BAINA MOHAMED ALI SALIM wa S.L.P 19180, Dar es salaam (ambaye katika mkataba huu ataiwa "MWENYE NYUMBA" kwa upande wa kwanza, NA ABDIKADIR HASSAN wa mobile No. 0744163208 Dar es Salaam (ambaye katika mkataba huu ataitwa "MPANGAJI") kwa upande wa pili. KWA VILE mwenye nyumba anamiliki nyumba No. 18 plot No. 06 Mtaa wa Pemba/Livingstone, Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Dar es salaam (Ambayo kwenye mkataba huu itaitwa "Nyumba hiyo") na anataka kumpangisha Mpangaji, ghorofa ya tano apartment Na.1 kwa ajili ya kuishi. HIVYO MKATABA HUU UNASHUHUDIWA YAFUATAYO: 1. Mwenye nyumba kwa hiari yake amekubali kumpangisha mpangaji ghorofa ya tano apartment No.1 kwa ajili ya kuishi, na mpangaji hiyari yake amekubali kupanga nyumba hiyo kwa kipindi cha miezi 12. Kuanzia tarehe 05/04/2024 mpaka tarehe 04/05/2025. Na amelipa kodi ya miezi sita. 2. Kodi ya nyumba itakuwa 500,000/= (Laki tano tu) kwa mwezi, na kwa miezi sita itakuwa Tsh 3,000,000/= (Milioni tatu tu). 3. Mpangaji atatumia nyumba hiyo kwa ajili yakuishi. MPANGAJI ANAWAJIBIKA KUFANYA YAFUATAYO i. Kulipa kodi kama alivyokubaliana na mwenye nyumba katika mkataba huu. ii. Atalipa gharama za umeme atakaotumia. iii. Mpangaji haruhusiwi kupangisha mtu mwingine sehemu aliyopanga bila kupata idhini ya maandishi kutoka kwa mwenye nyumba. iv. Mpangaji hatafanya matengenezo yoyote kwenye sehemu aliyopanga bila kupata kibali kutoka kwa mwenye nyumba. v. Mpangaji atahusika mwenyewe kwenye marekebisho ya kitu chochote ambacho kitaharibika. vi. Mpangaji itamlazimu sehemu hiyo aliyopanga pamoja na mazingira wakati wote, sehemu ya nyumba aliyopanga pamoja na mazingira ya ndani na nje ni safi na ipo katika hali ya kuridhisha. vii. Baada ya muda wa mkataba kumalizika iwapo mpangaji atataka kuendelea au kutoendelea na upangaji katika sahemu hiyo itabidi utoe taarifa ya mwezi mmoja (1) kabla ya muda wa upangaji haujamalizika kwa mwenye nyumba na atawalazimu wakubaliane upya na kwa mkataba. Hali kadhalika na mwenye nyumba itabidi atoe notice ya mwezi mmoja (1) kwa mpangaji kama ataamua kumtoa. viii. Kwamba mpangaji atakapomaliza muda wake atakabidhi sehemu aliyopanga bila ya kuvunja au kuharibu sehemu yoyote ya fremu hiyo. ix. Mkataba utatawaliwa na sheria za Tanzania.
KWA KUTHIBITISHA MAKUBALIANO HAYA WAHUSIKA
WAMETIA SAINI MKATABA HUU KAMA IFUATAVYO:- IMETIWA saini hapa Dar es salaam na MOHAMED ALI SALIM Ambaye ninamfahamu leo hii tarehe: ____ Mwezi ____ Mwaka _______ _________________________ Saini _____________________________ MWENYE NYUMBA Anuani____________________________
IMETIWA saini hapa Dar es salaam na
ABDIKADIR HASSAN Ambaye ninamtahamu leo hii tarehe: ____Mwezi _______Mwaka ______ ________________________ Saini__________________________ MPANGAJI Anuani________________________