You are on page 1of 3

MKATABA WA KUPANGISHA FREM ZA BIASHARA

MAKUBALIANO HAYA yamefanyika leo tarehe………mwezi …………………..


…, 20……
KATI YA

_______________________________ wa S.L.P_____, _______________ (ambaye


katika Mkataba huu atajulikana kama “MWENYE FREM”) kwa upande mmoja.
NA

…………………………………………………… wa ambaye S.L.P. ………………,


Dar es Salaam (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “MPANGAJI”) kwa
upande mwingine.

KWA KUWA:-

A. MWENYE FREM anayo madaraka ya mwisho juu ya frem za biashara


zilizopo katika
_________________________________________________________.

B. MWENYE FREM yuko tayari kumpangisha MPANGAJI namba …… iliyopo


katika kiwanja kilichotajwa hapo juu kwa makubaliano yaliyo ndani ya
Mkataba huu. na MPANGAJI yuko tayari kupanga frem hiyo hiyo iliyotajwa
hapo juu kwa kuzingatia masharti yaliyo ndani ya Mkataba huu;

HIVYO BASI MKATABA HUU UNASHUHUDIA haya yafuatayo:-

1. MWENYE FREM anampangisha MPANGAJI frem iliyotajwa hapo juu


kwa kipindi cha miezi ……………….…… kuanzia tarehe………
mwezi…………………., 20…… hadi tarehe……… mwezi
………………………, 20..….

2. Kodi ya frem ni ________________kwa mwezi na MPANGAJI kwa


upande wake nakubali kulipa kodi ya kipindi chote cha mkataba huu
ambayo itakuwa ni shilingi ___________________________________

3. MPANGAJI anatanguliza kiasi cha kodi cha


____________________________________________________________
________________________________ itakayolipwa tarehe
……………………………. Kodi inayosalia ya ____________________
itatakiwa kulipwa kabla ya tarehe ____________________.

4. MPANGAJI atamruhusu MWENYE FREM au wakala wake katika muda


ufaao na kwa taarifa kabla ili aweze kukagua frem hiyo kwa madhumuni
ya matengenezo, marekebisho au ukaguzi wa kawaida.

5. MPANGAJI ataiweka frem katika hali ya usafi na uangalifu nyakati zote


na atalipa bili za umeme na maji zitakazotokana na matumizi yake katika
kipindi cha mkataba.
6. MWENYE FREM hatambugudhi MPANGAJI kwa kipindi chote cha
upangaji iwapo MPANGAJI atatimiza masharti ya mkataba huu.

7. MWENYE FREM atalipa kodi ya kiwanja.

8. Mkataba huu unaweza kuvunjwa kabla ya muda wake kumalizika na


upande wowote kwa kutoa taarifa ya mwezi mmoja ya maandishi ya
kusudio la kuuvunja kwa upande mwingine na endapo MWENYE FREM
ndiye anayetaka kukatisha mkataba atalazimika kumrudishia MPANGAJI
kiasi cha kodi ya muda uliobaki.

9. MWENYE FREM hatakuwa na jukumu la kutoa ulinzi kwa ajili ya


wapangaji

10. Frem zote zinapangishwa kama zilivo, na MWENYE FREM hatokua na


jukumu la kufanya marekebisho yoyote ili kuwezesha shughuli za
mpangaji.

11. MPANGAJI anakusudia kufanya matumizi ya kibiashara tu, ambapo


biashara itakayokuwepo ni ya ……………………………………………..

12. MPANGAJI atapaswa kuhakikisha anakabidhi frem katika hali


inayofanana na alivoipokea, ikiwemo na vifaa vyote alivokabidhiwa kama
mita ya LUKU na kadhalika

13. Hairuhusiwi MPANGAJI yoyote kufanya marekebisho ya aina yoyote


ikiwemo ya umeme bila kumshirikisha mwenye frem au muwakilishi
wake.

14. Mkataba huu utatafsiriwa kwa kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano


wa Tanzania.

Wahusika wametia saini mkataba huu kwa namna inayoonekana hapa chini.

IMESAINIWA na KUWASILISHWA hapa DSM ]


na ___________________________ ]
ambaye namfahamu binafsi/ ambaye ametambulishwa ]
kwangu na ……………………………………………. ] …………………………
ambaye namfahamu binafsi, mbele yangu leo tarehe……… ] MWENYE FREM
mwezi …………………………, 20……. ]

MBELE YANGU:

JINA:…………………………………………………….

ANWANI:………………………………………………

SAHIHI………………………………………………….

CHEO……………………………………………………
IMESAINIWA na KUWASILISHWA hapa DSM ]
na ……………………………………………… ]
ambaye namfahamu binafsi/ ambaye ametambulishwa ]
kwangu na ……………………………………………. ] …………………………
ambaye namfahamu binafsi, mbele yangu leo tarehe……… ] MPANGAJI
mwezi …………………………, 2013 ]

MBELE YANGU:

JINA:…………………………………………………….

ANWANI:………………………………………………

SAHIHI………………………………………………….

CHEO……………………………………………………

You might also like