You are on page 1of 3

Nafasi ya sekta binafsi katika uchumi

Miongoni mwa sababu zinazochangia nchi nyingi zinanzoendelea (Developing countries)


kuwa nyuma ya zile zilizoendelea (Developed countries) katika shughuli za uzalishaji ambazo
ndizo chachu ya maendeleo ni kutokana na kutokufanya vyema kwa sekta binafsi. Ni dhahiri
kwamba nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea hutofautiana katika uzalishaji, Ufanisi, na
Ubora wa sekta binafsi.
Sekta binafsi ni sehemu ya uchumi wa taifa ambayo haimilikiwi na serikali, shughuli zote za
uzalishaji katika sekta hii zinafanywa na makampuni, wafanyabiashara au mashirika binafsi
ambayo kwa kiasi kikubwa hulenga katika kukuza na kuboresha masilahi yao (faida) pamoja
na yale ya washirika wao (stakeholders) sana kuliko masilahi ya wateja (wananchi), ingawa
kumridhisha mteja (customer satisfaction) kwa kutoa huduma au bidhaa yenye ubora hubaki
kuwa jambo la msingi na linalopewa kipaombele katika kuamua maendeleo, ukuaji na uwepo
wa makampuni, mashirika na biashara za watu binafsi.
Nchi zenye mfumo wa ubepari (capitalism) ambazo zinaamini katika soko huria (Free market)
pamoja na zile zinazotumia mchanganyiko wa mifumo ya ubepari pamoja na ujamaa
(socialisim), zinahamasisha sana uwepo wa sekta binafsi kwa kutunga sera ambazo zinalenga
katika kuongeza mchango chanya na mkubwa katika uchumi wa taifa husika hasa katika
masuala ya ajira (employment rate), kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja (per capita
income) na vilevile katika kuchajiza uboreshwaji wa miundombinu.
Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazoendelea, licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye
utajiri mkubwa wa rasilimali duniani kwa kubarikiwa na wingi wa madini yenye thamani
mengineyo yakiwa hayapatikani sehemu nyengine yoyote zaidi ya Tanzania (Tanzanite),
Ardhi lenye rutuba (Arable land) inayoruhusu kilimo cha mazao tofauti ya biashara na nafaka,
kuwa na vivutio vya utalii kama mlima kilimanjaro ambao ndio mlima mrefu zaidi barani
Afrika na wapili duniani pamoja na kuwa na mbuga kubwa (Serengeti, na Ngorongoro) zenye
wanyama kama Simba, Tembo, Chui, Vifaru, na Twiga (big five wild animals) ; kuwa
pembezoni mwa bahari ya hindi ambayo ni tunu muhimu inayoweza kuchochea shughuli za
uvuvi, utalii pamoja na usafiri wa majini (maritime transportation), lakini pia kupitia tunu hii
Tanzania imekuwa lango (Gate way) la nchi zisizo na bahari (Landlocked countries) kama
Uganda, Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
(DRC) ambazo zinatumia bandari ya Dar es salaam katika biashara zao na mataifa mengine
(importation and exportation), lakini bado nchi hii yenye utajiri wa kila aina, ni miongoni
mwa nchi masikini duniani kwa kuwa na matatizo ya Ajira, changamoto ya Elimu ambayo
haizalishi wahitimu wajuzi, wavumbuzi, na wenye kukidhi vidego na mahitaji ya soko la
ajira (labor – market), changamoto ya huduma za afya, maisha duni (low living standard),
changamoto ya miundombinu hasa ya usafiri, afya, maji, elimu na nishati (inadquate
infrastructures), na maeneo mengine, kwa kiasi kikubwa ikichangiwa na kutokufanya vizuri
kwa sekta binafsi.
Kama ilivyo kwa serikali zote dunia kuweka mipango na sera mbalimbali za kimaendeleo
zikihimiza sana uwepo wa sekta binafsi yakiushindani itakayokuwa sehemu ya uchumi wa
nchi husika kwa kuchangia ukuaji wa pato la taifa, kwa kutoa ajira za kutosha, kuongeza
kipato cha mwananchi mmoja mmoja hasa wa hali ya chini itakayo saidia kupunguza hali
ngumu ya maisha kwa wananchi wa hali zote, kuisaaidia nchi kushiriki kikamilifu katika
biashara ya kimataifa kwa kuhakikisha uzalishaji wa bidhaa na huduma zenye ubora na za
kiushindani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia inafanya jitahada katika
maeneo mbalimbali hasa ya sera na miundombino itakayohakikisha ufanisi wa sekta binafsi,
swali la kujiuliza ni kwanini Tanzania bado ni miongoni mwa nchi masikini duniani licha ya
kuwa na kila sababu ya kutokuwa katika kundi hilo maana ina tunu ya kila aina zinaweza
kuizesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kufikia hadhi ya uchumi wa kati wa
kiwango cha juu (Upper- middle income economy) au kama ule wa nchi zilizoendelea
kiuchumi kama Afrika ya Kusini na mataifa mengine ya ulaya ? yapi ya msingi (prerequisites)
yatakayoiwezesha Tanzania kuwa na aina hii ya sekta binfsi iliyokuwa fanisi itakayo chochea
kikamilifu maendeleo ya kiuchumi, itakayoyafanya maeneno mengine ambayo ni nyeti kuwa
ya kiushindani kwa kuhakikisha uzalishaji na utoaji wa bidhaa na huduma zenye ubora
zitakazo kidhi mahitaji ya ndani na nje ya Tanzania ?
Ufanisi wa Sekta binafsi ambayo inajumuisha uwekezaji wa ndani na wa nje (Domestic and
Foreign Direct Investment), pamoja na sekta ambazo si rasmi (Informal sector) kama
wamachinga na Mama ntilie, unategemea sana maamuzi ya kisiasa (Political Decisions)
ambayo kwa kiasi kikubwa ndio huamua maendeleo, ufanisi na ukuaji wa maeneo mengine
yote ya nchi yaani maendeleo ya nyanja za kiuchumi, tamaduni pamoja na jamii. Sera,
mikakati na Dira bila kusahau utekelezaji (Implementations) wa mipango yote ya serikali ndio
huakisi ukuaji na maendeleo ya nchi, hivyo basi nchi pamoja na kutunukiwa na kila aina ya
rasilimali zilizopo juu na chini ya Ardhi, lakini bila ya kuwa na Uongozi bora (Good
governance) ambao ndio unajukumu la kuweka mipango pamoja na sera za kimaendeleo
zitakazo hamasisha na kuvutia uwekezaji wa nje na ndani, bado nchi hiyo itaendeleo kuwa
masikini miaka nenda rudi.
Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inakila sababu ya kuchukua hatua za
makusudi za kuitambua na kuutambua mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi wa
nchi. Kuutambua mchango wa sekta binafsi kwa maana ya kuweka sera na mipango
madhubuti ya kimkakati itakayochochea ustawi na ufanisi wa sekta binafi yote kwa ujumla
wake yaani kwa kuvutia uwekezaji wa ndani kwa kuweka mazingira rafiki ya kibiashara
ambayo yanaanzia kwenye usajili wa makampuni na mashirika binafsi lakini pia kwa
kuwawezesha wawekezaji wa ndani kwa kuwapa mitaji na mikopo isiyo au yenye masharti
nafuu, lakini pia kuwawekea mazingira mazuri ya masoko ya huduma na bidhaa. Lakini pia
sera na mipango ya serikali ielekezwe hasa katika kushawishi na kuvutia uwekezaji wa nje
(Foreign Direct Investment), kwenye hili serikali inahitaji mikakati na sera za mda mrefu
(structural reforms) amabyo itahakikisha na kuvutia uwekezaji wenye tija kwenye kila eneo
muhimu litakaloleta athari (significant impact) kwenye maendeleo na ukuaji wa uchumi wa
nchi. Maeneo kama ya taasisi za kifedha (financial institutions), Elimu, utalii, madini, kilimo,
nishati, pamoja na sekta ya usafirishaji ambayo ina maeneo mengi na nyeti amabyo yanahitaji
uwekezaji mkubwa sana, kwasababu kutokana na jeografia ya Tanzania, Bandari ya Dar es
salaam inahudumia nchi jirani zaidi ya sita (Uganda, Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi
pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC)), kama kukiwa na uwekezaji wenye tija
katika eneo hili la bandari, pamoja na maeneo mengine ambayo pia ni muhimu na nyeti ,
itaiwezesha Tanzania ndani ya miaka ijayo kuwa miongoni mwa nchi zenye nguvu sana
kiuchumi.
Kwa kuhitimisha, Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya mageuzi ya kiuchumi hasa ya
viwanda kama iliyo katika Dira yake ya maendeleo ya mwaka 2025, kwa kuipa nafasi na
kuiwekea mazingiza mazuri (Economic conducive environment) sekta binafsi kuwekeza
katika maeneo mbalimabli kama kilimo, utalii, Elimu, Afya, Tasisi za Fedha, na
miundombinu ya usafirishaji (ujenzi na upanuzi wa bandari za kiushindani) ambayo
itachochea ukuaji wa uchumi utakao tatua tatizo sugu la Ajira pamoja na kuakisi upatikanaji
wa bidhaa na huduma za maji, afya, Elimu, usafiri na nishati, zenye ubora zitakazo kidhi
mahitaji ya ndani pamoja na kushiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa (International
trade).

You might also like