You are on page 1of 1

Date 29/02/2020

Ndugu: Miriam Sanga.

YAH: KUSITISHWA KWA MKATABA WA KAZI

Mwanzoni mwa mwaka huu, Kampuni ilianza mchakato wa kurekebisha muundo na utendaji kazi
kutokana na mabadiliko ya Kibiashara na kimfumo, kama ilivyotoa taarifa yake ya tarehe 02 Januari
2020 kwa wafanyakazi wote juu ya mchakato huu na matokeo yake.

Kampuni inapenda kukupa taarifa kuwa, kutokana na zoezi hilo, ifikapo tarehe 31 Machi 2020 itakuwa ni
siku yako ya mwisho ya kufanya kazi nasi. Barua hii inatoa kusudio hilo, kwa kufuata sheria ya Ajira ya
Kazi na mahusiano Kazini ya Mwaka 2004, Kifungu cha 41: (1) – (5).

Kwa kipindi cha notisi hii, unapewa nafasi ya kutoingia kazini, na kutumia muda huo kuchukua fomu ya
uhakiki wa mali za Kampuni zilizokuwa chini ya uangalizi wako, zinazopatikana katika Ofisi ya Rasiliamali
Watu ili kuhakiki na idara husika na kuirudisha kabla ya siku yako ya mwisho ya notisi. Fomu hiyo ndiyo
itakayotumika kufanya malipo yako ya mwisho, ukiwepo mshahara wa mwezi Machi na stahiki nyingine
unazostahili.

Tafadhari, thibitisha kupokea Barua hii kwa kusaini sehemu iliyoandaliwa hapo chini, na kurudisha
nakala Ofisi ya Rasiliamali watu.

Tunakutakia ukamilishaji mzuri wa taratibu hizi kama zilivyoandaliwa.

Venite Zenda
Meneja Royal Highland LTD.
Tawi la Mbeya.

Mimi …………………………………., Nathibitisha kupokea Barua. Sahihi.....................Tarehe.......................

You might also like