You are on page 1of 17

MUHTASARI NA MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA TATU WA WANAHISA

UNAOISHIA 31/12/2019

TAREHE

14/11/2020-JUMAMOSI

ENEO

VIP BLUE PEARL HOTEL UBUNGO PLAZA

MUDA

SAA 02:00 HADI SAA 11:00 JIONI

MAHUDHURIO

WANAHISA

Waliohudhuria wenyewe- 500

Waliotuma wawakilishi-20

WAKURUGENZI

1. Dr. Zaipuna Obedi Yona– Mwenyekiti wa Bodi na mwongoza kikao.


2. Abdala Gonzi-Mjumbe
3. Emanuela Kaganda-Mjumbe
4. Mwajuma Hamza-Makamu Mwenyekiti
5. Phinias Opanga-Mjumbe

UDHURU
Ian Semakande

KATIBU-Mohamed Issa Simbano

WAGENI WAALIKWA
CMSA (1), DSE (1), Arch financial ltd (1) na wanachama wa JATU PLC (75)
MC WA MKUTANO

Nicholous Hillmary Fuime

o Mapokezi
• Kujiandikisha kwenye daftari la wageni
• Kupata Chai
• Kuingia ukumbini
• Burudani kutoka kwa wasanii wa JATU PLC.
o Ukaribisho: MC kuwakaribisha wageni na wanahisa waliofika katika mkutano wa tatu
wa wanahisa wa JATU PLC na kuwapa maelekezo ya kupata kifungua kinywa na
kukaribisha walio nje ya ukumbi kuweza kuingia ndani ili mkutano uweze kuanza saa
tatu kamili.

o Maelekezo namna ya kuketi: Upande wa kulia wa ukumbi uliandaliwa kwaajili ya


wanachama na wanahisa wa JATU PLC na Upande wa Kushoto uliandaliwa kwaajili wa
wageni waalikwa waliojiandaa kujiunga na JATU.

o Taarifa juu ya vyombo nya moto: packing zote za bure zifanyike nyuma ya jengo
ambako ni packing zilizo chini ya jingo. Packing ya mbele ya jengo ziko chini ya
TARURA na zinalipiwa.

o Taarifa juu ya Nyaraka Muhimu: Kila mgeni aliefika kwenye mkutano alitakiwa kua
na nyaraka muhimu au kuonana na vijana wa TEHAMA waliokua nyuma ya ukumbi kwa
ajili ya kusaidia katika masuala ya technolojia na kupakua hizi nyaraka katika mtandao
wa www.jatukilimo.co.tz)

1. Kitabu cha Kula ulipwe


2. Information memorandum/Waraka wa matarajio
3. Muhtasari wa taarifa ya kifedha iliyofanyiwa ukaguzi ya mwaka (2019)
4. Muhtasari na maazimio ya Mkutano mkuu wa pili wa wanahisa kwa mwaka 2018
5. Orodha ya wanahisa wote wa JATU PLC
6. Safari ya Jatu kuelekea soko la Hisa.

o Salamu ya JATU: JATU…Jenga Afya, Tokomeza Umaskini.


KUINGIA KWA MEZA KUU UKUMBINI

MC: Wimbo maalum kwa ajili ya kukaribisha wageni wa meza kuu ukumbini, na kabla ya
kufungua mkutano wajumbe wawili walituongoza kwa kuanza na sala, ili kupata baraka kwa
yale ambayo tunaenda jadili katika mkutano wetu, lakini pia sala hutuongoza kuanza salama na
kumaliza salama kikao chetu.

Madam Eva – kuwakilisha wakristu

Ustaadhi kuwakilisha waislam

MC: Utambulisho

Mc alianza kwa kujitambulisha na kuwashukuru ndugu wajumbe kwa kuitikia wito na kufika
kwa wingi. Kwenye meza kuu kuna makundi matatu, wajumbe wa bodi, watendaji wa Jatu Plc
na wageni waalikwa. Utambulisho wa wajumbe wa bodi ni kama ifuatavyo:

1. Dr. Zaipuna Obedi Yona– Mwenyekiti mwongoza kikao.


2. Abdala Gonzi
3. Emanuella Kaganda
4. Mwajuma Hamza
5. Phinias Opanga
6. Ian Semakande - Udhuru
Watendaji wa Jatu Plc wanawakilishwa na;

1. C.E.O – Peter Isare


2. General Manager – Issa Simbano
3. Finance Director – Aloyce Mushi

Wageni waalikwa, wanachama wa JATU PLC mabibi na mabwana itifaki imezingatiwa.

KUFUNGUA MKUTANO

Mwenyekiti: Dr. Yona alianza kwa kuwasalimu wageni waliohudhururia mkutano lakini pia
kuwakaribisha wanachama wote na wanahisa watarajiwa kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa
wingi katika kuhudhuria mkutano mkuu wa wanahisa watatu. Alisema kwamba “kama upo hapa
ndani leo wewe sio wa kawaida, na ninaamini hautabaki wa kawaida”. Alimaliza na kufungua
mkutano rasmi saa 04:35 asubui.

KUTHIBITISHA AKIDI

Katibu alianza kwa salamu ya JATU, kisha kutoa utaratibu wa akidi kwa kufuata katiba ya
kampuni (MEMART) inayowaongoza kunapokua na mikutano mikuu. Baada ya muongozo
kutoka kwa katibu mwenyekiti aliendelea na kikao.
KUTHIBITISHA AJENDA

Baada ya wajumbe kupitia agenda, mwenyekiti alikaribisha maoni kutoka kwa wanachama.
Lakini pia kwa faida ya wale ambao hawakuweza kua na ratiba, mwenyekiti alimkaribisha katibu
kuweza kuzisoma tena kwa wajumbe.

Katibu alianza kwa kusema kuna agenda 15 ambazo zilitumwa kabla ya siku 21 kutokana na
masharti ya katiba inavyosema kua kabla ya siku 21 ya mkutano mkuu wa wanahisa tangazo
linatakiwa kutolewa, kama tangazo letu linavyojieleza “Taarifa inatolewa kwamba mkutano
mkuu wa wanahisa na wakulima na wageni waalikwa uliositishwa tarehe 28/04/2020 baada ya
kuibuka kwa ugonjwa wa virusi vya corona utafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 14/11/2020
katika ukumbi wa VIP Blue Pearl Hotel, Ubungo plaza DSM. Agenda zitakazojadiliwa ni kama
ifuatavyo;

1. Kufungua Mkutano
2. Kuthibitisha Akidi
3. Kuthibitishwa na kupitishwa kwa Agenda
4. Yatokanayo na mkutano mkuu wa pili wa wanahisa uliofanyika tarehe 27/04/2018
5. Taarifa ya mchakato wa kuingia soko la Hisa
6. Ripoti ya kilimo kwa msimu 20/21
7. Kuzindua miradi mipya ya Kilimo 2020/2021
8. Huduma za uwakala ndani ya JATU PLC
9. Taarifa fupi ya Bodi
10. Taarifa ya kifedha iliyofanyiwa ukaguzi mwaka 31/12/2019
11. Gawio la Hisa 2019
12. Mapendekezo kutoka kwa wanahisa
13. Masuala mengineyo
14. Maamuzi ya mahali na tarehe ya mkutano ujao
15. Kufunga kikao.
Baada ya katibu kumaliza kusoma agenda kwa wajumbe Mwenyekiti aliuliza swali kama
wameafiki agenda na wajumbe wote walijibu NDIO, kwa kuridhia kwao kulimruhusu
mwenyekiti kuidhinisha kukubalika kwa agenda alitoa wasaa wa kutizama makala fupi kuhusu
historia ya JATU PLC.

MUHTASARI NA MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU 2018 KIUJUMLA.

Maadhimio yaliyotokana na mkutano mkuu wa pili wa wanahisa unaoishia 31/12/2018 yalikuwa


kama zifuatavyo,

ü Agenda ya 8, Kupitishwa gawio la faida lililopatikana kiasi cha Tsh 15,985,735,


ambapo walipendekeza kuwa ziongezwe kwenye hisa zao badala ya pesa taslim.
ü Agenda ya 9, Kupitishwa kwa makadirio ya bajeti ya fedha Tsh 7,500,000,000/=.
ü Agenda ya 10, Wanahisa walipitisha kiasi cha Tshs 200,000/= kwa wakulima
wanaoshiriki mradi wa umwagiliaji mkoani Manyara wilaya ya Kiteto kwa heka
moja, wanaomiliki hisa watachangia 30,000/= na wakulima wa Morogoro ni
20,000/=
ü Agenda ya 6, kupokelewa kwa ripoti ya bodi, kupitishwa kwa maamuzi ya
kuvunjwa kwa bodi ya mpito na kuundwa kwa kamati maalum ya usimamizi
ambayo itasimamia upatikanaji wa bodi mpya.

Baada Ya Kuwasilishwa Agenda Tajwa kuhusiana na ukamilifu wa taarifa, Mwenyekiti


alikaribisha maswali, maoni, au marekebisho yoyote kwa wanahisa baada ya muhtasari
kumalizika kusomwa. Hapakuwa na maswali wala maoni yoyote kwa hiyo kikao kiliendelea
baada ya kupokelewa kwa muhtasari wa 2018.

Baada ya mkurugenzi kukaribishwa, alisalimia kwa salamu maalum ya JATU akataoa ufafanuzi
zaidi kuhusu muhtasari uliokwisha kusomwa na Katibu, akasema ‘takribani mwaka mmoja na
nusu sasa hatujakutana tangu kupitishwa kwa maadhimio yaliyo kuwepo kwenye mkutano wa
mwisho wa mwaka wa 2018, sasa mkifutatilia kwa makini mtagundua vitu vya muhimu
tulivyokubaliana kwa ajili ya utekelezaji hadi tunapokutana tena leo bado hatujavikamilisha”. Ila
kwa leo nitajikita kwenye ajenda namba 5,6,7, na 8 kama ifuatavyo;

o Suala la soko la hisa


o Uzinduzi wa miradi mipya ya kilimo kwa msimu wa 2020/2021 na;
o Huduma ya uwakala wa bidhaa za Jatu Plc
o Kula ulipwe kampeni

Mchakato wa kuingia katika soko la hisa , ambapo ilikuwa ni moja ya lengo kuu la kampuni
kuingia DSE, baada yakufanikiwa kusajiliwa tarehe 20/10/2016 , kama kampuni ya umma
BRELA na kuhakikisha mchato wote wa kumalizia usajili wa kampuni katika soko la hisa
unafanyika kwa haraka na kwa wakati, ambapo vitu vilivyo hitajika ilikuwa ni rasilimali watu na
muundo wa mchakato mzima wa uendeshaji wa kila siku wa kampuni , walezi wa kutuongoza
ambao ni wasimamizi mbali mbali wakishirikiana na watalaam wa mambo ya fedha na kisheria
ambapo yote haya yanahitaji muda kujipanga.

MAMBO MUHIMU YA KUJUA PINDI JATU ITAKAPO INGIA KWENYE SOKO LA


HISA.

MKURUGENZI alitambua uwepo wa wanahisa wa makundi mawili tofauti la kwanza ni wale


wenye hisa kwa bei ya Tsh 2500/= na wale wa 1000/=, lakini pia idadi ya jumla ya wanahisa ni
1243 baada ya kufanya SHARE SPLIT (ONGEZEKO LA HISA) ambapo jumla ya hisa zitakazo
orodheshwa ni 2,164,349, kwa bei ya hisa moja itakuwa ni Tsh. 420. Hii ni kutokana na ripoti ya
kitalaam ambapo kilichofanyika kwa watu wa VALUATION REPORT juu ya thamani ya
kampuni ni kwamba kwa aliyenunua hisa moja kwa bei ya Tsh.2500 hisa hiyo imezaa ongezeko
la hisa 5 kwa aliyenunua kwa bei ya tsh.1000 imezaa hisa 2 na kwa aliyenunua kwa bei ya Tsh.
500 (Right Issue) hazijaongezeka zimebaki kama zilivyo.

Hivyo kwa kifupi JATU PLC haitafanya IPO bali inaenda kuorodhesha wanahisa wa awali
kwenye soko ili wale waliokuwa wameomba kurudishiwa fedha zao za hisa waweze kuziuza na
wale ambao wanahitaji hisa za JATU PLC waweze nunua, pia ili kupunguza ugumu kwa wale
waliotaka kuingia kwenye miradi ambapo kigezo cha kwanza ni lazima uwe mmiliki wa hisa,
ambapo ifikapo tarehe 23/11/2020 hisa za JATU PLC zitaingia sokoni rasmi kwa bei ya awali ya
Tsh. 420/=. Hivyo kwa wale wakulima ambao wanalima na Jatu niwakumbushe kuwa
makubaliano yetu ya kuwa na hisa 200 ni muda muafaka sasa kuhakikisha kila mmoja anatimiza
vigezo na masharti ili kuwa mkulima wa JATU PLC.

MUONGOZO WA HISA UTAKAVYO KUWA SOKONI.

Ifahamike kuwa hisa hazitakuwa zinauzwa na Jatu bali na watu wenye mamlaka hayo wanaoitwa
“Brokers” ndo wata shughulikia mchakato mzima ambaye pia tumemualika siku ya leo, ili aweze
toa elimu na miongozo pamoja na taratibu kwa wanahisa pindi hisa zitakapo ingia sokoni hiyo
tarehe 23/11/2020, na michakato yote juu ya uwendeshwaji wa kampuni itawekwa wazi ili kila
mtu afahamu uelekeo wa kampuni kwa ajili ya uwekezaji wake ndani ya JATU PLC. Pia
niwaombe msiondoke maana baadae tutakua na mtalaam kutoka Arch Financial Ltd yeye atatoa
ufafanuzi na elimu zaidi kwa kuwa wao ndo wenye mamlaka na uzoefu
KUUZA NA KUNUNUA HISA ZA JATU PLC

Masuala yote ya kununua na kuuza hisa kwa sasa yatashughulikiwa na mamlaka husika, akasema
“watu wengi wataingiwa tama ya kutaka kuondoka wakati huu wa mwanzo, ila niwahakikishie tu
kwamba tunaamini kesho itakuwa bora zaidi kuliko leo, hivyo nashauri mkiwa kama wanahisa
waanzilishi wa Jatu muendelee kuwepo mpaka mabadiliko yatakapo tokea na wote tufurahie
matunda ya kuanzishwa kwa JATU Plc”. Jambo muhimu la kuzingatia katika ununuzi na uuzaji
wa hisa inahitaji muda wa kutafakari zaidi usichukue tu maamuzi ya mkumbo au harakaharaka,
pia tutakuwa na wageni wengine tutawakaribisha kwenye mchakato huu ambao wanaweza
wakawa na haiba tofauti na sisi lakini tukubaliane nao katika kujifunza yale mambo mema
ambayo yatakuwa kwa ajili ya kunufaisha nakuleta ustawi wa kampuni yetu.

KUTHIBITISHA BODI YA WAKURUGENZI ILIYOPO NA KUJAZA NAFASI


ZILIZOWAZI

Mkurugenzi mkuu aliendelea kusisitiza kuwa tunaishi na kuongozwa na kile ambacho


tulikubaliana siku ya kwanza ambapo, kikibadilika msidhani kampuni itaishi kwa muda mrefu
kama lengo litapotea. Bodi tuliyonayo inapaswa kuongezwa kama katiba yetu inavyosema lakini
pia kwa kuzingatia sheria na kanuni za mamlaka ya Masoko ya dhamana na mitaji.

Hivyo tumeamua kuomba ushauri juu ya namna ya kutengeneza bodi ambayo ni pana na yenye
uwelewa tofauti tofauti na inajua nini kinaweza kufanyika katika kuhakikisha kuwa wazo la
JATU lina jengwa na kuimarika siku nyingi za usoni.

Bodi itakuwa na watu angalau 9, ambao watakuwa ni watu wenye ufanisi na uzoefu katika
biashara ambao watagawanyika katika makundi mawili ambayo ni wenye hisa nyingi na chache
wanaojulikana kama “Representative for majorit shareholders” na wale wenye hisa chache
wanao julikana kama “Representative for minority shareholders” pili tutakuwa na kundi la
waanzilishi wa kampuni ya JATU ambao hawa kazi yao kubwa nikusimamia malengo ya
kuanzishwa kwa kampuni hadi yatakapo timia, hawa haijalishi wana elimu gani bali watakua
wamebeba maono ya kampuni kwa manufaa ya wanahisa wote.
MATEGEMEO KUHUSU MIRADI MIPYA YA KILIMO 2020/2021.

Mwaka 2020 mambo yatakuwa mazuri maana jatu itaingia rasmi kwenye soko la hisa na itakuwa
inaaminika, hivyo mahitaji makubwa ya bidhaa zetu yataongezeka pia, hii itasababisha kampuni
ifanye vizuri zaidi, tutaweza kutimiza ndoto ya Jatu na kutosheleza soko la Africa mashariki.

- Tunatarajia kuwa na bei ya chini kuliko bidhaa zingine kwenye maeneo tutakayo
kuwepo.
- Pia tunaenda ongeza mawakala wengi ili kutusaidia kumfikishia mlaji bidhaa zetu kwa
urahisi zaidi kwa kuanza tunaanzia mkoa wa Dar es salaam kisha tutapanua wigo kwa
kuhakikisha tunafika kila mkoa, Ila kwa sasa tumefungua ofisi ambazo zinatoa huduma
kikanda.
- Tutafungua pia na Supermarket zenye bidhaa za Jatu zakutosha.
- “KULA ULIPWE” kampeni hii tutazidi iboresha ili kuhakikisha tunapanua wigo wa
masoko yetu ambapo gawio la faida litatolewa kwa kila mtu na kila mwezi kwa mtu
anaetumia bidhaa za jatu. Hivyo unaweza kukuza gawio lako na kupata gawio la
kudumu.
- Kipaumbele cha JATU PLC kutokana na idara ya miradi na utafiti ni kuibua miradi mingi
katika maeneo mbali mbali nchini kwani bado uhitaji wa bidhaa za nafaka ni mkubwa
mfano mboga mboga, matunda viungo, na vinywaji, lakini pia sera yetu inasema
panapokuwa na shamba lazima kiwanda cha Jatu kiwepo, na hatutakusanya viwanda
sehemu moja bali sehemu tofauti tofauti kulingana na mradi husika.
- Bidhaa zote tunazokula majumbani kwa familia zetu zikinunua katika mfumo wa JATU
MARKET APP sisi wenyewe ni mabalozi katika kuwaingiza watu katika mfumo huu
changamoto tumeshaanza zifanyia kazi ikiwemo ubora na upatikanaji wa bidhaa zetu
ambazo zinazozalishwa kwa sasa ni;
Ø UNGA (sembe na dona)
Ø Maharage (Kilindi-Tanga)
Ø Mpunga (Kilombero, Morogoro)
Ø Mafuta ya kupikia ya alizeti (Manyara, Kiteto)
MAZAO MAPYA YANAYO ENDA KUONGEZEKA KWA MWAKA 2021/2022
Ø Viazi lishe (mkoa wa Ruvuma) ambazo zinaendelea kusafishwa.
Ø Vitunguu
Ø Ndizi
Ø Mboga mboga (Kimbiji wilaya ya Kigamboni Dar es salaam).

Pia tumeanzisha JATU TALK, ili kuwawezesha watu wenye mawazo, maono au mtaji ili
kuweza kushiriki vizuri, ambapo mtu atapata mtaji, soko na wataalamu kwa kushirikiana na
kampuni. Baada ya mkurugenzi kuwasilisha mwenyekiti alikaribisha maswali kutoka kwa
wanahisa na wanachama;

MASWALI, MAONI, USHAURI KUTOKA KWA WANAHISA NA WANACHAMA.

Neema kavishe” kuanzia leo tar 23 je mwanachama anaweza akanunua hisa kwa utaratibu ule
ule wa zamani au kuna utaratibu mpya?

Jibu lilijibiwa na Lukwalo Daniel Semboja ambaye ni wakala wa soko la hisa“ kwa njia ya
IPO haina charges zozote ambayo ikiingia soko la hisa kwa mara ya kwanza kama jatu
ilivyoingia , huwa inakuwa haina gharama , na kwa wageni wanaoingia kupitia IPO itakuwa ni
bure lakini zikisha orodheshwa kuna kuwa na gharama , kwa saa 420*1000=420,000/= bila
gharama , lakini kwa watakao nunua sasa majina yataorodheshwa na tuta toa fomu na wata weka
siku moja na wale watakao nunua siku hiyo kwa IPO.

Swali lingine lilielekezwa kwa mkurugenzi kutoka kwa bwana ‘Felix Mdesa’, kulikuwa nag
harama ambazo zilikuwa zina ambatana na kufikisha hisa katika soko la hisa ambayo ni 30,000/=
nafikiri, je kama itatokea kujisahau kwa wale wanahisa wa mwanzo kwa kutokulipia hiyo
30,000/= kwenye orodha, watakuwepo.

Jibu (kutoka kwa mkurugenzi mkuu)

Wote walio nunua hisa atakama ni HISA 2 au 3, majina yao tayari yalishwa orodheshwa na
kupelekwa DSE, hivyo sisi tutajua namna ya kumkaba kwakua tunataratibu zetu atakapo kulima
tutajua namna ya kufanya kwa upande wa kampuni.

Fredmod, (mwanahisa), nimesikia bei ni 420 @hisa, je kiwango cha mwisho cha hisa ni ngapi?
Jibu (kutoka kwa mkurugenzi mkuu) “angaalau hisa 50, ila kwa wakulima hisa za chini ni
kuanzia 200”

(Mwanahisa) Uzoefu nilionao kwenye kampuni zingine zinazoingia kwenye soko la hisa huwa
zinatoa upendeleo kwa wanahisa wa mwanzo kwa bei nafuu kidogo ili wawe tofauti na wale
wanao nunua (wapya), sijui kama hilo linawezekana. Pia ningependa kujua kama WARAKA
WA MATARAJIO (PROSPECTUS) ulishatoka ili tujue tunaongeza hisa au lah?

Jibu (kutoka kwa mwenyekiti)

Kama ulinunua hisa mwanzo kwa sasa wewe tayari unaupendeleo kwa maana ya kwamba kama
ulinunua hisa zako kwa bei ya 2500 utakuwa na ongezeko la hisa tano kwa kila hisa moja
uliyonunua kwa bei ya Tsh.2500 kwa kugawanywa kwa Tsh 500 kwa hisa moja, zaidi ya wale
wanahisa wapya, na maadhimio yalikuwa ni kutoa hisa kwa bei ya chini kwa wanahisa na lakini
kubwa zaidi ni kutokana na valuation ripoti. Pia prospectus imetoka, itafute kama hujaipata na
pia kwenye mitandao na tovuti ya JATU PLC unaeza kupata nakala ya soft copy.

Suzan (Mwanahisa), Tofauti ya hisa za JATU SACCOS LTD ambazo zinaendelea kuuzwa na
hizi zinazo ongelewa hapa ambazo zitakuwa na bei ya 420/=, je hisa hizo ni tofauti na hizo
ambazo tunatakiwa kulipa ambazo ni Hisa 50 kwa bei ya Tsh. 2500?

Jibu (kutoka kwa mkurugenzi mkuu)

Naomba nianze kuelezea tofauti ya JATU Plc na JATU SACCOS LIMITED ni kwamba hizo ni
taasisi mbili tofauti na zina uongozi unaojitegemea, hivyo ili uweze kulima na JATU Plc ni
lazima uende ukaombe mkopo Jatu Saccos ltd kama unataka kulima kwa mkopo au kama
unataka mkopo wa maendeleo, kifupi ni kwamba sisi funganisho letu la pamoja ni JATU Plc,
hivyo ili uwe mwanachama wa JATU saccos nilazima uwe mwanachama wa JATU Plc lakini
HISA hizi zinatofautiana kabisa. Mgongano ni kwamba kwetu JATU PLC tuna masharti
kwanza lazima uwe ni mwanahisa wa JATU ili uwe mmiliki wa kampuni lakini katika kushiriki
miradi inayofanywa na kampuni. Saccos wao wanasema watakupa mkopo ili ukalime na JATU
PLC, na utaratibu wa saccos zote nchini lazima uwe na Hisa, kiingilio na akiba na pia
wameweka utaratibu wao ambao ni lazima kuufata ili kukidhi vigezo vya kukopeshwa.
Dainess Byabato, Mwanahisa,

Share zilizopo hapa tayari ndo hizihizi zitanyambulishwa au? Kuna 200,000/=iliyosomwa na
katibu kwenye mchanganuo ambayo tulikubaliana kwamba itarudishwa kwa wale waliochangia.
Je hiyo pesa inaweza ikatumika kuongeza hisa kwa atakaetaka?

majibu kutoka kwa mkurugenzi mkuu,

Hizo zilizonyambulishwa apo ndo tayari zishafanyiwa mchanganuo na ndizo zinakwenda


kwenye hiyo bei ya 420/=, tarehe 23/11/2020, pia kama kuna changamoto zozote zipo fomu za
kuwa silisha changamoto yoyote unayokutana nayo na itafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.

Ni kweli 200,000/= uliikopesha kampuni itarudishwa kama tulivyokubaliana, hivyo basi kwa
atakae penda ataenda kwa broker na atamsaidia kumpa maelekezo zaidi.

Mwanahisa), Tangu nimenunua hisa hazijawahi orodheshwa kwenye ukurasa wangu wa simu ya
kiganjani yaani JATU MARKET APP, je tatizo ni nini?

Jibu (kutoka kwa mkurugenzi mkuu) Tumeanza mchakato huo kwenye App, lakini
tukasimama hatukumaliza kuwa fikia watu wote kwa wakati mmoja, lakini punde baada ya
kumaliza kuingia kwenye soko hili la hisa tutaendelea na mchakato wetu wa kuweka taarifa za
hisa za mwanachama husika na tutaweka mchakato mzuri wa kuona hisa zako kupitia JATU
MARKET APP, na kwa sasa kama unapata changamoto kuhusu taarifa ya hisa hakikisha una
kumbuka namba yako ya uwanachama na utaangalia tarifa zako kutoka kwa wahasibu wetu pale
utakapo kwama kabisa.

JOSEPH AMIN, “Nimejiunga mwaka huu na jatu lakini pia ili niweze kulima kwa mkopo
natakiwa nijiunge na JATU SACCOS, ambapo nilipewa masharti ya kununua hisa, sasa basi
JATU Plc nilijiunga na nilisha anza kulipia kukodi shamba kwa ajili ya kilimo, je ili niweze
kutambulika kama mkulima wa JATU ni lazima niwe na hisa 200 na je kima cha chini kwa
mgeni aneanza ni ngapi?

Je nikitaka kuingia jatu plc bila mkopo, je ni lazima niingie jatu saccos?
Jibu (kutoka kwa mkurugenzi mkuu)

“Kama unajitosheleza unaweza lima pasi jiunga na SACCOS, lakini ishu ni kwamba pesa
utakayo tumia wewe ya kulima hekari tatu (3), ukiingia JATU Saccos kwa pesa hiyo hiyo unaeza
ukalima hekari tisa (9), ndo mana tunashauri uingie JATU Saccos lengo letu has ani kulima
hekari nyingi zaidi ili kupata malighafi zakutosha kwaajili ya kulisha viwanda vyetu na kupata
bidhaa za chakula zakutosha hata mwaka mzima, na pia faida ya JATU SACCOS LTD
inapunguza sintofahamu, ama maswali kuhusu hasara yoyote ukiipata, lakini kwa kuongezea
ukitaka kulima na JATU PLC lazima uwe na hisa 50 moja hadi kumi, ila kwa hekari zaidi ya
kumi ni hisa 200, ambapo ukienda Saccos wao nao wanautaratibu wao kutokana na sheria za
ushirika, ambapo wao bei ya hisa moja ni Tsh.2500 na unapaswa kuwa na hisa kuanzia hisa 50.

TAARIFA YA KIFEDHA NA GAWIO LA FAIDA KWA MWAKA 2019

Taarifa hii ilisomwa na mkuu wa idara ya fedha, kama ifuatavyo:

Mafanikio (mauzo)

Mauzo yalikuwa ni mara mbili kati ya mwaka 2018 ni sawa na Tshs million 250,000,000/=na
2019 ni million 564,000,000/=

MAPATO YA SIYO RASMI (tshirt, fomu n,k)

2018 ni million 145,000,000/= na 2019 ni million 318 hivyo yameongezeka kwa 120%.

MATUMIZI KWA UJUMLA MWAKA 2019.

Ni million 661,000,000/= kulinganisha na mwaka uliopita gharama zinaongezeka kwa sabbu


mbali mbali kama vile uchakavu wa mitambo, gharama za kuingia soko mla hisa.

FAIDA.

2019 kabla ya kodi million 40, 088,024/=

2018 kulinganisha na mwaka huu 15,985,735/=

N.B, kutoakana na uwekwzaji tunaofanya mitambo mingi tunayo nunua kuna kitu kinaitwa
“ware and care allowance” ambapo hii tunafaidika zaidi kwa ucahakavu wa msshine
unaohusishwa kimahesabu imetumika katika hali ambayo hatutaweza kulipa kodi mpaka apo
ambapo tutaongezeka kwenye mapato yetu lakini kwa sasa tunalipa tu kodi inayoitwa kodi ya
makadilio kwa kila mwaka.

KIPATO KWA KILA HISA KWA MWANAHISA KWA MWAKA 2019.

Hisa moja ni sawa n ash Tshs80.36/=, kutokana na kutolewa hisa za upendeleo kwa wanahisa
ambazo ni Tsh 500/= zilipunguza faida ikawa Tsh34.21/= lakini tunategeea tukiingia soko la hisa
hiyo hali itakuwa sawa na hisa zitapnda kulingana na mikakati yetu ambayo imelenga kuendelea
kukua kwa spidi na kuongeza uzalishaji ili kampuni kuzidi kutengeneza faida.

2019 tulitumia million 272, ambazo zilitumika kwenye uwekezaji wa mitambo 25%, kilimo ni
45%, godown, viwanja na majengo.

Pia tulikuwa na mkopom2018, ambayo ilitusaidia kugharamiashughuli za kampuni mpaka kufika


mwaka 2019, ongezeko hili ni sababu ya miradi mipya ya udhalishaji, kumalizika kwa sehemu
za viwanda na kufunguliwa kwa sehemu za kuuzia mazao yetu (Supermarkets).

MAONI YA KUHUSU TAARIFA YA KIFEDHA KUTOKA KWA MKAGUZI

Mkaguzi alisema hati ya taarifa aliyoipitia ni safi hivyo ili kupata taarifa hii kwa urefu zaidi
tembelea kwenye mtandao wa Jatu Plc ili uweze kuelewa zaidi.

GAWIO.

Faida iliyopatikana ni million 40,088,024/= lakini kwa sasa bodi inapendekeza kuwa pesa hiyo
isilipwe kwa wanahisa kama gawio bali iongezewe kwenye uwekezaji sababu kampuni yetu ipo
katika hatua za mwanzoni za ukuaji hivyo tunahitaji fedha nyingi zaidi.

Hisa zilizotolewa kwa mwaka 2019 (Issued share for 2019).

Zilitolewa kwa bei mbili kwanza ya 2500, ambapo ni jumla ya hisa 53790.

Na pili ni kwa bei ya 500 ambayo ni jumla ya hisa 919,000.


Baada ya ripoti ya fedha kuwasilishwa Mwenyekiti alikaribisha maswali kuhusu ripoti hiyo
kutoka kwa wanahisa;

“Mwanahisa” JATU ina miradi mingi mizuri, je kama mwanahisa ataenda nje ya mfumo wa
miradi ya Jatu. Je kampuni inaweza kununua mazao yake? kama maligafi?

Jibu Kutoka kwa mkurugenzi mkuu, “inawezekana, ila vigezo na masharti ya kampuni yetu
lazima vifatwe. Na kipaumbele ni kwa walikulima wetu waliolima na Jatu kwanza ili kuwapatia
uhakika wa soko kwanza na kama itatokea kampuni imepungukiwa ndo tunaweza kununua
kwako”

“Mwanahisa” kama mkulima naweza kutafuta soko nje, lakini si mwanachama wa jatu na
kumleta mteja na akawa anasambaziwa hizo bidhaa?

Jibu Kutoka kwa mkurugenzi mkuu, “ndio inawezekana”.

Swali kwa muhasibu kutoka kwa Mariam Godfrey Kusaja” kwenye gawio la mil 40,
naomba nielezwe faida ni kiasi gani? Thamani ni kiasi gani? Mpaka tunapata faida hiyo
uliosema?

Jibu; Hapo nimeelezea tu kwa ufupi lakini kwa upana zaidi rejea ripoti nzima ya fedha
inayopatikana kwenye tovuti yetu ya kampuni”.

Fatuma msuya “ukiagiza bidhaa kuanzia 30,000/= ulikuwa unaletewa bila ghrama lakini sahizi
mbona tuna chajiwa gharama ya usafiri?

Jibu kutoka kwa mkurugenzi mkuu, alisema faida ya bidhaa zetu zinabadilika kutokana na
umbali wanaoishi wanachama wetu, hivyo basi tulisitisha kusambaza bure sababu hiyo lakini
ilikuleta unafuuu wa gharama mwanachama unaeza kufidia hiyo kwenye gawio lako la kila
mwezi.”

Jumanne mwanga, kuna mpango gani wa kutumia malighafi zingine zinazo patikana kwenye
kilimo kama bidhaaa za malisho ya mifugo?
Jibu Kutoka kwa mkurugenzi mkuu

“Kuna mashudu yanapatina na pumba kutoka kwenye mahindi na alizeti ambapo huwa tunauza
lakini kwa sasa mkazo wetu mkubwa upo kwenye kuhakikisha tunakidhi mahitaji yote ya
mwanadamu kwanza alafu ndo tutakuja kwa wanyama wakufuga”

Mwanahisa, “nje na kuwasiliana kwa mtandao ni njia gani nyingine ipo ya mawasiliano maana
kwa sasa mtandao unasumbua sana!

Jibu Kutoka kwa mkurugenzi mkuu, ipo tunapatikana kwenye ofisi zetu zote, kwa hiyo
tembelea ofisi zetu za jatu zilizo karibu na unapoishi ambapo pia kwa sasa tumezigawa kikanda
zaidi mfano kanda ya pwani na Dar es salaam yote inahudumiwa na makao makuu ya JATU
PLC.

MAPENDEKEZO KUTOKA KWA WANAHISA

Katika ajenda hii Mwenyeketi alimkaribisha katibu kuwasilisha mapendekezo kama yapo
yaliyowasilishwa ofisini na wanahisa, ambapo katibu alisema hakuna mapendekezo yoyote
yaliyomfikia ofisini kwake na kila mwaka katika Mkutano Mkuu huwa tunatoa hii ajenda kwa
wawekezaji wet una wanahisa ili kupata maoni na mapendekezo yao juu ya nini wangependa
kifanyike au maboresho katika kampuni yao lakini hakuna hata mmoja aliyewahi leta.

Pia katibu alisisitiza kwa wanahisa wote pamoja na wanachama kua kuanzia sasa baada ya
kampuni kuingia soko la hisa lazima tubadilike yale maisha ya mazoea tuyaache kwanza
hatutatumia tena magroup ya whatsap kama sehemu yakupashana habari muhimu na nyeti za
kiofisi na magroup yote yatafungwa kisha tutatumia JATU TALK (MAZUNGUMZO YA
JATU) kama sehemu ya kukutana na kuzungumza mara kwa mara kwani dhana halisi ya
kuundwa kwa JATU TALK ni mazungumzo ya wanajatu ambayo hulenga mada mbalimbali
ikiwemo kuwakutanisha watu wenye mawazo na mitaji kisha kujadili kwa pamoja fursa za
kiuwekezaji.

Hivyo mnapo ona au kusikia matangazo, meseji au kupigiwa simu kuhusu mikutano mfike na
kama mtu anabanwa na majukumu bhasi tuma muwakilishi, lakini pia muwe mnasoma mihtasari
na maazimio yote ambayo yamejadiliwa na kupitishwa na wanahisa katika vikao mbali mbali,
ikumkumbukwe yanayopitishwa yanatuhusu sote, hivyo ni wajibu wa kila mwanahisa
kuhudhuria vikao vyote na kama hatofika bhasi atume muwakilishi kama tunavyofanya kwa
vikao vilivyopita na fomu za uwakilishi huwa zinatoka mapema kwa wale wanaotaka tuma
wawakilishi.

MENGINEYO.

Mwenyekiti alikaribisha mengineyo kutoka kwa wadau waliokuwepo kwenye mkutano;

o Ushauri ulitolewa na mama Nyakyoma Hasa Ukiwalenga Vijana, kwamba waitumie hii
fursa vizuri, ili waweze kujiwekea akiba zisizoisha za uzeeni, wasije wakafanya makosa
kama yeye aliegemea tu pesa ya kustaafia ndo iendeshe maisha yake na akapata
changamoto maana huwa hazitoshi.
o Obedi Daniel, alitoa maoni kuwa kampuni iendelee kuwahusisha kwenye mikuatno
mingine ata kama ni ile ile midogo midogo kabisa ili kusaidia kuleta uelewa zidi kwa
wanachama.
o Mohamed Magarya, alitoa shukurani kwa mkurugenzi mkuu kwa ushirikiano wake
aliouonyesha kwa kufika hadi shambani kwake kuangalia na akamshauri na mambo yake
yanaenda vizuri.
o Philip mathias, tunaomba muwape mafunzo wafanya kazi hasa kuhusu uendeshaji wa
kampuni yetu na namna ya kuhudumia watu maana sisi ni kampuni kubwa sana.
o Lini mnafunguo kituo Zanzibar? Mkurugenzi alijibu kwa kusema hivi karibuni jatu itafika
hadi Zanzibar na Africa nzima.
o Ushauri ulitoka kwa mwanachama philbert, kwamba kampuni inaweza ikaongeza zao
lingine la matunda la stafeli maana Tanzania yanastawi zaidi. Mkurugenzi akasema, hilo
linatakiwa liletwe kwenye ofisi zetu na yeyote mwenye wazo zuri tunaomba awasilishe
ofisini kwetu kupitia JATU TALK.

MAAMUZI YA KIKAO KIJACHO.

Kikao kitakuwa ni mwezi wanne (4) mwakani kuhusu tarehe tutawajulisha siku 21 kabla ya
mkutano mkuu ujao.
KUFUNGA KIKAO

Mwenyekiti aliairisha kikao majira ya saa 11:30 jioni ambapo kila dini ilitoa wawakilishi kwa
ajili ya kuongoza maombi kama ishara ya kushukuru kwa yale yote tuliyojadili na kuazimia
yaweze fanikiwa na hatimaye kufikia malengo tuliyojiwekea.

…………………. ……………

Mwenyekiti Katibu

You might also like