You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA KAMPUNI YA MADINI YA


TWIGA

Dodoma: Tarehe 22 Machi, 2020: Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.


Philip Isdor Mpango (Mb), amewateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Bodi ya Wakurugenzi
ya Kampuni ya Madini ya Twiga (Twiga Minerals Corporation Limited).

Wajumbe walioteuliwa ni

1. Bw. Casmir Sumba Kyuki


2. Bw. Michael Jonathan Kambi

Uteuzi wa wajumbe hao watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka
mitatu, unafuatia makubaliano mapya ya namna ya kuendesha Kampuni hiyo
kwa ubia, yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold, na kutiwa
saini tarehe 24 Januari, 2020, Jijini Dar Es Salaam.

Kampuni ya Madini ya Twiga inasimamia migodi mitatu ya Buzwagi, North


Mara na Bulyanhulu ambapo Barrick Gold inamiliki asilimia 84 ya hisa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki hisa asilimia 16.

Uteuzi wa wajumbe hao unaanza leo tarehe 22 Machi 2020

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

You might also like