You are on page 1of 26

OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA, S. L.

P 128 SUMBAWANGA

2012

Sumbawanga Ngara
Eng. Stella Martin Manyanya Mb Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Weka Manispaa yetu kuwa safi na Inayovutia ili kila mtu aseme Kwetu ni Sumbawanga

UDHIBITI WA MAZINGIRA

SUMBAWANGA NGARA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA S. L. P 128, RUKWA. APRILI, 2012

UTANGULIZI
Page 2 of 26

Mgaagaa na upwa hali wali mkavu, Mcheza kwao hutuzwa na Mwenye macho haambiwi tazama. Hii ni misemo au methali za wahenga wetu ambazo maana zake hazibadiliki kizazi hadi kizazi. Hivyo, methali hizi zimekuwa kama mafuta yaliyoamsha ari ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuandika kitabu hiki kinachochochea nafasi ya wananchi katika kujiletea maendeleo. Mara nyingi tumejielekeza kusema kuwa tumeshindwa kufanikiwa katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii yetu kwa visingizio mbalimbali. Hayo yanajitokeza zaidi hasa katika siasa za sasa chini ya vyama vingi ambapo malalamiko yamekuwa makubwa kuliko kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu huku hali ya kujitoa katika kuchangia shughuli za maendeleo imeshuka. Mara nyingi majibu ya wananchi na vyombo vyote vya dola katika mapungufu ya kutekeleza majukumu na wajibu wao imekuwa ni kwa ajili ya ukosefu wa fedha, na Serikali imekuwa ndiyo ikitupiwa lawama zaidi kuwa haiwajibiki kwa wananchi, haikusanyi kodi kutoka kwa wafanyabiashara, haina mipango mizuri ya uhifadhi wa mazingira na kila linalowezekana kusemwa ili mradi tu mtu akipata nafasi atasema. Aghalabu si rahisi kusikia taasisi mbalimbali zikiwemo za kibunge kujadili misingi ya matatizo ya wananchi bila kuitupia lawama Serikali, Serikali hii haijali watu, watu wana umaskini wa kutupwa lakini Serikali haijali, watoto wameshindwa kwenda shule kwa sababu ya Serikali, watu wakiona taka ziko barabarani sababu ni Serikali na kadhalika. Katika taarifa ya mwaka 2012 African Peer Review Mechanism (APRM) yaani Mkataba ambao umekubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kama mchakato wa kujifanyia tathmini inaeleza kuwa Watanzania wengi wanaamini kuwa Serikali ndiyo inastahili kufanya kila kitu kwa ajili yao. Kama ndivyo basi hilo ni tatizo kubwa. Baba wa Taifa Hayati Mwalimu alisisitiza juu ya umuhimu wa watu wote kufanya kazi kwa kusema kwamba, Ni lazima kila
Page 3 of 26

mtu atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Kwa hiyo suala la watu kuacha kufanya kazi na kutowajibika kwao wenyewe na familia zao ni kosa kubwa. Kwa mujibu wa katiba Sehemu ya pili Ibara ya 8(a) (d). Ni kweli kuwa pesa zina nafasi kubwa katika kurekebisha tatizo, lakini pesa peke yake si jibu la matatizo yote. Wananchi wakijituma wanaweza kutatua sehemu kubwa sana ya matatizo yao. Lakini pia ili kuona kuwa jitihada za wananchi pamoja na Serikali yao zinajulikana na zinaweza kupimika, ni muhimu sana mipango na mikakati mbalimbali kutengenezewa miongozo itakayofuatwa na kuweka kumbukumbu kimaandishi. Miongozo hiyo pia itasaidia katika kupima matokeo ya jitihada zilizochukuliwana kuthaminishwa. Tumeona mara nyingi katika maeneo ambayo wananchi wamejitolea, mchanganuo wa jasho lao haujitokezi moja kwa moja katika taarifa za kibajeti, na pengine hiyo inaweza kuwa sababu mojawapo ya kuwakatisha tamaa kwani michango yao haitoi maelezo ya kina na wakati mwingine haitolewi kimahesabu zaidi ya kusema, pamoja na michango ya wananchi. Kitabu hiki kinaelezea Mpango wa Kwanza unaohusu Uboreshaji wa Mazingira wa Manispaa ya Sumbawanga yaani Sumbawanga Ngara. Mpango huu ni mpango chochezi kwa maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Mafanikio ya mpango huu yataweza kuleta ari na kuigwa kwa Mkoa wote wa Rukwa.

Chimbuko Mpango huu wa Sumbawanga Ngara ulianzishwa mnamo tarehe 12 Januari 2012, chini ya uasisi wa Mkuu wa Mkoa Mhandisi Stella Martin Manyanya (MB) ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mpango huu ulizinduliwa tarehe 24 Februari na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa kuweka jiwe la msingi kwenye mnara wa Sumbawanga Ngara ambao umepewa heshima kwa akina mama, kama ishara ya utamaduni wao - ngoma ya Kingwengwe, ambayo huchezwa
Page 4 of 26

hasa na wanawake, ikizingatiwa kuwa mdau mkuu wa usafi kihistoria ni mama. Lengo la mpango huu ni kuhakikisha kuwa Manispaa ya Sumbawanga inakuwa kinara katika udhibiti wa mazingira Tanzania, hususani ndani ya manispaa hiyo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mafanikio ya kazi hii ni heshima kubwa kwa wananchi wote wa Manispaa ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla hasa kwa wale wa kipato cha chini ambao juhudi zao za hali na mali ndizo nguzo kuu ya ushindi kwani msafishaji ndiye msafi. Kupitia kitabu hiki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa imeandaa maelezo ya kina ya mpango huu wa Sumbawanga Ngara ambayo yatatumika kama mwongozo ama kioo cha tulikotoka, tulipo na tunakokwenda. Kutokana na mwongozo huu itakuwa rahisi kwa Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri zote za mkoa wa Rukwa pamoja na miji mingine ambayo bado haijafanikiwa katika udhibiti wa mazingira zikiwemo taka ngumu na miminika kuweza kujifunza na kuiga kutokana na matokeo yatakayopatikana kupitia mpango huu. Kwa kuwa sisi sote wananchi tuna kiu ya maendeleo ya kweli na mafanikio ya mpango huu kwa Mkoa wetu wa Rukwa hakika: Tumedhamiria, Tunaweza na Tutashinda!

Eng. Stella Martin Manyanya (MB) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Page 5 of 26

MPANGO WETU:

SUMBAWANGA NGARA

KAULIMBIU YETU: Weka Manispaa yetu kuwa safi na inayovutia ili kila mtu aseme kwetu ni Sumbawanga MKAKATI WETU: Uwajibikaji wa pamoja kwa ajili ya mazingira yetu. Tuwe nyumbani, tuwe kazini, hospitali, kwenye nyumba, kwenye maeneo ya umma hata kwenye michezo na popote pale ambapo tupo, usafi ni kipaumbele chetu. Tuifanye Sumbawanga ingare kuliko ilivyowahi kungara tangu kuwepo kwake. Kila mtu anaweza akatimiza wajibu wake kwa kuweka mji wake pamoja na maeneo yake yanayomzunguka na pia ahakikishe maeneo ya wazi ni safi. Saidia Manispaa ya Sumbawanga, Makao Makuu ya Mkoa wetu yawe safi kulingana na hadhi yake. Saidia Manispaa hii iwe safi ili iwe mfano kwa wilaya nyingine za mkoa wa Rukwa, Tanzania kwa ujumla na popote Duniani. Sumbawanga Ngara itafanikiwa endapo tutakuwa tumefanikiwa kudhibiti taka ngumu na miminika, kusafisha maeneo yote yanayotuzunguka ikiwemo kufyeka, kulima, kupanda miti na maua, kutengeneza mapambo
Page 6 of 26

ya mji pamoja na kuheshimu sheria za mipango miji na nyinginezo zinazohusiana.

TAKA NI NINI: Taka ni kitu chochote kinachoweza kuleta chukizo kwa wanaokiona kutokana na kutokuwa na mvuto au hali isiyo ya kawaida, kilichokaa pasipo mpangilio au kilichopo mahali pasipostahili, kinachotoa harufu mbaya, kinachotia kinyaa na mazingira yote yasiyokubalika.

MADHARA YA TAKA: Taka zina madhara mengi, zifuatazoni baadhi tu;


1.

Taka zinahatarisha afya, usalama na ustawi wa jamii. Taka inawanya watu au jamii ionekane kuwa sio wastaarabu au hawana uwezo, na zinashusha hadhi Taka zinaonyesha kuwa watu wake hawatii sheria za nchi yao na Manispaa yao. Taka zinafanya mji ushuke thamani yake na hadhi yake na hivyo kushusha hata bei ya bidhaa na kukosesha soko. Taka zinafukuza wageni.
Page 7 of 26

2.

3.

4.

5.

6.

Taka zinagombanisha familia na zinaweza kusababisha kukimbiwa na mpenzi wako au marafiki.

7. Taka zinakosesha amani, utulivu na utaratibu wa mtu au kitu.

FAIDA YA TAKA: Pamoja na madhara hayo kwa upande mwingine taka zina faida kwa kuwa kila siku miji inazalisha taka, na hivyo kutoa ajira ya kusafisha taka. Hivyo basi ni muhimu watu binafsi au vikundi vya watu kushirikiana na Manispaa yao kuhakikisha kuwa kila eneo linakuwa safi. Katika mpango huu wa Sumbawanga Ngara inategemewa kuzalisha jumla ya ajira zisizopungua elfu mbili (2000) kutokana na shughuli za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Mfano wa shughuli hizo ni pamoja na kusafisha mifereji, kufyeka, kuokota taka, kupakia kwenye magari ya taka, kuendesha magari ya taka, kusimamia shughuli za taka, kuuza taka rejea, kuchakata taka rejea, kutengeneza mboji, kutengeneza mapambo, kuanda miti, kuboresha barabara, kutengeneza matifali, kusukuma mikokoteni, kutengeneza vinyago, kupaka rangi, kuhamasisha na kutoa elimu, machapisho, kujenga mabango na kuandaa matangazo, kuuza vifaa mbalimbali kama matoroli, uma, majembe, mapanga, mifagio, uandishi wa habari za taka, kuanzishwa kwa vikundi vya ujasiriamali wa taka, upandaji wa miti na bustani na kadhalika.

MALENGO YA MILENIA 1. Kumaliza Umaskini na Njaa


2. 3.

Elimu kwa Wote Usawa wa Kijinsia

4. Afya ya Mtoto
Page 8 of 26

5. Afya ya Uzazi 6. Kupambana na Ukimwi 7. Mazingira Endelevu


8.

Mahusiano ya Kimataifa

Wajibu wetu hapa ni kujihusisha na kifungu cha saba kinachotutaka kuwa na mipango mahususi itakayofanya mazingira yetu kuwa endelevu. Katika kutilia mkazo inasisitizwa na Umoja wa Mataifa kuwa Usafi kwa wote kufikia 2015. Kampeni nyingi zimetangazwa mpaka siku za vyoo, lakini hadi leo bado kuna watu hawaheshimimu matumizi ya vyoo na maji salama.

Dira ya Taifa ya Tanzania 2025 Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 inatarajia kuona kuwa ifikapo mwaka 2025, endapo Wananchi wake watakuwa wamewezeshwa na kujengewa mazingira mazuri ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali walizonazo ikiwemo watu, ardhi, maji, madini, misitu na hali ya hewa na bila vitu hivyo kuharibiwa basi; a) Itakuwa na watu wa kiwango cha hali ya juu b) Amani, Utulivu na Umoja, c) Utawala Bora, d) Watu walioesoma na jamii iliyoelimika
e)

Uchumi wa kiushindani imara kwa faida ya wote.

Kwa hali hiyo ni muhimu kwa wadau wote wa kila eneo kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa. Kimsingi ustawi wowote ili kuwa endelevu lazima uzingatie wananchi wenyewe. Sera ya Mazingira

Page 9 of 26

Kwa kuzingatia umuhimu wa mazingira katika maisha ya Binadamu, kwani ndiyo hutoa hifadhi ya viumbe vyote vyenye uhai, na ndio msingi wa rasilimali ya kuwezesha kuondoa unyonge wa maskini na kuongeza uwezo wa watu wa kipato cha Watanzania, hivyo jukumu kuu la wadau wote ni kulinda Mazingira yetu kwa nguvu zote. Serikali ya Tanzania inatambua hatari hiyo ya kupoteza rasilimali hiyo na ndiyo maana ikatunga Sera ya Taifa ya Mazingira ya 1997 ikiwa na madhumuni yafuatayo;
1.

Kuhakikisha udumishaji, usalama na matumizi sawa ya rsilimali kwa mahitaji ya msingi ya sasa na vizazi vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya na usalama

2. Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea na hewa ambayo ndiyo husaidia uhai wetu.
3.

Kuhifadhi na kuendeleza urithi wetu na ule unaotegemewa na binadamu ikiwa ni pamoja na maisha ya viumbe wa aina ya viumbe wa aina mbalimbali na pekee nchini Tanzania.

4. Kurekebisha hali na maeneo yaliyoharibiwa pamoja na makazi ya watu mijini na vijijini ili watanzania wote waweze kuishi katika hali ya usalama, kiafya, kuzalisha bidhaa pamoja na kuishi katika mazingira mazuri na yenye kuvutia. 5. Kungamua na kufahamu mahusiano kati ya mazingira na maendeleo na kuhimiza ushirikiano wa mtu binafsi na jamii katika kuhifadhi mazingira.
6.

Kuendeleza kimataifa kuhusu ajenda ya Mazingira na kupanua ushiriki na mchango wetu kwa pande zote zinazohusika, ikiwa zinahusu nchi jirani na mashirika na mipango ya ulimwengu pamoja na utekelezaji wa mikataba.

Page 10 of 26

Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya 2003 (Small and Medium Entreprises (SMEs) Development Policy 2003) Sera hii inalenga kuwajengea mazingira mazuri na kufanya shughuli zao na kukua wajasiriamali wadogo na wa kati. Kwa kutambua shughuli hizo za kiuchumi zinaambatana na mambo mtambuka, Sera inasisitiza katika kuhakikisha kuwa pamoja na suala la jinsia na Ukimwi, suala la mazingira pia linapewa kipaumbele. Sera pia inasisitiza kutenga maeneo maalum ya kufanyia biashara na uendelezaji wa viwanda vya kati. Sera hii pia inasisisitiza juu ya umuhimu wa ubunifu katika kutengeneza shughuli za kujipatia kipato halali. Huduma ya taka ngumu katika Manispaa ya Sumbawanga kwa muda mrefu imekuwa ikitolewa na Manispaa yenyewe. Huduma hiyo imekuwa hasa ikizingatia kuondoa marundo ya taka ambayo yanazagaa ovyo, kupelekwa kwenye vizimba na hatimaye kupelekwa Dampo. Pamoja na msisitizo mkubwa katika ngazi ya taifa juu ya utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu, jukumu hilo kwa kiwango kikubwa bado lilizoeleka kuwa kama ni la Manispaa au Halmashauri kama majukumu ya Serikali. Elimu mbalimbali kupitia makongamano, vipeperushi na matangazo zimekuwa zikitolewa. Lakini hali ya kukubalika juu ya utekelezaji wake umekuwa ni mdogo sana. Tatizo kubwa zaidi imekuwa hasa pale Manispaa au halmashauri zinapohitajika kugharimia huduma yote ya taka, yaani taka za majumbani (takangumu na miminika) pamoja na za viwandani ikiwemo maeneo yote ya taasisi za umma na binafsi. Jambo jingine linalojidhihirisha ni juu ya vipaumbele vya bajeti, mara nyingi pamoja na watu wengi kuonekana kuchukizwa na
Page 11 of 26

utupaji holela wa taka pamoja na uchafuzi wa maeneo ikiwemo makazi kwa ujumla, suala la udhibiti wa taka limekuwa halipangiwi bajeti ya kutosha. Hii ni kwa upande wa Serikali na hata watu binafsi. Aghalabu ni mara chache kabisa au pengine hamna kukuta wadau wakiwa kwenye kikao cha mipango kutoa kipaumbele cha udhibiti wa taka. Manispaa imejikuta ikitoa huduma hafifu sana kutokana na kuwa na bajeti finyu katika eneo hilo sambamba na mzigo wote wa kudhibiti taka kuachiwa yenyewe. Kwa muda mrefu mifereji imekuwa haizibuliwi, barabara hazifyekwi ipasavyo, wadau kutiririsha maji hovyo na kuacha makazi yao katika hali isiyoridhisha, Biashara kufanyika katika mazingira machafu na holela, na kwa ujumla wake kuwa na mji hatarishi, usiopendeza na uliozubaa. Matokeo yake kumekuwa na athari za kiuchumi kama vile magonjwa ya milipuko ya hapa na pale na hivyo kuongeza gharama za matibabu, kuwa na nguvu kazi isiyo na tija, mji usiovutia kwa wananchi wenyewe na wafanyabiashara ikiwemo wawekezaji na watalii. Hali kadhalika imechangia kuwa na mzunguko mdogo wa pesa, kupungua kwa ajira ya moja kwa moja kutokana na shughuli za taka pamoja na zilezisizo za moja kwa moja kupitia faida zinazopatikana kutokana na mafanikio ya kazi za taka. Katika mashindano mbalimbali ya Manispaa, miji, Halmashauri, Sumbawanga imejikuta ikibwagwa kiusafi hata na miji midogo kama vile Mji wa Mpanda ambao sasa ni Makao Makuu ya Mkoa wa Katavi wakati mkoa wa Rukwa haujagawanywa. Mara nyingi ushindi wa Manispaa safi umekuwa ukichukuliwa na Moshi pamoja na Manispaa nyingine nje ya Rukwa. Baada ya kutafakari na kujifunza juu ya tatizo la taka katika Manispaa ya Sumbawanga, wadau wote kwa pamoja chini ya uasisi wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Eng. Stella Martin Manyanya Mb. wamedhamiria kuona kuwa Sumbawanga inangara kuliko ilivyowahi kungara na kuwa Manispaa safi, salama na
Page 12 of 26

inayovutia kuliko yote Tanzania kiasi cha kila mtu kujivunia na kuita Sumbawanga ni kwao. WADAU WA TAKA Ili mpango huu wa Sumbawanga Ngara kuwa endelevu, ni lazima ushirikishe jamii ya watu wote waishio Sumbawanga pamoja na taasisi zake za kiserikali na binafsi kama ifuatavyo. Pia ni muhimu Suala la Sumbawanga Ngara lifahamike kwa wadau wengine wote wa maendeleo waishio Mkoani Rukwa na nje ya mkoa. Kwa kushirikisha makundi ya wadau wote, umiliki wa mradi huu utakuwa ni wa wote kuanzia chini (grassroot), ngazi ya uwezeshaji hadi Serikali yaani Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Wananchi Hawa ni wananchi wa kawaida ambao pia ni wazalishaji wa taka za majumbani (domestic waste). Lakini pia wananchi ni nguvukazi katika kuondoa taka katika maeneo yao yanayowazunguka. Wananchi ndio wanufaika wakuu na wa moja kwa moja au kupitia fursa zinazoambatana na ajira za taka kama vile Usafishaji, taka rejea, mbolea na mboji, pamoja na kuchangia huduma ya taka. Wananchi hao wanaweza kuwa ni mtu mmoja mmoja au vikundi vya kijamii, wanawake, wanaume, vijana, wazee, walemavu na kadhalika. Serikali Kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na sera nzuri pamoja na sharia zinazosaidia kudhibiti taka. Kwa sasa Baadhi ya wadau wakuu katika eneo hili ni Wizara ya Tamisemi, Mazingira, Afya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga. Wajibu wao ni pamoja na kuboresha miundombinu ya taka pamoja na vitendea kazi kama magari, vizimba sehemu ya kutupa taka n.k.
Page 13 of 26

Wafanyakazi Wajiriwa wa Serikali pamoja na mashirika ya umma, Taasisi binafsi ambao watakuwa na wajibu wakuhakikisha kuwa familia zao zinatekeleza juu ya udhibiti wa taka, wakiwa kazini wana simamia ipasavyo kuhakikisha kuwa maeneo yao ya kazi yanakuwa safi. Kwa watumishi waajiriwa wa Manispaa wao ni wadau wakuu katika kuchangia taarifa za kitaalam pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria zinazohusiana na taka. Wafanyabiashara Kuhakikisha maeneo yao ya kazi na safi, Kuuza vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, chepe, koleo, buti, visibao na kuhakikisha kuwa shughuli zao zinafanyika katika maeneo yanayostahili na yaliyoelekezwa na Manispaa. Watu wa kujitolea Hawa ni watu waliohamasika na kuona kuwa mji wao unakuwa safi salama na mzuri. Wanaweza kuwa ni watu binafsi kama vile wakuu wa shule, madaktari, viongozi wa dini kama vile Askofu, Shehe, mapadre, wachungaji na wengineo kutoka katika jamii zetu ambao watajihusisha kufanya usafi wa moja kwa moja au kutoa hamasa ikiwa ni pamoja na michango ya kifedha. Vikundi na vilabu vya vijana vya Mazingira Hivi vitajihusisha kupitia maeneo wanayokaa au vilabu vyao vya shule katika kuhamasisha pamoja na kutekeleza moja kwa moja. NGOs, CBOs, Vyama vya Kujitolea, na Jumuia za kijamii Hizi ni asasi za kijamii na zisizo za kiserikali zinazoweza kuhusisha makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wanawake, wajasiriamali, wajane, wastaafu na kadhalika. Makampuni Binafsi Makampuni yatanufaika kutokana na kupata kazi za ukarabati wa miundombinu kama barabara pamoja na mifereji, kuwa
Page 14 of 26

wateja wa taka rejea kama vile vyupa vya plastiki, mipira, vyuma chakavu, karatasi, mapambo, kupata machine za taka rejea (waste recycling machines) na taka hai zinazoozeshwa na magari ya taka. Pia kuingia katika ushirika wa usafishaji pamoja na Serikali. Makampuni binafsi pia yanao uwezo wa kufadhili miradi midogo ya watu binafsi na vikundi vya wajasiriamali wa taka, na wapandaji wa miti, watengenezaji wa sanamu za mapambo. Makampuni haya yataweza kufaidika kutokana na kujulikana kwao kupitia matangazo ya midomo ya watu kwa kuwasifu baada ya kuona matokeo na hivyo kuwa marafiki wa bidhaa zao. Kutumia fursa ya kuboresha mwanga wa mitaa wanaweza kufunga mabango yao katika taa za barabarani ambazo watakuwa wamedhamini. Kwa ujumla wake makampuni yataweza kunufaika na ukuaji wa soko lao kutokana na kufahamika kwa wateja wengi zaidi, kwani watachukuliwa kama marafiki katika kuondoa kero zao. Marafiki wa Maendeleo Hao ni taasisi pamoja na Mashirika ya Kimataifa ambao kwa namna moja au nyingine wameguswa na mpango huu wa Sumbawanga Ngara. Hawa wanaweza kusaidia katika kutafuta vifaa vya kazi kama magari, Kuchangia fedha zitakazowezesha kurekebisha na kuboresha miundombinu ya taka kama vile mifereji, barabara za mji, maeneo ya soko, kutengeneza vipeperushi na vijitabu, kuchangia vifaa moja kwa moja kama matoroli, ufundi, kutafuta wafadhili na kadhalika. UCHAMBUZI WA TATIZO MKUKUTA Kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa ikitekeleza Mpango wa kupunguza Umaskini na Kukuza Uchumi (MKUKUTA) ambao juhudi mbalimbali zimetumika katika kutoa elimu pamoja na kuwawezesha wananchi. Katika eneo hili la kuboresha miji, hususani katika eneo la taka ngumu na taka miminika Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kama vile
Page 15 of 26

Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization ILO) imejaribu kutengeneza mikakati mbali mbali ili kuona kuwa miji inakuwa safi. Lakini nguvu kuwa imekuwa ikielekezwa hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.

Sheria za Mazingira na Taka, Sera Sheria ya Uhifadhi wa Mazingira Tanzania ya mwaka 2004 au kama ilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza (The Environmenta Management Act-EMA 2004) Sehemu ya sita (6) ya sheria inaelekeza wajibu wa mtu yeyote aishiye Tanzania kulinda na kuhifadhi Mazingira. Katika tafsiri neno Mazingira linajumuisha mambo yote yenye mahusiano yanayomzunguka Binadamu zikiwamo hewa, ardhi, maji, hali ya hewa, mwanga, harufu, vionjo, vijidudu au vimelea, shughuli za kilimo, ufugaji, mimea, rasilimali za kiutamaduni na masuala yoye yanayohusiana na shughuli za kiuchumi ikiwemo ujenzi. Waraka wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira unao elekeza kutenga siku ya usafi katika kila wiki. Kufuatana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kama vile (This Day of !st March 2010 ilyoandikwa na Simbarashe Msasanuri) na tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa hakujawa na viwango maalu kwa ajili ya usimamizi na upimaji wa shughuli za taka nchini. Tatizo la taka limeonekana kuwa ni suala sugu, na hivyo Serikali kulaumiwa kwa kushindwa kudhibiti suala la taka katika miji mikubwa na midogo. Katika taarifa za mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali za 2010 zinaonyesha kuwa uwezo wa Serikali katika kuondoa taka ngumu katika halmashauri ni chini ya asilimia hamsini 50% ya taka zinazozalishwa.Inakadiriwa kuwa uwezo wa kaya kuzalisha taka ni sawa na kilo 1.8 za taka za Manispaa ya Sumbawanga. Ukuaji wa uzalishaji wa taka za Manispaa ya Sumbawanga umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Na sasa ukuaji wa uzalishaji huo unakadiriwa kuwa ni tani 25,200 kwa mwaka. Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu ambayo
Page 16 of 26

inakadiriwa kuwa ni sawa na asilimia tatu 3% kwa mwaka. Hali hiyo inaonyesha kuwa ongezeko la uzalishaji wa taka litazidi kukua. Katika mkoa wa Rukwa kumekuwa na hatua mbali mbali zinazolenga kukuza uchumi wa watu wake. Hatua hizo zimepata kasi mpya zaidi hasa kutokana na jitihada za Serikali za kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tunduma hadi Sumbawanga, Sumbawanga hadi Matai, na Sumbawanga hadi Mpanda ambayo ni Makao Makuu ya mkoa wa Katavi, Kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwawezesha wananchi katika shughuli za ujasiriamali, kilimo na kadhalika. Aidha kwa malengo ya kiuchumi, kumekuwa na ongezeko la wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, nchi jirani kama Zambia, Malawi, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Burundi, Ruanda Kenya na kadhalika. Lakini pia kumekuwa na ongezeko la wageni kutoka nchi za mbali duniani kama Afika ya kusini, nchi za Mabara ya Ulaya, Asia na Marekani. Kumekuwepo pia na ongezeko la matumizi ya Bidhaa za viwandani ambavyo mara nyingi huhitaji vifungashio maalum na visivyooza kirahisi kama vile plastiki na vyuma. Ufugaji holela katika miji na matumizi ya ardhi yasiyozingatia sheria katika kuendesha shughuli za kiuchumi na kujamii, Kukosa uelewa wa kutosha juu ya suala zima la udhibiti wa Taka na uzuri wa miji kwa ujumla.Wafanya biashara ndogo ndogo (MSMEs) wamekuwa nao wakichangia suala la uchafuzi kutokana na kutozingatia taratibu za usafi, mfano anaweza akauza miwa, ndizi au mahindi wateja wake wakala hapo na maganda yake kutupwa ovyo. Suala la uchomaji ovyo wa taka, utupaji ovyo wa taka za mkononi limechukuliwa kama ni jambo la kawaida. Baadhi ya Wajasiriamali wadogo wadogo kama Mama Lishe, gereji, mafundi seremala, mafundi wa Ushonaji, Saluni, Maduka ya nyama, wenye maduka na shughuli nyingine wamekuwa wakiacha maeneo yanayowazunguka au sehemu wazofanyia kazi kuwa chafu, na wengine wakiamini sehemu hizo zikiwa chafu watachukuliwa kama biashara zao ni hafifu
Page 17 of 26

hivyo hawatalazimika kulipa kodi. Pia wengine wanaamini kuwa watachukuliwa kuwa bidhaa zao ni za kimaskini, hivyo ni kwa ajili ya watu wasio na uwezo kwani watadhani ni za bei nafuu. Kwa upande wa watu wasioheshimu sheria wanaamini kuwa sehemu hizo hawawezi kwenda watu wa kada Fulani, mfano viongozi hivyo kuwa ni sehemu salama kwao. Wakati mwingine watu wamekuwa hawajali hata tu kufyeka maeneo yanayozunguka viwanja na makazi yao. Magofu na majengo yasiyoisha yamekuwa ndio sehemu za kutupa taka na hivyo kuwa mazalio ya wadudu harishi kama vile mbu, nyoka nge na kadhalika. Baadhi ya watoto wamekuwa wakicheza katika maeneo hayo, na kuwa maficho yao ya kufanya vitendo viovu kama vile uvutaji bangi na madawa ya kulevya, hasa kwa watoro wa shule jambo ambalo ni hatari na linarudisha nyuma maendeleo yetu. Maeneo hayo pia huweza kutumika kama maficho ya Majambazi. Baadhi ya watu katika Jamii kutozingatia matumizi ya vyoo bora, Kujisaidia mahali pasipohusika kama vile vichakani, kukojoa pembezoni mwa barabara, kutiririsha maji machafu ovyo na wakati mwingine kuunganisha taka miminika kutoka mifumo ya vyoo vyao katika mifereji ya maji ya mvua, kumwaga maji machafu barabarani au katika maeneo ya wazi, mamlaka za Maji kutorekebisha kwa wakati mifumo ya maji safi na taka hasa mabomba yanapokuwa yamepasuka. Suala la upandaji miti na bustani za maua limechukuliwa kama ni suala la anasa na la hiari, na wakati mwingine kuchukuliwa kuwa ni suala la kiuwezo. Mtu maarufu, au kiongozi mkubwa, Taasisikubwa, pengine Mzungu ndiye anatakiwa kuwa na bustani nzuri ya maua. Kuna tabia ambazo zimekuwa kama ndio utamaduni wa kupenda kukatiza katika maeneo ya bustani bila kujali uharibifu wa maua, miti na mapambo yaliyowekwa. Sumbawanga Ngara ni pamoja na kuzingatia usafi wa mtu binafsi. Unaweza kukuta mtu anafanya biashara yake, nguo zake ni chafu, nywele chafu, vyombo anavyofanyia kazi
Page 18 of 26

vichafu, lakini kwa kweli ukifuatilia sababu za kuwa hivyo pengine ni kwa ajili ya uvivu tu. Gharama kubwa zinazojitokeza katika kuendesha shughuli za taka, uchakavu wa vitendea kazi na jukumu hilo kuachiwa Serikali kwa kiwango kikubwa. Hadi sasa Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga hawachangii moja kwa moja huduma ya taka pamoja na kuweka uzuri wa Manispaa (Solid waste management and Municipal Beautification). Matokeo Hasa katika siku za nyuma hali hiyo ilipelekea kuona taka za aina mbalimbali zikizagaa katika maeneo ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na kata zake hasa katika maeneo ya wazi, barabara, mifereji, kwenye makazi, kuzunguka maeneo ya Taasisi na kadhalika. Lakini pia kuwa na Mji usiopendeza au kuvutia, hasa kwa wageni wanaotoka maeneo mengine, na hivyo kuondoa ari ya kuwekeza katika mkoa wetu. Pamoja na kuwepo kwa sheria ndogo za udhibiti wa taka na uharibifu wa mazingira, kwa kiwango kikubwa sheria hizo zimekuwa hazizingatiwi na wadau. Lakini mbali na uwepo wa sheria hizo, bado hazitoshelezi kwani hazielekezi rasmi namna ya kukusanya, kutenganisha, kuhifadhi, kusafirisha, kuchakata na kutupa hasa kwa upande wa Manispaa, japo pamoja na mapungufu yaliyoainishwa hiyo haitoi unafuu kwa mkazi yoyote katika manispaa ya Sumbawanga kutokutekeleza matakwa ya sheria ndogo hizi.

Njia na mikakati ya kurekebisha hali 1. Mpango wa Sumbawanga Ngara kuwa ni kipaumbele cha mkoa na kuzungumzwa katika mikutano yake na vikao vyake. 2. Kuendelea kupata ushauri kutoka kwa wadau wa Mpango huu juu ya namna bora ya kushughulikia masuala yanayohusiana.
Page 19 of 26

3.

Kuhamasisha kwa kutoa elimu ili kukuza uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na mji unaovutia na udhibiti wa taka. Elimu hiyo itatolewa kwa njia ya vipaza sauti, redioni, kanisani, misikitini na kadhalika. Kushirikisha wadau mbalimbali na kuwa na kongano la usafi (Cluster initiatives) katika kuhifadhi mazingira kwa ujumla hususani kutoa fursa kwa vikundi kwa mfano, vikundi vya wanawake, vijana kutegemeana na majukumu yao, Makampuni na Taasisi za Umma na makundi ya kujitolea katika kusafisha na kuchangia. Serikali Kupitia Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa kuhakikisha kuwa miongozo ya mara kwa mara, ufuatiliaji na usimamizi wa taka na usafi wa Mji kwa ujumla unakuwa endelevu. Kuifanya siku ya jumamosi ya kila wiki kuwa ni siku ya usafi, kwahiyo wadau wote watatakiwa kushiriki katika zoezi hilo hususani katika maeneo yao wanayoishi. Pia Kila Ofisi na Taasis Kutenga saa moja katika katika wiki kwa ajili ya usafi wa maeneo yao ya ofisi. Kushindanisha mitaa ya Manispaa, Taasisi za Umma, Ofisi za Serikali, Jumuia za kidini na watu binafsi kiusafi ili kuwahamasisha wanajamii kushiriki kikamilifu katika kuweka mji wao safi na kuwavutia wengine kuishi katika Mkoa wa Rukwa.

4.

5.

6.

7.

8. Kupitia wanafunzi kuhamasisha juu ya Usafi, Upandaji miti na Bustani. 9. Kuhamasisha vikundi mbalimbali katika kubuni mikakati ya usafi.
10.

Kutumia vyombo vya Habari katika kutoa elimu ikiwemo kutangaza kwa vipaza sauti, Televisheni, radio, blog na magazeti Kuboresha sheria zilizopo
Page 20 of 26

11.

12.

Kuishirikisha vyombo vyote vya dola, Serikali, Bunge na Mahakama katika kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua zinazostahili wale wote wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa.

13. Kushindanisha vyuo vya elimu, chuo kikuu huria na vyuo vya uganga katika kubuni mikakati namna ya kuwasaidia wajasiriamali na shughuli za usafi katika Manispaa ya Sumbawanga
14.

Kufanya matembezi ya mshikamanokwa ajili ya kuchangisha fedha, na makongamano ya kuhamasisha wadau juu ya Mpango huu. Kutenga maeneo ya shughuli za kiuchumi na kuwapanga wadau kadiri inavyofaa. Kutafuta wafadhili ikiwa ni pamoja na kutafuta marafiki wa Manispaa ya Sumbawanga Kiusafi. Kuendelea kutoa elimu kupitia sanaa na michezo. Kuhamasisha wadau kuchangia gharama pamoja na kufadhili vikundi vinavyojihusisha na kazi za taka

15.

16.

17. 18.

Namna ya ushiriki wa wadau. 1. Mkuu wa mkoa atakuwa na wajibu wa kutoa maelekezo ya mara kwa mara kuhusiana na hali ya Usafi na mazingira kwa ujumla ya Manispaa ya Sumbawanga na Mkoa kwa ujumla ili kusaidia maboresho yanayohitajika.
2.

Mkurugenzi wa Manispaa ndiye mmiliki mkuu wa mpango huu katika kufuatilia kazi za kila siku pamoja na gharama zinazohusika, pamoja na kuratibu maendeleo ya Mpango huu kwa kushirikisha wadau wengine pale inapobidi.
Page 21 of 26

3. Halmashauri ya Manispaa itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi ya biashara na shughuli za Mpango huu. 4. Halmashauri ya Manispaa itatakiwa kuhakikisha kuwa kila wakati kunakuwa na sheria ndogo zinazikidhi uwezeshaji wa Mpango huu. 5. Halmashauri ya Manispaa itatakiwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na sehemu sahihi za kuhifadhi taka kama vile dampo, na maeneo ya muda ya kuhifadhi taka
6.

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga itatakiwa kuwa na vitendea kazi vya uhakika kama vile magari, mifagio na chepe.

7. Pale inapowezekana Halmashauri itasaidia vikundi binafsi vinavyojishughulisha na kazi za taka na mazingira kwa ujumla 8. Wadau wa Mpango kwa kushirikiana na Manispaa watasaidia katika kuchangia mawazo, rasilimali watu na fedha ikiwemo shughuli za kitaalam kama vile kuandaa maandiko mbalimbali yanayolenga kutafuta fedha na vifaa na kadhalika. 9. Kila Diwani atatakiwa kusimamia kiukamilifu utekelezaji wa Sumbawanga Ngara katika eneo lake.
10. Kila

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa au kijiji atatakiwa kuja na mkakati wa eneo lake ukitafasiri mpango huu katika mazingira halisi ya eneo lake. Mfano kutambua kaya, maeneo ya kuhifadhi taka, namna ya kuchangia gharama ikiwemo kusafisha, kupanda miti, nyasi, bustani, kuondoa vifusi, kufukia mashimo barabarani, kuzibua mifereji, kuondoa mizoga na kadhalika. familia/kaya, au Taasisi yoyote kutekeleza matakwa ya mpango huu. ile itawajibika

11. Kila

Page 22 of 26

12. Watu binafsi au Vikundi mbalimbali vyenye nia ya kufanya kazi za kibiashara kuhusiana na mpango huu vitatakiwa kusaidiwa kwa kuwakewa utaratibu maalum usio na usumbufu na kuwatafutia kituo maalum (informal) ambacho kitasaidia kutoa anuani yao.
13.

NGO na CBO kuhakikisha kuwa mpango huu unajulikana kwa wengi na hivyo kusaidia kufanya kampeni, makongamano na utetezi wa uharibifu wa mazingira.

14. Wanasiasa na viongozi wa dini watatakiwa kuunga mkono mpango huu na kuhamasisha wafuasi wao kupitia mikutano yao mbalimbali.
15.

Wanafunzi watatakiwa kupewa elimu juu ya Mpango huu na wao kuwa vinara kupitia vilabu vyao vya mazingira.

16. Vyuo na taasisi za elimu vitatakiwa kufanya tafiti na kubuni mikakati itakayosaidia kuongeza kasi ya udhibiti wa mazingira na kuongeza ajira bora kupitia mpango huu. 17. Kila kijiwe cha biashara kuweza kupewa elimu ya usafi mahali walipo kwenye shughuli zao .

Upimaji wa Utekelezaji Upimaji wa utekelezaji wa mpango huu utafanyika kwa kuangalia mambo yafuatayo: Kupitia ukaguzi utakaofanyia kila wiki, itaweza kubainishwa hali invyoendelea kwa kuona, kuuliza, kwa taarifa za kazi za ukusanyaji wa taka. Taarifa za magonjwa ya hospitali zitaonyesha kupungua kwa magonjwa yanayoambatana na uchafu

Ushuhua wa Macho Manispaa itapendeza Ustaarabu utaongezeka mfano vitendo vya wizi, kutupa taka ovyo, vijiwe kupendeza n.k
Page 23 of 26

Sifa kutoka kwa wadau wenyewe

HITIMISHO
Tumeamua kuanza mpango huu kwa manufaa ya Mkoa wetu wa Rukwa na Tanzania nzima kwa ujumla. Naomba sote tudhamirie na tujitoe kuufanikisha mpango huu kwa ustawi wa leo na kesho ya Sumbawanga yetu. Kama alivyosema yule Mwandishi wa Marekani Hellen Keller kwamba, Peke yetu tunafanya machache, pamoja tunafanya mengi. Tukijitoa sote kufanya kazi kwa bidii na ufahamu hata yale yanayoonekana hayawezekani yatawezekana na hata yale yanayoonekana magumu yatakuwa mepesi. Na tuanze sasa safari hii yenye heri na mafanikio tukimuomba Mungu atusaidie. Maandishi haya yatuongezee nguvu ya kuanza safari yetu ya kuhakikisha Sumbawanga inangara na halmashauri nyingine za Rukwa zifuate, Tutaendelea kuboresha siku hadi siku, huku tukivuna uzoefu na kuweza kuyachapisha rasmi. Inawezekana timiza wajibu wako.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Rukwa.

Page 24 of 26

Page 25 of 26

Sumbawanga Ngara
Tumedhamiria, Tunaweza na Tutashinda!

Page 26 of 26

You might also like