You are on page 1of 4

MKATABA WA AJIRA

Mkataba huu umefanyika hapa Dar es Salaam leo hii tarehe ………. mwezi ……… 2023

KATI YA

MAGNIFIQUE BUILDERS LIMITED wa S.L.P 38484 Jengo la Pegasus Mtaa wa


Nkurumah/Gerezani Dar es Salaam (ambaye katika mkataba huu anajulikana kama
“MWAJIRI”) neno ambalo litahusisha warithi halali wa mwajiri kwa upande wa
kwanza.
NA
NAKIJWA JOHN MMBUJI umri miaka……….…. Jinsia FE, mkazi wa Dar es Salaam,
Simu Na……………….………Barua pepe (Email) ……………………………….… ambaye
katika mkataba huu anajulikana kama “MWAJIRIWA”) kwa upande wa pili.
1. MWANZO WA MKATABA NA UKOMO WAKE:
Mwajiriwa atakuwa katika kipindi cha majaribio kwa muda wa Miezi mitatu tangu
tarehe atakayosaini mkataba huu wa ajira na utakoma tarehe…………………..
2. MAHALI PA AJIRA:
Kwamba ajira hii imefanyika hapa Dar es Salaam.
3. MAHALI PA KUFANYIA KAZI NI:
MAGNIFIQUE BUILDERS LIMITED, Pegasus House, Nkurumah Road/ Gerezani
Street, Adjacent Kamata Traffic Lights, P.O. Box 38484 Dar Es Salaam.
4. MAJUKUMU YA KAZI:
4.1 Kwamba mfanyakazi ameajiriwa kwa nafasi ya SALES OFFICER.
4.2 Kwamba majukumu yake ya kazi yatakuwa kadri ya atakavyopangiwa na
meneja wake siku kwa siku na kama ilivyoanishwa kwenye
kiambatanisho A kilichoko kwenye mkataba huu cha majukumu ya kazi
ambacho ni sehemu ya mkataba huu.
5. KIPINDI CHA MAJARIBIO:
5.1 Mwajiriwa atakuwa katika kipindi cha majaribio kwa muda wa Miezi
mitatu tangu tarehe atakayosaini mkataba huu wa ajira na utakoma
tarehe………………. Dhumuni la majaribio haya ya kazi ni kuweza
kutambua uwezo wa kazi wa Mwajiriwa kwa kazi Husika kabla
hajaajiriwa rasmi. Kama mkataba huu utavunjwa ndani ya muda wa
majaribio mwajiriwa atapewa notisi ya maandishi ya siku saba ya
kuvunjwa kwa mkataba huu.
5.2 Muda wa majaribio unaweza kuongezwa au kupunguzwa na mwajiri
pale atakapoona ni vema kufanya ivyo.
5.3 Kikomo cha muda wa majaribio. Mwajiri anatakiwa kumfahamisha
mwajiriwa kwa maandishi kuchaguliwa kwake katika ajira, kama tu
hakupata taarifa katika mkataba wake, Mwezi mmoja baada ya kuisha
muda wa majaribio.
6 MALIPO YA MSHAHARA NA MARUPURUPU
6.1 Mshahara wako utakuwa ni Tshs ______________________ kwa mwezi.
6.2 Posho ya kujikimu ni Tshs ……………………………. Kwa siku/ Mwezi.
6.3 Mwajiri anakubali kukatwa makato yafuatayo NSSF, PAYE pamoja na
makato mengineyo yalioanishwa kwa mujibu wa sheria za kazi hapa
nchini.

7 MASAA YA KAZI:
7.1 Kwamba masaa ya kawaida ya kazi yatakuwa kuanzia saa …….mpaka
____________ na usiku ni saa ……………. hadi saa ………………
7.2 Kwamba wiki ya kazi itanzaa……………. mpaka ……………………

7.3 Muajiriwa atalazimika kufanya kazi masaa ya ziada kwa kadiri


atakavyopewa maelekezo na muajiri ili kufikia malengo ya kazi kama
walivyokubaliana. Hata hivyo pande zote mbili zitakubaliana masaa ya
ziada ya kazi yatalipwa kiwango cha asilimia gani.
7.4 Hakutakuwa na malipo mengine ya ziada yaani (overtime)
pasipokuwepo makubaliano.
8 LIKIZO YA MWAKA:
8.1 Muajiriwa ana haki ya kupata likizo ya malipo ya siku 28 mfululizo
baada ya kutimiza miezi 10 ya kufanya kazi, siku za likizo zitajumuisha
pia siku za sikukuu zitakazoangukia kwenye likizo yake.
8.2 Kwamba siku za likizo zaweza kupunguzwa kwa siku ambazo muajiriwa
aliomba likizo ya dharura
8.3 Mwajiri hatakiwi kumfanyisha kazi muajiriwa wakati awapo likizo.
8.4 Kipindi cha sikukuu mwajiri akimhitaji mfanyakazi basi atamlipa
mshahara masaa ya ziada (overtime) kulingana na sheria za kazi.

9. LIKIZO YA UGONJWA AU AJALI:


9.1 Endapo muajiriwa ataugua au kupata ajali kazini, atapewa likizo yenye malipo
au ruhusa ya siku kati ya 7 au 14 (wiki moja au mbili) kutegemea na ukubwa wa
tatizo na pia uthibitisho wa cheti kutoka kwa daktari au mtaalamu wa afya
anayetambulika na serikali. Cheti husika ni lazima kiwasilishwe kwa mwajiri
pindi tuu kitapohitaji kwa uthibitisho.
9.2 Endapo muajiriwa atashindwa kuripoti kazini baada ya siku za ruhusa ya
ugonjwa kuisha, basi itamlazimu kuzifidia siku asizokuwepo kazini ama
kupunguza siku zake za likizo ya mwaka au kukatwa mshahara wa mwezi
husika.

10. LIKIZO YA UZAZI: KWA WANAWAKE


10.1 Mwajiriwa wa kike atastahili likizo ya uzazi katika mzunguko wa miezi
36 mfululizo, siku 60 endapo atajifungua mtoto mmoja na siku 90 akijifungua
zaidi ya mtoto mmoja kwa malipo ya nusu mshahra wake kwa miezi.
10.2 KWA WANAUME: Kwamba, muajiriwa wa kiume atastahili likizo ya
siku 3 yenye malipo katika mzunguko wa miezi 36 mfululizo, endapo mke wake
atajifungua na atatakiwa kumtaarifu mwajiri ndani ya siku 7 tangu mke wake
amejifugua na kuleta kadi ya kliniki ya mke wake.
10.3 Kujiunga na chama cha wafanyakazi
Mfanyakazi ana haki ya kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi kilichopo
kwa mujibu wa sheria

11. USITISHAJI WA AJIRA:


Kwamba, mkataba huu unaweza kusitishwa na upande wowote ule kwa kutoa
ILANI ya siku 28 au malipo ya badala ya notisi.
Kwamba usitishaji wa ajira utaambatana na sababu zinazohusiana na makosa ya
UTOVU WA NIDHAMU KAZINI, KUTOKUWAJIBIKA AU UTENDAJI
MBOVU WA KAZI, UTORO AU KUTOKUHUDHURIA KAZINI BILA
TAARIFA, MAHUSIANO MABAYA KAZINI, NA TABIA YA UNYANYASAJI.

12. MATUMIZI YA SHERIA.


Kwamba makubaliano haya yatatawaliwa na matakwa ya sheria ya ajira na
mahusiano kazini No.6 ya 2004.
Mwajiriwa ana haki ya kupewa mafao yoyote ambayo yametajwa katika Sheria
ya ajira na Mahusiano kazini ya 2004.

Makubaliano yamesainiwa na

_________________________ _______________________
MWAJIRI TAREHE

_______________________ ________________________

MWAJIRIWA TAREHE

UTHIBITISHO WA SAINI ZA HAPO JUU

JINA …………………………………..

SAINI ……………………………………

CHEO WAKILI

You might also like