwa yao kwa ukaribu na usiri. Kwa sasa, fungate
hapo juu yanaweza kutumika kwa mume zinasherehekewa kwenye maeneo mujarabu
wako baada ya kutiwa hatiani ingawa na mahususi kwa wanafungate.
hatujui ni kosa gani hasa ambalo mume Hiki ni kipindi ambacho wanandoa wapya
wako ameshtakiwa nalo. Na nilazima tueleze wanapata mapumziko kwa kushirikiana
kwamba utaifishaji siyo haki ya moja kwa mambo ya faragha, na nyakati za ukaribu
moja ya TAKUKURU au Mkurugenzi wa ambazo zinasaidia kuimarisha mapenzi
Mashtaka, na hivyo uwe tayari kuthibitisha kwenye mahusiano yao. Kipindi hiki kinawapa
kwamba uwekezaji haukutokana na mapato fursa ya kujuana kwenye mazingira mwanana.
ya uhalifu. Ufaragha huu unaaminiwa kuleta mapumziko
ya kiakili kuelekea mahusiano ya kimwili,
Ndoa ya siri na fungate ikiwa ni moja ya njia za awali za kuimarisha
ukaribu wao siku za mwanzo wa ndoa.
Ninataka kufanya harusi/ndoa ya siri na
Hivyo, ni uamuzi wako kama unataka
sitaki mtu yeyote ahudhurie ndoa/harusi
kwenda fungate ama la. Sheria haikulazimishi
yetu. Je, hii imeruhusiwa kwenye sheria
ila inawezekana mke wako ana matumaini
za Tanzania? Je, ni lazima kwenda fungate
hayo. Hapo ni wewe tu utakavyomudu
baada ya ndoa? Mke wangu anasisitiza
matarajio ya mkeo. Tunakutakia kila la heri.
kwamba fungate ni sharti la ndoa.
1 Desemba 2014 Kunyima haki ya matibabu kwa sababu
ya dini
Sheria ya Ndoa, 1971 inaeleza kwamba,
mtu yeyote anaweza kuhudhuria wakati Mimi nina imani kubwa kwamba Mungu
wa kufungisha ndoa ya kiserikali kwa kadiri ndiye mponyaji, na imani/dini yetu
nafasi katika ofisi ya Msajili wa Ndoa wa inakataza wazazi kuwapeleka watoto wao
38 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

hospitalini kupata matibabu. Tunaelekezwa Uponyaji wa miujiza/matibabu ya imani


kumwombea mtoto mgonjwa mpaka hayajathibitika. Kwa kushindwa kumpatia
atakapopona. Kutokana na hilo, sijawapatia chanjo mtoto wako, unahatarisha maisha
wanangu chanjo kadhaa. Je, kuna sheria yake kizembe. Tunakushauri umpeleke
inayopingana na imani hii? mwanao akapate chanjo.
8 Desemba 2014

Sheria inatoa uhuru wa kuabudi kwa kila


mtu nchini Tanzania. Hata hivyo, Sheria ya
Mtoto ya mwaka 2009 inaeleza wazi kwamba,
mtu yeyote hatamnyima mtoto matibabu kwa
sababu za kidini au imani nyinginezo. Hivyo,
kwa kumnyima mtoto wako haki ya matibabu,
unavunja sheria na unaweza kukumbana na
mkono wa sheria. Utafiti wetu umekutana na
aya ifuatayo kutoka kwenye Gazeti la Times la
Uingereza ambayo ni muhimu kwako.
Mapingamizi ya kidini kuhusu matibabu
ya kidunia yana mizizi ya kihistoria ambayo
ilianza mwishoni mwa miaka ya 1800 nchini
Uingereza ambapo dhehebu lililoitwa
Peculiar People (Watu wa Kipekee) liliishia
kushtakiwa kwa kuruhusu vizazi vya watoto
wao kufariki kutokana na maamuzi yao ya
kuwakataa madaktari na dawa. Hivi leo,
mara kwa mara makundi mengi ya kidini
yanakataa baadhi au huduma zote za afya
kwa sababu za kidini, yakiwemo makundi ya
Wakristo Wanasayansi, Mashahidi wa Yehova,
Waamishi na Wasayantoloji. “Wenye imani
kali hawa wanatuambia kwamba maisha yao
yapo mikononi mwa Mungu na sisi kama
madaktari, siyo Mungu,” anasema Dakt.
Lorry Frankel, Profesa wa Shule ya Tiba na
mwandishi wa Mtanziko wa Kimaadili kwenye
Tiba ya Watoto. Tunaheshimu imani za dini
za watu na tunajaribu kuendana nazo, lakini
hatuwezi kukataa matibabu ambayo yataokoa
maisha. Frankel anasema aliwahi kuwapeleka
Mahakamani waumini wa dini ya Mashahidi
wa Yehova ambao walikataa kutoa damu
kwa ajili ya watoto wao ambao walikuwa na
hali mbaya. “ Mungu anatupenda na sijawahi
kumnyima mtoto matibabu” anasema Frankel.
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 39

Sheria za Biashara,
Migogoro ya Kibiashara
na Haki Miliki

Katika ulimwengu kamilifu, biashara hufanyika kwa uaminifu na kwa kuheshimu


makubaliano. Kwa bahati mbaya, ulimwengu si kamilifu na hivyo siyo mara zote mambo
huenda sawia. Wakati mwingine wafanyabiashara huwadanganya wateja, hughushi
nembo/alama za biashara za kampuni shindani, hugombana na waleta bidhaa na hata
hupinga tafsiri ya mikataba. Mambo kama haya yanapotokea, wakati mwingine, huwa ni
lazima kutatua changamoto hizi kupitia mchakato rasmi wa kisheria, ikiwa ni pamoja na
upatanishi, usuluhishi au kufikishana mahakamani. Na wakati mwingine, inawezekana hata
kuwakamata wanaovunja mikataba na kuwaweka gerezani kwa miezi sita.
40 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Kuvunja mkataba mgogoro kwenye usuluhishi. Kwa kawaida


vipengele vya usuluhishi vimeundwa kwa
Niliingia mkataba na mtu ambaye alinilipa namna ambayo kama mgogoro utatokea,
malipo ya awali na malipo mengine
upande wowote ulioathirika unaweza
kulipwa baadaye, lakini ameshindwa
kupeleka mgogoro kwenye usuluhishi.
kunilipa deni lote, na muda tuliopatana
Hujasema iwapo mgogoro umetokea kwa
umeshaisha. Baada ya kufuatilia kwa
miezi mingi bila majibu yoyote kutoka sababu malipo hayajafanyika. Je, huo ni
kwake, yeye ameamua kulipeleka suala hili mgogoro ambao unaweza kutafsiriwa kwa
kwenye usuluhishi. Inanishangaza sana kuangalia kipengele cha usuluhishi? Hatuwezi
kuona upande uliokiuka masharti ndio kujibu hilo kwa sababu hatuna taarifa kamili.
unaopeleka suala hili kwenye usuluhishi. Ambacho tunaweza kusema kwa uhakika,
Nifanye nini? Ninachotaka ni pesa zangu tu. ni kwamba upande uliokiuka unaonekana
2 Januari 2012 kuamini kwamba kuna mgogoro mahala na
kwa hiyo umezuia malipo.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba Kwa kujali muda na kuzingatia kiwango
mkataba wenu una kipengele cha usuluhishi cha pesa, tunakushauri uendelee na
ambacho kinaelekeza mgogoro upelekwe
usuluhishi kwa sababu usuluhishi ni njia ya
kwanza kwenye usuluhishi kabla ya kwenda
haraka na mgogoro unaweza kutatuliwa
Mahakamani. Usuluhishi ni uamuzi wa
ndani ya wiki chache tu.
mgogoro kwa njia ya upatanishi unaofanywa
na mtu mmoja au zaidi, ambapo msuluhishi/ Mgahawa wa chakula bila mafuta
wasuluhishi ni mtu/watu huru wasio na unapotosha wateja
maslahi katika mkataba au mgogoro husika,
badala ya kwenda Mahakamani. Wasuluhishi Nimekuwa nikifanya biashara ya
uteuliwa na wahusika wenye mgogoro mgahawa kwa takribani miaka 30. Miezi
kulingana na masharti ya mkataba. sita iliyopita, umefunguliwa mgahawa
mwingine karibu yangu wenye jina ‘Kula
Msuluhishi ana wajibu wa kusikiliza pande
Chakula Kisicho na Mafuta’. Ingawa jina
zote mbili na kutoa tafsiri sahihi ya sheria
la mgahawa huo linamaanisha kuuza
na kwa misingi ya haki na usawa. Kulingana
chakula kisicho na mafuta, umekuwa
na na tafsiri ya kipengele cha usuluhishi
ukiuza kuku waliokaangwa kwa mafuta,
katika mkataba na usahihi wa maamuzi ya
vibanzi (chipsi), chipsi-mayai na vyakula
msuluhishi/wasuluhishi, tuzo iliyotolewa
vinginevyo vilivyopikwa kwa mafuta. Sijali
na msuluhishi/wasuluhishi inaweza
ushindani uliopo, lakini jina wanalotumia
kupingwa Mahakamani. Hujatueleza kama
linapotosha watu ambao wanaishia kwenda
mkataba ulioingia una kipengele cha hapo wakiamini watapata chakula kisicho
usuluhishi. Kama mkataba una kipengele na mafuta. Je, jina hili haliwapotoshi watu,
hicho, unatakiwa kwenda kwenye usuluhishi ninaweza kufanya nini juu ya jambo hili?
(ingawa umeanzishwa na mdeni wako). Swali langu la pili, ni je kampuni inaweza
Kama hakuna kipengele cha usuluhishi, kubadilisha jina baada ya kusajiliwa?
huhitaji kwenda kwenye usuluhishi badala
2 Januari 2012
yake unaweza kufungua kesi ya kudai fidia
Mahakamani. Sheria ya Makampuni itakuwa upande
Inaonekana umeshangazwa na kitendo wako iwapo kwa maoni ya Waziri wa
cha mtu aliyekiuka mkataba ndiye amepekeka Viwanda na Biashara jina ambalo kampuni
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 41

imesajiliwa nalo linapotosha uhalisia wa kwa jina la zamani, inaweza kuyafungua au


biashara/shughuli zake na kuna uwezekano kufunguliwa dhidi yake kwa jina lake jipya bila
wa kusababisha madhara kwa umma, athari yoyote.
anaweza kuelekeza kubadilisha jina lake.
Kama maelekezo ya Waziri hayakupingwa Mkataba kwa njia ya nukushi (faksi)
Mahakamani ni lazima yatekelezwe ndani Niliingia mkataba na muuza mbao kwa
ya kipindi cha wiki sita tangu tarehe ya ajili ya kuniuzia mbao kwa bei fulani.
maelekezo kutolewa au ndani ya muda zaidi Tulikubaliana masharti lakini kwa sababu ya
ya huo kama Msajili atakavyoona inafaa mazingira yaliyokuwepo tuliingia mkataba
kuruhusu. kwa njia ya nukushi (nukulishi/faksi).
Sheria inaeleza zaidi kwamba kampuni Muuzaji amegeuka na anataka kuongeza
inaweza, katika kipindi cha wiki tatu kuanzia bei ya mbao. Ninaweza kufanya nini?
tarehe ambayo maelekezo yalitolewa, 9 Januari 2012
kuiomba Mahakama kuyatengua; na
Mahakama inaweza kutengua maelekezo Kwanza kabisa ni lazima tuseme kuwa
hayo au kuyathibitisha na, kama hatuna taarifa kamili za kutuwezesha
ikiyathibitisha maelekezo, itabainisha kipindi kukujibu kwa ufasaha. Hata hivyo sheria
ambacho yanapaswa kutekelezwa. Kama zetu zinatambua mkataba wa mdomo na wa
kampuni inakiuka kutekeleza maelekezo maandishi. Kwa kesi yako, mbali na mkataba
husika chini ya kifungu hiki, itatozwa faini ya wa nukushi, kama unaweza kuthibitisha kwa
kuendelea kukiuka. matendo au namna nyingineyo kuwa hicho
Ushauri wetu ni wewe kumwandikia Waziri ndicho mlichokubaliana, tunaamini una kesi
wa Viwanda na Biashara, umweleze hali ilivyo, nzuri. Ushahidi wa ziada kuhusu mkataba
huku ukiainisha, kwa maoni yako, madhara wa nukushi unaweza kuhitajika kuthibitisha
ambayo umma utayapata kutokana na jina dhamira yenu. Mwanasheria wako anaweza
hilo linalopotosha. kukuongoza zaidi.
Tunajibu swali lako la pili kwa kukubali
Kukamatwa kwa mdaiwa
kwamba kampuni inaweza kwa azimio
maalumu na kwa idhini ya maandishi ya Nimeshinda kesi dhidi ya mtu na anakataa
Msajili kubadilisha jina lake. Kama Msajili kunilipa. Nimejitahidi sana lakini
atakataa kutoa idhini, atatoa sababu. Msajili inaonekana kama upole wangu kwenye
ataingiza jina jipya kwenye orodha ya usajili, kudai unatafsiriwa vibaya. Je, kuna
na hivyo jina jipya kuchukua nafasi ya jina la vifungu vya ukamataji kama sijalipwa?
zamani, na atatoa taarifa ya mabadiliko hayo Nini faida na hasara za njia hiyo?
kwenye Gazeti la Serikali. 13 Februari 2012
Ni lazima ieleweke kwamba, kampuni
kubadili jina, katika mazingira yaliyoelezwa Ndiyo, kuna vifungu ambavyo
hapo juu, hakuathiri haki yoyote au wajibu vinamruhusu mdaiwa kukamatwa ili
wowote wa kampuni na wala hakuharamishi kutekeleza Tuzo ya Mahakama. Sheria
mashtaka yoyote yaliyokwishafunguliwa ya Mwenendo wa Makosa ya Madai ya
na kampuni au yaliyokwishafunguliwa Tanzania inatamka kwamba mdaiwa
dhidi ya kampuni hiyo kwa jina la zamani. anaweza kukamatwa ili kutekeleza tuzo siku
Aidha, mashtaka yoyote ambayo kampuni yoyote nyakati za mchana na kupelekwa
ingeyafungua au yangefunguliwa dhidi yake Mahakamani haraka iwezekanavyo, na
42 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Mahakama inaweza kuamuru afungwe. Wakati haki ni lazima itendeke na


Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Madai ionekane inatendeka, pia kuna sera ya umma
pia inatamka kwamba kama tuzo iliyopelekea maarufu ambayo inasema ni lazima kuwe na
mdaiwa kukamatwa ni tuzo ya malipo ya ukomo wa mashtaka. Sheria ya Mwenendo
fedha, mdaiwa akilipa fedha za kwenye tuzo wa Makosa ya Madai pia inarahisisha hili
pamoja na gharama za afisa aliyemkamata, kwa kutamka kwamba hakuna Mahakama
afisa anaweza kumwachia huru mdaiwa mara itakayosikiliza shauri au sehemu ya shauri
moja. ambalo lina uhusiano wa moja kwa moja
Kifungo ni miezi sita na anaweza au linafanana na shauri la awali kati ya watu
kuachiliwa kabla ya miezi sita kama tu atalipa walewale au mmojawapo akidai kuhusu
au kwa maombi ya aliyeomba afungwe au suala lile linalofanana na shauri ambalo
kama mtu aliyeomba afungwe ameshindwa lilishafunguliwa na kutolewa maamuzi na
kumlipia mfungwa wake gharama za kujikimu Mahakama yenye mamlaka. Kwa hiyo ni
akiwa gerezani. lazima ujitetee kwenye shauri hili jipya na
Tafadhali, unataarifiwa kwamba sheria uibue hoja kuwa shauri hili limeshasikilizwa
inakutaka mshinda tuzo, kumlipia mdaiwa na kutolewa uamuzi na Mahakama.
wako gharama za kujikimu (kwa kadri ya
nafasi yake kimaisha) anapokuwa gerezani, na Sifuri ya ziada kwenye bei ya mkataba
kushindwa kulipa gharama hizo kwa kiwango
Niliingia kwenye mkataba ambapo thamani
kinachotakiwa kunaweza kufanya mdaiwa
halisi ya bei ya kwenye mkataba ilitakiwa
wako kuachiliwa huru. kuwa milioni 11 lakini tuliingia kwenye
Faida za kifungo ni kwamba mdaiwa mkataba huku kukiwa na ongezeko la
anaweza kukulipa kwa kuhofia kifungo. sifuri kimakosa kwenye oda ya manunuzi
Hasara kubwa ya njia hii ni kwamba, kama yaani Mil. 110. Tumemlipa muuzaji milioni
mfungwa hahofii kwenda jela miezi sita, 11 lakini anadai Mahakamani kwamba
utawajibika kuingia gharama za ziada za tumemlipa pungufu na anataka alipwe
kumhudumia akiwa gerezani na bado usiweze tofauti. Nimearifiwa kwamba Mahakama za
kulipwa. Pesa zote unazozitumia kumhudumia Tanzania mara zote zinampendelea mtu wa
mdaiwa akiwa gerezani zinaweza kuongezwa aina hiyo. Tufanye nini?
kwenye deni lako. 2 Aprili 2012

Kesi imerudiwa Kwanza kabisa kama kwa makusudi


mliacha sifuri moja kwenye mkataba
Nilishinda kesi miezi 18 iliyopita, baadaye
nikagundua kwamba niliowashinda kesi na thamani halisi ya bidhaa ni Shilingi
wamefungua tena kesi nyingine kwa jambo milioni 110, muuzaji anaweza kushinda na
lilelile lakini safari hii wamefungua kwenye mtaamuliwa kumlipa. Lakini, kama mlinunua
Mahakama nyingine. Na wala hawajasema bidhaa ambazo ni wazi kuwa thamani yake
chochote kuhusu ushindi wangu wa ile halisi ni Shilingi milioni 11 na mkaweza
kesi ya awali. Kwa upande wangu, naona kuthibitisha kwamba bidhaa hizo thamani
sina haja ya kujitetea kwenye kesi ambayo yake halisi ni kiasi hicho na yalikuwa makosa
imekwishaamuliwa tayari. Tafadhali naomba ya dhati, hatuamini kama mtashindwa
muongozo. Mahakamani.
12 Machi 2012 Pia, jaribu tena kuangalia iwapo kiasi
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 43

hicho kiliandikwa kwa maneno. Kwa kawaida na maeneo. Mamlaka ndiyo mmiliki wa
kwenye tafsiri, maandishi ya maneno makaburi na ndiyo yenyewe inayoamua tozo
yanasimama, ikiwa na maana kama kiasi za huduma ambazo zipo kwenye makaburi
kiliandikwa milioni 110 lakini maneno haya. Chini ya Kanuni hizo, hakuna maiti
yakasomeka milioni kumi na moja, basi ya mtu yeyote itakayoruhusiwa kuzikwa
uwezekano ni kwamba Mahakama itatafsiri sehemu nyingine yoyote nje ya maeneo hayo,
kiasi cha Shilingi milioni kumi na moja na si isipokuwa tu kwa kibali maalum kutoka kwa
mamlaka husika. Hii ina maana kwamba
milioni 110 (za tarakimu).
mabaki yote ya marehemu yanatakiwa
Kilichoelezwa hapo juu kinaweza kuleta
kuzikwa kwenye makaburi yaliyotengwa.
shida kama usambazaji wa huduma ulikuwa
Sheria ipo kimya iwapo mtu binafsi
si wa kiwango maalum. Unaweza kupitia
anaweza kumiliki makaburi yake binafsi
majadiliano yenu yote mliyoyafanya na kwa malengo ya kibiashara. Hata hivyo, kwa
kuyafanya sehemu ya ushahidi ili kuonesha kuwa inawezekana kwa jamii fulani ya dini
kwamba huduma mliyokubaliana ilikuwa ni kuwa na makaburi yake, hatuoni kwa nini
milioni 11 na siyo milioni 110. mtu binafsi asiruhusiwe kuwa na makaburi
Kwa kawaida Mahakama haiingilii kile yake iwapo makaburi hayo yapo kwenye
pande zimekubaliana, isipokuwa kama kuna maeneo ambayo yanaendana na mipango
uharamu/ubatili kwenye mkataba. Kama ya maendeleo ya miji kwenye mji husika.
nyaraka zako ziko sawa, hatuoni kwa nini Tunakushauri uwasiliane na mamlaka za
Mahakama isiamue upande wako. Wanasheria manispaa kwa ufafanuzi na muongozo zaidi.
wako wanaweza kukuongoza zaidi. Tozo yako ya pango ya kila mwaka
inafurahisha sana. Unachojaribu kushawishi
Sehemu za mazishi/makaburini ni kwamba utaingia mkataba na familia
ya marehemu ambapo utakuwa unapata
Kadiri muda unavyokwenda, gharama za
kiasi fulani cha pesa kila mwaka, ni kama
kupata sehemu za mazishi ya binadamu
kwenye makaburi ya Jiji zinazidi kumpangisha marehemu ili abaki kaburini.
kuongezeka. Ni nani anamiliki makaburi Tunajaribu kufikiria utafanya nini kama
haya? Je, mtu binafsi anaruhususiwa kuwa ikitokea hujalipwa, tuna hakika huwezi
na makaburi yake binafsi kwa malengo ya kufukua kaburi ili utoe mwili wa marehemu
kibiashara? Ninataka kuanzisha makaburi kwa sababu, kwa kufanya hivyo, utakuwa
yangu binafsi ambapo familia ya marehemu unavunja sheria. Angalia kwanza mpango
italipa kodi ya pango kila mwaka, ambayo wako wa biashara kwenye suala hili kabla ya
itajumuisha utunzaji wa makaburi yote kwa kuanza.
ujumla.
Mkataba wa kimataifa wa mauzo ya
16 Aprili 2012 bidhaa
Chini ya Kanuni za Serikali za Mitaa Niliagiza bidhaa kutoka kwa muuzaji
(Mamlaka za Miji) (Udhibiti Maendeleo) mchina nchini China ambazo ziliharibika
za 2008 ambazo zimetokana na Sheria ya sana zikiwa njiani kuja Tanzania. Mkataba
Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), mamlaka ulikuwa ni muuzaji anawajibika hadi bidhaa
pekee iliyopewa jukumu la kuteua au zitakapopakiwa kwenye meli kwa ajili ya
kutenga maeneo kwa ajili ya mazishi ni miji, kusafirishwa (FOB). Tatizo pekee ni kwamba
manispaa na majiji yanayohusika kutegemea hatuna hakika ni wapi tufungue shauri -
44 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Tanzania au China. Swala hili limetolewa Turudi kwenye swali lako. Kwanza uliuliza
taarifa kwenye ubalozi wa China ambao kama unaweza kulitolea taarifa Umoja wa
wanatupa ushirikiano lakini wanasema Mataifa. Jibu ni kwamba unaweza usifanikiwe
hili ni suala la kibiashara ambalo linahitaji kwa sababu UNICITRAL ilisaidia kuandaa
utatuzi wa pande husika. Makubaliano sheria, lakini haisimamii sheria hii moja kwa
yetu yanaongozwa na Mkataba wa Umoja moja.
wa Mataifa wa Mauzo ya Bidhaa (CISG). Swali lako la pili ni unawezaje kuendelea.
Je, tunaweza kufungua kesi Umoja wa Kama kuna njia zozote za kutatua mgogoro
Mataifa. Tafadhali tushauri tunaendeleaje. huu kwa amani bila kwenda Mahakamani
Mwanasheria wetu anasema tunatakiwa au usuluhishi, unatakiwa kuzingatia sana
kufungua shauri hapa. chaguo hilo. Katika utatuzi wa mgogoro kwa
23 Aprili 2012 njia mbadala, kwa kawaida kutakuwa na
kutoa na kuchukua (kuuma na kupuliza) na
Mkataba wa Kimataifa wa Mauzo ya Bidhaa,
unatakiwa kuwa mwepesi kubadilika wakati
ambao wakati mwingine unaitwa Mkataba
wa majadiliano.
wa Vienna, ni Mkataba unaosimamia biashara
Tuchukulie mkataba hauna kipengele
za mauzo ya bidhaa kimataifa. Mpaka kufikia
cha usuluhishi na njia mbadala ya utatuzi
Agosti 2010 ulikuwa umeridhiwa na nchi
imeshindikana, hapo huna uchaguzi
wanachama 77 na hivyo kuwa na idadi kubwa
mwingine zaidi ya kuendelea Mahakamani.
ya nchi wafanyabiashara, na kuufanya kuwa
Swali linalofuata ni utamshtaki wapi muuzaji.
ni miongoni mwa sheria zenye mafanikio
Hatujaona mkataba wa mauzo lakini kwa
makubwa sana. Tanzania haijaridhia mkataba
maoni yetu unatakiwa kufungua shauri
huu na hivyo hauwezi kutumika moja kwa
nchini China kwa sababu ni rahisi tu kwamba
moja hapa.
iwapo utashinda kesi utakuwa kwenye nafasi
Mkataba huu unaepusha matatizo ya
nzuri ya kutekeleza hukumu hiyo dhidi ya
kuchagua sheria za kutumika kwa sababu
msambazaji wa kichina. Kama utashtaki
wenyewe unatoa kanuni zinazokubalika,
Tanzania, hukumu iliyotolewa Tanzania haina
ambapo nchi wanachama, Mahakama na nguvu ya kisheria nchini China kwa kuwa
wasuluhishi wanaweza kuzitumia. Mkataba hakuna makubaliano ya utekelezaji hukumu
huu uliendelezwa na Tume ya Umoja wa kati ya China na Tanzania. Ni dhahiri upo
Mataifa inayoshughulika na Maendeleo ya kwenye wakati mgumu hivyo unatakiwa
Sheria za Biashara za Kimataifa (UNCITRAL) na kuonana na wanasheria wa Tanzania na China.
ulianza kutumika mwaka 1988.
Kupitishwa kwa mkataba huu kunatoa Hasara imesababishwa na zima moto,
sheria sawa na za kisasa kwa mauzo ya bidhaa bima inakataa dai langu
kimataifa ambazo zitatumika popote ambapo
Nilikuwa namiliki mgahawa mzuri na wa
mikataba ya mauzo ya bidhaa itafanyika
hali ya juu Dar es Salaam ambao uliungua
kwenye nchi wanachama. Katika mazingira kwa moto. Nashukuru zimamoto walikuja
hayo Mkataba huu utatumika moja kwa lakini moto ulikuwa mkubwa sana na
moja ili kuepuka kutumia kanuni za sheria ulisababisha hasara kubwa. Kampuni yangu
ya kimataifa binafsi ili kuchunguza sheria ya bima inataka kunilipa sehemu ndogo ya
zinazotumika kwenye mikataba, na hivyo dai halisi, inataka kupunguza kiasi hicho
kusaidia kuongeza uhakika na usanifu wa kutokana na uharibifu uliosababishwa na
mauzo ya bidhaa kimataifa. maji ya zima moto. Wakala wangu anasema
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 45

nichukue tu kiasi hicho kwa sababu Kutokuafikiana kuhusu msuluhishi


makampuni ya bima ni wajanja sana na
wanalindwa na sheria. Kampuni yangu ya Wakati wote niliamini kuwa usuluhishi
bima inasema sera yangu inahusu majanga ni njia bora ya kutatua migogoro, lakini
ya moto tu. Je, hiyo ni kweli? Tafadhali mwishowe nikagundua kuwa wakati
nishauri. mwingine unaweza kuchukua muda
mrefu zaidi kuliko Mfumo wa Mahakama.
25 Juni 2012
Kampuni yetu ina mgogoro na kampuni
Hatujaona sera yako ya bima ya moto nyingine iliyoko Dar. Wanasheria wetu
iliyotolewa na mbima wako kwa sababu wameshindwa kukubaliana juu ya nani
wakati mwingine kuna vitu vinaondolewa atakayekuwa msuluhishi. Ni mwezi wa tisa
kwenye mkataba wa bima ili kupunguza sasa na mgogoro wa nani awe msuluhishi
haujatatuliwa. Tufanye nini? Je, tunaweza
wajibu wa mbima. Hata hivyo, kwenye kesi
kwenda moja kwa moja Mahakamani?
yako maelezo ambayo yanaweza kukupa
2 Julai 2012
matumaini kidogo ni yale ya kwenye sheria
maalum ambayo inajihusisha na matukio Sheria ya Usuluhishi inaeleza cha kufanya
hayo. katika mazingira hayo. Inatamka kwamba
Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mahakama inaweza kumteua msuluhishi
Na. 14 ya 2002 kifungu cha 26 (2) kiko wazi kama kipengele cha usuluhishi kinasema
kwamba hasara yoyote iliyosababishwa na mgogoro utatatuliwa na msuluhishi mmoja,
na kama pande hazikubaliani baada ya
jeshi katika utekelezaji wa majukumu yake
mgogoro kutokea, watakubaliana kumteua
au matukio ya moto au majanga mengine
msuluhishi. Hivyo, unaweza ukapeleka
au likijibu mlio wa tahadhari ya moto, maombi Mahakamani na Mahakama
yatachukuliwa kuwa yamesababishwa na inaweza kumteua msuluhishi ili kuwawezesha
moto katika maana ya sera yoyote ya bima ya kuendelea na usuluhishi.
moto. Kuhusu uwezekano wa kwenda moja kwa
Kutoka na maelezo hapo juu, hata moja Mahakamani kuutatua mgogoro, hilo
kama sera yako imezuia fidia hiyo, ambayo haliwezekani kwani pande zote zilikubaliana
tunashangaa kuisikia, sheria itakulinda na kufanya usuluhishi kwanza. Hata hivyo kama
hivyo kipengele hicho hakitatiliwa maanani nyote mkikubaliana kuacha usuluhishi,
dhidi yako. Kumbuka kuwa wakati wote sheria Mahakama itakuwa na mamlaka ya kusikiliza
mgogoro huo. Vinginevyo mnatakiwa kujikita
inatawala dhidi ya mikataba binafsi.
kwenye usuluhishi.
Labda kama kuna taarifa unaficha,
tunaamini una kesi nzuri dhidi ya kampuni Alama (Nembo) ya biashara imesajiliwa
yako ya bima. Usikimbilie tu kumuamini na mtu mwingine
wakala wako inawezekana anataka tu
Nimekuwa nikitumia jina la kampuni
kufunga faili ili aendelee na mambo mengine.
fulani kwa miaka 30 iliyopita. Hivi karibuni
Mawakala wanafurahia kukusanya malipo na
nimegundua kwamba kuna mtu amesajili
mara nyingi wengi wao hawafurahii kufuatilia jina langu kama nembo ya biashara.
madai yako. Unahitaji kufanya maamuzi Wanasheria wangu wanasema muda wa
ya busara ya namna ya kuendelea na kupinga usajili huu umekwisha. Nifanyeje?
tunakushauri uwasiliane na wanasheria wako. 16 Julai 2012
46 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Kwa madhumuni ya swali hili, tunachukulia zetu kwa sababu tuliwalipa pesa zao
kwamba kampuni yako imesajiliwa kwa jina zote? Muuzaji anasema tusome mkataba
hilo hilo chini ya Sheria ya Makampuni kama na siyo barua-pepe tulizotumiana kabla
ilivyo kwenye Sheria ya Alama za Biashara na ya mkataba. Barua-pepe zinasema wazi
Huduma. Wafanyabiashara wengi wanaamini kwamba mashine ni ya kisasa na imetumika
kwamba mara wanaposajili jina chini ya sheria kwa miezi michache tu. Tafadhali tuongoze.
ya Makampuni basi haina haja ya kusajili jina 16 Julai 2012
hilo kama nembo ya biashara. Wanakosea. Ni
Hii siyo mara yetu ya kwanza kusikia
rahisi zaidi kusajili sehemu zote mbili kuliko hospitali za ndani kutapeliwa na kununua
kupigana vita kama unayotaka kuianza. mashine za kitabibu zilizopitwa na wakati.
Ili kuondoa nembo ya biashara katika Ingawa tunakuonea huruma, maswali yako
orodha ya usajili, unahitaji kufanya maombi hayako moja kwa moja. Hivyo tunahitaji
maalum kwa Msajili wa Nembo za Biashara. kuona mkataba mlioingia ili tuweze
Utahitaji kutoa maelezo ambayo yanajikita kuwaongoza. Hata hivyo, tutajaribu kujibu
kwenye kesi yako. Mmiliki wa nembo maswali yako kwa ujumla.
iliyosajiliwa naye anayo haki ya kujibu madai Kwanza, kwenye mkataba huwa kuna
yako kabla hamjasikilizwa. ahadi na masharti/hakikisho. Mnahitaji kuona
Sababu unazoweza kuzitoa kwenye ahadi na masharti ambayo msambazaji
maombi yako ni pamoja na wewe kuwa wa aliwapatia. Moja ya hakikisho huwa ni
kwanza kuanza kuitumia, ushindani usio kwamba mashine lazima iwe kwenye hali
wa haki, na kuchanganya wateja. Ni vyema nzuri. Kama hakuna kipengele hicho na
kumtumia mtaalam wa nembo za biashara ili mkanunua mashine kama ilivyo, basi itawawia
aweze kukuongoza kwenye mchakato huu. vigumu kurudishiwa pesa zenu.
Pili, mnaweza kuangalia kama mkataba
Kutapeliwa na muuzaji wa kifaa cha unasema kwamba mkataba huu ni mkataba
kupima mionzi kamili kati ya pande zote kuhusiana na
masuala yaliyomo ndani yake na unachukua
Muuzaji wa vifaa vya kitabibu aliiuzia
nafasi ya makubaliano mengine ya aina
hospitali yetu mashine ya matibabu kwa
yoyote nje ya mkataba, kama yapo.
njia ya mionzi (CT-scan) ambayo ni ghali
sana. Tuliifunga na muuzaji alituhakikishia Wanahisa tajiri, kampuni masikini
kwamba inafanya kazi vizuri sana. Ilichukua
wiki mbili kuifunga na tulitekeleza masharti Kuna kampuni kubwa sana na yenye
yote ya ufungaji. Wakati wahandisi wa mafanikio makubwa hapa Tanzania kiasi
kigeni walipotukabidhi, ndani ya masaa kwamba imefungua makampuni mengine
mawili tu tuliwaarifu wahandisi hao na madogo kwa kila biashara inayofanya.
muuzaji kwamba mashine haifanyi kazi Ninaiuzia bidhaa moja ya hizi kampuni
vizuri kama walivyotuhakikishia. Sisi siyo ndogo, na mara zote inasumbua kulipa.
hospitali kubwa na ilituchukua miaka Maswali yangu mawili: inawezekanaje
mingi kuweka akiba ili kununua mashine kampuni ndogo ishindwe kulipa madeni
na mwishowe tumetapeliwa. Baada ya yake wakati wanahisa wake ni makampuni
kuchunguza tuligundua kwamba mashine makubwa na inamilikiwa na watu wenye
ile kwa sasa haitumiki kwani imeshapitwa pesa? Pili, je, ninaweza kudai pesa zangu
na wakati siku nyingi kutokana na teknolojia moja kwa moja kwa wanahisa?
mpya. Tufanye nini ili kurudishiwa pesa 29 Oktoba 2012
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 47

Swali lako la kwanza la inawezekanaje moja kushikilia mali za kampuni nyingine


kampuni ndogo ishindwe kulipa madeni yake ambayo ina madeni, kuwa na umiliki sawa
hatuwezi kulijibu. Ni suala la kiuhasibu na wa kampuni mbili, kutumia ofisi hizo hizo
uiulize ofisi ya uhasibu. Swali lako la pili ni la na wafanyakazi wale wale, kutumika kwa
kufurahisa sana na tunalijibu hapa chini. kampuni moja kama kificho cha kampuni
Wamiliki wa kampuni ni tofauti na kampuni nyingine, kutokuzingatia taratibu za
yenyewe ikiwa na maana kwamba kampuni uendeshaji kampuni, kutokutenganisha
ni mtu kisheria au taasisi inayojitegemea taarifa za kampuni, mtu kuzichukulia mali za
na haitangamani na wanahisa. Wanahisa kampuni kama zake au kutumia wakurugenzi
wanamiliki hisa za kampuni na siyo mali zake. na maafisa wa kampuni.
Mali za kampuni zinamilikiwa na kampuni. Kuhusu sharti la pili, kitu cha msingi ni
Wanahisa vilevile kwa kawaida hawana wajibu kuthibitisha nia mbaya kwenye vitendo
vya kampuni. Kesi nyingi zimetoa fafanuzi
wa kulipa madeni ya kampuni kwa kuwa
zifuatazo juu ya mambo gani ambayo siyo
kampuni ndiyo iliyokopa na siyo mwanahisa
sehemu ya nia mbaya ya kampuni; ugumu
kwa majina yake. Kama umewahi kukopa
tu wa kutekeleza hukumu au kushindwa
utagundua kwamba benki inataka wanahisa
kukusanya madeni, mwanahisa kuipa
kusaini dhamana binafsi ambayo itawafanya
pesa kampuni ndogo ili kuisaidia kutatua
wanahisa walipe madeni ya kampuni kwa matatizo ya kifedha, ilimradi isiwe kwa
sababu kwa kawaida hawawajibiki kulipa lengo la kuendeleza udanganyifu. Matokeo
madeni hayo moja kwa moja. mengine ni pale inapoonekana aina fulani
Ili uweze kuwafikia wanahisa na kuwafanya ya kampuni inatumika kukwepa sheria au
wawajibike, unahitaji kuondoa mwavuli/ kanuni. Katika mazingira hayo pia, Mahakama
kinga/dhana ya kisheria kwamba kampuni imeonekana kuzikubali kesi za mikataba
hubeba majukumu yake yenyewe nje ya ambazo malalamiko yanahusu aina fulani ya
wamiliki wake. Ili uweze kufanikiwa kuondoa udanganyifu.
dhana hiyo unahitaji kuonesha mambo haya Hivyo ili uweze kuondoa kinga/dhana
mawili; kwamba kuna umoja wa umiliki ya kisheria ya kampuni kubeba majukumu
kwenye kampuni na kwamba hakuna tofauti yake yenyewe nje ya wamiliki wake, ni
iliyopo baina ya wanahisa na kampuni; na pili lazima ujiridhishe juu ya baadhi ya mambo
kwamba kama Mahakama itakataa kuondoa yaliyoelezwa hapo juu. Kama ilivyoelezwa
dhana hiyo kutasababisha dhuruma, kikwazo hapo awali kwamba kutengua dhana hii
ama udanganyifu. siyo kazi rahisi. Mwanasheria wako anaweza
Maombi ya kuthibitisha vigezo hivyo si kukuongoza zaidi.
kitu rahisi na kuna vizuizi/vikwazo kadhaa
Kufunga mitambo ya umeme kwenye
ambavyo ni muhimu kuviweka wazi. Hakuna
ardhi binafsi
idadi kamili au masharti ambayo kanuni
hii inaweza kutumika. Wakati mwingine Ninamiliki ploti Dar ambapo kuna kampuni
Mahakama imetumia tu moja ya mambo fulani ambayo inazalisha na kusafirisha
haya mawili. Mambo ya kuzingatia katika umeme ilinipa notisi kwamba inataka
kuondoa kinga/dhana hiyo ya kisheria kutumia ardhi yangu kupitisha nyaya za
kwamba kampuni hubeba majukumu yake umeme na watanilipa. Siwataki kwenye
yenyewe nje ya wamiliki wake yanahusisha ardhi yangu bila kujali kama watanilipa ama
kuchanganya pesa na mali za taasisi mbili la. Ninaweza kulipinga hili?
(yaani za mwanahisa na kampuni), kampuni 5 Novemba 2012
48 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Sheria ya Umeme inatamka kwamba wa Alama kwa kujaza taarifa ya kupinga


kampuni yoyote yenye leseni ya kuzalisha au ambayo inatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku
kusafirisha umeme itakuwa na haki ya kuingia 60 tangu siku ya tangazo na inatakiwa kuwa
kwenye ardhi yoyote ili kuisaidia kutekeleza kwenye fomu maalum kama ilivyotolewa
majukumu yake ya kutoa umeme na mmiliki kwenye Kanuni.
wa mali hataruhusiwa kuingilia haki au mali ya Taarifa ya pingamizi inapaswa kueleza kwa
kampuni hiyo. Pia kampuni imeruhusiwa na ufasaha sababu za pingamizi na inashauriwa
sheria baada ya kutoa notisi kwa mmiliki wa sana pia uambatanishe na picha za alama
eneo kuingia kwenye ardhi hiyo kwa malengo yako na uzilinganishe na zile zilizotangazwa
ya kufanya matengenezo ya mtambo huo. ili kuonesha ufanano au muendano ambao
Hata hivyo makampuni hayo yanatakiwa unaweza kusababisha mkanganyiko kwa
kumlipa fidia mmiliki wa ardhi hiyo na kama umma. Taarifa ya pingamizi ikishawasilishwa
kuna mgogoro wowote, mgogoro huo kwa Msajili wa Alama, Msajili atampatia
utatatuliwa na Mahakama yenye mamlaka. nakala mwombaji ambaye naye atatakiwa
Hivyo huwezi kumzuia mmiliki wa kuwasilisha maelezo kinzani juu ya taarifa
kampuni kuingia kwenye ardhi yako, kama yako ndani ya siku sitini za kuipokea.
utakuwa na tatizo unaweza kuwasiliana na Msajili atawasilisha maelezo kinzani kwako
mwanasheria wako ambaye atakusaidia na atapanga siku ya kuwasikiliza. Mara
kupinga Mahamani. atakapowasikiliza na kupitia ushahidi
uliotolewa kwake atatoa maamuzi iwapo
Kupinga usajili wa alama/nembo ya alama hiyo isajiliwe ama la. Kama hujaridhika
biashara
na maamuzi ya Msajili, unaweza kukata rufaa
Ninamiliki alama ya biashara nchini Mahakama Kuu. Kwa msaada zaidi tafadhali
Tanzania na hivi karibuni nimekutana wasiliana na mwanasheria wako.
na jarida la alama za biashara la Wakala
wa Usajili, Biashara na Leseni (BRELA)
Kipengele cha usuluhishi kwenye
likitangaza alama ya biashara ambayo
mkataba
kwa maoni yangu ni sawa, au inakaribiana Ninaingia mkataba wa usambazaji na
sana na alama yangu ya biashara. Ninataka kampuni ya kitanzania. Swali langu ni kwa
kuipinga. Tafadhali niongozeni juu ya nini nini kuwe na kipengele cha usuluhishi
cha kufanya. kwenye mkataba wakati Tanzania ina
11 Februari 2013 mfumo wa Mahakama? Kipengele
kinasomeka hivi: “Kutakuwa na msuluhishi
Sheria ya Alama/Nembo za Biashara
mmoja atakayeteuliwa na pande zote mbili
na Huduma inamtaka Msajili wa Alama za
kwa pamoja kwa gharama za pande zote”.
Biashara kutangaza alama ya biashara kwa Nini kitatokea kama hatutakubaliana juu ya
siku 60 kabla ya kuisajili. Madhumuni ya uteuzi wa msuluhishi?
kutangaza alama ni kutoa fursa kwa umma
11 Machi 2013
kupinga usajili wa alama hizo ikiwa ni sawa
au zinafanana na alama zao zilizosajiliwa Usuluhishi ni njia mbadala ya utatuzi
au zisizosajiliwa. Kwa hiyo ni wazo zuri kwa wa mgogoro na ni mbinu mojawapo ya
umma na mashirika mengine kufuatilia jarida usuluhishi nje ya Mahakama ambayo pande
la alama za biashara. Kuhusu pingamizi, zenye mgogoro zinawasilisha mgogoro
unaweza kupeleka pingamizi lako kwa Msajili huo kwa mtu mmoja au zaidi anayeitwa
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 49

msuluhishi ambapo pande hizo zinakubali zimeteua wasuluhishi ambao wamepewa


kufungwa na maamuzi ya msuluhishi ambayo uhuru wa kumteua mwamuzi au mtu wa tatu
yanaitwa tuzo. Ni mbinu ya usuluhishi na hawajamteua; (d) pale mwamuzi au mtu wa
ambapo msuluhishi anasikiliza kesi na kutoa tatu amekataa, hawezi au amefariki na nafasi
maamuzi ambayo kisheria yatazibana pande yake ipo wazi na wasuluhishi hawajaziba
zote. nafasi yake, yeyote kati yao anaweza kutoa
Usuluhishi una faida zake. Kutegemea notisi kwa pande zenye mgogoro au
na ukubwa wa makubaliano, kwa kawaida wasuluhishi, kulingana na mazingira, ya
utatuzi wa migogoro kwa usuluhishi ni kukubaliana kumteua msuluhishi, mwamuzi
njia rahisi, ya kuaminika, ya haraka, haina au mtu wa tatu.
usumbufu na ni bora zaidi tofauti na Sheria pia inaeleza kwamba iwapo uteuzi
Mahakama ambazo zinafungwa sana na haujafanyika ndani ya siku saba tangu siku
kanuni ambazo wakati mwingine ni mzigo ya kupata notisi, Mahakama inaweza, kwa
na ni ghali. Kupeleka mgogoro kwenye maombi ya upande uliotoa notisi na baada
usuluhishi hakuishushii hadhi Mahakama kwa ya kuusikiliza upande mwingine, kumteua
sababu bado unatakiwa uende Mahakamani msuluhishi, mwamuzi au msuluhishi wa
ili kusajili tuzo ili iweze kuwa amri ya tatu ambaye atakuwa na mamlaka sawa ya
Mahakama kwa ajili ya utekelezaji. Kwa sasa, kusikiliza mgogoro na kutoa tuzo/uamuzi
njia ya usuluhishi imeisaidia Mahakama kana kwamba ameteuliwa kwa idhini ya
kupunguza mrundikano wa kesi zinazosajiliwa pande zote. Pia tunakushauri uweke kipengele
Mahakamani. Kwa mikataba mikubwa, cha mahali pa kufanyia usuluhishi na lugha
tunapendekeza kipengele cha mkataba kiwe itakayotumika wakati wa usuluhishi. Kupeleka
na wasuluhishi wawili wanaoteuliwa na kila mgogoro kwenye usuluhishi hakuchukui haki
upande, na wao wamteue msuluhishi wa tatu yako ya kupeleka maombi yenye udharula
ambaye anaJulaikana kama mwamuzi, na Mahakamani, na Mahakama katika maamuzi
kuifanya idadi ya wasuluhishi kuwa watatu. yake yoyote itakayotoa itazingatia kwamba
Wakati mwingine hii inaonekana kuwa ghali pande zote zimekubaliana kusuluhishwa.
na hivyo pande zenye mgogoro huamua
kumteua msuluhishi mmoja tu. Deni dhidi ya Wizara
Nchini Tanzania usuluhishi unaongozwa
Niliiuzia Wizara nchini Tanzania vifaa vya
na Sheria ya Usuluhishi ambayo inatoa
matibabu na sijawahi kulipwa licha ya
mamlaka kwa Mahakama kumteua ahadi lukuki. Mwanasheria wangu anasema
msuluhishi pale ambapo hajateuliwa. Sheria kwamba kuishtaki Wizara moja kwa moja
hii inaipa Mahakama mamlaka ya kumteua haiwezekani. Sielewi kwa nini. Je, Serikali
msuluhishi, mwamuzi au msuluhishi wa inalinda kesi kama hizo? Tafadhali niongoze.
tatu katika mazingira yafuatayo: (a) pale 25 Machi 2013
ambapo makubaliano yanasema mgogoro
utawasilishwa kwa msuluhishi mmoja na Inawezekana kabisa kuishtaki Serikali kwa
baada ya mgogoro kuibuka pande zote mbili mujibu wa Sheria ya Mashtaka ya Serikali.
hawakubaliani na uteuzi wa msuluhishi; (ii) Kifungu cha 6 cha Sheria kinaeleza bila utata
kama msuluhishi aliyeteuliwa amepuuza au kwamba, bila kujali masharti ya vifungu
amekataa au hawezi kusuluhisha na nafasi vingine kwenye Sheria hii, kesi za madai
yake haijajazwa na pande zote hazijaziba zinaweza kufuguliwa dhidi ya Serikali kwa
nafasi; (c) pale ambapo pande zote mbili masharti ya kifungu hiki. (2) Hakuna kesi
50 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

dhidi ya Serikali itafunguliwa na kusikilizwa nchini Tanzania ikiwa ni kinyume na sheria


isipokuwa mlalamikaji amewasilisha mapema za hapa? Mwanasheria wangu anasema
kwenye idara au afisa anayehusika notisi kuwa kutokukata rufaa dhidi ya tuzo hiyo
siyo chini ya siku tisini juu ya nia yake ya kunaiweka kampuni yetu katika nafasi
kuishtaki Serikali, ikieleza msingi wa dai mbaya. Tafadhali niongoze.
lake dhidi ya Serikali na atatuma nakala 1 Aprili 2013
ya dai lake kwa Mwanasheria Mkuu wa
Usuluhishi unakusudia kuharakisha
Serikali. (3) Kesi zote dhidi ya Serikali, baada
upatikanaji wa haki. Kwa kawaida tuzo
ya kuwasilishwa kwa taarifa zifunguliwe
haiwezi kupingwa isipokuwa kwa kanuni
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na
za haki ya asili na pale ambapo wasuluhisi
nakala ya hati ya mashtaka ipelekwe kwenye
wamekuwa na utendaji mbovu. Tuzo pia
wizara ya Serikali, idara au afisa ambaye
haiwezi kutekelezwa kama ipo kinyume na
anatuhumiwa kutenda kosa hilo ambalo ni
sera ya umma na inakiuka sheria za nchi
msingi wa shtaka la madai. (4) Kesi zote dhidi
ambako utekelezaji utafanyika. Hayo yakiwa
ya Serikali zitafunguliwa Mahakama Kuu
kichwani mwako, kwa kuwa unadai tuzo
kwenye Kitengo cha Mahakama Kuu eneo
inakiuka sera ya umma na sheria za nchi, tuzo
ambapo dai limetokea. (5) Bila kujali masharti
inaweza kufutwa. Hilo pia limetamkwa chini
ya kifungu kidogo cha (3), Mwanasheria Mkuu
ya Sheria ya Usuluhishi ya Tanzania ambapo
anaweza, isipokuwa mtu mwingine anastahili
kushtakiwa, kushtakiwa au kuunganishwa kifungu cha 16 kinatamka wazi kwamba pale
kama mashtakiwa mwenza, kwenye kesi msuluhishi au mwamuzi ametenda vibaya au
yoyote dhidi ya Serikali. (6) Vifungu vya Sheria usuluhishi au tuzo imepatikana isivyo halali,
ya Watumishi wa Umma (Malipo ya Madeni) Mahakama inaweza kutengua tuzo hiyo.
vitatumika kwa afisa aliyeisababishia Serikali Kifungu cha 30 cha Sheria ya Usuluhishi
kupata hasara, gharama na fidia kutokana pia kinatamka kama ifuatavyo: Masharti ya
na kushindwa kwake kupata uwakilishi wa utekelezaji wa tuzo za kigeni; (1) Ili tuzo ya
kisheria kwenye kesi. Hivyo, kutokana na kigeni iweze kutekelezwa chini ya sehemu hii,
maelezo hapo juu unaweza kuona kwamba ni lazima: (a) iwe imetokana na mkataba wa
unahitaji kutoa notisi ya siku 90 kabla ya usuluhishi ambao ni halali chini ya sheria iliyo
kufungua shtaka. uongoza; (b) imetokana na baraza lililoundwa
chini ya makubaliano na liliundwa kwa
Kipengele cha usuluhishi kinazuia namna pande zilivyokubaliana; (c) imetolewa
kukata rufaa kwa kuzingatia sheria zinazoongoza
usuluhishi kiasi cha kuuwezesha upande
Niliingia mkataba na kampuni ambayo
wowote kuchukua hatua muhimu kubatilisha
imeingiza kipengele cha usuluhishi
tuzo kwenye chombo chenye mamlaka; (d)
kinachosema kwamba tuzo hiyo ni ya
mwisho, ina nguvu za kisheria na haiwezi imekamilika kwenye nchi ilikotolewa; na (e)
kukatiwa rufaa. Usuluhishi ulifanyika inahusu masuala ambayo ni halali kufanyiwa
nchini Kenya, ni wazi tuzo hiyo ukiisoma usuluhishi chini ya Sheria za Tanzania na
inakwenda kinyume na sera za umma utekelezaji wake ni lazima uwe haukinzani
na inakiuka sheria za Tanzania. Mkataba na sera ya umma au sheria za Tanzania. (2)
uliitaka kampuni yetu kutekeleza mkataba Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo
nchini Tanzania na kutumia sheria za hiki, tuzo ya kigeni haitatekelezwa chini ya
Tanzania. Je, tuzo hiyo inaweza kutekelezwa sehemu hii kama Mahakama imeridhika
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 51

kwamba (a) tuzo imebatilishwa kwenye Ikiwa uliingia kwenye aina hiyo ya
nchi ilikotolewa; au (b) mtu ambaye tuzo “makubaliano ya kutenganisha” na benki
inatakiwa kutekelezwa dhidi yake hakupewa yako, hapo benki inavunja wajibu wake. Hata
taarifa za usuluhishi kwa muda wa kutosha hivyo, kwa tujuavyo mazoea ya soko nchini
kumwezesha kupeleka utetezi wake au Tanzania na kwingineko, hatujawahi kukutana
alishindwa kutokana na sababu za kisheria na benki inayopokea fedha rundo na kuanza
na hakuwakilishwa vyema; au, (c) tuzo kuzitenganisha kabla ya kuziweka. Uhusiano
haijajibu maswali yote yaliyowasilishwa wa kawaida wa benki ya mteja ni kwa benki
au inamaamuzi juu ya mambo ambayo kulinda fedha zako. Unapaswa kushauriana na
yapo nje ya makubaliano ya usuluhishi: wanasheria wako lakini hakuna uwezekano
Isipokuwa kama tuzo haijajibu maswali yote wa kuiwajibisha benki.
yaliyowasilishwa Mahakama inaweza, ikiona
vyema, ama kuahirisha utekelezaji wa tuzo Kuvunja mkataba
au kuamuru utekelezaji wake kwa masharti Ninataka kuvunja mkataba ambao niliingia.
ya kutoa dhamana kwa mtu anayeomba Ni sababu gani za kisheria ambazo
kutekeza tuzo hiyo kama Mahakama itaona ninaweza kuzitumia ili kuvunja?
inafaa. (3) Kama mtu anayepinga utekelezaji 8 Julai 2013
wa tuzo ya kigeni anathibitisha kwamba kuna
sababu zaidi ya kutokuwepo kwa masharti Mikataba inatakiwa kuheshimiwa na
yaliyoainishwa kwenye aya (a), (b) na (c) ya sheria inakusudia kuhakikisha kwamba pande
kifungu kidogo (1) cha kifungu hiki, au uwepo zinazoingia mkataba zinaheshimu kusudio
wa masharti yaliyoainishwa kwenye aya ya (b) la mkataba ili kuhakikisha kwamba biashara
na (c) ya kifungu kidogo (2) cha kifungu hiki hazianguki. Sheria ya Mikataba, hata hivyo,
kinachompa haki ya kupinga uhalali wa tuzo, inawapa wahusika katika mkataba sababu
Mahakama inaweza, kama itaona inafaa, ama nyingi za kuvunja mkataba ikiwa tu sababu
kukataa kutekeleza hukumu ama kuahirisha hizo ni halali. Unaweza kuvunja mkataba
usikilizaji hadi kupita kwa muda ambao kama uliuingia kwa shurutisho, kudanganywa,
Mahakama itaona unafaa. Kabla hujajiamini yaani upande mwingine ulikuficha mambo ya
kupita kiasi kuhusu maoni yako, unatakiwa msingi kuhusu mkataba, ubatili wa mkataba
umtafute mwanasheria wako akuongoze. au kiini cha mkataba, kukosea jambo, yaani
akili za pande za mkataba hazikuendana,
Benki haifuati maagizo kama ni mdogo/mtoto, yaani yupo chini
ya miaka 18, kuvunja masharti ya mkataba,
Ninauza vocha za simu na kuweka
fedha zangu kwenye benki moja kubwa masharti ya awali hayakutekelezwa, n.k.
huko Mtwara. Ninapokwenda benki, Tunashauri mwanasheria wako akuongoze
nategemea msarifu kutenganisha noti za kwenye mkataba wako kabla hujafanya
Shilingi 500, 1000, 2000 na 5000. Tatizo chochote.
ambalo linanikabili kwa sasa ni kwamba
Kukodisha alama ya biashara
meneja mpya ameniambia nizitenganishe
mwenyewe kwa sababu inampotezea Ninamiliki alama fulani ya biashara ambayo
muda msarifu. Nashindwa kuelewa kwa inakua sokoni. Nimefuatwa na wageni
nini benki haitaki kufanya kazi yake. Je, kutoka nje ya nchi ambao wanataka
ninaweza kuishtaki benki? kutumia alama yangu ya biashara na
3 Juni 2013 wameniomba niwauzie. Sitaki kuuza alama
52 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

yangu ya biashara. Ninaweza kuzikodishia kwamba pande au wakili wake au wote,


kampuni hizi alama yangu ya biashara ili kama wanawakilishwa, wataarifiwa kwa
niendelee kuimiliki na kuifurahia baada ya kutumia Fomu Na. 3 iliyopo kwenye Jedwali,
mkataba wa kuikodisha kuisha? Tafadhali na watahudhuria kipindi cha upatanishi,
niongoze. isipokuwa kama Mahakama itaamuru
1 Julai 2013 vinginevyo.
Kutokana na maelezo hapo juu, unaweza
Una wazo jema. Kwa bahati nzuri, Sheria
kuona kwamba upatanishi ni lazima. Hata
ya Alama za Biashara na Huduma inamruhusu
mmiliki wa alama ya biashara kuikodisha kwa hivyo, Mahakama inakuruhusu kumtuma
mtu mwingine. Ila, inabidi uelewa kwamba mwakilishi ambaye atawasiliana na wewe ili
ukodishwaji huo ni lazima usajiliwe kwa uweze kukubali au kukataa upatanishi. Pia
Msajili wa Alama za Biashara. Mchakato wa elewa kwamba, upatanishi hauharibu kesi
ukodishaji siyo mgumu. Wanasheria wako yako hivyo usijali kwa sababu upatanishi
wanaweza kukuongoza zaidi. unafanyika kwa usiri.

Upatanishi mahakama ya biashara Kudanganywa na benki ya kigeni

Nimefungua kesi Mahakama ya Biashara Benki ya kigeni ilikuja Tanzania na


Masjala ya Dar es Salaam dhidi ya mtu kuniahidi faida kubwa kwa uwekezaji
ambaye sitaki kumuona tena kwenye mpya wa huduma/bidhaa ambazo ilikuwa
maisha yangu. Nimeshangaa kwamba inazianzisha Mashariki ya Mbali. Niliona
Mahakama imeamuru kwamba tujaribu huduma/bidhaa hiyo ina faida kubwa lakini
kutatua jambo hilo kwa njia ya upatanishi. mwishowe nilijikuta tayari nimepoteza
Je, hiyo ni lazima, ukizingatia sitaki asilimia 30 ya uwekezaji wangu. Kulikuwa
kupatana na huyu mhuni? na mambo ya msingi sana ambayo benki
22 Julai 2013 haikuniweka wazi. Je, ninaweza kushtaki?
28 Oktoba 2013
Kanuni za Mahakama ya Biashara
zinatamka kwamba mtu ambaye anaingia Kwanza kabisa, ni batili kwa benki
kwenye upatanishi atakuwa na mamlaka kushawishi biashara nchini Tanzania. Kama
ya mwisho ya kupatana juu ya suala lolote wewe ni Mtanzania, pia ni batili kwako
wakati wa upatanishi. Kanuni zinaendelea kufanya shughuli za kibenki nje ya nchi
kusema kwamba, mtu anayehitaji idhini ya bila idhini ya Benki Kuu ya Tanzania. Kwa
mtu mwingine kabla ya kupatana, kabla ya kuzingatia maelezo hapo juu, kama unaamini
muda wa kuanza upatanishi, atapanga namna kwamba benki ilikudanganya, una kesi dhidi
ya kuwasiliana na mtu huyo wakati wote wa yake na unaweza kuishtaki. Hata hivyo kesi
upatanishi, bila kujali kama utafanyika wakati yako itazingatia kipengele cha uchaguzi wa
wa saa za kazi au baada ya saa za kazi. sheria kilichopo kwenye mkataba ulioingia,
Kama kesi haikutatuliwa au ilifutwa ambapo uwezekano mkubwa itakuwa
chini ya kanuni hizi, Mahakama itazielekeza ni kufuata sheria za nchi ambako benki
pande zote kwenda kwenye upatanishi imesajiliwa. Kabla ya kushtaki tunapendekeza
baada ya kutoa amri hiyo, Mahakama umuone mwanasheria mbobevu kwenye
itamteua mpatanishi ambaye, ndani ya siku masuala ya benki za kimataifa. Ni lazima
7 baada ya kuteuliwa, atapanga tarehe ya uelewe kuwa hakuna uwekezaji usio na
kwanza ya upatanishi. Kanuni pia zinatamka vikwazo. Msemo wa zamani (wa kihasibu) ni
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 53

sahihi, kwamba: “Kadiri vikwazo vya biashara mwaka mmoja sasa hawajanilipa. Kiasi
vinavyokuwa vingi, ndivyo biashara hiyo ninachowadai hivi sasa kinakaribia
inavyotegemewa kutoa faida kubwa”. mamilioni ya Dola na nimekuwa napewa
ahadi hewa. Nilitoa onyo la mwisho kwa
Upande mwingine kushindwa kumteua mamlaka husika lakini niliambiwa niende
msuluhishi kuonana na mtu mkubwa ambaye mara
ya kwanza aliniambia nitalipwa, lakini
Tupo kwenye mgogoro na upande mwingine
baada ya kujibu kwamba siamini jambo
ambapo mkataba unatoa usuluhisi wenye
hili na kwamba nitasitisha usambazaji
wasuluhishi watatu. Mimi nimeshamteua
na kuwashtaki, alinitishia kwamba kama
msuluhishi wangu lakini upande mwingine
nitafanya hivyo, nitashtakiwa chini ya Sheria
unapiga chenga/unachelewa kumteua
ya Makosa ya Uhujumu Uchumi. Kwa ufupi
msuluhishi wake kwa miezi 2 sasa. Je, nifanye
alisema kwamba chini ya sheria za Tanzania,
nini?
hasa sheria hii, bidhaa hizi ni muhimu
3 Februari 2014 kwenye mahospitali na sina hiari zaidi ya
Kifungu cha cha Sheria ya Usuluhishi kuendelea kuzisambaza. Pia ameniambia
kinaeleza wazi kwamba pale mkataba kwamba kosa hili halina dhamana. Nifanye
nini?
unaposema mgogoro utasuluhishwa na
wasuluhishi watatu, kila upande kuteua 3 Februari 2014
msuluhishi mmoja na msuluhishi wa watatu Hii ni mara yetu ya kwanza kusikia staili
kuteuliwa na wasuluhishi wawili walioteuliwa hiyo juu ya wajibu wa kulipa kimkataba. Kama
na pande mbili, isipokuwa kama kutakuwa alichokisema afisa huyo ni kweli, basi muuzaji
na nia tofauti – kama upande mmoja yeyote wa vitu muhimu kwa uchumi, iwe
umeshindwa kumteua msuluhishi ndani nishati, maji, au ulinzi hawezi kushtaki wala
ya siku saba baada ya upande mwingine kudai. Na hakuna mtu atakayekuwa tayari
kumteua msuluhishi wake, na ameupatia kufanya biashara na Serikali ya Tanzania na
upande unaokaidi notisi ya kufanya uteuzi, itakuwa inakiuka misingi muhimu ya sheria za
upande ulioteua msuluhishi unaweza mikataba.
kumteua msuluhishi huyo kuwa msuluhishi Kwa kujibu swali lako, tukichukulia
pekee kwenye mgogoro na tuzo ya umetupatia maelezo sahihi, hakuna
msuluhishi huyo itazibana pande zote mbili kinachokuzuia kusitisha huduma, kudai malipo
kama kana kwamba aliteuliwa kwa idhini na kushtaki kwa mujibu wa mkataba wa
ya pande zote. Hivyo, kwa kuwa upande uuzaji. Uhujumu uchumi umeelezewa chini
mwingine hauteui msuluhishi wake, unaweza ya sheria na unahusu vitendo vilivyofanyika
kuendelea na msuluhishi mmoja na tuzo bila sababu za msingi na kwa malengo ya
itaubana upande wa pili bila kujali kwamba kuzorotesha uchumi au maslahi ya Tanzania
kipengele cha usuluhishi kilikuwa kinatamka au vinavyoweza kuharibu, kuzuia au kuingilia
wasuluhishi watatu. Mwanasheria wako utoaji wa hudumu muhimu au uendeshaji
anaweza kukuongoza zaidi. wake.
Kutokana na tafsiri hiyo, huwezi kushtakiwa
Kutishiwa uhujumu uchumi
chini ya sheria hii kwa kuwa unadai kihalali
Mimi ni muuzaji wa bidhaa za madawa fedha zako chini ya mkataba wa uuzaji/
muhimu pamoja na mashine kwenye usambazaji. Kama ungekuwa unafanya hivyo
baadhi ya hospitali za Serikali na kwa kinyume na sheria kwa lengo la kuzorotesha
54 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

uchumi au maslahi ya Tanzania, sheria hiyo fedha za kulipa? Je, Serikali inazingatia kwa
ingetumika. kiasi gani usuluhishi?
Kuhusu dhamana, tafadhali elewa 17 Februari 2014
kwamba hili ni kosa lenye dhamana. Hata
hivyo, dhamana haitatolewa kwenye Serikali inaingia mikataba mingi tu
mazingira yafuatayo: (a) kama inaonekana ambayo usuluhishi ni njia mojawapo
kwamba mtuhumiwa hapo awali aliwahi inayotumika kutatua migogoro. Tanzania pia
kuhukumiwa kwa kifungo cha miaka inayozidi imeridhia mikataba ya kimataifa inayotambua
mitatu; (b) kama mtuhumiwa hapo awali utekelezaji wa tuzo zinazotokana na
aliwahi kupewa dhamana na Mahakama usuluhishi.
na alishindwa kutii masharti ya dhamana au Kifungu cha 30 cha Sheria ya Usuluhishi
alitoroka; (c) kama mtuhumiwa ameshtakiwa kinatoa masharti ya utekelezaji wa tuzo
kwa kosa la uhujumu uchumi linalodaiwa za kigeni kama ifuatavyo; (1) Ili tuzo
kufanyika wakati mtuhumiwa ameachiwa ya kigeni iweze kutekelezwa chini ya
kwa dhamana na Mahakama; (d) kama sehemu hii, ni lazima: (a) iwe imetokana
itaonekana mbele ya Mahakama kwamba na mkataba wa usuluhishi ambao ni
ni muhimu mshtakiwa awekwe mahabusu halali chini ya sheria iliyouongoza; (b)
kwa ulinzi au usalama wake; (e) kama kosa imetokana na baraza lililoundwa chini ya
ambalo mtu anashtakiwa nalo linahusu
makubaliano na liliundwa kwa namna
mali yenye thamani inayozidi Shilingi
pande zilivyokubaliana; (c) imetolewa kwa
milioni kumi isipokuwa kama mtu huyo
kuzingatia sheria zinazoongoza usuluhishi
ataweka dhamana ya mali inayolingana
kiasi cha kuuwezesha upande wowote
na nusu ya thamani ya mali iliyohusika na
kuchukua hatua muhimu kubatilisha tuzo
inayobaki imewekewa dhamana; na (f) Kama
ameshtakiwa kwa kosa lililo chini ya Sheria ya kwenye chombo chenye mamlaka; (d)
Madawa Hatarishi. imekamilika kwenye nchi ilikotolewa; na (e)
inahusu masuala ambayo ni halali kufanyiwa
Utekelezaji wa tuzo ya usuluhishi nchini usuluhishi chini ya Sheria za Tanzania na
Tanzania utekelezaji wake ni lazima uwe haukinzani
Tupo kwenye majadiliano na Serikali na sera ya umma au sheria za Tanzania. (2)
kuhusu mradi wenye thamani ya mabilioni Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo
ya Dola ambao tunataka uwe na kipengele hiki, tuzo ya kigeni haitatekelezwa chini ya
cha usuluhishi kinachoruhusu kutumia sehemu hii kama Mahakama imeridhika
ama sheria za Kituo cha Kimataifa cha kwamba (a) tuzo imebatilishwa kwenye
Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) nchi ilikotolewa; au (b) mtu ambaye tuzo
au Mahakama ya Kimataifa ya Biashara inatakiwa kutekelezwa dhidi yake hakupewa
(ICC). Je, Serikali ya Tanzania inakubali
taarifa za usuluhishi kwa muda wa kutosha
kufanya usuluhishi na kama jibu ni ndiyo,
kumwezesha kupeleka utetezi wake au
je tuzo husika inaweza kutekelezwa
nchini Tanzania? Ni sababu zipi zinazoweza alishindwa kutokana na sababu za kisheria
kutumika kukataa tuzo ya usuluhishi na hakuwakilishwa vyema; au (c) tuzo
ya kigeni? Kama tukiishinda Serikali, je haijajibu maswali yote yaliyowasilishwa
inaweza kudai kwamba tuzo inakwenda au inamaamuzi juu ya mambo ambayo
kinyume na sera ya umma hasa ikiwa haina yapo nje ya makubaliano ya usuluhishi:
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 55

Isipokuwa kama tuzo haijajibu maswali yote hili siyo jambo ambalo Tanzania inaweza
yaliyowasilishwa Mahakama inaweza, ikiona kulimudu katika hatua ya sasa ya ushindani
vyema, ama kuahirisha utekelezaji wa tuzo wa kimataifa. Tunashauri upate ushauri wa
au kuamuru utekelezaji wake kwa masharti kitaalam/maalum kutoka kwa mwanasheria
ya kutoa dhamana kwa mtu anayeomba wako.
kutekeza tuzo hiyo kama Mahakama itaona
inafaa. (3) Kama mtu anayepinga utekelezaji
Mgogoro wa mpaka kwenye eneo la
utafutaji gesi
wa tuzo ya kigeni anathibitisha kwamba kuna
sababu zaidi ya kutokuwepo kwa masharti Tuna mgogoro na jirani ambaye ni mmiliki
yaliyoainishwa kwenye aya (a), (b) na (c) ya wa kitalu/eneo la utafutaji gesi na ametishia
kifungu kidogo (1) cha kifungu hiki, au uwepo kupeleka mgogoro wetu kwa Kamishna
wa masharti yaliyoainishwa kwenye aya ya wa Nishati na Petroli. Je, Kamishna huyu
(b) na (c) ya kifungu kidogo (2) cha kifungu ana mamlaka ya kuamua mgogoro huu, na
hiki kinachompa haki ya kupinga uhalali kama ndiyo, je maamuzi yake yanaweza
wa tuzo, Mahakama inaweza, kama itaona kukatiwa rufaa?
inafaa, ama kukataa kutekeleza hukumu 24 Februari 2014
ama kuahirisha usikilizaji hadi kupita kwa
muda ambao Mahakama itaona unatosha ili Majibu ya maswali yako yote mawili ni
kuuwezesha upande huo kuchukua hatua ndiyo. Kamishna wa Masuala ya Nishati na
muhimu kuliwezesha baraza lenye mamlaka Petroli anaruhusiwa kuamua migogoro kama
kubatilisha tuzo. hiyo. Pia, ni kweli, maamuzi yake yanaweza
Jambo jingine ambalo umelionesha, na kukatiwa rufaa. Hili limeelezwa chini ya
ambalo mara nyingi linatumika ni sera ya Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji Petroli, 1980,
umma ya kwamba iwapo tuzo itaruhusiwa ambapo inaeleza ifuatavyo:
kutekelezwa kwenye nchi ambayo inakwenda Kamishna anaweza kufanya uchunguzi
kutekelezwa ni kinyume na sera ya umma. juu ya na kuamua kuhusu migogoro
Kwa ujumla, kutokuwepo kwa fedha siyo baina ya watu wanaojihusisha na utafutaji
suala la sera ya umma na hivyo kuzuia au uendeshaji, ama miongoni mwao
utekelezaji wa tuzo ya usuluhishi. Kama wenyewe au miongoni mwao na pande
itathubutu kufanya hivyo, Tanzania itakuwa nyingine (isipokuwa Serikali) zisizohusika,
inavunja mikataba ya kimataifa ya usuluhishi. kuhusinana na (a) Mipaka ya eneo lolote la
Kuhusu Serikali inaupa uzito gani utafutaji au uendeshaji; (b) kitendo chochote
usuluhishi, tafadhali elewa kwamba kilichofanyika au kuacha kufanyika, au
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kinachodaiwa kufanyika au kutokufanyika,
inajishughulisha na mashauri mengi tu katika, au kuhusiana na utafutaji uendelezaji;
ya usuluhishi nje ya nchi, na inauchukulia (c) makadirio na malipo ya fidia kwa mujibu
usuluhishi kwa uzito mkubwa. Pamoja na wa Sheria hii; au (d) masuala mengine yoyote
kuupa usuluhishi uzito mkubwa, kama ambayo yapo kwenye sheria.
Serikali haitakwenda kwenye usuluhishi Mtu yeyote ambaye hajaridhika na
au ikishindwa kusimamia mchakato wa maamuzi, tuzo au amri ya Kamishna
usuluhishi vizuri, itaharibu sifa ya nchi iliyotolewa kwa mujibu wa sehemu hii
kwenye nyanja za kimataifa za biashara. Na anaweza kukata rufaa kwenda Mahakama
56 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

Kuu ndani ya siku 60 baada ya kutolewa kwa Kumshtaki Bwana Isaac Newton leo
maamuzi, tuzo au amri. hii haiwezekani kwa kuwa huna haki ya
kumshtaki. Pia, hakupandikiza fomula hii
Wanasayansi wa Magharibi kwetu na hivyo hauna haki ya kumshtaki kwa
wanadanganya uduni wa Afrika namna yoyote ile. Uwezekano wa kuwashtaki
Mimi ni mwanasayansi na nimegundua warithi wake pia uko mbali sana. Pamoja
mbinu/siri ambayo mataifa ya Magharibi na utafiti wako kuhusu F=MA, unaweza pia
yanaitumia kuhakikisha kwamba Afrika kuangalia mambo mengine yaliyopelekea
tunaendelea kubaki nyuma. Ninakaribia matatizo ya Afrika.
kutoa chapisho kwenye moja ya jarida Pia tunakushauri uzungumze na
maarufu kwamba fomula ya Kani = wataalamu wengine kwenye tasnia/fani
Tungamo X Mchapuko (F=MA) inapotosha yako ambao wanaweza kuoanisha F=MA
na haina uhalisia kwa Afrika. Kutumia kwetu na matatizo ya Afrika. Tunashindwa kuona
fomula hii kunatufanya tusiendelee. Nifanye uhusiano wowote na tumepata mtanziko.
nini kuiokoa Afrika? Ninaweza kumshtaki
mvumbuzi? Hakuna kampuni Tanzania yenye
4 Agosti 2014 uwezo wa kutukatia bima

Kwanza tunapenda kukushukuru kwa Sisi ni kampuni kubwa nchini Tanzania na


kutuandikia kutoka Gaborone. Kama jumla ya hatari na hasara zote tunazotaka
ilivyo kawaida yetu, tutakueleza ukweli, kuzikatia bima ni kubwa kuliko uwezo wa
kifedha/mtaji wa kampuni zote za bima
au kile tunachokiamini kuwa ni ukweli.
za ndani ukiziunganisha pamoja. Hatuna
Tunatumaini majibu yetu ya kawaida na
amani kukata bima ya ndani. Je, ni lazima
kweli hayatakukasirisha na utaendelea kuwa
kukata bima ya ndani? Tunaweza kujikatia
msomaji wa safu yetu.
bima wenyewe? Tunawezaje kulishughulikia
Fomula ya F=MA imekuwepo kwa jambo hili?
mamia ya miaka iliyopita, na ilivumbuliwa
25 Agosti 2014
na Bwana Isaac Newton. Sheria ya Newton
imethibitishwa kwa kufanyiwa utafiti na Sheria ya Bima iko wazi na inataka hatari
uchunguzi kwa zaidi ya miaka 200, na ni na hasara zote kukatiwa bima na makampuni
kipimo bora kabisa cha mienendo yetu ya ya nchini Tanzania. Kifungu cha 133 cha sheria
kila siku ya maisha. Fomula hii imefanya kazi hii kinatamka kwamba (1) Waziri, kwa kanuni,
katika miradi yote mikubwa ya kiuhandisi ataelekeza kwamba sehemu ya bima au bima
ambayo tumewahi kuisoma. Kimsingi fomula zote zinazogusa Watanzania au makampuni
hii ni kati ya fomula zinazotumika sana na yaliyopo Tanzania ya aina yoyote kukata bima
imefanya kazi ulimwenguni kote. Haina kwa makampuni ya Kitanzania. (2) Iwapo
mipaka ya kijografia wala kisiasa, na inafanya aina ya bima inayotakiwa kukatwa kwenye
kazi kwenye mazingira yote na bara lolote kampuni ya ndani haipatikani kwa mtu
duniani. anayetaka bima hiyo, mtu huyo atakata bima
Tunashindwa kuona mantiki ya swali lako ya kampuni isiyo ya Kitanzania isipokuwa
kivipi unadai kwamba fomula imeisababisha kwamba (a) mtu huyo atapata kwanza idhini
Afrika kuwa nyuma. Hujatoa uthibitisho ya maandishi ya Kamishna; na (b) anatekeleza
wowote kuhusu dai lako na tunaliona halina masharti ya kifungu cha 140. (3) Hakuna
mashiko kusema kweli. chochote kwenye kifungu hiki kitakachoathiri
Sheria za Biashara, Migogoro ya Kibiashara na Haki Miliki • 57

matakwa ya vifungu vya sheria kuhusu fedha Kamishna anaelekeza madai yalipwe
za kigeni zitakazo kuwa zikitumika wakati huo
nchini Tanzania au chini ya udhibiti wa Benki Je, Kamishna wa Bima anaweza kuilazimisha
Kuu ya Tanzania. kampuni ya bima kulipa madai hata
kama hayalipiki? Je, ni kitu gani ambacho
Zaidi, kifungu cha 140 kinaeleza kwamba
kampuni ya bima inaweza kufanya dhidi
sera yoyote ya bima inayomgusa Mtanzania
ya uamuzi huo? Je, Kamishna anaweza
au inayoigusa kampuni iliyosajiliwa Tanzania,
kupindua uamuzi wa Mtendaji Mkuu wa
ukiachilia mbali kampuni ya bima iliyosajiliwa
Kampuni au bodi?
chini ya Sheria hii, inayotolewa na kampuni
22 Septemba 2014
ya bima ya kigeni itatolewa kupitia ofisi za
wakala wa bima aliyesajiliwa Tanzania. Kamishna wa Bima ana jukumu la
Kutokana na maneno ya vifungu tajwa kusimamia sekta ya bima nchini, pamoja
hapo juu, ingawa ni lazima kukata bima kwa na kazi nyingine kama ilivyoelezwa chini
makampuni ya bima ya ndani, una hiari ya ya Sheria ya Bima, Namba 10 ya 2009. Yeye
kupata msamaha wa kufanya hivyo kwa si meneja wa kampuni ya bima wala si
kumwandikia Kamishna wa Bima ili kupata mkurugenzi na hawezi kupindua maamuzi
idhini yake huku ukieleza kwa nini hatari yoyote yanayohusu madai yasiyolipika ya
husika haiwezi kukatiwa bima nchini. Kukosa kampuni ya bima, Mtendaji Mkuu wake au
uwezo kwa kampuni za ndani inaweza kuwa bodi.
ni sababu nzuri lakini kampuni za ndani za Hii ni mara yetu ya kwanza tunasikia
bima zinaweza kuikabili hatari kupitia wakala malalamiko kama hayo dhidi ya Kamishna
wa ndani. lakini ikiwa unashurutishwa/unalazimishwa
Hivyo, huwezi kujikatia bima wewe kulipa, unaweza kukata rufaa ya uamuzi huo
mwenyewe. Tunakusihi sana uwasiliane kwa Baraza la Bima chini ya kifungu cha 126(4)
na wakala wako wa bima na/au Kamishna ambacho kinasema kwamba “mtu ambaye
wa Bima ili kuona kwamba hatari husika hajaridhika na uamuzi wa Kamishna chini
inalindwa na sheria za ndani, vinginevyo ya Sheria hii anaweza, kwa muda wa mwezi
unaweza kupata changamoto wakati wa mmoja kuanzia tarehe ambayo amepewa
kuwasilisha madai ya fidia. uamuzi huo kwa maandishi, kukata rufaa
Pia, unaarifiwa kwamba bila idhini ya kwa njia ya maombi ya maandishi kwa Baraza
Kamishna, fedha utakayolipwa na kampuni ambalo linaweza, kuidhinisha, kubadilisha,
ya bima ya kigeni kama fidia ya madai yako, kupindua au kutofautiana na uamuzi huo.
itatozwa kodi nchini kwa sababu ulikata bima Hatua hii lazima ifanyike ndani ya miezi miwili
kwa kukiuka Sheria ya Bima. tangu siku ya kuwasilisha ombi hilo.”
Mwisho, njia mojawapo ya kuepuka Ikiwa bado hujaridhishwa na maamuzi
kukata bima kwenye kampuni za ndani ya Baraza kwenye hoja za kisheria, unaweza
ni kutumia kampuni mama kukatia bima kukata rufaa Mahakama Kuu ndani ya mwezi
mali zake zilizopo nje ya nchi. Hili haliwezi mmoja tangu uamuzi huo ulipowasilishwa
kuJulaikana kwenye sheria yetu kwa sababu kwako.
ni maslahi yako yaliyopo nje ya nchi. Hata Ikiwa unachosema ni kweli, ambacho
hivyo, hili linatakiwa kushughulikiwa kwa tunadhani kinashangaza, tunaamini una
kufanya uchambuzi wa kina wa jambo husika, nafasi nzuri ya kufanikiwa. Tafadhali kumbuka
mtaalam wako wa bima anaweza kukuongoza kuwa uamuzi wa Kamishna unaokusudia
juu ya hili. kuukatia rufaa ni lazima uwe kwenye
58 • Maswali na Majibu na FB Attorneys

maandishi. Haitawezekana kwenda kwenye


Baraza kwa misingi tu ya shinikizo lolote,
mfano, la maongezi ya simu na Kamishna.
Haki za Walaji • 59

Haki za Walaji

Kuna namna nyingi ambazo haki za walaji zinaweza kukiukwa na wafanyabiashara ambao
kimsingi wanapaswa kuzijua vyema. Vivyo hivyo, wakati mwingine walaji nao, kwa kubahatisha,
hushtaki pasipokuwa na madai yoyote ya msingi. Katika sura hii, tumeweka mifano mingi ya
tabia zote hizi mbili. Watu hudai haki katika hali zote mbili, lakini siyo wakati wote haki na madai
huwa ni kitu kimoja.

You might also like