You are on page 1of 3

Nambari ya mnara _________________________

HTT INFRACO LIMITED Mkataba wa Upangaji Eneo

Jina la Eneo la Ardhi: __________ Nambari ya Eneo la Ardhi: ___________ Mkoa: _____________

Tarehe: ________________

1. Mkataba huu unaingiwa kati ya ________________ S.L.P ______, ____________, (Simu


______________) na HTT INFRACO LIMITED (Helios) S.L.P 105297, Dar es Salaam ambapo
Mpangishaji anairuhusu Helios kujenga, kuendesha na kudumisha mnara wa mawasiliano ya simu
ndani ya eneo lililozungushiwa uzio lenye mita _____ kwa mita _____ lililopo _____________ kama
linavyoonekana katika ramani iliyoambatishwa (Eneo la Ardhi).

2. Helios inaruhusiwa kushikilia eneo hilo la Ardhi kwa muda wa miaka 30 kuanzia tarehe __________
na ina haki isiyopingika ya kujenga na kudumisha mitambo kwenye mnara kama itakavyoona inafaa.
Helios pia ina haki isiyopingika ya kujenga na kudumisha mitambo ikiwa ni pamoja na jenereta,
matanki ya mafuta na bateri ndani ya eneo lililozungushiwa uzio.

3. Helios wanatakuwa na haki baada ya kumtaarifu Mpangishaji, kuruhusu chombo chochote, kampuni
yoyote msambazaji wa huduma ya mawasiliano ya simu kushiriki, kutwaa au kupanga eneo katika
mnara na kuwaruhusu kuweka mitambo yao kwenye mnara bila Mpangishaji kuomba fedha zaidi ya
fedha ya pango iliyokubalika katika Mkataba huu, isipokuwa tu pale Helios watakapotumia eneo zaidi
la Ardhi kuliko lile lililoainishwa katika Mkataba huu. Endapo Helios watatumia eneo zaidi la Ardhi,
Mpangishaji anaweza kuomba nyongeza ya fedha ya pango, ambayo itakubaliwa kwa pamoja kati ya
Mpangishaji na Helios, hata hivyo ongezeko hilo halitazidi theluthi moja ya fedha ya pango ya mwaka.

4. Helios na wateja wake wataruhusiwa bila kikwazo chochote, ndani ya masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa
wiki kuingia eneo la ardhi/eneo lililo juu ya ghorofa; hata hivyo itajitahidi pale inapowezekana, kuingia
ndani ya eneo hilo katika muda wa kazi. Kuingia katika eneo husika kutakuwa chini ya udhibiti wa
Helios, ikiwa ni pamoja na Mpangishaji kupata ruhusa toka Helios kabla ya kuingia katika eneo husika.

5. Helios watamlipa Mpangishaji fedha ya pango la mwezi ya Shilingi za Kitanzania


___________________ (TZS ______________________________) ikijumuisha asilimia 10% (ama
asilimia nyingine kama itakavyowekwa na sheria) na asilimia 1% ya ushuru wa stempu. Fedha hii
italipwa mara moja kwa mkupuo kila mwanzo wa mwaka wa malipo kwa hundi au kutumia
uhamisho wa kielektroniki kupitia akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti:
______________________, Namba ya Akaunti _________________, iliyoko benki
ya______________, tawi la _______________.

6. Mpangishaji na Helios wanakubaliana kwamba fedha ya pango iliyokubalika itaongezwa kila baada ya
miaka mitano kwa mujibu wa takwimu za mfumuko wa bei wa Tanzania (Tanzanian Consumer Price
Index (CPI)) kwa kipindi hicho ila ongezeko hilo halitazidi asilimia kumi na tano (15%) ya fedha ya
pango ya mwaka.

7. Helios wana jukumu la kupata, kuhifadhi na kuhuisha vibali na leseni zinazohusiana na ujenzi wa
mnara na operesheni katka eneo husika. Jina la Mpangishaji atalazimika kutoa kwa Helios nyaraka
yoyote (kama vile Hati ya Usajili wa Ardhi) ili kuthibitisha kwamba Mpangishaji ndiye mmiliki halali
wa eneo la ardhi litakalopangishwa kwa Helios.

8. Jina la Mpangishaji atatoa haki isiyopingika kwa Helios kutandaza nyaya (za umeme, teknolojia ama
nyaya za shaba) juu au chini kupita kwenye eneo linalopakana na mnara uliyopangishwa kwa Helios ili
nyaya hizo ziweze kufika kwenye mtandao wa mawasiliano husika. Kutotumika kwa haki hii
hakutamaanisha kuwa Helios wameachilia haki hii kwa mtu yeyote (Mpangishaji akiwemo).
Mpangishaji atahakikisha kuwa mtu yeyote atakayetandaza nyaya husika amepata idhini ya maandishi
toka kwa Helios kabla kuanza kazi husika.

1
9. Endapo kutakuwa na ukiukwaji wa Mkataba huu ambayo hautapatiwa ufumbuzi ndani ya siku 90
baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya ukiukwaji huo, basi aidha Helios au Mpangishaji anayo haki
kusitisha Mkataba huu. Mkataba ukisitishwa, Helios anakubali kuondoa mitambo na mali zingine
zilizoko kwenye eneo lililopangishwa.

10. Helios wana haki ya kuawaza (assign) Mkataba huu kwa mtu yeyote au kampuni nyingine kwa kutoa
taarifa ya kimaandishi kwa Mpangishaji.

11. Helios ana haki ya kuweka dhamana haki zake katika mnara na eneo lililopangishwa kwa kutoa taarifa
kwa Mpangishaji.

12. Mkataba huu utahuishwa moja kwa moja kwa masharti yale yale yaliyomo kwenye Mkataba huu labda
tu pale aidha Mpangishaji au Helios atawasilisha taarifa kwa mwingine isiyopungua miezi 3 kabla ya
muda wa kuisha kwa Mkataba huu.

13. Helios itakuwa na bima kuhusiana na pango lake kwenye eneo husika. Madhara yoyote, upotevu
wowote katika eneo lililopangishwa utakaotokana na Mpangishaji utafanyiwa matengezo kwa gharama
za Mpangishaji.

14. Mpangishaji anakiri kuwa na idhini ya kuingia Mkataba huu na Helios ikiwa ni pamoja na kuwa na
nyaraka zinazohusiana na umiliki wa eneo husika na kuwa kodi zote za Serikali kuhisiana na ardhi
husika zimelipwa. Jina la Mpangishaji atalipa gharama ambazo Helios itapata kuhusiana na madai ya
watu wengine kuhusiana na eneo lililopangishwa katika Mkataba huu.

15. Endapo kutakuwa na kutoelewana kati ya Mpangishaji na Helios bila kufikia muafaka ndani ya siku
21, mgogoro huo utasuluhishwa kwa njia ya Uamuzi (arbitration) kwa mujibu wa sheria ya Arbitration
Act; Sura ya 15 ya Sheria za Tanzania na Mkataba huu utaongozwa katika kutafsiriwa kwake na Sheria
za Tanzania.

16. Endapo Mpangishaji ataamua kuuza eneo la ardhi ambamo kuna mnara wa mawasiliano kama
ilivyotafsiriwa kwenye kifungu cha 1 hapo juu basi atatoa taarifa kwa Helios juu ya kusudio hilo ili
kumpa nafasi/haki ya mwanzo Helios kukataa au kushindwa kununua eneo hilo kabla ya kutoa nafasi
kwa wanunuzi wengine.

17. Endapo Helios au wateja wake watazuiwa kuingia ndani ya eneo liliopangishwa au kuendesha mitambo
kwenye eneo hilo kwa jambo lolote lililo nje ya uwezo wa Helios au Mpangishaji (tendo la Mungu),
ikiwa ni pamoja na radi, moto, gharika, vurugu ama mapigano ya kiraia, Helios hawatalipa fedha ya
pango mpaka pale Helios au wateja wake watakapoweza kurejesha shughuli zao kama kawaida.

18. Pande zote za mkataba huu zinakubali kwamba katika kipindi cha mkataba huu kunaweza kutokea
tukio/matukio au mazingira fulani ama ya kibiashara au kiufundi ambayo yatailazimisha Helios
kufanya zoezi la kuunganisha, kuoanisha ama kujumuisha minara yake iliyojengwa katika eneo moja.
Pindi mazingira hayo yatakapojitokeza, Helios atamwandikia Mpangishaji notisi awali ya siku
zisizopungua thelathini (30) kumfahamisha kusudio lake la kusitisha moja kwa moja mkataba huu. Na
pindi siku za notisi hii zitakapomalizika, mkataba huu utakuwa umesitishwa rasmi na Helios atamlipa
Mpangishaji kodi ya miezi mitatu (3) kama fidia kutokana na kusitisha mkataba huu kabla ya wakati.
Na endapo muda wa mkataba huu utakuwa chini ya miezi mitatu (3) kabla ya kufikia ukomo wake basi
Helios atamlipa Mpangishaji kipindi kilichobakia mpaka tarehe ya mwisho wa mkataba husika.

19. Mkataba huu unajumuisha makubalino yote kati ya Helios na Mpangishaji na unafuta makubaliano
yoyote ya awali, aidha yawe kimaandishi au la. Endapo kutakuwa na mgogoro kati ya Mkataba huu na
nyaraka nyingine yoyote, basi Mkataba huu ndiyo utakuwa halali.

UMESAINIWA na KUTOLEWA NA
NDUGU ………………………………….
ambaye ninamfahamu binafsi ama
nimetambulishwa kwake na ndugu
………………………. ambaye ninamfahamu
2
binafsi leo tarehe …….. Mwezi ……………………
_______________________________
Saini/Muhuri wa Mpangishaji

Jina: …………………………………

Wadhifa: Wakili/Hakimu/Kamishna wa Kiapo

Anuani: ………………………………

Saini: …………………………………

UMESAINIWA na KUTOLEWA kwa niaba ya HTT


INFRACO LIMITED leo Tarehe __________Mwezi
_________________________

Jina: GWAKISA STADI

Wadhifa: MKURUGENZI MTENDAJI

Anuani: S.L.P 105297, DAR ES SALAAM.

Saini:

Jina: MICHAELA MARANDU

Wadhifa: MKUU WA IDARA YA SHERIA

Anuani: S.L.P 105297, DAR ES SALAAM.

Saini:

You might also like