You are on page 1of 2

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA.

SEHEMU A.

MAKABIZIANO NA MALIPO

Mkataba huu ni wa mpangaji na mwenye nyumba, nyumba iliyopo eneo la Lemara Kikokwaru B nyumba
namba 04.

Mkataba huu ni kati ya ndugu..................................................................................................amabaye


nimpangaji na ndugu..................................................................................amabaye ni mwenye nyumba.

Mkataba huu ni wa miezi mitatu kuanzia tarehe ..........................hadi tarehe.......................

Kodi kwa mwezi ni Laki moja (Tsh.100,000/=) kwa chumba. Hivyo mpangaji amelipa Laki tatu tu
(Tsh.300,000) ambayo ni kodi ya miezi mitatu(3).

SEHEMU B

MASHARTI YA MKATABA

1. Mpangaji anatakiwa kulipa gharama zote za umeme na maji kwa kadri atakavyotumiaama kuelekezwa
na mwenye nyumba.

2. Mpangaji anatakiwa kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika maeneoyanayomzunguka pamoja na
maliwato.

3. Mpangaji hatakiwi kufanya marekebisho yoyote ya nyumba bila idhini ya mwenyenyumba.

4. Hairuhusiwi kwa mpangaji kumpangishia nyumba mtu mwingine

5. Endapo utapata mgeni na atakaa kwako zaidi ya siku moja ni sharti umtaarifu mwenyenyumba.

6. Mpangaji atatakiwa kuhama katika nyumba endapo mwenye nyumba atataka iwe hivyokwa kumpa
notisi ya kuhama mwezi mmoja (1) kabla ya kumaliza mkataba uliopo.

7. Endapo mpangaji atataka kuendelea na mkataba kwa miezi mingine atatakiwakumtaarifu mwenye
nyumba mwezi mmoja (1) kabla ya mkataba uliopo kumalizika.

8. Mpangaji anatakiwa kuhakikisha usalama na utulivu unapatikana muda wote wamkataba wake.

9. Uuzaji na utumiaji wa kilevi chochote kilichopigwa marufuku kisheria hairuhusiwi.

10. Hauruhusiwi kufanya biashara yoyote ndani au kuzunguka eneo la nyumba pasipoidhini ya mwenye
nyumba.

SEHEMU C

MAMBO YANAYOWEZA KUKATISHA MKATABA PASIPO KUPEWA NOTISI.


1. Ugomvi kati ya mpangaji na mpangaji, mpangaji na mwenye nyumba , mpangaji namajirani.

2. Matusi ya namna yoyote ile.

3. Kushiriki matukio ya wizi/ujambazi

4.Kudharau mamlaka.

Kwa kuthibitisha mkataba huu kwa pande zote zinaweka chini sahihi zao kwa makubaliano yote
yaliyoandikwa kwenye mkataba kwa hiari yao kama ifuatavyo:-

1. JINA LA MWENYE NYUMBA..

SAHIHI.................................................................................................

TAREHE.................................................................................................

2.JINA LA MPANGAJI ...................................................................................................................

SAHIHI.................................................................................................

TAREHE.......................................................................................................................

3. JINA LA MPANGAJI ANAEKANAYE

SAHIHI...........................................................................................................

TAREHE..................................................................................................................

You might also like