You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAJI

Simu: +255 (0) 26 2322602 Mji wa Serikali,


Tovuti: www.maji.go.tz Mtaa wa Maji,
Barua pepe:ps@maji.go.tz S. L. P. 456,

DODOMA.

Kigoma: 18 Oktoba, 2020


 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


 
HUDUMA YA MAJI KIGOMA KUZIDI KUIMARIKA

Mkoa wa Kigoma umejipanga kufikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama


kwa asilimia 85 kwa wananchi waishio vijijini na asilimia 95 kwa wananchi waishio mijini
ifikapo Desemba 2020.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA)


mkoani Kigoma Mhandisi Mathius Mwenda amesema hivi sasa hali ya upatikanaji maji
imepanda kutoka asilimia 56 ya mwaka 2015 hadi asilimia 67 kwa vijijini na asilimia 58
ya mwaka 2015 hadi asilimia 75.

Mhandisi Mwenda amesema jumla ya miradi 31 imetekelezwa na kukamilika, ambapo


kupitia Mpango wa Malipo kwa Matokeo (PbR) miradi imekamilika na jumla ya vituo vya
kuchotea maji 523 vinahudumia wananchi, na kupitia Programu ya Matokeo (PforR)
mpango ulikua kutekeleza miradi 19, ambapo 18 ilikuwa ya ukarabati na utanuzi, na
mmoja mpya. Kati ya miradi hiyo mitano imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi,
na utekelezaji wake umefanikishwa na wataalamu wa Wizara ya Maji kupitia utaratibu
wa force account.

Aidha, Mhandisi Mwenda ameainisha kuwa wataalamu hao wanaendelea kukamilisha


idadi ya miradi ya maji 10 inayotumia fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa (NWF). Pamoja
na hayo, baadhi ya miradi inatekelezwa kwa ushirikiano na Washirika wa Maendeleo,
ikiwamo serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Mataifa na Shirika la Water Mission na Islamic
Foundation. Miradi inayoendelea kutekelezwa inatarajiwa kukamilika Desemba 2020
itaongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi, salama na yenye
kutosheleza kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma.

Mkoa wa Kigoma unaundwa na wilaya sita ambazo ni wilaya ya Kigoma, Kasulu,


Kibondo, Kakonko, Uvinza na Buhigwe.

Kitengo cha Mawasiliano

You might also like