You are on page 1of 6

HAKI YA MAANDAMANO NA MIKUSANYIKO TANZANIA

Utangulizi
Haki ya kuundamana na kukusanyika ni haki za msingi kwa kila mtu, hizi ni haki

ambazo zimeruuhusiwa kwa mujibu wa sharia za ndani Pamoja na sharia za

kimataifa ambazo Tanzania imezisaini. Miongoni mwa sharia hizo za kimataifa ni

Tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka [1948], Mkataba wa kiafrika wa

haki za binadamu na haki za watu wa mwaka [1981], na mkataba wa haki za

kisiasa na kiraia wa mwaka [1966] kwa mujibu wa sharia za ndani ni Pamoja na

sharia mama ya nchi ambayo ni katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya

mwaka [1977] sura ya pili .

Katika ukurusa ntaenda kueleza uhalali wa haki hizi yaani haki ya kukusanyika

Pamoja na haki ya kuundamana na utaratibu wa kuzitekeleza kwa mujibu wa

sharia za nchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Uhalali wa maandamano na mikusanyiko Tanzania

Haki ya kuandamana na kukusanyika hizi miongoni mwa haki za msingi kwa

binadamu kama jinsi zilivyo haki zingine, hizi ni haki ambazo zinauhusiana na haki

za kisiasa na kiraia. Mikusanyiko na maandamo ni sehemu muhimu kwa binadamu


katika kuelezea mtazamo wake au kutoa maoni yake au kupinga jambo Fulani pia

inaweza kuwa kuunga mkono jambo Fulani na mengineyo mengi.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi yaani naamanisha sharia mama ya Tanzania [katiba

ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka [1977] sura ya pili Ibara ya (20)

ibara ndogo ya kwanza (1) ambayo imempa kila mtu haki ya kufanya maandamano

Pamoja na haki ya kukusanyika, kwa lengo la kueleza mawazo yao au kutoa maoni

yao hadharani. Sitotaka kuelezea sana katika hili kwa sababu sharia yenyewe iko

wazi kabisa ukerejelea kwenye katiba ya Tanzania sehemu ya tatu kwenye [BASIC

RIGHT AND DUTIES] ibara ya (20) ibara ndogo ya kwanza imeeleza wazi kabisa

na wala hilo halina ubishi kuwa kila mtu ana haki ya kuundamana Pamoja na

kufanya mikusnayiko ili kuelezea maoni yao hadharani.

Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumeafikiana kuwa haki ya kuundamana na kufanya

mikusamyiko ni haki halali kabisa kwa mujibu wa katiba ya nchi na sitotaka

kuzichambua sharia zingine za nchi juu ya uhalali wa haki hizi kwa sababu kwa

sababu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya pili

ndio sharia mama wa sharia zote na ndio sharia kuu na sharia yeyote itakayo

pingana na katiba basi hiyo sharia ni batiri kwa mujibi wa ibara ya (64) ibara

ndogo ya (5).
Utaratibu wa kufanya maandamano na mikusanyiko kisheria

Katika kipengele hichi naomba uwe makini unapo kisoma, ikotokea kuna chama

au taasisi au mtu anataka kufanya maandamano au mikusanyiko sehemu ya umma,

kwa mujibu wa sharia anatakiwa kutoa taarifa (notification) ya maandishi kwa

jeshi la polisi angalau masaa 48hrs kabla ya mikusanyiko au maandamano yanayo

kusudiwa kufanyika. Katika taarifa inatakiwa ieleze mahala ambapo maandamano

hayo yanakusudiwa kufanyika, muda wa maandamano au mkusanyiko huo

utafanyika pia inatakiwa kwenye taarifa hiyo ieleze lengo au kusudio la

maandamano hayo au mkusanyiko.

Na hapa naomba nieleweke vizuri, taasisi au chama au mtu itatakiwa kutoa taarifa

juu ya mkusanyiko huu au maandamano hayo kwa jeshi la polisi iwapo yatakuwa

yanakwenda au yatafanyika katika eneo la umma kama hayatakusudiwa kufanyika

eneo la umma baasi hakuna taarifa yeyote itatolewa na ieleweke kuwa hapa inayo

tolewa TAARIFA tu ni siyo maombi

Kwaiyo ni muhimu ikaeleweka kuwa jeshi la polisi halina maamlaka juu ya

uamuzi wa mikusanyiko au maandamano kama lingekuwa na maamlaka basi

sharia ingeemka anayeteka kufanya maandamano afanye maombi (application)

lakini badala yake linamtaka mkusudiwa kutoa notification (taarifa)


Maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani juu haki ya mikusanyiko na

maandamano Tanzania

Waziri wa mambo ya ndani ana maamlaka makubwa haswa kwenye maswala ya

kuundamana na kukusanyika. Waziri amepewe uwezo wa kuongeza vigezo

ambayo mtu anatakiwa kuivyipelek polisi kabla ya kufanya mikusanyiko au

maandamano.

Na ikitokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na polisi anatakiwa akate

rufaa kwa waziri wa mambo ya ndani na maamuzi yatakayo tolewa na waziri wa

mambo ya ndani ndio maamuzi ya mwisho na wala hayana rufaa.

Pia waziri wa mambo ya ndani amepewa maamlaka ya kuamurukuwa mkusanyiko

au maanadamano yeyote yasifuate sharia na taratibu zinahusu mikusanyiko au

maandamano na mtu anayeanda maandamo hayo au mkusanyiko huu atakuwa

ametenda kosa la jinai

Maoni yangu juu ya maamlaka ya waziri wa mambo ya ndani kuuhusu

mikusanyiko na maandamano
Katika mfumo wetu wa Tanzania wazari mambo ya ndani anakuwa ni mwanasiasa

wa chama tawala kwaiyo kitendo cha yeye kupewa maamlaka ya kuongeza vigezo

anaweza kuongeza vigezo ambavyo vitakuwa vigumu kwa mpinzani wake pia

kuamuru mkusanyiko au maandamo ya chama chake au taasisi aliyo na mslahi

nayo yafanyike , pia ukiangalia waziri wa mambo ya ndani amepewe maamlaka ya

rufani pale inapo tokea mtu hajaridhishwa na maamuzi yaliyo tolewa na chombo

cha polisi pia katika hili limetoa mwanya wa ukandamizaji ikitokea mrufani ni

mpinzani wa waziri wa mambo ya ndani, yaani kikubwa Zaidi maauuzi ya waziri

ndio yatakuwa ya mwisho na wala hayana ruufa, ambapo kwa taswira ya

Mahakama inapinga vipengele ambavyo vinapinga jambo kutokufika mahakamani,

katika mtizamo wa mahakama inataka ikotokea mtu haridhishwa na maamuzi

yaliyo tolewa na chombo chochote cha uongozi kwenda mahakama kuu kuomba

marejeo ya uuamuzi.

Mwisho kabisa naona sharia ingaemtaka wazi waziri ni aina gani ya maadamanona

mikusanyiko amabayo inaweza isifuate sharia kuliko kumuachia waziri mamlaka

makubwa ya kuuamua ni mikusanyiko na maandamano gani yasifuate taratibu za

kisheria, katika utawala wa kisheria unataka kufanya kazi kwa kufata usawa,

amapo ukirejere katika ibara ya (13) ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri

wa muungano wa taanzania yam waka 1977 sura ya pili ambayo inamtaka kila mtu
kuwa sawa mbele pasipo kuwepo na ubaguzi wa aina yeyote ile kulindw, kwaiyo

mpaka hapo maamlaka aliyo pewa waziri hayako sawa na katiba.

You might also like