You are on page 1of 6

MKATABA WA HUDUMA

TAREHE …. MWEZI ……. 2022

KATI YA

……………………………………………………………………

NA
………………………………………………………….

____________________________________________

MKATABA WA HUDUMA YA UWAKALA WA KUUZA VIWANJA

________________________________________________

MKATABA WA HUDUMA
Mkataba huu wa Huduma umefanyika leo tarehe ……. mwezi ……… mwaka…..……
Kati ya

MWANJISI INTERNATIONAL LIMITED wa S.L.P 59 BAGAMOYO3.


(ambaye katika mkataba huu atajulikana kama “MUUZAJI” kwa upande mmoja pamoja
na warithi wake).
Na
………………………….. ya S.L.P ……, (ambaye katika mkataba huu atajulikana kama
“WAKALA” pamoja na warithi wake kwa upande wa pili).
Ambapo, Muuzaji ni mmiliki wa viwanja vifuatavyo; Kiwanja No............. vilivyopo
kwenye Kitalu ‘SS’ eneo la KEREGE Bagamoyo, vyenye jumla ya eneo la Mita za Mraba
(Square Meters) …….......… (ambapo katika mkataba huu vitajulikana kama
“Viwanja”
Ambapo, Wakala…...........................………. (Describe the party); iliyopo Wilaya ya
Bagamoyo, mkoa wa Pwani na inayojishughulisha na utoaji huduma ya uwakala wa
kuuza, kununua na kupangisha mali zisizohamishika kwa watanzania kwa ujumla.

KWA KUZINGATIA VIPENGELE VYA HAPO JUU, MKATABA HUU UNASHUHUDIA


KAMA IFUATAVYO, KWAMBA:
Kifungu cha 1: Muda wa Mkataba

• Kwamba muda wa mkataba huu utakuwa ni kipindi cha miezi mitano (5) na
utaanza tarehe ...….. Hadi tarehe …….........
• Kwamba baada ya kuisha kwa muda wa Mkataba huu pande mbili zinaweza
kuhuisha mkataba huu kwa kipindi kingine baada ya kukubaliana.

Kifungu cha 2: Malipo ya uwakala

• kwamba Muuzaji anaridhia kuuza viwanja vyake kupitia Wakala na anampa Wakala
haki ya kipekee za kuuza ardhi yake kwa mujibu wa mkataba huu.
• kwamba Malipo ya rejesho kwa kazi ya uwakala itakuwa Shillingi za Kitanzania
………………………................kwa mauzo ya kila mita za mraba za viwanja husika
vitakavyouzwa kwa wakati. Aidha, rejesho hilo halitajumuisha gharama za kutafuta
masoko (matangazo).
• Kwamba Malipo ya rejesho la uuzaji wa viwanja yatapitia kwenye akaunti za benki
ya Muuzaji yenye akaunti namba …………………………. yenye jina
la………………………………….iliyoko ……………………….Bank tawi la
………………………..

Kifungu cha 3: Wajibu wa Muuzaji

3.1 Kwamba, Muuzaji ana wajibu wa kumkabidhi Wakala viwanja vyake anavyotarajia
kuviuza kupitia wakala ambavyo havina mgogoro wowote ule kwa ajili ya kuviuza;
3.2 Kwamba, Muuzaji atakuwa na wajibu wa kumkabidhi Wakala Nyaraka kivuli
ambayo ni Muhtasari wa upimaji; Ramani ya Mipango Miji na Ramani ya Upimaji ili
kumsaidia wakala hatua za uhakiki wa viwanja na utayarishaji wa hati miliki.
3.3 Kwamba, kwa kipindi chote cha mkataba huu Muuzaji atawajibika kumpa taarifa
Wakala pale atakapopata mteja ambaye amewasiliana na muuzaji moja kwa moja
ili kuepuka kuuza kiwanja mara mbili tofauti.
• Kwamba, Muuzaji kwa muda wote wa mkataba atamruhusu Wakala kuingia katika
eneo lake kwa ajili ya matangazo, kupeleka mteja, kukagua alama na kufanya
shughuli nyingine zinazohusaiana na msharti ya mkataba huu.
• Kwamba Muuzaji ana wajibu wa kuhakikisha taarifa na nyaraka anazotoa kuhusu
viwanja hivi ni sahihi kwa kadri ya uelewa wake hivyo Muuzaji atamlipa fidia Mteja
endapo itatokea hasara itakayosababishwa na taarifa zisizo sahihi.
• Kwamba Muuzaji ana wajibu wa kusaini mikataba ya mauziano kwa wateja
waliomaliza malipo yao.

Kifungu cha 4. Haki za Muuzaji

• Kwamba, muuzaji ana haki ya kupata taarifa ya mwenendo wa mauzo ya viwanja


vyake kila wiki.
• Kwamba, Muuzaji ni mmiliki halali wa viwanja husika hivyo ana haki ya kisheria
kuuza viwanja husika kwa kuzingatia Kifungu Na.3.3.
• Kwamba, ikitokea Muuzaji amepatwa na janga la asili kama vile kilema, magonjwa
au kifo, warithi/ wawakilishi wake wana haki na wajibu wa kutekeleza Masharti ya
mkataba huu kama sawasawa na makubaliano ya awali kati ya Muuzaji na Wakala
mpaka pale muda wa Mkataba huu utakapokwisha.

Kifungu cha 4: Wajibu wa Wakala

4.1 Kwamba Wakala ana wajibu wa kutafuta wateja na kuuza viwanja kwa wakati
uliokubalika kwenye mkataba huu.
4.2 Kwamba Muuzaji atauza kila Eneo la Mita Moja Mraba (1 Square Meter) kwa kiasi
............................................
4.3 Kwamba malipo ya kila kiwanja yatafanyika kwa awamu.

4.4 Kwamba Wakala ana wajibu wa kumpatia taarifa Muuzaji kila wiki kuhusu
mwenendo wa mauzo ya viwanja.
• Kwamba Wakala ana wajibu wa kulipa kodi za kisheria na gharama za watumishi
wake katika utekelezaji wa majukumu ya mkataba huu.

• Kwamba wakala ana wajibu wa kuwasaidia wateja walionunua Viwanja hivi


kufuatilia hati zao na kuhakikisha wanapata hati zao kwa wakati kwa gharama za
mteja.
Kifungu cha 5. Haki za Wakala

• Kwamba, Wakala ana haki ya kukabidhiwa na Muuzaji viwanja ambavyo havina


mgogoro wowote ule kwa ajili ya kuviuza na Nyaraka kivuli ambayo ni Muhtasari
wa upimaji; Ramani ya Mipango Miji na Ramani ya Upimaji ili kumsaidia wakala
hatua za uhakiki wa viwanja na utayarishaji wa hati miliki.

• Kwamba, kwa kipindi chote cha mkataba huu Wakala ana haki ya kupata taarifa
kutoka kwa muuzaji pale atakapotaka kuuza kiwanja ambacho kimeainishwa
kwenye mkataba huu.

• Kwamba, kwa muda wote wa mkataba Wakala ana haki ya kuingia katika eneo
lake kwa ajili ya matangazo, kupeleka mteja, kukagua alama na kufanya shughuli
nyingine zinazohusaiana na msharti ya mkataba huu.

HIVYO BASI;
• Pande zote mbili zinakiri kwamba wamesoma na kupokea nakala ya mkataba huu wa
Huduma na pia wamesoma na kuelewa haki na wajibu wao katika mkataba huu.
• Endapo Muuzaji au Wakala anakusudia kuvunja makubaliano haya basi inabidi upande
mmoja utoe taarifa ya mwezi mmoja kwa upande wa pili na hakutokuwa na gharama
yeyote ya kuvunja mkataba huu ambayo itaingiwa na yeyote kati ya pande hizi mbili;
bali pande zote mbili zinatakiwa kutekeleza wajibu wao kabla ya kuvunja mkataba huu
na kuhakikisha usitishwaji huo hauumizi upande wowote ule.
• Kwamba, endapo mgogoro wowote ukijitokeza baina ya pande mbili katika utekelezaji
wa mkataba huu mgogoro utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo baina ya wahusika wa
mkataba huu wa wapatanishi wao na endapo mgogoro huo hautopatiwa ufumbuzi,
sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazohusu mikataba zitachukua mkondo
wake.

Mkataba huu umeshuhudiwa na kutiwa saini na hawa wafuatao hapa chini:

UMEWASILISHWA na KUTIWA SAINI hapa


BAGAMOYO na ___________________________
_____________________________________________
ambaye namfahamu binafsi/ametambulishwa ________________
kwangu na _______________________________ MUUZAJI
leo tarehe______Mwezi___________________2022.

MBELE YANGU:

Jina: _____________________________________

Saini: _____________________________________

Anuani: ___________________________________

Cheo: ___________________________________

UMEWASILISHWA na KUTIWA SAINI hapa


BAGAMOYO na _______________________
ambaye namfahamu binafsi/ ametambulishwa _________________
kwangu na _______________________________ WAKALA
leo tarehe ________mwezi________2022.

MBELE YANGU:
Jina: ______________________________________
Saini: _____________________________________

Anuani: ___________________________________
Cheo: _________________________________

You might also like