You are on page 1of 12

SIFA ZA 13 ZA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


NDUGU BERNARD KAMILLIUS MEMBE
Na
1.

Sifa

Maelezo ya Mgombea

Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza Ndugu Bernard Membe amepata uzoefu mkuwa katika nafasi mbali
Taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika mbali za Serikali, Chama na Umma kama ifuatavyo:Uongozi wa shughuli za Serikali umma na
taasisi.

Mpaka kufikia harakati za uchaguzi Mkuu wa 2015 amekuwa


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa
takribani miaka nane na nusu kuanzia Januari 2007. Ni Waziri
wa pili ambaye ameshika wadhifa huo kwa muda mrefu katika
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akitekeleza Diplomasia ya
uchumi kwa vitendo; kutafuta wawekezaji kutafuta misaada na
kufuatiwa madeni, kufungua Balozi mpya, kutatua migogoro na
ulinzi wa amani.
Alikuwa Naibu Wazira wa Nishati na Madini kati ya Octoba
2006 hadi Januari 2007. Akiwa Nishati na Madini alianzisha
kitengo cha kusuluhisha migogoro kati ya wachimbaji madini
wakubwa na wadogo.
Alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia Januari
1

hadi Octoba 2006. Akiwa Wizara ya Mamo ya Ndani


alishughuikiwa

kupunguza

msongamano

wa

wafungwa

magereza na mahabusu rumande.


Ameliwakilisha Jimbo la Mtama lililopo Mkoani Lindi kama
Mbunge kwa Miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 2000 hadi
2015.
Amefanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Canada kwa
miaka 8 kuanzia mwaka 1992 hadi 2000 kama mshauri wa
Balozi na kwa nyakati mbali mbali alikaimu Ubalozi.
Alifanya kzi katika Ofisi ya Rais, Idara ya Usalama wa Taifa
kama mkuu wa Sekretariati kwa takribani miaka 8.
2.

Awe mwadilifu, asiyetiliwa shaka juu ya

Ndugu Bernard Membe hana tabia wala hulka na hajawahi

vitendo vya uadilifu mbele ya uso wa jamii

kuwa na tuhuma wala kashfa ya ubadhilifu, matumizi mabaya

ya Watanzania na awe mwenye hekima na

ya ofisi ya umma, rushwa ala ufisadi. Aidha amekuwa mstari

busara.

wa mbele katika kukemea wazi wazi aina zote za wizi, rushwa,


ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma. Vile vile,
Ndugu Bernard Membe hakusita kuchukua hatua pale ambapo
walio chini yake wamethiitika kufanya vitendo visivyo vya
kiadilifu.
Kwa hekima na busara alizojaliwa na Mwenyezi Mungu, mara
2

kadhaa ameaminiwa na Mawaziri wenzake kushika nafasi za


Uenyekiti kwenye SADC,Umoja wa Afrika (AU) na kwa sasa
ni Mwenywkiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki na Jumuiya ya Madola.
Ndugu Membe, mara kadhaa amealikwa kutoa mihadhara ya
kitaaluma kwenye vyuo vikuu na makundi tofauti ya wataalam
kwa nyakati mbalimbali.
3

Awe na angalau kiwango cha elimu ya chuo


kikuu au elimu inayolingana na hiyo.

Ndugu Bernard Membe ana Shahada ya Uzamili ya Masula ya


Siasa, Usuluhishi wa Migogoro, Uchumi na Mahusiano ya
Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha The Johns Hopkins kilichpo
Washngton DC, Marekani kati ya mwaka1990 mpaka 1992.
Aidha,Ndugu Bernard Membe ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam, Mlimani ambapo alisoma shahada ya kwanza ya
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa kuanzia mwaka 1980 mpaka
1984.
Ndugu Membe ni mhitimu wa kozi ya Usalama wa Taifa ya
Mwaka 1978 nchini Uingereza.
Ndugu membe amesoma pia katika Chuo Kikuu cha Chama cha
Mapinduzi, Kivukoni kati ya mwaka 1979 na mwaka 1980.
3

Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa

Ndugu Membe, ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na

kudumisha, kuimarisha na kuendeleza

Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ni Wizara ya Muungano kwa

Muungano wetu, umoja wetu, amani na

takribani nane na nusu akiwakilisha maslahi ya Tanzania Bara

utulivu wetu na mshikamano wa Kitaifa.

ya Visiwani kama inavyoelezwa na Katiba ya Jamhuri na Ilani


ya uchunguzi ya CCM. Kwa miaka yote hii, Ndugu Membe,
amekuwa akiwajibika kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Ali Mohamed
Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwasilisha
taarifa na kupokea maelekezo ya kuboresha mahusiano ya
Tanzania na nchi za nje. Ndugu Membe, aliifanya kazi hii kwa
dhamira makini ya kuhakikisha maslahi ya pande zote mbili za
muungano nje ya Tanzania yanasimamiwa ipasavyo. Aidha,
akiongoza Wizara hii ya Muungano, amejitahidi kuhakikisha
idadi ya Mabalozi wa Watumishi wengine

wa Wizara ya

Mambo ya Nje waliopo makao makuu na nchi za nje katika


Balozi za Tanzania inahusisha pande zote mbili kwa kiwango
cha juu.
Ndugu Membe, kama Waziri wa Mambo ya Nje ameshiriki
mikutano ya kila mara ya kamati ya kero za Muungano chini ya
Ofisi ya Makamu ya Rais na kutoa ufafanuzi juu ya masuala
4

yote yanayohusu mahusiano ya nchi za nje katika kudumisha


Muungano wa Tanzania. Kamati za kero za Muungano zilikuwa
zina lengo la kuhakikisha maeneo yote ambayo yana kero
zinazoyumbisha Muungano yanafanyiwa kazi na Mawaziri wa
sekta husika.
Ndugu Membe amekuwa akishauri na kuunganisha Jumuiya za
Watanzania wanaoishi nje pamoja na Balozi zetu ili kuwa za
kitaifa.
Vilevile, mwaka 1984 Ndugu Membe aliongoza jopo la
wanachuo wanafunzi wa CCM kwenye kufanya utafiti wa
kutuliza vuguvugu la mfarakano huko Zanziba.
Ndugu

membe,

binafsi

amesikika

kwenye

majukwaa

mbalimbali likiwemo Bungu la Jamhuri ya Muungano na


vilevile Bunge Maalum la Katiba akihubiri umuhimu wa
Muungano na Umoja wa Kitaifa.
Ndugu Membe ameshikiri kikamilifu katika kuchangia
amani, utulivu na maendeleo kwa kuboresha ujirani
mwema na nchi jirani.
5.

Awe

mwepesi

wa

kuona

mbali,

Ndugu Membe ameongoza Wizara ambayo ni nyeti kutokana na

asiyeyumbishwa na mwenye uwezo wa

jukumu lake la kusimamia na kuwakilisha nchi duniani kote.


5

kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala

Katika Uongozi wake alijikita kwenye usuluhishi wa migogoro

nyeti na muhimu ya Taifa kwa wakati

ya kisiasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na SADC. Mara

unaofaa.

kadhaa amewajibika kutoa msimamo kwa niaba ya Tanzania


bila

kutetereka

ili

kuhakikisha

maslahi

ya

Tanzania

yanasimamiwa. Ndugu Membe alisimama kidete kwenye kutoa


msimamo wa Tanzania kwenye vita vya ukombozi wa Comoro.
Aidha Ndugu Membe amekuwa mbele kwenye kusimamia
Tanzania kwenye mgogoro wa Ziwa Nyasa, DRC, Sri Lanka,
Visiwa vya Maldives, Burundi na Fiji. Ndugu Membe, sio
kiongozi anayekurupuka kwa kuwa ametanguliza maslahi ya
Taifa kwanza na kutoa maamuzi ya busara.
Aidha itakumbukwa kwamba Ndugu Membe kama Waziri wa
Mambo ya Nje alisimama kutetea maadili ya Taifa dhidi ya
ushoga ambao ulitaka kuchochewa nchini Tanzania kama
kigezo cha kupata misaada ya mataifa makubwa.
Ndugu Membe akiwa kama Waziri wa Mambo ya Nje alihusika
na uundaji wa kurugenzi ya Diaspora ambayo ni kiungo cha
Watanzania wote waishio nje ya nchi.
6.

Awe na upeo mkubwa na usiotiliwa shaka


kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze

o Ni wazi kuwa kama Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka nane


na nusu, Ndugu Membe amejengeka kuwa Mwanadiplomasia
6

kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na

aliyetukuka akiwa na dhamana ya kulinda na kutetea Sera ya

dunia yote kwa ujumla.

Mambo ya Nchi za Nje ya Tanzania yenye maslahi ya


kiuchumi. Mara zote amekuwa mwepesi wa kuomba ushauri na
kupata nasaha za viongozi wa juu waliostaafu nchini kwa
manufaa ya Taifa. Ndani ya kipindi hicho ameshikiria pia nafasi
zifuatazo: o

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika


likiwa na Makao Makuu yake Addis Ababa kati ya
mwaka 2008 na 2009.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya


Madola kwenye makao makuu London, Uingereza kati ya
mwaka 2013 na 2015.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya


Afrika Mashariki, ikiwa na Makao Makuu Arusha hapa
nchini kati ya mwaka 2009 na 2010.

Kiongozi wa timu ya Tanzania katika mazungumzo kuhusiana


na mpaka wa Ziwa Nyasa. Kazi ambayo bado anaendelea nayo
tangu mwaka 2012.
Kiongozi wa jopo la Mawaziri wa Mambo ya Nje kwenye
usuluhishi wa mgogoro wa Burundi mwaka 2015.
7

Amehutubia mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa mwaka


2010 na wa Umoja wa Afrika mara kadhaa kwa niaba ya Mhe.
Rais.
Amesimamia kikamilifu msimamo wa Tanzania katika masuala
mbalimbali ya kiuchumi, kiusalama, kisiasa na kijamii katika
majukwaa ya kimataifa ili kuhakikisha Tanzania inaendelea
kuwa Taifa imara na lenye kuheshimika kote duniani.
Amefanikiwa kupunguza gharama za uendeshaji katika Balozi
za Tanzania kwa kujenga majengo ya ofisi na makazi ili
kuepuka kodi za kila mwaka. Pia ameongeza kipato kwa Wizara
kwa kukodisha baadhi ya majengo ya Serikali nchi za Nje ili
kupunguza gharama na kujenga uwezo wa kujiendesha.
Amefanikiwa kulishawishi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kuanzisha Bajeti ya Maendeleo ukiacha utaratibu
wa awali wa Bajeti ya Matumizi ya Kawaida peke yake.
7.

Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteta au

Kama Mwanadiplomasia, Ndugu Membe katika kipindi chake

ufashisti, bali awe mtu anayeheshimu na

chote cha Uongozi hajawahi kuonesha hulka ya udikteta katika

kulinda Katiba ya nchi, sheria, utawala

utendaji kazi yake. Mafanikio katika kazi yake yametokana na

bora, kanuni na taratibu za nchi.

uwezo wake wa kidiplomasia wa kusimamia mazungumzo


mezani na sio vitani. Ndugu Membea ni mwanadiplomasia na
8

muumini wa sheria na utawala bora, katiba na kanuni za Chama


hasa kwa kuzingatia taasisi za serikali alizofanya kazi.
8.

Awe mtetezi wa wanyonge, wa haki za

Kama Waziri wa Mambo ya Nje, Ndugu Membe ameendeleza

binadamu, mzingatiaji makini wa

msimamo wa Tanzania kama nchi ya ukombozi katika kupinga

maendeleo ya raia wote na asiwe na tama

kuwanyanyasa na kukandamiza wanyonge kwenye nchi za

ya kujitafutia umaarufu wa mtu binafsi.

Sahara Magharibi, Libya, Cuba, Palestina na Kwengineko


duniani.
Vivo hivyo katika jimbo la Mtama, Ndugu Membe ameonyesha
mfano wa kuwasomesha wasiojiweza, kujenga vituo vya afya
kwa wale ambao wana uwezo wa chini na vile vile kuweka
miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuwakwamua kiuchumi
wale wasiojiweza.
Akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ndugu Membe alifanya ziara
nchini Uturuki ambayo moja ya manufaa yake ni kwa nchi hiyo
kuja kujenga Tanzania kituo maalum cha kuwasaidia,
kuwasomesha na kuwalinda watu wanaoishi na ulemavu wa
ngozi (albinism) ili kuepuka majanga na imani potofu dhidi
yako.
Ndugu Membe akiwa kama Waziri wa Mambo ya Nje
alihakikisha
9

Watanzania

wote

waliopo

kwenye

nchi

zilizokumbwa na machafuko kama Yemen na Afrika Kusini


wamerejeshwa nyumbani salama.
Ndugu Membe kama Mbunge amejenga Misikiti na Makanisa
jimboni mtama bila ubaguzi wa dini. Aida amelipia usafiri wa
mahujaji wa dini zote kwenda kushiriki kwenye hija zao
takatifu kwa nyakati mbalimbali.
9.

Awe mstari wa mbele katika kuzifahamu,

Kama Mbunge, Ndugu Membe amekuwa mstari wa mbele

kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza sera za

katika kuleta maendeleo katika jimbo lake ikiwa ni sehemu ya

CCM NA Ilani ya CCM ya uchaguzi.

kutekeleza nia ya CCM ya kuleta maisha endelevu kwa


watanzania wote. Ndugu Membe amefanya hivyo kwa
kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile maji,
ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati, ujenzi wa Barabara, Ujenzi
wa shule na huduma zingine za kijamii.
Kama Waziri, Ndugu Membe amekuwa mstari wa mbele
kutekeleza yaliyoagizwa katika ilani ya CCM kuhusiana na
kuitangaza Tanzania nje ya nchi na kuboresha mahusiano ya
Tanzania. Moja kubwa ambalo Ndugu Membe amelifanya ni
kuanzisha mchakato wa kuwatambua na kuwapa fursa
watanzania waliopo nje ya nchi kushiriki katika kuleta
maendeleo popote walipo.
10

10. Awe mpenda haki na mtu jasiri katika

Ndugu Membe amesimama bungeni na nje ya bunge, serikalini

kupambana na dhuluma na maovu yote

na nje ya Serikali kupinga dhuluma dhidi ya Serikali na

nchini.

Watanzania wote kwa ujumla.


Ndugu Membe pia kama Waziri, amesimama kidete ili nchi ya
Tanzania isiweze kudhulimiwa. Itakumbukwa kwamba suala la
chenji ya Radar liliwasilishwa Bungeni na Ndugu Membe kwa
kutetea maslahi ya Taifa. Aidha, Ndugu Membe ameendelea
kusimama kidete kuhakikisha kuwa Tanzania aipotezi sehemu
ya eneo lake katika ziwa Nyasa.

11. Asiwe ni mtu ambaye anatumia nafasi yake


ya Uongozi kujilimbilikizia mali.

Kama ilivyoelezwa kwenye sifa ya pili, Ndugu Membe katika


kipindi chake chote katika nyadhifa mbalimbali za uongozi
hajawahi kuonesha tabia ya kujilimbikizia mali. Aidha ni
muumini mkubwa wa kutaka mali za Taifa ziwe tunu ya
kunufaisha watanzania wote na sio watu binafsi kwenye nafasi
mbalimbali za uongozi wa umma.
Net worth???

11

12 Awe ni mtu anayekubalika na wananchi.

Ndugu Membe amekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama kwa


miaka 15 tangu mwaka 2000. Katika uchaguzi wa mwaka 2000
alipata kuramwaka.2005 alipata kura.. na mwaka
2010 alipita bila kupingwa. Kwenye chaguzi zote, Ndugu
Membe amechaguliwa kwa ushind wa kishindo nah ii ni
kutokana na uwezo wake wa kuleta maendeleo jimboni na
kutekeleza ilani ya chama na ahadi zake kwa wananchi wa
jimbo lake.

13. Awe na mtu makini katika kuzingatia


masuala

ya

uwajibikaji

wa

viongozi/watendaji na asiyevumilia uzembe


katika utekelezaji wa majukumu/wajibu

Ndugu Membe amesimama mara kadhaa kama Mbunge na


kuwasilisha taarifa Bungeni ambazo zimeisaidia Tanzania
kuwawajibisha baadhi ya viongozi na kuepuka hasara.
Ndugu Membe kama Waziri, amewawajibisha watendaji wake

waliokabidhiwa ili kuinua nidhamu ya kazi,

mara kadhaa katika Wizara ambao walionekana kwenda

tija na ufanisi.

kinyume na matakwa ya ajira yao na majukumu yao ya kazi.



Chaguzi zote za Chama cha Mapinduzi (CCM) hufanyika kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na Sheria za Uchaguzi, na
kila raia wa Tanzania anayejitokeza kugombea nafasi ya uongozi Serikalini kwa tiketi ya CCM sharti atimize
Masharti kama ambavyo imeanishwa katika Kanuni za Uchaguzi ndani ya CCM. Kwa mgombea nafasi ya Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania sharti awe na sifa kumi na tatu (13).
12

You might also like