Professional Documents
Culture Documents
19/07/2016.
AGENDA:-
1. KUFUNGUA KIKAO
2. KUSOMA MUHTASARI WA NYUMA
3. YATOKANAYO
4. KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
5. USALAMA WA WATOTO KUPANDA MAGARI WAKATAZWE.
6. HUDUMA ZA JAMII KAMATI
7. TAARIFA YA FEDHA
8. KUFUNGA KIKAO
M/kiti katika agenda hii alianza kwa kuwasaslimu wananchi kwa na kuwapa
pole ya safari na kuwapongeza kwa mahudhurio yao mazuri pia aliwataka
wananchi wawe huru katika kuchangia maoni, mawazo na hata ushauri
kutokana na ajenda zilizo kuwa zimeandaliwa katika mkutano na hatimaye
mkutano ulianza mnamo saa 7:00 mchana.
M/kiti katika agenda hii alitoa maelekezo juu ya ulizi na usalama kuwa ni jinsi gani
viongozi kuwa makini na eneo linalomhusu ili kuepukana na wizi au udokozi wa
ovyoovyo na zaidi ni kuudhibiti kabisa, pia m/kiti aliwaeleza wananchi kuwa hata
kama ni raia unamkuta mtu mgeni katika kaya ya mtu mwenyeji yeyote na
unauhakika ya kuwa hajamripotia katika ofisi ya kijiji kwa maana ya uongozi
wa kijiji au katika kitongoji ni lazima achukuliwe hatua za kisheria kwa
mwenyeji huyo ambaye amemhifadhi mtu mgeni bila taarifa yoyote.
AZIMIO
Wananchi wote kwa kauli moja waliridhia azimio la m/kiti pia walishauri
kuwa ni vizuri mwananchi mmojammoja awe mlinzi wa mali zake na za
mwenzake,pia wananchi waliazimia kuwa endapo kuna mwananchi yeyote
atapiga yowe isiyo na utaratibu wowote atatozwa faini ya tsh 30000/= na
wale wenye tabia ya kuwakamata wanawake porini kwa kuwabaka endapo
wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao .
M/kiti katika agenda hii aliwaelekeza wananchi kwa makini athari za rifti
kwa watoto kutokana na dunia ya sasa ilivyo basi aliwasihi wananchi kuwa ni
vizuri kila mzazi achukue jukumiu la kumlinda na kumuonya kila mtoto hata
kama sio wake juu ya kuomba lifti kwa watu wasiowajua.
AZIMIO
Wananchi wote kwa kauli moja waliridhia azimio na ushauri wa m/kiti kuwa
endapo mtoto mmoja ataathilika na hizo rifti madhara yatakuwa kwa wote
hivyo wananchi wote wawe na umoja juu ya suala hilo.
AZIMIO.
AZIMIO
Wananchi wote kwa kauli moja waliridhia taarifa iliyosomwa na mtendaji lakini kwa
maoni waliazimia/kushauri kuwa michango hichangwi kwa wakati na tatizo haliko
kwa mtendaji bali ni wenyviti wa vitongoji hivyo basi walishauri wenyeviti wa
vitongoji waiache tabia hiyo mara moja ili kujiletea maendeleo katika kijiji chetu .
..
M/KITI
KATIBU