You are on page 1of 5

TAARIFA KWA UMMA

MWISHO WA KUBADILI LESENI ZA ZAMANI ZA UDEREVA

JESHI LA POLISI TANZANIA NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TAREHE 10/04/2013

1. Utangulizi: Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tumeboresha mfumo wa leseni za udereva na kuanza kutoa leseni za kisasa zaidi (Smart Card) ili kuendana na kukua kwa teknolojia duniani. Zoezi la kutoa leseni mpya za udereva (Smart card) lilianza tarehe 1 Oktoba 2010 kwa awamu ya kwanza iliyohusisha mikoa tisa (9) na mwezi Machi mwaka 2011 Mikoa mingine 13 ilianza kutoa leseni mpya hivyo zoezi hilo kukamilika kwa nchi nzima. 2. MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWA MFUMO HUU:i. Kudhibiti ongezeko la ajali za barabarani nchini kwa: Kuinua kiwango cha udereva nchini kupitia mafunzo ya lazima kwa madereva wa mabasi hususani ya abiria kabla ya kubadili/kupata leseni mpya. Kuondoa tatizo la leseni za kughushi.

1 |Page

Kuongeza udhibiti wa mienendo ya madereva kwa kupitia kumbukumbu za makosa zitakazotunzwa kwenye leseni za madereva (point system). ii. Kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yasababishwayo na leseni za kughushi. iii. Kurahisisha upatikanaji wa takwimu za madereva nchini na hivyo kuisaidia serikali kupanga mipango yake vizuri. 3. MAENDELEO YA UBADILISHAJI/UTOAJI LESENI NCHINI:Hadi kufikia tarehe 08 April 2013 leseni zipatazo 716,256 zilikuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya hizo leseni 59,507 ni za kundi lenye madaraja ya C na nyingine 656,749 ni za makundi mengine. Mkoa ulioongoza kutoa leseni nyingi nchini ni Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo jumla ya leseni 332,930 zilitolewa. Kituo cha Kinondoni (Mayfair) kiliongoza kwa kutoa leseni 134,387kikifuatiwa na Ilala (Samora) leseni 115,590 na Temeke (Quality Plaza) leseni 82,953. Mikoa inayofuata ni Arusha leseni 50,945, Mwanza leseni 44,364, Mbeya leseni 33,932, Kilimanjaro leseni 32,635, Morogoro leseni 31,780 na Dodoma leseni 28,037.

4. MATAKWA YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI (The Road Traffic Act CAP 168 RE 2002) Sheria ya usalama barabarani (The Road Traffic Act CAP 168 RE 2002) kifungu namba 19 na 25, inatamka bayana kuwa: i) Kila mtu anayeendesha gari ni lazima awe na leseni inayoendana na gari analoliendesha,

ii) Ni kosa kuruhusu gari liendeshwe na mtu asiyekuwa na leseni halali, na


2 |Page

iii)

Ni kosa dereva kuendesha gari akiwa na leseni iliyokwisha muda wake.

5. AGIZO LA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA MADEREVA WOTE:Tarehe 09/01/2013 tulitoa Tangazo kwamba mwisho wa kubadili leseni za kuendeshea vyombo vyote vya moto itakuwa 31/03/2013 na kwamba baada ya muda huo hakutakuwa tena na ubadilishaji wa leseni. Katika kipindi hiki hususani wiki ya mwisho ya Machi idadi kubwa ya madereva wenye leseni za zamani walijitokeza kiasi cha baadhi ya vituo kutoa zaidi ya mara tatu ya Idadi ya kawaida na hadi sasa wamiliki wa leseni za zamani wameendelea kuja katika ofisi za TRA na polisi. Hata hivyo tumebaini bado kuna idadi kubwa ya madereva ambao wameshidwa kubadili leseni zao kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo; - Siku za kazi kuingiliana na sikukuu ya Pasaka, - Matatizo ya umeme na mtandao, - Kumalizia mafunzo ya PSV katika vyuo vya NIT na VETA, - Kuchelewa kupata vyeti vya PSV n.k. Kutokana na sababu hizo tumeamua kutoa muda wa mwezi mmoja zaidi ili kutoa nafasi kwa madereva wachache waliobakia kukamilisha taratibu za kubadilisha leseni zao na kwamba baada ya hapo hatutaongeza muda tena. - Wananchi wote wanatakiwa kuhakikisha wanatumia muda huu ulioongezwa kubadilisha leseni zao za zamani ili kujiepusha na usumbufu wanaoweza kuupata baada ya muda huu kumalizika. - Zoezi la ukaguzi wa leseni litafanyika nchi nzima.
3 |Page

- Jeshi la Polisi linawaagiza madereva wote wa vyombo vya moto kubeba leseni zao halisi kila watakapokuwa wanaendesha magari barabarani ili kuwapa fursa askari polisi kuzifanyia ukaguzi wa kina. - Madereva wenye leseni Daraja C, C1, C2, na C3 watembee na vyeti vyao vya PSV walivyosomea NIT, VETA na UJENZI Morogoro.

6. MAMBO YATAKAYOANGALIWA KATIKA UKAGUZI WA LESENI NI KAMA IFUATAVYO:(i) (ii) Kuhakiki kama dereva anayo leseni kwa mujibu wa sheria, Kuhakiki kama leseni imetolewa na Mamlaka husika,

(iii) Kuhakiki uhalali wa leseni kuhusiana na gari linalotumika. (iv) Kuhakiki kama dereva amesoma kihalali katika vyuo vya NIT, VETA, na Ujenzi Morogoro na kupata cheti cha PSV. 7. HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA KWA YEYOTE ATAKAYEKUTWA AMEKIUKA:A: Kwa wale watakaokutwa hawana leseni: i) Hawataruhusiwa kuendesha magari yao hadi itakapothibitika kuwa wanazo leseni halali,

ii) Ikithibitika kuwa dereva hana leseni kwa mujibu wa sheria, atafikishwa mahakamani mara moja na kama gari si la dereva husika, dereva huyo atafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wa gari hilo.

B: Kwa wale wataokutwa na leseni zilizokwisha muda wake: Dereva atakayekutwa anaendesha gari wakati leseni yake imekwisha muda wake atazuiwa kuendesha gari hilo na kufikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wa gari husika ikiwa gari analoliendesha si mali yake.

4 |Page

8. WITO WA JESHI LA POLISI NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA):Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania linatoa wito kwa madereva na wamiliki wote wa vyombo vya moto nchini kutoa ushiriakiano kwa kuzingatia wito huu ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwao na kwa abiria watakao kuwa nao. Aidha wamiliki hususani wa mabasi ya abiria wahakikishe wanawakagua madereva wao waliowaajili kuhakiki kama wanamiliki leseni halali na wamesomea katika vyuo vya NIT, VETA, au Ujenzi Morogoro na wanashauriwa kuwasiliana na polisi wanapokuwa na mashaka kwani nao watafikishwa Mahakamani kwa makosa ya madereva wao kutokuwa na leseni ipasavyo.

Mwisho ifahamike wazi kuwa hatuna nia ya kukomoa mtu yeyote katika zoezi hili kwani tunataka kusonga mbele katika uboreshaji wa mfumo huu hususani zoezi la Nukta katika leseni (Point system) na kuleta nidhamu kwa madereva wote wa vyombo vya moto nchini.

Tangazo hili limetolewa na:

KAMANDA WA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

KAMISHNA IDARA YA KODI ZA NDANI MAMLAKA YA MAPATO (T)

5 |Page

You might also like