You are on page 1of 43

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

TOLEO LA HABARI LA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI


TANZANIA
YALIYOMO

1. MFUKO WA SELF – SELF MF ................................................................................3


2. MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE (WDF) ..................................................6
3. MFUKO WA MISITU TANZANIA ............................................................................8
4. PRESIDENTIAL TRUST FUND FOR SELF RELIANCE(PTF) - MFUKO WA RAIS WA
KUJITEGEMEA ........................................................................................................ 12
5. PASS TRUST FUND ........................................................................................... 14
6. MFUKO WA KILIMO KWANZA (AGRICULTURE FINANCING WINDOW) .................. 17
7. MIFUKO YA UDHAMINI WA MIKOPO .................................................................. 18
8. MFUKO WA KUENDELEZA WAJASIRIAMALI WANANCHI (NEDF) ........................... 20
9. MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (YDF) ........................................................ 22
10. MFUKO WA PEMBEJEO WA TAIFA ................................................................... 23
11. MFUKO WA KUWASAIDIA MAKANDARASI (CAF) .............................................. 25
12. MFUKO WA NISHATI VIJIJINI (REF) ................................................................ 26
13. MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) ..................................................... 29
14. MFUKO WA ELIMU TANZANIA (TEF) ................................................................ 31
15. MFUKO WA UTT-MFI Plc ................................................................................ 35
16. MFUKO WA UWEZESHAJI WA MWANANCHI (MEF)........................................... 41

2
1. MFUKO WA SELF – SELF MF

Mfuko wa SELF umesajiliwa kwa Sheria ya Makampuni ya


mwaka 2002 chini ya Udhamini wa Serikali ‘Company Limited
by Guarantee’ tarehe 4 Septemba 2014 kwa jina la SELF
Microfinance Fund (SELF MF) yenye usajili Namba 112091.

Madhumuni ya Mfuko ni kutoa huduma endelevu za fedha kwa jamii ambayo


haijafikiwa na huduma rasmi za kifedha hususani jamii ya vijijini. Unatekeleza dhana ya
Serikali ya kupunguza umaskini kama inavyoelekezwa na MKUKUTA na MKUZA.

Walengwa
Walengwa wa Mfuko wa SELF, ni wajasiriamali wadogo hasa wale waishio sehemu za
vijijini; ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana, walemavu, wakulima ambao wamekuwa
wakikosa huduma rasmi za kifedha, na hivyo kushindwa kushiriki kikamiifu kwenye
shughuli za uzalishaji.

Majukumu ya Mfuko wa SELF:


(a) Kutoa mikopo kwa Asasi za fedha kwa lengo la kuwakopesha
walengwa wa Mfuko:Mfuko wa SELF, unatoa mikopo ya jumla yenye masharti
nafuu kwa asasi ndogo na za kati za fedha kama vile Mashirika yasiyo ya
Kiserikali (NGOs), Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Kampuni
za fedha zinazotoa huduma za mikopo na Benki; ili asasi hizo ziweze kutoa
mikopo, kwa jamii ambayo haijafikiwa na huduma rasmi za kifedha.

(b) Kujenga Uwezo wa Asasi Ndogo na za Kati za Fedha kwa njia ya Kutoa
Mafunzo na Vitendea Kazi: Mafunzo haya yanafanya wadau wa SELF waweze
kutoa huduma bora na endelevu kwa wajasiriamali walengwa wa Mfuko wa
SELF. Aidha, Mfuko huwajengea uwezo wajasiriamali wadogo ili waweze kufanya
shughuli za uzalishaji mali kwa tija na kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na
kuitumia mikopo hiyo vizuri, ili hatimaye waondokane na umasikini.

(c) Kuhamasisha na Kuelimisha Umma Kuhusu Huduma za Mfuko:


Mfuko wa SELF unafanya kampeni mbalimbali kwa lengo la kuelimisha umma
kuhusu shughuli za, na kutoa hamasa kwa wananchi ili waweze kuelewa
umuhimu wa kujiajiri, kujipatia mikopo na kuirejesha kwa wakati. Mfuko
umekuwa ukiandaa/kutengeneza na kusambaza machapisho yanayoelezea
utamaduni wa kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye na huduma bora za
mikopo,mkazo ukiwa katika kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya mikopo.

MASHARTI YA MIKOPO KWA ASASI ZA KATI NA NDOGO ZA FEDHA:


Asasi ya fedha inayohitaji mkopo kutoka Mfuko wa SELF inapaswa kutimiza masharti
yafuatayo:-

3
1. Iwe imesajiliwa kisheria. Katika kuthibitisha hilo, nakala ya Hati ya kuandikishwa,
leseni ya biashara, MEMARTS, malipo ya kodi, share certificates na Katiba ya
Asasi husika vinapaswa kuwasilishwa Mfuko wa SELF.

2. Iwe na Bodi ya Wakurugenzi yenye uwezo wa kusimamia shughuli za Asasi


husika, katika kuthibitisha hilo Asasi inapaswa kuwasilisha nyaraka
zinazoonyesha sifa na wasifu wa wajumbe wa bodi/wadhamini.

3. Iwe na watumishi wenye taaluma ya kuendesha na kusimamia vizuri utoaji wa


huduma ya mikopo (Kuweka na kukopa). Katika kuthibitisha hilo Asasi inapaswa
kuwasilisha nyaraka zinazoonyesha sifa na wasifu wa watumishi hao.

4. Iwe na uzoefu wa kutoa mikopo usiopungua mwaka mmoja; pamoja na rekodi


nzuri ya utendaji inayoonyesha kuwepo kwa utamaduni wa kurejesha mikopo
kwa wakati, na kuweka akiba Benki. Katika kuthibitisha hilo, Asasi inapaswa
kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa mahesabu iliyoandaliwa na Mkaguzi wa nje wa
Mahesabu anayetambulika kisheria.

5. Iwasilishe sera ya mikopo iliyoidhinishwa na bodi/wadhamini. Kwa vyama vya


ushirika wa akiba na mikopo sera iwe imeidhinishwa na mkutano mkuu wa
wanachama.
6. Iwasilishe mpango wa biashara (Business Plan) wa kipindi cha miaka mitatu,
unaoonyesha vyanzo vya mapato vya Asasi husika, na mahitaji ya fedha kutoka
kwenye Mfuko wa SELF.

7. Iwe na vyanzo vingine vya mapato vinavyoashiria uwezekano wa Asasi kuwa


endelevu hata baada ya mfuko wa SELF na wafadhili wengine kujitoa.

8. Vyama vya ushirika na Mikopo viwasilishe hati ya ukomo wa madeni


iliyopitishwana Mrajisi Msaidizi wa Ushirika.

9. Iwasilishe fomu inayoonyesha asasi husika imezingatia kikamilifu masuala


yanayohusu jamii na mazingira kwenye biashara za wateja/wanachama wake.

10. Iwasilishe barua toka kwenye Bodi/Wadhamini inayotoa ridhaa kwa uongozi
kukopa. Kwa vyama vya Akiba na Mikopo, kumbukumbu za kikao cha mkutano
mkuu wa wanachama ulioridhia uongozi kukopa fedha zinahitajika.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:


Makao Makuu ya Mfuko wa SELF Dar es Salaam, ambapo pia kuna Ofisiya
Kanda ya Mashariki, inayotoa huduma mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro,
Dodoma, Lindi na Mtwara. Ofisiya Kanda-Mbeya, inayotoa huduma kwenye mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Songwe na
Rukwa. Ofisi ya Kanda Mwanza, inayotoa huduma kwenye mikoa ya kanda ya ziwa

4
ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Simiyu na Geita na Ofisi ya Kanda -
Arusha, inayotoa huduma kwenye mikoa ya kanda ya Kaskazini ambayo ni Arusha,
Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Singida.

OFISI ZA MFUKO WA SELF.

Makao Makuu ya Mfuko wa SELF.Ofisi ya Kanda –Mbeya.

Barabara Mpya ya Bagamoyo - Kijitonyama, Karume Avenue, NSSF House,


Jengo la Letsya, GhorofayaTatu, S.L.P.1584 Mbeya, Simu: +255 25
2500259
S.L.P: 77760,Dar es Salaam, Tanzania, Fax: +255252500259.
Simu: +255 22 2700113, Fax: +255 22 2700117,
Tovuti: www.self.or.tz, Barua pepe: selfmf@self.or.tz

Ofisi ya Kanda-Mwanza. Ofisi ya Kanda–Arusha.

Barabara Mpya ya Bagamoyo - Kijitonyama, Karume Avenue, NSSF House,


Jengo la Letsya, GhorofayaTatu, S.L.P.1584 Mbeya, Simu: +255 25
2500259
S.L.P: 77760,Dar es Salaam, Tanzania, Fax: +255252500259.
Simu: +255 22 2700113, Fax: +255 22 2700117,

5
Tovuti: www.self.or.tz, Barua pepe: selfmf@self.or.tz
Barabara ya Kenyatta, Jengo la NSSF, Jengo la NSSF, Mafao House2nd Floor,
S.L.P: 3172, Mwanza, Simu: + 255 282505049, Old Moshi Arusha, S.L.P.1611, Arusha,
Fax: +255 282505050. Simu. 027 25 20154

2. MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE (WDF)

Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ulianzishwa kutokana na


Azimio la Bunge lililopitishwa Agosti,1993 na kwa mujibu wa
kifungu 17 (1) cha Sheria ya Exchequer and Audit Ordinance
(Cap 439) ya mwaka 1961 ambapo ulianza kufanya kazi mwaka
1993/94.

Dhumuni la Mfuko ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu hasa kwa wanawake wasio
na vigezo au sifa za kukopesheka katika taasisi za fedha ili waweze kujikwamua
kiuchumi na kupambana na Changamoto mbalimbali zinazowakabili kulingana na nafasi
yao katika familia na jamii.

Mfuko huu unaendesha shughuli zake katika halmashauri zote Tanzania Bara.

Walengwa wa Mfuko
Walengwa wanaotarajiwa kunufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ni:
(i) Wanawake wenye umri wa miaka 18 na kuendelea au wanawake walio chini ya
umri huo ambao wana watoto, watakaokidhi sifa za walengwa;
(ii) Kikundi, au mwanamke mmoja mmoja kutoka katika makundi maalumu; na
(iii) Wanawake wajasiriamali waliojiunga katika vikundi vya kijamii (VICOBA, VSLAs,
SILC, ROSCAs) na SACCOS wanaofanya shughuli za kiuchumi zikiwemo; kilimo,
uvuvi, ufugaji, viwanda vidogo, usafirishaji, madini na biashara mbalimbali halali.
Sifa za wanawake walengwa wa Mfuko
 Awe mjasiriamali katika eneo husika, kwa muda usiopungua mwaka mmoja;

6
 Wasiokuwa na sifa za kukopesheka katika Taasisi za fedha;
 Mwananke asiyekuwa na ajira rasmi;
 Mwenye mtaji usiozidi shilingi 200,000 katika mradi anaofanya.
Vigezo vya Utoaji wa Mikopo kwa Walengwa
Vigezo vya utoaji wa mikopo katika Mwongozo huu vitakuwa kama ifuatavyo:
i. Mikopo itatolewa kwa miradi ya kilimo cha mazao ya biashara na chakula,
ufugaji, uvuvi, biashara, usindikaji, viwanda vidogo, wachimbaji wadogo wa
madini, n.k. Kila mradi uwe na andiko la mradi;
ii. Uwepo wa fomu ya maombi iliyojazwa na mwombaji na kuwasilishwa kwa afisa
maendeleo ya jamii;
iii. Uthibitisho wa dhamana ya wanakikundi au kikundi cha mwombaji au
mwanakikundi mmoja mwenye umri wa miaka 18 au chini ya umri huo na
mwenye mtoto kudhaminiwa na wenzake wanne. Muda wa udhamini ni miaka
miwili na isizidi miaka mitano;
iv. Dhamana ya mali isiyohamishika au wadhamini wawili wenye mali
zisizohamishika kwa mkopaji binafsi;
(a) Mikopo itatolewa kwa riba ya asilimia 10 kwa mwaka.
(b) Riba hiyo katika ngazi zote itatumika kwa ajili ya kugharamia uendeshaji na
usimamizi chini ya udhibiti wa Afisa Masuuli (Accounting Officer) katika ngazi
husika;
v. Kabla ya kukopa vikundi vya Kijamii na SACCOS au mwanamke mmoja mmoja
wanatakiwa kufungua akaunti na kuweka asilimia 10 ya fedha inayokopwa;
vi. Kiwango cha utoaji wa mkopo kwa mwanamke mmoja mmoja kitategemea
andiko la mradi na kisizidi shilingi 1000,000/= Kwa vikundi vya kijamii au
SACCOS isizidi 20,000,000/-;
vii. Uthibitisho wa taarifa ya ushiriki wa mafunzo ya ujasiriamali na biashara kutoka
kwa Afisa Maendeleo ya Jamii;
viii. Usajili wa Kikundi cha wanawake na utambulisho wa Serikali ya Mtaa au kijiji;
ix. Mwombaji kuwa na vitambulisho vinavyotambulika kisheria.

7
Fomu ya Maombi ya Mkopo
Mwombaji wa mkopo anatakiwa kujaza fomu ya maombi ya mkopo na kuambatisha
mchanganuo wa mradi. Fomu hizo zinapatikana kwa Afisa Maendeleo/Mtendaji wa kata.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Chuo Kikuu Dodoma
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,
Sanduku la Posta 573,
Jengo Namba 11
40478, Dodoma
Simu: 255-22-2137679/2124857/2132526
Nukushi: 255-22-2133647/2138525
Barua pepe: ps@communitydevelopment.go.tz
Tovuti: www.mcdgc.go.tz
Au Tembelea Halmashauri ya Wilaya yeyote iliyokaribu nawe

3. MFUKO WA MISITU TANZANIA

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umeanzishwa kisheria (chini ya Sheria ya Misitu Sura
323 ya mwaka 2002), kama njia endelevu ya kuwezesha uhifadhi, usimamizi na
uendelezaji wa rasilimali misitu katika Mikoa
yote ya Tanzania Bara. Mfuko huu umeanzishwa
kwa lengo la kukabiliana na changamoto za
usimamizi wa rasilimali ya misitu hasa katika
kuimarisha utekelezaji wa Sera na Sheria ya
Misitu. Mfuko wa Misitu Tanzania ni Mfuko wa
Umma uliopo chini ya Wizara ya Maliasili na
Utalii. Mfuko huu unasimamiwa na Bodi ya
Wadhamini na utekelezaji wa shughuli za kila
siku hufanywa na Sekreatarieti ya Mfuko. Mfuko

8
wa Misitu Tanzania ulizinduliwa rasmi kupitia Waraka wa Hazina Na. 4 wa mwaka 2009
na ulianza rasmi utekelezaji wa majukumu yake Julai 2011. Mfuko wa Misitu Tanzania
unatoa aina tatu za uwezeshaji kulingana na mahitaji ya walengwa. Uwezeshaji huo ni:
Uwezeshwaji wa fedha; vifaa; na Stadi/Utaalam
Mfuko unatoa ruzuku katika maeneo matatu ya kipaumbele ambayo ni:

i. Uhifadhi, Uendelezaji na Usimamizi wa Rasilimali Misitu kupitia


shughuli za upandaji miti, uhifadhi wa misitu ya asili, uhifadhi wa vyanzo
vya maji na matumizi ya nishati mbadala;
ii. Uboreshaji wa Maisha ya Jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu
kupitia shughuli kama za ufugaji nyuki, uanzishwaji wa vitalu vya miti,
upandaji miti, ufugaji wa samaki nk.; na
iii. Utafiti ulengao kuboresha uhifadhi na usimamizi wa rasilimali misitu

Picha: moja za miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania

Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa aina tatu za ruzuku za ambazo kama ifuatavyo:

Ruzuku Ndogo: kiasi cha fedha kisichozidi Shilingi za Kitanzania (TZS) milioni
tano;Ruzuku ya Kati: kiasi cha fedha kinachozidi TZS milioni tano (5) lakini haizidi TZS
milioni 20;na Ruzuku Kubwa:kiasi cha fedha kinachozidi TZS milioni 20 lakini haizidi
TZS milioni 50

Walengwa wa Mfuko wa Misitu Tanzania


Mfukohuu unatoa ruzuku kwa wadau mbalimbali kwa kuzingatia maeneo matatu ya
kipaumbele ya Mfuko. wadau hao ni;watu binafsi, vikundi vya jamii, asasi zisizo za
serikali, jumuiya/taasisi za kidini, asasi/taasisi za mafunzo, asasi zisizo za mafunzo,

9
taasisi za utafiti, wizara, Idara, na wakala za serikali, pamoja na mamlaka za serikali za
mitaa. Hata hivyo, vikundi/asasi/taasisi zote zinatakiwa kuwa zimesajiliwa na mamlaka
zinazotambulika kisheria, wakati waombaji binafsi wanatakiwa kuwa na wadhamini
wawili wanaotambulika/wanaoaminika. Mfuko wa Misitu Tanzania huitisha/hukaribisha
maandiko ya miradi ya kuomba ruzuku kila mwaka hususan tarehe mosi ya mwezi
Februari na maandiko hayo hupokelewa kwa vipindi vitatu tofauti.

Muda wa kupokea maandiko ya miradi inayoomba ruzuku ya Mfuko Wa


Misitu Tanzania

Mwisho wa kupokea maandiko ya miradi inayoomba ruzuku ndogo ni tarehe 30 Juni na


31 Desemba ya kila mwaka, na mwisho wa kupokea maandiko ya miradi inayoomba
ruzuku ya kati na ruzuku kubwa ni tarehe 31 Machi ya kila mwaka. Aidha, maombi
yoyote yatakayowasilishwa baada ya tarehe ya mwisho ya kupokea maandiko ya miradi
hayatashughulikiwa.

Vigezo vya Kuchagua Miradi

Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa ruzuku kwa miradi itakayotimiza vigezo vifuatavyo:
Mradi unatoa faida ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja katika uhifadhi na
usimamizi wa rasilimali misitu; Mradi unatoa faida moja kwa moja au isiyo ya moja kwa
moja kwa walengwa; Shughuli ziwe wazi na kuwepo na uwajibikaji; Mradi wenye
ubunifu; Miradi ambayo matokeo yake yatatumika kuboresha usimamizi wa rasilimali
misitu; Uwezo wa mwombaji kufanikisha malengo na shughuli zilizopendekezwa; Uwezo
wa mwombaji kutekeleza na kusimamia shughuli za mradi; Uendelevu wa shughuli za
mradi zitakazotekelezwa; Ushiriki wa wadau; Mwombaji wa ruzuku ya kati na kubwa
aahidi kuwa atachangia asilimia 20 (fedha taslimu au hali na mali) ya jumla ya fedha
yote inayoombwa; na Mwombaji wa ruzuku aahidi uwepo wa watumishi wenye ueledi
wa aina ya mradi unaombwa ili kurahisisha utekelezaji..

Miradi iliyowezeshwa kupitia ruzuku ya Mfuko imesambaa katika mikoa yote Tanzania
Bara na imeoneshwa kwenye ramani ya Tanzania kama Kiolezo Na.1

10
RAMANI YA TANZANIA IKIONYESHA MIRADI INAYOFADHILI
NA MFUKO WA MISITU

Jumla ya Miradi : 2 Jumla ya Miradi : 12 Jumla ya Miradi : 9 Jumla ya Miradi : 4 Jumla ya Miradi : 13
Midogo: 2 Midogo: 6 Midogo: 5 Midogo: 2 Midogo: 10
Kati: 0 Kati: 5 Kati: 4 Kati: 1 Kati: 2
Mikubwa : 0 Mikubwa : 1 Mikubwa : 0 Mikubwa : 1 Mikubwa : 1

Jumla ya Miradi : 23 Jumla ya Miradi : 13


Midogo: 13 Midogo: 9
Kati: 5 Kati: 3
Mikubwa : 5 Mikubwa : 1

Jumla ya Miradi : 18 Jumla ya Miradi : 22


Midogo: 10 Midogo: 19
Kati: 7 Kati: 2
Mikubwa : 1 Mikubwa : 1

Jumla ya Miradi : 9 Jumla ya Miradi : 31


Midogo: 7 Midogo: 13
Kati: 2 Kati: 10
Mikubwa : 0 Mikubwa : 8

Jumla ya Miradi : 16 Jumla ya Miradi : 6


Midogo: 9 Midogo: 2
Kati: 3 Kati: 3
Mikubwa : 4 Mikubwa : 1

Jumla ya Miradi : 62 Jumla ya Miradi : 52


Midogo: 39 Midogo: 36
Kati: 17 Kati: 9
Mikubwa : 6 Jumla ya Miradi : 19 Jumla ya Miradi : 42 Mikubwa : 7
Midogo: 10 Midogo: 34
Kati: 4 Kati: 3
Mikubwa : 5 Mikubwa : 5
Jumla ya Miradi : 13 Jumla ya Miradi : 8
Midogo: 4 Midogo: 7
Kati: 5 Jumla ya Miradi : 53 Jumla ya Miradi : 42 Kati: 0
Mikubwa : 4 Midogo: 30 Midogo: 17 Mikubwa : 1
Kati: 12 Kati: 13
Mikubwa : 5 Mikubwa : 12
Jumla ya Miradi : 2
Midogo: 0 Jumla ya Miradi : 2
Jumla ya Miradi : 3 Jumla ya Miradi : 8 Midogo: 1
Kati: 0 Midogo: 4
Midogo: 1 Kati: 1
Mikubwa : 0 Kati: 3
Kati: 1 Mikubwa : 0
Mikubwa : 1 Mikubwa : 1

Kiolezo Na. 1: Ramani ya Tanzania ikionyesha miradi iliyo/inayofadhiliwa na


TaFF kwa aina ya Ruzuku katika Mikoa yote ya Tanzania Bara

Kwa maelezo zaidi wasiliana na


Katibu Tawala,
Mfuko wa Misitu Tanzania,
S.L.P. 11004,
Dar es Salaam.
Simu: +255 (0)222865816
Faksi: +255 (0)222865165
baruapepe: info@forestfund.go.tz Tovuti: www.forestfund.go.tz
11
4. PRESIDENTIAL TRUST FUND FOR SELF RELIANCE (PTF) - MFUKO WA
RAIS WA KUJITEGEMEA

Mfuko wa Rais wa Kujitegemea ulianzishwa 1983 chini ya


sheria ya Tanzania ya Baraza la Wadhamini kifungu cha 375
(“TRUST INCORPORATION ORDINANCE CHAPTER 375”)
kama chombo mahsusi cha kutia msukumo wa maendeleo
katika jamii hasa ya wale wenye kipato cha chini,

Hadi kufikia Mwezi Juni, 2016 Jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi 478.6 Milioni
ilitolewa kwa wajasiriamali 761, ambapo wanawake walikuwa 575 na wananume 186 .

1. DIRA YA MFUKO
“Tumedhamiria kuwa taasisi ya kifedha ambayo ni chaguo la vijana na
wanawake katika kuleta mabadiliko bora ya kiuchumi nchini Tanzania”
2. DHIMA YA MFUKO
“Kujenga uwezo kwa vijana na wanawake wa Tanzania kwa kuwapatia
huduma bunifu za kifedha na zisizo za kifedha kupitia wafanyakazi weledi,
ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa walengwa.”

3. MADHUMUNI YA MFUKO
Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea ni kuwa na chombo
mahsusi cha kutia msukumo wa maendeleo katika jamii hasa ya wale wenye kipato cha
chini, wakina mama na Vijana, na wafanyabiashara ndogondogo waweze kujiajiri
wenyewe hatimae waweze kujitegemea.

Lengo hili linatekelezwa kwa Mfuko:


a) Kuendesha mafunzo ya awali na endelevu ya uendeshaji na usimamiaji bora wa
biashara kwa wale wote wanaotarajia kupata na waliopata mikopo.
b) Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa walengwa wake ili kutekeleza madhumuni ya
kuanzishwa kwake.
c) Kuwajengea uwezo wa kujiwekea akiba walengwa wa Mfuko ili kuimarisha vipato na
mitaji yao.

4. WALENGWA WA MFUKO
i. Vijana ambao wamehitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo ufundi stadi
unatambuliwa na VETA,SIDO na vyuo vingine vya ufundi stadi.
ii. Wanawake wajasiriamali walio katika sekta ya uzalishaji mali.
iii. Kundi maalum la Vijana walemavu

12
5. VIGEZO VYA MIKOPO
a. Mikopo ya vijana
i. Uwe mkazi wa eneo lililolengwa
ii. Uwe na shughuli ya ujasiriamali inayoendana na fani uliyosomea
iii. Ujiunge katika kikundi cha watu kati ya watano hadi kumi waliotimiza masharti
kwa Mikopo ya UMOJA na VIFAA.
iv. Uwe mhitimu katika chuo kinachotambulika na VETA, NACTE, ama umepata
mafunzo ya ujasiliamali toka SIDO ama Taasisi za kijasiriamali.
v. Uhudhurie mafunzo ya Mikopo ya Ujasiriamali yatolewayo na Mfuko wa Rais wa
Kujitegemea kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali.
b. Mikopo ya akina mama
i. Uwe umepatiwa mafunzo ya ujasiriamali toka SIDO, VETA au Taasisi
inayotoa mafunzo ya ujasiriamali.
ii. Uwe mkazi wa eneo lililolengwa
iii. Uwe mjasiriamali katika sekta ya uzalishaji na sio ya uchuuzi.
iv. Ujiunge katika kikundi cha watu 5 hadi 20 waliotimiza masharti Kwa Mikopo ya
UMOJA na VIFAA.
v. Uhudhurie mafunzo ya siku saba ya Mikopo na Ujasiriamali yatolewayo na Mfuko
wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
6. RIBA:
Mfuko unatoza Riba kulingana na aina ya Walengwa wetu. Mikopo ya Vijana Riba ni
asilimia 1% kwa mwezi sawa na asilimia 12% kwa mwaka, na Mikopo ya Wanawake
wazalishaji mali ni asilimia 1.25% kwa mwezi , sawa na asilimia 15% kwa mwaka.
7. MUDA WA MAREJESHO: Muda wa marejesho kwa sasa ni kati ya miezi 4 hadi 12
kwa mikopo ya UMOJA na kwa mikopo ya Vifaa ni hadi miezi 24.

KIKUNDI CHA VIJANA CHA USELEMALA KILICHOPO


MJIMWEMA-MAKAMBAKO KIKIWA NA BAADHI YA
BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA KIKUNDI HIKI

13
BAADHI YA BIDHAA ZA ASILI ZINAZOTENGENEZWA
NA KIKUNDI CHA WANAWAKE KIITWACHO
HANDCRAFT KILICHOPO NJOMBE ENEO LA
SABASABA KATIKA JENGO LA SIDO.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:


Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea,
S. L. P 70000,
DAR ES SALAAM.
Namba ya Simu. General line: 22 2760450
Direct Line: 22 2760441
Barua pepe: mkurugenziptf@gmail.com
Tovuti: www.ptf.or.tz

5. PASS TRUST FUND

Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo


[PASS] ni chombo kilichoanzishwa mwaka
2000 kama mradi wa kuchochea uwekezaji na kukuza kilimo cha biashara na sekta
zinazohusika. Ilisajiliwa mwaka 2007 kama asasi isiyokuwa ya serikali kwa mujibu wa
sheria ya ushirikishaji wadhamini ya mwaka 2002. PASS ilianzishwa kwa ushirikiano kati
ya Serikali ya Denmark kupitia Ubalozi waouliopo Dar es salaam na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania (JMT) kupitia Wizara ya Fedha, kitengo cha fedha za nje.
Mwakilishi wa Serikali ya Denmark katika taasisi ya PASS ni Mh. Balozi wa Denmark na
mwakilishi wa serikaliya JMT ni mkurugenzi wa idara ya kuondoa umaskini katika
Wizara ya Fedha na Mipango. PASS inafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la
serikali ya Denmark (DANIDA).

Walengwa wa Mfuko
Mtu binafsi, vikundi vilivyosajiliwa, vyama vya wakulima au kampuni zinazojishughulisha
na miradi mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa kilimo (mazao,mifugo na uvuvi).

14
Vigezo vya Mikopo
a) KwaWaombaji wote
i. Kujaza fomu ya maombi ya huduma za PASS.
ii. Taarifa ya benki kwa miezi 12
iii. Ainisha mradi/biashara na mahitaji na Gharama zote zinazotakiwa katika mradi
wako.
iv. Kuchangia asilimia 25 ya gharama za mradi/biashara
v. Ainisha uzoefu katika mradi au biashara hiyo.
vi. Utambulisho kutoka mamlaka husika mahali mradi unapofanyika
vii. Uthibitisho wa Dhamana ya mkopo (kama leseni za makazi, dhamana za
kuhawilishwa, Hati ya nyumba na nyinginezo)
viii. Cheti cha usajili wa biashara Kama mradi/biashara imesajiliwa
ix. Leseni ya biashara (kama ipo)
x. Kulipia Ada ya maombi ya huduma za PASS

Pamoja na vigezo vilivyoainishwa kwenye kipengele (a) hapo juu,


yafuatayo ni vigezo vya ziada kwa aina mbalimbali za waombaji:

b) Mtu binafsi

i. Cheti cha usajili wa biashara Kama mradi/biashara imesajiliwa


ii. Leseni ya biashara (kama ipo)

c) Vyama vya Wakulima (AMCOS, SACCOS) naVikundi Vilivyosajiliwa

i. Cheti cha usajili wa biashara– Kama mradi/biashara imesajiliwa


ii. Leseni ya biashara (kama ipo)
iii. Mizania ya Mahesabu yaliyokaguliwa (Audited report)
iv. Muhtasari wa mkutano mkuu wa Chama
v. Namba ya TRA ya uthibitisho wa mlipa kodi(kama unayo)
vi. Cheti cha usajili wa SACCOS/AMCOS
vii. Masharti/katiba ya chama
viii. Wasifu wa viongozi
ix. Ukomo wa madeni kwa ajili ya SACCOS/AMCOS

d) Makampuni
i. Mahesabu ya Kampuni ya miaka 3 iliyopita yaliyokaguliwa
ii. Mahesabu ya kampuni ya mwaka husika mpaka mwezi wa mwisho kabla ya
maombi.

15
iii. Makadirio yote ya mradi kwa kipindi cha mkopo
iv. Wasifu wa Wakurugenzi
v. Mwongozo wa kampuni
vi. Marejesho ya kampuni ya mwaka ulioisha yaliyowasilishwa BRELA
vii. Cheti cha usajili wa kamapuni
viii. Leseni ya biashara na cheti cha kulipa kodi
ix. Makubaliano ya kikao cha bodi ya kampuni kuomba dhamana ya PASS
x. Mchanganuo wa biashara
xi. Dhamana za mkopo
xii. Uthaminishaji wa dhamana inayowekwa

Kabla Baada

Nyumba bora iliyotokana na kipato cha familia kuongezeka baada ya kuwezeshwa na PASS kupata
mkopo wa kunenepesha ngombe huko Monduli, Arusha

Kwa maelezo zaidi wasiliana Na:


MKURUGENZI MTENDAJI
JENGO LA PATEL , GHOROFA YA 3,
MTAA WA KISUTU
S.L.P 9490, DAR ES SALAAM
SIMU: +255 222110394/95;
FAX +255 222110392
B ARUA PEPE: pass@pass.ac.tz,
WEBSITE : WWW.PASS.AC.TZ

16
6. MFUKO WA KILIMO KWANZA
(AGRICULTURE FINANCING WINDOW)

UTANGULIZI
Mnamo mwaka 2009, Serikali ilifikia uamuzi wa kukuza
sekta ya kilimo na kuboresha uzalishaji kupitia azma ya
Kilimo Kwanza. Ili kutekeleza azimio hilo, Serikali ilitenga kiasi cha fedha shilingi
bilioni 42 za kitanzania kwa ajili ya kukopesha katika miradi yakilimo. Serikali iliiteua
benki ya TIB Development ltd na kuipa mamlaka ya kukopesha na kusimamia fedha
hizo kwa kufungua Dirisha maalumu la mikopo ya kilimo. Dhumuni kubwa ikiwa ni
kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya serikali katika kuwaletea wananchi
maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umaskini.

TARATIBU NA MASHARTI YA MIKOPO (lending guidelines)


1. Huduma (products)

Mikopo chini ya dirisha la kilimo inatolewa kuwezesha shughuli za uzalishaji, usindikaji


mazao na masoko (masoko ni kwa wakopaji wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji na
usindikaji wa mazao ya kilimo). Mikopo inayotolewa ni ya muda mfupi, muda wakati na
muda mrefu. Mwongozo unatambua shughuli za kilimo kuhusisha uzalishaji mazao
pamoja na ufugaji.

2. Walengwa

i) Wakulima wadogo wadogo na wakati waliojiunga katika vyama vilivyosajiliwa na


mamlaka husika kama vile Ushirika, na vikundi (out-growers of larger farms).
ii) Wakulima wa kati na wakubwa wanaoendesha kilimo cha kibiashara kupitia
makampuni. Uainishaji wa mikopo midogo, ya kati na mikubwa unazingatia Sera
yaTaifaya SME.
iii) Shughuli za kilimo za kati zinazoongeza thamani kama vile uhifadhi, usindikaji na
masoko.
3. Gharama zinazoambatana na mikopo

i) Riba inatozwa kwa kiwango cha asilimia tano (5%) kwa mwaka kwa wakopaji wa
moja kwa moja toka benki (direct borrowers). Taasisi zinazokopa kwa ajili ya
kukopesha (on-lenders) zinatozwa asilimia nne (4%) kwa mwaka ambapo
zitatakiwa kukopesha kwa asilimia isiyozidi nane (8%) kwa wakulima/wateja
wao. Viwango vya riba vinaweza kubadilika itakapobidi.
ii) Ada za kibenki (bank charges)zote zinazohusiana na mkopo ikiwa ni pamoja na
gharama za ushuru wa stampu, usajiri wa hati za dhamana, mikataba na
huduma mbalimbali zikiwemo za kisheria zitalipiwa na mkopaji.
iii) Kwa taasisi za kifedha (on-lenders), ada zote (bank charges) za mkopo
zitakazotozwa kwa mkulima (final borrower) zinatakiwa zisizidi asilimia mbili
(2%).
17
4. Muda wa Marejesho ni kati ya miezi sita hadi miaka kumi na tano (15) kwa
kutegemea aina ya mradi wa kilimo pamoja na makadirio ya hesabu (financial
projections).

5 Kipindi cha rehema (Grace period) kinatolewa kulingana na kipindi cha kukomaa
kwa mazao husika pamoja na makadirio ya mtiririko wa fedha (projected cash flow).
Katika kipindi hicho mkopaji atatakiwa kulipia riba ya mkopo ingawa malipo yatazingatia
msimu wa mapato.
Masharti husika kwa mkopaji atapatiwa na wahusika katika tawi na kanda husika.

Kwa maelezozaidiwasilianana :

MkurugenziMtendaji
TIB Development Bank,
S L P 9373,
DAR ES SALAAM

7. MIFUKO YA UDHAMINI WA MIKOPO

Chimbuko la Mifuko ya Udhamini wa Mikopo


inayosimamiwa na Benki Kuu:

Mageuzi katika sekta ya fedha ya mwaka 1991 yalijenga


mazingira bora ya soko huria na kuboresha huduma za
kifedha nchini. Hata hivyo, upatikanaji wa mikopo, hasa
kwenye sekta ya kilimo na kwa wajasiriamali wadogo na wa
kati (SME) ilibaki kama changamoto.

Katika juhudi za kukabiliana na changamoto hizo, mnamo mwaka 2002/03, Serikali kwa
kushirikiana na Benki Kuu ilianzisha Mfuko wa kudhamini mikopo kwa ajili ya mauzo ya

18
bidhaa za Tanzania nje ya nchi (Export Credit Guarantee Scheme (ECGS)).Madhumuni
ya mfuko huu ni kuhamasisha uzalishaji kwa ajili ya mauzo nje ya nchi ili kuchangia
kukuza pato la Serikali. Halikadhalika, katika mwaka wa fedha wa 2004/05, Serikali
ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa mikopo ya miradi midogo na ya kati(Small and
Medium Enterprise – Credit Guarantee Scheme (SME-CGS)). Mfuko huu unalenga
kukuza na kuendeleza miradi midogo na ya kati (SMEs) kwa kujenga mazingira ya
kuwezesha wajasiriamali wenye miradi midogo na ya kati kupata mitaji kwa njia ya
mikopo ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika ukuzaji wa uchumi, kukuza ajira na
kupunguza umaskini. Mifuko hii inasimamiwa na Benki Kuu chini ya makubaliano na
Serikali (Agency Agreement) kama njia ya mpito hadi hapo itakapoanzishwa taasisi
inayojitegemea.

Walengwa na Dondoo za Mifuko ya Udhamini:


Na. MAELEZO MFUKO WA ECGS MFUKO WA SME-CGS
1. Walengwa Mfuko unalenga wakopaji Mfuko unalenga wajasiliamali
wenye miradi mikubwa yenye wenye miradi midogo na ya kati
mahitaji ya kifedha ya kuanzia yenye mahitaji ya kifedha ya
TZS 500 million na kuendelea. kuanzia TZS 5 milionihadi TZS
500 milioni na itakayotolewa
kwa kipindi cha kati ya mwaka
1 hadi miaka5.
2. Kiasi cha Udhamini wa Mfuko huu ni Udhamini wa Mfuko kwa mkopo
Udhamini asilimia 75 (75%) kwa mikopo wowote hautazidi asilimia 50
ya muda usiozidi mwaka 1 na (50%) na hautahusisha riba
asilimia 50 (50%) kwa mikopo katika kipindi chote chamkopo.
itakayotolewa kwa mwaka 1 na
zaidi. Udhamini hautahusisha
riba katikakipindi chote
chamkopo.
3. Ada ya Mifuko itazitoza taasisi za fedha ada ya udhamini ya asilimia moja
Udhamini (1%) ya kiasi kitakachodhaminiwa kwa mwaka wa kwanza na
asilimia moja (1%) ya kiasi kinachobakia kwa miaka inayofuata.

Utaratibu wa utoaji Udhamini:


i. Wakopaji wanapaswa kupeleka maombi ya mikopo moja kwa moja katika benki au
taasisi ya fedha zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Mabenki naTaasisi za Fedha ya
Mwaka 2006.
ii. Baada ya kuchagua benki au taasisi ya fedha, muombaji atapeleka upembuzi
yakinifu wa mradi wake na mahitaji mengine kadiri benki au taasisi ya fedha
itakavyoelekeza.

19
iii. Benki au taasisi ya fedha itafuata taratibu zote za kibenki kabla ya kupitisha mkopo,
ikiwa ni pamoja na upembuzi makini wa mradi husika, kuangalia taarifa za muombaji
kuhusu taarifa ya mikopo mingine, aliyokwishawahi kupata na kusajiliwa (Credit
Information Bureau).
iv. Baada ya benki au taasisi ya fedha husika kuridhika na ubora wa mradi wa mkopaji
na kuridhia kutoa mkopo, benki au taasisi ya fedha itawasilisha maombi ya udhamini
kwenye mifuko husika ya udhamini, endapo mkopaji hatokuwa na dhamana ya
kutosha kupata mkopo.
v. Baada ya udhamini kutolewa, benki au taasisi ya fedha husika inawajibika kufuatilia
maendeleo ya mradi na marejesho na kuwasilisha taarifa kwenye mfuko wa
udhamini.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na :-


Kurugenzi ya Masoko ya Fedha
Idara ya Udhamini waMikopo
2Barabara yaMirambo,
11884 Dar es Salaam,
Simu: 2233568/2233569 | Nukushi: 223 4072
Barua Pepe: cgs @bot.go.tz
Tovuti: www.bot .go.tz

8. MFUKO WA KUENDELEZA WAJASIRIAMALI WANANCHI (NEDF)

Mfuko wa kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) ulianzishwa mwaka 1994 kwa


Azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kutoa mikopo kwa
wenye viwanda vidogo na wafanyabiashara wadogo Tanzania Bara kwa lengo la
kuondoa umasikini kwa kuanzisha na kuendeleza miradi yao katika sekta mbalimbali.

Mfuko huu unasimamiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kupitia ofisi
zake za mikoa.

Masharti/Vigezo vya utoaji Mikopo chini ya mfuko huu


i. Muombaji awe ni raia wa Tanzania
ii. Mradi/Biashara unaoombewa mkopo uwe umeasajiliwa
kihalali na wenye uwezo wa kukopesheka
iii. Makazi ya Muombaji yawe ya kudumu na yanatambulika
na kiongozi wa serilali za Mitaa

20
iv. Muombaji wa mkopo awe ndie mmiliki halali wa Mradi
v. Muombaji awe na uwezo na nia ya kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa
vi. Muombaji wa mkopo awe tayari kufungua akaunti ya Benki kwa jina la biashara
yake
vii. Kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja muombaje awe na wadhamini wawili wenye
dhamana
viii. Kwa Mikopo ya Vikundi muombaji awe tayari kujiunga kwenye vikundi vya
mshikamano na kuweka akiba ya mkopo kama dhamana ya mkopo

Muundo wa Mkopo

i. Muda wa Marejesho ni kuanzia miezi 6-36 kulingana na kiwango cha Mkopo


ii. Marejesho ya mikopo ya vikundi hufanyika kwa wiki au Mwezi
iii. Riba ya mkopo ni asilimia 18% kwa miradi ya uzalishaji na asilimia 22% kwa
miradi ya biashara
iv. Kiwango cha mkopo ni hadi shilingi milioni tano kwa miradi ya uzalishaji kwa
mikopo ya mtu mmoja mmoja.
v. Kiwango cha mikopo ya vikundi ni hadi Shilingi 500,000/= kwa mwanakikundi

Kwa maelezo zaidi wasiliana na anuani hapo chini au tembelea Ofisi


yeyote ya Mkoa iliyo karibu nawe.

SIDO Makao Makuu


Mfaume Road,
Upanga,
P.O. Box 2476,
Tel: (022) 2151945/8
E-mail: dg@sido.go.tz
Wed-site: www.sido.go.tz
Dar es Salaam.

21
9. MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (YDF)

Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) ulianzishwa rasmi


na Serikali mwaka 1993 chini ya Sheria ya Fedha (The
Exchequer and Audit Ordinance, cap 439), namba 21 ya
mwaka 1961 kifungu cha 17 (1). Lengo la kuanzishwa
kwa Mfuko huu ni kuwawezesha vijana kupata mitaji kwa
njia ya mikopo yenye masharti nafuu ili kuanzisha au
kuendeleza miradi yao ya uzalishaji mali. Mfuko huu
unasimamiwa na Halmashauri zote nchini Tanzania Bara.

Utaratibu wa kutoa na kurejesha mikopo ni kama ifuatavyo:-

(i) Kikundi cha Vijana ndicho huomba mkopo ambao hutolewa kupitia SACCOS ya
Vijana ya Halmashauri ya Wilaya husika.lengo ya kupitisha fedha hizi kwenye
SACCOS ni kuwapa vijana wenyewe umiliki na kujenga tabia ya kuweka na
kukopa miongoni mwa vijana
(ii) Wizara hupeleka fedha kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya (DED) ambaye
naye huzipeleka kwenye SACCOS husika. Wizara humwelekeza kwa maandishi
ni kikundi gani kinastahili kupewa mkopo.
(iii) Kikundi cha Vijana kabla ya kupewa mkopo, hubuni mradi na kuandaa andiko
ambalo hufanyiwa uchambuzi na kuthibitishwa na DED husika. Baadaye mradi
na taarifa za uhalali wa kikundi hupelekwa kwa RAS ambaye ndiye huleta
maombi hayo kwa Katibu Mkuu – Wizarani.
(iv) Wizara hufanya uchambuzi wa mradi, huchunguza taarifa za Halmashauri na
Mkoa kupitia fomu maalum iliyoandaliwa. Inapoonekana mradi unaoombewa
mkopo unafaa, hupewa mkopo.
(v) Mkopo urejeshwa Wizarani kupitia kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Halmashauri ya Wilaya husika baada ya kupokea fedha hizo kutoka kwenye
SACCOS ya Vijana ya Halmashauri yake.

22
(vi) Muda wa marejesho kwa sasa ni miaka miwili (2)
(vii) Riba ya mkopo ni 10% ambapo 5% ubakizwa kwenye SACCOS ya Vijana ili
kuiongezea mtaji. Aidha, 2% ubakizwa kwenye Halmashauri husika ili
kuwezesha usimamiaji, ufuatiliaji na uratibu wa mikopo itolewayo na Mfuko
katika maeneo yao. Aidha, 3% inayobaki urejeshwa kwenye Mfuko ili
kuuwezesha kuwa endelevu.

Kwa huduma hii, tafadhali tembelea Halmashauri yeyote iliyo karibu nawe.

10. MFUKO WA PEMBEJEO WA TAIFA

Mfuko wa Pembejeo (The Agricultural Inputs Trust Fund) ulianzishwa mwaka wa 1994
kwa Sheria ya Bunge Na. 9 ya mwaka wa 1994.Hivyo, kazi ya Mfuko wa Pembejeo ni
pamoja na:-
 Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa ajili ya
kugharamia usambazaji wa pembejeo za kilimo, uvuvi,
dawa za mifugo na zana ndogondogo zinazotumiwa
katika sekta hizo.
 Kuhakikisha kuwa pembejeo zinawafikia wakulima,
wavuvi na wafugaji kwa wakati na kwa bei nafuu.
 Kutoa mikopo ya matrekta mapya, matrekta madogo (power tiller) na kukarabati
matrekta machakavu ili kuboresha na kupanua maeneo ya kilimo nchini.
 Kufuatilia marejesho ya mikopo iliyotolewa ili Mfuko uwe endelevu (Revolving) na
waombaji wengine waweze kukopeshwa.

Walengwa wa mikopo ya mfuko wa pembejeo

a) Wakulima /Wafugaji katika vikundi kama vile:-


i. Mifuko ya Pembejeo ya wilaya.
ii. Vyama vya Ushirika vya Msingi,
iii. Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS),
iv. Vikundi vya uzalishaji katika kilimo na ufugaji vilivyosajiliwa,
b) Mawakala binafsi wa usambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo ikiwa ni
pamoja na mbolea, mbegu na madawa ya mifugo na mimea.
c) Watu binafsi wanaotaka kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta,
23
d) Wakulima wa kawaida pamoja na wale wa kilimo cha mkataba.
e) Mashirika yanayojishughulisha na kilimo pamoja na Taasisi za dini.

Aina ya mikopo inayotolewa, riba na muda wa mkopo

i. Pembejeo za kilimo, Uvuvi na Ufugaji, muda wa mikopo ni miaka miwili kwa riba
ya asilimia nane (8%) kwa mwaka.

ii. Mikopo ya matreka mapya, muda wa mikopo ni miaka mitano kwa riba ya 6-7 %
kwa mwaka.

iii. Mikopo ya matrekta madogo ya mkono (Power tiller), muda wa mikopo ni miaka
mitatu kwa riba ya 6-7% kwa mwaka.

iv. Mikopo ya kukarabati matrekta; muda wa mikopo ni miaka mitatu, riba 6-7%
kwa mwaka.

v. Mikopo ya nyenzo za umwagiliaji / Uchimbaji visima, muda wa mikopo ni miaka


mitatu kwa riba ya asilimia 6-7% kwa mwaka.

vi. Mikopo ya nyezo za usindikaji wa mazao, muda wa mkopo ni miaka mitatu kwa
riba ya asilimia 6-7% kwa mwaka.

Masharti ya kutoa mikopo

i. Mwombaji awe na dhamana ya mkopo isiyohamishika yenye hati miliki


inayokubalika na sheria za ardhi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
ii. Waombaji wa matrekta mapya, sharti wawe na mashamba yenye ukubwa
usiopungua ekari 50, kwenye wilaya ambako maombi yamepitishwa.
iii. Wasambazaji wa pembejeo, sharti wawe na uzoefu katika biashara hiyo kwa kipindi
kisichopungua miaka miwili. Mwombaji pia anatakiwa awe na leseni hai ya
biashara.
iv. Maombi lazima yaambatane na andiko la mradi likieleza shughuli inayoombewa
mkopo, mizania ya mapato na matumizi, na matarajio ya faida itakayopatikana ili
kumwezesha kurejesha mkopo katika kipindi muafaka.
v. mwombaji anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi kwenye Halmashauri ya
Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji husika ambako atapatiwa fomu ya maombi.
vi. Fomu ya maombi itajazwa na mwombaji na kuambatanishwa na kivuli cha hati
miliki ya dhamana, Ankara vifani, andiko la mradi, leseni ya biashara kwa
msambazaji wa pembejeo na barua ya uthibitisho wa kumiliki ekari 50 kutoka
Serikali ya Kijiji liliko shamba.

24
vii. Fomu iliyoambatanishwa na vielelezo vyote itawasilishwa kwa afisa Kilimo wa
wilaya hsuiaka ili ipitishwe.
viii. Fomu za maombi zilizopitishwa na Halmashauri ya Wilaya/Mji/ Manispaa
zitawasilishwa Mfuko wa Pembejeo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana Na:

Mkurugenzi Mtendaji
Mfuko wa Pembejeo
S. L .P 32081
DAR ES SALAAM
Simu: 022 2700191
Nukushi: 022 2774850
Barua pepe: agitif@kilimo.go.tz
Tovuti: www.agitf.go.tz

11. MFUKO WA KUWASAIDIA MAKANDARASI (CAF)

Historia ya Mfuko na Madhumuni Yake.

Bodi ya Usajili wa Makandarasi ilianzishwa kwa


mujibu wa sheria Na. 17 ya 1997 kama
ilivyorekebishwa mwaka 2008. Kazi za Bodi ni pamoja
na kusajili makandarasi, kuratibu mwenendo na kazi
zinavyofanywa na makandarasi na kuendeleza
makandarasi.

Bodi ya Usajili wa Makandarasi ilianzisha mfuko wa


kusaidia Makandarasi (Contractors Assistance Fund – CAF) mwaka 2002 kwa lengo la
kusaidia Makandarasi wazalendo kupata dhamana za zabuni na malipo ya awali. Bodi
inashirikiana na Benki kutoa dhamana hizi.

Madhumuni makuu ya Mfuko ni kusaidia Makandarasi wazalendo wadogo na wa kati


kuweza kupata dhamana za zabuni na malipo ya awali kama njia ya kuwawezesha
kushiriki katika kazi za ujenzi. Walegwa wa mfuko huu ni Makandarasi wazalendo wa
madaraja ya VII - IV kwa kazi za kawaida na daraja la III – II kwa kazi maalumu.

25
Vigezo vya wanufaika wa mfuko

Ili kunufaika na huduma za mfuko, walengwa wa mfuko kama walivyoainishwa


wanapashwa kujiunga ili kuwa wanachama wa mfuko.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na :


Msajili,
Bodi ya Usajili wa Wakandarasi,
S .L. P 13374,
Tetex House, 3rd Floor
E-mail:crbhq@crbtz.org
DAR ES SALAAM

12. MFUKO WA NISHATI VIJIJINI (REF)

Historia ya Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini ulianzishwa kwa Sheria Na. 8 ya


Mwaka 2005 na kuanza kazi rasmi mwezi Oktoba 2007,
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nishati
ya Mwaka 2003. Sheria ya Nishati Vijijini pamoja na
kuanzisha Wakala, pia imeanzisha Bodi na Mfuko wa Nishati
Vijijini.

Mfuko wa Nishati Vijijini (REF)

Mfuko wa Nishati Vijijini unasimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini kwa niaba ya Bodi.
Sheria pia imebainisha uwepo wa Wakala wa Amana (Trust Agent) pamoja na
majukumu yake. Wakala wa Amana huratibu upelekeji wa fedha kwa watekelezaji
pamoja na ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi husika mara baada ya
mikataba kusainiwa kati ya mtekelezaji na Bodi ya Nishati Vijijini.
Majukumu ya Wakala

Wakala unatekeleza majukumu yafuatayo kama yalivyoainishwa katika Kifungu cha 16


cha Sheria ya Nishati Vijijini:-

i. Kubuni, kuendeleza, na kutoa misaada ya kitaalamu kwa waendelezaji wa miradi


ya nishati vijijini;

26
ii. Kuainisha na kutathmini miradi ya nishati inayostahili ufadhili wa Mfuko wa
Nishati vijijini;
iii. Kuwajengea uwezo waendelezaji wa miradi ili kutekeleza mipango endelevu ya
nishati vijijini;
iv. Kuibua, kuhamasisha na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini;
v. Kuhamasisha matumizi ya nishati bora katika shughuli za uzalishaji mali, kilimo,
viwanda vidogo na vya kati na biashara ili kukuza uchumi vijijini;
vi. Kuwezesha upatikanaji na matumizi ya nishati bora kwa ajili ya huduma za
ustawi wa jamii vijijini kama vile afya, elimu, maji na mawasiliano.

Katika kufanikisha majukumu hayo, Wakala hutekeleza yafuatayo:-

i. Kuainisha miradi inayoweza kusaidia upatikanaji wa nishati bora vijijini;


ii. Kutoa mafunzo ili kuwajengea uwezo waendelezaji wa miradi ya nishati;
iii. Kutoa misaada ya kiufundi kwa waendelezaji wa miradi;
iv. Kutoa ruzuku kwa ajili ya upembuzi yakinifu, kuandaa mpango biashara na
upembuzi wa athari za mazingira kwa miradi ya nishati vijijini; na
v. Kutoa ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nishati vijijini.
.
Walengwa wa Wakala

Wakala hutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi za umma, sekta binafsi,
asasi zisizo za kiserikali na taaisisi za jamii ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi wa
vijijini wanapata huduma za nishati bora.

Fursa kwa Waendelezaji wa Miradi (Project Developers)

Fursa za Fedha

a. Ruzuku (Grants)
i. Ruzuku kabla ya uwekezaji (pre investment grants)
ii. Ruzuku wakati wa uwekezaji (development stage)
b. Mikopo ya Muda Mrefu (credit line facility);
c. Malipo ya kupunguza Hewa ya Ukaa (Carbon credits/Clean Development
Mechanism)
d. Kushindanisha Miradi yenye Ubunifu, mfano Lighting Rural Tanzania Grant
Competition.

27
Fursa za Mafunzo

a. Mafunzo ya kuongeza ujuzi wa Ufundi – yanatolewa kwa nadharia na vitendo:


i. Teknolojia ya Nishati Jua (Solar Energy)
ii. Teknolojia ya Nishati Upepo (Wind Energy)
iii. Teknolojia ya Nishati Tungamotaka (Biomass Energy)
iv. Teknolojia ya Nishati ya Maporormoko Madogo ya Maji (Small
Hydropower).
b. Mafunzo ya Kutayarisha Mpango Biashara (Business Plan):
i. Kwa ajili ya kuomba ruzuku REA na wafadhili wengine
ii. Kwa ajili ya kuomba mikopo katika mabenki.
c. Mafunzo yanayohusu masuala ya mazingira na jamii.
Fursa ya kuwa kwenye Mtandao wa kubadilishana taarifa na Uzoefu

i. Tanzania Renewable Energy Association (TAREA)


ii. Tovuti ya REA (REA Website)
iii. Mtandao wa Taasisi zinazowekeza katika Miradi ya Nishati.

Ruzuku ya kazi za Mwanzo za Mradi (Matching Grant)

Kugharamia wataalamu waelekezi kwa ajili ya shughuli zifuatazo:

i. Utafiti wa awali na wa hatua za mwisho (Pre-Feasibility na Full Feasibility


Studies);
ii. Utafiti wa mazingira na mahusiano ya kijamii;
iii. Utayarishaji wa andiko la Mpango Biashara (Bankable Business Plan);

Vigezo vya kupata ruzuku

Vigezo vya kuzingatia kwa mwombaji anayeaka ruzuku kutoka kwenye mfuko wa nishati
vijijini ni kama ifuatavyo;

a. Miradi ya Nishati Vijijini;


b. Teknolojia isiyoharibu mazingira;
c. Vigezo vya Mwombaji:
i. Awe amesajiliwa kama kampuni, umoja au NGO au Taasisi ya Serikali;
ii. Awe na leseni ya Biashara;
iii. Awe na Akaunti ya Benki;

28
iv. Awe na hati/kibali cha kumiliki Ardhi;
v. Awe na kibali cha kutumia maji (kwa miradi ya small hydropower);
vi. Awe amekubalika na serikali ya kijiji/kata au wilaya ya mahali anapokusudia
kutekeleza mradi;
vii. Awe na kibali cha mazingira;
viii. Aonyeshe kuwa mradi wake ni shirikishi kwa jamii.

Kwa maelezo zaidi wasiliana Na:

Mkurugenzi Mkuu,
Wakala wa Nishati Umeme Vijijini,
SLP 7990,
Dar es Salaam.

13. MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF)

TASAF ni Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ulioanzishwa na Serikali Mwaka 2000, ukiwa ni


moja wapo ya jitihada zake za kupambana na umaskini
Tanzania kwa kutumia dhana yaushirikishwaji jamii.
TASAF imetekelezwa katika Awamu Tatu kamai
fuatavyo:-
Awamu ya Kwanza (TASAF I) ilitekelezwa kwa kipindi
cha miaka mitano kati ya mwaka 2000 – 2005,
katikaHalmashauri maskini 42 zikiwemo 40 za
Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba. Miradi
1704 ya sekta mbalimbali yenye thamani ya Shilingi
Bilioni 72 ilitekelezwa.

Awamu ya pili ya (TASAF II) ilitekelezwa kwa miaka nane kuanzia mwaka 2005 hadi
2013, katikaHalmashauri zote Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba. Jumla ya
miradi ipatayo 14,437 ya sekta mbalimbali yenye hamani ya Shilingi Bilioni 430
ilitekelezwa.
Kutokana na haja ya kuhakikisha kuwa kaya maskini sana zinawezeshwa kutumia
huduma za jamii zilizopo, Serikali ilianzisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika
Awamuya Tatu ya TASAF (TASAF III) ambayo ilizinduliwa rasmi Mwezi Agosti, 2012 na
utekelezaji unaendelea mpaka sasa.

29
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III)
Ni Mpango wa kuwezesha kaya Maskini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa
kugharamia mahitaji muhimu. Utekelezaji unahusisha halmashauri zoteza Tanzania Bara
na Unguja na Pemba. Muda wa utekelezaji ni miaka kumi ambapo patakuwa na awamu
mbili za miaka mitano kilamoja.

Mpangounasehemukuunne:

i. Uhawilishaji Fedha kwa kaya maskini:


Kutoa ruzuku kwa kaya maskini sana hususan zenye watoto ili ziweze kukidhi
mahitaji muhimu ya kiwemo huduma za elimu na afya. Pia kutoa ajira za muda
kwa kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa kipindi
cha hari.
ii. Kuongeza kipato kwa kaya maskini kupitia uwekaji akiba na kukuza uchumi
wakaya za walengwa kwaku wawezesha kuwa na vyanzo vingi vya kuzalisha
kipato na kutumia utaalamu na teknologia za kisasa.
iii. Kuongeza kipato na kuboresha miundo mbinu inayolenga sekta za elimu, afya na
maji.
iv. Kujenga Uwezo katika ngazi zote za utekelezaji. Kaya iliyoandikishwa itapata
huduma zitolewazo na vitengo vyote.

Walengwa wa Mpango

Ni kaya maskini sana zinazo ishi katika mazingira duni na hatarishi zilizotambuliwa
na kuorodheshwa kwenye daftari la walengwa

Vigezovya kaya maskini ni:

i. Ina kipato cha chinisananasi cha uhakika ukilinganishana kaya zingine za


Kijijini/Mtaa/Shehia
ii. Haiwezi kumudu au haina uhakika wa kupata milo mitatukwasiku.
iii. Inaishi kwenye makazi duni sana.
iv. Kaya yenye watoto wenye umri wa kuwa shule lakini hawajaandikishwa au
wameacha shule kwa kushindwa kumudu mahitaji muhimu.
v. Ina watoto ambao hawaendi kliniki kupata huduma za afya kutokana na
halingumu ya maisha ya kaya

30
Kwa maelezo zaidi wasiliana Na:

Mkurugenzi Mtendaji
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
S L P 9381
Kilwa / Malindi Rd
Simu: +255-22-2123583(Tel)
Nukushi: +255-22-2123582(Fax)
DAR ES SALAAM

14. MFUKO WA ELIMU TANZANIA (TEF)

Historia ya Mfuko

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilianzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Elimu Na.8 ya
mwaka 2001 Sura ya 412 ikiwa na jukumu la kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu
wa Taifa. Madhumuni ya Mfuko wa Elimu ni kuongeza nguvu za serikali katika
kugharimia miradi ya elimu ili kuinua ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa,
katika ngazi zote za Elimu kwa Tanzania Bara na Elimu ya Juu kwa Tanzania Zanzibar.

Sifa za mwombaji

Mfuko wa Elimu hutoa ufadhili kwa njia ya ruzuku na mkopo nafuu kwa shule na taasisi
za elimu za umma na binafsi ambazo zenye usajili wa Mamlaka husika kama ifuatavyo:

a) Vyuo Vikuu – Kamisheni ya Vyuo Vikuo Tanzania (TCU) angalau usajili wa muda
b) Vyuo vya Ufundi – Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE) angalau usajili wa
muda.
c) Vyuo vya Ualimu, shule za sekondari, msingi na awali- Wizara ya Elimu na
mafunzo ya Ufundi (Usajili kamili)

31
Maeneo ya Ufadhili
Katika kutekeleza jukumu la utoaji ufadhili, Mamlaka imeweka vipaumbele vya ufadhili
ambavyo huboreshwa kila Mwaka kwa kuzingatia Sera na Mahitaji ya Kisekta. Aidha
Maeneo haya hujadiliwa kwa pamoja na Wizara Mama ya Elimu, Sayansi Teknolojia na
Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Maeneo ya kipaumbele kwa ujumla wake yamekuwa ni:-

 Vifaa vya kufundishia na kujifunza kama vitabu, vifaa vya Maabara, mashine na
mitambo mbalimbali, vitabu vya kiada na zana nyingine za kufundishia.
 Upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA, kufunga mitandao
 Mafunzo kwa Wakufunzi katika fani Maalum kwa taasisi za elimu ya Juu;
 Vifaa zaidizi na vile vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi wenye mahitaji
maalum (wenye ulemavu)
 Programmu maalum kuwezesha wanafunzi wa kike kujiunga na michepuo ya
sayansi katika ngazi ya Vyuo vikuu na Vyuo vya Ufundi;
 Ujenzi wa miundombinu ikiwemo mabweni, kumbi za mihadhara, madarasa,
maktaba na ofisi
 Mikopo kwa ajili ya Ujenzi, upanuzi na ukarabati wa majengo kwa shule binafsi
na vyuo vya elimu ya juu.

Taratibu za kuomba ufadhili

a) Taasisi inayoomba ruzuku au mkopo nafuu inapaswa kujaza fomu maalumu za


maombi ambazo ni Na. F1/03, na Fomu hizi zithibitishwe na kuidhinishwa na
mkuu wa taasisi husika.
b) Fomu hizo zitumwe kwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Elimu Tanzania, S.L.P.
34578, Dar es Salaam.
c) Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti ya Mamlaka: www.tea.or.tz
Vigezo vya kuomba mkopo nafuu

Kwa upande wa mkopo ni lazima maombi yaambatane na nyaraka za kuombea mkopo


kama inavyoainishwa katika tovuti ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (www.tea.or.tz) ikiwa
ni pamoja na nyaraka zifuatazo:

a) Hesabu zilizokaguliwa za kipindi cha miaka miwili ya fedha.


b) Mtiririko tarajiwa wa fedha (Cash Flow projection) wakati wa kipindi cha mkopo.

32
c) Mpango wa ulipaji mkopo ukitaja pia fedha hizo zinapatikana vipi (Details of
repayment plan)
d) Dhamana ya mkopo mali isiyo hamishika (Collateral of immovable asset 150% of
the value of the loan)
e) Gharama za ujenzi

Mafanikio ya Ufadhili wa Miradi toka 2003/4 - 2015/16

Kati ya Mwaka 2003/4 na 2015/16 Mamlaka ya Elimu Tanzania imeweza Kwa ujumla
kufadhili na kutekeleza miradi 2,161 yenye thamani ya TZS Billion 109,954,926,454.00.
Miradi iliyofadhiliwa mingi. Baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha karibuni ni
pamoja na:-

i. Ujenzi wa Nyumba za waalimu katika mazingira magumu kufikika, zinazowezesha


familia 240 kuishi
ii. Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule za Sekondari
iii. Ukarabati wa Maktaba za mikoa mfano Mkataba ya Mkoa wa Mbeya
iv. Ukarabati wa shule kongwe za serikali 11
v. Mafunzo ya waalimu wakufunzi zaidi ya 2000
vi. Mafunzo ya kujenga uwezo wa kufundisha masomo ya Kiswahili Hisabati na
kiingereza kwa waalimu wa shule za msingi na mafunzo ya kujenga uwezo wa
kufundisha masomo ya Biolojia, Kiswahili, Hisabati na Kiingereza waalimu wa
shule za sekondari, waalimu takriban 33,00 wemenufaika.
vii. Kufadhili miradi katika Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) kutekeleza programu
za ‘’School Ranking’’ , pamoja upatikanaji wa ‘’SMS Portal’’ ya Baraza na
utayarishaji wa vitabu vya mwenendo wa majibu na matokeo ya maswali ya
Mitihani ‘’Question Perfomance Per Candidate’’ (QPC,books )’’
viii. Kufadhili ujenzi wa vyumba vya mihadhara katika vyuo vikuu kikiwemo Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine,

33
Vyumba vya mihadhara, vyuo vikuu

ix. Kufadhili ujenzi wa Jengo la Utawala na kuandaa Mitaala ya Masomo ya Sayansi


na Teknolojia kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Mwalimu
Julius K. Nyerere, (MJNUAT) kilichoanzishwa Butiama, Mara.

x. Utoaji madawati shule za Msingi , hususan kwa kushirikiana na wadau


mbalimbali wanaojitolea

Madawati kwa shule za Msingi

xi. Mamlaka pia hutoa ufadhili kwa upande wa Zanzibar ,ikiwemo miradi ya Ufadhili
Mafunzo ya awali (pre entry) wanafunzi wa kike katika Sayansi

xii. Kuiongezea uwezo Idara ya Uthibiti ubora wa Elimu Msingi na Sekondari katika
kutekeleza majukumu yake kwa kuanzia na ukaguzi wa shule zilizopata ufaulu
hafifu katika mwaka wa 2014;
Kwa maelezo zaidi wasiliana Na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Elimu Tanzania
S L P 34578
DSM

34
15. MFUKO WA UTT-MFI Plc

UTT Microfinance Plc ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Fedha na Mipango,


ilisajiliwa mnamo tarehe 28 Juni 2013, chini ya sheria ya makampuni ya sheria za
Tanzania (Companies Act, Cap 212, R.E 2002) na kuanza rasmi shughuli zake
mnamo tarehe 1 Julai, 2013 ili kutekeleza Sera za Serikali za uwezeshaji wananchi
kiuchumi hususan wenye kipato cha chini na cha kati kwa kutoa huduma shirikishi za
kifedha ikiwemo mikopo yenye mashariti nafuu.

Malengo ya Mfuko

i. Kutoa huduma shirikishi za kifedha na mikopo midogo midogo kwa Wananchi -


mmoja mmoja, vikundi, SACCOS, NGOs, wajasiriamali wenye mitaji midogo na ya
kati, na Taasisi zenye kutoa huduma kwa wananchi wenye vipato vya chini.

ii. Kuhamasisha na kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kuwekeza katika mifumo


rasmi ya masoko ya fedha na mitaji miongoni mwa wananchi wenye vipato vya
chini,

Kutoa huduma shirikishi za kifedha (financial inclusive services) kama vile; uwakala wa
bima, uwakala wa benki, uwakala mkuu wa miamala ya fedha kupitia mifumo ya
Tehama

HUDUMA ZA UBUNIFU NA KIPEKEE ZITOLEWAZO NA UTT-MFI

Na. Huduma Nia na Madhumuni Walengwa Malengo


/Mkopo
1 Nufaika Kutoa fursa kwa wamiliki wa Wamiliki wa Kuhamasisha na
loan vipande, hisa na hati vipande, hisa na kujenga desturi ya
fungani zilizosajiliwa katika hati fungani kujiwekea akiba na
Soko la Hisa (DSE) kupata uwekezaji ili kujenga
mikopo uwezo wa ndani kimtaji
(Domestic Capital
Formation)

35
Na. Huduma Nia na Madhumuni Walengwa Malengo
/Mkopo
2 Pamoja Kukidhi Mahitaji ya mitaji Wafanyabiashara Kuwezesha na
loan kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kuimarisha biashara na
wadogo wadogo ambao ambao ukuzaji/uwekaji akiba
kwa namna moja au wamedhaminiwa na kutoa ajira –
nyingine hawakopesheki na wenzao katika husussani akina mama
katika mabenki vikundi. na vijana
3 Taasisi kuziba nakisi ya kifedha na SACCOS na Kuzijengea uwezo
loan kuziwezesha SACCOS na Taasisi ndogo za taasisi hizo kutimiza
taasisi ndogo za kifedha kifedha malengo ya utoaji
zinazo zijihushisha na huduma za kifedha na
ukopeshaji ili ziweze kuwafikia
kuendelea kutoa mikopo wananchi/wahitaji
kwa wanachama wao walio wengi zaidi
4 Mshahar Kuwawezesha watumishi wa Wote Walio Kusaidia watumishi wa
a Loan Serikali kutimiza mahitaji katika utumishi umma kupata rasilimali
yao ikiwemo ununuzi wa wa umma na vifaa mbali mbali
vifaa vya mahitaji ya (Watumishi wa Fursa kwa watumishi
nyumbani kama vile Serikali, kujiwekea akiba
vyombo vya usafiri, Samani Mashirika na (Forced saving)
za ndani n.k. Taasisi za
Umma)
5 Hati Kuwawezesha watoa Watoa huduma Kuwawezesha watoa
Malipo huduma na wakandarasi na wakandarasi huduma na
loan (waliopewa mikataba na waliohakikiwa na wakandarasi
(Contrac Serikali na Taasisi za UTT MFI wazalendo/wazawa
t Umma) kupata fedha za katika jitihada za
financin kukidhi mahitaji ya mtaji kukuza ajira nchini
g) kwa kuzingatia kazi
walizopewa.
6 Bima Kutoa fedha kwa ajiri ya Wakopaji katika Kusambaza huduma za
loan kukidhi mahitaji ya bima ya mkopo wa bima nchini kote ili
Afya, mali, maisha n.k kwa Pamoja; Wamiliki kupunguza hasara
watanzania wenye mapato wote wa zitokanazo na
ya chini na kati. vipande, hisa na majanga/madhira
hati fungani mbalimbali yakiwemo
zilizosajiliwa magonjwa na uharibifu

36
Na. Huduma Nia na Madhumuni Walengwa Malengo
/Mkopo
katika Soko la wa mali usiotarajiwa.
Hisa la Dsm,
wafanyabiashara
wadogo wadogo
na watumishi
walio katka sekta
binafsi
7 Salary Kuwasaidia watumishi walio Watumishi wote Kutimiza mahitaji ya
Advance katika sekta ya umma walio katika dharura ya kifedha
loan kukidhi mahitaji ya dharura sekta ya umma
(Serikali na
Taasisi zake)
8 Special Kutoa mikopo kwa miradi Wamiliki wa Kusaidia kukuza
Projects mahususi ambayo inalenga viwanda vidogo ujasiriamali na
loan kuzalisha bidhaa vidogo vya uzalishaji wa ajira mpya
zinazoongeza thamani ya usindikaji, kwa vijana.
mazao na kuzalisha ajira usagishaji,
mpya. ufumaji,
utengenezaji
nguo, na
utengenezaji
bidhaa n.k
9 Micro Kuwawezesha Wafanyabiashara Kutoa huduma mbadala
Leasing wafanyabiashara wadogo wadogo na wa ili kusaidia ujasiriamali
loan kukidhi mahitaji yao ya kati; walio katika na uzalishaji wa ajira
kifedha ili kupata vifaa ushirikiano wa kwa Wananchi wa
wezeshi vya biashara kibiashara na; kawaida
zikiwemo mashine Makampuni
mbalimbali zitakazo tumika mbalimbali
kama nyenzo na kuleta tija
na ufanisi katika kazi/
biashara.
10 Micro Kuwawezesha wananchi wa Wananchi wa Kuunga mkono jitihada
Housing kawaida waishio mijini na kipato cha chini za Serikali katika
Loan vijijini kumiliki nyumba bora na cha kati na kuhakikisha wananchi
za kuishi watumishi wote wa kawaida wanakuwa

37
Na. Huduma Nia na Madhumuni Walengwa Malengo
/Mkopo
walio katika na Makazi Bora
Utumishi wa
Umma
11 School Kutoa mikopo inayolenga Wamiliki wa Kuisaidia sekta ya elimu
Improve kukidhi mahitaji ya upanuzi Shule binafsi na katika kuboresha
ment wa huduma ya elimu kwa za Serikali mazingira ya
Loan shule husika ikiwemo ufundishaji na utoaji wa
kujenga madarasa mapya, elimu iliyo bora kwa
ununuzi wa samani, ujenzi wanafunzi
wa uzio nk.
12 Sanitatio Kuwawezesha Wafanyabiashara Kutekeleza sera za
n Loan wafanyabiashara wa wadogo na wa Serikali katika
huduma za usafi kukidhi kati;wanaojishug kuhakikisha mazingira
mahitaji yao ya kifedha ili hulika na bora kwa kila
kupata vifaa wezeshi vya biashara za mwananchi na kuepuka
biashara zikiwemo mashine huduma za usafi magonjwa ya mlipuko.
na nyenzo mbalimbali za wa
usafi. mazingira,maji
taka na maji safi.
13 SME's Kuwawezesha Wafanyabiashara Kusaidia Serikali kutimiza
Industrial wafanyabiashara wenye au wamiliki wa malengo ya kukuza uchumi
Loan Viwanda vidogo na vya kati Viwanda vidogo kupitia viwanda na
kukidhi mahitaji yao ya na vya kati. biashara.
kifedha ya uendeshaji wa
kila siku.
14 Agri- Kuwawezesha wakulima Wakulima Kuwawezesha wakulima
Business wadogo wadogo waliopo wadogo wadogo kupata Pembejeo,mbegu,
Loan katika vikundi kupata ambao mbolea na vitendea kazi
mikopo ili kukidhi mahitaji wamedhaminiwa mbalimbali ili kuboresha
ya kilimo cha biashara. na wenzao katika kilimo cha biashara.
vikundi.

38
Hadithi za Mafanikio
Mteja wa Pamoja Loan: John Malima

Kwa majina naitwa John Malima,ni mteja ambaye nimenufaika na mkopo wa vikundi.
Nilijiunga na UTT Microfinance miaka miwili iliopita. UTT Microfinance imenisaidia
kukuza biashara yangu ya kutengeneza fredge ambazo zinatumika motuary. Nimeweza
kununua vifaa mbalimbali ambavyo nisingeweza bila mkopo. Nilianza UTT MFI na
mkopo wa TZS 500,000 na sasa nimefikia hatua ya kupata mkopo wa TZS 3,000,000.
Mafanikio mengine ni kwamba nimeweza kuajiri watanzania wenzangu nilianza biashara
yangu nikiwa na watu wawili na sasa nina watu sita ambao nimewaajir

Mteja wa Contract Financing: Egom Investment Ltd

Egom Investment Ltd ilianzishwa mnamo July 2013. Tulijiunga na UTT Microfinance Plc
2014 kama wateja wa mkopo wa Hati Malipo [Contract Financing]. Mkopo huo
ulituwezesha kufanya kazi mbali mbali za UTT Microfinance Plc. Tulifanya marekebisho,
matengenezo na ukarabati wa tawi lao la Zanzibar pamoja na Makao makuu ya UTT
Microfinance. Hii imetupa fursa ya kupanua wigo wetu wa biashara na kukutana na

39
fursa chanya kwa kampuni yetu. Kutaja wachache tumeweza kufanya kazi na UTT PID,
World Lung Foundation , NSSF na Amend ORG ( NGO ya kimarekani) . Binafsi
tumeweza kukuza kampuni yetu kwa kuajiri zaidi ya wafanyakazi wa msimu 300 kwa
mwaka na wafanyakazi wakudumu wawili. Kampuni yetu pia iko katika hatua za mwisho
za kupanda daraja kutoka daraja la 6 kwenda la 4. Tumeona mafanikio makubwa ya
kujiunga na UTT Microfinance Plc

Mteja wa Hati Malipo: Dellbics Group Ltd

Kampuni ya Dellbics Group Ltd ilianza rasmi mwaka 2009.Tumefaidika na mkopo wa


UTT Microfinace Plc. wa Hati Malipo ambapo ilitusaidia kuhakikisha kwamba
tunakamilisha kazi za ukarabati wa matawi yake. Lakini kwa kufanya hivyo kazi yetu
imeonekana kwa wengi na kutuongezea fursa za kupata kazi nyingine. Baada ya hapo
tumeweza kufanya kazi na Diocese ya Njombe pamoja na wateja binafsi. Tumekua
kiuwezo na uzoefu pia.Tunatarajia kufanya kazi nyinginie nyingi zenye tija na kuijenga
nchi kwa kupitia fursa mbalimbali zinazotolewa na UTT Microfinace Plc kwa siku za
usoni.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na


Afisa Mtendaji Mkuu,
UTT Microfinance Plc,
S.L.P 5474,
Ghorofa ya Nne Jengo la TANRE,
Mtaa wa Longido, eneo la Upanga.
Pia tuna matawi 12 katika mikoa ifuatayo;
Dar Es Salaam (5) Mwanza (2) Dodoma (1) Zanzibar (1) Mbeya (1) Arusha (2)

40
16. MFUKO WA UWEZESHAJI WA MWANANCHI (MEF)
Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi (MEF) ni moja ya mifuko ya uwezeshaji ambayo
inatumiwa na Serikali katika kusaidia utekelezaji wa jitihada mbalimbali za uwezeshaji
wananchi kiuchumi. Mifuko huu ulizinduliwa tarehe 23 Januari,
2008 ambapo malengo yake makuu yamekuwa ni kuondoa
tofauti za kiuchumi baina ya watanzania.Katika utekelezaji wa
malengo hayo Mfuko huu umekuwa ukiwezesha utoaji wa mitaji
kwa wajasiriamali kupitia program ya udhamini wa mikopo
inayopelekea uanzishwaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi
miongoni mwa watanzania.
MEF iko chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi
(NEEC) , ambayo ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2005 kwa Sheria ya Taifa
ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (sheria namba 16 ya mwaka 2004) ikiwa na jukumu
la kusimamia, kufuatilia na kuratibu masuala yote yanayohusika na uwezeshaji
wananchi kiuchumi.

Mfuko huu unafanya kazi katika Mfumo wa kutoa dhamana za Mikopo kwa kushirikiana
na Mabenki na Taasisi za Fedha, ambapo kwa sasa unafanya kazi kwa kushirikiana na
Benki ya TPB(TPB Bank Plc), katika programu ya udhamini wa mikopo kwenda kwa
vikundi vya VICOBA na vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS).

Walengwa wakuu wa Mfuko huu ni vikundi vya kiuchumi kama vile Vikundi vya VICOBA
pamoja na Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) hususani SACCOS za
Wanawake, Vijana na Bodaboda.
.
Vigezo vya Utoaji wa Mikopo
1. SACCOS
i. SACCOS iwe imesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika.
ii. Iwe na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia na kupata mafunzo kuhusu uendeshaji
wa SACCOS.
iii. Iwe na kamati ya mikopo iliyopata mafunzo ya namna ya kujadili, kutoa,
kusimamia na kufuatilia mikopo yote inayotolewa na chama.
iv. Iwe na katiba na sera zinazosimamia uendeshaji wa shughuli za chama kama
mikopo n.k
v. Iwe na Kamati ya Usimamizi iliyopata mafunzo ya namna ya kusimamia SACCOS.
vi. Iwe na uzoefu wa kukopeshana usiopungua mwaka mmoja na kuwa na kiwango
kizuri cha marejesho kisichopungua asilimia 95.
vii. Iwe na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za kiuhasibu za chama.
41
viii. Iwe na Ofisi inayotambulika.
ix. Utoaji wa mikopo uzingatie taratibu za ushirika kama kuwa na hisa na akiba
zinazotosha mkopo unaoombwa na mwanachama.
x. SACCOS itatakiwa kuweka asilimia 30(Cash Cover) ya kiwango cha Mkopo
itakayomba ambayo itatumika kama sehemu ya Dhamana yake kwa Mkopo
iliouomba

xi. Muda wa marejesho ya mkopo ni kati ya mwaka 1-2, hivyo hautazidi miaka
miwili.
xii. Kiwango cha Mkopo kwa Mwanachama mmoja mmoja katika SACCOS hakitazidi
Shilingi milioni 5.
xiii. Riba ni asilimia 13 kwa mwaka
xiv. Ada ya Mkopo ni asilimia 2
xv. SACCOS itakayohitaji kupata Mikopo katika Baraza la Uwezeshaji ni sharti ifungue
akaunti katika Benki ambayo inashirikiana na Baraza katika utekelezaji wa
Programu husika.
xvi. Mikopo yote itakayodhaminiwa na Baraza itatakiwa kukatiwa bima ya maisha ya
mkopo.

2. Kikundi cha VICOBA

i. Kikundi cha VICOBA kiwe kimesajiliwa aidha Ofisi ya Maendeleo ya Jamii au


Brella.
ii. Kiwe na uongozi uliopatikana kidemokrasia na pia kupata mafunzo kuhusu
uendeshaji wa mfumo wa VICOBA.
iii. Kiwe na kamati tendaji iliyopata mafunzo ya namna ya kujadili, kutoa, kusimamia
na kufuatilia mikopo yote inayotolewa na kikundi.
iv. Kikundi kiwe chini ya asasi/Taasisi inayotambulika kuwa ni Mwamvuli wa vikundi
vya VICOBA.
v. Kiwe na Katiba na sera zinazosimamia uendeshaji wa shughuli za kikundi kama
vile mikopo n.k
vi. Kiwe na uzoefu wa kukopeshana usiopungua mwaka mmoja na kuwa na kiwango
kizuri cha marejesho kisichopungua asilimia 95.
vii. Kiwe na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za kiuhasibu za kikundi.
viii. Kiwe na sehemu maalum inayotambulika ya kufanyia shughuli zao.
ix. Utoaji wa mikopo uzingatie taratibu kama vile, mkopo utakaotolewa usizidi mara
3 ya hisa ya mkopaji.

42
x. Kikundi kitatakiwa kuweka asilimia 30 (Cash Cover) ya kiwango cha Mkopo
kitakachomba ambayo itatumika kama sehemu ya Dhamana yake kwa mkopo
iliouomba.

xi. Muda wa marejesho ya mkopo ni kati ya mwaka 1-2 hivyo hautazidi miaka
miwili.
xii. Kiwango cha Mkopo kwa Mwanachama mmoja mmoja katika Kikundi cha VICOBA
hakitazidi Shilingi milioni 3.
xiii. Riba ni asilimia 13 kwa mwaka.
xiv. Ada ya Mkopo ni asilimia 2.
xv. Kila kikundi cha VICOBA kitakachohitaji kupata udhamini wa Mikopo katika
Baraza la Uwezeshaji ni sharti kifungue akaunti katika Benki ambayo
inashirikiana na Baraza katika utekelezaji wa Programu husika.
xvi. Mikopo yote itakayodhaminiwa na Baraza itatakiwa kukatiwa bima ya maisha ya
mkopo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia anwani ifuatayo;

Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
12 Barabara ya Kivukoni
S.L.P. 1734 Dar-Es-Salaam
Simu: +255 22 2137362
Simu/Nukushi: +255 22 2125596
Barua Pepe : neec@uwezeshaji.go.tz
Tovuti : www.uwezeshaji.go.tz

Benki ya Posta Tanzania (TPB)

Makao Makuu
LAPF Towers
Bagamoyo Road
P. O. Box 9300
Dar Es Salaam
Tanzania
Simu: +255 22 2110621/2
Nukushi: +255 22 2114815
Barua Pepe : corporateaffairs@postalbank.co.tz
au tembelea Tawi lolote la Benki ya Posta lililopo karibu nawe

43

You might also like