You are on page 1of 5

DEGRA AUCTION MART

For Your Prosperity


P.o Box 619 Kahama; Nyihogo Street; Plot No.54, House No.33
Email Address:degrafinanceltd@gmail.com, Contacts: +255 752 710485/659 302 825
DEALERS & AUCTIONEERS IN PROPERTY VALUE, COMMISION AGENTS & DEBT COLLECTORS

MKATABA WA UKUSANYAJI MADENI / UNADISHAJI MALI


MKATABA HUU WA UKUSANYAJI MADENI NA UNADISHAJI MALI
Umeingiwa leo tarehe ____ Mwezi ______ 2022
KATI YA

Wa S.L.P (ambao katika mkataba huu watajwa tu kama (“MWAJIRI”) kwa


upande mmoja
NA
DEGRA AUCTION MART wa S.L.P 310 KAHAMA.SHINYANGA-TANZANIA
(ambao katika mkataba huu watajwa tu kama “WAKALA” kwa upande wa pili.

KWA KUWA mwajiri anahitaji kufanikisha ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja
wake walioshindwa kulipa marejesho kwa mujibu wa mkataba wa mikopo yao.
NA
KWA KUWA mwajiri anaona kwamba kuna umuhimu wa kumteua mtu mwenye
taaluma uwezo na weledi wa kufaa atakaye kusanya madeni hayo kutoka kwa wadaiwa
sugu.
NA
KWA KUWA anazo sifa hizo na amekubali kufanya kazi hiyo ya ukusanyaji wa madeni
hayo kutoka kwa wahusika (wadaiwa).
KWA HIYO MKATABA HUU UNASHUHUDIA MAKUBALIANO YAFUATAYO
1. Kwamba Mwajiri amemteua wakala ili afanye kazi ya kukusanya madeni hayo
kutoka kwa wadaiwa na wakala amekubali uteuzi huo.

2. Kwamba, wakala atawajibika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo wake wote.

3. Kwamba Mwajiri (Kampuni) atatoa nyaraka zote na Ushirikiano kwa Mkusanya


madeni kwa kumwonyesha walipo wadaiwa na dhamana zao.
1
DEGRA AUCTION MART
For Your Prosperity
P.o Box 619 Kahama; Nyihogo Street; Plot No.54, House No.33
Email Address:degrafinanceltd@gmail.com, Contacts: +255 752 710485/659 302 825
DEALERS & AUCTIONEERS IN PROPERTY VALUE, COMMISION AGENTS & DEBT COLLECTORS

4. Kwamba MWAJIRI (Kampuni) atalipa gharama mbalimbali atakazotumia


WAKALA kama vile Matangazo n.k ambazo baadae zitalipwa na mdaiwa kwa
kuongezwa kwenye deni la mdaiwa husika aliyesababisha kuingia kwa gharama
hizo.

5. Kwamba endapo kutakuwa na majadiliano juu ya MDAIWA na deni lake ni


lazima yashirikishe pande zote mbili.

6. Kwamba wakala atafanya kazi zake kwa mwongozo na maelekezo ya mwajiri na


pale itakapotokea upotoshaji wa aina yoyote juu ya mdaiwa na mali zake basi
mwajiri atawajika kwa upotoshaji huo.

7. Kwamba, makubaliano haya yatakuwa ya kipindi cha miezi______ tu kuanzia


tarehe mpaka tarehe na makubaliano haya
yanaweza kuuhishwa kwa kusainiwa tena.

8. Kwamba MWAJIRI NA MWAJIRIWA watafanya Tathimini ya pamoja kila


baada ya siku thelathini (30) yaani mwezi mmoja kwa ajili ya kuangalia
mwenendo wa kazi.

9. Kwamba sheria zitakazotumika katika mkataba huu ni za jamuhuri ya muungano


wa Tanzania.

10.Malipo ya wakala:-

 Ni jukumu la mwajiri kuwatambulisha wakala kwa wadaiwa wao wa madeni


na kama hilo litahitaji gharama zozote, basi gharama hizo zitalipwa na
mwajiri.

(i) Ulipaji kwa Hiari Upande Wa Mdaiwa.

(a) Malipo katika kipengele hiki yatajumuisha jumla ya deni analodaiwa mdaiwa,
asilimia kumi (25%) ya deni, pamoja na gharama za ufuatiliaji/usafiri deni
kama itakavyoelezwa katika kipengele (c) hapo chini.

2
DEGRA AUCTION MART
For Your Prosperity
P.o Box 619 Kahama; Nyihogo Street; Plot No.54, House No.33
Email Address:degrafinanceltd@gmail.com, Contacts: +255 752 710485/659 302 825
DEALERS & AUCTIONEERS IN PROPERTY VALUE, COMMISION AGENTS & DEBT COLLECTORS

(b) Mwajiri atamlipa wakala asilimia kumi tu (25%) ya deni lililokusanywa na


kuwasilishwa kwake, pamoja na gharama za ufuatiliaji wa deni hilo kwa mujibu
wa mkataba huu, lakini wakala hatakuwa na haki ya kuchukua fedha zozote
kutoka kwa mdaiwa kwa kisingizio kwamba wanajilipa kabla ya kuwasilisha
makusanyo hayo kwa mwajiri.

(c) Wakala atalipwa Tshs. 20,000/= (elfu ishirini tu) tu, ikiwa ni gharama za
ufuatiliaji) kwa kila mdaiwa atakayekabidhiwa kwake na ambae anapatikana
ndani ya wilaya aliyochukulia pesa. Pia wakala atalipwa kati ya Tshs.
100,000/= (laki moja tu) hadi Tshs. 300,000/ (laki tatu) kwa wale wadaiwa
watakaofuatiliwa nje ya Wilaya na Mkoa waliochukulia pesa,

(d) Jumla ya gharama zote zilizoainishwa katika sehemu hii ambazo ni asilimia
25% na gharama za ufuatiliaji deni zitalipwa na mdaiwa na sio mwajiri na kama
zitakavyoainishwa kwenye notisi ya madai atakayopewa na wakala.

(ii) Ulipaji utakaohusisha kutumia nguvu.

(a) Iwapo mali za mdaiwa zitakamatwa mf; mifugo na kumfanya wakala kuswaga
mifugo hiyo kwa zaidi ya 3km basi mdaiwa huyo atalipa gharama za uswagaji
wa mifugo hiyo ambazo ni Tsh. 30,000/= (Elfu Thelathini) kwa kila mfugo na
kama vitu vya ndani vitakamatwa na kumfanya wakala kukaa na vitu hivyo kwa
maana ya uhifadhi, basi gharama za uhifadhi huo zitatozwa kulingana na
thamani ya mali husika.

(b) Iwapo mali za mdaiwa/dhamana zitakamatwa na wakala na kutangazwa kuuzwa


kwa mnada wa hadhara na hatimae kuuzwa mdaiwa huyo atakumbana na
gharama za mnada na matangazo Shilingi za kitanzania laki tatu tu (Tsh.
300,000/=) na kama mdaiwa huyo atawahi kukomboa mali zake zisipigwe
mnada basi atalazimika kulipia gharama za matangazo Shilingi laki mbili (Tshs.
200,000/=).

11.KUVUNJA MKATABA
Mkataba unaweza kuvunjika wakati wowote iwapo upande mmoja hautaridhika na
utendaji kazi wa upande mwingine kwa kutoa notisi ya siku thelathini (30) ya
kusudio la kuvunja mkataba.

3
DEGRA AUCTION MART
For Your Prosperity
P.o Box 619 Kahama; Nyihogo Street; Plot No.54, House No.33
Email Address:degrafinanceltd@gmail.com, Contacts: +255 752 710485/659 302 825
DEALERS & AUCTIONEERS IN PROPERTY VALUE, COMMISION AGENTS & DEBT COLLECTORS

HIVYO BASI, wahusika wametia saini zao hapa chini katika namna na tarehe
kama inavyoonekana hapa chini;

IMETIWA LAKIRI YA ……………………………


……………………………………………………….
MUHURI
NA KUWASILISHWA mbele yetu leo tarehe
…………. Mwezi wa …………… Mwaka ……...

JINA:……………………………………… …….….
SAINI: ………………………………………………
ANUANI: …………………………………………...
WADHIFA: …………………………………………

IMETIWA LAKIRI YA DEGRA AUCTION MART


NA KUWASILISHWA mbele yetu leo tarehe MUHURI
……Mwezi wa…………… Mwaka ……………….

JINA: …………………………………………….
SAINI: …………………………………………...
ANUANI: …………………………………..…....
WADHIFA: ……………………………………...

UMESHUHUDIWA MBELE:
Jina: …………………………………
Sahihi: ………………………………
4
DEGRA AUCTION MART
For Your Prosperity
P.o Box 619 Kahama; Nyihogo Street; Plot No.54, House No.33
Email Address:degrafinanceltd@gmail.com, Contacts: +255 752 710485/659 302 825
DEALERS & AUCTIONEERS IN PROPERTY VALUE, COMMISION AGENTS & DEBT COLLECTORS

Anwani: …………………………….
Cheo: KAMISHINA WA VIAPO

You might also like