You are on page 1of 5

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA

KATI YA

ELIAMIN NGATARA SOMI


(MWENYE NYUMBA)

NA

………………………………………………………………………………………………………………………….

(MPANGAJI)

KATIKA NYUMBA ILIYOPO KIWANJA NAMBA …………., BLOCK …………… KATA YA


NYAMANORO, HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEMELA, MKOA WA MWANZA.
MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA
Makubaliano ya mkataba huu yameafikiwa na kutiliwa saini leo tarehe ……….. Mwezi wa ……….
Mwaka ……………….

BAINA YA

ELIAMIN NGATARA SOMI wa S.L.P……………….. MWANZA (Ambaye ndiye mmiliki wa Nyumba, na


upande wa kwanza wa mkataba)

NA

…………………………………………………………………………………………. wa S.L.P ………………………………………….


Mwenye namba ya simu …………………………. /…………………………. (Ambaye ndiye mpangaji wa
nyumba na upande wa pili wa mkataba).

KWA KUWA, Mwenye nyumba ni mmiliki halali wa nyumba hiyo iliyopo katika kiwanja Na
……………, Block …………, Kata ya Nyamanoro, halmashauri ya wilaya ya Ilemela, Mwanza.
NA KWA KUWA, Mpangaji amefikia makubaliano ya kimkataba na mwenye nyumba ilikuitumia
nyumba kama Mpangaji, kwa malipo ya kodi ya TSH. MILIONI TANO TU, kama kodi ya Mwaka
mmoja (Miezi 12) kwa mujibu wa masharti na makubaliano yaliyo afikiwa katika mkataba huu.
NA KWA KUWA, mwenye nyumba amekubali kuipangisha nyumba kwa Mpangaji.

HIVYO BASI, MKATABA HUU UNAJENGWA NA MAKUBALIANO YAFUATAYO.


1. KWAMBA, Imekubaliwa na pande zote mbili kwamba kodi ya Nyumba itakuwa inalipwa
kwa Mwaka mmoja (1), ambayo ni fedha taslimu TSH. 5,000,000/=

2. KWAMBA, Mpangaji atakata 90% (Asilimia tisini) ya kodi yote TSH. 5,000,000/= Na
kumkabidhi mwenye nyumba TSH. 4,500,000/=. Stakabadhi ya malipo yatakayofanyika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
3. KWAMBA, makato ya TSH. 500,000/= kama asilimia kumi 10% ya malipo yote yatalipwa
na Mpangaji kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

4. KWAMBA, Mpangaji atalipa hela ya kodi kwa fedha taslimu (Cash) kwa Mwenye
nyumba.

5. KWAMBA, Mkataba huu umesainiwa na kuanza kufanya kazi kisheria kuanzia tarehe
……..Mwezi ……… Mwaka …………….. Na siku ya mwisho ya mkataba huu itakuwa tarehe
………Mwezi …………. Mwaka ………………

6. KWAMBA, Mpangaji atatimiza masharti yote ya pango kama kulipa bili zote za umeme
na maji kwa kuwa nyumba hiyo inajitegemea.

7. KWAMBA, kipindi cha upangishaji katika mkataba huu ni mwaka mmoja ambapo
mpangaji atapaswa kuzingatia usafi wa Nyumba hiyo, nje na ndani ya Nyumba.

8. KWAMBA, Mwenye nyumba kwa wakati muafaka anayo haki kuingia katika nyumba
husika pale inapobidi ili kukagua nyumba na kiwanja.

9. KWAMBA, Mpangaji haruhusiwi kumpangisha nyumba husika Mpangaji mwingine bila


idhini ya Mwenye nyumba.

10. KWAMBA, Eneo la kupaki gari ni haki ya wapangaji wote.

11. KWAMBA, Mwenye nyumba hatahusika na uharibifu wowote utakaosababishwa na


Mpangaji, ila Mpangaji atawajibika kwa uharibifu wowote.

12. KWAMBA, Endapo upande wowote wa mkataba huu utakuwa na nia ya kuongeza muda/
kipindi cha mkataba, notisi ya mwezi mmoja itatolewa na upande husika wa mkataba.

13. KWAMBA, Upande wowote wa mkataba huu ukitaka kusitisha mkataba huu basi
unawajibika kutoa notisi/ taarifa ya miezi mitatu kabla ya tarehe ya mwisho ya mkataba
huu.
KWA KUTHIBITISHA: Yote yaliyotangulia, pande zote mbili za mkataba (Mwenye nyumba na
Mpangaji) zinaweka sahihi ya makubaliano ya kutekeleza yaliyoafikiwa hapo juu kama
inavoonekana hapo chini.

UMESAINIWA hapa MWANZA na,


ELIAMIN NGATARA SOMI
Ametambulishwa na ………………………………………..
……………………………………………….
Ambaye namfahamu binafsi mbele yangu leo Mwenye Nyumba.
Tarehe …….... Mwezi………..Mwaka.

MBELE YANGU
Jina:
Sahihi:
Anuani: S.L.P ………………………………………..
Namba za simu: ……………………………………………………
Wadhifa ……………………………………

UMESAINIWA hapa MWANZA na,


……………………………………………………………………………………..
Ambaye namfahamu binafsi /Ametambulishwa na .
…………………………………………
…………………………………………………………………………..
Ambaye namfahamu binafsi mbele yangu leo Mpangaji wa Nyumba.
Tarehe …….... Mwezi………..Mwaka.
MBELE YANGU
Jina:
Sahihi:
Anuani: S.L.P ………………………………………..
Namba za simu: ……………………………………………………
Wadhifa ……………………………………

You might also like