You are on page 1of 2

CHUO KIKUU CHA TAIFA (SUZA)

KURUGENZI YA SHAHADA ZA AWALI (DUS)

WANAFUNZI WAPYA: TANGAZO KUHUSU USAJILI, MIKOPO NA MALIPO KWA MWAKA WA


MASOMO 2021/2022

Makaribisho
Kwanza tunachukua nafasi hii kukukaribisha SUZA na tunaomba ujisikie kuwa upo nyumbani kabisa na
tunakuhakikishia kuwa umefanya chaguo sahihi kuja kusoma SUZA. Karibu sana.

Taratibu za Usajili
Usajili wa Chuo kwa wanafunzi wapya na masomo utaaanza tarehe 20 Oktoba 2021 hadi tarehe 5
Novemba 2021. Ili uweze kusajiliwa na kuanza masomo inabidi ukamilishe yafuatayo: (i) ulipe angalau
nusu ya ada ya masomo (angalia katika account yako utakuta jumla ya ada) (ii) ujaze fomu ya ukaguzi
wa daktari (medical form); (iii) Baada ya kulipa (angalau nusu) na kujaza fomu unatakiwa kurejesha
fomu hizo kwa maafisa wanaofanya usajili katika kampasi utakayosoma pamoja na kopi ya vyeti vyako .
Ratiba ya usajili itabandikwa katika mbao za matangazo au kama mtakavyojulishwa siku ya orientation.
Siku ya kwanza shughuli itakuwa ni (orientation) kukaribishwa na kusikiliza maelezo muhimu kutoka
kwa viongozi. Vilevile unatakiwa ujuwe kuwa baada ya hapo wakati mmoja yanaweza kufanyika
matokeo tofauti, mfano, usajili na mafundisho ya matumizi ya library (library induction), au usajili na
masomo, kujaza medical form na masomo, kwa hivyo ni muhimu kujipanga na ujue unakwenda wapi ili
usikose mambo muhimu. Siku ya mwisho ya usajili itatangazwa.

Utaratibu wa malipo
Malipo yote ya chuo yatafanyika kutumia “control number” ambayo mwanafunzi ataipata katika akaunti
yake. Malipo ya ada ni nusu ya jumla ya ada ya masomo kwa mwaka. Zaidi kuhusu malipo na namna
ya ulipaji utatolewa na wahasibu wa chuo siku ya ukaribijishaji (orientation)
Upatikanaji wa nambari za usajili
Namba za usajili zitapatikana utakapokamilisha usajili au kama itakavyotangazwa. Baada ya kupata
namba yako ya usajili unatakiwa ujisajili mtandaoni ambako ndiko utakapoweza kuona masomo yako
pamoja matokeo yako wakati ukiwa chuoni. Kushindwa kufanya hivyo kunapelekea kukosa kupata
taarifa zako muhimu kama malipo, matokeo n.k na hatimae utawajibika kulipa faini itakayotangazwa na
chuo. Kama hujui kujisajili katika mtandao tunaomba mtafute mwanafunzi wa mwaka wa pili au wa tatu
akufahamishe (MAELEZO ZAIDI YA NAMNA YA KUJISAJILI ONLINE YATAPATIKANA KATIKA MBAO
ZA MATANGAZO).

Mikopo

Wanafunzi wenye masuala yoyote yanayohusu mikopo wanatakiwa waonane na ofisa dawati la mikopo
wa Chuo, anapatikana Idara ya Fedha jengo la utawala kampasi ya Tunguu. Taarifa zaidi za malipo
(kwa wanafunzi wenye mkopo tu) zitapatikana katika mbao za matangazo. Wanafunzi wote
wanatakiwa kulipa nusu ya ada iliyobakia WIKI MBILI za semista ya pili.

Kuanzia siku utakayoanza Chuo hadi mwaka wa mwisho wa kuwepo kwako Chuoni unatakiwa uwe na
utamaduni wa kupitia mbao za matangazo na mtandao mara kwa mara kwa ajili ya kupata taarifa zote
na kujua nini kinaendelea chuoni, usisubiri kusikia taarifa kutoka kwa rafiki/shoga yako.

Ahsanteni na karibuni sana SUZA. Tunawatakia masomo mema

LIMETOLEWA NA
KURUGENZI YA SHAHADA ZA AWALI
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR
SUZA

You might also like