Professional Documents
Culture Documents
TRAINING CENTRE
MIKOCHENI A
P.o.Box 33158, Contact: Office. 0742-466965.
DAR ES SALAAM-TANZANIA
JINA LA MWANAFUNZI/MWOMBAJI…………………………………….
ARIZONA VOCATIONAL TRAINING CENTRE,MIKOCHENI A inakukaribisha sana
kujiunga na kozi ya Ushonaji na ubunifu wa mavazi ( Tailoring and fashion design) sekta hii
inakuwa kwa kasi kubwa hapa nchini, ni sekta inayo ajiri vijana wengi.
Malengo yetu Arizona vtc ni kutoa mafunzo kwa ubora wa hali ya juu hivyo kuwawezesha
wahitimu wetu kunufaika na fursa za ajira katika sekta hii inayokuwa kwa kasi hapa nchini.
MAZINGIRA YA CHUO.
Chuo chetu kipo kwenye mazingira tulivu, madarasa makubwa yenye mwanga na hewa safi. Ni
mazingira bora ya kujifunzia. Tunao walimu wenye taaluma ya kutosha kumuelisha na wenye
kiu ya mafakio ya wanafunzi wao.
FAIDA YA KUJIUNGA NA KOZI YA USHONAJI NA UBUNIFU WA
MAVAZI(TAILORING AND FASHION DESIGN)
1. AJIRA ya UHAKIKA: Wahitimu wetu wamekuwa wakifanya vizuri katika soko la
AJIRA hivyo kuacha sifa nzuri kila wanapoajiriwa katika viwandana taasisi mbalimbali.
2. Utafundishwa na walimu mahiri na wenye kipaji na uzoefu wa kufundisha
wanaozingatia taaluma ya ufundishaji.
3. Sekta hii ni pana sana hivyo kupitia maarifa na ujuzi atakaopata chuoni mhitimu
anauwezo wa kuamua kuajiriwa au kujiajiri.
4. Kupitia fani hii mhitimu anaweza kujiajiri kwa kufungua kiwanda kidogo cha kushona na
kubuni mitindo ya mavazi, hivyo kuunga mkono juhudi za serikali za kuanzisha na
kukuza viwanda nchini.
5. Baada ya kumaliza mafunzo kwa Nadharia na vitendo na kufaulu mitihani yake kwa
kupata alama nzuri mhitimu atatunukiwa cheti.
6.
MUDA WA KOZI NA GHARAMA ZAKE.
Kozi ya Ushonaji na ubunifu wa mavazi(Tailoring and fashion design) inatolewa kwa muda
miezi mitatu (3 months)
- Utasoma nadharia na vitendo
- Fomu ya kujiunga ni (10,000) tu
- Ada yake ni laki tisa tu(900,000/= tshs)
● Mwa nafunzi unapaswa kuwa mwangalizi wa mashine anayotumia pamoja na vifaa vyote
wanavyotumia.
● Mwanafunzi kama hata hudhulia wiki nzima bila taarifa yoyote huta hesabika kama
mwanafunzi wetu.
● Mwanafunzi anapaswa kizingatia muda wa kuingia darasani na kutoka darasani
● Mwanafunzi anapaswa kulipa ada kupitia benki kwa akaunti ya chuo utakayopewa na mhasibu
hapa ofisini na si vinginevyo
● Mwanafunzi hakikisha unapewa risiti kwa malipo yote utakayofanya chuoni. Kama umefanya
malipo na hukupewa risiti unawajibu wa kuidai.
● Mwanafunzi unapaswa kuzingatia utaratibu wa kulipa ada kila ufikapo muda wa kufanya malipo
kama ulivyoelekezwa ofisini.
● Mwanafunzi atakayeshindwa kulipa ada kwa utaratibu wa kupunguza kila mwezi uliowekwa na
chuo atasimamishwa masomo mara moja.
● Mwanafunzi zingatia kutunza risiti zako za malipo ya ada ni muhimu mpaka utakapohitimu na
kutunukiwa cheti.
● Mwanafunzi unapaswa kukamilisha malipo yako ya ada kabla ya kufanya mitihani yako ya
mwisho.
● Ni lazima mwanafunzi atii na kufuata sheria zote zilizoorodheshwa hapo juu na zile
nyingine utakazoendelea kupewa pindi awapo chuoni.
Baada ya kuhitimu hakikisha unachukua cheti chako mapema kabla ya kupita miezi miwili baada
ya hapo kutakuwa na TOZO kwa kuchelewa kuchukua cheti.
Mimi --------------------------------------------------- nimesoma na kuelewa maelezo yaliyotolewa
hapo juu na nimeamua kwa dhati kujiunga na masomo kwa kozi ya Ushonaji (tailoring)
---------------------------------- ----------------------------------
Sahihi Tarehe