You are on page 1of 1

MKATABA WA MAKABIDHIANO YA BAJAJI

Mimi …..(mmiliki) nimeamua kumkabidhi bajaji ndugu …..(Dereva) awe dereva wa bajaji
yenye namba ya usajili MC 390BPY kwa makubaliano ya kufanya kazi kila siku kwa malipo ya
shilingi 20,000/=(Elfu ishirini) kwa siku bila kukosa.

MASHARTI YA MAKABIDHIANO
i. Mmiliki wa bajaji atawajibika kununua vipuri (spear) pamoja na matengezo makubwa tu.
ii. Dereva hapaswi kubadilisha spear yoyote pasipo kupata taarifa toka kwa mmiliki
iii. Dereva atahusika na matengenezo madogo madogo tu
iv. Dereva atahusika kulaza bajaji na maegesho(parking) sehemu yenye usalama wakati wa
usiku ikiwa ni pamoja na gharama zake.
v. Dereva na atahusika na kufanya ukaguzi wa Bajaji kila siku kabla na baada ya kazi na
kuhakikisha ipo katika hali ya usalama na usafi
vi. Mmiliki/Mdhamini/Msimamizi atakua na wajibu wa kumukagua/kumsimamia/kumpata
maelekezo ya kazi dereva pamoja na njia/safari/barabara za kwenda/kutokwenda bila ya
maelekezo
vii. Dereva atajilipa mwenyewe katika mapato ya kila siku baada ya kutoa hesabu ya siku
viii. Dereva atahusika na adhabu zote za kiundeshaji ambazo zitasababishwa na
kutokuzingatia taratibu za udereva barabarani pamoja na gharama zake.
ix. Kushindwa kufuata mashariti hapo juu kipengele cha i-viii kwa pande zote mbili(Mmiliki
na Dereva) itapelekea mkataba huu kuvunjwa wakati wowote baada ya kujiridhisha
kwamba chombo(bajaji) kipo katika hali yake ya kawaida(bila hitilafu yeyote)

MKATABA HUU UMEFANYIKA KATI YA WAFUATAO;

Jina la Mmiliki : …... Sahihi ……………. Tarehe

Jina la Msimamizi: ………… Sahihi……………. Tarehe

Jina la Dereva : …………. Sahihi…………… Tarehe

WADHAMINI:

Mdhamini wa Dereva; ……………: Sahihi……………. Tarehe

Mdhamini wa Mmiliki; ……………: Sahihi……………. Tarehe

Mkataba huu umefanyika mbele ya Mwenyekiti wa Mtaa na kutambuliwa na Mwanasheria.

MWENYEKITI MTAA MWANASHERIA

Jina…………………………… Jina……………………………

Sahihi…………………………. Sahihi………………………….

Tarehe Tarehe

You might also like