You are on page 1of 3

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY


PRESS RELEASE

Zanzibar Machi 25, 2020

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali


Mohamed Shein amewataka wananchi kuacha ukaidi na kufuata
kikamilifu maelekezo ya Serikali, ikiwa ni hatua za kuunga mkono
juhudi za Serikali katika kukabiliana na Virusi vya Ugonjwa wa
Corona.

Dk. Shein amesema hayo Binguni Mkoa wa Kusini Unguja, alipolitembelea


eneo linalojengwa Hospitali kuu ya Kisasa, mahala ambapo pia itajengwa
Taasisi ya Utafiti ya Wizara ya Afya.

Amesema katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo, Serikali tayari


imetowa malekezo kadhaa, ikiwa njia ya kujikinga na virusi vya ugonjwa
huo, hivyo akawataka wananchi kuacha ukaidi na kutekeleza maelekezo ya
kudumisha usafi kama inavyoelekezwa.

Alisema Virusi vya Ugonjwa wa Corona ni janga la Kimataifa na ni maradhi


yasiotaka mzaha wala hayachaguwi aina ya mtu wa kuamuathiri, hivyo ni
vyema wananchi wakaondokana na ushindani na kuzingatia maelekezo ya
Serikali.

Alieleza kuwa Serikali imeingia katika vita dhidi ya adui asieonekana na


hivyo ikalazimika kuchukuwa hatua mbali mbali za dharura ikiwemo kuzuia
Kongamano la dini pamoja na kuzifunga skuli zote na wanafunzi kukosa
taaluma.

Shein alisema Serikali haiwezi kuainisha ukubwa wa gharama


inazopoteza kutokana na hatua ilizochukuwa katika kukabiliana na virusi
vya ugonjwa wa Corona, sambamba na athari za kiuchumi zitokanazo na
kuvurugika kwa sekta ya utalii, ambayo huchangia asilimia themanini ya
Pato la Taifa.
Rais Dk. Shein aliwataka wananchi kuondokana na upotoshaji kupitia
mitandao ya kijamii.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa wananchi kuondokana na mikusanyiko,


hususan katika eneo la Hospitali kuu ya Mnazi mmoja pamoja na maeneo
ya masoko, kwa kigezo kuwa hatua hiyo inaweza kuwa chanzo cha
kusambaa kwa viusi hivyo, pale itakapotokezea mtu mmoja kuwa navyo.

Katika hatua nyengine, Dk. Shein alilisistiza azma ya Serikali ya kujikita


katika kufanya uchunguzi wa maradhi mbali mbali kwa kigezo kuwa hakuna
tiba muafaka bila ya kuwepo uchunguzi, hivyo akabainisha dhamira ya
Serikali katika kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la Maabara katika
eneo hilo la Binguni.

Alisema Serikali imefikia uamuzi wa kukamilisha jengo hilo mahala hapo


kwa kuzingatia mazingira bora yaliopo, ambayo yamejitenga na eneo la
makaazi ya wananchi.

Aliwahakikishia wananchi kuwa jengo hilo litakamilika katika kipindi kifupi


kijacho na kuwekewa vifaa vyote muhimu ili kukidhi mahitaji na malengo
yaliokusudiwa.

Aidha, alisema Serikali itakamilisha miradi yote ya Maendeleo iliyokwisha


anzishwa, ikiwemo ya ujenzi wa Nyumba Kwahani, Michenzani Moull,
Barabara, Mahakama Kuu na mingineyo pamoja na kuanzisha miradi
mipya, huku akibainisha kuwa endapo kutatokezea upungufu wa fedha
itaangalia namna ya kukamilisha miradi hiyo.

Mapema, Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed, amesema Wizara hiyo


imejiandaa kikamilifu kushirikiana na Serikali ya Watu wa China katika
dhana ya kukuza utalaamu ili kuleta ufanisi wa maabara itakayojengwa.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar


Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822

E-mail: abdya062@gmail.com

You might also like