You are on page 1of 27

KWA NINI JESHI LA POLISI LIMEKUBALI

MKATABA HUU NA WACHINA?


TANZANIA NA CHINA YATILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA
KIBIASHARA

Dar es Salaam

Kampuni ya Tamoba ya nchini Tanzania imetiliana saini ya makubaliano ya


kibiashara na kampuni ya Hytera ya nchini China kwa lengo la kupambana na
matukio ya kihalifu kwa vyombo vya usafiri ikiwemo Bajaji na Pkipiki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya


kutiliana saini hiyo, Mkuu wa mawasilino kanda malum ya Dar re Salam ACP
Angela Kibiriti wakati akimuwakilisha Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es
Salaam Lazaro Mambosasa, amesema kuwa, madereva wa boda boda wamekua
wakikabiliwa na changamoto ya matukio ya kihalifu.

“Madereva wa Bajaji na Pikipiki wamekua wakikabiliwa na changamoto kubwa ya


matukio ya uhalifu, hivyo wakifungiwa vifaa hivyo katika vyombo vyao vya usafiri
vitaweza kuwasaidia sana, kwani vina uwezo wa kutoa taarifa nzima ya tukio
linalotokea tena kwa wakati” amesema ACP Angela Kibiriti.

Amesema kuwa, kazi ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha wanalinda raia na mali zao,
hivyo kuwepo kwa mfumo unaofunguwa katika Pikipiki na Bajaji kutaweza
kuwasaidia kuweza kupambana na matukio ya kihalifu kutokana na matukio ya
kihalifu yanayotokea kwa madereva wa Bajaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tamoba, Joseph kimisha


amesema kuwa, vifaa hivyo vitaingia nchini Tanzania baada siku 40 vikitokea
nchini China huku, akibainisha kuwa makubaliano hayo yamelenga kuwanyanyua
madereva wa boda boda na Pikipiki kutoka kiwango cha chini na kuweza kupata
kipato cha juu.

Amesema kuwa, vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia madereva hao kuwapa ulinzi
madereva hao kwa masaa 24 ambapo vitakua vikionesha tukio linapotokea moja
kwa moja na kuweza kupata msaada wa haraka.

“Vifaa hivyo vinauwezo mkubwa sana kwani vinarekoda ambayo inaweza kurekodi
matukio yote pamoja na huduma ya WhatsApp ambayo itawasaidia wakuu wa
vituo wote kuweza kuona matukio moja kwa moja” amesema Kimisha

Ameongeza kuwa, mfumo huo utaanza kuanzia kituoni ngazi ya Kata, wilaya hadi
Mkoa ambapo madereva hao watavaa unifom maalum ambazo pia zitaweza
kuwaingizia kipato kutokana na mabango yatakayokuepo nyuma ya uniform hizo.

“Tulikubaliana sisi na Jeshi la Polisi, Kampuni ya mawasiliano ya TTCL na kampuni


ya Hytera kwamba unifom hizo zikachukuliwe nchini China kwa Bei ya shilling
100,000 ambapo madereva wataweza kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi
minne ” amesema kimisha

Naye, Afisa Habari wa Bodaboda Wilaya ya Ilala Ally Bakari amesema kuwa,
wanaishukuru sana Kampuni ya Tamoba kwani wamekuja kwa lengo la kuwasaidia
madereva wa Bajaji na Pikipiki katika matukio ya kihalifu ambayo yamekua
yakiwakumba siku hadi siku.
Habari zenu ndugu wanajamii wa hapa. Mimi ni mgeni hapa kama mnavyoweza kuona
majina yangu halisi hapo juu. Nimelazimika kutumia jukwaa hili huru kufikisha
dukuduku langu kwa waheshimiwa ili kuepuka vikwazo ambavyo huenda ningekumbana
navyo kama ningetumia njia nyingine. Naamini wengi wenu mmepata dukuduku pia
kuhusu swali langu hapo juu na labda kuhusu nia ya muuliza swali, naomba subira zenu,
najaribu kuwa mwangalifu ili niweze kueleweka vema.

Kwanza nianze kwa kulipongeza jeshi letu kwa hatua hiyo waliyofikia, kumbe wanajali na
kuzingatia hali halisi iliyopo katika usafiri wa bodaboda, kwa kweli kwa upande wangu
nilikuwa na uhakika mkubwa sana tena kwa asilimia mia moja kuwa hawajali chochote
kinachotokea katika usafiri wetu huo, hawajali chochote kuhusu ajali za kila siku
zinazotokea; hawajali kuhusu wizi na uporaji wa pikipiki uliotapakaa kila kona ya nchi;
hawajali chochote kuhusu sifa na utambuzi wa madereva wa bodaboda, hawajali chochote
kuhusu sare na kofia za kukinga majeraha n.k, kwa hakika mimi niliamini hivyo, lakini
sasa angalau wamejaribu kunibadili mtazamo, lakini pamoja na hilo bado na simama na
swali langu hapo juu, kwa nini mkataba huu na “wachina” na sio ule wa machi 2017?
Nimeuliza swali hili kutokana na uhusiano wangu mkubwa na masuala haya ya “matatizo
ya bodaboda” hapa inchini, na hasa kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo haya
yanayoonekana kujenga usugu. Ningependa kusema tu hapa, huenda mimi ndiye mtanzania
niliyetafiti zaidi ya wengine wote kuhusu masuala haya ya bodaboda na kufauru kwa kiasi
kikubwa kuona njia ya kuyakabili matatizo haya. Nilitafiti na kuandaa mfumo wa
kukabiliana na matatizo haya na kuuwasilisha kwa taasisi saba za serikali, miongoni
mwao, tatu zinalihusu jeshi letu hili la polisi. Mfumo huo nimeuweka hapa, Nakupa nafasi
upitie alafu nitahitimisha dukuduku hili.
MFUMO MPYA WA KURATIBU USAFIRI
WA BODABODA NCHINI TANZANIA

S.L.P 3696,
DAR ES SALAAM
SIMU NO.0762 990 405

MFUMO HUU ULIOPEWA JINA LA “PIKIPIKI YANGU


NAFASI YANGU” NI MFUMO UNAOHUSISHA
MPANGILIO WA NAMBA NA HERUFI ZA UTAMBUZI,
KANUNI NA SHERIA

CO832821
YALIYOMO

1. UTANGULIZI……………………………………………………………………………………….UK 1

2. LENGO KUU……………………………………………………………………………………….UK 2

3. MFUMO HUU MPYA…….………………………………………………………………………..UK 4

4. MUUNDO MPYA WA VYAMA VYA BODABODA………………………………….……..UK4

5. KUONDOA WAMILIKI WA PIKIPIKI KATIKA BIASHARA …………………………..UK 5

6. MUUNDO WA UONGOZI NA MAJUKUMU YA VIONGOZI ………………………….UK 6

7. MFUMO WA UTAMBUZI WA WANACHAMA …………………………...……………UK 8

8. MFANO WA REJESTA YA KITUO ………………………………………………………..UK 10

9. SAMPULI YA MFUMO(HALMASHAURI X)……………………………………………..UK 13

10. NYENZO ZA MFUMO ………………………………………………………………………… UK 14

11. VITUO VYA BODABODA……………………………………………….…………………….UK 15

12. FAIDA ZA MFUMO ……………………………………………….……………………………UK 15

13. ALAMA ZA UTAMBUZI …………………………………………………………...……..UK 16,17

14. HITIMISHO ……………………………………………………………………………………..UK 1


UTANGULIZI
Usafiri wa kutumia pikipiki za magurudumu mawili maarufu kama bodaboda,
umeshamiri sana katika kila kona ya nchi yetu, hasa kutokana na urahisi wake wa
kuweza kufika hata katika maeneo yasiyoweza kufikika kwa urahisi kwa kutumia usafiri
wa aina nyingine kama magari.

Hata hivyo, usafiri huu umekuja na changamoto zake nyingi katika jamii kama
vile ajali kuongezeka na kusababisha vifo, vilema na hasara nyingi, lakini pia
kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu wa kutumia pikipiki na kupelekea mashaka mengi
kwa jamii, na hasa abiria wanapotumia usafiri huo kwa nyakati za usiku, na kwa wale
wanaokwenda sehemu za mashambani katika maeneo ya vijijini, kwa sababu inakuwa
vigumu kwao kuweza kutambua iwapo watu wanaotoa huduma hiyo ni wema ama la,
kutokana na kutokuwapo kwa mfumo maalumu unaowezesha kuthibitisha uhalali wa
watoa huduma na hivyo kuleta mashaka mengi kwa abiria.

Kutokana na changamoto hizo, kumekuwapo na majaribio mbalimbali ya kuweka


mifumo itakayosaidia kuratibu shughuli hizi za bodaboda, kwa kuanzisha vyama vya
bodaboda nchi nzima kwa kuhusisha halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya
kwa kushirikiana na polisi, lakini tija imekuwa ndogo sana kwa sababu, mifumo iliyopata
kubuniwa imekuwa ni dhaifu sana, hivyo kushindwa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa
kutokana na kuhujumiwa kirahisi, au kushindwa kutekelezeka kama tutakavyoona kwa
mmoja wa mifumo hiyo uliowahi kubuniwa kwa manispaa za Temeke, Ilala na
Kinondoni, uliowataka bodaboda kuweka mikanda katika pikipiki zao kwa kutumia rangi
ili kuwatambulisha kwa wadau.
Binafsi niliazimia kutafiti na kubuni mfumo utakao weza kuratibu shughuli za
usafiri wa bodaboda kutokana na sababu kuu mbili.

Kwanza, ni uzoefu wangu wa kufanya shughuli za ubunifu tofauti tofauti nilizopata


kufanya kabla, na pili ni madhila mbalimbali jamii inayoyapata kama vile ajali zinazoleta
vifo vingi na ulemavu kwa watu, pamoja na uhalifu wa kutumia pikipiki, huku
kukionekana kukosekana njia bora za kukabiliana na madhila haya, kulinihimiza

1
kuchukua jukumu hili la kutafuta mfumo ambao utaweza kutatua, au kupunguza kwa
kiwango kikubwa matatizo yanayogubika shughuli za bodaboda hapa nchini.
Ningependa kuhitimisha utangulizi huu kwa kuwashukuru wadau mbalimbali
walioshirikiana nami kwa maoni na uzoefu wao katika changamoto za kusimamia na
kuratibu masuala ya bodaboda katika halmashauri nilizopata kutembelea pamoja na
vyama vya bodaboda hapa Dar es salaam na mkoa wa Pwani. Nawashukuru sana kwa
ushirikiano wao ulioniwezesha kuja na mfumo huu.

LENGO KUU
Lengo kuu la mfumo huu ni kuweka utaratibu madhubuti wa kuratibu na
kusimamia utoaji wa huduma ya usafiri wa bodaboda utakaoweza; (1) kuzuia bodaboda
wasio kuwa na sifa ili kuepusha ajali, (2) kupambana na wizi na uporaji wa pikipiki, (3)
kupambana na uhalifu unaofanywa kwa kutumia pikipiki, (4) kuwabaini bodaboda
wanaovunja sheria au kusababisha ajali na kutoroka, (5) kuziwezesha halmashauri
kukusanya mapato yake, (6)kuwapa bodaboda maslahi zaidi.

Ikumbukwe kwamba matatizo mengi yanayosababishwa na bodaboda


yanatokana na kulegalega kwa mwongozo wa mamlaka katika mifumo inayopaswa
kutumiwa na vyama vya bodaboda kuweza kuratibu shughuli zao kwa ufanisi
unaotarajiwa, kwani vyama mbalimbali vya bodaboda vimeachwa kujiamulia namna ya
kufanya kazi kadri vinavyoona inafaa, viongozi wengi wa vyama hivyo wamebakia na
kazi ya kupokea ada za wanachama bila kujali sifa za wanachama husika, kwani vyama
vingi havina kanuni au havifuati taratibu viliyojiwekea. “wewe ukija na pikipiki yako,
unaruhusiwa kuwa mwanachama, hawaulizi leseni ya udereva wala usajili wa
halmashauri,” unaruhusiwa kuwa mwanachama kwa kuwa unaweza kuegesha popote
pikipiki yako na kupakia abiria, kilicho muhimu ni kulipa ada zao, basi, unakuwa
mwanachama. Siku moja nikiwa mjumbe katika moja ya vikao vya chama kimoja cha
bodaboda hapa jijini, nilishangaa kuona kuna aina nyingi za wanachama, waendesha
pikipiki ni wanachama, waendesha Bajaji ni wanachama, wamiliki wa pikipiki ni
wanachama, lakini hata pikipiki zikisajiliwa kama wanachama, sasa katika mwingiliano
wa namna hii, huwezi kutarajia kupatikane mfumo bora wa kuratibu shughuli za
bodaboda kwa sababu ni vigumu kuchanganua na kujumuisha kwa mantiki, vigezo
2
tofauti namna hii ,ili kuvitumia katika mfumo mkakati. Katika mfumo huu ni madereva
wa bodaboda pekee wanao husika bila kuchanganya na watu wengine wowote.

Hapa chini ningependa kutaja sababu tano, zilizosababisha kukwama Kwa mfumo
mmoja uliowahi kudhaniwa unaweza kuwa njia mojawapo ya kusimamia udhibiti wa
shughuli za bodaboda, uliowataka bodaboda kupaka rangi pikipiki zao kwa mtindo wa
mistari pamoja na vigezo mbalimbali ili kuweka utambuzi.
1. Katika mfumo huo, vigezo vya utambuzi ni vingi, na vinahusisha pande nyingi,
kama vile namba ya usajili katika halmashauri, aina ya pikipiki (miguu mitatu au
miwili), namba ya dereva na namba ya kituo cha maegesho. Sasa mkusanyiko
wa vigezo vyote hivi unafanya mfumo wa utambuzi kuwa mgumu kwani, ni
vigumu kwa wadau kuweza kusoma na kutambua kwa urahisi mfumo huo
unaohusisha mambo mengi yaliyochanganywa na hivyo kutokuwa rahisi kusoma
na kutambua vigezo hivyo, nakufanya rahisi kwa baadhi kugushi bila kutambulika
kirahisi.

2. Kuingiliana kwa vigezo vya utambuzi kati ya halmashauri, dereva na mmiliki,


kulitatiza zoezi zima, kwani dereva wa chombo anaweza kubadilika ili hali namba
yake imewekwa katika pikipiki au pikipiki kuhamishwa kituo.

3. Rangi za utambulisho (mikanda) haikuzingatia muundo wa pikipiki pamoja na


rangi zake, kwa mfano, mkanda mwekundu uliopendekezwa kwa manispaa ya
ilala hauwezi kuonekana vyema ukiwekwa katika pikipiki nyekundu ambazo ni
nyingi karibu asilimia tisini.

4. Wamiliki wanakuwa wazito kukubali mpango huu kwa sababu utashusha ubora
wa pikipiki zao endapo zitaongezwa rangi za ziada tofauti na mwonekano wa
asili, kwa sababu itawawia vigumu kuuza pikipiki zao endapo itabidi kufanya
hivyo.
5. Mchakato wa kukusanya vigezo na kuweka rangi ulisababisha urasimu pamoja na
gharama kuwa kubwa.

3
MFUMO HUU MPYA
Katika mfumo huu ilihitajika kuzingatia mambo makubwa mawili. Kwanza ni
kupata utaratibu mzuri wa kuwapanga bodaboda katika namna itakayowezesha
kuratibu shughuli zao wao wenyewe katika vyama vyao, kwani ni vigumu kutumia
mamlaka nyingine kama polisi kwa kuwa bodaboda ni wengi sana na hawatumii njia
maalumu, lakini pia kuna maeneo yasiyokuwa na polisi kama vijijini, hivyo ni muhimu
dhima kubwa ya usalama ikaratibiwa katika vyama vyao.
Pili ni kubuni nyenzo imara za utambuzi wa watu na pikipiki, zitakazowezesha
utaratibu (mfumo) uliopatikana kuweza kufanya kazi kwa urahisi bila kuacha
sintofahamu yoyote kwa wadau ambao ni bodaboda wenyewe, abiria na vyombo vya
uratibu na usalama kama Halmashauri na polisi.

MUUNDO MPYA WA VYAMA VYA BODABODA

Baada ya kufanya utafiti, nilifaulu kupata mfumo niliojiridhisha kuwa ni mzuri,


kuviwezesha vyama vya bodaboda na halmashauri kusimamia suala hili kwa urahisi,
ingawa kulijitokeza changamoto katika muundo wa vyama vya bodaboda.

Kwa mfumo niliopata, italazimu vyama hivi vijengwe katika muundo mpya ili
viweze kuendana vyema na mfumo huu, kwani vyama hivi kwa sasa havijulikani
vimeundwa kwa sura gani, kwa sababu haijulikani kama ni vya wilaya au Mikoa. Hivyo
imenilazimu kupendekeza vyama hivyo viwe vya kiwilaya na kushuka kwenye kata,
halafu kituo cha bodaboda, ili viweze kuendana na mfumo uliopatikana, lakini pia
kuendana na mamlaka za serikali za mitaa, ambazo zimepewa dhamana kisheria
kusimamia na kuratibu shughuli za bodaboda. Mchoro katika kurasa inayofuata
unaonyesha muundo mpya ninaopendekeza wa vyama vya bodaboda.

4
VIONGOZI WA WILAYA

VIONGOZI WA KATA

KITUO A KITUO B KITUO C KITUO D KITUO E

Ni muhimu vyama vya bodaboda kufanya kazi Kwa kutumia sheria za


halmashauri (by laws) Ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Hivyo Ni muhimu
sheria kuwapa uwezo bodaboda kukamata au kuzuia pikipiki zisizo halalishwa kufanya
kazi katika maeneo yao, na pia wao wenyewe kuwajibika kwa sheria hiyo.

KUONDOA WAMILIKI WA PIKIPIKI KATIKA BIASHARA


Katika mfumo huu, ninapendekeza halmashauri mbalimbali kutoa leseni Kwa
watu wanaoendesha bodaboda moja Kwa moja, Kama wanavyotoa Kwa watu wengine
wanaofanya biashara zao katika halmashauri husika. Lengo hapa ni kuwaondoa kabisa
wamiliki wa pikipiki katika biashara hii, ili bodaboda wapate maslahi bora bila kugawana
mapato na wamiliki wao, ili waweze kulipa kodi za serikali, bima za pikipiki,za afya na
pia waweze kukarabati pikipiki kwa wakati zinapoharibika bila kusubiri jambo hilo
lifanywe na wamiliki, jambo linalochangia ajali nyingi. Jambo hili ni muhimu kwa
sababu madereva wa bodaboda ndio wanaohusika moja kwa moja katika matukio
yanayohusu huduma hii kama vile ajali za barabarani, jua, mvua, baridi na matukio ya
uhalifu yanayowapa riski kubwa, hivyo ninapendekeza suala la kusajili pikipiki au
wamiliki wa pikipiki liachwe, isipokuwa, halmashauri kwa kushirikiana na vyama vya
bodaboda wapange vituo vya bodaboda katika kata, na kupanga idadi ya “NAFASI”
zinazohitajika kulingana na mahitaji ya biashara na nafasi hizo zitolewe kwa vigezo
vitakavyowekwa na mamlaka, na ziwe za kudumu kwa muda mrefu.
5
Nimetaja neno nafasi kwa herufi kubwa ili kutia msisitizo kuwa “nafasi hujaa au
kupungua”, hivyo ni muhimu nafasi hizi kuzingatia maslahi ya pande zote ili bodaboda
waweze kunufaika lakini pia halmashauri ziweze kupata stahili zake. Hivyo ni muhimu
kuzingatia jambo hilo, siyo kuweka nafasi 20 mahali panapostahili nafasi 10.

Katika mfumo huu, ninapendekeza mamlaka ziwaamuru bodaboda kufanya


mikakati itakayo wawezesha kutumia pikipiki zao binafsi nasio kutumia za watu
wengine, kwani kwa kufanya hivyo itawapa utulivu barabarani kwa kuwaondolea presha
ya kutafuta pesa za wamiliki wao, lakini pia kuwahakikishia maslahi zaidi jambo
litakalowapa utulivu zaidi barabarani na hivyo kupunguza matukio ya ajali. Jambo hili si
gumu, linawezekana kwa urahisi, kwa sababu wale watakaokuwa wamepata nafasi
katika vituo vya bodaboda, wataweza kupatiwa mikopo ya pikipiki kwa kutumia
dhamana ya nafasi zao katika biashara hii. Endapo pikipiki zitamilikiwa na bodaboda
wenyewe, watakuwa makini kuzilinda zisikutwe na majanga kama ajali, kuzikodisha au
kuziacha hovyo kwa watu wengine wanaoweza kufanya ajali au matukio ya uhalifu.
Katika mfumo huu, ninapendekeza kwamba pikipiki zenye alama za kumnasibisha
na dereva wake, zisitumike kibiashara au kibinafsi na mtu mwingine yeyote, labda ikiwa
alama za utambulisho zimeondolewa ili kuimarisha udhibiti na usalama.
Ikiwa watu wenye vigezo watakosekana kwa sasa kujaza nafasi zitakazopangwa,
mamlaka zinaweza kuanza na watu waliopo sasa, lakini zitoe muda maalumu kwa watu
kutafuta vigezo hivyo. Watakaoshindwa kuvipata ndani ya muda huo waondolewe.

MUUNDO WA UONGOZI NA MAJUKUMU YA VIONGOZI


Kama nilivyopendekeza kurekebisha muundo wa vyama vya bodaboda.
Ninapendekeza ngazi ya juu ya vyama hivi (Ngazi ya wilaya), kuwe na mwenyekiti na
makamo wake, katibu na makamu wake pamoja na mtunza hazina. Katika mfumo huu,
ninapendekeza mamlaka makubwa ya uratibu wa bodaboda kuwa katika ngazi ya KATA,
miradi na shughuli za maendeleo zisimamiwe katika ngazi hii, nitaeleza sababu hapo
mbele. Katika ngazi ya kata, kuwe na mwenyekiti, katibu na Mweka hazina. Halafu
katika ngazi ya chini yaani (kituo) cha bodaboda, kuwe na kiongozi wa kituo hicho na
msaidizi wake watakaochaguliwa na wanakituo husika.
6
Kwa maoni yangu ni vyema viongozi wa wilaya, watokane na viongozi wa kata,
na viongozi wa kata watokane na viongozi wa vituo ili kuwezesha viongozi kuzijua vema
shughuli zinazoendelea katika vyama vyao, kwani itakuwa lazima kiongozi wa wilaya
kujua matatizo ya ngazi ya kata, na kiongozi wa kata kujua matatizo ya ngazi ya kituo,
hali itakayoleta ufanisi mzuri katika vyama vya bodaboda.

Ningependa pia kupendekeza kazi za viongozi katika kila ngazi zilizopendekezwa


katika mfumo huu. Kazi za viongozi wa Wilaya ziwe kuu nne, ambazo ni;-
1. kuitisha na kusimamia mikutano ya viongozi kutoka ngazi ya kata.
2. kuwakilisha wanachama katika vyombo vya mamlaka kama halmashauri, polisi
nk.
3. kutunza kumbukumbu mbalimbali za chama na kushirikiana na viongozi wa chini
kutatua matatizo ya wanachama.
4. Wawe na mamlaka ya kuidhinisha, kurekebisha au kufuta adhabu wanazopewa
wanachama na wavamizi kutoka uongozi wa kata.
Katika ngazi ya Kata, hapa ndipo panatakiwa papewe uzito mkubwa kama
nilivyobainisha hapo nyuma, niliona hivi kwa sababu kuleta majukumu muhimu katika
ngazi hii ambayo ni eneo dogo na watu wachache, itawezesha wanavituo na viongozi
wao kuweza kujisimamia na kutatua changamoto zao kwa wepesi, kwani watakuwa
karibu-karibu tofauti na hali ya sasa ambapo viongozi wanafanya kazi katika maeneo
makubwa na watu wengi sana, hivyo kutokuwa karibu changamoto zinapojitokeza.
Hivyo, nimependekeza viongozi katika ngazi hii wapewe majukumu muhimu ambayo
ni;-
1. Kuitisha na kuendesha vikao katika kata yao.
2. kushirikiana na mamlaka kubuni vituo na nafasi kulingana na mahitaji ya wadau.
3. Kutunza michango na nyaraka katika kata.
4. Wawe na kanuni za kuonya, kutoza faini, kusimamisha kazi au kuondoa moja
kwa moja watovu wa nidhamu na wavamizi.
5. Kuchangia gharama za kuendesha ofisi ya Wilaya. N.k

7
Katika ngazi ya chini kabisa ambayo ni kituo cha Bodaboda, napendekeza kazi za
kiongozi wa kituo kuwa:-
1. Kusimamia sheria, kanuni na kutoa taarifa zinazohusu nidhamu ya wanakituo
kwa uongozi wa kata kama vile ulevi, uvutaji bangi nk.
2. Kuthibitisha utambuzi na uhalali wa wanakituo pamoja na pikipiki zao.
3. Kukamata wavamizi na wavunja sheria za barabarani.
4. Kuhakiki ubora wa pikipiki kama vile taa, breki, honi, kofia ngumu nk.
MFUMO WA UTAMBUZI WA WANACHAMA
Katika mfumo wa utambuzi uliopatikana. Bodaboda watatambuliwa kwa NAMBA
na HERUFI zilizopangwa ili kutambulisha (nafasi zao), (vituo vyao) na (kata zao) kwa
wakati mmoja. NAFASI katika vituo zitatambuliwa kwa namba. kuanzia 1 hadi mtu wa
mwisho kulingana na nafasi za kituo husika.
VITUO vitatambuliwa kwa herufi, kuanzia A hadi kituo cha mwisho katika kata,
kwa mfano, kama vituo katika kata husika ni vinne, kituo cha mwisho kitatambuliwa
kwa herufi “D”
Utambuzi wa KATA katika halmashauri, nimependekeza utolewe kwa namba pia,
kuanzia 1 hadi kata ya Mwisho.
Huu ni mfumo rahisi sana wa utambuzi kwa wadau wa shughuli hii kuanzia
abiria, wanachama, halmashauri na hata polisi wa usalama barabarani, kwa sababu ni
rahisi sana kwao kusoma mpangilio huu wa utambuzi kwa mfano, namba ya utambuzi
ya mtu mwenye nafasi ya kwanza (1) katika kituo “A” Kata namba 1, itasomeka 1A1.
Namba ya utambuzi ya mtu wa pili katika kituo hicho ni 2A1. Lakini namba ya mtu wa
7, kituo C, Kata hiyo hiyo itasomeka 7C1.
Hapa inamaanisha namba ya kwanza ni nafasi ya mtu katika kituo, ambazo ni 1,2
na 7. Herufi ya kati ni jina la kituo yaani A, A na C. Namba za mwisho ni kata husika
ambayo ni (Kata namba 1) katika halmashauri.
Mfumo huu wa namba utafanya kazi tatu (3) muhimu sana, ambazo ni:-
(1) Kutambua watu,
(2) Kuratibu watu,
(3) Kujenga mfumo wa data base utakao unganisha halmashauri zote nchini kama
inavyofafanuliwa hapa chini.
8
Mfumo huu umepangwa namna hii ili kuwarahisishia wadau kusoma, kutambua
na kukumbuka kirahisi namba hizi pale inapobidi, kwani jambo hilo ni muhimu kwa ajili
ya usalama. Kwasababu itakuwa rahisi Kwa vyombo vya usalama kujua mahali pa
kuwapata wahusika wa matukio mbalimbali yanayosababishwa na bodaboda, kwakua,
kwa sasa, wahusika wengi wa matukio ya pikipiki hutoroka bila kupatikana kabisa.

Mpangilio huu wa namba za utambuzi, zinazo unganisha pamoja vituo vya boda
boda na mahali vilipo, utaratibu wenyewe (automatic) mfumo huo kwa ufanisi mkubwa
kwa sababu unawapanga bodaboda katika utaratibu unaoratibika kwa mpangilio
(systematic) maalum, unao zuia mwingiliano wa watu vituoni (tazama uk.13)

Katika kurasa zinazofuata 10, 11, na 12 nimetoa mfano wa rejesta za wana vituo
katika kata, zi nazoweza kutumika katika vyama vya Bodaboda, Halmashauri na hata
polisi. Rejesta hizi zina data mbali mbali kuwahusu wao binafsi kama majina yao, leseni
zao za udereva, pikipiki zao na maeneo ya vituo vyao ambayo ni (kata na mitaa) kwa
maeneo ya mijini, na (kata na vijiji) kwa maeneo ya mashambani. Mfumo huu wa
rejesta ambao utawekwa katika DATABASE, utasaidia sana kupambana na wizi pamoja
na uporaji wa pikipiki, zinazoibiwa eneo moja la nchi na kupelekwa eneo jingine na pia
kutambua pikipiki zinazotumiwa na wahalifu.
Data za bodaboda zitapatikana kwa kutumia simu ya mkononi, kwa kupiga
namba maalum na kujaza data moja wapo kati ya kadhaa zinazohusiana na pikipiki
husika, kama vile namba ya usajili wa pikipiki,namba ya injini ya pikipiki au namba ya
chesisi ya pikipiki, na hivyo wanunuzi wa pikipiki,polisi au watu wengine wowote wenye
mashaka yoyote na pikipiki hizo, hasa zile ambazo zinadhaniwa kuibwa mahali, au
kutiliwa mashaka yoyote, wataweza kuingia katika data bezi hii, ili kutambua iwapo
pikipiki husika zimepata kutumika mahali fulani nchini; na wahusika wa vyombo hivyo ni
wakina nani; na ikiwa wameibiwa au la. Pia data bezi hii itaweza kutambua pikipiki
zilizoibwa kwa boda boda pindi zitakapotaka kusajiliwa upya kama bodaboda katika
maeneo mengine ya nchi.

9
MFANO WA REJESTA YA KITUO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
ORODHA YA WANACHAMA –BODABODA KATA NAMBA 1 (KIPAWA)

KITUO A 1(NAFASI 10)


No. JINA LA KATA NAMBA YA NAMBA YA NAMBA YA NAMBA AINA YA
MWANACHAMA LESENI YA PIKIPIKI CHASESI YA PIKIPIKI
UDEREVA INJINI
M-Mtaa
K-Kijiji
1 MUSSA HASSAN 1A1 MC 752 25037891 SUN LG
AKZ
2 JUMA ISMAIL 2A1 MC 207 37256910 SUN LG
JMZ
3 ISRAEL MICHAEL 3A1 MC 709 5325726 BOXER
AKL
4 ANDREA JOHN 4A1 MC 938 FEKON
BCD
5 EZEKIEL J0AIROS 5A1 YAMAHA
6 THOMAS ILUNGA 6A1
7 EZRO KAJORO 7A1
8 JUMA BARONGO 8A1
9 JAMSON KANIKI 9A1
10 JUMA SWED ALLY 10A1

KIONGOZI WA KITUO –THOMAS ILUNGA


KIONGOZI MSAIDIZI-JUMA ISMAIL

10
KITUO B 1(NAFASI 12)

No. JINA LA KIPAWA NAMBA YA NAMBA YA NAMBA NAMBA AINA YA


MWANACHAMA LESENI YA PIKIPIKI YA YA PIKIPIKI
M-airport UDEREVA CHASES INJINI
I
1 GEORGE KHAMIS 1B1 MC 210 ZZL SUN LG
2 HAMPREY KANINGO 2B1 MC 720 BPK SUN LG
3 JOSEPH HAULE 3B1 MC 101 GCK BOXER
4 JOEL M. NGONYANI 4B1 7087252D MC 700 EFL FEKON
5 SAMSON MWIJAGE 5B1 MC 108 CKL YAMAHA
6 JUMA HORONGO 6B1
7 KHAMIS JOSHUA 7B1
8 KANCHULE SIMEON 8B1
9 KAJUGE HORONGO 9B1
10 CHACHA ITINGE 10B1
11 HAMZA NGONYANI 11B1
12 ITAMBO HAULE 12B1

KIONGOZI WA KITUO –KAJUGE HORONGO


KIONGOZI MSAIDIZI-SAMSON MWIJAGE

11
KITUO C 1(NAFASI 15)
No. JINA LA KIPAWA NAMBA YA NAMBA YA NAMBA YA NAMBA AINA YA
MWANACHAMA LESENI YA PIKIPIKI CHASESI YA PIKIPIKI
M-Sido UDEREVA INJINI
1 ZUGABY CHOMBO 1C1 MC 302 SUN LG
ZZL
2 SHOMARY HABIB 2C1 MC 207 SUN LG
BCK
3 JOSIA NEHEMIEAH 3C1 MC 213 BOXER
ADO
4 JAPHET ITUNDA 4C1 MC 117 FEKON
ABD
5 HOMBOPA ITAHO 5C1 MC 108 YAMAHA
CKL
6 PAULO HIZA 6C1
7 JACKSONS SHOMARY 7C1
8 IMANI GOMBELE 8C1
9 ISMAIL PETER 9C1
10 JOSIAH SAMBELWA 10C1
11 KAJUNA BUBERWA 11C1
12 SAID ZONGOLA 12C1
13 BABU LUNGONDA 13C1
14 WILLIAM KADIGO 14C1
15 JUMA KAJORO 15C1

KIONGOZI WA KITUO –IMANI GOMBELA


KIONGOZI MSAIDIZI-KAJUNA BUBERWA

12
HALMASHAURI X

Katika ukurasa huu, nimeonyesha mfano wa namba za utambuzi katika


Halmashauri X, yenye kata 4, vituo 24 vya bodaboda, vyenye wanachama 240. Katika
halmashauri hiyo, chini ya utambulisho wa kata (kata 1, kata 2..) kuna majedwali yenye
majina ya vituo ndani ya kata hizo kuanzia kituo cha kwanza (A1) chenye
bodaboda wanaotambuliwa kwa namba (1A1, 2A1, 3A1…..) hadi kituo cha mwisho (F4)
chenye bodaboda wanaotambuliwa kwa namba (1F4, 2F4, 3F4…) namba hizi
zinawatofautisha bodaboda wa kituo kimoja na kingine, lakini pia wa kata moja na
nyingine ili iwe rahisi kwao kujiratibu kwa kuzuia kuingiliana katika maeneo
watakayopangiwa. Mfumo wa namba hizi za bodaboda ndio utatumika kujenga data
base ya bodaboda wa nchi nzima kwa kuunganisha halmashauri zote nchini.

KATA 1 KATA 2
A1 B1 C1 A2 B2 C2
D1 E1 F1 D2 E2 F2

1A1 1B1 1C1 1D1 1E1 1F1 1A2 1B2 1C2 1D2 1E2 1F2
2A1 2B1 2C1 2D1 2E1 2F1 2A2 2B2 2C2 2D2 2E2 2F2
3A1 3B1 3C1 3D1 3E1 3F1 3A2 3B2 3C2 3D2 3E2 3F2
4A1 4B1 4C1 4D1 4E1 4F1 4A2 4B2 4C2 4D2 4E2 4F2
5A1 5B1 5C1 5D1 5E1 5F1 5A2 5B2 5C2 5D2 5E2 5F2
6A1 6B1 6C1 6D1 6E1 6F1 6A2 6B2 6C2 6D2 6E2 6F2
7A1 7B1 7C1 7D1 7E1 7F1 7A2 7B2 7C2 7D2 7E2 7F2
8A1 8B1 8C1 8D1 8E1 8F1 8A2 8B2 8C2 8D2 8E2 8F2
9A1 9B1 9C1 9D1 9E1 9F1 9A2 9B2 9C2 9D2 9E2 9F2
10A1 10B1 10C1 10D1 10E1 10F1 10A2 10B2 10C2 10D2 10E2 10F2
KATA 3 KATA 4
A3 B3 C3 A4 B4 C4
D3 E3 F3 D4 E4 F4

1A3 1B3 1C3 1D3 1E3 1F3 1A4 1B4 1C4 1D4 1E4 1F4
2A3 2B3 2C3 2D3 2E3 2F3 2A4 2B4 2C4 2D4 2E4 2F4
3A3 3B3 3C3 3D3 3E3 3F3 3A4 3B4 3C4 3D4 3E4 3F4
4A3 4B3 4C3 4D3 4E3 4F3 4A4 4B4 4C4 4D4 4E4 4F4
5A3 5B3 5C3 5D3 5E3 5F3 5A4 5B4 5C4 5D4 5E4 5F4
6A3 6B3 6C3 6D3 6E3 6F3 6A4 6B4 6C4 6D4 6E4 6F4
7A3 7B3 7C3 7D3 7E3 7F3 7A4 7B4 7C4 7D4 7E4 7F4
8A3 8B3 8C3 8D3 8E3 8F3 8A4 8B4 8C4 8D4 8E4 8F4
9A3 9B3 9C3 9D3 9D3 9F3 9A4 9B4 9C4 9D4 9E4 9F4
10A3 10B3 10C3 10D3 10D3 10F3 10A4 10B4 10C4 10D4 10E4 10F4

13
NYEZO ZA MFUMO
Katika utaratibu wa mfumo huu, Bodaboda watalazimika kutumia nyenzo
mahususi, zitakazowapa utambulisho maalum barabarani kama vile sare rasmi na kofia,
lakini kuna mambo mawili ya msingi zaidi:-
Kwanza, ni kitambulisho atakachotembea nacho dereva wa bodaboda
kitakachokuwa na picha yake, pamoja na vigezo vingine vya kumtambulisha yeye
binafsi, lakini ni lazima kiitambulishe pikipiki yake kwa kuonyesha namba ya usajili ya
pikipiki na namba ya chesisi ya pikipiki.
Pili, ni alama maalumu ya kutambulisha pikipiki ya bodaboda iwapo barabarani
kama inavyokuwa kwa teksi au usafiri mwingine wa umma. Alama hii ambayo
itazalishwa nje ya nchi ndio alama maalum (nembo) itakayotofautisha pikipiki za
bodaboda na zile za binafsi itakayokuwa katika mfumo wa stika mng’aro (reflector) ili
kuifanya itambulike kwa urahisi hata wakati wa usiku.
Alama hii ni nyenzo muhimu itakayowezesha mfumo huu kufanya kazi kwa
urahisi, kwa sababu, bodaboda watakaokosa sifa za kupata nafasi katika vituo
vilivyotengwa, hawataweza kupata alama hizi kwa kuwa zinaambatana moja kwa moja
na nafasi zilizotengwa katika vituo vya bodaboda (ona uk.16) hivyo pikipiki zote
zisizokuwa na alama hii, hazitatambuliwa kwa vyovyote katika shughuli za bodaboda na
itakuwa vigumu kwao kujinasibisha na bodaboda.
Alama hii itatofautishwa kwa rangi kati ya Halmashauri moja na nyingine hasa
zilizojirani, na itawekwa katika kibati maalumu kilichopo juu ya gurudumu la mbele la
pikipiki (ona uk.17) ili iwe rahisi kuonekana kwa wadau wote wa huduma hii.(Ni
muhimu alama hii kuwekwa katika pikipiki ili kurahisisha utambuzi, na hasa pale pikipiki
inapokumbwa na matatizo).
Endapo mwanachama atalazimika kubadilisha pikipiki yake, atalazimika
kuifungua alama hii na kuihamishia katika pikipiki mpya bila usumbufu wowote,
isipokuwa, atalazimika kubadili taarifa za pikipiki katika uongozi wake. Na Wendapo
alama hii itaharibika, au kupotea kutoka kwa muhusika, muhusika atalazimika kutoa
taarifa kwa uongozi wake kwa kumbukumbu za usalama pamoja na mchakato wa
kurejeshewa alama yake.

14
Alama hii ina sifa nne za kuiwezesha kutumika kwa ufanisi kama ninavyozitaja hapa
chini;-
(1)Imebuniwa kuwa “nembo” maalum ya utambuzi kwa kuyapa sura ya kibunifu,
maumbo ya herufi zake ilikupata haki ya kumiliki nembo hiyo (2) Imebuniwa kuwa
salama, isiyoweza kuzalishwa kirahisi kutokana na muundo wa herufi zake
(3)Imebuniwa kuweza kutambulika kirahisi hata wakati wa usiku (4) Imebuniwa kuhimili
hali za jua na mvua.
VITUO VYA BODABODA
Haya ni maeneo ambayo wanachama kadhaa katika kata, watayatumia kama vituo vya
kusubiri abiria, wanakituo hawa watapata nafasi katika vituo hivi kulingana na nafasi
zilizoamriwa kwa vituo husika na kila mmoja atapewa namba ili kujaza nafasi moja.
vituo hivi ni muhimu kuwa na utambulisho, ambapo vitatambulishwa kwa herufi A,B,
C... pamoja na namba ya kata yenye kituo hicho, mfano jina la kituo A katika kata
namba 1 litakuwa A1, kituo B litakuwa B1, lakini jina la kituo A kata namba 2, litakuwa
A2 na kituo B litakuwa B2(rejea uk 13). Vituo hivi vitatambulishwa kwa vibao maalum
kama vya ishara za barabarani ambavyo vitakuwa katika umbo kama la yai lililosimama.
Vibao hivi vitakuwa na rangi mbiliambazo ni kijani nyepesi, ufito na maandishi meupe.
FAIDA ZA MFUMO
1. Mfumo huu utaweza kuzuia kikamilifu watu wasio na sifa kufanya kazi za
bodaboda kutokana na mfumo bora wa utambuzi na udhibiti ili kuepusha ajali.
2. Mfumo huu utawezesha ujenzi wa DATABASE ya bodaboda wote hapa nchini,
itakayosaidia kupambana na wizi pamoja na uporaji wa pikipiki, lakini pia
kupambana na uhalifu wa kutumia pikipiki.
3. Mfumo utawezesha mpango na matumizi bora ya vituo vya bodaboda kutokana
na jambo hilo kupangiliwa vyema katika mfumo huu.
4. Mfumo utasaidia bodaboda wenyewe kuratibu shughuli zao kwa urahisi bila
kutegemea mamlaka za serikali.
5. Mfumo utarahisisha maboresho mbalimbali katika usafiri huu, kwa kuwa takwimu
za bodaboda zitajulikana kwa usahihi na wepesi zaidi.
6. Mfumo utapunguza ajali kwa kiwango kikubwa kwa kuboresha maslahi,
kushurutisha weredi/ nidhamu ya madereva kwa kuondoa fursa za uvamizi.
7. Mfumo utawezesha bodaboda kuvaa mavazi maalumu (sare) za kuwatambulisha
bila kukwepa.
8. Mfumo utaongeza mapato ya serikali kwa kuzuia mianya ya kukwepa kulipa nk.

15
Hii ni alama maalum ya kutambulisha pikipiki ya bodaboda ikiambatana na namba ya
utambuzi wa dereva husika, ambayo ni “1” ya kituo “A” katika kata namba “4” ya
halmashauri fulani hapa nchini. Mambo haya yameambatanishwa pamoja ili kupunguza
au kuondoa uwezekano wa watu kughushi alama, kwani namba hiyo ndio ileile
itakayokuwa kifuani na mgongoni kwa bodaboda.

16
Hapa inaonekana picha ya pikipiki ya bodaboda yenye alama ya utambuzi juu ya
gurudumu la mbele la pikipiki. Alama hii itawekwa mahali hapo katika pande zote mbili
na si mahali pengine popote ili kuwawezesha wadau kutambua kwa urahisi pikipiki
halali za bodaboda.Pia alama hii itasaidia kuwatambua bodaboda wasio vaa sare
pamoja na watu wasio na sifa za kutumia pikipiki za bodaboda.

17
HITIMISHO
Kutokana na changamoto mbali mbali zinazosababishwa na kutokuwepo kwa mfumo
madhubuti wa kuratibu usafiri wa boda boda, ni matarajio yangu kuwa,mamlaka
zilizopewa jukumu la usimamizi wa huduma hii, zitazingatia kwa uzito mfumo huu
wenye lengo na uwezo wa kukabiliana na matatizo mtambuka ya bodaboda kama vile
ajali, uporaji na wizi wa pikipiki, uhalifu n.k ili kuleta faida mtambuka zinazotarajiwa
kwa wadau wote wa usafiri huu.

Katika mfumo huu, bodaboda watalazimika kupata nafasi hizo katika halmashauri zao
wao binafsi, kwa kuwa nafasi (namba), hazitawahusu wamiliki wa pikipiki au pikipiki
kama ilivyo sasa, jambo litakalorasimisha biashara hii kwa kuwasajiri waendesha
bodaboda moja kwa moja, ili kuondoa tatizo la sasa la kushindwa kuwatambua
wahusika katika matukio mbali mbali.

Mfumo huu wenyeuwezo wa kutumika “kidigitali” na “analojia”, utatekelezwa kwa


kushirikisha Halmashauri, vyama vya bodaboda na taasisi binafsi (Kampuni),
itakayokuwa na jukumu la kuandaa na kuendesha DATABASE ya bodaboda pamoja na
vifaa vitakavyotumika katika mfumo huu, na pia kutafiti na kubuni maboresho
mbalimbali yatakayofanya usafiri huu kuwa wa salama na uhakika.

18
19
20
21
Sasa tuangazie kuhusu mkataba huu uliotiwa saini mwezi juni 2019. Kwanza imesemwa kuwa ni
mkataba kati ya Tanzania na China?!, halafu yakatajwa makampuni mawili, moja la kienyeji na
lingine la kichina?! Lakini hapo hakuna raisi, waziri au mabalozi kutoka katika nchi hizo
mbili?! Lakini muhimu zaidi imesemwa ni kifaa kinachofungwa kwenye pikipiki. Na mwisho
nililoliona hapo wanasema ni mkataba wa kibishara. Sasa sijui ni biashara gani hiyo inayotaka
kufanywa katikati ya madhila haya yanayogharimu roho za watu kama sio viungo vyao?.
Tuache hayo, tuzungumze la msingi kuhusu “kifaa”. Ningependa kukumbusha, mimi nilitafiti
suala hili kwa miaka, kwa kifaa hiki kinachoelezewa hapa, hakiwezi kuwa na tija yoyote,
kwanza kina gharama za kuhudumia, lakini hata ikiwa kwa bahati kikajaribu kufikia lengo lake,
bado kina lengo la kutatua tatizo moja pekee la kurekodi uhalifu badala ya kuuzuia usitokee.
Matatizo ya bodaboda ni mtambuka; kuna matatizo ya bodaboda wenyewe kama kugoma kuvaa
sare na kofia ngumu, kukosa sifa, wizi na uporaji wa pikipiki, ulevi, uvutaji bangi n.k; kuna
matatizo ya kimamlaka kushindwa kuratibu bodaboda kwa mfano, pikipiki kuzagaa hovyo mjini
na trafiki kushindwa kusimamisha bodaboda au kukamata zinapovunja sheria za usalama
barabarani. Lakini pia kuna matatizo ya abiria kushindwa kutofautisha kati ya bodaboda
walioidhinishwa na wavamizi wa shughuli hizi na hivyo kujikuta wakiingia matatizoni bila
kujua. Matatizo yote haya kwa ujumla wake yanafanya suala la bodaboda kuwa tata sana, ndio
maana hali imebaki kuwa hivyo ilivyo tangu usafiri huo uanze hapa nchini yapata miaka kumi na
miwili sasa. Na hali hiyo si hapa Tanzania pekee, Kenya, Uganda, Nigeria n.k hali ni hiyo hiyo.
Mfumo huo wa machi 2017 umeshughulika na matatizo yote hayo kwa ukamilifu

Sasa, kwa tofauti hii kubwa kati ya kifaa hicho cha mchina na mfumo niliouwasilisha kwao, kwa
nini nisiwe na dukuduku moyoni, na wala sio wivu au choyo ya kiswahili iliyonizonga, kwa
kuona mchina kapata dili kiulaini tena kwa kidude tu anachodai kuwa anacho huko kwao.

Nimetafakari jambo hili kwa zaidi ya siku 50, nikaona hapana, lazima niondoe dukuduku.

22

You might also like