You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO CP SABAS, AMEAGIZA


GODBLESS LEMA (MB) ATAFUTWE NA AKAMATWE POPOTE ALIPO
KWA TUHUMA ZA KUTOA TAARIFA ZA UONGO

Ndugu Wanahabari,

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, mapema jana


amewasili mkoani Singida na kutoa ufafanuzi wa matukio ya mauaji ya watu 14
yaliotokea mkoani humo wilayani Manyoni kuanzia mwaka jana mpaka kwaka
huu mwezi wa pili.

Aidha katika kutoa ufafanuzi huo Kamishna CP Sabas alisema taarifa hizo za
uongo ambazo zilisambazwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema huku
akimtaka kujisalimisha katika kituo chochote cha Polisi, huku akitoa maagizo
kwa Kamanda Polisi Mkoa wa Singida kumtafuta Mh Lema popote alipo na
akamatwe.

Kamishna CP Sabas amesema Mnamo tarehe 29/2/mwaka huu huko katika


Wilaya ya Manyoni wakati wa kutoa salamu kabla ya mazishi ya marehemu
Alex Jonas ambaye alikutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
sehemu mbalimbali za mwili wake katika Eneo la Mbugani, Godbless Leama
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini alionyesha orodha ya watu 14
ambayo pia aliiweka katika mitandao ya Kijamii akidai waliuawa kwa
kuchinjwa Wilayani Manyoni bila ya kuwa na uhakika kama taarifa hizo ni
sahihi huku akilituhumu Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kushindwa kutekeleza
wajibu wake.
1
Cp sabas ameeleza ukweli wa matukio hayo ni kama ifuiatavyo;

1. Sichelela Mosses, (22), Mkazi wa Sayuni, tukio lililotokea tarehe 13/8/2019


majira ya usiku huko maeneo ya Mnarani barabara ya kuelekea Itigi ambapo
Binti huyo alikutwa ameuawa. Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa mauaji
hayo yametekelezwa na mume wake aitwaye Rashidi s/o Hamisi
akishirikiana na Timoth s/o Leonard, sababu ikiwa ni wivu wa mapenzi kwa
kumtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi watu wengine.
Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa pamoja na vielelezo vyote
vilitumika kwenye mauja hayo.

2. Abdallah Lyama, (38), Mkazi wa Kihanju, Itigi, alifariki dunia tarehe


26/8/2019 saa 2 usiku wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya St.
Gaspar Itigi, Wilayani Manyoni kutokana na shambulio la kupigwa kwa
fimbo pamoja na mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na
Rajabu s/o Juma, Msambaa, (42) akishirikiana na Haruna s/o Hamisi, kwa
pamoja walikuwa wanamtuhumu marehemu kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mtoto wa dada yake Rajabu s/o Juma, aitwaye Asha d/o Miraji,
Msambaa, (19). Tukio hilo lilitokea tarehe 25/8/2019 huko maeneo ya Mji
Mpya, Itigi walipomvizia marehemu akiongea na Binti huyo kichochoroni.
Mtuhumiwa Rajabu s/o Juma amekamatwa na juhudi za kumtafuta
mwenzake zinaendelea.

3. Rajabu Abasi, (36), alifariki dunia tarehe 14/9/2019 usiku akiwa anapatiwa
matibabu katika Hospitali ya St. Gaspar, Itigi kutokana na tukio la
kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtuhumiwa aitwaye Mohammed
Abdi, tukio lililotokea tarehe 13/9/2019 saa 3 usiku huko katika Kijiji cha
Mwamagembe. Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo
mtuhumiwa alimfumania marehemu akiwa na mke wake nyumbani kwa
mtuhumiwa. Mtuhumiwa amekamtwa na upelelezi umekamilika.

4. Martini Motekwa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, ambaye


inasadikiwa kuwa ana upungufu wa akili na akiwa hana makazi maalum,
mwili wake ulikutwa kwenye kibanda alichokuwa akijihifadhi nyakati za
usiku ukiwa umechomwa moto. Katika uchunguzi mwili huo pia ulibainika
kuwa na jeraha kichwani ambalo linasadikiwa kusababishwa na kitu chenye
ncha kali. Bado uchunguzi wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea

5. Hamad Hussein, (37), mkazi wa Manyoni alifariki dunia baada ya


kushambuliwa na wananchi wanaosadikiwa kujichukulia sheria mikononi
2
kwa kutumia fimbo na mawe kutokana na tuhuma za wizi wa mifugo.
Mtuhumiwa mmoja aitwaye Hussein s/o Mrisho amefikishwa mahakamani
kuhusiana na tukio hilo.

6. Emmanuel Meso, (50), Mkazi wa Kijiji cha Maweni, Tarafa ya Kintinku,


alifariki dunia kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za siri. Mwili
wake uligundulika tarehe 8/11/2019 alifajiri ukiwa umetupwa porini. Katika
uchunguzi wa Polisi imebainika kuwa watu nane wanasadikiwa kuhusika
katika kutenda kosa hilo linalohusishwa na imani za kishirikiana. Aidha
katika tukio hilo yupo Mganga wa Jadi anayesadikiwa kuwatuma
watuhumiwa kuchukua shemu hizo za siri. Watuhumiwa wote
wamekamatwa na upelelezi umekamilika, waliokamatwa ni Abdul
Muhengwa, Henry Madinda, Stephano Ligoha, Juma Kassim, Makayola
Gaudence, Regina d/o Jacob, Wami s/o Ngalya, na Anderson s/o Sabini.

7. Mika Saimon, (38), alifariki dunia kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali
katika sehemu mbalimbali za mwili katika tukio lililotokea tarehe
15/11/2019 saa 10 jioni huko Kitongoji cha Idodoma, Tarafa ya Nkonko,
ambapo marehemu aliuawa na mtoto wake aitwaye Saimon s/o Mika kwa
akishirikiana na mama yake mzazi aitwaye Mea d/o Mwarabu pamoja na
rafiki wa mtoto wake aitwaye Robert Elia ambapo walikuwa wanataka
kurithi shamba la baba yao. Watuhumiwa wote watatu wamekamatwa na
upelelezi wa Polisi umekamilika.

8. Mshoma Ngassa, (30), Mkazi wa Itigi alifariki dunia kwa kupigwa kwa
fimbo kichwani na mume wake aitwaye Mariyambelele Senzo katika tukio
lililotokea tarehe 21/11/2019 saa 2:30 asubuhi huko Majiweni, Kata ya
Mitundu ambapo chanzo cha kifo ni wivu wa kimapenzi ambapo
mtuhumiwa akimtuhumu mke wake kutembea na mwanaume ambaye bado
hajafahamika. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa Polisi
umekamilika.

9. John Logion, (60), Mkazi wa Mitundu alifariki dunia katika tukio lililotokea
tarehe 22/11/2019 saa 11 jioni kwenye shamba la mihogo, lilnalomilikiwa na
Anthony Lipiti huko Itigi. Uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini kuwa
chanzo cha tukio hilo ni wizi ambapo marehemu alikwenda kwenye shamba
la mtuhumiwa kwa nia ya kuiba mihogo na mtuhumiwa kutumia mwanya
huo kumshambulia kwa kumpiga na kitu kizito kichwani. Mara baada ya

3
tukio mtuhumiwa alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea kwa
kushirikiana na Viongozi wa Eeneo husika.

10. Michael Charles, (35), Mkazi wa Mwamagembe alifariki 1/1/2020 wakati


anapatiwa matibabu katika Zahanati ya Mwamagembe, Itigi kutokana na
taarifa za kujeruhiwa na Fatuma d/o Ramadhani tukio lililotokea tarehe
21/12/2019. Katika tukio hilo inasadikiwa kuwa Fatumaa d/o Ramadhani
ambaye ni Mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi marehemu alimpiga kwa
jiwe kichwani na kisha kumvuta sehemu za siri kutokana na ugomvi wa
uchafuzi wa mazingira katika eneo la nyumba wanayoishi. Hata hivyo tukio
la kujeruhiwa halikuripotiwa Polisi hadi muathirika alipofariki. Baada ya
tukio la kujeruhi mtuhumiwa alotoroka juhudi za kumtafuta zinaendelea.

11. Issa Abdallah (2), ambaye alikuwa mlemavu wa miguu alifariki dunia
tarehe 24/1/2020 saa 12 jioni huko katika Kitongoji cha Ibonoa, Kata ya
Sanjaranda – Itigi kutokana na kunyongwa na mama yake mzazi kwa kile
kinachodaiwa kukosa mahitaji kutoka kwa baba wa mtoto aitwaye Abdallah
s/o Muna, (56), Mnyaturu aliyemtelekeza bila matunzo. Mtuhumiwa
amekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika

12. Jumanne Ndelemo, (22), alifariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye
ncha kali na kaka yake wake aitwaye Hamisi s/o Ndelemo, kutokana na
kumfumania akiwa na mke wake. Tukio lilitokea tarehe 5/2/2020 saa 3:30
usiku huko katika Kijiji cha Makasuku, huko Sasajila na mtuhumiwa
amwekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.

13. Heri Mamba alifariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki yenye namba
za usasjili MC 273 CDK aina ya FEKON. Kutokana na uchunguzi wa awali
wa Polisi imebainika kuwa marehemu alikuwa amelewa huku akikatiza
barabarani bila kuchukua tahadhari. Mtuhumiwa Ombeni s/o Chanzi,
Mgogo, (35), mkazi wa Chinyika amekasmatwa na amekiri kutenda kosa
hilo na si kuchinjwa kama ilivyodaiwa kwenye malalamiko.

14. Alex Jonas, (40), dereva bodaboda, aligundulika kufariki dunia tarehe
26/2/2020 saa 1 asubuhi na Uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini
chanzo cha kifo cha marehemu pamoja na wahusika wa tukio hilo.

Katika Taarifa ni za upotoshaji zenye lengo la kuleta taharuki kwa Jamii pamoja
na kuwachonganisha Wananchi na Jeshi lao la Oilisi.

4
Mwisho Kamishna Sabas amesema kuwa hakuna Mwanasiasa au mtu yoyote
atakaetumia Jeshi la Polisi kama kimvuli cha kujipatia umarufu, huku
akiwaonya anasiasa wanaojifanya kuwa ni wasemaji wa Jeshi la Polisi
amewaonya na kusema kuwa jeshi halitamvumilia mtu au kiongozi yoyote
atakaeichafua serikali kwa namna moja au nyingine.

You might also like