You are on page 1of 2

MUHTASARI WA KIKAO CHA WANACHAMA

WA MOROGORO FAMILY
27.08.2023
AGENDA
1. KUFUNGUA KIKAO
2. UTAMBULISHO
3. KUIPITIA RASIMU YA KATIBA
4. UCHAGUZI WA VIONGOZI
5. MENGINEYO
6. KUAHIRISHA KIKAO

1. KUFUNGUA KIKAO
- Mwenyekiti wa muda ndugu Admin Dullah alimuomba mjumbe mmoja kutufungulia
kikao kwa kujikabidhi mbele ya Mwenyezi Mungu mnamo majira ya saa kumi na nusu.

2. UTAMBULISHO
- Baada ya kujikabidhi mbele ya Mwenyezi Mungu wajumbe wote walijitambulisha ili
kufahamiana wakati kikao kinaendelea.
3. KUIPITIA RASIMU YA KATIBA
- Katiba ilipitiwa kwa kufuata kipengele kimoja baada ya kimoja na wajumbe
walipendekeza yafuatayo:-

i. Lengo kubwa la chama hiki kuwaunganisha wana Morogoro na kuishi kama


familia moja kwa kusaidiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali
yakiwemo;-
a. Kusaidiana na kushirikiana katika matatizo, shida na raha mbalimbali
b. Kushiriki masuala ya kijamii na kudumisha maelewano baina ya
wanakikundi
c. Kuhakikisha wanakikundi wanashiriki kikamilifu katika shughuli za
uhifadhi wa mazingira.
ii. Kiingilio cha wanachama kiwe Tsh. Elfu kumi (10,000/=)
iii. Ada ya kila mwezi ni Tsh. Elfu kumi (10,000/=)
iv. Pesa zilizotolewa mwanzo zitatumika katika kutengenezea katiba na
kukamilisha usajili wa chama, Hivyo Wanachama wote waliotoa 5,000 hapo
awali na watakaojiunga wote watatoa upya kiingilio cha Tsh. 10,000/=
v. Wajumbe walipendekeza kuwa mwanachama akifariki au kufiwa na tegemezi
basi kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi 10,000/= kwa ajili ya
rambirambi.
vi. Endapo aliyefariki ni mwanachama basi mali zake zote zitarudishwa kwa
familia.
vii. Baada ya kuipitia na kuifanyia marekebisho katiba wajumbe walikubaliana na
yaliyomo kwenye katiba.

4. UCHAGUZI WA VIONGOZI
- Kisha ukafanyika uchaguzi wa viongozi kama ifuatavyo;-
S/N NAFASI JINA
1. MWENYEKITI ABDALLAH MBAYA (ADMIN DULLAH)
2. MAKAMU KHALIFA MUTABUZI
3. KATIBU DOMINICK DOMINICK
4. K/MSAIDIZI ISSA TWAIBU
5. MTUNZA HAZINA IRENE MANGOLI
6 MSAIDIZI ABDALLA CHIKO

5.MENGINEYO
- Wanachama wote wajitahidi kupata bima ya afya
- Mchakato wa kusajili kikundi ufanyike kwa haraka kadili iwezekanavyo
- Zifunguliwe akaunti ya Bank ya CRDB na LIPA KWA NAMBA ya mitandao ya simu
- Upande wa Bank kuwe na masignatory wane (4) na wawili kati ya hao wanaweza kutoa
pesa.
- Taarifa ya fedha itakuwa inasomwa kila mwisho wa mwaka, hivyo mwisho wa mwaka
huu (mwezi wa kumi na mbili) kutakuwa na mkutano mkuu wa tathimini)

6. KUAHIRISHA KIKAO
- Mwenyekiti aliwashukuru sana wajumbe wote kwa kuacha shughuli zao na kuja kwenye
kikao.
- Kikao kiliahirishwa majira ya saa kumi na mbili jioni.

Ripoti hii imeandaliwa;


Imeandaliwa na :- imepitishwa na:-
___________________ __________________
DOMINICK DOMINICK ABDALLAH MBAYA
KATIBU MWENYEKITI

You might also like