You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


Anwani yaSimu “Hazina” DODOMA. Barabara ya Jakaya Kikwete

Simu Nambari: +255 – 26 - 2963101. Jengo la ‘Treasury Square’

Fax Nambari: +255 26 2963100 SANDUKU LA BARUA 2802,


Baruapepeps@mof.go.tz
40468 DODOMA,

TANZANIA.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKAGUZI WA MADUKA YA


KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI

Dodoma, 1 Aprili, 2019: Katika kutekeleza majukumu yake ya


kuhakikisha kuwa Sekta ya Fedha inachangia ipasavyo utulivu na ukuaji wa
uchumi nchini, Benki Kuu ya Tanzania ilibaini uwepo wa maduka ya
kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalikuwa yakiendeshwa pasipo kuzingatia
Sheria ya Foreign Exchange Act 1992, Kanuni za The Foreign Exchange
(Bureau de Change) Regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017 na
Taratibu za utoaji wa huduma za ubadilishaji wa fedha za kigeni. Kufuatia hali
hiyo, zoezi maalum la ukaguzi wa kina kwa maduka hayo lilifanyika Arusha
Novemba 2018 na kwa Dar es Salaam siku ya tarehe 27 Februari 2019, 1 na 8
Machi 2019 kwa kuhusisha vyombo vya Dola na kubaini ukwepaji mkubwa wa
kodi na uvunjaji wa Sheria.

Zoezi hili limebaini pia uondoshwaji wa fedha katika mfumo rasmi wa


fedha na kuelekezwa kwenye mifumo ya utakasishaji wa fedha haramu,
kupokea Amana kutoka kwa wafanyabiashara kinyume cha matakwa ya leseni
za biashara husika, kudhoofisha thamani ya shilingi, pamoja na mambo
mengine ambayo yalianza kuathiri usalama wa nchi kwa ujumla. Kwa mfano,
baadhi ya maduka yaligundulika kutumia fedha nyingi za Tanzania kununua
fedha za kigeni lakini fedha kidogo za kigeni ziliuzwa na hakuna taarifa ya
matumizi ya fedha za kigeni zilizobaki.

Ni vizuri ieleweke kuwa, zoezi la ukaguzi wa maduka ya kubadilisha


fedha za kigeni lilitekelezwa kwa kuzingatia Sheria za nchi tofauti na
malalamiko na tuhuma mbalimbali zilizotolewa za kudai uwepo wa ukiukwaji
wa Sheria na haki kwa wamiliki wa maduka hayo. Jambo la kushangaza ni
kwamba hakuna mmiliki yeyote wa duka aliyewasilisha malalamiko kuhusiana
na zoezi hili kwenye mamlaka husika. Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania na
1
Mamlaka nyingine za Serikali zinafuatilia kwa umakini ili kubaini ukweli wa
tuhuma hizo zinazotolewa.

Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza majukumu yake kwa umakini.


Hivyo, Serikali inauthibitishia umma wa Watanzania kuwa katika zoezi la
ukaguzi wa Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni hakuna fedha au mali
yeyote iliyotaifishwa. Taratibu za kisheria zilifuatwa wakati wa kuchukua
vielelezo mbalimbali zikiwemo fedha, kompyuta, simu za viganjani, mashine
maalum za kuhifadhi taarifa na taarifa mbalimbali ili kusaidia uchunguzi.
Aidha, lengo la zoezi hili sio kufuta biashara ya maduka ya kubadilishia fedha
za kigeni kwa watu binafsi, bali ni kudhibiti ukiukwaji wa sheria uliokithiri,
ukwepaji wa kodi na utakatishaji wa fedha haramu. Maduka machache ya
kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalizingatia Sheria na Kanuni za Foreign
Exchange na masharti ya biashara hiyo yaliachwa kuendelea na utoaji wa
huduma hiyo.

Hivi sasa Serikali imeandaa Kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya


maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba
leseni za uendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisi yeyote na
masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.

Kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo


hayatatoa athari kwa sekta ya fedha na uchumi jumla, na inakuwa yenye
manufaa kwa nchi. Kwa kuzingatia maduka mengi yaliyokaguliwa
yamefungwa, Benki Kuu ya Tanzania imechukua tahadhari ya kuhakikisha
huduma ya ubadilishaji fedha za kigeni inaendelea nchini kwa kutolewa na
benki zote pamoja na Shirika la Posta. Benki Kuu ya Tanzania itakuwa inatoa
taarifa kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo na kuzihimiza benki za biashara na
Shirika la Posta kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na huduma katika maduka
yaliyofunguliwa na benki hizo na Ofisi ya Posta.

Kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa biashara ya


kubadilisha fedha za kigeni, thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa
fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri. Kabla ya zoezi la
udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha ya kigeni dola ya Marekani ilikuwa
inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hivi
sasa dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,300. Aidha, Benki za
biashara kwa wastani hivi sasa zinakusanya jumla ya dola za Marekani milioni
15 kwa siku. Ni matarajio ya Serikali kuwa udhibiti huu utaziwezesha Benki za
biashara na taasisi nyingine kuuza fedha za kigeni kwa wingi kwenye soko la
fedha za kigeni na hatimaye kuongeza akiba ya fedha za kigeni.
2
Serikali inatoa tahadhari kwa wananchi kutoshiriki kwenye biashara ya
kubadilisha fedha za kigeni kwa njia zisizo halali. Hivi sasa kuna taarifa kwa
baadhi ya maeneo ya mipakani na majiji ya Dar es Salaam na Arusha
wamejitokeza watu wanaofanya biashara haramu ya kubadilisha fedha za
kigeni ambao wamewaathiri baadhi ya wananchi kwa wizi. Vyombo vya
usalama ikiwemo jeshi la polisi vimeongeza nguvu katika kuhakikisha biashara
hii haramu (Black Market) inatokomezwa na hivi sasa wahalifu saba
wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Serikali inapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa inayo akiba ya


fedha za kigeni ya kutosha zipatazo dola za Marekani bilioni 4.67 hadi tarehe
30 Machi 2019 zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi
kwa kipindi kisicho pungua miezi 4.8. Hivyo, wasiwasi kuwa Serikali
imechukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni
kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si ya kweli hata kidogo. Aidha,
hofu kwamba nchi inarejea katika kipindi cha nyuma ambapo fedha za kigeni
zilikuwa zinatolewa kwa vibali (rationing) ili kukidhi mahitaji ya fedha hizo
kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, nazo hazina msingi.

Mapato ya Nchi yanayotokana na vyanzo vya fedha za kigeni kwa kuuza


bidhaa na huduma nje ya nchi yalikuwa na thamani ya dola za Marekani
milioni 8,554.5 kwa mwaka unaishia Februari 2019 ikiwa ni ongezeko la
asilimia 1.4 ikilinganishwa na fedha za kigeni zilizopatika mwaka unaishia
Februari 2018. Ongezeko hilo la mapato ya fedha za kigeni kwa Nchi
yamechangiwa zaidi na uuzaji wa bidhaa zisizo asilia nje ya nchi zikiwa na
thamani ya dola za Marekani milioni 3,878.5 sawa na asilimia 10.3
ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Vile vile, huduma zilizotolewa nje ya
nchi kama vile usafiri na usafirishaji na utalii ziliingiza jumla ya dola za
Marekani milioni 4,074.1 sawa na ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa kiasi
kilichopatikana mwaka ulitangulia.

Aidha, Serikali inachukua fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa nchi yetu
ina akiba ya chakula cha kutosha ambacho kina utoshelevu wa asilimia 124
kwa mwaka huu wa fedha 2018/19. Hivyo, Serikali haitarajii kutumia fedha
za kigeni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi isipokuwa tu kama ikitokea hali
ya ukame ikawa mbaya katika siku zijazo.

Serikali, kupitia Benki Kuu ya Tanzania, inawataka wafanyabiashara ya


huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kuzingatia na kutii Sheria ya Foreign
Exchange 1992, Kanuni ya Foreign Exchange (Bureau de Change) Regulations
2015 na marekebisho ya mwaka 2017, Masharti ya biashara ya huduma ya
3
kubadilisha fedha za kigeni na Maelekezo ya Msimamizi (BOT) wa Sekta ya
Fedha Nchi. Mwisho Serikali inawapongeza wananchi wa Tanzania kwa kuwa
waelewa na watulivu wakati wote zoezi la ukaguzi likiendelea, licha ya
kujitokeza kwa taarifa za upotoshwaji wa zoezi hili.

IMETOLEWA NA:
DKT. PHILIP ISDOR MPANGO
WAZIRI YA FEDHA NA MIPANGO

You might also like