You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA


Anuani ya simu: “Msajili wa Hazina” Jengo la CHC zamani,
Dar Es Salaam 33 Mtaa wa Samora Machel,
Simu Nambari: +255-222-121-334 50 Mtaa wa Mirambo,
Nukushi: +255-222-110-046 Sanduku la Barua 3193,
Barua pepe: tr@tro.go.tz 11104 DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI YAKITWAA KIWANDA CHA KUCHAKATA KOROSHO LINDI (BUKO).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kupitia Ofisi ya Msajili wa


Hazina (OTR) yenye dhamana ya kusimamia mali za Serikali kwa sehemu
ambazo Serikali imefanya uwekezaji, imekitwaa Kiwanda cha Kuchakata
Korosho Lindi maarufu kama BUKO kilichojengwa mwaka 1978 na kufanya
uzalishaji kwa kipindi cha miaka nane tu kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani
10,000 kwa mwaka huku lengo likiwa ni kufikia tani 60,000 kwa mwaka.

Akizungumza katika kikao cha awali na Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi kuelezea


utaratibu mzima ulivyokua mpaka Serikali kufikia uamuzi huo kabla ya zoezi la
utwaaji wa kiwanda uliofanyika kiwandani eneo la Viwanda la Jamhuri
pembezoni mwa barabara iendayo Mtwara, Kaimu Msajili wa Hazina (TR)
Ndg.Peter Gwagilo, amesema hii ni sehemu tu ya utekelezaji wa kasi na Sera ya
urejeshaji viwanda vilivyobinafsishwa au kuuzwa na Serikali miaka ya nyuma na
kubainika kutofanya kazi kwa tija kama ilivyotarajiwa kwa mujibu wa mikataba
iliyoingiwa na wawekezaji husika hivyo viwanda kufa au kufanya kazi kwa
kusuasua kutokana na uwekezaji hafifu tofauti na makubaliano.

Kaimu Msajili wa Hazina akitanabaisha nia njema ya Serikali katika urejeshaji wa


viwanda vya mtindo huu amesema utwaaji hufanyika baada ya kujiridhisha
kutokana na zoezi linalofanyika kila baada ya miezi mitatu la ufuatiliaji na
tathmini kuangalia utekelezaji wa mikataba ya uwekezaji iliyoingiwa lengo
mahususi likiwa ni kujiridhisha utekelezaji wa mikataba ambayo Serikali
imeingia na mwekezaji.

Ndg.Gwagilo amewasihi wawekezaji walioingia mikataba ya uwekezaji na


Serikali kutekeleza kama mikataba inavyoainisha kwani zoezi la urejeshaji
Taarifa kwa Umma (OTR) Page 1 of 3
viwanda hivi bado ni endelevu na Serikali inaendelea na taratibu zinazotakiwa
katika kupata wawekezaji wengine wenye uwezo, tija na nia madhubuti ya
kuwekeza kwenye viwanda hivyo na tayari utwaaji huu umeshafanyika kwenye
mikoa kadhaa ikiwemo ya Kilimanjaro (Kiwanda cha kutengeneza madawa ya
mimea Moshi na Kiwanda cha Kukoboa Mpunga Kilimanjaro), Tanga (Kiwanda
cha Magogo ya Mbao) na sehemu nyingine kama Kiwanda cha Maziwa UTEGI
mkoani Mara, ambapo kwa awamu hii jumla ya viwanda 12 kikiwemo hiki cha
Korosho Lindi kilichokwishatwaliwa vinatarajiwa kurejeshwa Serikalini baada ya
kujiridhisha vya kutosha kuwa mwekezaji ameshindwa kuwekeza kulingana na
mkataba.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg.Godfrey Zambi akipokea ujumbe wa


wataalamu Wilayani Kilwa kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina na Ofisi ya Rais
tayari kwa zoezi hilo amesema, “Naishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa
Hazina kufanya maamuzi haya sahihi kwani kiwanda hiki hakijawahi kufanya
uzalishaji wenye tija kwa Taifa kama tulivyotarajia na hii inatokana na madhaifu
yaliyobainika katika zoezi zima la ubinafsishaji lililofanyika awali miaka ya
nyuma ambapo kwa sehemu kubwa mikataba hii ndiyo imeigharimu Serikali
yetu.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga ameitaka Ofisi ya


Msajili wa Hazina kutokata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali
inazokumbana nazo katika mazoezi haya ya ufuatiliaji, kufanya tathmini na
utwaaji pale inapolazimu kwani Serikali ni moja na hivyo ni vema kuwa na
utaratibu wa mawasiliano ya moja kwa moja na Msajili wa Hazina katika
kuyazungumzia haya kuepusha wazungumzaji wengi kwa jambo moja jambo
linaloweza kuleta upotoshaji wa taarifa.

Hali kadhalika nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ndg.Rehema Madenge


ameishauri Serikali kufanya maamuzi ya kukiendesha yenyewe kiwanda hiki
kutokana na uwekezaji na uendeshaji duni kabisa wa mwekezaji katika kiwanda
hiki uliopelekea kutokuwepo kwa uzalishaji na badala yake kutumia majengo
kama maghala ya kuhifadhia mazao na vitu mbalimbali kwa kuyakodisha kitu
ambacho ni tofauti kabisa na lengo la Serikali katika ubinafsishaji na uuzaji wake
kwa wawekezaji.
Taarifa kwa Umma (OTR) Page 2 of 3
Pamoja na hilo Ndg.Madenge amekiri kuwa nyota njema sasa inaonekana
kwani ni mwanzo mzuri kuanza kwa zoezi la utwaaji viwanda hasa katika mkoa
wake wa Lindi kwani bila hivyo Serikali itakua haiwatendei haki wakulima na
wananchi wake kwa ujumla kama viwanda vilivyo karibu nao havifanyi kazi ili
kupata soko la malighafi zao ambazo ni mazao yao.

Aidha, Katibu Tawala ameisihi pia Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina
kuhakikisha inawafanyia upekuzi wa kina sana kabla ya kuwachagua
wawekezaji wanaojitokeza na kuonyesha nia ya kutaka kupatiwa viwanda kwa
kubinafsishwa au kuuziwa ili kufanya uwekezaji wenye tija ili kuleta faida
itakayochagiza ukuaji wa uchumi wa nchi, kuboresha kipato na hali ya maisha
ya mwananchi mmoja mmoja hali kadhalika kukua kwa pato la Taifa.

Taarifa hai ya ufuatiliaji na tathmini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina imeeleza kuwa,


“Kulingana na Kifungu 7.1 na 7.2 cha Mkataba, mwekezaji alitakiwa kuwekeza
kiasi cha USD 600 kwa ajili ya kufanya ukarabati na kuboresha kiwanda ndani ya
miezi sita baada ya kukabidhiwa kiwanda tarehe 11 Mei, 2005; kulingana na
kifungu cha Mkataba 5.1. Mwekezaji alifanya uwekezaji mdogo kwa kukarabati
baadhi ya mashine pamoja na majengo. Hata hivyo, kiwanda kilifanya kazi kwa
mwaka mmoja 2007/08 na kusimamisha uzalishaji hivyo mpaka kufikia siku hii
ya kutwaliwa hakuna uzalishaji unaoendelea hivyo Serikali imefanya maamuzi
ya kukirejesha kiwanda hiki Serikalini kufuatia kusimama kufanya kazi kwa
muda mrefu na mwekezaji kutoonesha jitihada zozote za uendelezaji wa
kiwanda.”

Imetolewa na:

Gerard Julius Chami


Mkuu wa Kitengo
Uhusiano, Habari na Mawasiliano,
Ofisi ya Msajili wa Hazina,
LINDI.
09 Novemba, 2018.

Taarifa kwa Umma (OTR) Page 3 of 3

You might also like