You are on page 1of 6

Wauguzi

Habari hii inawahusu yeyote anayehitaji kufahamu utaratibu wa kufuata ili


kufanikiwa kufanya kazi nchini Marekani kama RN/Nurse/Muuguzi/Nesi jinis
inavyoelekezwa katika tovuti ya Serikali ya Marekani. RN ni nani? tovuti hiyo
inafananua, soma hapa “Registered Nurses“

Ninafahamu njia mbili ambazo nitazieleza hapa. Kabla hujachagua ni njia ga ni


uifuate, huna budi kujua kuwa njia zote zinakuhitaji uwe:
 Umesoma na kufika katika kiwango cha shahada ya uuguzi (Degree of
Nursing holder).
 Na leseni hai ya Uuguzi inayokubalika katika ngazi za kimataifa mf.
Leseni iliyotolewa na inayotambulika na chama cha wauguzi Tanzania nk.

Njia ya Kwanza: Fuata maelekezo kwa kujiandikisha katika tovuti ya


Commission on Graduates of Foreign Nursing Schools® : (CGFNS)

1. Utatakiwa kufungua anwani ya barua pepe (bure) katika tovuti ya
CGFNS ambayo wataitumia kukufahamisha maendeleo ya kila
kinachofanyika na ulichofanya katika maombi utakayowatumia.

2. Utatumiwa ama unaweza kupakua fomu toka kwenye tovuti hiyo.


Fomu hizi zina maelekezo yanayojitosheleza ya nini cha kufanya.
Kwa ufupi, fomu moja utatakiwa kujaza maelezo yako na kisha
kuwatumia CGFNS, fomu ya pili utatakiwa kuipeleka katika chuo
ulichosomea shahada ya Uuguzi, wataijaza na kuipiga muhuri
kisha hakikisha wanaituma CGFN S, fomu ya tatu utatakiwa
kuipeleka Wizara ya Afya kwenye kitengo kinachohusika na
Wauguzi ambapo wataijaza na kuipiga muhuri, vilevile hakikisha
nayo wanaituma CGFNS.
3. Utatakiwa kulipia gharama za kushughulikia tathmini ya kiwango
chako cha elimu ikilinganishwa na kile cha Marekani kupitia
Credentials Evaluation Services. Hapa watachambua elimu yako na
kuidhinisha endapo ina kiwango sawa na cha Muuguzi aliyesomea
Marekani. Jinsi ya kulipia, utatakiwa kufuata utaratibu waliouweka
wao.

4. Endapo CGFNS watathibitisha kuwa elimu yako ina kiwango


kinachokubalika Marekani, utatakiwa kuchagua tarehe na mahali
pa kufanyia mtihani wa awali yaani Certificaion Program
Qualifying Exam, (CP) maelekezo ya ziada yanapatikana hapa:
Requirements for the Certification Exam.

5. Ni jukumu lako kufuatilia kwa kupiga simu na kuulizia hatua


iliyofikiwa katika kushughulikia maswala yako kwani, maombi
yanayotumwa CGFNS ni mengi mno toka pande zote za dunia.

6. Unatakiwa kufanya mtihani wa Kiingereza. Wakati unajiandikisha


kwa mtihani huo, ni lazima uwajulishe kuwa majibu yako
yatumwe na wao moja kwa moja CGFNS na namba ya kituo cha
CGNFS. Unao uchaguzi kati ya mitihani miwili ya Kiingereza
ambayo unaweza kufanya na ambayo inakubalika CGFNS, nayo ni
aidha TOEFL ama IELTS. Maelezo haya pia yanapatikana kwenye
tovuti ya CGFNS. Ukiwa Dar es Salaam, ninadhani unaweza
kujiandikisha kwa mtihani wa TOEFL pale Mlimani, Chuo Kikuu
kitengo cha Kompyuta (UCC) ama unaweza kupata maelezo pale
Hilton Learning Center iliyopo Kinondoni - Mwembeni,
inatizamana na jengo la Hugo. Kwa mtihani wa IELTS maelezo
yanapatikana katika ofisi za British Council.

7. Ukifashafanya mtihani wa CP, endapo umefaulu, utatumiwa barua


na cheti toka CGFNS inayokuruhusu kutafuta mwajiri katika nchi
ya Marekani ambaye atatakiwa kukutumia barua ya ajira ambayo
utaitumia kuombea VIZA katika Ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania ili upewe VIZA ya kukuruhusu kufanya kazi nchini
Marekani.

8. Utakapofika Marekani, utatakiwa kufanya hatua ya mwisho


ambayo ni kujiandaa kwa mtihani wa kupata leseni ya kufanyia
kazi nchini Marekani, mtihani huo unajulikana kama NCLEX.
Maelezo na utaratibu wa jinsi ya kujiandikisha kwa mtihani wa
NCLEX yanapatikana kwenye tovuti ya National Council of State
Board of Nursing (NCSBN)

Njia ya pili: Njia hii unaweza kuitumia kwa ajili ya kufanya mtihani wa NCLEX
moja kwa moja unaokuwezesha kupata leseni ya kufanya kazi nchini Marekani
kama RN bila kufanya mtihani wa CP-CGFNS . Njia hii itafanikiwa tu endapo:

o Unauhakika ama umeshapata VIZA yoyote ilenitakayokuwezesha
kuingia nchini Marekani
o Umeshafanya na kukamilisha utaratibu ulioelekezwa katika namba
1-6 katika maelezo hapo juu.
o Umeshatuma maombi katika bodi ya Uuguzi katika Jimbo la
Marekani unalotarajia kufanya kazi na kujibiwa endapo
wanaruhusu kufanya mtihani wa NCLEX moja kwa moja bila
kufanya mtihani wa CP-CGFNS. Jimbo la California, Arizona na
machache mengineyo yanatoa uhuru kwa njia hii, kuhusu majimbo
mengine ya Marekani, unahitaji kusoma maelek ezo katika fomu
zao. Bodi hizo zinapatikana National Council of State Board of
Nursing (NCSBN).

 Utakapofaulu mtihani wa NCLEX ukiwa nchini Marekani, utatakiwa


kutafuta Mwajiri nchini humo atakayekuwa tayari kushughulikia
utaratibu wa kukupatia kibali cha kazi na kubadili aina ya VIZA uliyojia
ili kupata VIZA ya kazi ama “Kadi ya Kijani” = Green Card. Hakikisha
kuwa unafanya mtihani wa NCLEX mapema kabla ruhusa yako ya
kuwepo ndani ya Marekani haijaisha (kama una ruhusa ya miezi 6,
hakikisha umejiandikisha kufanya mtihani miezi 4 kabla ya muda kwisha
kwani utaratibu huchukua muda mrefu kwa wewe kutumiwa majibu
unayoyahitaji sana katika kuanza taratibu za Uhamiaji).

Angalizo: Mitihani mingi ya Marekani haifuati mfumo wa mitihani ya Uingereza


tuliyozoea kuandika majibu ya kujieleza mfano: short answers ama essays.
Mithiani ya Marekani mingi ama karibu yote ya fani zote ni ya uchaguzi yaani
“Multiple Choices Questions” (MCQ) ambayo ni migumu na ya kukanganya
akili - usiombe wala usidhani wala usiifananishe na maswali ya uchaguzi
uliyozoea Tanzania, hiyo ni ch a mtoto! Hii mitihani yao ni ya kuvuruga akili.
Hawahitaji jibu sahihi tu, wanajua majibu yote ni sahihi, wao wanahitaji jibu
sahihi ZAIDI. Watu hawa wanaelewa kuwa unafahamu mambo mengi hivyo
wamejenga mfumo unaotesa katika kugundua mitego. Ninaufananisha mfumo
wao na hali ya kumjenga mtu kuwa “specific” na si “general.
Usisahau: Fanya maandalizi kwa kujiandikisha katika vituo vya kujipiga msasa
kama vile Kaplan (wana madarasa unayoweza kuhudhuria ana kwa ana (ukiwa
nchini Marekani) ama kujisomea kwenye mtandao (ukiwa nje ama ndani ya
Marekani). Pia wana benki ya maswali (Q-bank) unayoweza kuyatumia kujifua.
Pia, tumia www.google.com kutafuta zaidi juu ya CGFNS na NCLEX lakini
kuwa macho na majambazi, wezi, wadanganyifu, wababaishaji, walaghai, n.k.
wa mtandaoni wanaojidai wanafahamu sana kuhusu mitihani hii na habari za
uhamiaji nchini Marekani. Kama unajiamini kuwa unaweza kujisomea peke
yako, basi, nunua vitabu vya maandalizi na ujisomee kwa muda walao wa miezi
2 KWA JUHUDI na MAARIFA.
——~–~———~–~—-~——~–~———~–~—-~——~–~———~–~—-~——~–~
———~–~—-~——

Orodha ya tovuti za vitengo vinavyoshughulika na Uuguzi katika majimbo ya


Marekani inapatikana katika tovuti ya NCSBN.

——~–~———~–~—-~——~–~———~–~—-~——~–~— ——~–~—-~——~–~
———~–~—-~——
Contact CGFNS/ICHP:

Mailing Address: 3600 Market Street, Suite 400. Philadelphia, PA 19104-2651


USA

Automated Phone System

(to check status): (215) 599-6200 24 hours a day; 7 days a week Requires CGFNS
ID Number & Date of Birth

Applicant Inquiries: (215) 349-8767*

Business Office: (215) 222-8454*

*Hours of operation: Monday through Thursday: 9:00 am to 5:

00 pm (USA Eastern Time) Friday: 9:00 am to 4:30 pm (USA Eastern Time)

Kujua majira katika majimbo ya Marekani ili ufahamu wakati gani muafaka
kupiga simu, tafadhali soma hapa: Time Temperature ama hapa: Time
Maelezo ya ziada ya wapi na jinsi ya kujifua kwa mtihani wa NCLEX na ile ya
Kiingereza, bofya hapa

Ikiwa nimesahau jambo na nikalikumbuka, basi nitaliongeza wakati ujao.


Endapo una nyongeza, tafadhali nifahamishe kupitia kisanduku kilichopo katika
ukurasa wa “Tuwasiliane” hapo juu.

1 Comment Add your own


 1. Subi  |  at

Please find the forwarded message below and if you can, pass it to those
you think may be interested!
To Ndossi: Thank you brother for caring and sharing.

———- Forwarded message ———-


From:
Date: Thu, May 8, 2008 at 2:30 AM
Subject: Fw: INTERNATIONAL JOB OPPORTUNITIES
To: Subi Nukta
Hi Subi
Could you please post this on the gradnurses in case somebody wants to
contact this agency?
thanks

From: Donna Stevens


Sent: Wednesday, May 07, 2008 1:57 PM
To: ndosie
Subject: INTERNATIONAL JOB OPPORTUNITIES

Dear Mwidimi
We have your details from a previous UK enquiry. Can you confirm if you
wish to continue on our database.
Our recruitment company has expanded and we now recruit for the USA
and Middle East.
If any of these locations would be of interest to you and you wish to have
further details, please let me know.
We currently are recruiting for ICU nurses to work at the Henry Ford
Hospital, Michigan - Detroit. The successful nurse will gain a 2 year
contract, green card for life inc. immediate family members, and a
relocation allowance. We will fully support your NCLEX process and
immigration aswell as your transition to the destination.

I look forward to any feedback that you may have.


Kind Regards
Donna Stevens
Nursing Consultant
07958 656 439
donna.stevens@hcl-international.co.uk
Nursing Division - USA
DD: 0845 303 9090

HCL International
http://www.hcl-international.co.uk

HCL International: Permanent talent: Permanent solutions

Permanent recruitment specialists for Doctors, Nurses, AHPs and


Pharmacists.

HCL International, part of the HCL plc group of companies incorporates


Bluecare Medical and Nurselink Worldwide

You might also like