You are on page 1of 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU


TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

M K O A WA R U K WA

OFISI YA MKUU WA MKOA,

Anuani ya simu: REGCOM


Simu Na: (025) 2802137/2802138

S.L.P. 128,

Faksi Na: (025) 2802217/2802380

SUMBAWANGA.

Barua pepe: rasrukwa@yahoo.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAREHE 23/04/2015
Katibu Tawala wa Mkoa,
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa,
Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa,
Maafisa Waandikishaji
Ndugu Waandishi wa Habari, na
Wageni waalikwa
Napenda kuwakaribisha kwenye Kikao hiki ambacho nitawaelezea
mchakato wa Uandikishaji wa Wananchi wetu katika daftari la
kudumu la wapiga kura ambalo tofauti na awamu zilizopita, safari
hii uandikishaji utafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya
uandikishaji ijulikanayo kama Biometrix Voter Registration (BVR).

2. MAFUNZO
Ndugu Wanahabari,
Mafunzo kwa Watendaji wetu ambao watahusika na zoezi hili
tayari yamekwisha fanyika kama ifuatavyo: Mafunzo kwa ajili ya Mratibu wa Mkoa, Maafisa
Waandikishaji na Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya
jimbo yalifanyika tarehe 27 28/04/2015 yakifuatiwa na
Mafunzo ya Maafisa waandikishaji ngazi ya Kata
yaliyofanyika tarehe 18 19/05/2015 kwa Halmashauri zote
na mwisho Mafunzo ya BVR Opereta na Waandishi Wasaidizi
yaliofanyika tarehe 21 22/05/2015.
Nia kubwa ya Mafunzo haya yalikuwa ni kuwapa uelewa
wahusika na hasa namna ya kutumia Teknolojia mpya kwa
Mashine zijulikanozo kama BVR Kits lakini vile vile Mfumo
mpya utakaotumika.
3. VIFAA
Ndugu Wanahabari,
Katika zoezi hili la uboreshaji wa daftari vifaa mbalimbali
vimegawawiwa kwenye Halmashauri zetu na TUME YA
UCHAGUZI MKUU. Vifaa hivyo vitagawiwa kwa mujibu wa
maelekezo ya Tume kwa kuzingatia idadi ya vituo na idadi ya
wapiga kura wanaolengwa kuandikishwa katika maeneo husika.
Vifaa hivi vimegawiwa katika hatua mbili. Hatua ya kwanza ni
Tume kuvipeleka kwenye Halmashauri na hatua ya pili ni
Halmashauri kuvisambaza kwenye Vituo vya kujiandikisha.
Nimeambiwa baada ya zoezi hili kukamilika Afisa Mwandikishaji
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika anatakiwa
kuvikusanya vifaa vyote na kuvihakiki na kuwasiliana na Tume
kwa ajili ya utaratibu wa kuvirudisha Tume. Vifaa hivyo ni:1. Fomu: Na1,Na.2 ,Na.3A, Na. 3B, Na.4, Na.5, Na.6, Na.7
2. Bango la Kituo cha kuandikisha wapiga kura
3. Kalamu ya wino mweusi
4. Kadi ya Plastiki (PVC)
5. Begi
2

6. Boksi
7. Utepe wa gundi
8. Gundi nzito na pini
9. Mfuko mdogo wa plastiki, na
10.
Sanduku la vifaa BVR. Vifaa vyote vimeshapelekwa na
Halmashauri zote na nimeelezwa wahusika wote
wameshapewa maelekezo ya namna ya kutumia vifaa hivyo.
Pia kama ilivyosisitizwa vifaa hivi vitunzwe vizuri katika hali
ya usafi na usalama. Hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi
ya wakaopoteza vifaa hivyo au kuviharibu kwa makusudi.
VITUO VYA KUANDIKISHA
Ndugu Wanahabari
Mkoa wetu una Vituo vya kuandikisha wapiga kura 748 kwa
mchanganuo ufuatao: Halmashauri ya Manispaa
218
Halmashauri ya Wilaya Nkasi 190
Halmashauri ya Wilaya Kalambo
158, na
Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga 182 , Vituo hivi
vimeainishwa na Maafisa waandikishaji na vimesaidia sana
hasa kwa TUME kufanya maamuzi mbalimbali kwa
kuzingatia vituo hivyo. Kwa utaratibu wa TUME YA
UCHAGUZI Vituo vitafunguliwa saa 1.30 asubuhi hadi 12.00
jioni.
6. MAOTEO (PROJECTION) YA WATAKAO JIANDIKISHA
Ndugu Wanahabari,
Maoteo (Projection) ya wanaotegemewa kuandikishwa kwa Mkoa
wetu ni kama ifuatavyo:1.
2.
3.
4.

Halmashauri ya Manispaa
107,000
Halmashaurii ya Sumbawanga
141,000
Halmashauri ya Kalambo
124,000
Halmashauri ya Nkasi
152,000
3

7. SIKU YA KUANZA UANDIKISHAJI


Ndugu Wanahabari,
Kwa mujibu wa ratiba yetu tunategemea kuanza zoezi la
kuandikisha wapiga kura kwenye daftari letu la kudumu tarehe
24/05/2015 hadi tarehe 23/06/2015 zoezi hili litakuwa la siku
28. Napenda kuwapa taarifa kuwa vifaa vimeshafika kwenye
vituo tayari.

8. SIFA ZA KUANDIKISHWA
Ndugu Wanahabari,
Ili mtu aweze kuandikishwa kuwa mpiga kura anapaswa kuwa na
sifa zote zitakazohitajika kwa mujibu wa Sheria. Sheria hizo ni
pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
1977, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343 na Sheria ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa Sura 292. Kwa mujibu wa Sheria hizo
nilizotaja sifa kuu za mpiga kura ni:(a)
Kuwa raia wa Tanzania, na
(b)
Kuwa na umri wa Miaka 18 au zaidi vile vile kwa raia
wote watakaokuwa wametimiza umri wa Miaka 18 ifikapo
tarehe ya Uchaguzi.
Kwenye kipengele hiki cha sifa mtu anaweza kukosa sifa
kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa mujibu wa Sheria ya Taifa
Uchaguzi Sura ya 343 Kifungu Na. 11(i) na Sheria ya Serikali
Mitaa Sura 292 Kifungu cha 9 (i) Mtu anakosa sifa
kuandikishwa kwa sababu zifuatazo:(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)

Ana uraia wa Nchi nyingine


Amethibitika rasmi kuwa ana ugonjwa wa akili
Amehukumiwa kifo na Mahakama
Ametumikia Kifungo zaidi cha Miezi Sita
Amezuiliwa na Sheria kuandikisha kuwa mpiga kura
4

za
ya
za
za

(vi) Hatakuwa ametimiza umri wa kupiga kura ifikapo tarehe


siku ya uchaguzi

9. MAWAKALA WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU


LA WAPIGA KURA NA WATAZAMAJI
Ndugu Wanahabari,
Kwa mujibu wa Kifungu cha 15 (A) (i) cha Sheria ya Uchaguzi Sura
343 na Kifungu cha 17 A (i) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Sura ya 292 vyama vya Siasa vyenye Usajili wa kudumu
vinapewa nafasi ya kuteua mtu mmoja kwa wakala wa uboreshaji
kwa kila Kituo cha uboreshaji. Kila Chama kitafanya uteuzi wa
Wakala husika na kumtaarifu Mwandikishaji kwa maandishi
kuhusu uteuzi huo. Mawakala hao watakuwa na wajibu wa
kufuatilia zoezi la uboreshaji, kushirikiana na waandishi wasaidizi
kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio
kuwa na sifa na kuandika idadi ya watu walioandikishwa na jina la
mtu wa Mwisho. Pia Mawakala hawataruhusiwa:(a)
Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la uboreshaji.
Msimamizi wa Kituo ndiye mwenye ya mwisho ya juu ya nani
anastahili/ hasitahili kuandikishwa.
(b)
Kufanya Kampeni za Kisiasa
katika Kituo cha
Uandikishaji, na
(c)
Kuorodhesha majina ya watu wanao jiandikisha. Natoa
wito kwa Mawakala walioteuliwa na Vyama vyao kuzingatia
haya vinginevyo atakayekiuka atachukuliwa hatua za
Kisheria.

WATAZAMAJI

WA ZOEZI LA UBORESHAJI

Ndugu Wanahabari,
5

Kutakuwepo
na
watazamaji
wa
Ndani
na
Kimataifa
wanaoruhusiwa kutazama mchakato wa uboreshaji utakaofanyika
katika vituo mbalimbali. Watzamaji kabla ya kutembelea Vituo
mbalimbali vya uandikishaji ni lazima wapewe idhini na Tume ya
Uchaguzi. Mpaka sasa Mkoa wa Rukwa umepokea watazamaji wa
ndani watatu (3) na wanazo barua
za Tume ambazo
wameziwasilisha kwa Maafisa waandikishaji.

WITO WANGU
Ndugu Wanahabari,
Na Maafisa wa Tume, napenda kuchukua fursa hii kuwaomba
Kwanza, Wananchi kuwa watulivu wakati wote wa zoezi
Pili, kuwatakia watendaji wote wa Tume kuzingatia Miongozo
waliopewa
Tatu, kuvitaka vyama vyote vya siasa kufuata utaratibu
uliwasilishwa na Tume kwenye zoezi hili na kuwa kamwe
zoezi hili lisitumike kupotosha watu. Watu waachiwe
wajiandikishe kwa HIARI na UTASHI unaozingatia Sheria ya
nilizotaja hapo juu.
Nne, Changamoto yoyote itakayojitokeza iripotiwe mapema
kwa Maafisa waandikishaji na Mratibu wa Mkoa ili iweze
kuripotiwa kwenye TUME ili ipatiwe ufumbuzi.
Tano, Vyama vihamasishe watu kwa kuzingatia Sheria
zilizowekwa na TUME na Serikali kwa ujumla.

Mwisho,
Nichukue fursa hii kuwatakia wananchi ushiriki unaozingatia
Sheria na unaoendelea kudumisha mshikamano, umoja na Amani
tuliyo nayo.
6

IMETOLEWA LEO TAREHE 23/05/2015 NA:


Eng. Stella M. Manyanya
Mkuu wa Mkoa
RUKWA

You might also like