You are on page 1of 4

HIGHER EDUCATION STUDENTS LOANS BOARD

46 Sam Nujoma Road - Mwenge, P.O.Box 76068, 14113 Dar es Salaam, Tanzania
Tel: (General) +255 22 2772432/2772433; Fax: +255 22 2700286;
E-mail: info@heslb.go.tz; Website: www.heslb.go.tz

MASWALI NA MAJIBU KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA 2017/18


1. Swali: Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa?

Jibu: Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewa


kidogo kufunguka, mwombaji anashauriwa kutoka na kujaribu kuingia
tena (refresh) katika mtandao ili aweze kundelea na hatua zinazofuata.

2. Swali: Je ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi/mlezi

Jibu: Vyeti vya kuzaliwa na kifo cha mzazi/wazazi lazima kihakikiwe/vihakikiwe


na RITA kabla havijapakiwa (upload) na kuambatanishwa kwenye
maombi ya mkopo kisha kutumwa HESLB.

3. Swali: Je kama nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambacho


hakijahakikiwa na RITA, nifanyeje?

Jibu: Uhakiki wa cheti cha kuzaliwa au kifo ni hitaji muhimu ili kukamilisha
maombi ya mkopo. Ni lazima kuhakiki vyeti husika, kisha uvipakie
(upload) kwenye OLAMS kwenye vidirisha vya kuambatanishia
(attachments) na baadae vyeti vyote viliyohakikiwa vitumwe HESLB.

4. Swali: Kama sikuwahi kumfahamu mzazi wangu, nitajaza nini ?

Jibu: Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea au


kusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au
msimamizi zithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo
nyaraka rasmi za kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.

5. Swali: Je nikikosea applicant category natakiwa kufanya nini?

Jibu: Unatakiwa kusoma kwa umakini miongozo iliyotolewa na hatua muhimu


ili usikosee katika kipengele chochote cha ujazaji na uwasilishaji wa ombi
1
lako. Ikiwa kuna taarifa iliyosahaulika au kurekebishwa baada ya
kukamilisha na kuwasilisha maombi yako, unatakiwa kuandika barua ya
kuomba kufanyiwa marekebisho, na kuituma HESLB kwa njia ya EMS.

6. Swali: Nitafanyaje nikigundua kosa au upungufu wa taarifa baada


ya kukamilisha, ku-print na kutuma maombi yangu?

Jibu: Unatakiwa kuandika barua ya kurekebisha/kusahihisha taarifa za


kipengele husika, kisha uitumie HESLB kwa njia ya EMS.

7. Swali: Je kama nimehitimu kidato cha sita au diploma mwaka


2017 nitaambatanisha nini?

Jibu: Kama umehitimu kidato cha sita mwaka 2017, unatakiwa kutaja index
number ambayo itatumika kuhakiki matokeo kutoka mamlaka husika.
Kwa mhitimu wa diploma, unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo
(transcript).

8. Swali: Kama nikilipa na nisipopata namba ya muamala ili nikamilishe


maombi yangu, nifanyeje ?

Jibu: Ni lazima kuzingatia maelekezo na hatua muhimu ikiwa ni pamoja na zile


za kulipia. Ikiwa utalazimika kulipia tena ili uweze kukamilisha maombi
yako, unashauriwa kuandika barua HESLB yenye taarifa za muamala
ulioshindikana, ili uweze kurejeshewa pesa yako baada ya kuhakikiwa
kwa kushirikiana na watoa huduma wetu.

9. Swali: Nitanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB, NMB,


M-pesa, AirtelMoney, Tigo-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea?

Jibu: Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kuchagua na
kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au sehemu uliyoko wakati
ukifanya malipo.

10. Swali: Kama mwaka jana au kabla nilikuwa na umri chini ya miaka
30, je mwaka huu naweza kuomba?

Jibu: Vigezo na sifa za kuomba na kupangiwa mikopo vya 2017/18 ndivyo


vitakavyotumika kwa waombaji wenye sifa na uhitaji. Kila mwombaji
anashauriwa kusoma mwongozo na maelekezo kwa umakini ili kujipima
kama anakidhi sifa na vigezo husika kabla ya kuomba.

2
11. Swali: Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani, na ninatakiwa
kulipia 25% kabla ya kuomba tena, je nitafikiriwa kwa vigezo vya
zamani ?

Jibu: Waombaji wote watapimwa na kupangiwa mikopo kwa mujibu wa uhitaji


wao na kwa kutumia mwongozo na vigezo vya mwaka huu wa 2017/18.

12. Swali: Kama ninao wazazi wasiokuwa na uwezo, je niwasilishe


uthibitisho wa aina gani ili kupata mkopo?

Jibu: Unatakiwa kusoma kwa umakini mwongozo wa mwaka 2017/18 ambao


unaelekeza namna ya kuthibisha uhitaji wako wa mkopo. Muombaji
ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na hali hiyo ithibitishwe
na mamlaka husika. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwa uhalisia
na ukweli wake.

13. Swali: Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha


masomo, natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu ?

Jibu: Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yako yatapimwa
kwa mwongozo na vigezo vya mwaka 2017/18.

14. Swali: Nimelipa lakini HESLB haijanitumia ujumbe wa kuendelea


na maombi, nifanyeje?

Jibu: Unatakiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika.


Kama utapata changamoto ya aina yoyote, unatakiwa kuwasiliana na
Kitengo Cha Usaidizi na Watoa Huduma (HelpDesk) kwa namba ya simu
+255 22 550 7910 au anuani pepe helpdesk@heslb.go.tz inayoonekana
kwenye tovuti yetu kwa ajili ya ufafanuzi na msaada zaidi.

15. Swali: Je nikiingiza namba yangu isiyokuwa ya NECTA, mfano


ya nje ya nchi, nitawezaje kuendelea kuomba mkopo?

Jibu: Unatakiwa kuiandika namba-tambulishi (index number)


iliyotumika (isiyokuwa ya NECTA), Majina yako kamili, Jinsia pamoja na
namba ya simu kwa usahihi na ukamilifu, kisha tengeneza namba ya
malipo (generate payment control number). Baada ya hapo mfumo
utakupatia namba ya kidato cha nne tofauti na ile uliyojaza awali (Isiyo ya
NECTA) kulingana na format yetu ya namba za kidato cha nne. Namba
hii mpya itatokana na ile namba iliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA),

3
ukipata ugumu wowote usisite kuwasiliana na Kitengo cha Msaada
(HelpDesk) kwa ufafanuzi zaidi.

16. Swali: Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia ya


simu inayoonyeshwa kwenye mtandao?

Jibu: Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi
(HelpDesk), kwa simu +255 22 550 7910 au kwa barua pepe
helpdesk@heslb.go.tz. Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto
husika kwa njia ya barua pepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia
kama itahitajika. Kumbuka kuandika mawasiliano yako ya simu
itakayotumika kukupigia.

17. Swali: Kama niko mwaka wa pili au wa 3, naweza kuomba mkopo


pia ?

Jibu: Muombaji ambaye tayari yuko chuoni, anaruhusiwa kuomba


mkopo kama inavyofafanuliwa katika mwongozo wa mwaka huu.

You might also like