You are on page 1of 6

MUHTASARI

WA MKUTANO MKUU MAALUM WA KAWAIDA WA WANAHISA


WA KAMPUNI YA JATU PLC


TAREHE
04.08.2018


SIKU
JUMAMOSI


ENEO
OFISI KUU ZA JATU PLC


MUDA
04:00 Asubuhi - 08:45 Mchana




















JENGA AFYA TOKOMEZA UMASKINI NA JATU PLC

1
Kikao kilikua na ajenda kuu SABA ambazo ni,
1. Kufungua kikao
2. Kupokea ripoti ya wanahisa walio weka ahadi ya kunua hisa kwa mwaka 2018
3. Utaratibu wa kupokea gawio la hisa la mwaka wa kifedha kwa mwaka 2017/2018
4. Mchakato wa kwenda soko la hisa, ambapo kutakuwa na wataalam wanaosimamia zoezi
zima la DSE
5. Matokeo ya mradi wa kilimo kwa msimu wa mwaka 2017/2018
6. Mengineyo
7. Kufunga kikao



AJENDA YA KWANZA
Kufungua kikao
Katika ajenda hii mwenyekiti ndugu Eva Damas Kapinga aliwasalimu wajumbe na
kuwakaribisha, kisha alituongoja kwa sala ya kipekee kabisa kwani kikao chetu kwa mara ya
kwanza kilifunguliwa kwa nyimbo ya TAIFA, yote hii ni ishara tosha kuwa JATU PLC ni yakila
mtanzania ambaye anapenda kuwekeza, tunamkaribisha sana. Baada ya nyimbo yetu
pendwa, mwenyekiti alitufungulia kikao chetu rasmi satano na dakika ishirini na tano asubui
(05:25).


AJENDA YA PILI
Kupokea ripoti ya wanahisa walio weka ahadi ya kunua hisa kwa mwaka 2018
Katika ripoti hii ambayo ilitolewa na mhasibu wa jatu plc Bi Esther Marino, kuwa mpaka kufikia
siku ya leo ya tarehe 04/08/2018, tuna jumla ya fomu 200 za wanahisa walizojaza kwaajili ya
kununua hisa, ambazo ni jumla ya hisa elfu tisini na nne mia nane na nane (94,808) zenye
jumla ya thamani ya shilingi milioni mia mbili thelathini na saba na elfu ishirini. (237,020,000).


AJENDA YA TATU
Utaratibu wa kupokea gawio la hisa la mwaka wa kifedha kwa mwaka 2017/2018,
Kuhusu utaratibu wa kupokea gawio la hisa kwa mwaka wa kifedha wa 2017, hapa kulitolewa
ufanunuzi na mhasibu kuwa, ili kujua kuwa kila mwanahisa amepata gawio kiasi gani, kila
mwanahisa ili ajue kila hisa moja imepata faida ya shilingi ngapi inakubidi uchukue hisa moja
unagawanya na jumla ya hisa zilizonunuliwa kwa mwaka 2017, kisha unazidisha mara faida
iliyopatikana ambapo utapata shilingi hamsini na sita pointi nne. Hivyo ili kujua umepata

2
gawio kiasi gani kwa mwaka 2017 ni kitendo cha kuchukua hisa zako zote ukazidisha mara
hamsini na sita pointi nne, utajua umepata faida kiasi gani. Mfano unahisa hamsini ukizidisha
mara hamsini na sita pointi nne utapata shilingi 2820, hii ni fedha ila tulikubaliana katika
mkutano mkuu wa wanahisa kuwa gawio letu litagawiwa kwa kuongezewa hisa. Kwaiyo 2,820
ukigawanya katika mfumo wa hisa ambapo hisa moja ya jatu plc ni 2,500 utapata hisa 1.128
kwa makadirio ya kimahesabu ni sawa na kusema mwenye hisa 50 amepata faida ya hisa
moja.


AJENDA YA NNE
Mchakato wa kwenda soko la hisa ambapo kutakuwa na wataalam wanaosimamia zoezi
zima la DSE

Katika ajenda hii kulikua na wageni waalikwa ambao ni Ndugu RICHARD MANAMBA huyu ni
mtaalam kutoka soko la hisa na mitaji na mshauri wa maswala ya kibiashara, Ndugu MAFURU
& CO ADVOCATE ambaye ni wakili na kazi yake kubwa nikupitia maswala ya kisheria na
kushauri kulingana na sheria zinazo tumika katika kuanzisha na uendeshwaji wa kampuni ya
umma na mwisho ni Ndugu OCTAVIAN KESSY huyu ni mkaguzi na mtaalam wa mambo ya
kifedha.
Lengo ni kuhakikisha ifikapo mwezi wa kumi na moja mwaka 2018, kampuni ya jatu plc
inaingia kwenye soko la hisa na kukaribisha umma wote kila kona ya Tanzania, ili waweze
nunua hisa za jatu plc. Baada ya utambulisho huo mfupi mkurugenzi ndugu Peter Isare Gasaya
aliwakaribisha wataalam hao kisha kutoa maelezo kwa kina kuwa kazi iliyopo mbele yao
nikuandaa nyaraka muhimu zinazohitajika kwenye soko la hisa na mitaji kabla ya kampuni
kuingia kwenye soko hilo na kuuza hisa kwa umma.
Moja ya suala lililo jadiliwa na wataalam hawa ni kuhusu kupungua ama kubakiza bajeti
pendekezwa ya 7.5 Bilioni, hapa mkurugenzi aliwaeleza wanahisa kua kama tukisema
tupunguze bhasi itabidi tuanze upya kubadili mpango biashara wetu na kuingia makubaliano
mapya tena, ila ili kupata majibu ni vema tukapiga kura ili kujua niwangapi wanasema
tupunguze na wangapi wanasema tuende nayo hiyo hiyo bajeti pendekezwa ya 7.5 Bilioni.
Katika kupata majibu ilibidi kura zipigwe na matokeo yalikua kama ifuatavyo ‘’waliosema
bajeti pendekezwa isipungue ni 54 na waliosema ipungue ni 47, kura zilizoharibika ni 10, jumla
yawapiga kura ni 111’’. Kwa matokeo hayo tajwa hapo juu ni Dhahiri kuwa walio na kura
nyingi ndio washindi ambao waliomba tuendelee na bajeti pendekezwa kama ilivyo yaani 7.5
Bilioni.



3
AJENDA YA TANO
Matokeo ya mradi wa kilimo kwa msimu wa mwaka 2017/2018
Kuhusu matokeao ya mradi wa kilimo kwa msimu wa kwanza wa mwaka 2017/2018, hii ilikua
ajenda kubwa na ikisubiriwa kwa shauku kubwa na wanakilimo wote. Hapa mwenyekiti
alimkaribisha Mhasibu wa jatu plc kutoa taarifa fupi kuhusu mradi wa kilimo ambapo alitoa
ufafanuzi kuwa katika ekari 728 za mahindi zilizolimwa mpaka sasa tumefanikiwa kuvuna
ekari 628 ambapo tumefanikiwa kupata wastani wa magunia kumi na moja (11) kwa kila ekari
(yaani tumepata kuanzia magunia nane hadi kumi na tano). Hivyo kwa wastani tumefanikiwa
kupata jumla ya magunia 6,908.
Bei ya soko kwa sasa ni shilingi 310 kwa kilo moja ya mahindi hivyo kila gunia litauzwa shilingi
27,900, kwa wastani huo wa magunia 11 tunatarajia kupata shilingi 306,900 kwa kila ekari.
Hii italeta faida ya shilingi 56,900 kwa ekari kwa sababu gharama za shamba kuanzia kupanda
mpaka kuvuna zilikuwa ni shilingi 250,000 kwa ekari moja.
Pia aliongezea kwakusema kuwa, tunatarajia kuanza msimu wa pili wa kilimo mnamo mwezi
wa 11 mwaka huu, hivyo kwa wanachama walionunua mashamba msimu wa kwanza hatua
inayofuata ni kung’oa visiki kwa gharama ya 100,000 kwa ekari.
Kwa wanachama walionunua mashamba msimu wa pili yaani kiteto mashamba ya 200,000
kwa ekari na kilombero mashamba ya 500,000 kwa ekari wataingia kwenye msimu huu wa
kilimo kwa kuchangia gharama zifuatazo:


• MCHANGANUO WA GHARAMA ZA KULIMA EKARI 1 KILOMBERO:
1. Kuandaa shamba: 100,000/=
2. Mbegu: 50,000/=
3. Dawa: 80,000/=
4. Mbolea: 85,000/=
5. Ng’olezi: 100,000/=
6. Kuvuna: 120,000/=
7. Kusomba na kuhifadhi: 65,000/=

JUMLA: 600,000/=
8. Usimamizi wa shamba: 100,000/=
JUMLA KUU: 700,000/=
Zingatia: Gharama za usimamizi wa shamba zitalipwa mara tu baada ya mavuno.


4
• MCHANGANUO WA GHARAMA ZA KULIMA EKARI 1 CHA KITETO:
1. Kuandaa shamba: 50,000/=
2. Kupanda: 20,000/=
3. Mbegu: 60,000/=
4. Kupalilia: 50,000/=
5. Dawa: 40,000/=
6. Kuvuna: 30,000/=
JUMLA: 250,000/=
8. Usimamizi wa shamba: 50,000/=
JUMLA KUU: 300,000/=

Zingatia: Gharama za usimamizi wa shamba zitalipwa mara tu baada ya mavuno.

AJENDA YA SITA
Mengineyo
Katika ajenda hii wajumbe wengi walipata wasaa wakutoa maoni, maswali na kutoa pongezi
kwa uongozi. Baadhi ya wajumbe hao ni DESDERIUS MBEKENGA alisimama nakusema sina
swali, ila baada ya Mkurugenzi kuongea nimepata nguvu, sasa hili lilikua shamba la majaribio
kwaiyo tuongeze nguvu, ili tufikie lengo. Baada ya kikao hiki tuje na mawazo ili tuweze jadili
siku hiyo ya kilimo. Abeid Kasabalala yeye alitoa pongezi, kisha akasema watu ni wavivu
wakusoma, tengenezeni utaratibu wa kusoma mihutasari ya vikao ili tuweze kuyafanyia kazi
kwa wote haya tunayokubaliana. Elibariki Tweve, Je kilimo kitakua na kikao kingine au
tumejuisha kwenye kikao hiki cha leo?. Katika kujibu swali hili mkurugenzi alitoa ufafanuzi
kuwa tutakua na kikao kingine maalum cha kilimo chenye kutoa tathmini juu ya mchakato
mzima wa kilimo cha 2017/2018 mara tu zoezi la uvunaji wa alizeti kukamilika. Hapa tutajua
gharama zote tulizotumia kwenye kilimo kwa msimu wa kwanza, changamoto na jinsi ya
kuboresha kabla hatujaanza msimu wa pili yaani 2018/2019.

Pia Gloria Mzanva alikua na maswali mawili, mosi Je ile gharama uliyosema imeshuka vipi
mbona imepanda tena? Pili ulisema tunaweza toa hata gunia 20, sasa mbona imekata hadi
nusu? Hapa mkurugenzi alisema kwakua hiki kilikua kilimo cha mwaka wa kwanza
changamoto ni nyingi na zingine hatukuzifahamu hapo awali, mfano kwa sasa tunaingia
gharama ya usimamizi wa shamba pamoja na ushuru wa shilingi 1500 kwa kila gunia moja hizi
nimalipo ya mapato ya halimashauri hivyo imetubidi kupandisha gharama ili kumudu
gharama zilizoongezeka kwa sasa kwa kipindi hiki cha mavuno ambazo kwakua
hazikutangazwa hapo awali jatu plc imedi aingie gharama ya kuzilipa na ndio maana matarajio
yetu ya kushusha gharama za kilimo zimeshindikana badala yake zimeongezeka na hapa
tutaongeza gharama ya usimamizi wa shamba tu kwa kila ekari moja ambapo kwa kiteto
itaongezeka shilingi 50,000 na kwa kilombero itaongezeka 100,000 kwa kila ekari na hizi
zitalipwa mara tu baada ya mavuno. Kuhusu magunia kupungua ni kutokana na sababu kuwa

5
kilimo chetu tulilima kwakutegemea nvua ni kwahili lazima tuwe wakweli kilimo cha
kutegemea nvua kina changamoto hilo hata sisi halikua kusudio letu tunashukuru kwa wastani
huu wa gunia 11 kwa kila ekari, kazi kubwa tuliyonayo hivi sasa nikuboresha mradi wetu wa
kilimo ili tufanye kilimo cha kisasa, hapo ndipo tunaweza jiuliza swali shida iko wapi na
tunadhana zote nzuri na za kisasa za kilimo.


AJENDA YA SABA
Kufunga kikao
Mwisho kikao kiliahirishwa na mwenyekiti wa bodi ya jatu plc majira ya sanane na dakika
arobaini na tano (08:45) mchana hadi tutakapo itisha kikao kingine maalum kwaajili ya
wanakilimo kupata mchanaganuo kamili kuhusu mradi wa kilimo cha 2017/2018 katika ofisi
kuu za jatu.









IMEANDALIWA NA;

……………………………….
MOHAMED ISSA SIMBANO,
KATIBU MKUU-JATU PLC.

You might also like